Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

Breaking News!
A federal appeals court refused Thursday to reinstate President Donald Trump's ban on travelers from seven predominantly Muslim nations, dealing another legal setback to the new administration's immigration policy.

In a unanimous decision, the panel of three judges from the San Francisco-based 9th U.S. Circuit Court of Appeals declined to block a lower-court ruling that suspended the ban and allowed previously barred travelers to enter the U.S. An appeal to the U.S. Supreme Court is possible.

The court rejected the administration's claim that it did not have the authority to review the president's executive order.

Ruling: 3-0
 
9th Circuit Court of Appeals (“nutty 9th” or the “9th Circus”) is the most liberal Court of Appeals in the US.

Its ruling is not a surprise to many.

'SEE YOU IN COURT'
 
9th Circuit Court of Appeals (“nutty 9th” or the “9th Circus”) is the most liberal Court of Appeals in the US.

Its ruling is not a surprise to many.

'SEE YOU IN COURT'
Mpaka sasa Trump kapigwa chini mara mbili mbele ya majaji wanne; conservatives wawili na liberals wawili. Awali wataalamu wengi wa Sheria na Katiba walimshauri asikate rufaa, yeye kama kawaida alivyo king'ang'anizi akakaidi. Na hata sasa anashauriwa kwamba hili shauri likifika Supreme Court kama lilivyo hawezi kushinda na badala yake ni heri ajikite katika kuandika Executive Order upya inayoweza kusimama mbele ya korti.
 
Hii kesi itachukua muda kufikia tamati huko Supreme Court kwa sababu itahusisha mjadala mrefu wa kikatiba juu ya mamlaka ya rais na ukomo wake na kama executive order imekiuka katiba au la.
 
Mpaka sasa Trump kapigwa chini mara mbili mbele ya majaji wanne; conservatives wawili na liberals wawili. Awali wataalamu wengi wa Sheria na Katiba walimshauri asikate rufaa, yeye kama kawaida alivyo king'ang'anizi akakaidi. Na hata sasa anashauriwa kwamba hili shauri likifika Supreme Court kama lilivyo hawezi kushinda na badala yake ni heri ajikite katika kuandika Executive Order upya inayoweza kusimama mbele ya korti.

Na hii case ikienda Supreme Court na Trump Administration ikashinda utasemaje?
 
Trump kakubali yaishe!?

=====
Amempigia simu Xi ili waboreshe uhusiano wa US na China. Trump kakubali one china policy!
Trump speaks with China’s Xi, agrees to uphold ‘One China’ policy
Nadhani utakubaliana nasi kuwa wakati tunaongelea hili suala tulikuwa na ufahamu mzuri tu

Kwanza, tulieleza jinsi dunia ilivyofungamana

Unakumbuka uhusiano tuliosema wa 'Trump na Russia maswahiba, kisha Israel na US undugu, halafu China na Russia dhidi ya US, na Russia na Iran.
Tukamalizia na US na Mexico tukieleza, emerging market za BRICKS, EU na US.
Tulieleza karata ya North Korea na Nyuklia deal pamoja na middle east zitakavyomsumbua

Tuliweka perspective, US haiwezi kuwa na policy zisizofungamana na dunia kwasababu za kiuchumi na kiulinzi.

Ndicho kinatokea, tulibezwa na mashabiki na manazi kwa mayowee tu

Trump sasa anampigia simu Rais wa Mexico baada ya tweet kujibiwa kwa tweet!

Tukasema one China policy si sera ya Marekani ni ya China tangu Reagan na kwamba Trump hana ubavu wa kwenda kinyume

Trump alitaka kuitumia Taiwan kama weakness ya China bila kujua China ni second economy na trade partner wa Marekani. China inabeba karata ya N.Korea na Iran

Mexico imebuma, China deal anajirudi, Iran karudi katika sera za OB
Karudi katika sera za Obama si za ndani hata za nje ni pamoja na Obamacare

Utakumbuka tulieleza Obamacare basically ni template ya Republican.
Leo hawawezai kuifuta, hawana wazo mbadala na wala Trump hana

Haikufutwa siku ya kwanza na kila mmoja anaitumia kwa mwaka au zaidi
Obama wala hatetei , wanaotetea ni wananchi wenyewe. Legacy!

Kuongoza Taifa si sawa na kuongoza kampuni. Hilo linajidhihirisha katika kesi ambayo ameshindwa mara mbili. Hakuwasiliana na DOJ wala wanasheria.

Alimtumia R.Guillian ambaye alimwaga 'mchele' sera aliyopendekeza ilihusu Waislam

Katika kesi aliyoshindwa, suala si haki ya exec order au nia.
Tatizo hakujua nchi inaongozwa kwa utawala wa sheria, ndipo alipokwama

Hilo lnajidhihiri kwa washauri wake kama Kellyanne Conway.
Utakumbuka tulisema huyu ni wa kupuuzwa kuanzia mwanzo.

Conway kaenda kutangaza biashara za Ivanka akiwa katika ofisi ya umma
Kwingine inawezekana siyo US ambapo kila kitu kinaangaliwa kwa mantiki

Hakufuata maadili na hilo tayari limeleta tatizo ingawa ameomba radhi

Sasa utajiuliza kwanini Trump anajirudi?
Jibu ni kuwa timu yake ya watu kama akina Tillerson wanaoijua dunia kiuchumi na fungamano la siasa wameanza kumsaidia

Mwanzoni hakuelewa kabisa kuwa oval office siyo Trump tower

Tusemezane
 
Hii kesi itachukua muda kufikia tamati huko Supreme Court kwa sababu itahusisha mjadala mrefu wa kikatiba juu ya mamlaka ya rais na ukomo wake na kama executive order imekiuka katiba au la.
Ni kweli Rais anayo madaraka makubwa lakini ukomo wake ni Katiba na hii ndiyo sababu mpaka sasa Trump kapigwa chini mbele ya majaji wanne tofauti.
Na hii case ikienda Supreme Court na Trump Administration ikashinda utasemaje?
Hii case ikienda kama ilivyo mbele ya Supreme Court nafasi ya Trump administartion kushinda ni finyu na huenda ikazua maswala mazito zaidi kuliko hiyo. Ziko kesi nyingi tu zinasubiri kufunguliwa dhidi ya utawala wake kuhusiana na tuhuma za kukiukwa kwa vipengele vya Katiba na asipoangalia hiyo miaka yake minne inaweza kutawaliwa na kesi moja baada ya nyingine.

Hiyo Executive Order ya travel ban yake ya hovyo isiyozingatia Katiba imeipa Airline Industry hasara ya mamilioni ya dola (karibia USD 200,000,000). Tukiacha hiyo imeleta usumbufu mkubwa (suffering) kwa raia na wakazi halali wa Marekani na ndugu zao. Huko kukurupuka pia sasa kunahatarisha ajira ya msemaji wake Kelly-anne Conway na kuna uwezekano wa kushtakiwa.
 
Kwani Obama hakushtakiwa?

Kwani Obama hakuwahi kushindwa kwenye Supreme Court?

Sir, kesi lazima ziwepo hata zisizo na kichwa wala miguu!! Dept of Justice za Administrations zote zilikuwa na kesi nyingi za kudeal nayo!! Kwahiyo hamna cha ajabu kwenye huo utabiri wako.

Una uhakika hiyo Order haijazingatia katiba?

law.jpg


Halafu wakati unaongelea hasara ya USD 200,000,000 kwenye Airline industry kutokana na restriction, Unajua ni hasara kiasi gani US walipata kutokana na Sanctions ambazo Obama aliwapiga Russia?
 
Kwani Obama hakushtakiwa? Kwani Obama hakuwahi kushindwa kwenye Supreme Court?
Una tofauti gani na wale limbukeni ambao kila tukimkosoa Rais wetu Magufuli wanamtaja Lowassa...hata hivyo hongera, naona ajabu leo hujamtaja Clinton!
Una uhakika hiyo Order haijazingatia katiba?
Uliisikiliza hukumu iliyotolewa? Trump administration baada ya kugundua uharamu wa Executive Order kama ilivyotolewa siku ya kwanza kwa maandishi, walijaribu kujitetea kwa madai kwamba order hiyo ya awali ilikuja kufanyiwa marekebisho baadaye bila kujua kitendo hicho hakikubaliki. Ndio maana wataalamu wanamshauri Trump aandike mpya inayozingatia matakwa ya Katiba.
Halafu wakati unaongelea hasara ya USD 200,000,000 kwenye Airline industry kutokana na restriction, Unajua ni hasara kiasi gani US walipata kutokana na Sanctions ambazo Obama aliwapiga Russia?
Obama, Obama, Obama...hivi nyie watu mna tatizo gani? Je umesikia jinsi wasaidizi wa Trump walivyojaribu kumhujumu Obama kwa kuiwekea vikwazo Urusi?
 
Obama, Obama, Obama...hivi nyie watu mna tatizo gani? Je umesikia jinsi wasaidizi wa Trump walivyojaribu kumhujumu Obama kwa kuiwekea vikwazo Urusi?
Mwanzo walikuja na hoja kuwa Trump amekwenda ku shake up Washington.

Kadri muda unavyosonga mambo yanabadilika

Utetezi rahisi ni kusema Obama alifanya abcd. Sasa kama wanamtuhumu kusababisha matatizo iweje wafanyie kazi na utetezi wao kwa template yake?

Kwamba kama Obama ilileta hasara ya Bilioni 1 hiyo ina justifu Trump kufanya nyingine! please ! yaani argument hadi mtu unajiuliza, just for the sake of!

Trump alijaribu kufanya distortotion ya exec order. Ukweli ukajulikana

Wakafanya distortions ya mambo mengine. Obama akatuma salam kuwa yupo alipo

Mfano ni deal ya Iran ambayo kitabu cha Obama ndicho kinatumiwa to the letter

Shambulio la Yemen walichukua credit na kusema ni amri ya Trump.
Spicer akasema limefanyika kwa ufanisi.

Baada ya backlash ya society wanasema mpango ulianza wakati wa Obama

Ndivyo ambavyo akina Ted Cruz hawaelezi ACA yao ipo wapi wanashambulia Obamacare

Haya yote ni kwa lengo la kutafuta utetezi baada ya kuanza vibaya na kwa failures

Ni katika kutafuta kujificha na kumchafua Obama

Kitu kizuri na ningependa waendelee nacho, kadri wanavyomshambulia Obama kuna mambo mengi yanajulikana aliyafanya katika oval office kimya kimya

Hapa ndipo Legacy ya Obama ilipo, the man stands tall
 
Hatimaye Ikulu ya Trump yakubali yaishe baada ya rufaa yake kutupwa na jopo la majaji watatu kwani kuendelea kulishupalia agizo hilo kunaweza kuzua utata zaidi. Sasa wanapanga kurudi mezani na kuanza kuandika Executive Order mpya na makini itakayozingatia sheria na isiyoenda kinyume na Katiba ya nchi.

Hii imekuja baada ya kuona uwezekano wa kupata ushindi kwenye Supreme Court ni mdogo kwa namna amri hiyo ilivyotolewa mwanzo na kusainiwa kwa mbwembwe na Trump. Hili ni pigo na linatoa funzo kwa uongozi huu mpya chini ya Trump kuwa makini zaidi katika utekelezaji wa shughuli za kila siku za serikali.

CC: El Jefe
 
Hatimaye Ikulu ya Trump yakubali yaishe baada ya rufaa yake kutupwa na jopo la majaji watatu kwani kuendelea kulishupalia agizo hilo kunaweza kuzua utata zaidi. Sasa wanapanga kurudi mezani na kuanza kuandika Executive Order mpya na makini itakayozingatia sheria na isiyoenda kinyume na Katiba ya nchi.

Hii imekuja baada ya kuona uwezekano wa kupata ushindi kwenye Supreme Court ni mdogo kwa namna amri hiyo ilivyotolewa mwanzo na kusainiwa kwa mbwembwe na Trump. Hili ni pigo na linatoa funzo kwa uongozi huu mpya chini ya Trump kuwa makini zaidi katika utekelezaji wa shughuli za kila siku za serikali.

CC: El Jefe
Asante sana kwa taarifa. Nitafurahi mara nyingine mkipata habari kama hizi muwe mnaweka na vyanzo vyake.
 
SAKATA LA RUSSIA NA WAPIGA KURA 'FAKE'

Tunarudi nyuma kidogo kukumbusha kuhusu suala la wapiga kura haram 3-5M aliosema Trump

Trump alipotoa kauli ya kuunda tume kuchunguza wapiga kura haram tulisema hivi
1. Ima alifanya hivyo katika kuondoa watu katika mijadala kama la marufuku za Visa
2. Au alikusudia ili kutafuta mbinu za kujenga 'uhalali' wa madai yake popular vote

Tuleleza hakuna ushahidi wa madai na historia inaonyesha si zaidi ya watu 1000 kipindi cha miaka kadhaa waliowahi kushtakiwa na kuhukumiwa kutoka na upiga kura haram

Republican hawakuta uundwaji wa tume, walikataa hata kusikia madai hayo

Walichotaka kuepuka ni fedheha lakini pia kuamsha mambo mengine

Hawa Republican wanajua tatizo linalotokana na kuendeleza chunguzi

Ugomvi wa Trump na media akiwaita dishonest people nao haukuwa mzuri

Waandishi wanatabia ya kuthibitisha mtu kwa ukweli au uongowanapotuhumiwa

Sakata la Russia kuingilia uchaguzi linarindima kwa nyuma na kwa kasi.
Hakuna hitimisho hadi sasa, inatosha kusema linarindima kichini chini na kwa nguvu likifuatiliwa na wale aliowaita 'fake'

Sec of press kaulizwa na kauli yake ilikuwa 'uchaguzi umekwisha na Trump alishinda, muhimu ni kujielekeza kwa kazi anazotengeneza na hatua anazochukua'

Hapa kuna tatizo.

Ikiwa Trump aliona haja ya kuunda tume ya kuchunguza wapiga kura haramu, ni kwa vipi basi aone uchunguzi dhidi ya Russia kuingilia uchaguzi si tatizo la kuzungumziwa?

Rais Trump hakuona mahesabu ya siasa . Kuunda tume kunajenga mazingira ya uchunguzi dhidi yake.

Ugomvi na media unakoleza udadisi wa suala hilo na ugomvi na IC utam prove wrong

Tusemezane
 
TARATIBU YANATIMIA

SIASA ZA DUNI SIYO ZA KISHABIKI, ZINA MANTIKI

Wanajamvi, mtakumbuka tuhuma zilizoelekezwa kwetu kwamba hatuko fair kwa Trump
Tulisema kinachofanyika ni kuziangalia siasa za nchi zilizokomaa kwa mantiki si ushabiki

Baadhi ya wenzetu walisombwa na kauli za akina Kellyanne Conyway, Trump anabadilisha mwelekeo wa US katika siasa za ndani na nje.

Tulisema, US ina siasa 'core' zisizobadilika kirahisi hata kama viongozi wanabadilika

Taratibu kila tuliyojadili yanajitokeza kwa upana na uhalisia wake, ndivyo tutakavyojadili

1. Obamacare imesemwa na Trump ni 'very complicated' huenda ikakamilika mwaka 2018
Tulihoji wakati wa kampeni, sera yake iko wapi?

Wenzetu wakasema atafuta kwa kalamu siku ya kwanza ili kuondoa legacy ya Obama. Walisema bila kujua uzito wa ACA kijamii, siasa na uchumi

ACA ni hadithi kwasababu mwaka 2018 ni kuelekea midterm. Ugumu wa ACA unaweza kusababisha kupoteza congress, likely senate ambayo tofauti ni maseneta 3 na VP

Joto linapanda kiongozi wa Republican kuzomewa na kukatisha mkutano jimboni

Kwa lugha rahisi Obamacare haitafutika na ikifutwa itafuta wengi katika congress

2. Ya Mexico, ukuta hautalipwa na ukijengwa atakayelipa ni mlipa kodi wa US
Wakati sera za GOP ni 'fiscal conservatism' moja ya sifa zake ni kupunguza kodi

Hilo Trump atalifanya hivi karibuni kutekeleza ahadi

Tatizo linalomkabili na kusigishana na House na senate chini ya GOP.
Kwanza, kutafuta pesa za infrastructure inayokusidiwa.

Pili, Kupunguza kodi kunako athiri ongezeko la deni la Taifa

Republican watakubalianaje na ujenzi unaoongeza deni ?
Endapo mwananchi atalipia, nalo litakuwa na impact kwa kuelekea midterm.

3. Tukaeleza dunia ilivyofungamana kiuchumi na kisiasa, kwamba sera za America first zitaiweka US katika wakati mgumu

Tukumbuke mkanganyiko tuliowahi kusema mapema kabisa

Uhusiano Trump na Russia, US na Israel, China na US, N.Korea na China, Russia na Iran, china na Russia, US na Europe, Middle east na US, Israel na middle east, Japan na Korea, Japan na US

Katika kampeni Trump kwa kuelewa au makusudi ya kupotosha wafuasi wanaodhani ana mwelekeo mpya kama tunavyosikia na kusoma alizungumza bila kujali mahusiano hayo.

Tayari yupo katika rekodi ya kumshambulia Russia UN. Kabadili mismamo kuhusu Taiwan, anaongea na Shinzo Abe wa Japan na kuahidi kuwa nyuma ya Japan 100%

Upande wa pili, North Korea imeendelea na majaribio ya makombora ikiwa ni salam za China kujibu karata ya Trump kuitumia Taiwan ku negotiate na China.

Trump aliahidi kuondoa majeshi nje na kufikiria kuruhusu nchi kama Japan kumiliki silaha za Nyuklia. Leo anasema yupo nyuma ya Japan 100%. Kulikoni? nyuma bila majeshi?

Inaendelea
 
Inaendelea

ZIARA YA SHINZO ABE, PM WA JAPAN

Ziara hii imetokea katika muda mfupi tangu alipokutana na Obama na Trump
Ziara imelenga mambo mawili makubwa, uchumi na usalama

Rais Trump alioingia madarakani alikutana na CEOs wa makampuni ya magari ya America
Hilo liliacha makampuni kutoka nje katika taharuki kubwa

Dhana ya Trump ilikuwa America first. Makampuni ya nje yakasema yataendelea kutengeneza magari Mexico yakiwemo ya Japan na Ujerumani.

Katika kutafuta win win situation Trump amekutana na Abe.Mkakati mzuri sana

Japan inataka iwe na access na soko la US ambako makampuni yake yamefanya vizuri

Katika mwaka 2016 makampuni sita ya kwanza katika uuzaji US ni kutoka Japan
Na mwaka huo huo katika kampuni 10 za North America, sita ni zaJapan

Soko la US ni muhimu kwa Japan na Shinzo inaelekea amefika kutetea masilahi ya nchi

Upande mwingine Trump anataka kuyarudisha makampuni hayo kutengeneza ajira

Katika soko la dunia, 'vita' ya biashara na Japan haitakuwa na matokeo mazuri kwa US
Japan ni mshiriki mkubwa wa biashara na US,pia anatawala kiasi biashara za dunia

Katika kuhakikisha kuna win-win situation, Shinzo ametumia 'udhaifu' wa US kuchomeka hoja ya hatari ya N.Korea na majaribio ya makombora, ni katika joint conference

Jaribio la makombora limekuja baada ya Trump kuwa na maongezi na kiongozi wa China

Hili linafuatilia mtafaruku baada ya Trump kukurupuka na kuanza mahusiano na Taiwan

China imetumia karata ya N.Korea katika kuhakikisha Trump anarudi mezani, na amekiri kutambua sera ya one China.

Hili ni sawa na lile la Mexico ambapo Trump alidhani ni rahisi rahisi

China ina karata nyingine muhimu ya Iran ambayo nayo kama Korea imekunjua makucha

Kitendo cha Shinzo 'kumlazimisha' Trump kuunga mkono Japan kwa 100% tayari kimevunja hoja ya kampeni.

US haiwezi kuunga mkono bila majeshi. Je, aliyosema Trump ataondoa majeshi ndiyo hayo?

Tulisema mwanzoni kabisa kuwa US haina majeshi nje kama burudani.
Kuna sababu za kiuchumi na kiulinzi. Gharama haziepukiki na wala kuyaondoa

Hili la Japan linaingia katika orodha ya mambo aliyoshindwa kabla ya kuyaanza

Tusemezane
 
Hatimaye Ikulu ya Trump yakubali yaishe baada ya rufaa yake kutupwa na jopo la majaji watatu kwani kuendelea kulishupalia agizo hilo kunaweza kuzua utata zaidi. Sasa wanapanga kurudi mezani na kuanza kuandika Executive Order mpya na makini itakayozingatia sheria na isiyoenda kinyume na Katiba ya nchi.

Hii imekuja baada ya kuona uwezekano wa kupata ushindi kwenye Supreme Court ni mdogo kwa namna amri hiyo ilivyotolewa mwanzo na kusainiwa kwa mbwembwe na Trump. Hili ni pigo na linatoa funzo kwa uongozi huu mpya chini ya Trump kuwa makini zaidi katika utekelezaji wa shughuli za kila siku za serikali.

CC: El Jefe

Options zote tatu zipo mezani, wala uamuzi kuhusu option ipi ichukuliwe haujafanywa.

Wewe unasema EO ya Immigration imeenda kinyume na katiba, unaweza kuniambia katika ruling ya 9th circuit USCA wali-cite provisions zipi za statute au constitution ambazo zimekuwa contravened?

Pia ifahamike kuwa 9th Circuit ndiyo USCA ambayo rulings zake zinaongoza kwa kuwa overturned kwenye SCOTUS (80% mwaka jana) ukilinganisha na circuits zote.

Katika sense of urgency, kuandika EO nyingine immediately ni optimal decision wala hiyo haimaanishi kuwa uwezekano wa kupata ushindi SCOTUS ni mdogo, tunasubiri Judge Neil Gorsuch apitishwe kwanza kuwa Ass. Justice ili conservatives wawe watano, hamna anayetaka tie huko SCOTUS.
 
Halafu niseme tu kwa wale watu wanaoshikilia bango Obamacare, kuwa haitafutwa na kwamba ikifutwa itafuta wengi Congress waelewe tu kwamba wataofutwa Congress mwaka 2018 ni Democrats na sio Republicans maana ni ya kwao.

Kuna watu wengi tu walimpigia Rais Trump kura kwa ahadi ya ku-repeal na ku-replace Obamacare maana ilikuwa na bado inawaumiza.

Sasa kuna Congressional Democrats wanachochea wananchi kufanya fujo kwenye Town halls za Republicans wakati wanaulizia alternative ya ACA iko wapi.

(a) Kuna Democrats wanaamini/wanaaminishwa kuwa Alternative ya ACA haipo na kwamba Rais Trump hana healthcare plan yake.

(b) Kuna Democrats wanaamini/wanaaminishwa kuwa kama Health Plan ya Trump ipo basi ni mbaya ukilinganisha na ACA na itawaacha watu 20M+ bila coverage.

Democrats wanataka Rais Trump aje na Healthcare Plan yake kabla ya Mid-term elections ya 2018 kwa matumaini kuwa ni mbaya ili waiponde then iwasadie kuongeza seats kwenye Senate.

Katika hilo Republicans wana either (a)mkakati na (b) njia ya ku-bypass filibuster ya democrats.

MKAKATI:

Rais Trump yupo smart sana, anawaacha wanapiga kelele, wakati hiyo Plan itakapofika Congress kabla ya Mid-term elections watakuwa na wakati mgumu either kulinda 'legacy ya Obama' au kupinga kila kitu kama wengi wao walivyoamua kufanya.

Na hiyo itaishia kuwa-cost wao zaidi kwenye Mid-term elections na Republicans wanaweza kupata Senators 60+, ukizingatia kuna Senators 10 (Democrats) wanaenda kwenye re-elections kwenye States alizoshinda Rais Trump.

KU-BYPASS FILIBUSTER:

Ili kupitisha mabadiliko ya kisheria kama health care law kunahitajika simple majority tu (51 votes). Ila Senate Minority (in this case Democrats) wanaweza ku-filibuster bills wasizotaka, ili kumaliza filibuster (cloture) kunahitajika Senate votes 60 (two-third) na Republicans wana 52 (simple majority).

Ina maana Senators 41 wanaweza kuwasumbua Republicans kwenye Senate katika ku-repeal na ku-replace Obamacare, Democrats wana Senators 46, hivyo wanaweza kuleta usumbufu.

Kuna kitu kinaitwa 'Budget Reconciliation' ilianzishwa na Congressional Budget Act ya mwaka 1974, inatumika ku-bypass filibuster na kuweza kupitisha mabadiliko au sheria mpya kwa simple majority. Pia kuna ka-rule kadogo kanaitwa 'Byrd Rule' inayoweza kuwa invoked na Senator kwenye reconciliation.

Democrats walitumia 'reconciliation' mwaka 2010 kupitisha Obamacare na Republicans waliitumia kupitisha Restoring Americans' Healthcare Freedom Reconciliation Act ya mwaka 2015 iliyokuwa ina-repeal Obamacare lakini Obama alii-veto Januari, 2016.

Hiyo Health Care Bill ya Republicans ilipita Senate (52-47) na House (240-181). Republicans walishindwa kwa sababu Rais alikuwa Democrat, mwaka huu wana kila tool muhimu ya kuwezesha ku-repeal ACA.

Ishu inakuja kwamba chama fulani hakiwezi tu kutumia Reconciliation Bill kila kikijisikia. Na hivyo kuna limit ya idadi ya Reconcilliation Bills tatu (3) tu kwa mwaka mmoja wa bajeti.

Kila mwaka Senate na House wana-establish budget resolution na reconciliation inafanya vipande vya budget resolution kuwa sheria. Senate inaweza kutumia elements tatu za Reconciliation (matumizi, mapato na kiwango cha deni la taifa) katika reconciliation bill moja au kadhaa.

Lakini kama Reconciliation Bill moja ikishatumia elements zote zatu hairuhusiwi kuwa na Bill nyingine hadi Congress wapitishe Budget resolution nyingine.

Katika Congress, Rais Trump na Republicans wanataka kupitisha Tax Reform kwa kutumia reconcilliation bill, na ita-affect elements mbili ambazo ni matumizi na mapato.

Kwahiyo sheria ya Congressional Budget inawazuia Republicans kutumia Reconcilliation Bill kupitisha healthcare law ya Rais Trump mwaka huu hadi Congress wapitishe Budget resolution nyingine mwaka unaofuata wa bajeti.

Point hapa ni PRIORITY, which one goes first, Rais Trump afanye lipi mwaka huu na lipi afanye mwakani. Amesema anataka afanye Tax reform mwaka huu ili kujaribu kupunguza kodi eg. Corporate 35% hadi 15% na kujenga Ukuta kati ya US na Mexico.

Sasa, hivi vitu mtu hawezi kuvijua bila kujua Congress inavyofanya kazi. Ndio maana Rais Trump anaona process ni 'complicated' na wananchi wengi hawaelewi hivi vitu.

Kwa mtu asiyejua atasema Rais Trump hana mbadala wa ObamaCare ndio maana anasema Repeal na Replace inaweza kufanyika mwaka 2018. The good thing ni kwamba with President Trump, it will be done.
 
'FAKE NEWS' ZINAPOKUWA ' NEWS'

Russia na hacking inarudi kwa nguvu

Gen Flynn aiweka WH njia panda, VP katika wakati mgumu

Kulikuwa na habari za kuchanganya umma lengo ni kuonyesha CNN inatangaza habari 'fake'
Wengi waliamini wengine tulitilia shaka. Futalia uzi huu mabandiko 441 Kuendelea.

Duru za Siasa: Matokeo ya Uchaguzi Marekani

Kuna habari za salacious siku CNN walipotoa habari zinazofanana zenye mantiki tofauti

Salacious wali publish report ya mtaalam wa M15 ya Uingereza akieleza ushiriki wa Russia

CNN walieleza habari katika 'dossier' intel comm iliyo wa brief Obama na Trump
CNN walieleza uwepo wa nyongeza ya kurasa ikihusisha uchunguzi wa afisa mst. wa M15

CNN hawaku publish nyongeza ya taarifa wala hawaku publish report ya salacious

Kilichofanywa na 'transition team' ni kuchanganya habari ili CNN ionekane ina habari fake

Katika uzi huo huo bandiko 444 na 448 tuliuliza maswali bila majibu
Tulihitimisha kwa kusema ni suala la muda tu tutafahamu ukweli au uongo na fake news

Habari iliyopo sasa hivi kutoka kwa CNN walioitwa fake ni kuhusisha uchunguzi wa Russia

Habari inasema Intel comm imeweza ku link taarifa na zile za afisa mstaafu M15(nyongeza)

Hili linaonyesha CNN hawakuwa na news fake, walichosema kuhusu briefing ni kweli

Kinachoendelea ni waandishi waliosemwa kutengeneza'fake' wa CNN wanaendelea kufuatilia timbwili.
Intel community inafuatilia kwa ukaribu na tayari wana link na uchunguzi unaendelea

Hakuna conclusion iliyofikiwa, kilichopo ni taarifa za uchunguzi kwenda mbali zaidi ya inavyodhaniwa

Wakati huo huo mshauri wa ulinzi na usalama wa Trump Gen Flynn aliwahi kukanusha kuwa simu yake na balozi wa Russia siku Obama alipoweka vikwazo haikuhusisha suala hilo bali maongezi ya kawaida

VP Pence alikwenda katika TV akitetea kauli ya Flynn.

Taarifa iliyopo intel comm imebaini maongezi ya vikwazo kati ya Flynn na Balozi wa Russia.

Gen Flynn amesema hakumbuki kama alizungumzia suala la sanction na balozi, akibabaika
Hili linaiweka WH katika wakati mgumu kwasababu linamhusu VP na Trump aliye tweet

Mchanganyiko wa hayo mawili pamoja na suala tax yatazua tatizo siku za mbeleni


Tusemezane
 
Back
Top Bottom