Mlenge
R I P
- Oct 31, 2006
- 2,125
- 2,291
Ndugu yangu Mlenge, ningekushauri ujikite kwenye siasa za dunia ya tatu kama Tanzania, hii ya kimataifa inakuzidi kimo. Hii ni kama katoto ka chato kushiriki katika mijadala inayohusu matumizi silaha za nyuklia. Hiyo dola kaa tu ukiisikia, dola ni currency ya dunia na ndio maana hata katoto kama wewe kanaisikia. Dola ikiyumba, uchumi wa dunia unayumba. Uchumi wa Tanzania ukiyumba, ule wa jirani zetu wala hautashtuka! Kalaghabaho!
Mkuu Mag3;
Yawezekana kweli masuala ya kimataifa yamenizidi kimo, lakini hiyo haihusiki na usahihi wa hoja nilizotoa. Kujadili usahihi wa hoja kwa vigezo vya kimo cha mtoa hoja, si mahala pake kwenye jamii ya wanazuoni, hasa wa aina ya fikra za hali ya juu - great-thinkers..
Kukataa hoja kwa minajil ya kuangalia imetolewa na nani huitwa Ad hominem logical fallacy.. Hata saa iliyokufa husema kweli mara mbili kwa siku.
Hukutubainishia iwapo zilizosemwa ni kweli changamoto kuu kwa Marekani au la. Tujaalie na sababu za kuweka hoja hizo. Utakuwa umetufaa sana.