Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

Breaking News: 8 jaw-dropping lines from Trump’s phone calls with Mexico and Australia!

Simu alizopiga Rais Donald Trump kwa Marais wa Mexico na Australia baada tu ya kuapishwa mwezi Januari mwaka huu zimeanza kuvuja na zinatia aibu kweli kweli. Vuteni subira...
Tunarudi nyuma tuliposema ugomvi wake na media na jinsi anavyo zi attack si jambo zuri
Katika simu, Trump anamwambia Rais wa Mexico akae kimya kuhusu wall, wakati yeye anaeleza atajenga na wamekubaliana. Yaani anamweka Rais wa Mexico kikaangoni! Rais wa Mexico kasema kama no!

Kuna habari kuwa katika deal za biashara Trump husainisha watu makubaliano ya kutosema jambo husika
Hii ni katika kuficha taswira yake na ndivyo ilivyotokea kwa University fake. Kawalipa kawasainisha

Hata alipomtimua Prebius inaripotiwa walikaa kwa saa 1 wenyewe, baada ya hapo Prebius akawa mpole licha ya matusi kutoka kwa Mooch

Hawa watu anaotimua kwa tweet kama Comey na Prebius wana mengi vifuani, kwa US news ni 'mali'
 
Breaking News: 8 jaw-dropping lines from Trump’s phone calls with Mexico and Australia!

Simu alizopiga Rais Donald Trump kwa Marais wa Mexico na Australia baada tu ya kuapishwa mwezi Januari mwaka huu zimeanza kuvuja na zinatia aibu kweli kweli. Vuteni subira...

Leaking of classified information kwenda kwenye media ina-represent failure ya US Intelligence community.

Kwa IC kushindwa kuzuia leaks kunahatarisha usalama wa US. Leaks zinafanyika WH ambapo maamuzi mengi yanafanywa kila siku sidhani kama ni jambo la kushabikia.

Hopefully uchunguzi unaoendelea wa kamati za Judiciary na Intelligence kwenye House na Senate utakuja na solution.
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Mkopo aliopata kutoka benki ya serikali ya Urusi kwa ajili ya biashara zake.
Unaweza kututajia jina la hiyo 'benki ya serikali ya Urusi iliyompatia mkopo' Trump kwa ajili ya biashara zake.

Ilimpatia kiasi gani?
 
Donald Trump...Rais dhaifu na mwoga kuwahi kutokea nchini Marekani!

Rais wa Marekani Donald Trump kadhihirisha kwamba yeye ni kiongozi mwoga na dhaifu kuliko viongovi wote waliomtangulia na inaonekana anayemtia hofu zaidi si mwingine bali ni Rais wa Urusi Vladimir Putin. Trump aliingia madarakani kwa mbwembwe na kuanza kusaini maagizo ya kiutendaji (executive orders) hadharani huku akiwa amezungukwa na wasaidizi wake pamoja na waandishi wa habari. Lakini leo kasain mswada wake wa kwanza mkubwa uliopitishwa kwa kishindo na Congress ya Marekani kwa kificho bila mbwembwe kama kawaida yake.

Je ni kitu gani kinamtia woga hadi aufyate kama alivyofanya leo?

Jibu ni Vladimir Putin. Wamarekani walio wengi wanajiuliza ni kitu gani kimemsibu Rais wao hadi ashindwe kutoa hata tamko Wamarekani zaidi ya 700 walipotimulia nchini Urusi na balozi yao kutiwa hekaheka? Ingekuwa imetokea katika nchi yoyote ile Trump hangenyamaza ama kwa vyombo vya habari au mtandaoni kwenye twitter lakini hapa kabana kimya. Mswada ambao amelazimika kuusign ni ule unaoiwekea Russia vikwazo na amefanya hivyo shingo upande huku akiitupia Congress lawama kwa kuchukua hatua kama hiyo.

Je ni kwa nini Trump anamuogopa Putin kiasi hicho?

Tusemezane.

Ieleweke kwamba Rais Tump sio Rais wa kwanza wa US ku-sign bill asiyoipenda kisa tu ina veto proof votes (two-third kwa House na Senate).

Angeweza kui-veto lakini ingekuwa kazi bure maana kwa hizo idadi za kura ingerudi Congress wangeipitisha kuwa sheria bila hata saini yake.

Kila mtu alitegemea Russia ange-respond. Sasa wewe ulitaka Trump asifu Congress kwa kazi nzuri walioifanya? Hoja ya Trump ni kuwa hizo additional sanctions zinaharibu sera yake ya ku-get along with Russia.

Lakini tukumbuke pia kuwa US waliwahi ku-get along with Russia before. Kwa mfano kipindi cha JFK na Ronald Reagan. Kwahiyo Trump sio Rais wa kwanza wa US kutaka mahusiano mazuri baina ya nchi yake na Russia.

Political witch hunt ya 'Russia collusion' ndio imewaharibu members wa Congress. Uchunguzi wa 'Russia collusion' ni kitu ambacho Trump, team yake na kila mtu angetaka kuona inaisha haraka huku Mueller akiwa fair kwenye hitimisho lake.Naamini baada ya hapo Trump ataweza kuimarisha uhusiano baina ya US na Russia.

Trump amekuwa calm na kutoa lawama kwa Congress kwa kuharibu sera yake, ni kitu cha kawaida. Hata Obama aliwahi kulaumu Congress mara kibao kwa kumletea bills alizoona hazifai (bahati nzuri hazikuwa na veto-proof votes). Rais anapo-veto au kusaini bill asiyoipenda anapaswa kutoa maelezo na ndicho Trump alichokifanya.

Katika mazingira kama hayo ulitegemea Trump awaambie nini Russia ambao nao wame-respond?. Ni kwamba jitihada zake za kuboresha uhusiano na Russia zimerudishwa nyuma zaidi.
 
Unaweza kututajia jina la hiyo 'benki ya serikali ya Urusi iliyompatia mkopo' Trump kwa ajili ya biashara zake.

Ilimpatia kiasi gani?
Siwezi kuwatajia kwani mimi siyo mchunguzi, ila kuwa na subira kidogo; sijui kama unakumbuka kuwa katika mojawapo wa mikutano ya Don Jr na warusi iliyokuwa imefichwa ni ule wa Meneja wa Benki ya serikali ya urusi. Ukisibiri kidogo tu basi utasikia mengi; leo hii grand jury imeitishwa kufumua swala hilo. Isingekuwa hili, Trump asingekwa na wasiwasi namna ile kiasi cha kuficha tax return zake muda wote huu. Inawezekana kuwa special counsel tayari alishapata nakala za returns hizo kutoka IRS na zinaashiria mambo mabaya ndiyo maana akaitisha grand jury.
 
1. Nadhani zilikuwa chini kuliko kiwango kilichovukwa leo
2. January wamesema ilikuwa 20,000-point mark
------
Hata hivyo huku kwenye masuala ya miamala ya fedha ama forex, yaani walimu wangu, inabidi mfanye kazi ya ziada kunifundisha maana niko shallow mno. Ombi hili limfikie hata na mwalimu wangu wa masomo ya zaida El Jefe
Mkuu Tujitegemee, stock market index ni kipimo cha wastani wa bei za hisa kadhaa. Huo wastani ndio watu hutumia kuangalia performance ya soko kwa ujumla.

Kwa mfano, Dow Jones Industrial Average (DJIA) ni stock market index inayojumuisha hisa za makampuni makubwa 30 katika sekta ya viwanda. Nasdaq composite inajumuisha zaidi hisa za makampuni ya IT. S&P 500 inajumuisha hisa za makampuni makubwa 500 yaliyokuwa-listed kwenye NYSE au Nasdaq. Hizo ni Stock market index tatu zinazofuatiliwa sana US.

Dow ikipanda kwa mfano, haimaanishi bei za hisa zote 30 zimepanda, hapana, ina maana kuna hisa nyingi katika hiyo index zimepanda bei, au hisa chache kati ya 30 zimefanya vizuri sana na kupandisha wastani.

Kupanda kunamaanisha kuna taarifa nzuri za kiuchumi na pia kutoka kwenye kampuni au makampuni iliyo/yaliojumuishwa kwenye hiyo index ya soko la hisa. Kwa maana hiyo wawekezaji wapo optimistic au kwa maana nyingine wanategemea mazuri. Lakini pia index zinaathiriwa na taarifa za kisiasa kwani hizo taarifa zinaathiri bei za hisa.

Sasa sera za Trump zina-play part sana kwenye kupanda au kushuka kwa stock market index kama Dow Jones, S&P 500, au Nasdaq Composite. Zikipanda zinaashiria mambo mazuri ndio maana Trump anapewa na mda mwingine anajichukulia credit.

Dow haijawahi kufika point 22,000 katika historia. Ndio mara ya kwanza.
 
Panapofuka moshi hapakosi moto, halafu ndani ya WH kuna mvujishaji mzuri sana wa habari anaweka vitu hadharani piece by piece au pia inaweza ikawa ni Warusi ambao si ajabu wanajua kila afanyalo. Baada ya kuona DT hana msaada wowote kwao wameamua kumchoma taratibu.

Siwezi kuwatajia kwani mimi siyo mchunguzi, ila kuwa na subira kidogo; sijui kama unakumbuka kuwa katika mojawapo wa mikutano ya Don Jr na warusi iliyokuwa imefichwa ni ule wa Meneja wa Benki ya serikali ya urusi. Ukisibiri kidogo tu basi utasikia mengi; leo hii grand jury imeitishwa kufumua swala hilo. Isingekuwa hili, Trump asingekwa na wasiwasi namna ile kiasi cha kuficha tax return zake muda wote huu. Inawezekana kuwa special counsel tayari alishapata nakala za returns hizo kutoka IRS na zinaashiria mambo mabaya ndiyo maana akaitisha grand jury.
 
Follow the money:

170803135336-restricted-0803-trump-russia-mueller-investigation-large-tease.jpg

One year into the FBI's Russia investigation, Mueller is on the Trump money trail - CNNPolitics.com
 
Ieleweke kwamba Rais Tump sio Rais wa kwanza wa US ku-sign bill asiyoipenda kisa tu ina veto proof votes (two-third kwa House na Senate).
El Jefe, kumbuka kwamba hapa hatuongelei theluthi mbili za kura, hapana, tunaongelea kura 98-2 sawa na asilimia 98% za Senate na 419-3 sawa na asilimia 99% za House halafu Rais asite ku-sign...hii haijawahi kutokea!
Angeweza kui-veto lakini ingekuwa kazi bure maana kwa hizo idadi za kura ingerudi Congress wangeipitisha kuwa sheria bila hata saini yake.
Hangethubutu kui-veto hata kama haipendi na huu ni ushahidi mwingine kwamba kuna a very serious issue hapa...analinda nini hadi apinge maamuzi ya asilimia 98% ya Congress?
Kila mtu alitegemea Russia ange-respond. Sasa wewe ulitaka Trump asifu Congress kwa kazi nzuri walioifanya? Hoja ya Trump ni kuwa hizo additional sanctions zinaharibu sera yake ya ku-get along with Russia.
Sera yake? Una maana gani mwenzangu...kwamba sera za Trump zinapingana na sera za chama chake? Kweli unajua unachokizungumza? Kwamba Rais wa Marekani ana nguvu za kuweza kufanya maamuzi yanayopingana na Congress? Kwanza kaukwaa Urais si kwa kupata popular votes za Wamarekani, kapata Urais kwa kushinda electoral votes ingawa wapiga kura walio wengi walimkataa.
Lakini tukumbuke pia kuwa US waliwahi ku-get along with Russia before. Kwa mfano kipindi cha JFK na Ronald Reagan. Kwahiyo Trump sio Rais wa kwanza wa US kutaka mahusiano mazuri baina ya nchi yake na Russia.
Toka mwaka 1917 Marekani haijawahi ku-get along na Russia na hakuna wakati unaweza kudai mahusiano yalikuwa mazuri. Wanavumiliana tu.
Political witch hunt ya 'Russia collusion' ndio imewaharibu members wa Congress. Uchunguzi wa 'Russia collusion' ni kitu ambacho Trump, team yake na kila mtu angetaka kuona inaisha haraka huku Mueller akiwa fair kwenye hitimisho lake.Naamini baada ya hapo Trump ataweza kuimarisha uhusiano baina ya US na Russia.
Usiwe na haraka ndugu yangu...kama unaamnini uchunguzi unaofanyika ni witch-hunt, vuta subira. Bila shaka unaona Trump anavyojaribu kumpiga vita Special Counsel Muller, je anaogopa nini? Leo kahutubia base yale huko West Virginia na hotuba nzima anatafuta huruma ya wapenzi wake (wale wale aliodai hata akimpiga mtu risasi hadharani hawawezi kumuacha). Woga mkubwa umeanza kumuingia kipenzi chako na kwa sasa ni swala la muda tu.
Trump amekuwa calm na kutoa lawama kwa Congress kwa kuharibu sera yake, ni kitu cha kawaida. Hata Obama aliwahi kulaumu Congress mara kibao kwa kumletea bills alizoona hazifai (bahati nzuri hazikuwa na veto-proof votes). Rais anapo-veto au kusaini bill asiyoipenda anapaswa kutoa maelezo na ndicho Trump alichokifanya.
Ya Obama yalikuwa tofauti kwani wakati huo Congress haikuwa mikononi mwa chama chake tofauti na sasa ambapo Congress yote iko mkononi mwa GOP. Trump hakutoa sababu yoyote zaidi ya kulialia kuwa inamweka pabaya yeye na wafadhili wake wa Kirusi.
Katika mazingira kama hayo ulitegemea Trump awaambie nini Russia ambao nao wame-respond?. Ni kwamba jitihada zake za kuboresha uhusiano na Russia zimerudishwa nyuma zaidi.
Hakuna kiongozi wa Marekani aliyewahi kukaa kimya huku taifa kama Urusi ikiwafukuza raia wake kama alivyofanya Putin. Tukumbuke pia jinsi Trump alivyomsifia Putin kwa kutojibu mapigo Obama alipowafukuza Warusi kwa tuhuma za ujasusi. What hold has the Russian President over the US President Donald Trump?
 
Siwezi kuwatajia kwani mimi siyo mchunguzi, ila kuwa na subira kidogo;

Ina maana uliandika kitu ambacho hukijui au unachokihisi. Kwanini wewe kwa upande wako hukuwa na 'subira kidogo' kabla ya kuandika vitu ambavyo huna uhakika navyo?

sijui kama unakumbuka kuwa katika mojawapo wa mikutano ya Don Jr na warusi iliyokuwa imefichwa ni ule wa Meneja wa Benki ya serikali ya urusi.

Ni mkutano baina ya Don Jr. et al. na 'meneja wa benki serikali ya Urusi' au na 'Mwanasheria aliyehusishwa na Russia'?

Ukisibiri kidogo tu basi utasikia mengi; leo hii grand jury imeitishwa kufumua swala hilo.

Grand jury imeitishwa kufumua suala la 'benki ya serikali ya Russia' na Trump?

Kitendo cha Mueller kuitisha grand jury ni kumpa uwezo wa kupata ushahidi wowote anaoutaka na kuwaonyesha grand jury ili waamue kama wanaochunguzwa wawe indicted au lah.

Sasa wewe umejuaje ushahidi ambao special counsel atau-subpoena wakati hajafanya hivyo? Au ndio muendelezo wa kuhisi?

Isingekuwa hili, Trump asingekwa na wasiwasi namna ile kiasi cha kuficha tax return zake muda wote huu.

Kwa maoni yako, kuchunguza tax return za Trump za miaka 10 iliyopita (kabla Obama hajawa Rais) ni reasonable scope inayoendana na 'Russia collusion' story?

Uchunguzi lazima uwe na scope ambayo ni reasonable kulingana na facts of the case. Maana tax returns za Trump zinaweza kuchunguzwa hata za miaka 40 iliyopita, lakini hiyo, kama siyo kupoteza mda, itasaidia vipi kujibu swali la msingi?

Inawezekana kuwa special counsel tayari alishapata nakala za returns hizo kutoka IRS na zinaashiria mambo mabaya ndiyo maana akaitisha grand jury.
Special counsel kuitisha grand jury ni sehemu ya process, inayoashiria uchunguzi unaelekea mwishoni.

Kwanza inampa special counsel uwezo wa kutoa subpoena ya ushahidi (watu kuja kutoa ushahidi+documents) kama hajapata ushahidi wote lakini pia kwa wao kuamua kama kuna wrongdoing ambayo inayoweza kupelekea kuwa charged.

Badala ya kuhisihisi kama Mueller amepata documents fulani au hajapata, na kuendekeza kuwa ahead of investigations zinazoendelea, kwanini usi-deal na kile ulicho na uhakika nacho kwanza?
 
Siwezi kuwatajia kwani mimi siyo mchunguzi, ila kuwa na subira kidogo; sijui kama unakumbuka kuwa katika mojawapo wa mikutano ya Don Jr na warusi iliyokuwa imefichwa ni ule wa Meneja wa Benki ya serikali ya urusi. Ukisibiri kidogo tu basi utasikia mengi; leo hii grand jury imeitishwa kufumua swala hilo. Isingekuwa hili, Trump asingekwa na wasiwasi namna ile kiasi cha kuficha tax return zake muda wote huu. Inawezekana kuwa special counsel tayari alishapata nakala za returns hizo kutoka IRS na zinaashiria mambo mabaya ndiyo maana akaitisha grand jury.
Uchunguzi kwa sasa umejikita zaidi katika mambo matatu yanayomhusu Donald Trump...
  1. Collusion with Russia
  2. Obstruction of Justice
  3. Financial dealings (crimes)
 
El Jefe, kumbuka kwamba hapa hatuongelei theluthi mbili za kura, hapana, tunaongelea kura 98-2 sawa na asilimia 98% za Senate na 419-3 sawa na asilimia 99% za House halafu Rais asite ku-sign...hii haijawahi kutokea!

Ilishawahi kutokea tena sio mbali, mwaka jana (2016), kipindi cha Rais Obama.

Bill ya Justice Against Sponsors of Terrorism Act (JASTA) ilipitishwa Senate bila kupingwa hata na Senator mmoja (unanimously), yaani ilipita kwa 100%.

Ikatoka Senate ikaenda House, huko nako ikapita bila kupingwa (100%).

Rais Obama sio tu alisita ku-sign alii-veto!. Wakati unashangaa 98% au 99% unasahau kuwa Obama ali-veto kilichopitishwa na Congress kwa 100% both chambers.

Ilivyorudi Congress, Senate waka-override veto ya Obama (97-1). House nao waka-override veto ya Obama (348-77). Na ikawa sheria bila saini ya Obama.

Hangethubutu kui-veto hata kama haipendi na huu ni ushahidi mwingine kwamba kuna a very serious issue hapa...analinda nini hadi apinge maamuzi ya asilimia 98% ya Congress?

Obama alikuwa analinda nini kupinga maamuzi ya asilimia 100% kwenye JASTA? Na sio tu alithubutu, bali alii-veto maamuzi ya 100% ya Congress.

Unahisi kulikuwa na 'very serious issue'? Au 'very serious issue' ni kwa Trump tu?

Sera yake? Una maana gani mwenzangu...kwamba sera za Trump zinapingana na sera za chama chake? Kweli unajua unachokizungumza? Kwamba Rais wa Marekani ana nguvu za kuweza kufanya maamuzi yanayopingana na Congress? Kwanza kaukwaa Urais si kwa kupata popular votes za Wamarekani, kapata Urais kwa kushinda electoral votes ingawa wapiga kura walio wengi walimkataa.

Obama aliweza kupingana na maamuzi ya Congress na ilikula kwake.

Kwani umeambiwa ni lazima Trump aifuate Republican party platform katika maamuzi yake? Hata hivyo, historia inaonyesha POTUS wengi huwa hawafuati platform za vyama vyao wakati wa utekelezaji wa sera zao.

Tumerudi kwenye mambo ya popular vote tena? Wapiga kura wengi waliomkataa Trump ni wa California na New York, bahati nzuri walishindwa kumzuia kuwa Rais. Trump alishinda swing States 9 kati ya 13. He has 'no way' ikabadilika he is the 45th POTUS. Get over it.

Toka mwaka 1917 Marekani haijawahi ku-get along na Russia na hakuna wakati unaweza kudai mahusiano yalikuwa mazuri. Wanavumiliana tu.

Vipi kuhusu mahusiano kati ya US na Cuba? Rais Obama alifanyaje?

Au kujenga uhusiano akijenga Obama ni sawa ila akijenga Trump sio sawa? Acha double standards mkuu.

Usiwe na haraka ndugu yangu...kama unaamnini uchunguzi unaofanyika ni witch-hunt, vuta subira. Bila shaka unaona Trump anavyojatibu kumpiga vita Special Counsel Muller, je anaogopa nini? Leo kahutubia base yale huko West Virginia na hotuba nzima anatafuta huruma ya wapenzi wake (wale wale aliodai hata akimpiga mtu risasi hadharani hawawezi kumuacha). Woga mkubwa umeanza kumuingia kipenzi chako na kwa sasa ni swala la muda tu.

Kwahiyo Trump akitoa concerns za genuine zinazohusu conflict of interest ya special counsel ni sawa na kumpiga vita? Na vipi wale R's walio Congress waliosema Mueller afutwe kazi mbona wao huwazungumzii au wewe unamuandama Trump tu? Naamini uliwasikiliza wanasheria wa Trump, ungejibu hoja zao badala ya kusema Mueller anapigwa vita.

But all in all, Special Counsel anakaribia kumaliza kazi yake ya 'uchunguzi', kwahiyo lets not get ahead of ourselves here.

Ya Obama yalikuwa tofauti kwani wakati huo Congress haikuwa mikononi mwa chama chake tofauti na sasa ambapo Congress yote iko mkononi mwa GOP. Trump hakutoa sababu yoyote zaidi ya kulialia kuwa inamweka pabaya yeye na wafadhili wake wa Kirusi.

Hata Obama alikuwa analia hadi na Democrats wenzake. Trump ametoa sababu tayari, labda kama wewe hujapenda sababu aliyotoa.

Obama aliingia madarakani akiwa na majority Congress AKAPOTEZA na hakuwahi kurejesha majority both chambers hadi akamaliza mda wake.

Hakuna kiongozi wa Marekani aliyewahi kukaa kimya huku taifa kama Urusi ikiwafukuza raia wake kama alivyofanya Putin. Tukumbuke pia jinsi Trump alivyomsifia Putin kwa kutojibu mapigo Obama alipowafukuza Warusi kwa tuhuma za ujasusi. What hold has the Russian President over the US President Donald Trump?

Mag3 huyo Putin we unamchukia kwa kipi hasa? Kwani US huwa hawaingilii uchaguzi wa nchi zingine?

Intelligence Communities zilisha-conclude kuwa 'Russia meddling' haikuwa na impact yoyote kwenye matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2016.

Ngoja D's waendelee kumtafuta mchawi ni nani, wakija kushtuka R's wana Senators 60+. Wengine kama akina Gov. Jim Justice (West V.) wanaendelea kuhamia R party.
 
Ilishawahi kutokea tena sio mbali, mwaka jana (2016), kipindi cha Rais Obama. Bill ya Justice Against Sponsors of Terrorism Act (JASTA) ilipitishwa Senate bila kupingwa hata na Senator mmoja (unanimously), yaani ilipita kwa 100%....
Hapana, unakosea, ilipita bila kupingwa ndiyo lakini haikupigiwa kura. The original vote was passed by a voice vote not requiring individual lawmakers to record their positions.
Obama alikuwa analinda nini kupinga maamuzi ya asilimia 100% kwenye JASTA? Na sio tu alithubutu, bali alii-veto maamuzi ya 100% ya Congress.
Obama alitaka a recorded vote of the positions of all lawmakers...kura ipigwe na kuhesabiwa ili kuweka rekodi sahihi kwa sababu alijua hiyo ya asilimia 100% haikuwa sahihi na kweli iliporudishwa ilipitishwa na Congress kwa asilimia 79% tu.
 
"
El Jefe, post: 22646257, member: 387168"]Leaking of classified information kwenda kwenye media ina-represent failure ya US Intelligence community.
Simu ya Trump haikuwa classified na hiyo siyo classified information.

Pili, Trump alisema anapenda 'leaks' na kushabikia Wikileaks . Imekuwaje leo!!

Tatu, Katika uzi huu tulieleza kwa kirefu tatizo la Rais Trump, intel community na Media
Tulisema ku attack 'fourth state' na Intel community ni kutafuta matatizo

Imechukua miezi 6 kukubaliana na analysis yetu ambayo uliita porojo na chuki. Karibu

Leaks zinazotokea zina source na sababu nyingi
1. Usidhani kumfukuza Comey wa FBI kwa tweet mkutanoni kulipendeza intel community. Ilikuwa ni uncivilized way, iliudhi wengi akiwemo DHS Jeff Session wakati huo

Kukanusha Russia meddling wakati IC zote zimetoa uthibitisho ni kudhalilisha IC.
Ndivyo alivyofanya jana Virginia ''witch hunt'' kwa maana IC zilikuwa wrong

Kumbuka meddling inaungwa mkono na Republicans na Democrats ndiyo maana senate ikapitisha 98-2, House 419-3 suala la vikwazo kwa Russia.

Congress inaamini IC, Trump hakubaliani na vyote viwili.
Kwa muktadha huo kuna 'juhudi' za kum prove wrong

2. Kuna internal strife and power struggle. Prebius na Scaramuuci ni kielelezo

Kuna Nepotism akina Bainon na Right wing wakiona kunyofolewa licha ya jitihada zao.

Kumtimua Prebius kwa kumtumia Mooch sijambo linalopendeza wengine.
Prebius ni sehemu ya 'the establishment' kumbuka na ana mengi anayojua

3. Kuna 'patriot' wanaoona mambo yanavyokwenda na kuamua lu leak info kunusuru nchi
Ndivyo James Comey alivyofanya kwa mujibu wake baada ya kuombwa kuwa loyal
Kwa IC kushindwa kuzuia leaks kunahatarisha usalama wa US. Leaks zinafanyika WH ambapo maamuzi mengi yanafanywa kila siku sidhani kama ni jambo la kushabikia.
Hapa ndipo Rais Trump anatakiwa ku 'drain the swamp' Hapaswi kulalamika bali kufanyia kazi
Kwanza alisema ni Obama loyalist ambao amewaengua wote. Analalamika nini?

IC haijashindwa , bali dharau ya Trump kwa IC ndilo tatizo kama nilivyoeleza hapo juu
Hopefully uchunguzi unaoendelea wa kamati za Judiciary na Intelligence kwenye House na Senate utakuja na solution.
Kuna msemo 'Hakuna siri Washington'
Trump si wa kwanza wala wa mwisho. Muhimu ni discipline kuanzia kwake mwenyewe
 
Senators push bill to protect Mueller - CNNPolitics.com

Hakuna mhimili uliojichimbia chini zaidi kuliko mwingine! Ebo! Rais anaweza kuwekewa kipingamizi cha kutimiza uchwara wake.
John McCain alipozungumza senate chamber alisema 'Leg branch and exec branch' zipo at par hakuna aliyejichimbia ardhini zaidi

Katika kuhakikisha Trump hafanyi atakavyo, Congress imepitisha bill ya vikwazo kwa ikaweka Veto. Kwamba Trump hawezi kubadili hadi bill iletwe katika congress tena

Kumfukuza Mueller hakutawezekana. Maseneta wa pande zote wanasema hilo likitokea basi watapendekeza congress iteue Independent prosecutor.
Mueller ni special counsel, lakini IP ana uwezo wa kufungua na kuendesha mashtaka

Pili, kumfukuza Mueller huku Trump akiwa tayari ametahadhrisha kuhusu financial deal kutaunganishwa na Comey na hapo vyama pembeni US kwanza. Itakuwa mbaya sana

Kwa kuhofia hilo leo imeripotiwa Mueller anaangalia financial deals za Trump
Tayari grand Jury imeundwa,haina maana kuna tatizo, inaonyesha investigation inaendelea.
 
Back
Top Bottom