East African Federation (EAF) public Views

Ndugu Mkenda,

I see that you want those that believe "from the heart" to convince you. I believe, but not from the heart. I am not even sure that I have one. See how you like this anyway:

We are singly too small a market to attract much attention. The community, as a single market, is more attractive to investment. A market with 100 million consumers has a lot more negotiating clout than three disjoint markets with a third of the customers each.

The East African Tourism Market is enormous. It is beneficial for us to have a common policy on such things as pricing and environmental protection, than to compete among ourselves.

Within an East African Community, you, Mr. Mkenda, will have the whole of Nairobi, Dar and above all, Kampala, as your playground. That, I submit, bits having Kariakoo only as your home ground.

I do not know what you do for a living, but whatever it is, I am sure you will agree with me that it is beneficial to you to be able to do it not only in Tanzania, but within anywhere in East Africa.

Augustine Moshi
 
Kenya: Artur Brothers Arrested After Airport Gun Drama

The East African Standard (Nairobi)
June 10, 2006
Posted to the web June 9, 2006
Standard Reporter
Nairobi

Alleged Armenian brothers Artur Margaryan and Artur Sagarsyan drew guns and triggered a terror alert at the Nairobi's Jomo Kenyatta International Airport (JKIA) on Thursday night.

And police yesterday afternoon recovered eight guns and 100 rounds of ammunition in the compound of the brothers' residence in Nairobi's up-market Runda estate.

The same afternoon in a dramatic turn of events the men who recently addressed a news conference at the airport's VIP Lounge, were back at JKIA to face deportation.

The men who have previously swaggered into and out of the airport without restriction were locked in the Prohibited Immigrants room to await deportation.

That triggered fresh controversies for their acts were clearly of a criminal nature which should have seen them arraigned, but they were treated as if they had entered Kenya unlawfully.

That prompted the Leader of the Official Opposition, Mr Uhuru Kenyatta, to accuse the Government of covering-up the illegal acts of the Armenians.

The Liberal Democratic Party chairman, Mr David Musila, asked President Kibaki to tell Kenyans the true story of the Armenian. It emerged yesterday that the brothers had unrestricted access to Kenya's biggest airport given them by a senior Kenya Airport Authority (KAA) official without surrendering their guns.

Margaryan and Sagarsyan forced their way out of the airport with over 12 bags they yanked from the baggage's conveyor belt before they could be opened up for inspection.

Investigations by the Saturday Standard revealed that the passes for the brothers were issued on February 10 while the other three for their "aides" were issued on Thursday morning hours before they turned up at the airport to receive their "brother" and "sister" from Dubai.

The man and woman arrived with the bags with unidentified cargo and it was on their arrival that the airport drama began. Sagarsyan and Margaryan were allowed into the airport without screening, a privilege the KAA security booklet last revised in 2004 says is reserved for President and Cabinet members. The only other category of people exempted from this stringent rule is foreign envoys, and special groups who must be escorted to the plane's elevator by armed police.

When the police later opened one of the bags following a commando raid at their plush Runda home, they found several fake local, foreign, diplomatic and Government vehicle registration plates.

They also found black balaclavas, the kind of which the hooded policemen who raided the Standard and KTN offices donned. The bag was also stuffed with pistol holsters and camouflage military jackets.

In the compound were 11 cars, some bearing GK plates. The vehicles included a BMW, three Toyota Harriers and other luxurious saloon cars.

An official Criminal Investigation Department (CID) letter granting Margaryan the powers of a police officer was also found in the house.

The police team also seized three computers and videotapes, which insiders revealed were similar to those taken away by the police during the March 2 media raid on Standard Group offices.

The criminal acts by the Armenians are bound to lower the rating of Kenya's airport security. And Kenya will have to give a written explanation to the International Civil Aviation Authority within seven days for the acts of the foreigners were openly kid-gloved by security forces.

After hours of procrastination and a ping-pong game of conflicting orders, the police moved in.
 
It is frightening what some officials can do for a buck. I hope that they investigate thoroughly and prosecute all officials, however high, who might be implicated.

Augustine Moshi[/b]
 
Je Rwanda na Burundi ijiunge na East Africa Community ( EAC)?

Unasemaje??
--------------------------------------------------------------------------
Ngara wapinga Rwanda, Burundi kukaribishwa EAC

Chanzo kikuu ni vita, ukabila
Wasema watavuruga amani nchini

Na Manyerere Jackton, Ngara


WANANCHI katika Wilaya ya Ngara, mkoani Kagera, wanapinga nchi za Rwanda na Burundi kupewa uanachama katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Msimamo wa wananchi hao umefahamika kwenye mikutano iliyohutubiwa na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Diodorus Kamala, juzi.

Naibu waziri huyo yuko katika ziara ya kuitambulisha wizara, kueleza fursa zinazotokana na jumuiya hiyo; na kukusanya maoni mbalimbali ya wananchi, yakiwamo ya ama, Burundi na Rwanda ziruhusiwe kujiunga, au zisiruhusiwe.

Akiwa katika Kijiji cha Kabanga, wilayani Ngara ambako ni mpakani mwa Tanzania na Burundi, wananchi walitoa maoni yao kwa uwazi na kupinga kwa nguvu zote, Burundi na Rwanda kupewa uanachama kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Aliyeanza kutoa maoni yake ni Suleiman Minani, na akasema: Kujiunga kunahitaji muda, hawa wamekuwa katika mapigano kwa muda mrefu, wametuletea uhalifu, hasa ujambazi. Hapa Ngara ujambazi umeletwa na wakimbizi hawa.

Sisi Watanzania Kiswahili ndicho kitambulisho, Warundi na Wanyarwanda sasa wakizungumza Kiswahili, wanaonekana ni Watanzania.

Kwa nini serikali inachelewa kutoa vitambulisho kwa raia wake? alihoji.

Mwananchi huyo alitoa mfano kwa kusema wakati fulani alisafiri na Wanyarwanda kwenda Mwanza. walifika kwenye kizuizi, na akastaajabu kuona wakitoa kadi za uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na kuruhusiwa kuendelea na safari.

Mimi nilipita kwa kitambulisho cha gazeti, hatuna vitambulisho na viwango vya kuoleana ni vikubwa, kule (ngambo upande wa Burundi) tuna wajomba, mimi nashauri wasubiri kujiunga kwenye jumuiya, wakiruhusiwa sasa, usalama wetu utayumba, alisema.

Mwananchi Seleman Senduka, alisema: Kabla ya kuwakaribisha Rwanda na Burundi, kwanza tujue sisi (Kenya, Tanzania na Uganda), tumefaidika vipi na Jumuiya yetu.

Naye Jason Bahina, alisema: Sisi Watanzania hatuna matatizo ya ukabila na vita; wenzetu wanamalizana kwa kuuana. Wanahukumiana kwa kuangaliana pua.

Kabla ya kuwakaribisha, CCM ifanye kwanza kazi ya kisiasa, ijiridhishe kama kweli kujiunga kwao hakutaleta mgogoro. Kilichosambaratisha jumuiya ya kwanza ni tofauti za kisiasa, kwa hiyo kabla ya kuwakaribisha Rwanda na Burundi, lazima mataifa haya yaeleweke siasa zao.

Mwananchi mwingine, Joseph Balindie, yeye alisema wananchi wana wasiwasi mkubwa kuona Rwanda na Burundi, zinataka kujiunga kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Tuna wasiwasi, tabia za wenzetu-kuwashirikisha ni ngumu, wale wanauana, kuwashirikisha si rahisi, alisema.

Naye Gideon Ruvulahende (66), alisema: Kuungana ni jambo zuri, sasa kama Rwanda na Burundi nao wanataka kuungana na sisi, kwanza wapewe masharti ya kuumaliza ukabila wao.

Japhet Israel (62), alisema kwa umri wake huo, hajawahi kusikia Rwanda na Burundi kuna amani.

Alikiri kuwa wananchi katika nchi hizo ni ndugu zetu, na kwamba hata baadhi yao wanafanana na Watanzania, lakini kwa suala la kuwakaribisha kwenye jumuiya kwa sasa, haliafiki.

Tukiungana tutaharibu usalama wetu, kwanza wajirekebishe, wajue sote tu Waafrika, wajue Watutsi na Wahutu wote ni Waafrika-wajue weupe (Watutsi) na weusi (Wahutu), ni Waafrika, wakijua hivyo, sasa ndipo wakaribishwe kujiunga, alisema Israel.

Ofisa Uhamiaji Mkuu wa Kituo cha Kabanga, Harride Mwaipyana, alitumia fursa ya mkutano huo wa hadhara kutoa maoni yake.

Nipo hapa kuanzia mwaka 1999, nimesoma tabia za pande zote. Tusikurupukie kitu bila kukijua. Sisi Tanzania, Kenya na Uganda tunajuana tabia zetu.

Tabia za hawa wenzetu (Rwanda na Burundi) ni mbaya-hawana amani, wanabaguana, kuna vikao vya usiku vya kujadiliana. Wanakutana kwa mambo ya siri wakitumia viji-sherehe, wanaalikana.

Ukiwaingiza hawa, nchi itaharibika, wanapenda kutawala, wanajiona ni bora kuliko mtu yeyote duniani, tusiwakaribishe kabisa. Tuchukue muda mrefu sana.

Mheshimiwa Naibu Waziri naomba ulichukue hili kwa umuhimu wa kipekee.

Ujambazi wameleta wao, alisema Mwaipyana, akionekana dhahri kuchukizwa na Rwanda na Burundi kujadiliwa kujiunga kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Maoni kama hayo yametolewa na wananchi wengi katika maeneo mengi ambayo Dk. Kamala ameyazuru.

Chanzo: Tanzania Daima
 
Tujiulize hizo nchi zilizomo humo kwenye hiyo jumuiya zimenufaika vipi?

kabla hatujajua kama hawa jamaa wanaweza kutufaa au la basi ni vyema tuangalie kwanza waliomo na faida za jumuiya yenyewe!
 
Tafiti,
Tuangalie picha pana. Tatizo la nchi hizo ni "overpopulation."Aliwahi kusema Mwalimu Nyerere kuwa ukiwachukua Wahutu na Watusi uwatupe Mtwara, watasahau Uhutu na Utusi wao. Na kama hiyo inaweza kutokea utakuwa ni mchango mkubwa sana kwa ubinadamu na utulivu na amani. Tusikubali kujibanabana na hii mipaka waliyotuwekea wakoloni.
 
lakini pia tukumbuke jumuiya ya ulaya wazungu wameipigania kutokana na marketing opportunities na pia kujaza nafasi kutoka katika nchi za vishoka.

Sisi tuna kipi cha kumarket isijekuwa na sisi tunataka kuwawekea wakubwa soko pana, balozi Kibelloh, DEAN of East African missions hapa London then aliwahi kunukuliwa akisema katika Afrika Open Day 30th April 2004 aliwahi kunukuliwa akisema kuwa nchi hizi zikijiunga hata investors watakuja kwa wingi kwa vile watakuwa wanakuja katika soko la sio la watu 35m wa tz bali 90 milions east africans...

Mimi argument yangu ni kuwa tujiandae kwanza manake this time wenzetu kenya wametuacha sana katika mitandao ya kiuchumi na mitaji kwao sio issue, wao wana uwezo wa kuangalia opportunities katika bigger picture sisi hatuwezi kabisaaa bado biashara zetu ni vile vile, nikienda tanzania na kurejea baada ya mwaka mmoja unawakuta wengi wapo pale pale katika makazi na vituo vile vile no advance...sana sana watakutaka uwape wao advance kidogo wasukume biashara, unajiuliza benki hizi za hapa nyumbani hawazioni..

kuna dalili nzuri tuone hizi 500m 'za lowassa' zitatumikaje na vijana mikoani....
 
hawa majamaa ni wakora sana kama wakurya sasa wasomali, rwanda , Burudi na Uganda nadhani hawajawa na sifa za kuja EA Com lakini basi tu .Ni wakora sana hawa watu
 
Tafiti,
When will we be ready? Tayari Rwanda na Burundi wanatutegemea kwa bandari. Natofautiana na balozi Kibelloh. Tuungane kwa manufaa yetu wenyewe na si kwa sababu wawekezaji watamiminika. Wawekezaji si wakombozi. Usafirishaji wa bidhaa za Burundi kutoka bandari ya Dar utawapa ajira wabongo.

Na hayo malori yanayokwenda Burundi yanaweza kugundua kitu ambacho ni adimu Dar na kuanzisha biashara. Murangira, Wakurya tayari tunao Tanzania, kama ni wakora basi tumeganda nao. Tupanue upeo wa kuona kwa kuzingatia historia. Zanzibar leo kusingekuwa na mwungano ingekuwa haina tofauti na Comoro---kupinduana kila kukicha. Waacheni ndugu zetu waingie katika jumuiya
 
Ukweli ni kwamba tayari wabongo wenye kuona mbali wameshaona kuwa Kagame hana nia njema na sisi, yaani bongo, katika kikao kimoja cha serikali ilishakaririwa kuwa anajaribu kutafuta kila mbinu ya kutuchokoza ili tuingie naye Vitani, ndio maana labda atakapotoka kwenye power ndio tutaangalia kama na wao wajiunge nasi kwenye EAC!
 
Nchi za Afrika Mashariki bado hazijawa tayari kuwa Federation. Kilichopo ni kutafuta njia za kulaliana tu kiuchumi.

Wenye ndoto za Federal Government ya East Africa sasa ni wakati muafaka waachane na ndoto hizo. Tunachohitaji Tanzania ni maendeleo yetu na wala si miungano isiyokuwa na manufaa kwetu.

Hebu tuige nchi nyingine zilizofanya bila ya miungano - Japan, Korea Kusini na pia Singapore ambayo ilijitowa kwenye muungano wake na Malaysia na kuonyesha maajabu ya maendeleo.
 
Hofu ndogo ya kuwakaribisha hao jamaa ni kutimia kwa ndoto za Museveni za kurejesha the Hima empire (well,in a modern version,of course).

Hofu yangu kubwa kiasi ni kama ile ya kwenye hoja ya "Tafiti then Jadili".Mimi naiangalia kwa mtizamo wa ki-mtaani.Hivi suppose mtu anaamua kuoa.Then nadhani kwa wenye busara huwa hawakimbilii kuongeza watoto kabla hata hawajiimarisha katika ndoa hiyo.Wenyewe wanasema kuoa si kazi,kazi kumudu ndoa...na kuzaa si kazi kazi kutunza mtoto.Well,back to serious talk.Wakati hata hatujajua kama kweli hii EAC ina manufaa kwetu kuna haja gani tena ya kuongeza members (wadadisi wa mambo wanaiona EAC ya sasa kuwa imerudia makosa yaleyale yaliyoivunja 1977 ie kutanguliza political ambitions in front of common sense,yaani reality on the ground).

Hofu yangu kubwa zaidi ni hali halisi inayozikabili baadhi ya nchi wanachama wa EU baada ya kuzikaribisha baadhi ya nchi za Ulaya mashariki kujiunga na jumuiya hiyo.Watetezi wa mpanuko huo walikuwa wakidai kuwa miongoni mwa mafanikio itakuwa ni kukua kwa soko...Tayari,Wapolishi wameshawaonyesha Waingereza nini maana ya "ushirikiano".Matarajio ya awali kwamba pengine Wapolishi wangekuja in terms of makumi elfu yamegeuka kuwa malaki.

Warning:tulipowakaribisha kama wakimbizi,walianza kuwindana humohumo kwenye makambi na hatimaye kuwageuza wenyeji wao wajione kama wako kwenye uwanja wa vita.
 
Kwanza mimi niseme wazi kuwa ni Mbunge. Msimamo wangu nilikuweka wazi katika hotuba yangu Bungeni kuhusu na suala hili.

Burundi na Rwanda ziingie JAM mapema iwezekanavyo. Nchi hizi kuwa katika familia ya Afrika Mashariki itasaidia sana ku'stabilize' amani. Hii ndio nia kubwa. Amani katika nchi hizi itadumu iwapo nchi hizi zipo ndani ya Jumuiya. Itakuwa ni rahisi kwa Kenya, Uganda na Tanzania kufuatilia kwa karibu masuala ya Demokrasia na haki za binaadamu katika nchi hizi kama sehemu ya peer review.

Pili, kuna suala la kiuchumi. Nchi hizi zina watu. Watu wanatumia bidhaa mbalimbali. Bidhaa nyingi zinatoka Tanzania, Kenya na Uganda. Hivyo nchi ni soko la bidhaa zetu. Tukiingiza Rwanda na burundi katika JAM tunakuwa tumeongeza wateja milioni kumi na tano katika soko.

Kuna watu wanasema eti, kujiunga kwa nchi hizi kutaleta vita. Huu ni upuuzi. Hebu tuangalie, Uganda kuna vita ya LRA, je katika miaka hii ya JAM vita hii ya Kony imeingia Tanzania?

DRC ni mwananchama wa SADC, Tanzania ni mwanachama wa SADC, DRC walikuwa wakipigana na mpaka sasa kuna mapigano. Je, vita hii imeingia Tanzania au Afrika Kusini?

Burundi na Rwanda, kijiografia ni sehemu ya JAM. Kama tunakumbuka Historia, nchi hizi zilikuwa ni sehemu ya Wilaya 14 za Tanganyika (DeutchOstafrika). Hawa ni wenzetu, na waje!

Zitto Kabwe
 
Mlalahoi!
Hiyo warning yako inatisha kama ni kweli. Yaani hata kwenye kambi za ukimbizi Uhutu na Utusi viliendelea kutawala? Kama asemavyo Chifu Ihunyo, basi iko kazi
 
Hapana. Wanahitaji muda kujiandaa kutoka katika mfumo waliopo na kwa hizi nchi tatu za afrika mashariki nazo kuimarisha demokrasia.
 
Rwanda and Burundi should not join the EAC. They will bring their burdens to EA, wars, political stresses, population explosion, etc
 
Hivi ni kweli mpaka hivi sasa hatujui faida za EAC?? eti tusubiri tuone faida!! come on guys
 
Licha Ya Kukaribisha Burundi Na Rwanda Kujiunga Na Eac,mimi Napenda Kuziomba Hizo Nchi Ziungane Na Kuwa Nchi Moja Kama Mataifa Makubwa Yalivyofanya Kwani Maendeleo Yako Nadani Ya Bara Letu So Tukiungana Na Kuwa Kitu Kimoja Tutaweza Kuutokomeza Umaskini.

Ukiangalia Nchi Za Bara La Africa Ni Vipande Vidogo Vidogo Sana Katika Nchi Kama America Au Hata South Africa, Kwa Hiyo Tuungane Na Tuwe Na Raisi Mmoja Na Wafuasi Wake Kama Vile Senetors And Governors Kutoka Kila Nchi Shiriki.

I Know It Will Take Time But Finally Inawezekana Kwani Ni Plans Tuu Na Makubaliano.
Good Lucky.
 

Similar Discussions

22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom