Easy TV kulikoni?

Zanta

JF-Expert Member
Apr 4, 2011
2,028
788
Wanabodi, jana ilipofika saa sita usiku chanel za mzee Mengi zikawa hazionyeshi tena, sasa naomba kuuliza ni kwamba Mzee Mengi kajitoa ili tununue king‘amuzi chake au kuna nini hapa? Hawa tcra wanafanya kazi gani maana star tv ilishajitoa mapema sasa huu si tutakua na utitiri wa ving‘amuzi ? Mwenye details ya hii mambo naomba anijulishe
 
Kuepusha huo usumbufu nunua ving'amuz vyote,ndio malengo au dhumun la tcra mkuu kama ulikua hujui.
 
Hawa Easytv nilikua nawakubali sana. Ila nimegundua ni wababaishaji wakubwa,hawana huduma kwa wateja,simu zao hazipatikani.
 
Mm binafsi piga Ua, Hata Channel zote za Kibongo wakiamua ku-izira Easy TV, sitohama kwani wao Ndio walio ninywesha Maji ya Digitali kabla hata ya Hao TCRA hawajaamua hii Nchi iingie katika Mfumo wa Kidigitalia.

Pamoja na kutokuwa na Customer Care lakini Huduma zao ni Superb kuliko Ving'amuzi vingine achilia Mbali Baba-lao ambao ni DSTV

TCRA ni ndumi la kuwili kwani walishatoa tamko kuwa Kila Kisambuzi kitakacho pewa leseni lazima wahakikishe kuwa wanarusha Channel za Nyumbani zote bure. Kwa Mantiki kuwa kama kifurushi ulicholipia kimeisha, basi uendelee kuona Channel zote za Bongo/Nyumbani bure hadi pale utapopata tena hela ya kwenda kulipia.

Ufuatiliaji umekuwa ZIRO.
 
Mm binafsi piga Ua, Hata Channel zote za Kibongo wakiamua ku-izira Easy TV, sitohama kwani wao Ndio walio niloninywesha Maji ya Digitali kabla hata ya Hao TCRA hawajaamua hii Nchi iingie katika Mfumo wa Kidigitalia.

Pamoja na kutokuwa na Customer Care lakini Huduma zao ni Superb kuliko Ving'amuzi vingine achilia Mbali Baba-lao ambao ni DSTV

TCRA ni ndumi la kuwili kwani walishatoa tamko kuwa Kila Kisambuzi kitakacho pewa leseni lazima wahakikishe kuwa wanarusha Channel za Nyumbani zote.

Ufuatiiaji umekuwa ZIRO.
tcra majanga sana sijui twende wapi
 
Inaniuniza sana pale wale tulio wapa dhamna ya kutusimamia wanatututosa ! TCRA please tunaomba jibu
 
Kesho lazima niwaibukie wanipe majibu ya kueleweka

Mimi nimekwenda kwa wakala wao akaniambia kuwa amewasiliana nao wakamwambia kuwa channel hizo labda zinaweza kurudi baada ya wiki moja. Neno "labda" limenikatisha tamaa kabisa.

Ilikuwa hivi hivi ilipopotea hewani Startv. Kama ukipata mda ebu pitia kwa ofisi zao utuletee majibu ya kueleweka
 
Easy TV wameanza kuwa wezi na hawana heshima kwa wateja wameshindwa kusema sababu tumebaki tunakisia tu TCRA wameacha wafanye atakacho kuna macheannel mia ya wachina maajabu
 
kwakweli hao Easy TV wasifikirie kabisa kuzitoa channel za IPP kwenye mfumo wao
Ndo wameshazitoa hizo mzee yaaniyamebaki maumivu kwetu wakati tcra wamekaa wanaangalia tu, ilianza star tv sasa za mzee mengi
 
Mimi nimekwenda kwa wakala wao akaniambia kuwa amewasiliana nao wakamwambia kuwa channel hizo labda zinaweza kurudi baada ya wiki moja. Neno "labda" limenikatisha tamaa kabisa.

Ilikuwa hivi hivi ilipopotea hewani Startv. Kama ukipata mda ebu pitia kwa ofisi zao utuletee majibu ya kueleweka
Mkuu sikupata muda wa kupitia ila lazima niwabukie la sivyo wturudishie chetu twarudisjie dekoda yao
 
Mimi mwenzenu nipo tofauti sana, huwa sina mzuka na hizi televisheni za bongo.

So far katika Easy TV kuna Channel Ten, TBC hizi zinatosha kwa vipindi vya kitanzania na taarifa za habari ukiongezea na Clouds na DTV huko wapenzi wa burudani wataendelea kuburudika.

Hao ITV, EATV na Capital wana lipi la maana mnalolikosa???
 
hivi kuna anaejua undani wa Easy TV? Ofisi yao kuu iko wp? Inamilikiwa na nani? Na makeke yangu yooote bado sijawahi kukutana na mtu anasema anafanya kazi ofisi zao hata kwa kupitia rafiki wa rafiki yake rafiki yangu...mweeee:hand:
 
Easy TV wana ofisi zao kuu pale ilipo ZhongHua Garden Mikocheni (Victoria).

Mmiliki wake ni mzee mmoja wa Kichina na muda mwingi huwa anakuwepo hapo ofisini kwao.

hivi kuna anaejua undani wa Easy TV? Ofisi yao kuu iko wp? Inamilikiwa na nani? Na makeke yangu yooote bado sijawahi kukutana na mtu anasema anafanya kazi ofisi zao hata kwa kupitia rafiki wa rafiki yake rafiki yangu...mweeee:hand:
 
hivi kuna anaejua undani wa Easy TV? Ofisi yao kuu iko wp? Inamilikiwa na nani? Na makeke yangu yooote bado sijawahi kukutana na mtu anasema anafanya kazi ofisi zao hata kwa kupitia rafiki wa rafiki yake rafiki yangu...mweeee:hand:

Ofisi zao zipo pale Moroko, jengo ilipo zhonghua garden. Mbona kwangu channel za Mengi zipo? Ila star tv ndo iliondolewa kitambo sana.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom