Eac political integration: Tanzania tukikubali tumekwisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eac political integration: Tanzania tukikubali tumekwisha

Discussion in 'International Forum' started by Abdallah M. Nassor, Nov 21, 2011.

 1. Abdallah M. Nassor

  Abdallah M. Nassor Verified User

  #1
  Nov 21, 2011
  Joined: Mar 20, 2008
  Messages: 592
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 180
  Ni mara chache sana kwangu ku-Post humu kwani muda mwingi huwa ni mtazamaji tu. Lakini kwa hili nimeona ni wajibu wangu kuitetea nchi yangu ajili ya wajukuu zetu. Ni ukweli usiopingika kuwa idadi ya watu katika nchi za Rwanda, Burundi na Uganda ni kubwa ukilinganisha na ukubwa wa eneo la nchi hizo tofauti na Tanzania. Takwimu zinaonesha kuwa Rwanda inakaliwa na watu 326/km za mraba, Burundi ni watu 223/km za mraba , Uganda ni watu 114/km za mraba, na Tanzania ikiwa na wastani wa watu 36/km za mraba. Kwa takwimu hizo ni dhahiri kwamba majirani zetu wana tatizo la kutokuwa na ardhi ya kutosha na hivyo kuingia nchini kwa lengo la kujitafutia maisha katika kilimo na ufugaji. Waganda na Wanyarwanda wanalazimisha kwa kila aina ya mbinu waikalie Tanzania kwani hapa kuna ardhi ya bure bure. Watanzania tuwe macho, tukikubali tu, tumekwishaa
   
 2. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Nchi nyingine sio kwamba zina maeneo madogo lakini Tanzania ndiyo inaeneo kubwa kuliko watu. Tanzania ni kubwa kuliko Nigeria ambayo ina watu 140M!!. Watu si tatizo ndugu Tatizo kubwa ni wizara ya ardhi na usumbufu wa kutoa vibali vya viwanja kwa Watanzania. Kama watu wa mijini wanasumbuliwa hivyo je watu wa vijijini ni vipi?. Tatizo la ardhi likipatiwa ufumbuzi tusiwe na wasiwasi kwani watu kuja nchini si kitu kibaya. Hapa US watu wanakuja kila siku kwa miaka mingi lakini nchi haijai! na maendeleo yanaongezeka. Inabidi tufikirie tofauti kidogo kama tunataka kuendelea.

  Swali: Je ni kwanini US wanatoa vibali vya kuishi na hata uraia kwa yeyote hata sisi wabongo? sio kwasababu wanatupenda bali wanajua tunaleta maendeleo. Leo hii Mtu yeyote ni ruksa kununua nyumba hapa na kuweka pesa kwenye bank!
   
 3. only83

  only83 JF-Expert Member

  #3
  Nov 21, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Definitely true...The problem is,as you talk these critical issues in front of politicians who having big economic and political self interest and to few Tanzanians who are not aware about these issues they tend to ignore you..But in reality we need to make suspicious research on these issues before we decide to embark in this political federation....otherwise we will suffer a lot days to come!!
   
 4. IHOLOMELA

  IHOLOMELA JF-Expert Member

  #4
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 826
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 80
  mkuu, Tanzania na US ni sawa na Maini na Matembele. Sisi hatujawa tayari kihivyo kukaribisha wageni, hasa katika soko la ajira. Wewe sapoti ya US sababu wamekupa uraia wapate wa kuzibua sewage, tuachie tujadili Tz yetu.
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Nov 21, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  This is very myopic and full of fear mongering. We should face the EAC with confidence believeing that in unity there is strength.
   
 6. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #6
  Nov 21, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  No way papa...:lol:

  Hapa tulipofikia panatosha tusubiri tuone faida yake kwanza. Kwa sasa hakuna haja ya kun'gan'gania ku-fast-track further integration kama political federation na upuuzi mwingine, hizi nchi bado zina matatizo ya ndani mengi mno. Kama EU wenyewe pamoja na uhodari wao wa kufanya mambo bado pananuka ije kuwa EAC?
   
 7. IHOLOMELA

  IHOLOMELA JF-Expert Member

  #7
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 826
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 80
  Uko sahihi mkuu
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Nov 21, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Basi wahimize Wazanzibari nao wajitenge kwa sababu muungano hauna manufaa kwa utaifa wao.
   
 9. T

  Topical JF-Expert Member

  #9
  Nov 21, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mnaogopa bure..integration inakuja hiyo ndio realities..

  Wenye kutafuta fursa watapata na wenye kulala muendelee kulala
   
 10. T

  Topical JF-Expert Member

  #10
  Nov 21, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Siamini kama unahitaji muungano na waswahili
   
 11. D

  Dotowangu JF-Expert Member

  #11
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  tanzania ni kubwa mno..kuna maeneo mengi tu yamekaaa domant hayalimwi na wala hayafanyiwi uwekezaji wowote toka nchi hii ipate uhuru.. Mi sioni tatizo waje tu ili nchi hii iendelee.. Tanzania tumelala sana.. Kwa mfano huku ninakoishi tuna shida ya maji lakini wamekuja wachina wakaweka kambi yao kwa ajili ya kutengeneza barabara wamechimba visima vya maji na kwenye kambi yao hawana shida ya maji kama sisi tulio nje.. Kuna wasukuma huku wanafuga ng'ombe kuazia mamia ila wameshindwa kuuza hiyo mifugo na kuchimba mabwawa kwa ajili ya mifugo yao wanahangaika nayo kutwa nzima kutafuta maji...ukiwauliza eti wanasema msukuma hufuata maji... Na sio maji yamfuate msukuma..
   
Loading...