DV Lottery-Travel Ban ya Tanzania na ujio wa Biden

The Tomorrow People

JF-Expert Member
Jul 11, 2013
2,662
2,744
Niende moja kwa moja Kwenye mada!!

Sote tunakumbuka Trump alituwekea Travel Ban kwa wa Tanzania wanaoshiriki Kwenye DV Lottery. Kuna tetesi kwamba ujio wa Biden White House pamoja na mambo mengine utafuta hili katazo kwa maana Democratic Party wana support sana immigration.

Mwisho kabisa, tarehe 10 November 2020...ndio siku ya mwisho kufanya application kwa mwaka huu. Jaribu bahati yako huwezi jua.
 
Vikwazo vikiwekwa ni rahisi ila kutoka ni issue check Zimbabwe hadi Leo Bado Kuna vikwazo havijatoka Richa ya uongozi kabadilika... Vikwazo vinaweza Zidisha ongezwa, Usidhani Biden ndio ataregeza watu kwenda US ...
 
Democrats walikuwa wanapinga sera nyingi sana za Trump, kama ukuta wa Mexico, nadhani hata hiyo ya lottery waliipinga, tatizo wanaweza punguza idadi ya watu wanaoruhusiwa kuingia nchini kwao kupitia hiyo lottery, coz ilionekana wengine wanakwenda kujihusisha na uhalifu.
 
Ngoja tuone kama Biden atakuwa muumini wa "American Interest" kwenye maamuzi ya Pompeo.

So far, America wanajiita the country of lots of possibilities kwa yeyote mwenye ndoto. Hii inawafanya kupata best brains from all over the globe.

Tanzania based on the potential in place, tunaweza pia kutengeneza "Tanzanian dream" kwenye cross-cutting sectors.

Ili Tanzania dream yenye kujenga uchumi jumuishi kwa kuongeza thamani raw materials zinazalishwa ndani na kuuza qualitative and quantitative final products.

Wakifungua milango sawa, ila wakiendelea kutufungia iwe changamoto positive kwetu kutoboza hapa.

Indian, wazungu, Chenese it happens wao wamekuwa na access na credit na wamekuwa wakifaidika na kuchakata (ndani ya Tz au nje ya Tz) raw materials toka ardhi yetu (pamba, korosho, chai, katani, cocoa, ufuta, minerals products, mpaka Avocado za Njombe) na kuzi-export; wakienda US inakuwa sehemu ya kula bata.
 
Vikwazo vikiwekwa ni rahisi ila kutoka ni issue check Zimbabwe hadi Leo Bado Kuna vikwazo havijatoka Richa ya uongozi kabadilika... Vikwazo vinaweza Zidisha ongezwa, Usidhani Biden ndio ataregeza watu kwenda US ...
Umeanza vizuri comment yako lakini mfano ulotowa ni mbaya sana, kwani hakuna lilobadilika katika utawala wa Zimbabwe. Utawala wa Zimbabwe ni wa mfumo wa punda yule yule lilobadilika ni soji. Hakuna kilichobadilika Zimbabwe hususan katika abuse of human rights, ufisadi na mauaji ya raia. Hakuna nchi iliyoiwekea vikwanzo Zimbabwe inayoweza kuridhika na kinachoendelea hivi sasa kiasi cha kuondoa vikwazo vyao.

Kwa Tanzania, kuwekewa ngumu juu ya kuingia USA na Trump ni zaidi juu ya reputation ya watanzania waliyoyafanya wakiwa marekani kuliko uvunjaji wa haki za binaadamu wa serikali ya Tanzania. Hata hivyo kwa yaliyotokea kabla na baada ya uchaguzi katika sehemu mbali mbali za Tanzania hasa Visiwani huenda vikwazo vya kuingia USA kwa watanzania vitachukua muda kulainishwa.
 
Back
Top Bottom