EAC: Waarabu wa Pemba, wnajuana kwa vilemba

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
1. Tanzania-Wapinzani bado wanafukutwa na matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana uliowapa ushindi CCM. Wanadai uliandamwa na hujuma ikiwemo ya kuiba kwa kura. Na sasa, kuna fukuto la chaguzi za Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri. Rais John P.J. Magufuli wa Tanzania ndiye Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo.

2. Kenya-Chaguzi karibu zote zimekuwa zikigubikwa na ukabila, ukanda na ghasia za hapa na pale. Rais wao Uhuru Kenyatta alikuwepo.

3. Uganda-Rais Yoweri Museveni alibadili katiba kumruhusu kugombea tena. Anang'ang'ania madaraka tangu mwaka 1986.Amegombea tena mwaka huu na kushinda 'kibabe'. Ndiye Msuluhishi Mkuu wa mgogoro wa kisiasa wa Burundi. Museven ni jenerali wa jeshi la Uganda.

4. Rwanda-Rais Paul Kagame aliyeingia madarakani tangu mwaka 1995, amebadili katiba ili agombee tena na tena. Yuko madarakani kwa miaka zaidi ya 20. Demokrasia Rwanda,wakati wa uchaguzi, huwa 'demoghasia'. Kama alivyo Museven, Kagame ni jenerali wa jeshi la Rwanda.

5. Burundi-Rais Pierre Nkurunzinza amelazimisha kugombea kwa muhula wa tatu. Nchi yake sasa iko kwenye machafuko. Burundi inapita katika kipindi kigumu. Wakati wa uchaguzi, wapinzani walisusia lakini uchaguzi ukafanyika na Nkurunzinza kuapishwa. Hajali,anaendelea kuongoza.

6. Sudan Kusini-Rais Salva Kiir yuko kwenye mgogoro wa kivita na Makamu wake Riek Machar. Wasudan Kusini wako vitani. Vita ina rangi ya kikabila. Ni kati ya kabila la dinka la Rais Kiir na lile la nuer la Machar.

Katika sura hii, nani wa kumnyooshea kidole mwenzake? Hawa ni 'Waarabu wa Pemba, wanaojuana kwa vilemba'

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Back
Top Bottom