Katoma
Senior Member
- Mar 11, 2008
- 133
- 10
Wana-JF ningeomba kupata mawazo yenu kuhusu mila ya hawa wenzetu waDachi. Kila mwaka huko Uholanzi katika sikukuu za Krismasi, huwa Father Christmas (Santa Claus) anatembea akiambatana na wasaidizi wake ambao wanaitwa Zwarte Piet ambao huwa wanajipaka chokaa ili waonekane kama watu weusi. Hii inatokana na mila yao tokea kale kuwa msaidizi wa Santa Claus alikuwa mtu mweusi, ingawa kiukweli tuseme alikuwa mtumwa.
Je kwanini hawatumii watu weusi asilia na sio kujipaka chokaa?
Anyway the big deal kwangu ni kuwa, huyu Zwarte Piet kimila anatakiwa awe na tabia fulani fulani katika maonyesho wafanyao mtaani na katika party mbali mbali wakati wa Krismasi. Mara nyingi huwa anafanya vituko ambavyo vinamfanya aonekane kama zezeta, au stupid, na huwa huongea kwa kidachi kisichoeleweka. Hii hasa hasa inatokanana na enzi za ubaguzi/utumwa ambapo watu weusi walikuwa considered wapumbavu au wasio na thamani ukilinganisha na watu weupe.
Anyway, soma zaidi kuhusu hii mila hapa:
[ame]http://en.wikipedia.org/wiki/Zwarte_Piet[/ame]
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=rU3m50RxJzA&feature=related[/ame]
What's your take??