Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

GEN. FLYNN AACHIA NGAZI

Aya ya mwisho ya bandiko hapo juu tulisema 'suala la Russia na Gen. Flynn' litaleta tatizo
Tayari tatizo limetokea, mshauri wa usalama wa Trump Gen Flynn amelazimika kujiuzulu

Ni baada ya habari zaidi kuhusu maongezi yake na balozi wa Russia kubainika
Habari zinamweka VP Pence katika wakati mgumu kwani alisimama kumtetea kwa hilo

Kulikuwa na kiwewe, Kellyanne Conaway tuliyesema ni wa kupuuzwa, alisema Rais anasimama na Flynn. Masaa machache Spicer kaeleza Rais kutathmini suala la Flynn

Habari zilikuwa nzito zikimwelekea Trump siku nzima
Kwanza, tweet ya Trump baada ya Obama kuweka vikwazo kwa Russia

Wengi wanahoji uhusiano wa mshauri wa ulinzi na Russia na kama alitumwa na Trump

Pili, state dept chini ya S.Yates aliyefukuzwa(act AG) inaonyesha WH ilitaarifiwa kuhusu Flynn.

Tatu, kwanini kulikuwa na maongezi ya kidiplomasia ya Team Trump, Obama akiwa Rais

Swali, Trump alijua lini kuhusu Flynn na kwanini kulikuwa na cover up ya suala zima

Hapa panaunganishwa na suala la Russia hacking ambalo linachunguzwa.

Kujiuzulu kwa Flynn ni damage control lakini damage yenyewe bado na itasumbua sana

Watu wanajiuliza sana kuhusu uhusiano wa Trump na Russia! kulikoni?


Tutawajuza kinachoendelea
 
Obama aliona mbali...hata hivyo kujizulu kwa Flynn kunaweza kufungua mlango kwa makubwa zaidi. Kwa Wamarekani issue kama hii haiishi hivi hivi kwani pamoja na kujiuzulu uchunguzi wa kina lazima ufanyike na si ajabu mtego ukawanasa waliomo na wasiokuwemo. Let's stay tuned.

The increase in the number of the less intelligent Adolf Hitlers being voted into office is alarming and is enough proof that something must definitely be terribly amiss somewhere. What is the world coming to...I wonder!
 
"Mag3, post: 19717534, member: 10873"] kujizulu kwa Flynn kunaweza kufungua mlango kwa makubwa zaidi
Kujiuzulu kumeondoa ile 'executive privilege'' kwamba ni mfanyakazi wa WH na anaweza kuitwa katika kamati ya bunge na kukaa kimya
Kwasasa akiitwa lazima aseme neno, hapa ndipo mambo yanafunguka zaidi
Kwa Wamarekani issue kama hii haiishi hivi hivi kwani pamoja na kujiuzulu uchunguzi wa kina lazima ufanyike na si ajabu mtego ukawanasa waliomo na wasiokuwemo. Let's stay tuned.
Wamarekani issue yoyote inayoonekana kuwadhalilisha wataifuatilia sana. Kwanza, news ni biashara. Pili, kuna politics kubwa n.k.

Intel comm imenasa mawasiliano ya Flynn aliongea nini kuhusu vikwazo.
Russia hawaku react ilivyotegemewa, wakipata 'accolade' ya Trump 'Putin ni smart'
Yaani anamdhalilisha Obama

Well, ile tweet kwasasa ina 'haunt'. Kuna uhusiano wa Vikwazo, Flynn, tweet, hacking n.k.

Maswali, je, Flynn akiwa mshauri wakati wa kampeni na transition, alifanya hivyo kama mtu binafsi au alitumwa na Trump?
Na kama ilikuwa personal initiative, je ali report back kwa Trump?
Na Trump alijua lini kuhusu hayo?
Kwanini WH haikushughulikia kauli ya state dept? Kwanini WH ilikuwa na cover up

Kujiuzulu kwa Flynn kuna maana mbili
1. Kumnusuru VP na aibu ya kutetea jambo lenye sura ya uovu wa Taifa
2. Kuzima mjadala ili kutoenda mbali zaidi na kugusa maaneo mengine makubwa
3. Kumwepusha Rais na dhahma inayokaribia ya hacking, vikwazo, tweet n.k

Tatizo ni Trump, ameshakosea kuanzia mwanzo

a)Intel comm inajaribu kumuonyesha inavyofanya kazi na hapa lazima watapiga ''mfupa''
b)Ugomvi na media unaongeza uzito kwa habari nzima. Pressure ya jana aliisikia WH

Kwa hali inapoelekea siku moja mtu akiamka na kusikia kuna 'impeachment' haishangazi. Haya mambo yanachimbwa na mwisho ukweli utaonekane
 
Nilijua povu lazima likutoke, utasubiri sana hiyo 'impeachment' ya POTUS.

Halafu mkuu huwezi kuandika mwenyewe humu, mara 'tutawabaharisha', 'tutaelezea', ina maana haya maandishi huwezi kuyasimamia wewe kama wewe?

'Tuta' tuta 'tuta' 'tuli', 'tuta', si uandike 'nita', 'nita', 'nitaelezea', 'nitawahabarisha'. Then unavyosema utatuhabarisha, kwani una source ya taarifa ambayo ni unique kwako wewe au ni hizo liberal sources ambazo kila mtu anaweza ku-access?
 
Nilijua povu lazima likutoke, utasubiri sana hiyo 'impeachment' ya POTUS.
What you are hearing is just the tip of an iceberg and what was being awaited has just happened...the resignation of one who, we were assured by the POTUS, was one of his best and it is only 25 days since inauguration and already one of the best has proved a non-starter.

From now on I bet things are going to move a little faster, the theory of isolation is being put to work...do you remember Trump's campaign chairman Paul Manafort...that was the first step. He resigned over Russia connection and now Flynn has followed his footsteps!

Have you heard that the POTUS is eyeing nobody else but Governor Christie of Bridgegate...and for what? Stay tuned. The boat is sinking and someone is clutching at straws. The wise ones will soon start jumping ship...people who sacrificed their own blood for freedom know better.
Halafu mkuu huwezi kuandika mwenyewe humu, mara 'tutawabaharisha', 'tutaelezea', ina maana haya maandishi huwezi kuyasimamia wewe kama wewe?

'Tuta' tuta 'tuta' 'tuli', 'tuta', si uandike 'nita', 'nita', 'nitaelezea', 'nitawahabarisha'. Then unavyosema utatuhabarisha, kwani una source ya taarifa ambayo ni unique kwako wewe au ni hizo liberal sources ambazo kila mtu anaweza ku-access?
Starting to split hairs, eh?

Lock her up, lock her up, lock her up...!
 
General Flynn resigned because of a matter of TRUST and NOT any legal aspect.

There is nothing wrong, nothing illegal in the then incoming National Security Advisor's discussions with the Russian ambassador about sanctions in December. That is part of his job.

By the way, when your pal uses 'we','we', 'we', who are the others he keep referring to?
 
General
By the way, when your pal uses 'we','we', 'we', who are the others he keep referring to?
Tuta' tuta 'tuta' 'tuli', 'tuta', si uandike 'nita', 'nita', 'nitaelezea', 'nitawahabarisha'. Then unavyosema utatuhabarisha, kwani una source ya taarifa ambayo ni unique kwako wewe au ni hizo liberal sources ambazo kila mtu anaweza ku-access?
Mkuu unafahamu kwa sijibu post zako,tumejikita kujadili yanayotokea kwa upana

Umeninukuu kama kawaida ukamvamia Mag3 bila hoja

Huna hoja unaangalia spelling na herufi. Pengine upo forum wrong mkuu

Nimelazimika kukujibu hili ili kukuonyesha stara za majadiliano.

Neno 'mimi' kwa lugha yetu ya kiswahili na pengine zingine ni dalili ya majivuno (narcissism), kiburi (arrogance) na dharau kwa uchache wa kusema

Maneno 'sisi, tuta, tume, n.k.' yanaonyesha uungwana katika mjadala
Tunashirikisha kila mmoja hata kama tuna mitazamo au maoni tofauti

Kwa maneno mengine aliyeandika au msomaji ni mshiriki wa mjadala

Viongozi mahiri wanaojua kuongea hutumi neno sisi.
Mfano, Nyerere alitumia sana 'tuliamua, tulikubaliana, mumetuchagua, tunawatumikia' hata pale maamuzi hayo hayakugusa wengi.
Obama alikuwa anatumia neno 'we' kuonyesha uungwana

Kwasababu wengi hawajui matumizi, wapo wanaonekana arrogant tu kwa lugha.
Si kwamba maneno yao ni tofauti bali uchaguzi wa maneno unabeba ujumbe

Kuhusu suala la source, kama unazo una fursa ya kuanzisha uzi na kujadili

Midhali upo unasoma ukubali unachosoma si lazima kikufurahishe,hatupo hapa kupendeza

Nadhani unaweza kuona kila tulichokieleza kinavyojidhihiri dhahiri shahiri kwa siasa za US

Unaweza kujifunza, lakini pia una hiari ya kutochangia au kutosoma kabisa, ukaendelea na shughuli zako eneo jingine unalodhani lina fit haiba, wajihi, stara,busara na hekma zako

Wanajamvi tunaendelea na mjadala wa Turmoil (timbwili) la WH na Trump
 
Okay sir, naona umejidhihirisha rangi yako halisi. Hutaki mawazo tofauti ndio maana wakitokea watu wenye mawazo tofauti na wewe unashindwa kuficha hasira yako.

Hauna tofauti na wale wanaoblock watu wenye mawazo tofauti na wao kwenye mitandao. Inaonekana ingekuwa ndani ya uwezo wako ungeniblock kwenye hii thread yako.

Tofauti yako na mimi ni kwamba mimi simchukii mtu mwenye mawazo tofauti na mimi katika debates au discussion kwa sababu I believe I don't have monopoly of the best opinions or best ideas.

This is what happens katika mijadala inayohusisha watu wanao-assume they 'know it all' . Hata Viongozi wengi wa Afrika wanashindwa kuvumilia mawazo tofauti na yao, hawapendi kupingwa, lakini utashangaa wale wanaofanana nao wanawaponda humu kwenye Jamii Forum.

Nimeonekana napingana na mawazo yako hasa yanayoonyesha chuki za wazi dhidi ya Rais Trump. Ukiandika uongo humu au subjective opinions zako hutaki mtu akukosoe badala yake watu wasome tu 'wajifunze', that is far from a healthy and a constructive discussion.

Hao viongozi unaosema walikuwa wanatumia neno 'sisi' au 'we' walikuwa wanazungumzia 'team-work' lakini pale walipofanya wao tu walitumia 'I', mfano Obama alipokuwa aki-sign EO hakutumia 'we'.

Sir, to the extent kuwa mawazo tofauti na yako unayachukulia kama 'spelling error na herufi' ni dhahiri huna cha kujifunza kutoka kwa wengine bali kila mtu inabidi ajifunze kutoka kwako.

Let me just reiterate, I have never been more humbled and more open minded with high standards of decorum in my conversations, however, what I saw here is clear vacuousness.

The notion that as a supporter of Pres. Trump I should not wholly engage in discussions in a thread started by somebody who hates Pres. Trump is entirely ridiculous. The whole notion is preposterous.

But I'm not astonished, I engage in discussions with real libtards many times and in many places and I'm kind of used to their prejudice.

Sir, since you like only those who agree with you in your thread, have a nice four years of relentless and unfettered attacks on the Trump Administration.
 
"El Jefe, post: 19739340, member: 387168"]Hutaki mawazo tofauti ndio maana wakitokea watu wenye mawazo tofauti na wewe unashindwa kuficha hasira yako.
Kila mara upo hapa ukiwa na mawazo tofauti. Je, umeona lini mtu amekutukana licha ya wewe kutukana!Hvi hapo hujifunzi kitu kweli. Kwamba, unatukana watu wapo kimya!
Inaonekana ingekuwa ndani ya uwezo wako ungeniblock kwenye hii thread yako.
Mbona unaandika kila siku nani ameshakuzuia au amesema usiandike
Tofauti yako na mimi ni kwamba mimi simchukii mtu mwenye mawazo tofauti na mimi katika debates au discussion kwa sababu I believe I don't have monopoly of the best opinions or best ideas.
I don't hate either! this is an open forum.

Lakini pia mjadala lazima uende kwa ukweli si ushabiki na unazi bila substance

Umesema 'nilijua utakuja na povu' hiyo tu ni lugha dhaifu kwa mtu mwenye hoja.
Siku zote silaha rahisi na nyepesi kwa watu wa aina hiyo ni matusi.

You got into my nerves ulipozungumzia kwanini tunatumia maneno ya 'wingi' kama tuna, tunasema na ukarudia kwa Mag3 we, we we.

Yaani hakuna ulichoona katika mbandiko cha kujadili bali hayo maneno.
Ulichotaka ni ku dilute mjadala uonekane kama ulivyo. Watu hawana interest na hayo

Hizi habari za spelling error, typo n.k. ni too low kwa 1/2 page uliyoandika
Hapo ndipo nikaona nikupe shule ya matumizi ya maneno
Nimeonekana napingana na mawazo yako hasa yanayoonyesha chuki za wazi dhidi ya Rais Trump.
Tunajadili habari zilizopo sasa kama unadhani ni chuki you're entitled to your opinion
Ukiandika uongo humu au subjective opinions zako hutaki mtu akukosoe badala yake watu wasome tu 'wajifunze', that is far from a healthy and a constructive discussion.
Hatuandiki kitu kisichokuwepo. Kinachoendelea ndicho kinajadiliwa
Flynn ameachia ngazi, hiyo ni habari. Uchunguzi unaendelea ni habari.

Obamacare imeshindika kuftwa siku 1, ni habari. NAFTA haiwezi kufutwa kirahisi, ni habari

Katika habari kuna uchambuzi wa kila mtu. Hapo kuna opinion na mara nyingi tunasema hivyo. Opinion za mtu ni ngumu sana kuwa sahihi au zenye makosa.

Hivyo kukosoa opinion ya mtu ni kosa. Kinachoweza kufanywa katika opinion ni ku differ.

Kwamba, kuna hoja zinaangaliwa kwa mtazamo tofauti.

Hivyo lazima uelewe opinion inakuwaje , inakuwa rebuttal vipi na si suala la kukosoa tu

Mfano, ukisema kwa mawazo yako Obama alikuwa kiongozi mbovu sana, sitaweza kukukosoa. Ni mawazo yako. Ninachoweza kufanya ni kukuonyesha kuwa hakuwa mbovu kwa mawazo yangu ambayo si lazima yawe sahihi. Huo ndio mjadala

Lakini pia lazima uwe na back up ya unachozungumza. Tulisema, Obamacare haiwezi kufutwa kwa siku moja kwasababu inaingiliana na mambo mengine.

Nakumbuka ulisema atafuta kwa kalamu, kwasababu ulisikia na kuamini tu.

Tunaofanya analysis leo tunasimama na kusema 'umeona'? Tulikuwa na ufahamu si ushabiki
Sir, to the extent kuwa mawazo tofauti na yako unayachukulia kama 'spelling error na herufi' ni dhahiri huna cha kujifunza kutoka kwa wengine bali kila mtu inabidi ajifunze kutoka kwako.
Ninajifunza, si matumizi ya 'tuna, tume, we' hayo hayasaidii mtu yoyote the least to say. Ninajifunza substance si flimsy argument
The notion that as a supporter of Pres. Trump I should not wholly engage in discussions in a thread started by somebody who hates Pres. Trump is entirely ridiculous. The whole notion is preposterous.
Ni mawazo yako! ...

Wanajamvi, tunaendelea na Timbwili la WH na jinsi gani mambo yalivyo

Inafuata
 
TIMBWILI LINAFUKUTA 'NYUMBA NYEUPE'

WH Yamtosa Flynn, yapalilia moto zaidi

Kama tulivyoeleza siku za nyuma, sakata litaisumbua sana WH
Kilichofanyika ni kumtosa Flynn kwa kilichosema kukosekana kwa uaminifu (lack of trust).

Ni kuficha uso wa VP na wenzake waliozunguka kupiga debe Flynn hakujadili vikwazo

Kwa wenzetu US hoja haizimwi kirahisi, na habari inayotokazamagazeti huwa si nzima. Mara nyingi huacha nafasi ili mtu ajichanganye, hoja zianikwe

Vikwazo viliwekwa na Obama siku za mwisho kabisa za utawala wake.
Na siku hiyo ndiyo Flynn alikuwa na simu na balozi wa Russia

Kisha Trump akasema ' alijua bwana Putin ni smart' baada ya kutojibu mapigo

Siku sita baada ya kuapishwa, Dept of justice ilimtaarifu Rais habari alizotoa Flynn si kweli
Na kwamba, hilo linaweza kutumiwa kumtapeli siku zijazo

Siku takribani 10 baadaye Washington post liakeleza mawasiliano kati ya Flynn na Balozi yakihusisha vikwazo ingawa hakukuwa na details zaidi

Baada ya hapo ndipo ikawa ndiyo habari ya viunga kuanzia LA hadi NY
WH walikaa kimya hadi pale CNN walipotoa taarifa kuwa Inte comm inachunguza

FBI walikuwa na taarifa lakini hawakueleza nini kinaendelea

Na kwamba, Obama na Trump walitaarifiwa mapema uwepo wa mawasiliano yasiyo ya kawaida kati ya maafisa wa Timu ya Trump na maafisa wa kipepelezi wa Russia

Huu ni muhtasari, suala linakuwa pana zaidi.
Kwanini Trump alipotaarifiwa na DOJ hakuchukua hatua dhidi ya Flynn mara moja? Kwanini alisubiri hadi magazeti yakaandika?

Tayari mhausiano ya mambo hayo yanaaza kujitokeza.
Kwamba, FBI walipaswa kufanya walichofanya kwa Clinton, hawakufanya

Swali kubwa zaidi, Flynn alifanya mawasiliano katika capacity gani?
Kama mtu binafsi? Alitumwa? na kama alitumwa na nani?

Inajidhihiri zaidi kuwa makachero wa Russia walikuwa na mawasiliano ya karibu sana na mara nyingi sana na timu ya Trump. Je, ni akina nani na walimwakilisha nani?

Hapo ndipo utata wa tax, mahusiano ya Trump na Russia, Flynn na Trump, Trump na timu yake, hacking ya Dem accounts n.k. yanapohojiwa na si Dems tu bali Rep

Suala lipo mikononi mwa 'the establishment na Intel community' ambazo Trump alizizogoa

Inaendelea....
 
General Flynn resigned because of a matter of TRUST and NOT any legal aspect.
Are you living in a bubble? Did you even listen to his close aides, Kellanne Conway and Sean Spicer and what the POTUS himself said today about still having complete trust in General Flynn? FYI he threw the blame to fake news and criminal leaks.
There is nothing wrong, nothing illegal in the then incoming National Security Advisor's discussions with the Russian ambassador about sanctions in December. That is part of his job.
Are you sure of this? Then why did he have to lie about it! Without fake news and criminal leaks, the lie would have lived on and everything would be just normal...is that how you see it too?
By the way, when your pal uses 'we','we', 'we', who are the others he keep referring to?
He is referring to "we", all of us. It is the polite way of referring to a group like what we have here unless you consider yourself not one of us, are you? Oh, I was forgetting we are the libtards, aren't we?

El Jefe, hebu fikiria kama Mkuu Nguruvi3 angekuwa anatumia maneno kinyume na hayo, je ungemuelewaje? Au ni yale yale ya hero wako...mimi pekee nitafanya, mimi pekee ninaweza, mimi, mimi, mimi...! Hata hivyo inafuatana na malezi ya mtu, wengine wamekulia mazingira yasiyo ya umimi, mazingira yanayotambua ushirikiano wa pamoja...si changu changu. Kwa mbali naanza kupata picha kwa nini tabia zako zinaendana na za hero wako na wabinafsi wengine.
 
Kujiuzulu kwa Flynn kuna maana mbili
1. Kumnusuru VP na aibu ya kutetea jambo lenye sura ya uovu wa Taifa
2. Kuzima mjadala ili kutoenda mbali zaidi na kugusa maaneo mengine makubwa
3. Kumwepusha Rais na dhahma inayokaribia ya hacking, vikwazo, tweet n.k



Ni ajabu mtu aliyeendesha kampeni kwa kutumia leaks kuwabamiza wapinzani wake na kuvisifia vyombo kama wikilieaks, leo analalamikia leaks akiziita criminal. Trump karibu atachanganyikiwa, alilikoroga na sasa alinywe tu bila kulalamika hovyo.
 
MTAZAMO WA WIKI SIASA ZA US

Kama wiki zilizotangulia hii nayo haikukosa matukio kadhaa ya kujadili mengine yakishangaza kidogo

TRUMP AKUTANA NA PM WA TRUDEAU WA CANADA

Canada ni mshirika mkubwa wa biashara na US, na US ni soko kubwa la Canada
Nchi hizo pamoja na Mexico zinaunda umoja wa NAFTA

Katika mazungumzo, kauli zilikuwa za kupima Trump akisema NAFTA itafanyiwa 'tweaking'
Tweaking kwa maana ya kufanyiwa adjustment. Hili ni kinyume na tishio la kuvunja NAFTA
Katika kampeni,alisema NAFTA ni mkataba disaster wa Bill Clinton, hata kama hakuwa mwanzilishi

Hivyo hitimisho ni kuwa NAFTA itakuwepo, ahadi nyingine aliyovunja

PM WA ISRAEL
Naye kama wengine alifika DC kukutana. Israel na US ni washirika wa karibu sana

Kubwa lilionekana ni usuluhishi wa Israel na Palestine.
Trump alisema taalika nchi nyingine za kiarabu kushiriki katika usuluhishi

Akasema atakubali Israel na Palestine wakikubaliana one state au two state solution
Hili lilichukua habari kwa upande wa middle east kutokana na msimamo usioeleweka

Hoja: Palestine imelilia haki ya Taifa lao kwa muda wa mingi sana.
Hilo linaungwa mkono na nchi za Kiarabu na EU kwa pamoja.

Siasa za US kwa miaka takribani 40 ni za two state solution

Kwa upande wa Israel, one state solution inapingwa na Jews kwa hofu kuwa kuzaliana kwa Waarabu kunaweza kupoteza Utaifa wao na ni tishio kwa siku za mbeleni

Hoja ya Trump ilichanganya dunia kwa mantiki anapozungumzia one or two state solution ana uelewa wa nini anachoongelea? Na je, siasa za US middle east zimebadilika?

Siku iliyofuata balozi wa US-UN alisema msimamo ni two state solution kuweka mambo sawa

Swali lililojitokeza katika mkutano huo ni kuhusu anti semetism(chuki dhidi ya Waisrael) katika miji na viunga vya US.

Trump hakukemea tabia hiyo zaidi ya kujinasibisha na binti yake aliyeolewa na Musirael

MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI
Katika hali isiyo ya kawaida, mkutano na waandishi uliandaliwa haraka
Tofauti, huu ulitoa fursa kwa waandishi wote na si wa kuchagua kutoka 'media' friendly

Hata hivyo, mkutano umezungumziwa na magazeti duniani ulikuwa wa kasheshe
Trump hakujibu maswali hasa lile la Israel na anti Semitics, au lile la Russia na Flynn

Inaendelea.....
 
MKUTANO NA WAANDISHI
Inaendelea...

Kwa hakika mkutano huo ulionyesha sehemu ya pili ya Rais Trump na jinsi anavyotatizika kujibu hoja

Ni mkutano uliokuwa wa kigomvi kwa aina fulani, akikataa kujibu maswali au kujibu nje ya swali

Alizungumzia kurithi nchi yenye matatizo ya kiuchumi kazi zikienda nje, siasa za mashariki ya kati n.k.

Hoja: Kwa kushambulia rekodi ya Obama bila takwimu ilikuwa kukwepa hoja na mambo yanayomkabili
Obama alitengeneza ajira kwa miezi 74 mfululizo akiongeza idadi kila mwezi. Hili hakusema
Obama akiingia madarakani nchi ilikuwa inapoteza ajira kwa malaki
GDP ilikuwa -0.6 na alipoondoka ni takribani 1.5
Takwimu zinaonyesha pato la mtu kuongezeka na kuimarika kwa sekta ya ujenzi

Kwa ufupi, Trump amerithi nchi nzuri kuliko Obama alivyoipokea kutoka kwa Bush

Trump aliulizwa kuhusu Russia. Hakujibu kama maafisa wake walishiriki au alijua.
Alichofanya ni kuhamisha mjadala kwa kutuhumu fake news na vyombo vya habari, na leaks

Aliulizwa kama leaks zilikuwa za kizushi 'phony' akasemani za kweli.
Akaulizwa iweje leak ziwe za kweli na news za leak ziwe fake? Alijibu ni kwa sababu news ni fake.

Hoja: Trump analalamika kuhusu leaks, tunakumbuka alivyo shangilia wikieleaks ilipotoa habari za Haillary. Iweje basi leo aone ni jambo baya? Wazungu wanasema 'checken are coming home to roost'

Kama mtakumbuka tuliwahi kusema ugomvi na Intel community havitamsaidia.
Leaks zinatokea si kwa bahati mbaya , ni kutokana na matamshi ya siku za nyuma dhidi ya IC

Maelezo yake ya kukwepa hoja yalimtia katika tatizo jingine. Trump alisema ameshinda viti 303 ikiwa ni idadi kubwa katika historia ya US. Mwandishi alimpa namba za Obama zilizokuwa juu.

Trump akasema anazungumzia Republican, mwandishi akampa namba za Reagan.
Mwisho akasema ndivyo alivyoambiwa! ikiwa ni kwa mshangao wa wengi. Ilikuwaje hakujua ukweli huo

Mengi yaliyohusu siasa za ndani na nje hakuyajibu kama kiongozi wa Taifa kubwa.
Hilo lilionyesha ni kwanini hapendi vyombo vya habari, mkutano uliweka wazi udhaifu

Imefika mahali vyombo vya mrengo wake sasa vinaanza kumsema tofauti na kumpamba

Wiki ilianza na Flynn, ikaendelea na Russia, ikafutiwa na waziri mteule kushindwa kuungwa mkono na Republican, Mteule wa kumrithi Flynn akakata kazi kwasababu ya 'chaos' na mkutano vurugu na waandishi. Haikuwa wiki njema kwake kabisa

Mkutano wa Security na NATO Ujerumani, inafuata

Tusemezane
 
MKUTANO WA USALAM MUNICH

Mkutano huo wa usala 'security conference' unafanyika katika Jiji la Munich Ujerumani

Jana waziri mwandamizi wa Ujerumani alisema US inahitaji NATO kama ambavyo NATO inaihitaji
Waziri huyo alipeleka ujumbe kuwa NATO ni muhimu kwa usalama wa US kinyume na inavyoonekana

John McCain naye aliongea. Katika hotuba yake Senator McCain alimshambulia Rais wake Trump bila kumtaja jina kwa sera zake. Ingawa hakumtaja, ni dhahiri aliyosema ndiyo afanyayo Trump

VP Pence kaongea leo akisema US inaunga mkono NATO bila shaka.
Kikubwa alichosisitiza ni wanachama kutimiza wajibu wao wa kulipia ada husika

Matamshi ya VP yanapingana na sera za Trump aliyesema NATO ni obsolete akimaanisha ni ya kufutwa

Kwa sasa nchi nyingi na hasa wanachama wa NATO hawana uhakika na sera halisi za US

Wakati huo huo Pence anaionya Russia kuhusu hali ya siku za karibuni inayohusu Russia

Katika hali isiyo ya kawaida ' inaripotiwa' maafisa wa usalama wa Russia wanadai kuwasiliana na maafisa wa kampeni ya Trump. Ingawa taarifa hazina uthibitisho, kinachoweza kuelezeka hapa ni kuwa endapo maafisa wa Trump walihusika, basi Trump atakuwa hana la kusema kuhusu Russia

Hayo yakiendelea Trump ameendelea na mikutano akishambulia media kwa kinachosema fake news.

Trump katika hali nyingine anaongelea electoral college mara nyingi kana kwamba ni suala muhimu
Hili linaeleza kuwa baada ya sintofahamu nyingi Trump amepoteza kujiamini akihisi ushindi unahojiwa

Kushambulia vyombo vya habari si kwa bahati mbaya.
Ni njia ya kuwaondoa watu katika mambo kadhaa yanayoonekana kupwaya.
Kwanza, kujiuzulu Flynn, kuhusishwa maafisa wake na Russia n.k

Ni kawaida , kunapotokea jambo asilopendelea Trump anaweza kuzusha mjadala wenye utata
Lengo ni kuwaondoa watu katika maongezi na hilo amelitumia na kufanikiwa sana huko nyuma

Tatizo linalomkabaili ni vita yake na media. Kwa nchi nyingi media house ni mhimili wa nne

Vita yake haiwezi kuwa na matokeo mazuri mbele ya safari.

Tusemezane
 
FAKE NEWS ZINAPOTOLEWA NA MLALAMIKAJI
'Shambulio la Sweden' lisilokuwepo

Mara nyingi Rais Trump amevituhumu vyombo vya habari kwa fake news

Ni majuzi tu ali tweet na kutaja vyombo hivyo kama maadui wa wananchi wa US

Media zilimuonyesha mbele ya mkutano electoral college aliyoshinda hailingani ya Obama au Bush
Hivyo habari yake ilikuwa fake na ikawekwa sawa na watu anaowatuhumu

Lakini kubwa katika hiyo 303 ni kuwa baada ya kubanwa alisema 'ameambiwa'
Kwa Rais wa US na mgombea alipaswa kujua hilo bila kusubiri kwani ni katika mambo yanayomgusa

Mwanzoni wa mabandiko baada ya uchaguzi, tulisema kuwa kauli zake za kampeni au transition haziwezi kupewa uzito na kauli kama Rais na kwamba, muda huo umepita na sasa ni utawala

Tulisema Rais wa US ni mkubwa na kauli yake inazizima duniani popote

Ni kwasababu hizo lile dege kubwa la airforce one lina kila zana za kumwezesha kufanya kazi popote
Mara zote safari za Rais wa US zinalipiwa na nchi ikiwa ni pamoja na ujumbe anaoambatana nao

Jana limetokea jambo lililoishtua dunia na pengine kutia walakini wa nini kinaendelea US?
Akiwa katika mkutano , Rais Trump aliongelea suala la wakimbizi.

Akatolea mfano wa maafa yaliyotokea juzi nchini Sweden kwa msisitizo mkubwa wa hoja
Taharuki ikazuka si US tu bali nchi za Ulaya ikiwemo Sweden yenyewe

Hakuna aliyekuwa na taarifa ya maafa kutoka Sweden siku ya alhamisi. Taharuki moja kwa moja

Imekuja eleweka Trump alikuwa anaangalia documentary channel ya Fox iliyoeleza wakimbizi na uhalifu nchini Sweden.

Documentary imeandaliwa na mswidi wa Mrengo wa kulia na kurushwa na TV yenye bawa la kulia

Trump haieleweki ali ielewea au ilikuwaje akatoa taarifa za kushtua.

Hayo yamekuwa ni maongezi katika social media, waziri mkuu wa zamani wa Sweden aki tweet, 'huyu bw alikuwa anavutaja nini wakati anasema hayo'.

Ubalozi wa Sweden nao ukihoji maelezo ya tukio ambalo halikutokea

Asubuhi ya leo ilikuwa damage control,alizungumzia wakimbizi na kutoa mfano wa alichokiona Fox
Ni utetezi wa ilimradi kwasababu kauli yake haikueleza hivyo

Media zinahoji wapi mkuu wa nchi anapata taarifa zake?
Kupitia cable au ni kupitia maafisa wake ambao muda wote wapo pamoja?

Ilikuwaje akaenda mrama kiasi hicho? Wapi watu wa usalama wa ku 'brief' mzee matukio

Media nazo zikijibu mapigo, anayekataa fake news ndiye mtengenezaji wa fake news

Tusemezane
 
FAKE NEWS ZINAPOTOLEWA NA MLALAMIKAJI
'Shambulio la Sweden' lisilokuwepo

Mara nyingi Rais Trump amevituhumu vyombo vya habari kwa fake news

Ni majuzi tu ali tweet na kutaja vyombo hivyo kama maadui wa wananchi wa US

Media zilimuonyesha mbele ya mkutano electoral college aliyoshinda hailingani ya Obama au Bush
Hivyo habari yake ilikuwa fake na ikawekwa sawa na watu anaowatuhumu

Lakini kubwa katika hiyo 303 ni kuwa baada ya kubanwa alisema 'ameambiwa'
Kwa Rais wa US na mgombea alipaswa kujua hilo bila kusubiri kwani ni katika mambo yanayomgusa

Mwanzoni wa mabandiko baada ya uchaguzi, tulisema kuwa kauli zake za kampeni au transition haziwezi kupewa uzito na kauli kama Rais na kwamba, muda huo umepita na sasa ni utawala

Tulisema Rais wa US ni mkubwa na kauli yake inazizima duniani popote

Ni kwasababu hizo lile dege kubwa la airforce one lina kila zana za kumwezesha kufanya kazi popote
Mara zote safari za Rais wa US zinalipiwa na nchi ikiwa ni pamoja na ujumbe anaoambatana nao

Jana limetokea jambo lililoishtua dunia na pengine kutia walakini wa nini kinaendelea US?
Akiwa katika mkutano , Rais Trump aliongelea suala la wakimbizi.

Akatolea mfano wa maafa yaliyotokea juzi nchini Sweden kwa msisitizo mkubwa wa hoja
Taharuki ikazuka si US tu bali nchi za Ulaya ikiwemo Sweden yenyewe

Hakuna aliyekuwa na taarifa ya maafa kutoka Sweden siku ya alhamisi. Taharuki moja kwa moja

Imekuja eleweka Trump alikuwa anaangalia documentary channel ya Fox iliyoeleza wakimbizi na uhalifu nchini Sweden.

Documentary imeandaliwa na mswidi wa Mrengo wa kulia na kurushwa na TV yenye bawa la kulia

Trump haieleweki ali ielewea au ilikuwaje akatoa taarifa za kushtua.

Hayo yamekuwa ni maongezi katika social media, waziri mkuu wa zamani wa Sweden aki tweet, 'huyu bw alikuwa anavutaja nini wakati anasema hayo'.

Ubalozi wa Sweden nao ukihoji maelezo ya tukio ambalo halikutokea

Asubuhi ya leo ilikuwa damage control,alizungumzia wakimbizi na kutoa mfano wa alichokiona Fox
Ni utetezi wa ilimradi kwasababu kauli yake haikueleza hivyo

Media zinahoji wapi mkuu wa nchi anapata taarifa zake?
Kupitia cable au ni kupitia maafisa wake ambao muda wote wapo pamoja?

Ilikuwaje akaenda mrama kiasi hicho? Wapi watu wa usalama wa ku 'brief' mzee matukio

Media nazo zikijibu mapigo, anayekataa fake news ndiye mtengenezaji wa fake news

Tusemezane
Sidhani Kama Trump atamaliza miaka yake 4.
 
Sidhani Kama Trump atamaliza miaka yake 4.
Wanaojua system inavyofanya kazi Marekani tayari wanaliona hilo isipokuwa wale aliowahi kudai hawawezi kumuacha hata akimpiga mtu risasi hadharani mtaani...hao ndio hivi sasa anazunguka akiongea nao. Kwa umbumbumbu wake anaamini siku zote watakuwa naye ila asichoelewa ni kwamba muda si mrefu hata wao wataanza kuhoji kulikoni?

Angekuwa na akili angetulia na kujiuliza kama wapo watu (wadadisi wa mambo) wanazo info zozote juu yake ambazo wanasubiri tu muda muafaka wazianike. Kinachowazuia kwa sasa ni unyeti wa hizo info na inabidi wajipe muda unaotosha kuzihakiki na kujiridhisha kwamba ni za kweli ama hapana. Matendo na matamshi yake ndiyo yatamkaanga.

Mtu ana mwezi moja tu madarakani na tayari anahusishwa na kashfa kibao na hata ungekuwa shabiki wake wa kutupwa ni lazima uanze kujiuliza maswali kadhaa. Akae chonjo sana na huu ugomvi wake na vyombo vya habari, mwisho wake hauwezi kuwa salma kwake. Anatoa nafasi ya kuchokonolewa zaidi na kila anapofungua mdomo wake anajizika zaidi na zaidi.
 
Kambi ya Trump kila mara wanajikuta kwenye wakati mgumu kujaribu kufafanua, kutetea au kuzipooza kauli kauli tata za kiongozi wao. Na hapo wana hofu kubwa kwamba wasipokuwa makini uchaguzi wa mid term mwakani 2018 republicans wanaweza kushindwa vibaya kwenye viti vya senate na congress na kuwapa fursa democrats kuchukua usukani. Endapo hili litatokea democrats kuchukua uongozi wa bunge Trump atajikuta kwenye wakati mgumu Zaidi na anaweza hata kuwa impeached.
 
Trum amerudi jukwaani, kasisitiza kutimiza ahadi zake
=======
Keeping promises

“Basically, all I have done is keep my promise,” Trump said, reminding CPAC attendees of his campaign platform and the steps he has taken to implement it – from cracking down on illegal immigrants and building a border wall to repealing Obamacare and reviewing “terrible” trade deals.

“Remember the lie, 28 times? ‘You can keep your doctor, you can keep your plan?’ Over and over you heard it. So, we’re going to repeal and replace Obamacare,” he said, referring to his predecessor’s pitch for the healthcare mandate.

“Politically, the best thing to do is nothing. Let it implode. Two years, don’t do anything. Democrats will come to us and beg,” he said. “But it’s not the right thing to do to the American people.”

“The era is empty talk is over. Now is the time for action,” Trump said

==>‘Fake news, military budget, trade deals’: Trump speaks at CPAC
 
Back
Top Bottom