EATV, 5 CONNECT: Mpenzi zaidi ya mtu mmoja ni umaarufu au?

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,603
2,000
Kuna akina dada wawili wapo live studio wakitetea hoja ya kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja. Mmoja anasema anao watatu ambao anawapanga na hawajawahi kugongana. Kuna mwanaharakati anapinga hii ishu ila inaonekana kama anazidiwa na hawa mabinti......wadau mna mtazamo gani?
 
Roulette

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
5,600
0
kwa kweli nashangaa sana. yaani siku hizi wizi na utapeli umekua ndio ujanja hadi watu wanajivunia TV? alafu maboyfriend wake wakimuuliza alikua anasema nini TV atawadanganya tena eti she was acting just for the sake of the broadcast ila ana mmoja tu?
 
Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,603
2,000
Mtu mzima kwa ajili ya kutoa pesa na matunzo, mpenzi wa pili ni Sharobaro kwa ajili ya kujirusha na starehe na mpenzi wa tatu ndio wa ukweli.
 
Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,603
2,000
Kuna mmoja anaponda kuwa mila na desturi kwa sasa hakuna kwa sababu watu wanafunga ndoa tayari wana mimba.
 
Roulette

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
5,600
0
Mtu mzima kwa ajili ya kutoa pesa na matunzo, mpenzi wa pili ni Sharobaro kwa ajili ya kujirusha na starehe na mpenzi wa tatu ndio wa ukweli.
Sasa huyo wa ukweli ana kazi gani? au ni mapambo tu? na asiseme she has feelings for him coz utampendaje mtu alafu unamchukulia watu wa2 in addition? bora nisichangie tena hapa, nisije nikaonekana mi mjinga...
 
Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
206,316
2,000
Kuna akina dada wawili wapo live studio wakitetea hoja ya kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja. Mmoja anasema anao watatu ambao anawapanga na hawajawahi kugongana. Kuna mwanaharakati anapinga hii ishu ila inaonekana kama anazidiwa na hawa mabinti......wadau mna mtazamo gani?

tatizo ni kuwa aibu sasa ndicho tunachojivunia kwa sababu kwenye ulimwengu wa uzalishaji hatumo......................au tumebaki wachache sana na wazalishaji kamwe hawajivunii aibu yao..........
 
Ave Ave Maria

JF-Expert Member
Apr 22, 2011
10,742
0
Mtu mzima kwa ajili ya kutoa pesa na matunzo, mpenzi wa pili ni Sharobaro kwa ajili ya kujirusha na starehe na mpenzi wa tatu ndio wa ukweli.

Huu mchezo mi nimeanza kuushuhudia tangu nikiwa skonga. Nikiangalia wengi wao nilowaona wanafanya hivi yaani sioni sababu ya msingi zaidi ya tamaa tu!
 
Cantalisia

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
5,224
1,195
Kilichobaki ni kumwomba mungu atunusuru na hizi style mpya za maisha ya mapenzi zinazokuwa modifaidi kila kukicha,kama hiyo nayo ni hoja ya kutetewa tena hadharani kwenye tv inayoonekana africa mashariki yote,basi kila aliyesimama na angalie asidondoke!
 
Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,603
2,000
Huu mchezo mi nimeanza kuushuhudia tangu nikiwa skonga. Nikiangalia wengi wao nilowaona wanafanya hivi yaani sioni sababu ya msingi zaidi ya tamaa tu!

Hali hii kwa kweli inasikitisha.......
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom