EAC- Tanzania Tunaona Mbali Wenzetu Wanapaswa Kujifunza

MIDFIELD

JF-Expert Member
May 27, 2013
1,944
701
Yapata miaka kadhaa sasa wakati wa awamu ya nne ya Mheshimiwa Jakaya shirikisho la Afrika Mashariki lilipatwa na bundi fulani ambaye alisababisha kamgogoro ka chinichini baina ya Tanzania na nchi tatu za shirikisho hili ambazo ni Kenya, Uganda na Rwanda.

Nchi hizi tatu ziliunda kaumoja ndani ya shirikisho, kakiitwa kwa kimombo COALITION OF THE WILLING, yaani muungano wa wenye utayari.

Haka kashirikisho ni kama kaliitenga nchi kama Tanzania na Burundi kwa kile kiliichoitwa eti Tanzania ni nchi kubwa lakini iliyolala (The Sleeping Giant).

Hii ilikuwa na maana Tanzania ni nchi inayochelewesha mchakato wa kukamilisha kuundwa kwa shirikisho hili. Hivyo waliamua wao kwenda mchakamchaka na kuiacha Tz ambayo kihistoria ndio mwanzilishi/muasisi wa hii EAC.

Kimsingi Tanzania sio kama ilikuwa inachelewesha mchakato, bali ilitaka tusiharakishe kuungana bila kuangalia kwa kina masuala nyeti kama ardhi na mengineyo ambayo baadaye yanaweza kutuletea shida ktk shirikisho letu. Pia ikumbukwe kwamba huko nyuma tulishakuwa na shirikisho hili likaja likavunjika kutokana na sababu kadhaa.

Hivyo basi ilipaswa kwenda kwa umakini mkubwa ili tusije tukarudia makosa yaliyolivunja shirikisho hili awali. Wenzetu walituona hatuna maana, na matokeo yake wakajiunga fastafasta, wananchi wa nchi zao inasemekana wakawa free/huru kuingia nchi nyingine bila kikwazo.

Sasa nini matokeo yake?
Leo hii Uganda na Rwaanda hawaivi chungu kimoja. Wamefungiana mipaka, wananchi hawavuki nchi moja kwenda nyingine na hadi uchumi na biashara baina ya nchi hizi vimeathirika. Sijajua Kenya inawasaidiaje hawa wenzake kwa sasa.

Lakini ninachota kusema ni kwamba, Tanzania tuliyajua haya ndo maana hatukutaka mchakamchaka. Kuunda jumuiya ni hatua na siyo suala la fumba na kufumbua.

Wenzetu wanapaswa kutambua sisi Tanzania hatukuwa wajinga kama wanavyofikiria. Bali tunaona mbalii, na wanapaswa kujifunza kutoka kwetu.

Nawasilisha
 
Ukiwasha kuwa na "initial velocity" kubwa hata kama utapata misukosuko ya hapa na pale bado utaweza kwenda mbali. Tanzania ilianzishwa kwa misingi imara ya kuijenga nchi, kwa hiyo haiwezi kutetereka na vitu vidogo vodogo.
 
HUKU EAC KUMEDORORA. ECOWAS WAMESHAFIKIA KUANZISHA SARAFU MOJA. MNAJITAPA TU BURE. NCHI IMEPATA UHURU MIAKA 60 SASA, BADO IPO KWENYE UMASKINI WA KUTUPWA.

CCM MTOKE BASI.
Unaelewa madhara ya sarafu moja hasa kwa hizi nchi zetu zenye kupika data
 
Ukiwasha kuwa na "initial velocity" kubwa hata kama utapata misukosuko ya hapa na pale bado utaweza kwenda mbali. Tanzania ilianzishwa kwa misingi imara ya kuijenga nchi, kwa hiyo haiwezi kutetereka na vitu vidogo vodogo.
Swadakta. Umenena kweli mkuu
 
HUKU EAC KUMEDORORA. ECOWAS WAMESHAFIKIA KUANZISHA SARAFU MOJA. MNAJITAPA TU BURE. NCHI IMEPATA UHURU MIAKA 60 SASA, BADO IPO KWENYE UMASKINI WA KUTUPWA.

CCM MTOKE BASI.

Ni kweli ECOWAS wameshajitahidi lakini bado nao pia wana changamoto za kutosha sana tu kwani bado kuna conflict kibao ndani ya nchi zao na ufisadi mwingi, mfano Nigeria. Sarafu moja bado hawajaanza kutumia bado ni katika process tu japo wamepiga hatua. Na hilo sio suala rahisi kihivyo. Angalia Ulaya kwa sasa imeanza kumeguka na wao ndo walikuwa watu wa kupigiwa mfano. Uingereza inayojitoa ilikuwa inatumia sarafu yake haikuungana na wenzake kwenye sarafu. Suala la umaskini naamini kwa sasa tunameanza kujielewa. Tunakoelekea ni kuzuri kwani kila mtanzania kwa sasa anajituma kufanya kazi ili kuimarisha uchumi wake binafsi lakini pia wa nchi kwa jumla. Cha maana hapa naamini sio chama, ni sisi watanzania kujitambua na kuacha longolongo na uvivu. Tufanye kazi kama ambavyo Amiri Jeshi Mkuu anatuhimiza. Naamini wote tukiimba wimbo mmoja kwa tune moja, tutatoboa tu. Tufanyeni kazi waungwana
 
Back
Top Bottom