DVD ya FMES =FAIL? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DVD ya FMES =FAIL?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Game Theory, Jun 6, 2008.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  ES alituahidi DVD yapata wiki mbiliz zilizopita...half way through huyu mzaramo akatuambia ohhh nitaiweka kwenye YOUTUBE kisha akabadilsha nyimbo kuwa atampa MKJJ aiweke kwenye KLH news...

  can we confirm kuwa ES naye ni katika JF fail brigade?

  [​IMG]
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Jun 6, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Tuliza ball.. hivi mnafikiri kuna watu wameajiriwa kukaa na kukopy na kurusha DVDs... ni vizuri tuulizane kiungwana. Kwani kuna mwajiriwa wa JF au KLH News hapa... Hii sense ya entitlement inatufanya tuonekane kama liberal democrats.. Badala ya kuulizana kiungwana au hata kwa PM kweli mnamuanzishia mtu mada...
   
 3. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mimi naomba mmpatie muda wa kuiandaa jamani, uzuri ni kuwa kesha ahidi, huwezi jua bana, labda mambo ya teknolojia ya jinsi ya kututundikia yanaweza kuwa yanamzingua. As long as anayo, basi kuna siku ataileta au kumpatia mtu ailete hapa jamvini, tusianze kum-label ili hali bado yuko nasi hapa na bado hajatamka yaliyomsibu kuhusiana na hili....

  SteveD.
   
 4. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mwanakijiji,

  Tatizo ahadi ni deni, na "Word is Bond"
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Jun 6, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  sasa si unamuuliza mtoa ahadi.. ndio mtu aje na dhihaka.. na ahadi zinavunjwa ndio ulimwengu wa halisia ulivyo.. and the law of entropy applies pia hapa... lakini ahadi haijavunjwa inawezekena imechelewesha au mtu katingwa au vitu ishirini elfu.. kwanini mtu asimuulize kwenye PM kumkumbisha ahadi hiyo? Hivi anajuaje kama bwana FMES hali yake ni nzuri, familia ni nzuri, kazini mambo mswano kiasi cha kuwa comfortable enough kuanza kutuma hizo DVDs. Mimi niliambiwa na mtu aliyempatia hizo DVD tangu mwanzo.. na waliniambia wataniunguzia.. guess what.? Sikuanzisha mada kusuggest kuwa wamefail kwa vile hazijaja when I thought they should have.. hallo?
   
 6. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Umegundua kwamba Mtanzania ukimwahidi kitu halafu usipotimiza hata hajali?

  Naweza kumwambia rafiki yangu, "e bwana samahani jana nilishindwa kukupigia kama nilivyoahidi..." halafu kabla hujamaliza kumwambia kwa nini ulishindwa anakukatisha, "...no no no, ni sawa tu, najua utakuwa ulitingwa..."

  NO, hujuia kama nilitingwa, ngoja nikueleze kwa nini nilishindwa, huwezi kutitetea kwa kushindwa kutimiza ahadi yangu bila kujua ni kwa nini nilishindwa...

  LOL!
   
 7. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #7
  Jun 6, 2008
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  nafikiri pia ni vizuri kumuuliza JK kiungwana na sio kumuanzishia mada/thread ! lol mtumieni barua pepe au barua...mhm!
   
 8. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #8
  Jun 6, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kuhani, je utaondoa vipi ile adha ya kumbatiza mtu jina pale atakapojitokeza na kukamilisha ahadi yake, isitoshe ahadi ya kujitolea?!
   
 9. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #9
  Jun 6, 2008
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  ahadi ya aina nyingine ni ipi kama sio kujitolea ??
   
 10. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #10
  Jun 6, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Yani Mwanakijiji, nilikuwa naandika posti yangu ya hapo juu wakati wewe unatuma hii ya kwako. Halafu umesema yale yale ya kutingwa niliyo kuwa naandika wakati wewe unaposti! LOL!

  Ha haa laaa!

  Kutingwa haku justify kutotimiza ahadi na kunyamaza kimya. Inabidi ufahamishe uliowaahidi kwamba utashindwa kutimiza ahadi, kama ambavyo "ukitingwa" na ugonjwa unamfahamisha bosi kwamba siwezi kuja kazini kama nilivyoahadi kufanya kila asubuhi.

  Huyu ambae unasema hatujui kama ametingwa tumawona hapa akishiriki mijadala kila siku tokea ahadi itolewe!
   
 11. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #11
  Jun 6, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Jina gani?

  Kwamba sio mtunza ahadi?

  Ukiahidi kujitolea kuja kunitembelea Jumanne halafu usije, tukakutana Jumatano sehemu husemi kitu chochote, Alhamisi nikakwita wewe sio mtunza ahadi, halafu Ijumaa ndio ukatokea. Unadhani ile sifa mbaya ya kutotunza ahadi niliyokupa Alhamisi umeifuta?
   
 12. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #12
  Jun 6, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kada, nitatoa mfano, kama ahadi zote hizi mbili ziko sawa then, ahadi zote ni za kujitolea...

  --- sera za CCM kuleta maisha bora kwa kila mwananchi na kupambana na ufisadi kwa miaka yote iliyopo madarakani kama mojawapo ya kupatiwa kura za wananchi ni ahadi isiyo ya kujitolea, ni ahadi ambayo imelipiwa na wananchi kwa kuwapa CCM kura ili wawe madarakani. Wasipotimiza hilo linakuwa deni na hawana haki ya kusema kuwa tulijitolea.

  --- nchi ya Sweden kutamka kuwa itasaidia bajeti ya Taifa kwa mwaka 2009-2010 kwa asilimia 20 kama Serikali ya Tanzania itakuwa imekamilisha mpango wa kueneza umeme nchi nzima au mpango wa kusambaza maji ya bomba nchi nzima kufikia mwisho wa 2008, ni ahadi ya kujitolea isiyo deni, maana kama Sweden wanapata matatizo ya dharura kitaifa hivyo kushindwa kutimiza ahadi yao, Tanzania haiwezi kuidai Sweden kwa kutotimiza ahadi hiyo.... vivyo hivyo, serikali isipotimiza yale masharti iliyopewa, Sweden wanaweza wakaendelea na mpango wao wa kusupport bajeti au wanaweza kukatisha.

  Swali Kada: je, ahadi hizo mbili hapo juu zote ziko sawa, yaani ni za kujitolea?!
   
 13. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #13
  Jun 6, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  DVD ya FMES = Sera Za CCM Kupitia Chairman Kikwete = (FAIL)?!
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Jun 6, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  Kuhani.. kuna vitu nimejifunza katika maisha yangu haya mafupi.. la kwanza ni kuwa sayari ya dunia hainizunguki hata kama ningependa sana.

  Pili, maisha hayana haki utakuwa unakatishwa tamaa mara nyingi

  tatu, usiassume vitu bila kufuatilia, jaribu kufuatilia na tafuta chanzo

  nne, kama inabidi kulalamika basi toa nafasi mtu kujieleza na upate kumuelewa kama hutakubali maelezo yake hilo ni jambo jingine..

  tano.. usibatize watu majina tu kwa vile havikuendana na unavyotaka.

  Katika kuandika kwangu kwingi kuna vitu ambavyo sijavifanya hadi sasa; sijawahi kumuita JK jina lolote ambalo si la kwake au siyo cheo chake; Pamoja na mgongano wangu na Lowassa sikuwahi kumbatisha jina lolote lile ambalo si la kwake.. nikitumia kejeli au kebehi vyote navitumia katika majina yao na vyeo vyao. Nikisema kitu kuhusu jambo fulani najaribu kufuatilia kuna usahihi wake na kupata maelezo zaidi badala ya kuchukulia assumption zangu kuwa ni sahihi..

  Na mwisho, nikikosea najirudi kwani huo ndio uungwana na sitarajii kumpendezesha kila mtu. Lakini kama kutingwa watu hutingwa, na naamini ni ubinadamu kuwapa watu nafasi nyingine. Ni kwa sababu hiyo alipojiuzulu Lowassa makala yangu ya kwanza haikuwa ya kushangilia kuanguka kwake kama wengine...

  Ndio maana kamwe sitaanzisha mada ya kumgusa mwanachama yoyote hapa kwa namna yoyote ya kumfanya awe duni, sitombatiza mtu jina lolote la kebehi au kejeli, na wala katika kupingana kwangu sitatumia hoja za nguvu. Sasa tuko tofauti naelewa..

  so ambao mnajisikia mmesalitiwa, kwamba mioyo yenu imevunjwa kwa sababu "ahadi haikutimizwa" na wale ambao kwa namna moja wanaona kuwa "wameachwa solemba" naomba mgangamale tu mjipe moyo na msikate tamaa. Tumkumbushe ndugu yetu FMES kuhusu ahadi yake hiyo na tusimuone kafail kwa vile we didn't get what we wanted when we wanted tit.....
   
 15. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #15
  Jun 7, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mwanakijiji,

  Lakini ukiahidi si ni lazima utimize? Bora kukaa kimya kuliko kutoa ahadi ambazo huwezi kuzitimiza.

  Mkuu FMES, timiza ahadi yako mkuu.
   
 16. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #16
  Jun 7, 2008
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  naamini sio vibaya kumkumbusha mtoa ahadi kuhusu ahadi
  aliyoitoa. tatizo linakuja maneno gani yanatumika katika huko
  kukumbusha. na hili la kubatizana majina nadhani imezidi kuliko.
   
 17. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #17
  Jun 7, 2008
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Well if you want to be purer than pure you better be pure. DVD kutoka kwa FMES na thread imeanzishwa lakini GT bado anasuasua kama utingo wa dala2. Karibu kwa GT's theory.
   
 18. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #18
  Jun 7, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kama ka fail basi uko naye draw maana uliwahi kuleta uzushi hapa na uka fail mwishowe yeye hadi sasa hakuna neno la kizushi wala mtu kupinga aliyo yasema .Mpe muda
   
 19. YournameisMINE

  YournameisMINE JF-Expert Member

  #19
  Jun 7, 2008
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 2,451
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 145
  GT,
  uchokozi huo....friday yote hii unataka kumwaribia weekend mwenzio!! ushindwe na ulegee.....GT, worst person of the dayyyyyyy.
   
 20. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #20
  Jun 7, 2008
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  ni vizuri ungeanzisha thread yako nyingine na wewe ya kumkumbusha, na sio kuja kudandia na kuvuruga watu wanachoongea... siku nyingine kama vipi usichangie tu !
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...