Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

Unamaanisha nini unaposema "impeachment" sio suala la kisheria bali ni "political process"?
Anayefungua mashitaka ya impeachment ni bunge.
DOJ & SPECIAL COUNSEL wanapeleka mapendekezo tu kutokana na report ya uchunguzi then bunge ndio linaamua kufungua mashitaka ya impeachment au la. Kwa mujibu wa sheria za DOJ hawana uwezo wa kumfungulia mashitaka ya jinai raisi alieko madarakani na hio imeelezwa pia na Mueller kwenye tamko lake.
 
Kwa hio kwa sababu Mueller "hajapendekeza" impeachment specifically kama alivofanya Starr ina maana case closed? Unatumia ripoti ya Ken Starr kama kipimo kwamba Mueller nae alipaswa kuandika kwa muundo ule ule ndio uridhike?

Naona unataka tu kuendeleza ligi ya ubishi usio na maana yoyote.

Kutokupendekeza "impeachment" explicitly maana yake hamna clear grounds za impeachment, kitu kinachopelekea "case closed".

Lakini haimaanishi kuwa Dems hawawezi kuanza "impeachment proceedings," hapana! bali itakuwa ni impeachment isio na "merit".

Prosecutor lazima atende kama prosecutor, kuna standards za ku-practice na wala sio suala la Ken Starr kuwa kipimo.
 
Anayefungua mashitaka ya impeachment ni bunge.
DOJ & SPECIAL COUNSEL wanapeleka mapendekezo tu kutokana na report ya uchunguzi then bunge ndio linaamua kufungua mashitaka ya impeachment au la. Kwa mujibu wa sheria za DOJ hawana uwezo wa kumfungulia mashitaka ya jinai raisi alieko madarakani na hio imeelezwa pia na Mueller kwenye tamko lake.
Ni political process kwa sababu mwisho wa siku kitakachoamua ni wingi wa kura za wabunge ndio zitasema rais amekosea aondoke madarakani au la.
 
Ni political process kwa sababu mwisho wa siku kitakachoamua ni wingi wa kura za wabunge ndio zitasema rais amekosea aondoke madarakani au la.

Unaweza kutoa ufafanuzi kidogo juu ya huo wingi wa kura za kuweza kumtoa Rais madarakani? Je, Dems wanaweza kumtoa Rais Trump madarakani ikizingatiwa kuwa wana majority kwenye House?
 
Unaweza kutoa ufafanuzi kidogo juu ya huo wingi wa kura za kuweza kumtoa Rais madarakani? Je, Dems wanaweza kumtoa Rais Trump madarakani ikizingatiwa kuwa wana majority kwenye House?
Mchakato unaanzia kwenye HOUSE then unaenda juu kwenye SENATE. Democrats wakianzisha mchakato wanaweza kufanikiwa kwenye ngazi ya HOUSE lakini wakienda SENATE ambako Republicans ni majority watagonga mwamba. Na ndio maana mpaka sasa hivi bado wanajishauri endapo waendelee na mchakato hivyo hivyo au wapotezee.

Ndio maana nimesema impeachment in general ni SIASA sababu kwa mazingira ya sasa ni mpambano wa Republicans vs Democrats na kila kambi imeegemea upande wake hakuna matumaini ya kubadilika!
 
Umeeleweka mkuu!

Kwahiyo kwa maoni yako, kwa mazingira ya sasa ni CASE CLOSED au CASE NOT CLOSED? Ukizingatia hakuna Republican hata mmoja aliyesema ana-support impeachment!
 
Umeeleweka mkuu!

Kwahiyo kwa maoni yako, kwa mazingira ya sasa ni CASE CLOSED au CASE NOT CLOSED?

Kwa maoni yangu ni 50/50 lolote linaweza kutokea.

Yote yatategemea na jinsi kesi itakavyofunguliwa na ushahidi utakaotolewa. Endapo kutakuwa na hoja nzito itawaweka wabunge wa republican ktk wakati mgumu endapo wataendelea kumtetea Trump inaweza kuwagharimu kwenye uchaguzi mwakani.

Ukiangalia hoja nyingi zinazojengwa sasa hivi sio masuala ya COLLUSION na warusi bali OBSTRUCTION OF JUSTICE ambayo nayo ni kosa kisheria. Kitendo cha WH kuwazuia baadhi ya watumishi kufika mbele ya congress kwa mahojiano pamoja na kuzuia tax return za bwana mkubwa inaweza kujengewa hoja au kesi ya obstruction of justice mbele ya safari.

Like i said before.... its 50/50
 
Nimeelewa maoni yako, ila ulivyosema "endapo kutakuwa na hoja nzito" unamaanisha mpaka sasa hujaona hoja nzito ya kuwashawishi Republicans? Je, unafahamu kuwa hamna Republican hata mmoja anae-support impeachment?

Je, unafahamu kuwa ni Dems 35-38 kati ya 238 wanaounga mkono impeachment kwa sasa (kwa mujibu wa Pelosi)? Unakubali kwamba kwa namba hizo hoja ya "impeachment" bado haina nguvu hata kwa Dems wenyewe?

Je, unafahamu kuwa zaidi ya asilimia 60 ya wamarekani hawataki impeachment dhidi ya Trump? (Ikizingatiwa kuwa wana taarifa ya Mueller mkononi).Unafikiri ni kwanini wananchi wengi hawawaungi mkono Dems kwenye hili?
 
Nimeelewa maoni yako, ila ulivyosema "endapo kutakuwa na hoja nzito" unamaanisha mpaka sasa hujaona hoja nzito ya kuwashawishi Republicans? Je, unafahamu kuwa hamna Republican hata mmoja anae-support impeachment?

Je, unafahamu kuwa ni Dems 35-38 kati ya 238 wanaounga mkono impeachment kwa sasa (kwa mujibu wa Pelosi)? Unakubali kwamba kwa namba hizo hoja ya "impeachment" bado haina nguvu hata kwa Dems wenyewe?

Je, unafahamu kuwa zaidi ya asilimia 60 ya wamarekani hawataki impeachment dhidi ya Trump? (Ikizingatiwa kuwa wana taarifa ya Mueller mkononi).

Ni kweli spika Nancy Pelosi amekuwa haungi mkono hoja ya impeachment pamoja na shinikizo kutoka caucus ya chama chake... lakini kwa mwendelezo wa matukio ya sasa ambapo WH haiko tayari kutoa ushirikiano wowote ule kwa congres na wamewakataza watu wao kutoitikia wito kwenda kuhojiwa na kamati za bunge, pamoja na kukataa kutoa tax returns inawageuza hata wale ambao mwanzoni walikuwa hawaungi mkono impeeachment kuanza kubadili mawazo yao. Kwa kifupi ni Trump mwenyewe ndio anawapush Democrats wamuimpeach... he is daring them to do it. Pelosi mwenyewe kwa sasa anaanza kuona kwamba hakuna namna nyingine ya kukabiliana na Trump isipokuwa impeachment proceedings manake njia za kawaida zimeshindikana.

Kuhusu republicans wanaounga mkono impeachment wameanza kidogo sana kujitokeza mfano Representative Justin Amash wa jimbo la michigan (R)
 
House Dems wana Representatives 235 wakati wanahitaji 218 tu kupitisha impeachment trial dhidi ya Trump, Justin Amash ni mtu mmoja na Republicans kwenye House hawana impact kwenye uamuzi wa Dems.

Unamaanisha nini ulivyosema "njia za kawaida zimeshindikana kukabiliana na Trump"? Unahisi kwanini Dems wengi hawaungi mkono "impeachment"? Unafahamu kuwa kuna uchunguzi unaendelea DOJ kuhusiana na namna uchunguzi dhidi ya Trump ulivyoanza?

Pia unafikiri ni kwanini zaidi ya asilimia 60 ya wananchi hawawaungi mkono Dems kwenye njia ya impeachment?
 
..lakini kwa mwendelezo wa matukio ya sasa ambapo WH haiko tayari kutoa ushirikiano wowote ule kwa congres na wamewakataza watu wao kutoitikia wito kwenda kuhojiwa na kamati za bunge, pamoja na kukataa kutoa tax returns inawageuza hata wale ambao mwanzoni walikuwa hawaungi mkono impeeachment kuanza kubadili mawazo yao. Kwa kifupi ni Trump mwenyewe ndio anawapush Democrats wamuimpeach... he is daring them to do it.

Unafahamu kuwa kuna baadhi ya Dems kama Adam Schiff na Jerry Nadler walidai kuwa Trump ndiye anamzuia Mueller kuhojiwa Congress?

Unafahamu kuwa hata Obama na Clinton waliwahi ku-invoke executive privilege kuzuia Congress kupata taarifa? Je, kitendo hicho sio cha kawaida kufanywa na Rais anapoona inafaa kufanya hivyo?

Rais kutoa tax returns ni obligation au ni custom? Kila mtu anajua kuwa House Ways and Means Committee inatumika kisiasa kuhitaji taarifa za tax za Trump, hivyohivyo kwa House Oversight Committee kutaka financial records za Trump. Je, unadhani ni sahihi Trump kucheza michezo ya kisiasa ya Dems wakati kuna mambo mengi ya muhimu ya kutekeleza?
 
Ni political process kwa sababu mwisho wa siku kitakachoamua ni wingi wa kura za wabunge ndio zitasema rais amekosea aondoke madarakani au la.
Yes ni political process kwasababu mchakato mzima unasimamiwa kisiasa. Chief Justice ana preside kura katika senate bila kutumia kipengele chochote cha mahakama

Ni political process kwasababu uamuzi hatugemea utashi wa wapiga kura
Rais Clinton aliokolewa na maseneta 2, mchakato mzima ukaishia hapo. Hakuna appeal

Kinachofanyika katika impeachment ni kuwa na ushahidi wa kutosha kushawishi wajumbe
Katika House hakuna shaka, tatizo lipo katika senate ambako lazima maseneta 20 watoke GOP

Ili kupata ushahidi, Chair Nadler alitaka unredacted Mueller report with all underlying evidence
Hapa ndipo baadhi wanachanganya au hawaelewi. Underlying evidence hazikuombwa kwa Mueller kwasababu alipokabidhi ripoti hakuwa na kauli yake. Ndiyo maana AG Barr alisema '' it is my baby''. Hakuna mahali kundi lolote limeomba underlying evidence kwa Mueller

Ni kwa msingi huo AG Barr alikataa kutoa taarifa nzima na underlying evidence, na katika kukwepa hilo akamwambia Rais atumie executive privilege ili taarifa na underlying evidence ziwe katika mamlaka ya WH

Kwanini Mueller aliliongelea jana? Ni kwasababu alikuwa anawaeleza Wamarekani kuwa Taarifa yake na ushahidi vipo DOJ, viungani DC wanasema ali 'insinuate'' kuwa ameweka mchakato kwa congress na vidhibiti vipo

Ninaposoma habari kuwa Dems walitaka Mueller apeleke underlying evidence, napigwa na mshangao. Tupo dunia tofauti, Mkuu Kichuguu anasema first amendment ya kila mtu inalindwa
 
Kwa hio kwa sababu Mueller "hajapendekeza" impeachment specifically kama alivofanya Starr ina maana case closed? Unatumia ripoti ya Ken Starr kama kipimo kwamba Mueller nae alipaswa kuandika kwa muundo ule ule ndio uridhike?

Naona unataka tu kuendeleza ligi ya ubishi usio na maana yoyote.
Mkuu Mwalimu, Ukiona mtu analinganisha embe na nanasi kwa kuangalia kuwa yote ni matunda, yana majani, yanaota ardhini, yana utamu bila kuelewa tofauti zake ujue kuna tatizo

Ken Starr alikuwa independent counsel aliyeteuliwa na majaji watatu wa DC Circuit
Ndiyo maana taarifa yake ilikwenda kwa majaji na congress na kwamba hakukuwepo nafasi ya Rais Clinton kutumia ''executive privilege'' kwa namna yoyote. Taarifa ya Ken Starr ipo wazi

Mueller ni special counsel chini ya DOJ. Kwa sheria yupo chini ya AG wa US
Ndiyo maana taarifa yake aliifikisha kwa AG ambaye ni mkuu wa DOJ
Kwa mantiki hiyo shinikizo lililpozidi AG akamshauri Rais Trump aifiche taarifa kwa exec privilege

Kwahiyo impeachment ya Trump inatakiwa iende pamoja na underlying evidence ambazo DOJ kwa kumtumia Trump na exec privilege wamezificha.
Nancy Pelosi na Nadler wanatumia mahakama ili kuweza kupata underlying evidence

Ukiisoma taarifa ya Mueller ni tofauti na ya AG Barr aliyefanya watu wakabugia matango pori
Barr anasema Mueller amesema hakuna collusion kati ya Russia na Trump
Mueller anasema hakuna sufficient evidence za conspiracy kati ya Trump na Russia

Hapa kuna neno, anaposema sufficient tayari anatueleza kuna evidence ambazo haziku rise katika level ya kuendesha mashtaka. Hii haina maana kuwa hakuna evidence kwa wanaosoma between the lines bali haikufikia kiwango cha mashtaka

Kwa upande wa obstruction of justice, AG Barr alisema hakukuwepo na conclusion ya Mueller
Again, ukisoma vizuri Mueller ameainisha hoja 10 za obstruction of justice
Kwa maana nyingine kinachotakiwa ni underlying evidence ili kuanza mshtaka katika congress

Hiyo ndiyo sababu Barr na Trump wametumia exec privilege kwani kuficha underlying evidence kunabakiza hoja ambazo hazisimami wima zenyewe

Katika hoja za Mueller hakuna mahali palipo na underlying evidence kwa maana yake halisi kama mwenzetu anavyotuaminisha na wala hakuna mahali hoja imekuwa underlined na hivyo kuwa underlying evidence

Wote wawili, independent counsel na Special counsel wana majukumu sawa, tofauti yao ni eneo au mamlaka zinazowasimamia

Ulingano kuwa wote wanachunguza Marais bila kujua mamlaka zao unaeleza jambo, hasa ubishi tu kwavile kuna keyboard mbele
 
Ili kupata ushahidi, Chair Nadler alitaka unredacted Mueller report with all underlying evidence
Hapa ndipo baadhi wanachanganya au hawaelewi. Underlying evidence hazikuombwa kwa Mueller kwasababu alipokabidhi ripoti hakuwa na kauli yake. Ndiyo maana AG Barr alisema '' it is my baby''. Hakuna mahali kundi lolote limeomba underlying evidence kwa Mueller

Ni kwa msingi huo AG Barr alikataa kutoa taarifa nzima na underlying evidence, na katika kukwepa hilo akamwambia Rais atumie executive privilege ili taarifa na underlying evidence ziwe katika mamlaka ya WH

Kwanini Mueller aliliongelea jana? Ni kwasababu alikuwa anawaeleza Wamarekani kuwa Taarifa yake na ushahidi vipo DOJ, viungani DC wanasema ali 'insinuate'' kuwa ameweka mchakato kwa congress na vidhibiti vipo

Ninaposoma habari kuwa Dems walitaka Mueller apeleke underlying evidence, napigwa na mshangao. Tupo dunia tofauti, Mkuu Kichuguu anasema first amendment ya kila mtu inalindwa
Executive privilege inatumiwa na Rais kuzuia taarifa kwa Congress, mahakama na umma kwa sababu kuu mbili: usalama wa taifa na faragha (privacy) ya wafanyakazi wa WH.

Bill Clinton ali-claim executive privilege mara 14 wakati wa uchunguzi wa Whitewater na Monica Lewinsky ikiwemo kumzui mke wake (Hillary Clinton) ku-testify na kujizuia yeye mwenyewe ku-testify. Hizo claims zilishindwa mahakamani.

Mtu unaposema "Clinton hakuwa na nafasi ya kutumia executive privilege kwa namna yoyote", ni vyema akaangalia upya historia.

Kingine, kuhusu executive privilege ya Trump kwenye ripoti ya Mueller na underlying evidence, Trump wala hakuwa na nia ya kutumia executive privilege. Ndio maana ndani ya ripoti ya Mueller iliyo public mawasiliano ya White House yapo wazi.

Tatizo Dems walikuwa wakimsukuma AG Barr kutoa taarifa ambazo haruhusiwi kutoa kisheria kwa maana ya grand jury materials. Ndio maana Barr akawaambia hazitoi na haoni exception ya kuzitoa, kwamba kama wanazihitaji waende mahakamani. Dems wakamtishia Barr kumshtaki kwa kudharau Congress (contempt).

Ni muhimu ukifahamu Federal rules of criminal procedure 6(e), ili kuelewa kwanini grand jury materials zinalindwa, na kwanini AG Barr alisema haoni exception zilizopo kisheria kama zina-apply kwenye case ya ripoti ya Mueller na underlying evidence zake.

HJC chini ya Nadler walipomtishia AG Barr kumshtaki kwa kudharau Congress kwa maana ya kukataa kutoa full report (yenye grand jury materials) na underlying evidence, ndipo Barr alipomuomba Trump atumie executive privilege ili Dems wakafuate agizo (order) mahakamani kupata taarifa hizo.

Hata hivyo, AG Barr amekataa kuwasaidia Dems kwenda mahakamani kupata taarifa hizo kama wanavyomuomba. Hii ni kwa sababu Dems hawamuheshimu AG Barr, huwezi kumdharau mtu na kutishia kumshtaki halafu ukamuomba akusaidie jambo ambalo ni hiari yake kusaidia au kutosaidia.

Mahakama ndiyo itakayoruhusu Dems waone Full report na underlying evidence. Na itakuwa ni vyema hizi kesi za executive privilege na grand jury zikaamuliwe Supreme Court.

Kuhusu underlying evidence, haina haja ya kutumia kejeli, kila mtu anajua Jerry Nadler ali-issue subpoena kwa AG Barr kwa ajili ya kupata Full report na underlying evidence! Na hata posts zangu za nyuma niliandika hivyo.

Hata hivyo baadhi ya Dems baada ya kuona Barr hatoi ushirikiano, walidhani wanaweza kum-subpoena Mueller alete transcripts zake! Kama walivyom-subpoena McGhan alete underlying evidence (documents na transcripts) alizompa Mueller. Hizi documents na transcripts ni sehemu ya full underlying evidence zilizo chini ya AG Barr wanazotaka Dems.

Nilikuomba uonyeshe wapi nilisema underlying evidence zimepigwa mistari umeshindwa kuonyesha, sio vizuri kutunga vitu!

Kwahiyo, unaweza kujibu na kukashifu ukidhani watu hawaelewi au wanachanganya kumbe wewe ndio hujaelewa.
 
Ukiona mtu analinganisha embe na nanasi kwa kuangalia kuwa yote ni matunda, yana majani, yanaota ardhini, yana utamu bila kuelewa tofauti zake ujue kuna tatizo

Ken Starr alikuwa independent counsel aliyeteuliwa na majaji watatu wa DC Circuit
Ndiyo maana taarifa yake ilikwenda kwa majaji na congress na kwamba hakukuwepo nafasi ya Rais Clinton kutumia ''executive privilege'' kwa namna yoyote. Taarifa ya Ken Starr ipo wazi

Mueller ni special counsel chini ya DOJ. Kwa sheria yupo chini ya AG wa US
Ndiyo maana taarifa yake aliifikisha kwa AG ambaye ni mkuu wa DOJ
Kwa mantiki hiyo shinikizo lililpozidi AG akamshauri Rais Trump aifiche taarifa kwa exec privilege

Kwahiyo impeachment ya Trump inatakiwa iende pamoja na underlying evidence ambazo DOJ kwa kumtumia Trump na exec privilege wamezificha.
Nancy Pelosi na Nadler wanatumia mahakama ili kuweza kupata underlying evidence

Ukiisoma taarifa ya Mueller ni tofauti na ya AG Barr aliyefanya watu wakabugia matango pori
Barr anasema Mueller amesema hakuna collusion kati ya Russia na Trump
Mueller anasema hakuna sufficient evidence za conspiracy kati ya Trump na Russia

Hapa kuna neno, anaposema sufficient tayari anatueleza kuna evidence ambazo haziku rise katika level ya kuendesha mashtaka. Hii haina maana kuwa hakuna evidence kwa wanaosoma between the lines bali haikufikia kiwango cha mashtaka

Kwa upande wa obstruction of justice, AG Barr alisema hakukuwepo na conclusion ya Mueller
Again, ukisoma vizuri Mueller ameainisha hoja 10 za obstruction of justice
Kwa maana nyingine kinachotakiwa ni underlying evidence ili kuanza mshtaka katika congress

Hiyo ndiyo sababu Barr na Trump wametumia exec privilege kwani kuficha underlying evidence kunabakiza hoja ambazo hazisimami wima zenyewe

Wote wawili, independent counsel na Special counsel wana majukumu sawa, tofauti yao ni eneo au mamlaka zinazowasimamia

Ulingano kuwa wote wanachunguza Marais bila kujua mamlaka zao unaeleza jambo, hasa ubishi tu kwavile kuna keyboard mbele

Mamlaka ya Special Counsel au Independent Counsel haiathiri hitimisho la ripoti yake:

Nixon ndiye Rais wa kwanza kumteua Special Prosecutor (Archibald Cox) mwaka 1973 ili kuchunguza Watergate. Hakukuwa na sheria ya kusimamia uteuzi wa Special Counsel wala mamlaka na mipaka yake. Ndio maana Nixon aliweza kumtimua Cox alipohitaji WH tapes na akasumbua katika kumteua Jaworski akidai hawakuwa na mamlaka hayo.

Mwaka 1977, Congress wakapitisha sheria ya Ethics in Government Act (EGA) ili kuunda utaratibu wa kumteua wachunguzi maalum (special investigators).

Katika utaratibu huu AG anaanzisha uchunguzi, akiona kuna haja kuwepo uchunguzi maalum anapeleka hilo ombi mbele ya majaji watatu ili wateue mchunguzi maalum (independent counsel). Pia Congress inaweza kumuomba AG aanzishe uchunguzi. Huyu mchunguzi anafanya uchunguzi kwa Approval ya AG. AG au Congress walikuwa na mamlaka ya kumuondoa huyu mchunguzi maalum.

Huu ndio utaratibu uliotumiwa kumteua Ken Starr mwaka 1998, ambaye alikuwa approved na AG Janet Reno. Mwaka huohuo (1998) Supreme Court wakaamua kuwa sheria ya EGA ya mwaka 1977 ni constitutional (8-1). Huku Justice Scalia pekee akiipinga, akisema sio constitutional kwa sababu inapoka mamlaka ya mhimili wa Executive na kuunda mhimili wa nne wa serikali. Kwa maoni yake, Independent Counsel alikuwa na mamlaka makubwa ya DOJ ya uchunguzi na uendeshaji wa mashkata. EGA ili-expire mwaka 1999 na haikuwa 'renewed'.

Toka mwaka 1999, kanuni mpya ya Code of Federal Regulations ndio inatumika kumteua mchunguzi maalum (Special Counsel). Kanuni hii imempa mamlaka makubwa AG kwenye uteuzi wa mchunguzi maalum na kusimamia uchunguzi wake. Congress inaweza kumuomba AG ateue mchunguzi maalum. Huyu mchunguzi anaweza kuondolewa na AG. Special Counsel ana mamlaka kama US Attorney.

Huu ndio utataribu unaotumika hadi leo na ndio aliotumia AG Rod Rosenstein kumteua Bob Mueller mwaka 2017.

Ukiangalia utaratibu wa uchunguzi wa Ken Starr na Bob Mueller, Congress sio mteuzi wala msimamizi wa mchunguzi maalum bali ni mtumiaji wa ripoti za mchunguzi maalum kwa ajili ya shughuli zake za kikatiba za "oversight".

Independent Counsel Starr na Special Counsel Mueller wote walikuwa na mamlaka sawa ya kushtaki makosa.

Katika taratibu zote mbili bila AG kuamua, kusingekuwa na teuzi za wachunguzi maalum. Tofauti ndogo ya utaratibu wa teuzi za Mueller na Starr hakuwezi kuathiri hitimisho za ripoti zao, na kumfanya Mueller ashindwe kuhitimisha na kutoa mapendekezo baada ya uchunguzi. Na kusingekuwa na watu wanaotaka kumuuliza Mueller sababu za kufanya hivyo.

Kingine, Mueller anaposema "insufficient evidence to warrant a charge of criminal conspiracy" baada ya miaka miwili ya uchunguzi, maana yake hamna "indictment" kwenye criminal justice system. Utakuwa ni ujuha kwa mtu kuhitaji underlying evidence ili kumcharge Trump kwa kosa hilohilo la conspiracy kwa sababu definition ya "conspiracy" inayotumika ni ileile.

Kitendo cha Dems kusubiri underlying evidence kwa ajili ya kesi ya "obstruction", maana yake kwa ripoti jinsi ilivyo hawaoni hoja nzito? Kwamba episodes 10 za Mueller hazisimami wima zenyewe?
Mueller amesisitiza kuwa ripoti yake ndio ushahidi wake, kwamba haoni cha kuongeza! maana yake ripoti yake inasimama yenyewe.

Dems hawahitaji underlying evidence ili kuanzisha impeachment! Wanaweza tu kuanza then kisheria watapata full report na underlying evidence na watahoji watu wote wanaowataka. Kimbembe ni kwamba hawawezi kupata grand jury materials bila kuanza mchakato huo. Mpira upo kwa Dems, wanatakiwa kuamua cha kufanya na mwisho wa siku hawawezi kumuondoa Trump.
 
Hasira za Trump kuelekea kwa Mueller zinatokana na nini? Ikiwa anaamini ripoti ya Mueller haijamkuta na makosa kwa nini ana hasira nae? View attachment 1112704
Hapo naona Trump anatoa maoni yake kuhusu jambo ambalo anaamini lingeweza kuondoa 'impartiality' ya Mueller kwenye uchunguzi wake. Hata hivyo ofisi ya Maadili ya DOJ haikukubaliana na maoni hayo.
 
Hasira za Trump kuelekea kwa Mueller zinatokana na nini? Ikiwa anaamini ripoti ya Mueller haijamkuta na makosa kwa nini ana hasira nae? View attachment 1112704
Ninawajua marais saba tu wa marekani kuanzia na Jimmy Carter. Ukiachia George H.W. Bush, marais wingene wote wa republican walikuwa na mapupungufu sana intellectually; ila Reagan alikuwa na busara ya kujua intellectual limitations zake akajicontrol kwa kujizungusha na washauri wazuri, kujenga nidhamu ya kuwasikiliza, na kutumia kipaji chake cha kuongea , na hivyo akafanikiwa sana. George W. Bush alitaka kumwiga Reagan, lakini akapungukiwa na busara kidogo na akshindwa kujijengea heshima aliyopata reagan. Bahati nzuri G.W. Bush alikuwa na malezi mazuri hivyo mapungufu yake yakawa neutralized na tabia zake binafsi. Huyu jamaa naona ndiye takataka sana. Ana miaka sabini lakini amekuwa kila siku mlalamishi wa kutaka attention tu; anajivuna kuwa uchumi umekuwa imara chini yake huku ikiwa wazi kuwa hakubadilisha trajectory ya Obama, aliingia kweye msafara wakati uko kwenye lango halafu anajivuna kuwa ni yeye aliyeingiza msafara ndani. Haya mambo ya kuwa anaandika twitts kila wakati kulalamika lalamika, au kudai kusifiwa ni dalili ya utoto sana, na nadhani marais wengine wote wameshamjua; Rais wa China hana taimu naye tena. Trump hanywi pombe ila naona amezeeka na akili ya kitoto.
1113188
 
Kama ulishindwa kutetea hoja zako au kujibu zangu ungeweza kutumia busara ukakaa tu kimya na sio ku-quote kila kitu bila "substance" ili kuonyesha kuwa angalau umejibu.

Kama uelewa wako ndio sahihi kuliko, ungeuonyesha kwa kupangua hoja zangu kwa kutumia ukweli halisi na sio kuandika vitu visivyojenga hoja zako!
Unfortunately huwa siwezi kurudia kuandika vitu ambavyo viko wazi. Kwa mfano unaposema hivi
1113451

Ina maana hufuatilii habari hizo kwa karibu na wala hujui hili hapa

Unaposema hivi

1113455
Unaonyesha kutokujua namna ya kuunganisha habari za kisheria. Mueller anasema kuwa yeye hakuwa amepewa mamlaka ya kumshitaki Trump, na pia amesema utaratibu wa fairness unamzuia kumtuhumu mtu ambaye atashindwa kumpeleka mahakani akajitetetee. Kwa hiyo akasema hawakumtuhumu kwa hatia, na pia hawakuona kuwa hana hatia. Hiyo ni neutral conclusion ambayo Barr asingeitumia kusema kuwa hana Trump hatia. Hana mamlaka ya kusema nani ana hatia au hana hatia; kazi yao ni kutuhumu na kuziachia mahakama kuamua kama kuna hati au vipi.

Analysis yako hapa haina msingi wowote.

1113480
Prosecutor anakutuhumu tu anapodhani una hatia. Iwapo wangemwona hana hatia, wangesema kuwa hatumkuta na hatia yoyote ya kumtuhumu. Kuna lugha nyingi za kutumia, kwa mfano hakuna ushahidi wowote, au ushahdi tuliopata hautoshi kumtuhumu, kama ambavyo walivyosema kwenye volume 1. Hata hiyo conclusion ya volume 1, ilisema tu ushahidi upo wa conspiracy, lakini hautoshi kuprove beyond reasonable doubts- standard ya criminal prosecution.

Nafikiri hiki kipande hiki chini ndicho hukuelewa kabisa, inagwa nimeshakigusia hapo juu. Huwezi kumtuhumu mtu ambaye huwezi kumshitaki akajitetea. Mueller alifanya kazi chini ya huo msingi kuwa huwezi kumshitaki Rais; kwa hiyo asingeweza kusema kuwa kuwa ana hatia, kwa vile hakuwa na uwezo wa kumshitaki (Department policy) na kumpa nafasi ya kujitetea (principles of fairness). Kama unakumbuka mwaka 2016 kabla ya uchaguzi, Combey alilaumiwa sana kwa kumtuhumu mams Clinton halafu na kuishia kusemahakuna ushahidi wa kutosha kumshitaki. Hiyo inaitwa character assassination ambayo wanasheria hawafanyi hivyo mahakamani.

1113495
Kabla sijamaliza kipande hicho; usichukue neno "actual charge" kama muujiza fulani in isolation; nimekwelza hapo juu ni kuwa unamptuhumu mtu, lazima apewe nafasi mahakani kujitetea dhidi ya tuhuma hizo.

1113501

Sentensi hiyo ndiyo nyepesi kuliko zote. Anakuambia kuwa criminal justice system aliyokuwa akiendesha haina mamlaka ya kumtuhumu rais kwa makosa; katiba ina utaratibu mwingine wa kufanya hivyo. Maana yake nikuwa utaratibuhuo mwingine ndio utumike.

Again; bado ninaheshimu first ammendment rights zako.
 
Kwa ufahamisho tu, House ilipoanza impeachment proceedings dhidi ya Richard Nixon, wengi wa Republicans hawakuunga mkono lakini hizo proceedings ndizo ziliibua ushahidi uliowawezesha hata hao Republicans kubadilisha msimamo. Kabla ya hapo alikuwepo Republican mmoja tu aliyejitokeza na kuunga mkono impeachment ya Nixon lakini baada ya ushahidi wa tapes kuibuliwa kwenye proceedings ndipo na wenzake walipounga mkono.

Hali kama hiyo ndiyo ipo mpaka sasa lakini tofauti inayojitokeza wakati huu ni Spika Pelosi kutaka kabla ya hizo proceedings kuanza ushahidi zaidi upatikane na anajua utapatikana. Hivyo anawataka Democrats kwenda taratibu bila pupa ili wananchi wapate muda wa kutosha wa kujua kwa nini Donald Trump awe impeached. Viongozi wengi wastaafu wa GOP tayari wanaanza kujitokeza kuunga mkono wazo la kumtaka Rais Trump awe impeached.

Katika wiki ya kesho mengi zaidi yataibuliwa kulingana na kesi zinazoendelea mjini New York chini ya grand juries zilizoundwa na Robert Mueller ambapo baadhi ya redactions alizofanya AG Barr zimeamriwa zianikwe kwa wananchi. Na hapa ndipo Trump anapopata wazimu kwa nini impeachment haianzi mara moja kama alivyotegemea yeye. Alitaka impeachment ianze huku wananchi walio wengi ikiwa bado hawajui kinachoendelea lakini Pelosi katia breki.

Hasira yote ya Trump inaanzia hapo; mipango yake na wanasheria wake imevurugika kwani hawajui ni lini House itaanza proceedings na hajui ushahidi utakaokuwa umepatikana wakati huo. Ndugu zangu Marekani mambo kama haya huenda taratibu na si kwa pupa kama wengi wananvyofikiria. Sheria ya Marekani inawalinda sana wenye tuhuma mbali mbali na ni pale tu ushahidi unatosheleza ndipo hatua huchukuliwa na hili Pelosi analijua fika.

Halafu ipo hii dhana inayoenezwa zaidi na GOP kwamba impeachment inaweza ikawaathiri sana Democrats kwenye uchaguzi ujao. Hii ni kweli inaweza ikatokea kama Democrats hawakujipanga vizuri lakini kwa style ya Pelosi ya kukataa kukurupuka bila ushahidi wa wazi na unaojitosheleza. Pia wanafuatilia matamshi yote ya Trump na kila kauli anayotoa inachunguzwa kwa umakini mkubwa kwa sababu wanajua woga wake ndio unamfanya aropoke hovyo.
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom