Zanzibar 2020 DW: Jussa anapendekeza kuundwe Serikali ya Umoja wa Kitaifa Visiwani Zanzibar

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,062
103,264
Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha ACT Wazalendo Ismail Jussa Ladhu anaeuguza majeraha baada ya kupigwa walipokuwa wanafanya maandamano Visiwani Zanzibar katika Maandamano hayo ya tarehe 29 mwezi wa Oktoba yalikuwa ya amani ila maafisa wa usalama waliwavamia na kuwajeruhi baadhi ya viongozi wa upinzani.

Mwandishi wa DW, Thelma Mwadzaya amezungumza Kinagaubaga na Jussa kuhusu siasa za visiwani Zanzibar na Jussa anapendekeza kuundwe serikali ya umoja wa kitaifa visiwani Zanzibar.

My Take
Kuunda serikali na CCM hii hii au?

Update:
Mahojiano ya Jussa na DW (Sauti)
 
nikiona maneno ya hivi tena kutoka kwa wanasiasa wa upinzani nachoka kabisaa, sijui kama aliziona maiti za wale vijana wa Zanzibar waliouwa kikatili kabisa tare 27, 28 na 29 Oktoba
We uliziona, kwa hiyo
 
CCM sikilizeni habari vizuri ,mnaweza kudanganyana nyinyi kwa nyinyi,wenyewe kwa wenyewe ,na mkaaminiana ,leo sio aibu wala ajabu kiongozi anaetokana na CCM kuapa kwa jina la Mwenyezi Mungu ilihali anazungumza na kusema uongo.

Kamsikilize tena Jusa.

CCM imewafanya mpaka mapadri na mashehe hawamuogopi Mwenyezi Mungu,wamekuwa wanafiki mchana kweupe.
 
#Ni yeye Jussa Ladhu
#Ni yeye Zito Kabwe.
ACT Zanzibar wana jambo lao la serikali ya umoja wa kitaifa.
 
Kwanini hamuendi mahakamani kutafuta haki Kama mmeibiwa...mkiambiwa pelekeni ushahidi hata wa karatasi moja hamna...Sasa mnacholilia nin
Kwa katiba iliyopo haitoi mwanya huo wa kwenda mahakamani matokeo ya Urais yakishatangazwa
 
Maalim Seif alishaongea na Magufuli wakaelewana kipindi kile Maalim alivyoenda ikulu.
 
Hivi kweli Jussa amesema na kushauri haya? Kama kweli kasema basi leo ndio mie nahakikisha kweli wanasiasa woooooote wa Tanzania wanaweka mahitaji yao mbele na wanawatumia wananchi kufikia malengo yao tu!

Hivi Jussa amesahau ule msemo wa unakula na kipofu lakini humshiki mkono? Kuna manufaa gani yatakayofikiwa kwa kuwa na serikali ya umoja wa kimataifa Zanzibar? Si tuliwahi kuwa nayo huko nyuma? Nini kilipatikana na nini kilibadilika? Hakuna kilichobadilika punda alikuwa yule yule lilibadilika ni soji tu!

Siamini kiongozi kama Jussa ambae mwenyewe amepewa kichapo cha mbwa, anataka watu waliopewa vichapo vya mbwa na kujikuta na ulemavu wa milele, watu waliopoteza maisha yao, mali zao na nguvu zao, watu waliopoteza ndugu zao, wazee wao na watoto wao washau yote hayo na wakubali Seif sharif na viongozi wenzake wapewe nyadhifa katika serikali ya umoja wa kitaifa. Siamini Jussa anataka Wazanzibari wa ACT baada ya yote waliyoyafanya na maumivu yote waliyoyapata kwa sababu ya kuunga mkono chama cha ACT, Jussa yuko tayari kukaa meza moja na CCM. CCM hii hii ambayo iliidhinisha na kufumbia macho vipigo vya wanachama wa CUF.

To be honest hata sijui kwa nini nashangaa, ACT inaongozwa na Seif Sharif ambae ni mahiri sana katika kuwaendea kinyume wenzake kwa manufaa yake binafsi. Aliwaendea kinyume akina Aboud Jumbe na wenzake pale viongozi wa serikali ya Zanzibar (akiwemo Seif Sharif) walipokwenda kwa Nyerere kutaka Tanzania iwe na serikali tatu.

Sote tunajua aliwaendea kinyume mara tu alipoahidiwa na Nyerere kuwa atamtayarisha kuwa Rais wa zanzibar siku za mbeleni. Seif huyu huyu akaamua kuwaendea kinyume CCM baada ya kuona kuwa ahadi aliopewa na Nyerere haikuwa ya kweli na akaamua kuleta matata ndani ya chama na hatimae kufukuzwa CCM mwaka 1987.

Seif huyu huyu aliwaendea kinyume wazanzibari wenzake mwaka 2010 akiwa kiongozi wa CUF pale alipokubali kuingia katika serikali ya mseto na CCM ilhali wanachama wake walijitoa mhanga na kuhakikisha kuwa anashinda uchaguzi na alishinda. Alisahau kuwa watu wamepigwa, wamepoteza mali zao na wengine kuuliwa kwa sababu tu ya kutaka CUF ishinde, lakini alipoonyeshwa fupa tu, Seif alilirukia na kuchukua cheo cha chief of minister of zanzibar.

Na sasa anataka kufanya yale yale tena!!!!!!!!!
 
Kwanini hamuendi mahakamani kutafuta haki Kama mmeibiwa...mkiambiwa pelekeni ushahidi hata wa karatasi moja hamna...Sasa mnacholilia nini

Mahakama gani hiyo? Mahakama ya Tanzania ni CCM, majaji ni CCM, wakili ni CCM, polisi ni CCM unamshitaki CCM na unategemea nini kitachotokea?
 
Serikali ya umoja wa Kitaifa na walioiba uchaguzi?

Kama wapinzani huko Zanzibar wana akili za kuku namna hii basi CCM iendelee kuwatandika tu maana hawana akili!
Quote by Niccolò Machiavelli: “Keep your friends close, keep your enemies closer.”
Who is Niccolò Machiavelli?
Niccolò di Bernardo dei Machiavelli was an Italian Renaissance diplomat, philosopher and writer, best known for The Prince, written in 1513. He has often been called the father of modern political philosophy and political science.
 
Back
Top Bottom