DVI: Kampuni hewa inayotumia jina la Azam Media na kuchota mabilioni ZBC kinyume cha sheria

nokwenumuya

JF-Expert Member
Jun 29, 2019
810
2,851
DVI: KAMPUNI HEWA INAYOJIPATIA MABILIONI AZAM MEDIA, IMETUMIA JINA LA AZAM MEDIA NA KUCHOTA MABILIONI ZBC KINYUME CHA SHERIA
  • Ni kampuni ya mfukoni iliyosajiri jina DUBAI, UAE. Inamilikiwa na Mfaransa Gael Lancrenon.
  • Hana Nyaraka halali wala ofisi Dubai, anatumia anuani ya Kampuni ya Ushauri wa kufungua makampuni kama anuani ya ofisi yake.
  • Mnyetishaji wangu akijifanya ni mteja toka Uganda, wakachati akiwa Dubai, akashindwa kumwambia ofisi ilipo ili aitembelee, Whatsaaap chati iko hapo utaisoma.
  • Tetesi ni kuwa mfaransa huyo anashirikiana na Broadcast Manager wa Azam Media kujipatia kazi, wakati hana sifa.
  • Yeye anasema kampuni yake imefanya kazi mbili Azam Media, zenye thamani ya 5,000,000 US Dollar (Zaidi ya bilioni 11 za Kitanzania)
  • Anatumia mitambo na ofisi za AZAM MEDIA kuyaaminisha makampuni mengine kuwa ana uwezo na kampuni yake ni halali huko DUBAI.
  • Tayari ameshajiingiza katika Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) na kufanya kazi huku akiwa hana sifa, huku akijinasibu ndie amefanya Installation ya mifumo mingi ya AZAM MEDIA, na kuwa yeye ndio hutoa Msaada wa Kiufundi (Technical Support).
  • Usajiri wa Kampuni yake ambayo haina Leseni, ofisi, wala haitambuliki na mamlaka za kodi za Dubai hauhusiani na kazi za Media wala Broadcasting.
  • Tumemfuatilia hadi anapodai ana ofisi na tumekuta hana, anaendesha biashara kitapeli.
  • TAKUKURU ichunguze kampuni hii hewa inapataje kazi ZBC? Waangalie bei za kazi alizowahi kufanya, na achunguzwe ilikuwaje akawa anapewa kazi kama Single Source wakati hana sifa wala kampuni yake haifanyi kazi kwa taratibu zinazotakiwa?

UTANGULIZI
DV International, ni jina la kampuni hewa au tuseme ya kitapeli ambayo imejiingiza hapa nchini na tayari kuna baadhi ya kazi wanasema wamezifanya Azam Media, na Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC).

Mmiliki wake anayeonekana mbele ni Gael Lancrenon, mfaransa. Anasema ofisi yake iko – Ras Al Khaimah, 1401 Aspect Tower – Business Bay, P.0.Box 181921, DUBAI, UNITED ARAB EMIRATES. Baada ya kufuatilia katika anuani hiyo tumekuta hiyo ni ofisi ya kampuni ya ALLIANCE BUSSINESS COUNCIL LIMITED, kampuni ambayo inajihusisha na usajiri wa makampuni na utafutiaji wa Leseni wa makampuni huko DUBAI. Hivyo hana ofisi Dubai, wala hana compliance Zaidi ya Certificate of Incorporation.

Mhusika wa kampuni hii inaonekana ana ushirikiano mkubwa na Broadcast Manager wa AZAM MEDIA, ajulikanaye kwa jina la SIVAJITH SADASIVAN. Ambae ndie amemleta AZAM MEDIA, na kuuhakikishia uongozi wa AZAM kuwa DV International ni kampuni kubwa Dubai, na kuwa ni tawi la kampuni ya Digital Video International ya Ufaransa, japo katika usajiri wao DUBAI kama nilivyoscreenshort taarifa zake za usajiri wao sio tawi la kampuni yoyote.

Gael anatumia namba zifuatazo; +33614171529 (Namba ya Ufaransa na ndio huitumia kwa mawasiliano haswa Whatsaap), +971501048897 (UAE), na akija Tanzania huwa anatumia +255754318051 kufanya mawasiliano akiwa nchini.

MAHUSIANO YAKE NA AZAM MEDIA
Anajinasibu kuwa kampuni yake hiyo ndio imetengeneza mifumo ya Azam TV na kuwa yeye ndio anaisimamia, anasema amefanya kazi na Azam zenye thamani ya Zaidi ya Dola milioni tano (5,000,000/- USD).

Ana uhusiano wa karibu na Broadcast Manager wa AZAM MEDIA, ajulikanaye kwa jina la SIVAJITH SADASIVAN, ambaye ndie anajua alimtoa wapi na kumuingiza nchini na kuwezesha yeye kupata kazi. Kwa namna yeyote ni mshirika wake katika upigaji.

Zaidi anatumia ofisi za AZAM MEDIA kuwaaminisha watu wengine, zikiwemo taasisi za serikali kuwa yeye ndio amefanya AZAM MEDIA kuwa hapo ilipo, na ili kuwaaminisha huwaambia watu waende AZAM MEDIA na anawaonyesha mitambo ya AZAM ili wamuamini na kumpa kazi.

Mtu wetu alijifanya ni Mteja toka Serikali ya Uganda, akafanya nae mazungumzo kwa njia ya Whatsaap na wakakubaliana aje Nchini wakutane katika ofisi za AZAM MEDIA, yaani kiufupi anatumia ofisi za AZAM MEDIA kufanikisha utapeli wake.

AZAM MEDIA ni kampuni kubwa, ifanye uchunguzi ili kubaini namna mtu huyu anavyoitumia vibaya kampuni yao na kuifanya ofisi hiyo kijiwe chake kila anapokuja nchini.

NAMNA ALIVYOJIPENYEZA ZANZIBAR BROADCASTING CORPORATION (ZBC)
DV international kwa mujibu wa mtoa taarifa wetu amefanya kazi kadhaa hapo ZBC, kwanza hizo kazi kazifanya katika mazingira yasiofuata sheria ya manunuzi Zanzibar. Hizo kazi alikuwa anapewa kama Single Source wakati hana sifa hizo.

Mamlaka za kuchunguza rushwa zifuatilie namna hawa watu walipeana kazi bila ya kutangaza Tender, na Zaidi waangalie bei ambayo alitolea huduma hizo katika mazingira hayo.

Ana watu anaoshirikiana nao toka AZAM MEDIA, waliomshika mkono na kumpeleka ZBC. Na kuna watendaji wasio waaminifu ndani ya ZBC wanaoshirikiana nae katika kufanya miradi hewa ya mabilioni ZBC na kujipatia pesa nyingi isivyo halali.

Na kwa kuwa huyu Gael sio mtu wa Broadcasting basi kuna watu wanaomtumia kufanya deal chafu na kisha wanagawana pesa, ndio maana hata akifanya kazi za mabilioni bado hawezi kukodi hata fremu aonyeshe ndio ofisi maana baada ya dili hugawana pesa na kusubiri dili jingine la kutengenezea pesa.

NB: NIMEWEKA CHAT YAKE NA MTU ALIYEJIFANYA ANATOKA UGANDA, PIA OFFICIAL SEARCH YA JINA LAKE LA KAMPUNI INAYOONYESHA KAZI ALIZOSAJIRIWA KUFANYA.

DVI REG. DETAILS.png


GAEL.jpg
 

Attachments

  • WHATSAAP CHAT WITH GAEL-DVI.pdf
    517.4 KB · Views: 38
Kama anapata pesa na hao AZAM na ZBC wanaridhika na wanachohudumiwa sioni shida.

Kama ni masuala ya kuwa na ofisi nk ni masuala ya waliopewa hizo kazi na wanalipwa pesa kufanya kazi hizo,kwa hiyo wafanye wajiridhishe.(taasisi za serikali)

Mwavheni mfaransa wa watu awapige pesa wateja wake.
 
Kama anapata pesa na hao AZAM na ZBC wanaridhika na wanachohudumiwa sioni shida.

Kama ni masuala ya kuwa na ofisi nk ni masuala ya waliopewa hizo kazi na wanalipwa pesa kufanya kazi hizo,kwa hiyo wafanye wajiridhishe.(taasisi za serikali)

Mwavheni mfaransa wa watu awapige pesa wateja wake.
zabuni za serikali zinapatikana kwa utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria. Mtu pekee serikali inayoruhusu awe Single Sourced ni Manufacturers tu.
 
Ni wivu tu,mtu alipwe mabilioni yote hayo ashindwe kulipia pango la ofisi dubai kweli,lingine kazi inafanyika haifanyiki,kazi za IT na telecom haziitaji kuwa na lijiofisi kuuubwa ni akili tu na watu basi
Ndio hali ilivyo, na kazi imefanywa vilivyo. Ni kweli hana ofisi, nafirikiri angalia hata chat ya whatsaap alipoombwa kutembelea ofisi yake akasema atafanya organisation. kwani umesahau hata RICHMOND kamati ya Bunge ilienda kutafuta ofisi zake hadi USA na wakakuta hiyo kampuni haipo huko?

Wapigaji wetu kwa kushirikiana na wageni wanaweza fanya lolote. Au la basi tukuombe utembelee Ubalozi wa UAE hapa uwaulizie kuhusu hii kampuni kisha utupe mrejesho wako. Research inapingwa kwa Research.
 
Kama anapata pesa na hao AZAM na ZBC wanaridhika na wanachohudumiwa sioni shida. Kama ni masuala ya kuwa na ofisi nk ni masuala ya waliopewa hizo kazi na wanalipwa pesa kufanya kazi hizo,kwa hiyo wafanye wajiridhishe.(taasisi za serikali)
Mwavheni mfaransa wa watu awapige pesa wateja wake.
Apakuwe pesa kabisa
 
ndio hali ilivyo, na kazi imefanywa vilivyo. Ni kweli hana ofisi, nafirikiri angalia hata chat ya whatsaap alipoombwa kutembelea ofisi yake akasema atafanya organisation. kwani umesahau hata RICHMOND kamati ya Bunge ilienda kutafuta ofisi zake hadi USA na wakakuta hiyo kampuni haipo huko?

wapigaji wetu kwa kushirikiana na wageni wanaweza fanya lolote. Au la basi tukuombe utembelee Ubalozi wa UAE hapa uwaulizie kuhusu hii kampuni kisha utupe mrejesho wako. Research inapingwa kwa Research.
Mkuu hiyo michango ni ya kubwa ndiyo maana inakuwa vigumu hata kusubiri wafungue office watu wanajua hakuna kitu kitakuja mbele yao.
 
Hili nalo linawezekana kuwepo, kama Rais alihudhuria utiaji saini wa mradi wa bandarini ambao juzi aligundua ni dili la wajanja, hata hao ZBC sioni kama wanaweza kukwepa kuingizwa chaka na wajanja, ila jambo la kushangaza inaonekana hao jamaa licha ya kutokuwa na ofisi lakini bado wanatoa huduma nzuri sababu sijaona popote ZBC wakilalamikia huduma wanazopewa.
 
Hili nalo linawezekana kuwepo, kama Rais alihudhuria utiaji saini wa mradi wa bandarini ambao juzi aligundua ni dili la wajanja, hata hao ZBC sioni kama wanaweza kukwepa kuingizwa chaka na wajanja, ila jambo la kushangaza inaonekana hao jamaa licha ya kutokuwa na ofisi lakini bado wanatoa huduma sababu sijaona popote ZBC wakilalamikia huduma wanazopewa.
Hawawezi kulalamika hata kama huduma sio nzuri sababu watumiaji wa huduma pia huwa ni sehemu ya wanufaika.

Lakini jambo la muhimu katika sheria za manunuzi ya umma ni kufuata taratibu, kuanzia utangazwaji hadi mwisho kuwa awarded.

Sasa kampuni inapata kazi kubwa bila kupitia tender, zaidi ni kampuni isiyo na sifa. Na uzuri nchi husika ina ubalozi wake hapa na watendaji wetu wa serikali hawaoni umuhimu hata wa kuhakiki uwepo wa hiyo kampuni, na sababu kubwa huwa wako kwenye mgao.
 
Back
Top Bottom