Duru Za Siasa: U.S Chini ya Donald J. Trump

Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,071
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,071 2,000
Wanajamvi

Uchaguzi wa US umekamilika jana baada ya D.J Trump kuwa Rais wa 45
Leo ilikuwa siku ya kwanza kamili ya Trump kama Rais wa US

Uzi utakuwa utaangalia serikali mpya na mwelekeo wa siasa na uchumi
Siasa za Marekani , taifa lenye nguvu katika uso wa dunia zinaathari kubwa duniani

Ni kwa kuzingatia hilo, uzi utaleta kwa kadri, yanayojiri katika Taifa hilo

Tutaendelea kumalizia hotuba ya Trump baada ya kutawazwa katika uzi huu
Duru za Siasa: Matokeo ya Uchaguzi Marekani

Rais Trump, mfanyabiashara aliyefanikiwa katika biashara ameondoka katika utawala wa makampuni na sasa ni mtawala wa umma na Taifa la Marekani

Kuchaguliwa kwake kama mtawala wa juu wa Taifa lenye ushawishi umekuja na mshtuko kutokana na nafasi aliyopewa katika uchaguzi wa ndani ya chama cha Republican na ule mkuu

Kuna mitazamo tofauti kuhusu kuchaguliwa kwa Trump. Kwasababu zozote ambazo wachunguzi wanaendelea kuzifuatilia kisiasa , uchumi, jamii n.k. Trump ndiye Rais wa Marekani

Siku ya kwanza, Trump amekumbana na changamoto za utawala wa nchi na si kampuni binafsi

Katika historia ya miongo michache ya Marais wa US, siku ya kwanza haikuwa nzuri kwake

1. Maandamano ya wanawake duniani
2. Ziara iliyozua utata katika Intelligence community (IC)

Tutajadili mambo hayo mawili na picha ya haraka ya nini kitarajiwe kwa siku za usoni

Tusemezane
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,071
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,071 2,000
Naomba pia kuuliza maana ya neno "GOP"
Nimekuwa nikilisoma mara kwa mara kwenye siasa za marekani.
GOP inasimama badala ya maneno Grand old party ambayo ni Republicans
Ni jina la utani ambalo lilianzia na maneno gallant old party, nyumbani kwa wahafidhina(conservatives) hawa ukisikia neno right wing au bawa la kulia ndio wenyewe
Ukisikia left au bawa la kushoto ni Democrats

Conservatives ni watu wanaolinda thamani zao za asili wasiokubali mabadiliko kirahisi

Kwa Marekani wengi ni waumini au kwa jina lingine utawasikia 'evangelical''
Hao ndio wasiotaka kusikia abortion au ushoga at least kwa nyakati hizo za real GOP

GOP wanaamini katika fiscal conservatism na fiscal policy ambazo zinaundwa na vitu kama kodi , serikali ndogo , soko huria na uangalifu katika madeni n.k.
Lakini si hilo pia ni ''waumini' wazuri wa sera za ulinzi na ubabe

Hapo nyuma nimekueleza kuhusu iliyokuwa GOP kwa kuangalia zama hizo si hizi za Trump
Ni kwanini!
- Trump si conservative , huyu aliwahi kuwa Democrats na wala hajulikani anasimamia wapi
-Soko huria kwasasa siyo soko la maana iliyokusudiwa.
Kuna monopoly ndiyo maana unaona mtifuano kuhusu biashara.
Hapa kuna element za ubabe,nguvu ya Marekani haipo katika jeshi tu, ipo katika uchumi pia
-Abortion, haieleweki Rais Trump anasimamia wapi, leo anasema hili kesho anasema lile
- Ubabe ni kama unaouona sasa kwa mizengwe dhidi ya Iran

Orodha ni ndefu, inatosha kusema zile thamani na misingi ya GOP hazijulikani.

Kwa mfano, serikali ya sasa ina madeni makubwa kufika kiwango cha ''debt ceiling''

Kwa bahati mbaya wahafidhina waliomsumbua sana Rais Obama , sasa wamekaa kimya hata pale misingi na thamani za Republicans zikigeuzwa kulia kushoto na Trump

Republican iliyopo ni ile ya mfano wa GOP siyo hii Republican ya Trump

Arguably, kutokana na mabadiliko ya nyakati na jamii ''demographic' GOP wanapaswa pia kubadilika wakisimama katika misingi yao kwa kuzingatia hali ya wakati uliopo

Kwa mfano, siku za nyuma kidogo GOP walianza kujipenyeza katika ngome za Democrats kama vile watu wa rangi mbali mbali, kushirikisha akina mama na hata kufikiria namna ya umiliki wa silaha kutokana na matukio.

Walianza kushirikisha vijana na kuondoka katika zama za wazee weupe ili kuvuta kundi hilo

Republicans ya Trump haieleweki ipo wapi. Hili ndilo linawapa taabu sana kama ilivyokuwa katika chaguzi ya 2018 ambapo vijana wengi wa Dems waliwatupa nje wazee wa GOP

Sasa kama ni hivyo, swali linalokuja inakuwaje Trump ameshinda uchaguzi?

Kuna sababu nyingi sana ikiwemo uwepo wa wahafidhina wa vijijini ambao huwaelezi kitu
Hawa ni wale walioaminisha ''Mexico italipa gharama za ukuta'' wakashangilia kwa nguvu

Ukiangalia ramani ya uchaguzi utaona vijijini ni GOP na mijini ni Democrats
Kosa la Democrats hasa uchaguzi uliopita ni kutoingia vijijini wakijua mijini tu inatosha

Kosa la pili ni kujiamisha kuhusu majimbo. Kwa mfano, uchaguzi uliopita walipoteza Indiana au Michigan. Kumbuka uchaguzi wa Marekani siyo popular vote ni electoral college
Kwahiyo hesabu hufanyika si kushinda tu bali wapi pa kushinda

Pamoja na hayo,Russia ilichangia kubadilisha matokeo. Hakuna takwimu za wapi walifanikiwa kwa namba ingawa leo May 14 kuna taarifa za ''hacking' za Russia kule Florida

Kuathiri matokeo si kuiba kura, ni pamoja na kitu kinaitwa voters suppression kwamba kuna ushawishi kwa wapiga kura kutoshiriki kwa kulenga makundi kadhaa
Uchaguzi uliopita uliona hilo kwa upande wa Democrats ambapo wengi hawakupiga kura

Voters suppression ilionekana maeneo ambayo Republicans walikuwa na magavana kwa kufanya gerrymandering, kudai vitambulisho, ukazi na kuweka vituo mbali sana ili wapiga kura wasiweze kwenda hasa maeneo ya watu wa rangi

Huu ni mtazamo wa jumla na si lazima ushabihiane na maoni mengine

Tusemezane
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,071
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,071 2,000
BIUNGANI DC NA YANYOJIRI

AG BARR ANYWEA, SASA KUTOA RIPOTI YA MUELLER ZAIDI
FLYNN ALIKUWA NA ''TAPE'' INAYOMGUSA RAIS TRUMP

Mambo yanazidi kubadilika viungani DC kila uchao. Mbinu ya kushambulia Iran ilikuwa kupoteza hoja ya Mueller. Kwa hali iliyotengenezwa na AG Barr, ngoma ni mbichi na fukuto ni kubwa

Siasa za viunga vya DC ni kubwa na zinahitaji wajuvi. Rejea bandiko 856 la Mag3 aliyegusia kuhusu Mueller kutawanya kesi. Kilichosemwa ndicho kinajidhihiri taratibu

Taarifa ya Mueller ilikuwa na mambo yote kwa ujumla. Kwa kujua mbinu za kutaka kuificha, Mueller akapeleka kesi zingine katika ngazi ya state na si federal ambako AG Barr ana ushwishi

Katika mabandio ya nyuma tulieleza kwa kirefu kuhusu underlying evidence. Tulisema si kauli ''zilizopigiwa mstari'' kama alivyoshadidia mwenzetu mmoja.
Tukasema inaweza kuwa ni memo, tape n.k.

Katika kesi alizopeleka katika state, moja ni ile ya mshauri wa usalama wa Rais Trump M.Flynn

Flynn alitoa ushirikiano wa kutosha kwa mchunguzi Mueller ambaye alipeleka vidhibiti vya kila kilichotokea. Moja ya mambo yaliyojitokeza ni wanasheria wa Trump kuwasiliana na Flynn wakieleza mtazamo wa ''Mzee Trump'' katika kuweka ''mambo saw'' Hii ipo katika tape

Hawa walimtaka Flynn adanganye ambalo ni kosa achilia mbali kosa la obstruction of justice

Taarifa ya Mueller ina yote hayo lakini AG Barr aliyaficha kwa kisingizio cha grand jury material

Hakimu ameamuru redacted katika mahakama ya itolewe. Hii maana yake ripoti ya Mueller inaanikwa kitaalamu ikimwacha AG Barr akiwa anashangaa. Tulisema itatoka ni suala la muda

Kwa kuchelea hilo AG Barr sasa ameamua ile less redacted itolewe kwa House members

Hilo halitasaidia kwani chair Nadler anataka na underlying evidence kama tape

Nadler alipokataa kataka kusoma taarifa nusu akitaka underlying evidence alijua anataka nini

Kwa kuangalia kesi 12 zilizoko mahakamani na mabazo ushahidi utahitajika kutolewa hadharani, ile taarifa ya Mueller iliyofichwa na Barr sasa inamegwa vipande vipande na kuanikwa

Tuwakumbushe wasomaji, tuliposema kuna uchafu unafichwa, haya yanayotokea ni sehemu tu, kuna habari nzito zitafuata. Barr sasa kanywea na inaonekana jahazi linazidi kujaa maji

Tusemezane
 
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Messages
10,393
Points
2,000
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined May 31, 2008
10,393 2,000
Taarifa ya Mueller ilikuwa na mambo yote kwa ujumla. Kwa kujua mbinu za kutaka kuificha, Mueller akapeleka kesi zingine katika ngazi ya state na si federal ambako AG Barr ana ushwishi
Mueller anamjua Trump ndani na nje. Alijua toka awali ripoti yake itakavyochakachuliwa na hivyo alijipanga vilivyo.
Taarifa ya Mueller ina yote hayo lakini AG Barr aliyaficha kwa kisingizio cha grand jury material
Barr kama nilivyosema hapo mwanzo...aliyakoroga na sasa itabidi ayanywe. Alitoa ripoti ya uongo Congress na sasa ni kweli anajuta.
Hakimu ameamuru redacted katika mahakama ya itolewe. Hii maana yake ripoti ya Mueller inaanikwa kitaalamu ikimwacha AG Barr akiwa anashangaa. Tulisema itatoka ni suala la muda
Na hili litafanyikwa hadi ripoti nzima iliyokuwa redacted imeanikwa wazi hadi wale wazito wa kuamini waisome kwa macho yao jinsi alivyoachwa uchi Trump.
Nadler alipokataa kataka kusoma taarifa nusu akitaka underlying evidence alijua anataka nini
Mimi naamini Spika Pelosi tayari anajua mengi yaliyomo ndani ya ripoti na ndiyo maana anawaomba wenzake waende taratibu huku nguruwe akijikaanga kwa mafuta yake mwenyewe na ndiyo maana alisema na nanukuu, "Trump is self-impeaching". Hata Nadler kwa sasa ameshawishika baada ya kumsikiliza Pelosi.
Kwa kuangalia kesi 12 zilizoko mahakamani na mabazo ushahidi utahitajika kutolewa hadharani, ile taarifa ya Mueller iliyofichwa na Barr sasa inamegwa vipande vipande na kuanikwa
Hakuna kilichofichwa hakitafichuliwa na ni swala la muda tu. Kwa sasa hakuna hata haja ya kumwita Mueller kwani uongo wa Barr utaanikwa hadi vipofu wauone na ndio maana Pelosi anasema na naukuu, "Barr lied to Congress!"
Tuwakumbushe wasomaji, tuliposema kuna uchafu unafichwa, haya yanayotokea ni sehemu tu, kuna habari nzito zitafuata. Barr sasa kanywea na inaonekana jahazi linazidi kujaa maji
Mueller alijua kuna udanganyifu utafanyika na alichukua hatua ya kuhakikisha ukweli hauzikwi. Barr aliingia kichwa kichwa kwenye mtego na sasa kanasa...chezea Marekani!
 
Mwalimu

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
1,511
Points
1,500
Mwalimu

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
1,511 1,500
Michael Flynn told Mueller people connected to Trump admin or Congress attempted to influence him

BIUNGANI DC NA YANYOJIRI

AG BARR ANYWEA, SASA KUTOA RIPOTI YA MUELLER ZAIDI
FLYNN ALIKUWA NA ''TAPE'' INAYOMGUSA RAIS TRUMP

Mambo yanazidi kubadilika viungani DC kila uchao. Mbinu ya kushambulia Iran ilikuwa kupoteza hoja ya Mueller. Kwa hali iliyotengenezwa na AG Barr, ngoma ni mbichi na fukuto ni kubwa

Siasa za viunga vya DC ni kubwa na zinahitaji wajuvi. Rejea bandiko 856 la Mag3 aliyegusia kuhusu Mueller kutawanya kesi. Kilichosemwa ndicho kinajidhihiri taratibu

Taarifa ya Mueller ilikuwa na mambo yote kwa ujumla. Kwa kujua mbinu za kutaka kuificha, Mueller akapeleka kesi zingine katika ngazi ya state na si federal ambako AG Barr ana ushwishi

Katika mabandio ya nyuma tulieleza kwa kirefu kuhusu underlying evidence. Tulisema si kauli ''zilizopigiwa mstari'' kama alivyoshadidia mwenzetu mmoja.
Tukasema inaweza kuwa ni memo, tape n.k.

Katika kesi alizopeleka katika state, moja ni ile ya mshauri wa usalama wa Rais Trump M.Flynn

Flynn alitoa ushirikiano wa kutosha kwa mchunguzi Mueller ambaye alipeleka vidhibiti vya kila kilichotokea. Moja ya mambo yaliyojitokeza ni wanasheria wa Trump kuwasiliana na Flynn wakieleza mtazamo wa ''Mzee Trump'' katika kuweka ''mambo saw'' Hii ipo katika tape

Hawa walimtaka Flynn adanganye ambalo ni kosa achilia mbali kosa la obstruction of justice

Taarifa ya Mueller ina yote hayo lakini AG Barr aliyaficha kwa kisingizio cha grand jury material

Hakimu ameamuru redacted katika mahakama ya itolewe. Hii maana yake ripoti ya Mueller inaanikwa kitaalamu ikimwacha AG Barr akiwa anashangaa. Tulisema itatoka ni suala la muda

Kwa kuchelea hilo AG Barr sasa ameamua ile less redacted itolewe kwa House members

Hilo halitasaidia kwani chair Nadler anataka na underlying evidence kama tape

Nadler alipokataa kataka kusoma taarifa nusu akitaka underlying evidence alijua anataka nini

Kwa kuangalia kesi 12 zilizoko mahakamani na mabazo ushahidi utahitajika kutolewa hadharani, ile taarifa ya Mueller iliyofichwa na Barr sasa inamegwa vipande vipande na kuanikwa

Tuwakumbushe wasomaji, tuliposema kuna uchafu unafichwa, haya yanayotokea ni sehemu tu, kuna habari nzito zitafuata. Barr sasa kanywea na inaonekana jahazi linazidi kujaa maji

Tusemezane
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,071
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,071 2,000
JIMBONI WASHINGTON NA VIUNGA VYAKE DC

RAIS TRUMP ASHANGAA KUTOAMBIWA YA FLYNN

Chururu chururu za habari zinaendelea kuvuja katika viunga vya DC zikimwandama Rais Trump
Zile habari nyeti zilizochimbiwa taratiibu zinavuja na kumwacha mtupu

Watu husema wanasiasa ni waongo na hilo si geni, hata hivyo Rais Trump ni kiboko
Ana uwezo wa kuongopa bila kupepesa macho tena akiwangaaliwa wahanga wake bila haya
Rekodi zake za karibuni zilifikia uongo 10,000 tangu aingine madarakani, ya leo ni kali zaidi

Rais Trump leo ame tweet akilaumu kuwa akiwa yeye na Hillary kama wagombea hakuambiwa matatizo yaliyokuwa yanamkabili mshauri wake wa usalama bw Michael Flynn

Nyaraka zinaonyesha timu ya wanasheria wa Trump ikimsihi Flynn agangamare kwani kinyume chake itakuwa dhalili kwa Rais Trump. Hapa ni baada ya Flynn kukubali kutoa ushirikiano na Mueller na kwamba sasa tape ipo wazi itaanikwa wiki ijayo

Huu ni uongo mkuwa kwani Rais Trump akiwa mgombewa alitahadhrishwa na vyombo vya usalama kuwa Flynn alikuwa anachunguzwa kwa deal zake na ni mtu asiyefaa katika wadhifa

Aliyekuwa Acting AG, Sally Yates alimtahadharisha Trump na WH kuwa Flynn alikuwa compromised na Russia na ni vema akae naye mbali
Gharama za kauli za Yates ilikuwa kutimuliwa kazi na Rais Trump

Timu ya Trump iliwahi kukiri kuwa baada ya uchaguzi Rais Obama alikutana na Rais Trump na kumtahadhirisha kuhusu Michael Flynn.

Msemaji wa kampeni ya Trump aliwahi kusema Obama ametoa ushauri huo kwasababu Flynn alikuwa critic mkubwa wa Utawala wake

Leo Rais ana tweet mchana kweupe kwamba hakuambiwa au kutahadharishwa

Hili si jambo la bahati mbaya, Trump anajua ule utitiri unaomfuata bila kuzijua siasa za DC utamsikiliza tu na kuamini. Hata hivyo kwa kiwango alichofikia, hii ni dhalili kubwa achilia mbali kashfa inayotokana na kauli za Flynn

Tusemezane
 
Bavaria

Bavaria

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2011
Messages
45,688
Points
2,000
Bavaria

Bavaria

JF-Expert Member
Joined Jun 14, 2011
45,688 2,000
GOP inasimama badala ya maneno Grand old party ambayo ni Republicans
Ni jina la utani ambalo lilianzia na maneno gallant old party, nyumbani kwa wahafidhina(conservatives) hawa ukisikia neno right wing au bawa la kulia ndio wenyewe
Ukisikia left au bawa la kushoto ni Democrats

Conservatives ni watu wanaolinda thamani zao za asili wasiokubali mabadiliko kirahisi

Kwa Marekani wengi ni waumini au kwa jina lingine utawasikia 'evangelical''
Hao ndio wasiotaka kusikia abortion au ushoga at least kwa nyakati hizo za real GOP

GOP wanaamini katika fiscal conservatism na fiscal policy ambazo zinaundwa na vitu kama kodi , serikali ndogo , soko huria na uangalifu katika madeni n.k.
Lakini si hilo pia ni ''waumini' wazuri wa sera za ulinzi na ubabe

Hapo nyuma nimekueleza kuhusu iliyokuwa GOP kwa kuangalia zama hizo si hizi za Trump
Ni kwanini!
- Trump si conservative , huyu aliwahi kuwa Democrats na wala hajulikani anasimamia wapi
-Soko huria kwasasa siyo soko la maana iliyokusudiwa.
Kuna monopoly ndiyo maana unaona mtifuano kuhusu biashara.
Hapa kuna element za ubabe,nguvu ya Marekani haipo katika jeshi tu, ipo katika uchumi pia
-Abortion, haieleweki Rais Trump anasimamia wapi, leo anasema hili kesho anasema lile
- Ubabe ni kama unaouona sasa kwa mizengwe dhidi ya Iran

Orodha ni ndefu, inatosha kusema zile thamani na misingi ya GOP hazijulikani.

Kwa mfano, serikali ya sasa ina madeni makubwa kufika kiwango cha ''debt ceiling''

Kwa bahati mbaya wahafidhina waliomsumbua sana Rais Obama , sasa wamekaa kimya hata pale misingi na thamani za Republicans zikigeuzwa kulia kushoto na Trump

Republican iliyopo ni ile ya mfano wa GOP siyo hii Republican ya Trump

Arguably, kutokana na mabadiliko ya nyakati na jamii ''demographic' GOP wanapaswa pia kubadilika wakisimama katika misingi yao kwa kuzingatia hali ya wakati uliopo

Kwa mfano, siku za nyuma kidogo GOP walianza kujipenyeza katika ngome za Democrats kama vile watu wa rangi mbali mbali, kushirikisha akina mama na hata kufikiria namna ya umiliki wa silaha kutokana na matukio.

Walianza kushirikisha vijana na kuondoka katika zama za wazee weupe ili kuvuta kundi hilo

Republicans ya Trump haieleweki ipo wapi. Hili ndilo linawapa taabu sana kama ilivyokuwa katika chaguzi ya 2018 ambapo vijana wengi wa Dems waliwatupa nje wazee wa GOP

Sasa kama ni hivyo, swali linalokuja inakuwaje Trump ameshinda uchaguzi?

Kuna sababu nyingi sana ikiwemo uwepo wa wahafidhina wa vijijini ambao huwaelezi kitu
Hawa ni wale walioaminisha ''Mexico italipa gharama za ukuta'' wakashangilia kwa nguvu

Ukiangalia ramani ya uchaguzi utaona vijijini ni GOP na mijini ni Democrats
Kosa la Democrats hasa uchaguzi uliopita ni kutoingia vijijini wakijua mijini tu inatosha

Kosa la pili ni kujiamisha kuhusu majimbo. Kwa mfano, uchaguzi uliopita walipoteza Indiana au Michigan. Kumbuka uchaguzi wa Marekani siyo popular vote ni electoral college
Kwahiyo hesabu hufanyika si kushinda tu bali wapi pa kushinda

Pamoja na hayo,Russia ilichangia kubadilisha matokeo. Hakuna takwimu za wapi walifanikiwa kwa namba ingawa leo May 14 kuna taarifa za ''hacking' za Russia kule Florida

Kuathiri matokeo si kuiba kura, ni pamoja na kitu kinaitwa voters suppression kwamba kuna ushawishi kwa wapiga kura kutoshiriki kwa kulenga makundi kadhaa
Uchaguzi uliopita uliona hilo kwa upande wa Democrats ambapo wengi hawakupiga kura

Voters suppression ilionekana maeneo ambayo Republicans walikuwa na magavana kwa kufanya gerrymandering, kudai vitambulisho, ukazi na kuweka vituo mbali sana ili wapiga kura wasiweze kwenda hasa maeneo ya watu wa rangi

Huu ni mtazamo wa jumla na si lazima ushabihiane na maoni mengine

Tusemezane
Maelezo mazuri sana mkuu.

Nashukuru mno.
 
Forum statistics

Threads 1,295,951
Members 498,495
Posts 31,228,868
Top