Dvd za hayati munga tehenan wa gazeti la jitambue zinauzwa

Kitomai

JF-Expert Member
May 21, 2009
1,060
281
DVD zilizorekodiwa na Muasisi wa Elimu ya Utambuzi Tanzania, Munga Tehenan, zinapatikana katika ofisi ya FAJI iliyopo katika ofisi ya Rombo Kimara,

Majina ya DVD zinazouzwa ni:Wewe ni nani?, Kijiamini na kutojiamini, Upendo na uhusiano, na Maswali na Majibu, Bei ni tshs 10,000 kwa kila moja, vitini vinavyoendana na mikanda hiyo vinapatikana kwa bei ya shs 500.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na 0763 627003 au 0715 627003, 0682 974 397 au 0712 458656.

Wote mnakaribishwa.
 
Jamani huyu jamaa alikufa lini?? nilikua namfuatilia kwa karibu sana na kipindi chake cha TBC then kikatoweka ghafla!!! R.I.P munga
 
kwa kweli nimeshtushwa na kusikita, sikujua kama huyu jamaa alikwishaitwa na muumba....
 
Huyu jamaa alikuwa na elimu na uelewa wa saiokolijia nilikuwa sikosi kununua gazeti lake la jitambue na kusikiliza kipindi chake TBC enzi hizo. Hizo CD nitazitafuta aksante sana
 
msiba wa huyu jamaa sitausahau mpaka naondoka hapa duniani
RIP munga ..tutanunua
 
Mbona mnaongea kwa kifupi fupi tu, hebu wekeni mada wazi nasie wengine tuliopo mbali na home tuelewe
 
Hivi au mie kiswahili F hayati si ni neno la mtu aliyekufa muda kidogo au inakuwaje jamani?TBC nadhani imeanzishwa miaka ya 90 hivi na kabla ya hapo ilikuwa inaitwa TVT...sasa bachi kawa hayati huyu tena? nikosolewe kama sielewi maana ya hayati jamani.
 
Kiswahili wengi naona kinatusumbua! Hasa ss ambao lugha ya wanza ni "kabila" teh teh!
Nijuavyo mm, neno "hayati" linatumika kwa mtu aliyekuwa na umaarufu mpana kiasi, pia mwenye heshima kubwa. eg. Hayati JKN, Hayati MJ, Hayati B.Marley, kama mm siku nikifa nitakumbukwa kama Hayati Amoeba.
 
DVD zilizorekodiwa na Muasisi wa Elimu ya Utambuzi Tanzania, Munga Tehenan, zinapatikana katika ofisi ya FAJI iliyopo katika ofisi ya Rombo Kimara,

Majina ya DVD zinazouzwa ni:Wewe ni nani?, Kijiamini na kutojiamini, Upendo na uhusiano, na Maswali na Majibu, Bei ni tshs 10,000 kwa kila moja, vitini vinavyoendana na mikanda hiyo vinapatikana kwa bei ya shs 500.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na 0763 627003 au 0715 627003, 0682 974 397 au 0712 458656.

Wote mnakaribishwa.
Mkuu izo dvd zipo mpaka sasa?
 
Hivi au mie kiswahili F hayati si ni neno la mtu aliyekufa muda kidogo au inakuwaje jamani?TBC nadhani imeanzishwa miaka ya 90 hivi na kabla ya hapo ilikuwa inaitwa TVT...sasa bachi kawa hayati huyu tena? nikosolewe kama sielewi maana ya hayati jamani.
Hayati na Marehemu ni maneno yanayotumiwa na Binadamu kujipa umaarufu baada ya kufariki wakithani kwamba huo waendako wanaenda na heshima walizokuwa nazo duniani. Thubutu, ubaguzi na thulumati zako zote unaziacha huku duniani, huko baada ya nguo unazoondoka nazo kuoza, unaenda kuwa uchi kama ulivyokuja. Eti Hayati = Mfu aliyekuwa na Heshima Dunia enzi za uhai wak; na Marehemu = Mfu aliyekuwa hana heshima duniani enzi za uhai wake.
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom