Duru za siasa: Uchaguzi ni juu ya ilani/sera na hatma ya nchi

Sisi ni waoga sana wa kujijenga kifikra na kutafakari mambo. Hatupendi kujiuliza maswali mpaka tufike mwisho wa kuuliza na balbu ituwakie tujitambue.

Tunapenda kufanya delegation ya kila kitu.

Tuna wachumi wakutosha wanaoweza kutuliangalia taifa na kufanya mipango inayoendana na Sera na hata Ilani. W anachohitaji ni motisha na changamoto kubuni mfumo mizuri wa uchumi iwe ni kwenye kilimo, ufugaji, uvuvi, viwanda vidogo na hata vikubwa: processing and manufaturing na kwa sekta zote, binafsi na zilizo chini ya serikali.

Lakini badala ya kufanya empowerment na hata kutoa imani na kuwaamini wachumi wetu, tunathamini tafiti, tathmini na mapendekezo ya watu wasio Watanzania, wasio na mahusiano ya karibu na jamii kwa kuelewa kwa mapana na marefu maisha, tabia na mifumo yetu ya asili.

HIi peke yake inaweza kuwa ni Sera ya kuwawezesha wazawa.

Lakini kwa kuwa tafsiri na mtazamo wetu uko kwenye kumpa mtu cheo, fedha au dili, hatuoni sababu ya kuanza kuangalia ni jinsi gani wataaluma na wataalamu wa nyumbani wanavyoweza kutumika kujenga mfumo imara wa uchumi, uzalishaji, elimu, afya bila usiasasiasa na kujuanajuana.

Leo tukikaa chini na kufunguka na kuanza kuulizana the 6 to 8 why's on why Ujamaa na Kujitegemea vilitushinda au Azimio la Arusha, utakuta wengi wataishia why ya 2 au 3, na kuanza kunyoosha vidole vya lawama au kutoa sababu na si kurudi kwa undani mpaka tuweke orodha nono ya mambo yaliyosababisha Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ishindwe na tukaleta mapinduzi mapya ya Azimio la Zanzibar ambalo kipaumbele kimekuwa ni kujenga uchumi kwa kutegemea FDI na mikopo.

Kwa upinzani, wanachoweza kuhubiri mpaka waingie ikulu na kupimwa ni Sera na ahadi ambazo ni mpaka wazifanyie kazi, ndipo wananchi tunaweza kusema sera zao hazikuleta manufaa.

Lakini kutokuwa madarakani , hakuunyimi ukawa kujiandaa vizuri kuwa wepesi kuingia madarakani na kuanza implementation.

I would hope kuwa sasa hivi regardless ya matokeo, kuna jopo la wataaluma na wataalamu wa kila sekta na nyanja katika ukawa wakisuka vizuri sera zao collectively na kuonyesha mshikamano wa kuongoza nchi kwa ufanisi na si kuanza kubabaika tena kama suala la mgombea urais na wagombea udiwani na ubunge lilivyokuwa.
 
HATUHITAJI BAUNSA WA PUSH UP

TUNAHITAJI MABAUNSA WA 'BONGO ZA VICHWANI' MAONO, NA MIPANGO

TUNAHITAJI MAWAZO NA FIKRA ZA KIMAPINDUZI

Mapinduzi yanayoongelewa ni ya kumkwamua Mtanzania kutoka lindi la umasikini.

Miaka 50 hatuwezi kumsingizia mkoloni kwa shida zetu

Inasikitisha,tulidhani wagombea watajikita kueleza matatizo, kuyaanisha na kutupa njia za ufumbuzi

Tunaona wakitambiana kwa afya zao. Wameacha hoja, wanageuza majukwaa uwanja wa mabaunsa

Vituko haviishi, baada ya mabonanza ya wasanii sasa tunaona mengine.

Taifa hili halina upungufu wa mabaunsa na wala halihitaji baunsa

Tunahitaji ‘mabaunsa' wanaotumia vichwa vyao kujibu hoja za wananchi;

1 Tueleza kwanini sisi ni masikini kwa miaka 50.
Kwanini sisi ni kundi la nchi 25 masikini sana duniani, tukiwa pia kundi la HIPC

2. Baunsa atakayetueleza kwanini deni la taifa ni trilioni 40, tukiwa kundi la 25 na mwanachama wa HIP

3. Kwanini mfumo wetu wa elimu ikiwemo ufahamu ‘literacy' umepungua kutoka asilimia 90 sasa tupo 60

3. Atakayejibu hoja, ni vipi wazazi walale mzungu wanne, wao wakifuja, kuiba na kupora nchi

4 Lini tutaandika katiba ya nchi kulingana na sisi na wakti kama watu huru

Kilimo kwanza ilikwamaje na sasa wanakwamuaje

5. wanini chakula kinauzwa nje, halafu tunaagiza chagula.Kwanini hatuwezi kuhifadhi nafaka

6. Waeleze,kwanini waligeuza viwanda maghala yakuhifadhi chumvi,.

Orodha inaendelea

Haya ndiyo tunataka kuyasikia si kupiga push up majukwani.

Tunataka mabaunsa wanaopiga push up za ubongo

Hizi push up za majukwaani ni kielelezo cha kukosa fikra, hoja na maono

Tunahitaji vision na mission si wabeba vyuma. Tunataka kiongozi wa kuliunganisha taifa si Mr Tanzania

Tusipofikiri na kujiuliza, wakimaliza push up watatuambia ''Hawajui kwanini sisi ni masikini''
 
Nimezungumzia uchumi kijuujuu sana lakini kuna kitu cha kumjibu Rais Kikwete leo aliposema haelewi kwa nini Tanzania ni masikini.

Ama aliutaka Urais kama mbwembwe au hakujiandaa kuwa Rais.

Umasikini wa Tanzania unachangiwa na mkazi wa Dar kutumia masaa 6 barabarani akitoka nyumbani na kwenda kazini na kurudi nyumbani.

Mtu huyu ambaye anaamka saa 10 asubuhi kuwahi msukumo wa maji kwenye bomba na umeme wa Tanesco, hupndoka na kukaa barabarani. Akifika kazini, uchovu wa njiani humfanya aende kutafuta kifungua kinywa. Akirudi kazini, Tanesco wamefanya vitu vyao tena, joto kali, na huishia kwenda kutafuta lunch, na kubangaiza kupata walau fedha za mboga ya watoto. Akiwa amerudi kutoka lunch anawaza ya mme, mke na watoto, anawaza kama hausigelo na hausiboi walikumbuka kununua maji na kujaza simtank, anajiuliza kama Tanesco umeme ulirudi japo kwa masaa kadhaa. Anaiwaza safari ya kurudi nyumbani na hajui atafika nyumbani saa ngapi.

Mtu huyu wa Dar ambapo ndipo kitovu cha uzalishaji mali wa nchi kwa takriban 80% ya mapato kutokana na vitu ambavyo si Kilimo, madini na Mifugo, anapaswa kufanya kazi kwa masaa 8 kwa siku. uhalisia wa muda huyu ndugu anaotumia kufanya kazi kwa siku ni masaa 4, mengine productivity is almost zero.

Viwanda, madhirika makampuni yanayomtegemea mtu huyu wa Dar, nayo yanakumbwa na shida za maji na umeme. Fikiria hiki ni kiwanda cha kuzalisha pembejeo, zile boilers zinahitaji maji for cooling, zinahitaji umeme, zinahitaji mfanyakazi aliye attentive, lakini production cost na challenges za production zinafanya kiwanda kina shindwa kufikia malengo ya kuzalisha, mwenye kiwanda anatafuta mkubwa na kumuweka sawasawa na kuondolewa kodi ili aweze walau kupata kipato cha kulipa watu mishahara.

Just imagine kama kiwanda hiki kingekuwa na umeme na maji tosha na reliable labor kufika kazini wakiwa tayari na nguvu na mori na hata kiwanda kuwa na shift 2 hadi tatu, je tungekuwa na Rais ambaye haelewi kwa nini Taifa lake ni masikini pamoja na rasilimali zote zilisoko?
 
Tatizo ni lile lile la kwamba hakuna sera/Ilani. Mambo yanafanyika kutokana na utashi wa watu.

Ndivyo ilivyokuwa kwa elimu. Lowassa na JK walipoingia madarakani kulikuwa na mitazamo tofauti.

Lowassa akisisitiza kuhusu elimu , Jk akiwa hana uhakika nini kifanyike.
owassa alipoondoka , Pinda akaja na kilimo kwanza. Haikuwa sera wala ilani ya CCM.

Kilimo kwanza ilitangazwa bungeni kwanza, wataalamu wa kuunga unga wakapewa kazi kwa maagizo ya kuzingatia kilimo kwanza, na si planning. Kwamba wahakikishe wanafuata maagizo ya wanasiasa na si ya utaalamu wao. Utashi wa mtu au watu na si sera/Ilani

Nimedonoadonoa hoja yako na ukweli ni kwamba nafikiri madhaifu ya awamu ya nne yanatokana na "mamlaka ya juu" kukosa vision ya kitaifa hata kutumia kwa ufanisi mawazo ya PM wake kujenga taifa imara kupitia mfumo mzuri wa Elimu na KIlimo.

Utashi wa Lowassa wa elimu na wa Pinda wa kilimo, ulitakiwa ufanyiwe tathmini ya makini ya dharura na kupewa kipaumbele cha hali ya juu na hata kufanyiwa micro management na watu kama BRN walipaswa kuwa wanaouliza maswali yote ya kwanini kwanini na ilikuwa kwanini mpaka kieleweke.

Lakini hata kama nikimpa tano kwa sera ya kulitangaza Taifa kuwa mahali poa pa kuja kutalii na kufanya biashara, wenzetu wanatarajia kuwa watakuja kwenye nchi yenye fluid movement, si ukiritimba na umangimeza.

Wanatarajia wakija, kuna umeme, maji, competent labor force, functional systems za miundombinu, uchukuzi na kujali muda (time is Money).

Sasa tunaitangaza nchi kuwa kuna neema, hata watalii kuja kuangalia Tembo wananza kuuliza tembo wamejificha? kisha huamua kupitia kenya maana fluidity ya mambo Kenya ni bora kuliko Tanzania.

Hivyo kwa miaka 10, Kikwete amewekeza kuitangazia Tanzania kwa wawekezaji na kuwa kuna vivutio vya kutosha, lakini kama umeme na maji ni shida, basi projection zangu za income na growth lazima zifidiwe na hapo ndipo mtu anaomba msamaha wa kodi na ushuru kwa miaka 5 na anapewa!

Kama tunataka kuendelea, lazima tuwe na viongozi wenye vision na weneye uwezo wa kuweka sera zinazoeleweka na kuzifanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuunda timu na kuzimamia Sera ifanikiwe na si kuachwa kwa wengine waifanyie kazi!
 
Nimedonoadonoa hoja yako na ukweli ni kwamba nafikiri madhaifu ya awamu ya nne yanatokana na "mamlaka ya juu" kukosa vision ya kitaifa hata kutumia kwa ufanisi mawazo ya PM wake kujenga taifa imara kupitia mfumo mzuri wa Elimu na KIlimo.

Utashi wa Lowassa wa elimu na wa Pinda wa kilimo, ulitakiwa ufanyiwe tathmini ya makini ya dharura na kupewa kipaumbele cha hali ya juu na hata kufanyiwa micro management na watu kama BRN walipaswa kuwa wanaouliza maswali yote ya kwanini kwanini na ilikuwa kwanini mpaka kieleweke.

Lakini hata kama nikimpa tano kwa sera ya kulitangaza Taifa kuwa mahali poa pa kuja kutalii na kufanya biashara, wenzetu wanatarajia kuwa watakuja kwenye nchi yenye fluid movement, si ukiritimba na umangimeza.

Wanatarajia wakija, kuna umeme, maji, competent labor force, functional systems za miundombinu, uchukuzi na kujali muda (time is Money).

Sasa tunaitangaza nchi kuwa kuna neema, hata watalii kuja kuangalia Tembo wananza kuuliza tembo wamejificha? kisha huamua kupitia kenya maana fluidity ya mambo Kenya ni bora kuliko Tanzania.

Hivyo kwa miaka 10, Kikwete amewekeza kuitangazia Tanzania kwa wawekezaji na kuwa kuna vivutio vya kutosha, lakini kama umeme na maji ni shida, basi projection zangu za income na growth lazima zifidiwe na hapo ndipo mtu anaomba msamaha wa kodi na ushuru kwa miaka 5 na anapewa!

Kama tunataka kuendelea, lazima tuwe na viongozi wenye vision na weneye uwezo wa kuweka sera zinazoeleweka na kuzifanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuunda timu na kuzimamia Sera ifanikiwe na si kuachwa kwa wengine waifanyie kazi!
Mkuu , nadhani JK hajaitangaza Tanzania kwa njia muafaka.

Alichotekeleza ni sera/Ilani ya CCM ya kuomba omba. Safari 410 hazina tija ukilinganisha na alipoikuta na kuiacha nchi

Kwa ufupi, safari 410 katika wastani wa siku 1 kwa safari ni sawa na siku 410 ambazo ni sawa na mwaka 1.

Tukifanya wastani wa siku 1 kwa safari, ina maana Rais hakuwa ofisini kwa mwaka 1 katika 10 aliyokaa madarakani
Jaribu kufanya wastani wa siku 5........

Katika muda huo tunaambiwa alikuwa anavutia FDI n.k. Takwimu za kimataifa zinaonyesha tupo nyuma ya mjirani zetu ambao marais wao hawasafiri na hata kama wanafanya , katika miaka 10 hawajafikia hata safari 50

Wawekezaji wanataraji kuwekeza katika mazingira yanayohakiklisha usalama wa mitaji yao.

Pale wanapogundua kuwa hakifanyiki kitu ila kwa rushwa, wanaposikia madili yanayohusisha serikali , wanakosa imani ya kuweka mabilioni yao katika 'volatile and hostile environment ' kama ya Jserikali ya JK

Lakini pia wanajiuliza, kama kuna sababu za kubebea jenereta wakija na mitaji yao.

Wanajiuliza kama kuna sababu za 'simtank' kwasababu hakuna maji.

Wanapoangalia eneo kama Nairobi, hawana sababu za kuwekeza Dar

Ndio maana mashirika mengi na balozi nyingi zina ofisi Nairobi.

Katika mtazamo huo, kiongozi hakuwa na vision wala mission. Mawaziri wakuu waliojaribu hawakuweza kwasababu zile zile za mazingira mabovu ya uongozi. Kama walivyo wawekezaji hata mawaziri wakuu yamewakuta

Haionekani kama Watanzania wamejufUnza jambo.

Mwaka 2005 tuliambiwa kiongozi ni mzuri anapendeza.tukiangalia nyuma Watanzania ni masikini na fukara kuliko 2005.

Sasa tunaambiwa kuna baunsa wa push up. Hatujiulizi , tunashangilia tu.

Hatujishughulishi kufikiri kuwa tunataka Baunsa wa kichwa ili tuondoke hapa tulipo

Hatujiulizi , miaka 50 nguo inaongezeka viraka badala ya kupata mpya. Tunakazana kuweka viraka! hatufikirii zaidi hapo
 
MABILIONI YA JK YAPOTEA

MAGUFULI /CCM HAWATAKI HOJA YA KATIBA. wANAVIZIA WANANCHI WAINGIE MKENGE


Tumeshuhudia mambo yaliyofanywa na serikali kinyume na sera/Ilani. Ni utashi wa mtu au watu. JK aliahidi mabilioni kwa wafanyabiashara ndogo kama wamachinga na mama Ntilie. Hiyo ilikuwa ahadi tu wala haikuwa katika ser/ilani ya chama

Mabilioni yakagawiwa kama njugu bila maandalizi ya aina yoyote. Hatujui mabilioni yamerudishwa au yamepotea. Hakuna tathmini ya tija .Ni utaratibu ule ule wa Kilimo kwanza, kwamba mtu au watu bila kutumia utaalamu wanaamua jambo tu

Kwa nchi nyingine, pesa za umma zinakuwa na matumizi maalumu. Hili la mabilioni lingeondoka na serikali husika na wahusika

Hizi ndizo athari za ahadi badala ya sera/ilani au mipango

Udanganyifu unaendelea. Magufuli haelezi mwendelezo wa kugawa mapesa kama ya JK utamsaidiaje Mtanzania.
Naye kama walivyo wengine, ni sehemu ya mabilioni yaliyogawiwa bure na kupotea

Ili kutuondoa katika hoja za msingi, Magufuli anaonekana akipakuwa wali. Haya ya msingi haongelei kabisa
Ni kama asivyoongelea suala la katiba.Wapinzani na UKAWA tumeanza kuwasikia wakizungumzia katiba na msimamo wao

Magufuli haongelei katiba yu busy akipiga push up. Leo wananchi wanajadili push up za Magufuli kama ndilo tatizo la umasikini

CCM/Magufuli hoja zilizo mbele kama chama tawala kwa miaka 50 hazina majibu.
Kinachofanyika ni kupumbaza wananchi kwa kupakuwa vyakula na push up

CCM/Magufuli wanajua hasira za wananchi dhidi ya uhuni wa katiba uliotendeka Dodoma.

Wanajua wananchi hawakuridhishwa na mchakato ulivyokuwa handled. CCM hawataki kuzungumzia katiba kwasababu kuu mbili

1. Kutoudhi Wazanzibar . Kwamba, ni kuamsha hasira ambazo kwa pamoja bila itikadi ni dhidi ya CCM.
JK/CCM wamefanya kazi ya kuondoa mafuta na gesi ili kuwafurahish. Wasichojua,mfumo mzima wa utawala na CCM imechokwa

2. Hawataki kuzungumzia ili kuwasahulisha Watanganyika namna katiba yao ya sasa ilivyo na matatizo.
Kwa mfano, uwezekano wa mgogoro wa kikatiba ni mkubwa sana endapo wapinzani watazuia 2/3.
Katiba ya 1977 haina majibu ya nini kifanyike katika hali kama hiyo

CCM/Magufuli wanakaa kimya wakitegemea kuwa baada ya uchaguzi watarudisha suala la katiba ya Cheng/Dr Francia

Hutawasikia wakizungumzia jambo, kwanza kuepusha hasira zilizopelekea CCM kuchukiwa na jamii
Pili, wametega, watarudisha katiba pendekezwa kwa nguvu wakijua wananchi ni wapjinga tu kama ilivyozoeleka miaka 50

Wananchi watambue CCM inawachezea. Hatuhitaji push up, tunataka atoke mbele na kueleza anamsimamo gani

Bila kumbana, ataendelea na push up kama ndilo tatizo la nchi. Huu ni ujinga na upuuzi tunaoukubali hadharani

Push up tunayotaka kusikia kutoka kwake ni kuona , kutambua, kufafanua na kutoa majibu ya wananchi wanaolala sakafuni Muhimbili, wanafunzi chini ya mbuyu, wazazi mzungu wa nne, wafanyakazi wanaotembea marathon kwasababu hawana sh 500 ya daladala na wale wanaoishi chini ya dola 1 kwa siku. Tunamtaka aeleza dira ya taifa si kupumbaza umma kwa push up

Push up ni kielelezo cha kukosa fikra. Lini uliwahi kumuona Nyerere akipiga push up jukwaani. Tusikubali kupumbazwa na huu ujinga

Hatumuulizi Magufuli kuhusu katiba, tunashangilia push up. Tusipowauliza watapiga push up halafu ''hawajui kwanini sisi ni masikini''

Badala ya kutafuta jibu la kwanini sisi ni masikini, wanazunguka duniani wakijitambulisha na kuaga wakiwa na bakuli la omba omba.
Harukuwauliza! kwanini wasifanye misele nchi ikizama katika umasikini, majirani wakitushinda kila mahali

Sisi tunashangilia push up na si fikra na maono! Watanzania ni shiiida amkeni!
 
Sisi tunashangilia push up na si fikra na maono! Watanzania ni shiiida amkeni!

Nguruvi3,

Ukiangalia jukwaa la Siasa au Jukwaa la Uchaguzi, ukienda Twitter, whatsapp tunashangilia push up, mipasho, vijembe, kutambiana na kubishana juu ya kura za maoni na mambo mengine mengi yasiyohusu maendeleo ya Taifa letu na hayana tija.

Si suala la kutowazungumzia wagombea, lakini ni mara ngapi turudie na kulazimishana ama kutuhumu au kumtetea mgombea tunayemtaka?

Je tumeshachukua fursa kupitia hoja na ahadi zao na kuzioanisha na Sera na ilani zao?

Tumebeza laptop za Magufuli na Elimu bure ya Lowassa badala ya kuhoji na kutaka blue print zao za mfumo wa Elimu!

Wanaoendesha kampeni, ndio wanaohujumu na kushangaza zaidi, wanashauri mambo mepesi mepesi ya ujanjaujanja na kimjinimjini na umati unashangilia na kufurahia.

Lakini, ikifika Januari 1 2016, Kama kawaida yetu tutakuwa mstari wa mbele kuanza kuorodhesha tena matatizo na malalamiko yetu upya, huku nafasi ya kudhibiti madhaifu na maZoea ya kudanganywa tunaipuuzia sasa hivi na kukaa kulumbana ushabiki na vitu visivyo na tija!

Basi nasi tuanZe push up maana haiwezekani tuahangilie uhodari wa Magufuli na tusiwe tayari kwa ukakamavu wa mwili na fikra!
 
Rev. Tuna nafasi ipi kuepuka kudanganywa? Iwapi imani ya kufikiri kuwa kuna hoja mpya wanaweza kutujibu? Tutachacha.
 
Adui anayelihujumu Taifa letu ameshajiingiza katika kila kona ya nchi na jamii yetu. Anajua ujinga wetu, udhaifu wetu na anahakikisha tunaendelea kuwa wanyonge na masikini!

Adui huyu ametufanya tuache kuongea mambo ya maana na msingi kwa Taifa letu, ametugeuza katika mkondo wa udaku, mipasho na kukosa kabisa kuongelea sera na ilani ambazo zingetuondoa kutoka unyonge, umasikini, unyonyaji, ufisadi na utegemezi.

Kwa bahati mbaya sana, si siri kuwa Adui huyu ameshikilia kwa nguvu na kupandikiza mizizi mikubwa na magugu ya uhujumu ndani ya Chama Tawala.

Chama Tawala kinang'ang'ani amadaraka ili kulinda maslahi ya Adui huyu na si kutaka kuwatumikia Watanzania na kuyashinda masumbufu yao ya kila siku.

Ni wazi ili tubadilike, tunalazimika kuachana na CCM!
 
Katika mjadala huu niliochelewa kuuona nimevutiwa sana na uchambuzi wa rev.Kishoka na Nguruvi3. Kwa hakika nimeshindwa kujizuia kunukuu baadhi ya masuala ambayo nimekubaliana nayo kimtazamo katika makala yangu ya Raia Mwema ninayoimalizia muda huu kujibu makala ya Dr.Kigwangalla. Ni coincidence kwamba katika mambo mengi yaliyochambuliwa yapo kwenye Policy yetu mpya ya Elimu na asilimia kubwa tumeyawaeka katika ilani yetu.Nataraji kuungana nanyi kuelezea na kuchambua baadhi ya masuala kadhaa

Kwa mfano Katika utendaji wa serikali mpya ijayo kwenye ilani ya CHADEMA kwa mfano tumeeleza kuwa tumeandaa Mkakati mpya wa kuondoa umaskini ambao utakuwa na nguzo tano ambazo ni pamoja na Kupunguza matumizi ya serikali na mashirika yake na kuimarisha utendaji na uwajibikaji,Kukuza pato la serikali kwa kudhibiti ukwepaji na misamaha ya kodi holela na kuhakikisha nchi inawekeza katika sekta muhimu na inapata gawio halisia kutoka wawekezaji,Kukuza uchumi kwa sera na sheria endelevu ikiwa ni pamoja na kukuza biashara na uwekezaji hasa katika sekta za madini, kilimo, viwanda, ufugaji na uvuvi na kuondoa kodi kwa wanyonge,Kuimarisha huduma za umma kama elimu, afya, maji na makazi, na mazingira, Kuimarisha utawala bora na mfumo wa haki na sheria chini ya Katiba ya Wananchi.


Chini ya misingi hii na ili kufanikisha mkakati wa kuondoa umaskini, serikali Itakayoundwa na UKAWA chini ya Rais Edward Lowassa itatoa kipaumbele katika Elimu itatayogharamiwa na serikali kwa kila Mtanzania kutoka elimu ya msingi hadi Chuo Kikuu na pia, Kuimarisha elimu ya teknolojia, ustadi na ufundi inayojenga uwezo wa kujiajiri na ushindani katika soko la ajira,Ujenzi na uimarishaji wa miundombinu ya elimu ikiwa ni pamoja na shule za Kata, Kusimamia ubora wa viwango vya elimu kote nchini,Kuimarisha taaluma na mitaala katika mashule,Kuondoa utoro darasani, na kuboresha afya za wanafunzi, Kuboresha maslahi na vitendea kazi kwa walimu ikiwa ni pamoja na nyumba, posho ya kufundishia, usafiri na zana za teknolojia, Kufuta michango ya maabara ya shule za kata



Nchi za Brazili, Mauritius na Sri-Lanka zimepiga hatua kubwa kimaendeleo kwa haraka baada ya kuwekeza kwenye elimu na kuweka mazingira bora ya kumpunguzia mzazi mzigo ili pia kujenga taifa lenye raslimali watu yenye ujuzi.



Bajeti ya Wizara ya Elimu ni Takribani Shilingi Bilioni 794 wakati ripoti mbalimbali zinaonyesha kuwa sekta ya madini pekee inalipotezea taifa Shilingi Trilioni 2.5 kwa ukwepaji kodi na misamaha holela ya kodi kwa mwaka. Hivi fedha hizi Shilingi 2,500,000,000,000 haziwezi kuingizwa katika bajeti ya elimu kusomesha watoto na wadogo zetu?
 
Last edited by a moderator:
Katika mjadala huu niliochelewa kuuona nimevutiwa sana na uchambuzi wa rev.Kishoka na Nguruvi3.

Bwana Saaanane,

Tunashukuru kwa kuja kutuchungulia na hata kutengeneza "desa".

Lakini, kwa nini msitumie wakati huu wa kampeni kuwaelimisha kwa kina na kuchambua kwa kina na urahisi sera zenu za elimu, afya, maji, ajira na ardhi ili wananchi wapate cha kujipimia tofauti na waliyoyaona miaka 50? Ingekuwa rahisi sana mkaachana na mabishano ya kwenye jukwaa na CCM mkajikita zaidi kunadi sera zenu kwa ufasaha ili wananchi hasa vijijini waelewe na kuona ni vitu vinawezekana na si ahadi za kuomba kura.

Kwa upande mwingine, naomba usome hii makala ya Economist kuhusu Nigeria. NItaifungulia mada yake pekee!

Can Nigeria's Buhari take on the import monster and win? | The Economist
 
Bwana Saaanane,

Tunashukuru kwa kuja kutuchungulia na hata kutengeneza "desa".

Lakini, kwa nini msitumie wakati huu wa kampeni kuwaelimisha kwa kina na kuchambua kwa kina na urahisi sera zenu za elimu, afya, maji, ajira na ardhi ili wananchi wapate cha kujipimia tofauti na waliyoyaona miaka 50? Ingekuwa rahisi sana mkaachana na mabishano ya kwenye jukwaa na CCM mkajikita zaidi kunadi sera zenu kwa ufasaha ili wananchi hasa vijijini waelewe na kuona ni vitu vinawezekana na si ahadi za kuomba kura.

Kwa upande mwingine, naomba usome hii makala ya Economist kuhusu Nigeria. NItaifungulia mada yake pekee!

Can Nigeria's Buhari take on the import monster and win? | The Economist

Rev. Kishoka,

Asante sana sana.

Kimsingi katika kampeni tumetengeneza timu tofauti zenye majukumu tofauti

Kwa mfano kwenye swala la kufafanua Ilani nimetumia media yaani magazeti na kwenye vipindi vya Televisheni na hata muda mfupi ujao nitakuwa Live ZBC katika mada isemayo "Nafasi ya Zanzibar katika ilani za vyama"

Tumeendelea kutumia local Radios na kuwapa maelekezo maofisa wetu wa Sera na wanasiasa popular kwenye kanda husika watumie FM Radios kufafanua Ilani

Pia ninatarajia kuambatana na mgombea Urais kwa baadhi ya maeneo ya kimkakati kwa ajili ya kunadi ilani yetu
 
Last edited by a moderator:
Asante sana Ben Saanane kwa maelezo yako..

Ila kuna swala ambalo silielewi ni kwanini walimu wajengewe nyumba? Na kama tukiwajengea walimu nyumba uoni kuwa kuna umuhimu wa kuwajengea nyumba Polisi, wanajeshi, manesi na wengineo? Siamini katika kujenga taifa lenye utegemezi (kwangu mimi unapompa walimu nyumba bure ni utegemezi) Nilitegemea muwalipe walimu mishahara mizuri na kutokana na hii mishahara mizuri hawa walimu wataweze kujenga nyumba zao au hata kupanga katika nyumba wanazopenda wao au zinanoendana na hadhi zao..

Pia tukirudi katika mfumo wetu wa elimu nafikiri ni wakati mhafaka kufumua mfumo tulio nao na kuja na mfumo ambao utaendana na dunia ya leo. Hii ni pamoja na miaka minne ya mwanzo watoto wafundishwe masomo matatu Hesabu, Kiswahili na English.. Wale watoto wasiojiweze darasa basi uwekwe utaratibu wa kufundishwa kwa muda wa ziada, (na mwalimu tofauti wa masomo yanayowasumbua hao watoto) Tuwape walimu uwanja mpana wa ubunifu wa jinsi ya kuwafundisha watoto, madarasa awe na wastani wa wanafunzi 35 hii itakuwa ni rahisi mwalimu kumfuatilia mtoto, kuwe na utaratibu wa mwalimu kukutana na kuongea na mzazi wa kila mtoto mara moja au mbili kwa mwaka.. (hapa mzazi atapewa maendeleo ya mtoto wake na nk na hii itajenga husiano kati ya mwalimu na mzazi) kuwepo na mashindano ya kimkoa ya watoto au kitaifa katika masomo ya Hesabu, English na Kiswa.. (kwa shule ya msingi) hii itasaidia mwalimu kujipima alipo na anapokwenda na kubadilishana ufundishaji kwa zile shule zinazofanya vizuri. na nk..

Nafikiri kukisha fanya hayo hapo juu na mengineyo tutapinga hatua kwenda mbele katika swala zima la Elimu.
 
Last edited by a moderator:
Naona Lawama tu kuhusu kushapu,kanakwamba Magufuli ni bubu,mbona mikutano yote anazungumza,juu ya serikali yake ya awamu ya tano,jinsi itakavyokua atakua na mchezo na wazembe,
 
Hadith Hadith? Uongo njoo, utamu kolea!
Jamani ni Lini kweli watanzania tumeshuhudia ILANI ya chama ikitimizwa? mbona kila tunaloshuhudia zaidi ni ile Ilani ya IMF iloandikwa na watalaam kutoka nje ndio inayopewa kipaumbele zaidi..Je watyanzania mko tayari kuanza na kile mlichonacho pasipo mikopo yenye masharti magumu ambayo ndio haswa inayoongoza nchi yetu..Anayodai nguruvi3 ni mambo mazito ya nchi za wenzetu walokuwa na uwezo lakini kina sisi tutabakia kudanganyana tu maana Maskini huishi kwa kujazwa matumaini..

Nakumbuka miaka ya 80s baada ya kuacha Ujamaa na Kujitegemea kulivishwa joho la IMF wakaliita Structual Adjustment Program (SAP) kama muarobaini wa kuondoa Umaskini nchini. M[pango huo ikapitiwa na wataaluma wetu wakaipinga sana tu lakini wakapuuzwa na chama kikabadilisha Katiba na kuweka Ilani yake. Kama alivyosema Rev. Kishoka tumeendelea kupuuza wataalam wetu wenyewe kwa miaka yote kwa sababu ya aidha Umaskini wetu ama kutojiamini wenyewe ndio mwanzo wa siasa hizi za matumuaini na mabadiliko kila Uchaguzi. Tumekuwa tukivikwa majoho haya kila baada ya miaka mitano wakitupima tumefikia wapi ilihali mipango hii ndiyo chachu ya Ufisadi wenyewe na Ilani za chama hubakia ahadi hewa.

Hawa IMF na World bank ni wafanya biashara na wapo kutengeneza faida kama Benki zinginezo. Huwezi kusema benki ni huduma bora kwa sababu inatoa mikopo pasipo kuelewa kwamba Benki ni wafanyabiashara na wanaweza kukuweka katika Utegemezi miaka yote kutokana na riba wanazokusanya. Ndivyo IMF inavyo operate, interest zao kwanza na sio vinginevyo. Hizi habari za ILANI ya chama kusema kweli mimi huwa sipendi kuzitumia kabisa kwa sababu Uhalisia wake haupo ikiwa hawatuonyeshi fedha zitatoka wapi? wafadhili wa mitradi hiyo kina nani na wanataka nini?. Ili wataalam wetu wayapime mazuri na mabaya ya miafaka hii. Otherwise hizi siasa ni hadith inayopendeza kusikiliza..
 
Ukawa tutarejesha heshima ya Tanzania kimataifa

RaiaMwema Toleo la 427
14 Oct 2015
Na Ben Saanane

KUPITIA makala hii, naamini Watanzania watatumia fursa ya uchaguzi Oktoba 25, kuifufua Tanzania ya Mwalimu Nyerere kupitia sanduku la kura kwa kuichagua Serikali ya Ukawa.
Mwasisi wa taifa letu, Mwalimu Nyerere aliipenda Tanzania na Afrika, hakupenda ukandamizaji ndani na nje ya mipaka yetu.Tanzania ilijiweka katika ramani ya dunia kutokana na msimamo na uongozi shupavu wa Mwalimu Nyerere kiitikadi, kifalsafa na kimaono.
Aliposimama katika Jukwaa la Umoja wa Mataifa kule New York, Afrika na mataifa mengine yaliyopinga ukandamizaji yalikuwa nyuma yake. Aliposimama katika Jukwa la Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), kule Addis Ababa-Ethiopia, wanamajumui (Pan-Africanist) walisimama nyuma yake.
Hakika Afrika na dunia katika changamoto za leo itamkosa sana gwiji huyu mwana halisi wa Afrika. Kwa Tanzania siku ya leo ni msiba zaidi. Tutapata fursa ya kupunguza majonzi haya kwa kuifufua Tanzania ya Nyerere Oktoba 25, kwa kufanya mabadiliko kupitia sanduku la kura na kuichagua Serikali ya Ukawa.
Itakuwa hatari sana kumchagua Rais mwenye upeo mdogo kimataifa. Rais asiyejua hata Saddam Hussein alikuwa Rais wa nchi gani? Anasema hadharani kwa ujasiri kuwa alikuwa Rais wa Kuwait? Yaani kama hajui mtu maarufu wakati wa vita ya Marekani na Iraq, Saddam Hussein alikuwa Rais wa nchi gani ataelewa nini kuhusu sera ya Tanzania Mashariki ya Kati na Bara Asia? Kweli ataweza kuirejesha heshima ya Tanzania ya Mwalimu Nyerere katika ramani ya dunia? Ataelewa nini kuhusu diplomasia ya uchumi?


Katika dunia ya leo pale ambapo dunia yetu inafanywa kama kijiji, huku mataifa yakiungana na kuridhia uhusiano wao juu ya masuala mbalimbali na hasa ya kiuchumi, taifa kuwa na sera ya nje makini inayolinda maslahi yetu katika uhusiano wetu na mataifa mengine ni kitu muhimu sana. Ukitazama namna mataifa yenye viongozi makini yanavyoendesha siasa zake za nje, utakuta suala la maslahi ya kiuchumi limepewa kipaumbele sana. Diplomasia ya uchumi ndio kiongozi wa nchi miongoni mwa mataifa mengine.
Hivyo ni jambo lililo wazi kuwa hata wakija hapa, habari yao kubwa itakuwa ni diplomasia ya uchumi. Watanzania tutumie fursa hii kujiuliza je, Tanzania kama taifa huru limejiandaa vipi katika uhusiano huu ili kuhakikisha kuwa raia wake wanafaidika na uhusiano huo? Sera yetu ya nje inasemaje? Wagombea urais na vyama vyao wanasemaje kuhusu nafasi ya Tanzania katika medani za kimataifa? Sera zao zinalinda vipi maslahi yetu wote?
Je, viongozi wetu wanaitekeleza hata sera ya serikali iliyotokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM)? Haya tunayoyashuhudia hivi sasa ikiwemo safari nyingi za gharama kubwa za Rais wetu aliyefikisha idadi ya ziara zaidi ya 410 nje ya nchi (zaidi ya mwaka mmoja ) katika awamu zake mbili madarakani, ni utekelezaji wa sera yetu wenyewe? Je, utekelezaji wa sera yetu unaleta uwiano mzuri na sera za mataifa mengine na jumuiya za kimataifa?
Je, sera hiyo inaleta uwiano mzuri na sera zetu za ndani na hasa katika masuala ya uchumi? Je, tunaweza kusimama na kuizungumza sera hiyo kwa mwananchi wa kawaida na akatuelewa na kuona maslahi yake kama Mtanzania ndani yake? Je, inatekelezeka?
Maneno Diplomasia na Sera ya Mambo ya Nje yamekuwa yakitumika wakati mwingine kumaanisha kitu kimoja (Interchangeably), ingawa yana maana tofauti.
Kwa mfano diplomasia maana yake ni uhusiano wa kimataifa kati ya nchi na nchi na kati ya nchi na mashirika ya kimataifa (Mult-National Corporations). Uhusiano huu hutengenezewa mbinu na mikakati endelevu (sustainable strategies) ya utekelezaji wake kwa kila nchi kupitia sera zao za mambo ya nje.

Sera ya Mambo ya Nje (Foreign Policy) ni tamko la nchi lenye kutoa mwongozo na mwelekeo kuhusu madhumuni, malengo na misingi ya nchi katika kuhusiana na nchi, mashirika ya kimataifa na wadau wengine nje ya nchi. Tamko hili pia ni mwendelezo wa sera ya ndani ya nchi kama vile kwenye sera ya elimu, viwanda na biashara, nishati, ulinzi, afya, kilimo na vitu vingine kama dira ya maendeleo . Sera ya Mambo ya Nje ya nchi ni chombo kinachobeba dhana na mbinu za utekelezaji wa diplomasia.
Sera hutoa mwelekeo juu ya misimamo ambayo nchi inaipigania na ile isiyokubaliana nayo katika medani za kimataifa na itataka kutambuliwa msimamo wake wazi kupitia sera. Sera hii ndiyo kitambulisho cha taifa husika katika kulinda tunu (values) zake na kujipambanua miongoni mwa mataifa. Kwa hiyo ni jambo muhimu kwa kuwa ni utambulisho wa nchi kimataifa, na tamko hili huakisi sera na misingi ya ndani ya nchi husika.
Kwa kawaida mratibu mkuu (coordinator) wa utekelezaji wa sera hii ni Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, na sera hii hutekelezwa na serikali nzima na wadau wengine ndani ya nchi, ambao shughuli zao zinahusiana na masuala ya kimataifa.
Mkuu wa nchi ndiye mwanadiplomasia namba moja, na Waziri wa Mambo ya Nje ni mwanadiplomasia namba mbili katika nchi yoyote. Hawa ndio sura ya nchi mbele ya dunia na ndiyo maana inabidi kuwa makini sana katika uchaguzi hasa uchaguzi wetu mkuu kwani Uchaguzi Mkuu pamoja na kuwa unamchagua Rais wa Watanzania lakini pia unamchagua mtu atakayebeba haiba ya Watanzania nje ya nchi, misimamo yake ndiyo itakayowakilisha Watanzania nje ya nchi.
Ni lazima kuwa na Rais mwenye uzoefu wa kiuongozi, mwanadiplomasia kwa muonekano na kifikra. Tanzania ina sera ya mambo ya nje ya mwaka 2001 ambayo ilipaswa kutoa mwongozo katika kufikia malengo ya nchi nje.
Kama zilivyo nchi nyingine nyingi baada ya Uhuru tulikuwa na sera ya ukombozi ndiyo maana tulijikuta tumechagua maadui na marafiki wakati wa ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika.

Diplomasia yetu sasa tofauti na awali, inatakiwa ilete manufaa ya kiuchumi ikiwa ni pamoja na kufungua masoko kwa biashara za Watanzania, bidhaa, kuvutia wawekezaji na kuongeza watalii. Mkakati huu wa kutekeleza sera, umepewa jina la Diplomasia ya Uchumi.
Diplomasia, kama ilivyo mikakati mingine inayo vigezo na vipimo vyake. Diplomasia hufanyiwa tathmini mara kwa mara ili kuendana na mabadiliko ya kidunia.
Uimara wa diplomasia ya nchi ni ushawishi wake kimataifa. Ushawishi wa nchi, kihistoria umekuwa ukiambatana na nguvu ya kiuchumi au kijeshi (Diplomasia ya Nguvu). Nguvu hizi mbili ni matokeo ya sera za ndani ya nchi. Pamoja na kuwa, si lazima kuwa kila nchi yenye moja au vigezo hivyo viwili kufanikiwa katika diplomasia. Ziko nchi ambazo zimefanikiwa sana kuwa na ushawishi mkubwa, pamoja na kutokuwa na nguvu hizo duniani, kutokana na uimara wa sera yake ya mambo ya nje, na wanadiplomasia wake (Nguvu ya Diplomasia).Tanzania chini ya Mwalimu Julius Nyerere na Wanadiplomasia kama akina Salim Ahmed Salim ilikuwa miongoni mwa nchi hizo.
Tanzania imekuwa ikitoa misimamo mikali katika medani za kimataifa chini ya Mwalimu Nyerere kutokana na haiba na misimamo yake kifikra iliyobeba mantiki za kiushawishi kidiplomasia miongoni mwa mataifa makubwa.
Tanzania kama mwanachama wa jumuiya ya kimataifa ni lazima irejeshe heshima na utambulisho wake uliopotea baada ya utawala wa Mwalimu Julius Nyerere.
Serikali ijayo chini ya Ukawa imepanga kuanzisha harakati mpya za kuwezesha kuwepo mfumo wa uchumi na biashara duniani wa haki na usiokandamiza nchi changa na pia kuendelea na harakati za kujenga msingi wa nchi masikini kushirikiana zaidi ikiwemo kufanya biashara zaidi baina yetu. Ni harakati za kurekebisha taasisi za utawala wa siasa za kimataifa zizingatie matakwa na maslahi ya mataifa mengi zaidi
Lazima kuendelea kupambana na ukoloni-mamboleo (Neo-Colonialism) ambao kila kukicha unachukua sura mpya ikiwemo kuhusisha misaada kwa nchi yetu na maslahi ya kibiashara ya mashirika ya nchi zinatoa misaada hiyo, kupewa masharti ya kupata misaada isiyo na msingi, na mashinikizo ya kufuata sera na kuchukua misimamo isiyo na manufaa kwa nchi yetu.
Tanzania imeshindwa kutoa misimamo yake thabiti kwenye majukwaa ya kimatifa kukemea udhalilishji wa kushinikizwa kupewa misaada kwa masharti ambayo ni kufuru katika Imani ya dini zote hasa masharti ya ndoa za jinsia moja.
Yote haya ni kwa sababu sera yetu imepoteza mwelekeo na diplomasia yetu sio ya uchumi bali ni diplomasia ya kuomba na kushukuru kutoka kwa mataifa makubwa yenye kiu na ndoto za ubeberu.
Serikali mpya ya Ukawa inalenga kuhakikisha kuwa utambulisho na sifa ya Tanzania kimataifa inabebwa na Watanzania nje ya nchi badala ya sifa ya Rais kutunukiwa shahada lukuki zisizo na tija katika medani za kiuchumi.
Diplomasia yetu kimataifa ni lazima ilenge katika utamaduni, uchumi na biashara kuliko ilivyo sasa ambapo diplomasia yetu ni ya kisiasa zaidi na haimgusi Mtanzania wa kawaida. Rais wa nchi anapowekeza katika sifa na ufahari binafsi kwa kutunukiwa medali ambazo hazina manufaa kiuchumi kwa Watanzania sio diplomasia ya uchumi bali ni diplomasia inayotumikia na kutumikishwa kisiasa.
Majirani zetu Kenya kwa mfano, wanapotoka nje ya mipaka yao na kujitambulisha kuwa wao ni Wakenya moja kwa moja wanatambulika kutokana na umahiri wao katika mchezo wa riadha. Riadha ni mchezo lakini unakuza uchumi wa Wakenya na utambulisho wao kimataifa.
Nchi kama India na wananchi wake kwenye sura ya kimataifa wanatambulika kwa umahiri wao katika teknolojia ya mawasailiano, famasia na katika nyanja za utabibu huku mataifa kama Ujerumani, China na Japan, raia wake wakionekana kuwa mahiri katika Uhandisi. Ni lazima sera msukumo sahihi wa sera zetu za ndani kama nilizoeleza katika mfululizo wa makala zilizopita ulenge kuhakikisha Watanzania wanabobea katika nyanja mbalimbali ambazo zitaleta ushawishi katika diplomasia yetu kimataifa na kuwa sura ya Tanzania nje ya mipaka yetu.
Ndio maana katika ilani ya Chadema inayoungwa mkono na Ukawa tumewekeza na kuipa kipaumbele elimu kwa sababu ni kupitia elimu tu tunapoweza kutoa vichwa ambavyo vitaweza kuiweka Tanzania katika ramani ya juu kimataifa.
Iwe katika soka, filamu au muziki ni lazima elimu ipewe kipaumbele ili tuweze kufikia hatua walizofikia wenzetu kama Nigeria na Nollywood yao, Marekani na Hollywood yao.
Katika ushawishi kimataifa, mataifa makubwa kama Marekani yalitambua umuhimu wa kuitumia burudani kupitia muziki, mpira wa vikapu, filamu katika kueneza ubeberu wa kiutamaduni (cultural imperialism) kiasi ambacho vijana wengi duniani wakafikia hatua ya kuiga utamaduni wa Marekani katika mavazi, katika kutembea na pia hata watu wa daraja la kati wa nchi mbalimbali wakawa wanaiga staili za maisha za Wamarekani katika maisha ya kila siku ili waonekane kuwa wameendelea na hata katika lugha imekuwa hivyo hivyo. Hiyo yote ni mikakati iliyosukwa kueneza ubeberu wa kiutamaduni.
Kupitia mkakati huo taifa la Marekani likaendelea kupata ushawishi katika maisha ya kila siku ulimwenguni na wakati huo huo wanamuziki, wacheza filamu na wanamitindo wa Marekani wakaendelea kunufaika kiuchumi kutokana na kazi zao kuwa na ushawishi kwa watu wengi duniani na kuwa soko la shughuli zao huku pia taifa la Marekani likiingiza fedha nyingi.
Hapa Afrika, Nigeria na Afrika Kusini zinakuja kwa kasi katika kutumia tasnia ya filamu na muziki kueneza utamaduni wao hapa Afrika na kuwa na ushawishi. Tanzania haiwezi kuendelea kubaki nyuma.
Vilevile, katika kulenga kuitumia nafasi ya kidiplomasia kukuza uchumi wetu; serikali ijayo ya Ukawa itaandaa sera maalumu kati ya Tanzania na nchi au kanda mbalimbali ambazo ni muhimu kimkakati kama Tanzania na Umoja wa Ulaya (EU), Tanzania na nchi za Asia Mashariki (SEATO), Tanzania na nchi za Ukanda wa Pacific, Tanzania na Mashariki ya Kati na pia Sera ya Tanzania katika ushirikiano wake na mtangamano wa kikanda (regional Intergration) kama vile Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), SADC na katika njia ya kuelekea (roadmap) katika Umajumui wa Afrika (Pan-Africanism) kupitia dhima ya Tanzania kwa Umoja wa Afrika (AU).
Ni kupitia mikakati hii tutakapoweza kutumia utalii wetu kukuza uchumi, pia kulinda rasilimali za nchi yetu na kukomesha uporwaji wa rasilimali za taifa letu.
Kwa mfano, Tanzania ina uhusiano na baadhi ya nchi ambazo sio wazalishaji wa vito vya Tanzanite lakini nchi hizo ndio wauzaji wakubwa wa Tanzanite duniani kuliko mzalishaji wake halisi Tanzania. Kama Balozi zetu zingekuwa makini hali hii ingerekebishwa.
Kuna nchi ambazo korosho ya Tanzania imeuzwa kwenye soko la kimataifa kuliko Tanzania wakati wazalishaji halisi ni Tanzania. Haya yote ni kutokana na serikali yetu kutokuwa makini katika diplomasia ya uchumi.
Teuzi za mabalozi wetu nje zimekuwa teuzi za kulipa fadhila badala ya teuzi zinazozingatia taaluma. Tuna mabalozi na wanadiplomasia wasioifahamu sera iliyopo na pia hawaelewi maana ya diplomasia ya uchumi. Wanadhani kuiwakilisha Tanzania nje ni kushiriki dhifa za kitaifa wanazoalikwa na viongozi wa nchi wenyeji na kutoa visa kwa raia wa kigeni kuja Tanzania tu basi.
Serikali ijayo ya Ukawa itazingatia weledi katika teuzi za mabalozi na maofisa wa balozi zetu nje. Ni lazima idara muhimu ya Usalama wa Taifa ihusishwe kikamilifu katika teuzi za maofisa hawa. Ni lazima tuzingatie taaluma na uzoefu katika nyanja za uchumi, biashara, uhandisi na intelijensia ya uchumi ili tuweze kubadili mfumo wa ushirikiano kati ya Tanzania na jamii ya kimataifa.
Teuzi ni lazima zizingatie msingi mkuu wa uadilifu na uzalendo. Watanzania waliowahi kwenda nje ya nchi na waliopo watakubaliana name kuwa mabalozi wetu wengi na baadhi yao maofisa wa ubalozi wamepoteza uzalendo na hadhi ya kutumikia nafasi zao.
Watanzania waliopo nje hawaoni ofisi za balozi zao kama nyumbani kwao kutokana na jeuri, viburi na manyanyaso wanayopewa na baadhi ya maofisa wa ubalozi kinyume na ilivyo kwa nchi nyingine. Wafanyabiashara wanaofanya biashara za nje hawapewi ushirikiano wa kutosha kutoka ofisi za ubalozi wa Tanzania. Hii yote ni kutokana na balozi zetu kujaza maofisa wasiokuwa na uzalendo, wavivu, wazembe na wabinafsi waliopindukia huku wakilipwa kwa kodi za Watanzania. Hatuwezi kuendelea kwa namna hii, tutaishangaza dunia.
Watanzania wanaofanya kazi nje ya nchi maarufu kama wana-diaspora wanaweza kuwa mabalozi wetu wazuri kiuchumi ikiwa mikakati thabiti itawekwa. Watu hawa wana mchango mkubwa sana katika maendeleo ya nchi yetu kiuchumi hasa katika sekta ya elimu, afya na nyinginezo, Watanzania hawa wanaofanya kazi au biashara wamekuwa wakitafuta fursa za kuwekeza nchini na kurudisha nyumbani walichovuna nje na pia kuwasaidia ndugu zao.
Kwa mfano nchi kama Nigeria mwaka 2013 wana-diaspora (Wanigeria waishio nje ya nchi) walirudisha kati ya dola za Marekani bilioni tano hadi 10 kwa mwaka yaani zaidi ya trilioni 10 na 20 kwa fedha za Kitanzania ambazo zinakaribiana na bajeti yetu ya mwaka 2014/2015.
Tanzania inapaswa kufuata nyayo hizi kwa kuwapa wana-diaspora umuhimu mkubwa katika kukuza uchumi wa taifa letu.
Pia serikali mpya ya Ukawa itatetea haki za binadamu, usawa wa nchi na kuimarisha ushiriki wa Tanzania katika diplomasia ya kimataifa. Tanzania haitakubali kufumbia macho ukandamizaji wa haki za binadamu na itasimama kidete kupitia nafasi yake kulinda ustawi wa demokrasia, utawala bora na kutetea haki za binadamu kwa kuwa tunaamini dunia ni yetu sote na hakuna mwenye haki ya kukandamiza haki ya mwingine.
Tutasimama kidete kusimamia misingi ya uanzishwaji wa Umoja wa Afrika, Mkataba wa Uanzishwaji wa Umoja wa Mataifa (UN Charter) kama ambavyo Tanzania chini ya Mwalimu Julius Nyerere ilivyofanya katika medani za kimataifa.
Ni katika misingi hii, tutaheshimu ujirani mwema, kulinda na kuheshimu mikataba na majukumu ya kimataifa (International Obligation) ambayo Tanzania iliridhia.
Tutaimarisha Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja na kudai mabadiliko ya mfumo ili kuleta usawa wa nchi shiriki. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN Security Council) lina changamoto ambazo tumekua tukizipigia kelele hasa juu ya upanuzi wa wigo wa kidemokrasia na utendaji wake unaozingatia maslahi ya wachache na hivyo kubeba ajenda za mataifa yenye nguvu kuamua juu ya masuala mazito ya dunia. Amani ya dunia imewekwa rehani kwa mataifa haya matano tu.
Naomba nimalizie kwa leo, kwa kuwataka wasomaji wangu na Watanzania kwa ujumla mtafakari sana siku ya leo tunapoadhimisha miaka 16 ya kifo cha Baba wa Taifa. Tunayo fursa ya kuirejesha Tanzania inayojisikia fahari na itakayotembea kifua mbele miongoni mwa mataifa na pia raia wenye ujasiri wa kujitambulisha kuwa Watanzania miongoni mwa raia wa mataifa mengine.
Kupitia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015, tunayo fursa kupitia sanduku la kura kumchagua Rais atakayesimamia kuirejeshea Tanzania nafasi yake kimataifa na kuwanufaisha Watanzania kupitia nafasi ya Tanzania kimataifa.
Ni hatari sana kuendelea na uongozi na mfumo wa chama tawala, CCM, ulioporomosha heshima ya taifa letu mbele ya uso wa dunia. Kwa bahati mbaya, CCM wamemsimamisha mgombea John Magufuli ambaye ameonyesha upeo mdogo sana katika masuala ya kimataifa. Ndio maana sikuona ajabu kuona akimtaja Rais wa zamani wa Iraq Saddam Hussein, kama Rais wa Kuwait mbele ya mkutano wa hadhara.
Sikushangaa zaidi alipoonyesha upeo mdogo kwa kutaja kuwa Muammar Ghaddafi wa Libya aliondolewa madarakani na wananchi wa Libya wakati Watanzania na hata dunia inajua kuwa Muammar Ghaddafi aliondolewa kwa njama za mataifa ya nje kupitia azimio namba 1973 la Baraza la Umoja wa Mataifa, lililoweka zuio la kuruka kwa ndege za kivita (no-fly zone) na kusababisha Majeshi ya Kujihami ya Marekani na Nchi za Magharibi (NATO) kuishambulia Libya. Ndiyo maana hapo juu nimegusia umuhimu wa kupanua wigo wa kidemokrasia ndani ya Umoja wa Mataifa. Haya ya Libya yasingefanyika kama kungekuwa na haki tunayoipigia kelele ndani ya Umoja wa Mataifa.
Magufuli bila haya au kutokana na kutoelewa masuala ya kimataifa haoni kuwa Serikali ya Tanzania ilikuwa na fursa ya kuitetea Libya kupitia Umoja wa Afrika na au Balozi wake wa kudumu kule Umoja wa Mataifa. Ni kutokana na Tanzania kupoteza imani kimataifa ndio maana imekosa ujasiri wa kupaza sauti kama Tanzania ya Nyerere ilivyokuwa mstari wa mbele kutetea haki na kulinda amani ya dunia.
Naamini Serikali ya Chadema itakayoundwa kwa ushirikiano wa vyama washirika wa Ukawa itairudishia Tanzania ujasiri wake wa awali. Edward Lowassa ambaye anatazamia kushinda Uchaguzi Mkuu kwa bahati nzuri ana uzoefu mkubwa kimataifa na hadi Bunge lilipovunjwa alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje. Kutokana na ufinyu wa nafasi, naomba kuishia hapa kwa leo. Tukutane Jumatano ijayo Mungu akipenda.

Mwandishi wa makala haya ni Ben Saanane,Ni Mkuu wa Idara ya Sera na Utafiti CHADEMA anapatikana kwa namba 0768078523.


- See more at: Raia Mwema - Ukawa tutarejesha heshima ya Tanzania kimataifa
 

KUPITIA makala hii, naamini Watanzania watatumia fursa ya uchaguzi Oktoba 25, kuifufua Tanzania ya Mwalimu Nyerere kupitia sanduku la kura kwa kuichagua Serikali ya Ukawa.
Mwasisi wa taifa letu, Mwalimu Nyerere aliipenda Tanzania na Afrika, hakupenda ukandamizaji ndani na nje ya mipaka yetu.Tanzania ilijiweka katika ramani ya dunia kutokana na msimamo na uongozi shupavu wa Mwalimu Nyerere kiitikadi, kifalsafa na kimaono.
Aliposimama katika Jukwaa la Umoja wa Mataifa kule New York, Afrika na mataifa mengine yaliyopinga ukandamizaji yalikuwa nyuma yake. Aliposimama katika Jukwa la Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), kule Addis Ababa-Ethiopia, wanamajumui (Pan-Africanist) walisimama nyuma yake.



Ben Saanane,

Nini msimamo wa CHADEMA na UKAWA kuhusu Western Sahara?
 
Adui anayelihujumu Taifa letu ameshajiingiza katika kila kona ya nchi na jamii yetu. Anajua ujinga wetu, udhaifu wetu na anahakikisha tunaendelea kuwa wanyonge na masikini!

Adui huyu ametufanya tuache kuongea mambo ya maana na msingi kwa Taifa letu, ametugeuza katika mkondo wa udaku, mipasho na kukosa kabisa kuongelea sera na ilani ambazo zingetuondoa kutoka unyonge, umasikini, unyonyaji, ufisadi na utegemezi.

Kwa bahati mbaya sana, si siri kuwa Adui huyu ameshikilia kwa nguvu na kupandikiza mizizi mikubwa na magugu ya uhujumu ndani ya Chama Tawala.

Chama Tawala kinang'ang'ani amadaraka ili kulinda maslahi ya Adui huyu na si kutaka kuwatumikia Watanzania na kuyashinda masumbufu yao ya kila siku.

Ni wazi ili tubadilike, tunalazimika kuachana na CCM!
Mkuu tuliposema tofauti kati ya majukumu na sera watu walituona wehu. Leo tunasikia wagombea wakisema watajenga madaraja, viwanja vya ndege n.k. Wamesahahu hayo ni majukumu ya serikali ya nchi yoyote duniani hata ya dikteta. Hatujaambiwa vinajengwa kwa kutumia sera gani na kwanini

Nadhani wanaotututhumu wanaweza kuona jambo, kama hawaoni basi tuendelee tu gizani gizani tukiahidiwa kla mmoja kuletewa umeme ndani ya nyuma na bomba la maji uani.
 
Baada ya kupitia ilani /dira ya chadema, azimio la Tabora na ilani ya CCM, nimekuwa dissapointed na CCM, Dira ya nchi ni MKUKUTA ambao kiini chake ni nchi za nje, ili ku seal hii dira wameichukua na kuiingiza kwenye ilani ya chama, lini tutatoka kwenye madeni ya world bank etc , lini serikali itamiliki kwa ufanisi miradi mikubwa ya maendeleo na huduma za jamii?
lini tutafanya maendeleo kwa kuanzia kwa wadau wa kuu wa maendeleo ambao ni wananchi, kama inavyofanyika kwenye nchi zinazoendelea?
Viongozi wa ccm wanaipeleka hii nchi katika lindi la umaskini na madeni,
kama kuna mabadiliko yeyote tunayohitaji kufanya ni kuanza kubadili vyama tawala na kuchagua vyama vinavyokubaliana na matakwa yetu , hata kama ni matakwa ya kubadilisha katiba, hiyo itakuwa chachu ya viongozi wa nchi kutimiza matakwa ya wananchi na kututoa kwenye utawala wa World bank and Co
"Ilani" ya CCm imenisikitisha sana
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom