nokwenumuya
JF-Expert Member
- Jun 29, 2019
- 810
- 2,851
- Thread starter
- #61
Hii ni report ya official search ya hii kampuni.Soma hapa. DV International imesajiliwa 1998 Ufaransa. Wewe ushahidi huna kuthibitisha tuhuma zako dhidi ya huyo Mzungu zaidi ya kiherere. Onyesha wapi Azam Media wameilipa hiyo kampuni $5 million?
Toute la donnée des sociétés | SocieteInfo.com
societeinfo.com
1. Inaonyesha wamesajiriwa 2014, sio 1998 kama walivyokutuma uwatetee.
2. Wameulizwa ni branch? Jibu lako hapo ni NO, maana yake sio tawi la kampuni yeyote.
3. Kazi walizosajiriwa kufanya hakuna hata moja inayowahusisha na kazi za Broadcasting au Media, hizi ni professionals services, sio kila kima anafanya.
Na zaidi hawana license, ofisi wala haitambuliki na mamlaka za kodi UAE.
Kumbuka leo unaweza kwenda Brela ukasajiri kampuni. Ila ili upewe license kwanza lazima usajiri TIN, ili utambulike kama mlipa kodi, na lazima upeleke mkataba wa pango wajue address yako.
Ukishapata TIN ndio sasa unaweza kwenda kuomba leseni kwa mamlaka husika kulingana na aina ya biashara.
Kama ni level za Halmashauri utapata leseni Class B, kama kitaifa unapata leseni toka Brela kwa niaba ya Wizara ya Viwanda na Biashara.
Na kama ni professional service au business mfano supply ya Broadcasting Equipment basi lazima on top of leseni Class A ya Brela lazima upate leseni ya TCRA.
Hivyo hivyo katika professionals zingine.
Hivyo unajitahidi sana kuwatetea, unfortunately unakula pesa zao bure.
Na uzuri pia unaweza kwenda mwenyewe kwenye website ya Wizara ya Economy UAE na ukafanya official search kuhusu kampuni hiyo na jinsi inavyofanya kazi zake.