masha deno
Member
- Mar 2, 2013
- 64
- 17
Mungi,
..we dont need these ppl as much as u think.
..rejea jarida la New York Times ambalo limeeleza kuwa ktk nchi 45 duniani, Tanzania ni namba 7 kwa vivutio vya utalii. Uganda imeshika nambari 32, Kenya na Rwanda sikuziona kabisa.
..tunachopaswa kufanya ni kuimarisha VIWANJA VYA NDEGE, kujenga HOTELI nzuri zaidi, na kuimarisha MIUNDOMBINU inayoelekea ktk mbuga zetu za wanyama na vivutio vingine. pia tunapaswa kuongeza TRAINING kwa wafanyakazi ktk sekta ya utalii. Tu-train watumishi toka wale wa ubalozini wanaotoa visa, maofisa uhamiaji wanaopokea wageni ktk viwanja vya ndege, mpaka kwa mtu wa mwisho anayehudumia mtalii.
..zaidi tunapaswa kufungua UKANDA WA KUSINI, na KUSINI MAGHARIBI, kwa utalii. Kwa mfano, kuna mbuga kama Selous, Udzungwa,Ruaha, etc etc ambazo bado hazijulikani kama zile za Serengeti, Ngorongoro, na Manyara.
..EAC siyo muarubaini wa matatizo yetu wa-Tanzania. Mwanzoni tuliambiwa jumuiya itamaliza tatizo la ajira Tanzania, 10 yrs down the road tumegundua kwamba siyo kweli.
..WATANZANIA TUCHAPE KAZI. HAKUNA MJOMBA WALA JIRANI ATAKAYEKUJA KUTULETEA MAENDELEO.
cc Geza Ulole, Ngongo
Hahaha who is laughing now ?
Last edited by a moderator: