Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,444
- 7,801
Namsikia mwanajamvi mwenzetu EA Radio akiwa na Zembwela, mtangazaji anaibua hoja ya mitandao kutumika kudhalilisha watu na kadhalika, seduce me inasindikiza kusubiri mjadala. Nitawajuza majadiliano..
======
Zembwela anaanza kwa kusema yeye ni mmoja wa mashabiki wa wake kwa maana ni mmoja wa vijana ambao wanathubutu, wanapenda na wanafanya. Zembela anauliza, nini kinasukuma watu kutumia mitandao tofauti na madhumuni hasa ya kupashana habari, kuelimishana!
Maxence: Nakushukuru hasa kwa kuonyesha hasira zako kwa yanayotokea, hata siku za nyuma nilisema, mimi sidhani kama kutengeneza sheria, kukimbilia kuzileta na kuanza kuzitekeleza haraka itaokoa kile tunachokiona.
Tunachokiona mitandaoni ndio jamii ya watanzania, mtu anapokuwa nyuma ya keyboard anapata uhuru wa kujipambanua, yeye ni nani haswa. Kama JamiiForums, malengo yetu makuu ni matatu ambayo ni kukujuza kinachojiri kwa namna yoyote, kukuunganisha na watu na kukuburudisha.
Wanaouza visu nadhani wanauza kwa ajili ya kukatia nyama lakini wapo wanaotumia kukatia shingo za watu, unaweza kuiona fimbo ukadhani kwa ajili ya kuulia nyoka lakini mtu akatumia kumpiga binadamu na kumuua.
Pia hii inatumika kwenye mitandao, imetengenezwa kwa nia njema ila watumiaji wanaweza wakatumia tofauti na tunavyotarajia, nilienda mikoani nikakutana na mteja wetu ambae anaitumia JamiiForums tofauti hata na sisi tulivyotarajia, hatukuwahi kufikiria watu wanatumia JamiiForums kwa mtindo huo.
Kwa hio najua hata wengine wanapoingia Facebook, kuna watu wanaingia kupunguzia stress zao, kuna wengine wanaingia kuwasiliana na rafiki zao, wengine wanaingia kwa ajili ya kuibia watu, wengine kwa ajili ya kuarifu watu na wengine hawajui nini kimewapeleka wakajikuta wamedumbukia mle.
Dhamira ya mtu ndio inayopelekea yanayotokea yatokee.
Hata ukitengeneza sheria nzuri kiasi gani lakini tuelewe lazima tuanzie kwenye misingi, tunakuja na vitu vinatokea vinaisha. Bahati mbaya tangu tumeingia kwenye utandawazi, hatuwezi kukwepa kinachotokea.
Tuna kizazi ambacho mtoto anamaliza darasa la saba, mtoto anapewa simu ina kila kitu, haina restriction ya aina yoyote. Mwaka 2009 mapinduzi yaliingia Tanzania, tulipata mkongo wa Taifa na mtandao ukawa available kwa watu wengi.
Nchi yetu ilifanya vyema kukubali utandawazi, wengi wanafanya vyema sema kuna watu wachache lakini wanaweza kupaza sauti.
Zaidi soma=Maxence Melo: Watanzania wengi waoga pia kuna taasisi zinaogopwa hazipewi changamoto mtandaoni