Ear irrigation kwa njia ya sindano imeniletea hatari

Cathelin

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
2,071
3,992
Wakuu pole na mihangaiko.

Nasumbuliwaga na nta masikioni, ambapo nta ujirundika na kushindwa kutoka nje.

So nkawa naenda Kairuki pale Kuna madaktari wako vizuri Sana. Nilikuwa nasafishwa masikio yaani dakika tano washamaliza, Ila walikuwa wanatumia kakifaa utadhani unapuliziwa gesi sikioni yaani kifaa kinatoa uchafu wote na hakuna side effects unapata.

Sasa nilihamia mkoani kikazi sikio nta zikanisumbua tena, nikaenda hospital ya private na ni kubwa, basi walinisafisha sikio kwa kutumia bomba( syringe na maji) kweli walitoa uchafu.

Baada ya wiki nkaaza kupata maumivu ya mishipa/muscle zinazotoka kwenye sikio na kwenda kwenye ubongo, yaan hadi nerves za juu ya sikio kwenda kwenye brain zinauma, nadhani wakati wanaingiza maji, walitengua mishipa kwenye sikio, yaani ukiinama unaisi kizunguzungu, ukikimbia bado kichwa kinauma.

Sijui ntumie dawa gani kutibu hii mishipa inayoniuma, lakini pia nitumie dawa gani ili wax wasiwe wanaziba sikio Mara kwa Mara.

Msaada jamani.
 
kwanini unavichezea viungo vyako sensitive namna hiyo? yaani nta tu unakimbilia kuingizwa mabomba ya gesi na mabomba maji as if una masikio ya chuma?
 
Back
Top Bottom