El Jefe
JF-Expert Member
- Sep 13, 2016
- 293
- 364
Sidhani kama kuna kipya kwenye hii kesi. Dems kwa hesabu zao wanataka waungwe mkono na public na Republicans kwa kufanya partisan hearing taratibu kwa mda mrefu, huku wakitafuta "conspiracy" ambayo Mueller amehitimisha haipo.Naona humjui Nancy Pelosi, DEMS wako pamoja tena sana tu. Impeachment itaendeshwa na House na hapo ndipo ushahidi wote wa alichonuia Mueller utakapoonekana wazi hata kwa waliopofuka kimapenzi na Trump.
Nancy anawataka DEMS kutokurupuka, anataka kwanza ripoti kamili ya Mueller ikiwepo kuwa-subpoena wahusika pamoja na Barr, Rosenstein na Mueller mwenyewe lakini mwisho ni impeachment, hakuna namna.
Kumbuka hata hiyo ripoti iliyotolewa na Barr bado ni redacted...zinazopenyezwa ni kwamba ripoti nzima ya Mueller ambayo lazima itapatikana kwenye impeachment process imemkaanga vibaya Trump mpaka kwenye tuhuma za conspiracy. Collusion is a non-issue.
Issue ya Rais Clinton ilikuwa ni ndogo sana kisheria labda kimaadili...eti kufanya mapenzi na intern. Kama Senate haitaafiki maamuzi ya House, hilo ni jambo lingine lakini halizuii House kutekeleza wajibu wake. Je unasemaje kuhusu Richard Nixon?
Je aliyofanya Trump angefanya Obama, kweli leo Republicans wangekaa kimya? Je unakumbuka walivyotaka kum-impeach kwa kutumia tu Executive Action kwenye swala la DACCA?
Hii ya kusema kwamba "unredacted report" inaonyesha "conspiracy" au "imemkaanga Trump" kwakweli sijui mnaitoa wapi, maana aliyehitimisha ni aliyefanya uchunguzi. "Conspiracy" ingekuwepo sehemu zilizofichwa, hitimisho la ripoti ingekuwa tofauti na ilivyo, it's just common sense.
Kuhusu "obtruction of Justice" ya Clinton kasome vizuri, ni zaidi ya "kufanya mapenzi na intern".
Dems waliopo House wafanye wanachofanya kwenye huo mkakati wao, lakini mwisho wa siku wakipeleka hiyo "trial" Senate itaishia "Acquittal". Huo ndio ukweli mchungu.
Kesi ya Nixon ilikuwa "too clear", "obstruction" yake ililenga kuingilia uchunguzi wa kosa la msingi alilofanya (underlying crime) ambayo ilikuwa ni kutuma watu kufanya "wiretapping" kwenye DNC HQ. Ushahidi ukawekwa, mtu hawezi kubisha, na ndio maana aliondoka mwenyewe mapema.
Kwa Trump, kesi ya "obstruction" imesimama hewani.