Duru Za Siasa: U.S Chini ya Donald J. Trump

Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,138
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,138 2,000
Wanajamvi

Uchaguzi wa US umekamilika jana baada ya D.J Trump kuwa Rais wa 45
Leo ilikuwa siku ya kwanza kamili ya Trump kama Rais wa US

Uzi utakuwa utaangalia serikali mpya na mwelekeo wa siasa na uchumi
Siasa za Marekani , taifa lenye nguvu katika uso wa dunia zinaathari kubwa duniani

Ni kwa kuzingatia hilo, uzi utaleta kwa kadri, yanayojiri katika Taifa hilo

Tutaendelea kumalizia hotuba ya Trump baada ya kutawazwa katika uzi huu
Duru za Siasa: Matokeo ya Uchaguzi Marekani

Rais Trump, mfanyabiashara aliyefanikiwa katika biashara ameondoka katika utawala wa makampuni na sasa ni mtawala wa umma na Taifa la Marekani

Kuchaguliwa kwake kama mtawala wa juu wa Taifa lenye ushawishi umekuja na mshtuko kutokana na nafasi aliyopewa katika uchaguzi wa ndani ya chama cha Republican na ule mkuu

Kuna mitazamo tofauti kuhusu kuchaguliwa kwa Trump. Kwasababu zozote ambazo wachunguzi wanaendelea kuzifuatilia kisiasa , uchumi, jamii n.k. Trump ndiye Rais wa Marekani

Siku ya kwanza, Trump amekumbana na changamoto za utawala wa nchi na si kampuni binafsi

Katika historia ya miongo michache ya Marais wa US, siku ya kwanza haikuwa nzuri kwake

1. Maandamano ya wanawake duniani
2. Ziara iliyozua utata katika Intelligence community (IC)

Tutajadili mambo hayo mawili na picha ya haraka ya nini kitarajiwe kwa siku za usoni

Tusemezane
 
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Messages
10,495
Points
2,000
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined May 31, 2008
10,495 2,000
Ndugu El Jefe Nafikiri tunachanganya mambo mengi mno kiasi cha kuishia kupoteza mtiririko mzima wa mada iliyopo mezani kwa sasa hivi na hii haitusaidii chochote. Hebu tupitie facts moja baada ya nyingine kwa umakini kuhusu sakata la Senate, Barr na Mueler bila kuchanganya mambo mengine kwanza;
Ukweli ni kwamba Mueller aliwasilisha pia brief summary ya ripoti yake yenye redactions ambayo Barr alitakiwa aitoe kama ilivyo lakini Barr aliiweka kapuni kumlinda Trump na badala yake akaandika ya kwake na kupotosha ripoti nzima...

Barr lied to Congress and that is a crime.
 
El Jefe

El Jefe

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2016
Messages
281
Points
500
El Jefe

El Jefe

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2016
281 500
Naona na wewe unataka kulisha wana JF matango pori. Kwa ambao wameweza kusoma ripoti yote na underlying evidence wameona wazi kabisa kwamba ugomvi wa Mueller na Barr ni hatua ya Barr kutoa maelezo ya uongo. Barr hakusoma yote na mengi aliyoulizwa jana alikuwa akiyasikia kwa mara ya kwanza na yalimtisha kidogo.
Wewe ndiye unayelisha watu "matango pori".
Kwanza, nje ya DOJ hamna aliyeona "underlying evidence" inayo-support ripoti ya Mueller. Hao unaosema wameona "underlying evidence" sijui wameionea wapi?

Usichanganye mambo, AG Barr amesoma ripoti yote kurasa 448 ila hakuangalia "underlying evidence".

"We accepted the statements in the report as factual record, we did not go underneath it to see whether or not they were accurately accepted"

"Underlying evidence" ni ushahidi wote uliokusanywa wakati wa uchunguzi, kwa mfano mahojiano, mamilioni ya documents, ripoti, records na records za mawasiliano. White House pekee walitoa documents millioni 1.4. Hizi ndizo Mueller alitumia kuandikia ripoti yake ya kurasa 448. Hizi ndizo AG Barr aliulizwa kama amezipitia.

Kwahiyo kwa wanaodhani kama Mag3 kuwa AG Barr kutoangalia "underlying evidence" maana yake hakusoma ripoti yote ya Mueller, wanakosea.

Lengo la Sen. Kamala kumuuliza AG Barr kama alishawahi kuagizwa au kuambiwa na mtu yeyote White House kuwa afanye uchunguzi wowote, ni kwa sababu Barr alisema anatathmini chanzo cha uchunguzi wa Russia. Cha kutisha hapo sijui kiko wapi.

Ripoti ambayo Mueller alitaka iwasilishwe Congress kama ilivyo ilikuwa ni ripoti waliyokwishaifanyia reductions zinazotakiwa kiutaratibu. Hii ndiyo sababu hakupendezwa kabisa na alichokuwa akifanya Barr kwani barua yake ya kwanza ilipotosha kila kitu kilichotakiwa kitolewe kwa umma.
Sio ripoti per se bali ni "introductions" na "executive summaries" za Vol I na II ambazo ni kurasa 19. Hizi ndizo Mueller alitaka ziwekwe wazi. AG Barr hakutaka kuweka wazi kurasa 19 halafu baadae aweke wazi kurasa 448, ndio maana akasubiri hadi alipotoa ripoti ya kurasa 448 kwa umma.

Hapa sijui wanalalamika nini!! Hizo wiki chache zilizopita kati ya Barua ya AG na "redacted" report ya Mueller kuwekwa wazi?

Mueller na Barr waliofautiana kwenye jambo ambalo halibadilishi chochote. Kwa sababu hizo "introduction" na "executive summaries" zipo wazi na ripoti nzima ipo wazi (redacted).

Seriously, Dems wanashikilia vitu visivyo make-sense. Labda kama ripoti isingetolewa kwa umma, which is not the case.

Hiyo ndiyo sababu hata Republicans baada ya kugundua kuwa Barr aliwalisha matango pori katika juhudi za kumlinda Trump, walikuwa wanapiga chenga kujadili ripoti na badala yake wanawaingiza Clinton, Comey, Lisa n.k. kwenye mjadala. Hata mwenyekiti Graham alionekana kushtushwa na baadhi ya maswali kama ya Kamila Harris.
Graham ameshtushwa!!!! Umewasikiliza SJC Republicans vizuri kwenye mahojiano na Barr? Hawataki hata kuendelea na mahojiano kuhusu ripoti ya Mueller kwa jinsi ilivyo ya kisiasa.

El Jefe, sijui Trump alikulisha nini...unamtetea utadhani uhai wako unamtegemea. Hadi leo hii msimamao wake ni kwamba haamini Urusi waliingilia uchaguzi wao wa mwaka 2016 na kwamba baada ya kumtizama Putin usoni anaamimi maneno yake zaidi ya wana usalama wa US! Barr hili anakwepa kulizungumzia kabisa...!
Mag3 , mimi nasimamia FACTS tu.
 
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Messages
10,495
Points
2,000
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined May 31, 2008
10,495 2,000
Mag3 , mimi nasimamia FACTS tu.
Who are you kidding...facts according to who? Trump? Maybe you mean alternative facts as Trump's WH would put it! Would your man recognize facts if they were staring at him right in the face? No, El Jefe, I sincerely believe you are not serious, you are just being disingenuous. Immediately Trump enters a room, you can be sure facts will be tossed outside the window and maybe all that will be left are none other but alternative facts, period. We are now entering big time league bigly (sic!), stay tuned.
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,138
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,138 2,000
JIMBO KUU LA DC NA VIUNGA VYAKE
AG BARR AKIMBIA KAMATI YA BUNGE

Jana Barr alikutana na kamati ya seneti chini ya uongozi wa Lindsey Graham wa Republicans

Haikuwa bahati mbaya, Barr alijua anakwenda kucheza uwanja wa nyumbani
Republicans hawakujishughulisha na masuala ya taarifa ya Mueller na ki-summary cha Barr

GOP walifanya hivyo makusudi kabisa ili kukuza suala la surveillance na ''spy'

Hili liliwahi kufanyiwa kazi na chair Nunes wa GOP wakimwita Susan Rice kama chanzo
Suzan Rice alikwenda na suala zima likafa kifo kutokana na ukweli uliowekwa hadharani

Leo Barr alikuwa akutane na kamati ya House chini ya Democrats
Chair Nadler alitaka Barr ahojiwe na Wabunge kisha watalaama wa sheria. Barr kachomoa

Kuhojiwa na wataalam wa sheria si jambo geni. Mwanamama Ford aliyemtuhumu Jaji Kavanaugh alihojiwa na wanasheria wa kamati ya Bunge. AG wa US kaamua kukimbia

Mbio za Barr zinatokana na barua mbili za Mueller zinazoeleza kutoridhishwa na hatua zake

Utetezi wa Mueller ni kuwa draft ya summary yake ya kurasa nne alimuomba Mueller aipitie
Mueller alikataa kwa makusudi kabisa kwavile tayari alikuwa na summary kwa ajili ya Public
Hakutaka kuweka mkono wake katika kurasa nne

Barua alizomwandikia ilikuwa ushahidi akijua Barr alitaka kuifanyanga taarifa yake.

Katika barua barua hizo Mueller alitumia maneno '' context, nature and substance na conclusion'
Kwa kiswahili summary hahikukidhi maudhui,asili na mantiki na wala haikuakisi hitimisho

Maneno hayo ni muhimu sana kwasababu yanafuta summary ya Barr kabisa na kubaki karatasi
Ni kutokana na barua hiyo, katika siku ya jana AG Barr alikuwa hana majibu akijiuma umma

AG Barr amekatazwa na ''wanasheria wa WH'' kwani ile road map ya Mueller sasa inatafuta miguu. Suala la Obstruction of justice linazidi kumuelemea Trump na Barr ndiyo Kinga

Kwahiyo kuna mkakati maalumu unaofanywa na Team Trump.
Kwanza kuhakikisha Barr anabaki kuwa AG kwavile kupitia kwake kuna taarifa nyeti sana za intelejensia zilizofichwa chini ya mwamvuli wa grand Jury.

Barr anajua kutoa taarifa hiyo hadharani ni mwisho wa Trump

Mkakati wa pili ni kuhakikisha Mcgahn, mshauri wa Trump hafiki mbele ya kamati ya Bunge

McGahn ndiye aliyeeleza kwa kina mkakati wa Trump kutaka kumfuta Mueller
Mkakati wa tatu ni kumponda Mueller ili taarifa na tango pori la Barr vibaki vichwani mwa umma

Matatizo ya mikakati hiyo ni yapi?
Inaendelea
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,138
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,138 2,000
Inaendelea..

Mikakati inayopangwa na WH na Barr itakuwa na matatizo makubwa kuliko suluhisho

1. Kitendo cha Barr kuingia mitini kinaondoa shaka kwamba nia yake si njema.
Hapa ni kwamba anapoteza crediblity hata kwa wachache waliokuwa na shaka
Kamati ina uwezo wa kumwita kisheria ''subpoena'' katika hili anaweza kushtakiwa

Seneti chini ya GOP haiwezi kuidhinisha impeachment ya Barr lakini Dems wakitaka wanawezakutumia sheria iliotumika mwaka 1935? ya kumfungulia mashtaka na kumfunga
Sheria hiyo inatumiwa na seneti na House tofauti bila kutegemeana

2. Kumzuia Mcgahn hakutafanikiwa. WH ili waive the executive privilege kwa kumruhusu Mcgahn kutoa ushahidi kwa masaa 30 mbele ya Mueller na taarifa ipo hadharani. Hakuna siri
Mcgahn ni Raia si mtumishi wa WH, sheria ilipomruhusu mwanzoni haiwezi kumzuia akiwa Raia

Kosa kubwa anafanya Trump kwa kusema Mgahn ni muongo na alitoa ushuhuda wa uongo
Mcgahn kama mtu mwenye credibility anataka ku testify ili asifishe jina
Katika hilo hatakuwa na mwanamana na Trump hasa akikumbuka anavyo kashifiwa

3. Mkakati wa tatu ni kumtuhumu Mueller. Huu hautafanya kazi tayari watu wamepoteza credibility na Barr na wanataka kumsikia Mueller. Kwa kumzushia na tayari Mueller kaonyeshwa kukerwa na upotoshaji atatoka kwa suprise akipata nafasi na kwa gharama kubwa ya Trump

Mueller akisema neno moja tu 'yes' ni tatizo kubwa . Mathalani, akiulizwa ikiwa taarifa ililenga obstruction of justice iende congress naye akasema ''yes'' kinachofuata ni impeachment

Tatizo kubwa zaidi ni kuwa kumshambulia mueller ni kushambulia timu nzima.

Haitachukua muda taarifa kile kilicho redacted na hasa uchafu uliofichwa utawekwa hadharani
Mueller alijaribu kuficha barua Washington DC, sasa zimekuwa kaa la moto sembuse redaction!

Mikakati hiyo imeambatana na jitihada za chini chini za kufuta Obamacare chini ya Barr
Republicans hawataki kusikia kitu hicho kabisa kwa kuchelea adhabu nyingine kwa njia ya kura

Haya yanamwacha wapi Trump?

Kwamba, suala la Barr na Mueller ndiyo habari ya mjini, lakini mhusika mkuu ni Trump na obstruction of justice. Republicans wameshikama kweli kwahili

Obamacare ikirudi katika maongezi kutakuwa na 'fatigue' ndani ya GOP

Rais Nixon alikuwa mbabe, jeuri na kiburi sana. Alikuwa na mikakati mingi sana
Mwisho wa siku Republicans walichoka, ndio waliomuondoa na si Dems

Kama kuna mtu anamsumbua sana Trump si Dems, ni AG Barr
GOP wanamlaumu kwani suala la collusion si zito kama analoendeleza la Obstruction of justice

Tusemezane
 
El Jefe

El Jefe

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2016
Messages
281
Points
500
El Jefe

El Jefe

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2016
281 500
Kwa aliyesikiliza SJC hearing, Republicans walishughulika na taarifa ya Mueller na mambo mengine. Waliuliza maswali kuhusu yaliyomo ndani ya ripoti ya Mueller na jinsi AG Barr alivyolishughulikia.

Hivi kelele zote hizi za Dems ni kwa sababu ya barua ya Mueller, kwamba hakukuwa na "context, nature and substance" kwa maana kwamba Barr hakuweka "Introductions" na "Executive summaries" za Vol I na II zenye kurasa 19 wazi kwa umma!!, hebu tutafakari tusiwe watu wa kumeza tu, hizo sehemu mbili na ripoti ya page 448 zipo kwa umma sasa hivi au hazipo?

Kwamba AG Barr amekatazwa na wanasheria wa WH limekaa kihisia zaidi na hamna ushahidi wowote.

Mtu anaposema kwamba taarifa "nyeti sana za intelijensia" zimefichwa chini ya mwamvuli wa grandy jury au Barr akitoa taarifa hizo ni "mwisho wa Trump" unajiuliza anatoa wapi kauli kama hizo ikiwa hakuna mtu yeyote nje ya DOJ aliyeona "grand jury materials"! Tusiongozwe na hisia. Kama mtu huelewi kwanini grand jury materials zinafichwa ni bora ukaelewa kwanza kabla ya kutumia hisia binafsi kupotosha.

Kusema kwamba Mueller anapondwa ili taarifa na "tango pori la Barr vibaki vichwani mwa umma", ni kutokuelewa kwa sababu ripoti nzima ya Mueller (redacted) ya kurasa 448 ipo "vichwani mwa umma" hata mda huu. Taarifa ya Barr ingeweza kubaki vichwani mwa umma kama kusingekuwepo na ripoti ya Mueller vichwani mwa umma. It's common sense. Na AG Barr alitaka umma usome ripoti na sio kulishwa chochote na Dems wa Congress. Matokeo yake umma ndio hautaki kumuhukumu Trump vibaya.

McGahn alihojiwa masaa 30 na Mueller, ni ujuwa kudhani kuna kitu ambacho aliacha kukisema kwenye hayo mahojiano. Republicans wamechoshwa na uchunguzi usioisha, huu uchunguzi umechukua miaka miwili+, kama sio siasa ni nini? Dems wana kila kitu kwanini wasichukue hatua wanazotaka kuchukua? Kuna mambo mengi ya maendeleo ya kufanya na sio kila siku kukalia viuchunguzi uchwara.
 
El Jefe

El Jefe

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2016
Messages
281
Points
500
El Jefe

El Jefe

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2016
281 500
Tunaendelea kusisitiza "credibility" ya Barr ipo kisiasa zaidi, na linatumiwa na Dems kwa sababu Barr hataki kuendeshwa nao.

AG Barr angependa sana Dems wakimshtaki mahakamani, na Dems wanajua wakienda huko mahakamani hata kwa kutumia sheria gani hawatafanikiwa. Hapa Dems wanapoteza.

Hili suala la "executive priviledge" kwa McGahn nalo linaweza kuishia mahakamani na huko Dems hawatafanikiwa. Kama White House ilimruhusu Mcgahn kutoa ushahidi kwa masaa 30 mbele ya Mueller na taarifa ipo hadharani, unajiuliza, kwanini Dems wasitumie tarrifa iliyopo? McGahn sio mtumishi wa WH kwa sasa lakini "executive priviledge" ya WH ni kwa ajili ya mawasiliano yote ya WH, labda kama ataenda kupiga stori zingine Congress. Hapa Dems wanapoteza tena.

Hata kama Mueller akisema alilenga "obstruction" ikaamuliwe Congress, kwamba kinachofuata ni "impeachment", hebu tujiulize, hiyo "impeachment" ya Dems itaishia wapi? Kila mtu anajua Senate haitaidhinisha hiyo "impeachment".Kwahiyo Dems wanapoteza tena.

Hivi mtu unaposema "uchafu uliofichwa utawekwa hadharani", Je, una ushahidi wowote kwamba grand jury materials ni chafu au ni hisia tu?

Kuna tabia ya kufananisha kesi ya Nixon na ya Trump, ni "obsession" tu, hamna kitu kingine. Hizi ni kesi mbili tofauti. Nixon alikuwa na "underlying crime" kwenye obstruction, hata umma ulimuhukumu vibaya, wakati Trump hana underlying crime. Tusiongozwe na hisia.

Habari ya ripoti ya Mueller hata sio habari inayo-trend U.S., ni kama vile umma umeshaichuja na hawana interest nayo tofauti na mwanzoni AG Barr alivyotoa ripoti ya Mueller kwa umma. Uchunguzi wa Mueller unazidi kuchuja kadri siku zinavyoenda.
 
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Messages
10,495
Points
2,000
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined May 31, 2008
10,495 2,000
Habari ya ripoti ya Mueller hata sio habari inayo-trend U.S., ni kama vile umma umeshaichuja na hawana interest nayo tofauti na mwanzoni AG Barr alivyotoa ripoti ya Mueller kwa umma. Uchunguzi wa Mueller unazidi kuchuja kadri siku zinavyoenda.
Naona unaishi US ya kusadikika, je unajua kwa nini Republicans wameanza kumkomalia Mueller? Conservative media sasa hivi iko obsessed na kuhoji credibility ya Mueller, and for what? Well, Watergate had the Nixon tapes. Mueller had Annie Donaldson’s notes. El Jefe, amini usiamini WH wanajua kilichomo ndani ya unredacted report ya Mueller na kama wanajua you can bet na wengine pia wanajua.

“What about these notes? Why do you take notes?” Trump asked McGahn during a tense Oval Office confrontation. “Lawyers don’t take notes. I never had a lawyer who took notes.” (McGahn told investigators Trump was referring to Donaldson’s notes, which the president thought of as McGahn’s.) Testimony ya mwanamama aliyekuwa Chief of Staff wa Maghan, Annie Donaldson, ipo kwa Mueller na sasa kilichobaki kwa Republicans ni kumchafua Mueller.

Je umejiuliza kwa nini badala ya kumtetea Mueller kwa kutoa ripoti wanayodai imem-exonerate Trump, wameamua kumshambulia? Ripoti kamili ya Mueller ina makubwa na ni swala la muda tu, kila kitu kitajulikana. Kwa Barr historia inajirudia na safari hii amelikoroga kweli kweli. Aliyetota hajui kutota...
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,138
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,138 2,000
"Mag3, post: 31325955, member: 10873" Republicans wameanza kumkomalia Mueller?
Kwa taarifa waliyosema ni 'gold std' waliyosema imem'exonerate' Trump

Conservative media sasa hivi iko obsessed na kuhoji credibility ya Mueller, what? Well, Watergate had the Nixon tapes. Mueller had Annie Donaldson’s notes. amini usiamini WH wanajua kilichomo ndani ya unredacted report ya Mueller na kama wanajua you can bet na wengine pia wanajua.
Conservative media zimebadilika ghafla. Kama utakumbuka AG Barr aliulizwa kama amewasiliana na WH kuhusu taarifa, alikiri kuwa wamewasiliana
Kuhusu Annie Donaldson hili nitalijadili kwani ni kiini cha taarifa kufichwa
Je umejiuliza kwa nini badala ya kumtetea Mueller kwa kutoa ripoti wanayodai imem-exonerate Trump, wameamua kumshambulia?
Trump alisema Mueller ni honorable person baada ya taarifa kutoka. Tuliwaonya wageni wa siasa za DC kuwa suala bado ni bichi

Ripoti kamili ya Mueller ina makubwa na ni swala la muda tu, kila kitu kitajulikana. Kwa Barr historia inajirudia na safari hii amelikoroga kweli kweli. Aliyetota hajui kutota...
Ripoti ina makubwa sana ndiyo maana AG Barr hakutumia executive summary ya Mueller
Amekataa kata kata kutoa taarifa nzima kwa kisingizo cha grand jury materials

Kwa suala la grand jury, hiyo siyo siri ya kuficha kwani mahakama inaweza kuidhinisha
Hata hivyo Barr alikuwa na fursa ya kuwatumia gang of eight kufanya redaction
Kilichotokea akawapa less redacted ambayo bado ni redacted

AG Barr anatumia grand jury kuficha uchafu akijua wapo watakaoamini anachokisema
Alifanikiwa kumpa Trump wiki 3 za ku-shape narrative lakini sasa ni kama amekwama

Maswali machache ya Kamala Harris yalimvua nguo kiasi cha kuonekana ni kituko

Taarifa ya Mueller itatoka tu. Nadler amekomalia itoke yote si kwasababu anahisi, la hasha anajua kilichomo. Lengo lake ni kutaka taarifa ionwe na Republicans na hapo ndipo kumeguka kwa Trump camp kunapoweza kutokea. Swali, ubabe wa Barr utasaidia kuzuia timbwili au ni dawa ya kupunguza maumivu kama ile aliyeitoa wiki zilizopita?
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,138
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,138 2,000
NDANI YA VIUNGA VYA DC
TRUMP AGOMA McGhan ASIENDE MBELE YA KAMATI

Baada ya vikaratasi 4 vilivyoitwa summary vya Bw Barr tulisema kabla AG alikuwa na hila
Jana alishindwa kutokea mbele ya kamati ya House chini ya chair Nadler

Ndani ya kamati ya seneti iliyokuwa dhahiri imepangwa, muda mchache aliokutana na maseneta wa Dems, AG Barr alikuwa ''embarrassment'' viungani DC

Sehemu kubwa alikuwa anagugumia ''mumbling' kama mtu wa mtaani, alipata wakati mgumu

Barr alikiri kuitoa taarifa bila kuisoma kwa kina akiacha waliyoibeba wakitahayari
Hivi inawezekanaje kuandika summary ya kitu asichokijua?
Tulisema hapa jamvini Republicans wanamlaumu kwani yanayoendelea ni kwasababu yake

Barr ameshindwa kuelewa lugha ya sheria kama ambavyo wafuasi wao wasivyoielewa
Mueller anasema ''nature, context and substance'' akimaanisha Barr alipotosha asili ya taarifa nzima kwa mfanokutumia neno collusion ambalo si lugha ya kisheria

Katika neno context, mfano ni kusema Mueller hakuhitimisha bila kujua mantiki ilikuwa nini

Na substance alimaanisha hoja nzito zilizoachwa na AG Barr makusudi katika kupotosha umma

Hapa jamvini lugha ya kisheria nayo inazidi kuonyesha kutoeleweka kwa wafuasi wa Barr

Chair Nadler anahitaji taarifa unredacted with underlying evidence alikuwa na maana sahihi

1. Unredacted alimaanisha taarifa isiyo haririwa kama alivyoiwasilisha Mueller

2. Underlying evidence
Hana maana ya kiswahili kuwa ni maneno yaliyopigiwa mstari

Mtu akisema taarifa ya Mueller ina underlying evidence atakuwa ametafisri lugha ya kisheria kwa kiingereza cha kawaida au kiswahili au kutojua kabisa maana ya neno hilo

Underlying evidence ina maana rahisi ''ushahidI wa viambatanisho' Inaweza kuwa kimemo, email, tape, picha nukuu, rejea , gazeti , kauli zenye uthibisho n.k

Redacted report ya Mueller haina underlying evidence hata moja, ina ina context and contents zinazoelekeza wapi underlying evidence ilipo kwa njia za rejea au viambatanisho

Hapo ndipo hoja ya kumzuia McGahn inapokuja. Kwamba, McGahn itabidi atoe ushahidi alioutoa kwa Mueller. Na Mueller ana mkanda wa rekodi ambao ni underlying evidence

Anne Donaldson ana memo aliyokuwa ananukuu. Maneno yake yapo katika taarifa
Kinachotakiwa ni hizo notes ambazo ndizo underlying evidence

Tahadhari; underlying evidence ipo katika english, kinachozungumziwa ni underlying evidence in legal terms.

Hapa ndipo watu wanachanganya mambo na kudhani ni mstari chini ya maneno

Kwa kuchelea vidhibiti hivyo na kwa uzito wake katika obstruction of justice, WH na DOJ wamepanga mkakati McGahn na Anne wasitokee mbele ya congress hata kwa dawa

Tusemezane
 
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Messages
10,495
Points
2,000
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined May 31, 2008
10,495 2,000
Breaking News: Mueller and House Judiciary Committee tentatively agree on May 15 for his testimony on Russia investigation!

The committee has been seeking to hear from Robert S. Mueller III amid disagreements about whether Attorney General William P. Barr mischaracterized the report in his congressional testimony and statements.

Kazi ipo...

UPDATE: Correction...
Habari mpya ni kwamba bado hawajaafikiana kuhusu tarehe, bado kuna majadiliano...tuendelee kusubiri!
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,138
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,138 2,000
MUELLER KUTUA NDANI YA HOUSE

LINDSYE GRAHAM AMRUHUSU SENETI, TRUMP HATAKI HOUSE

Kuna taarifa Mueller yupo katika majadiliano ya kufika mbele ya kamati ya House mwezi huu

Majuzi, mwenyekiti wa senate judiciary committee Seneta Lindsey Graham alisema ikiwa Muller atapendelea, anaweza kwenda kuongelea simu yake na AG Barr na si vinginevyo

AG akihojiwa mbele ya kamati ya seneti alisema haoni tatizo kwa Mueller ku-testify hadharani

Rais Trump ame tweet haoni sababu za Mueller kuhojiwa na kamati za Bunge

Mtiririko huo unaturidisha katika hoja ya msingi. Ikiwa taarifa ilikuwa ''total exoneration'' kama Trump alivyosema na ikiwa AG Barr aliwasilisha taarifa sahihi, na ikiwa hakuna kilichofichwa nini kinahofiwa kwa Mueller kuieleza taarifa yake?

Seneta Lindsey anasema Mueller aende kueleza maongezi ya simu. Hii ni baada ya kusema kamati yake haitajadili tena suala hilo akitumia maneno ''it's over''

Lindsey anajua tayari ameshamtibua Mueller ambaye inaelekea atakwenda kamati ya House
Hivyo anataka kumpooza kwa kumpangusa na si kumpa fursa ya kueleza nini kilichomo

AG Barr kusema hana tatizo na Mueller kueleza taarifa yake huku Rais akimshawishi kwa tweet Mueller asiitwe tayari wanajichanganya. Ikumbukwe wiki iliyopita maamuzi ya Mueller kwenda mbele ya kamati Rais Trump aliyaacha mikononi mwa Barr

Kwanini hawataki Mueller aende mbele ya kamati?
Kwanza, ni wazi Mueller ataiumbua taarifa ya kurasa 4 ya Barr na utetezi wake wote
Pili, Mueller ataeleza ni kwanini aliamua kumuandikia barua Barr kueleza kutoridhishwa naye
Tatu, Mueller ataeleza nini kilichomo ndani ya executive summary na kumuumbua Barr
Nne, Mueller atafafanunua hasa kipengele kinachohusu obstruction of justice
Tano, itabidi aeleze kuhusu memo ya Ms Anne Donaldson ambayo ni mwiba kwa Trump
Sita, itabidi afafanue kuhusu utata wa nani anapaswa kuchukua hatua, congress au Barr

Hofu kubwa ya Rais Trump ni kufikiri kuwa Mueller atajibu mapigo ya matusi ya ''hoax'' angry democrats, Mueller ni conflicted n.k.

Na kwa uhakika kabisa Mueller ameishika karata ya Rais Trump WH.
Hahitaji kurasa nne, anatakiwa aseme kwa mistari miwili tu ''ndiyo kuna abcd'

Huku joto la shinikizo kutoka kwa waendesha mashtaka zaidi ya 500 wakisema kuna uhalifu uliofanyika na kwamba katika hali ya kawaida Trump angefikishwa mbele ya grand jury

Kama tulivyowahi kusema vile vikaratasi 4 vya Barr (bandiko 765) vililenga kuwapunza wakimbiza ''mwenge'' wasiojua siasa za viunga vikubwa vya DC. Ngoma ndiyo kwanza inaanza

Tusemezane
 
Mwalimu

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
1,527
Points
1,500
Mwalimu

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
1,527 1,500
MUELLER KUTUA NDANI YA HOUSE

LINDSYE GRAHAM AMRUHUSU SENETI, TRUMP HATAKI HOUSE

Kuna taarifa Mueller yupo katika majadiliano ya kufika mbele ya kamati ya House mwezi huu

Majuzi, mwenyekiti wa senate judiciary committee Seneta Lindsey Graham alisema ikiwa Muller atapendelea, anaweza kwenda kuongelea simu yake na AG Barr na si vinginevyo

AG akihojiwa mbele ya kamati ya seneti alisema haoni tatizo kwa Mueller ku-testify hadharani

Rais Trump ame tweet haoni sababu za Mueller kuhojiwa na kamati za Bunge

Mtiririko huo unaturidisha katika hoja ya msingi. Ikiwa taarifa ilikuwa ''total exoneration'' kama Trump alivyosema na ikiwa AG Barr aliwasilisha taarifa sahihi, na ikiwa hakuna kilichofichwa nini kinahofiwa kwa Mueller kuieleza taarifa yake?

Seneta Lindsey anasema Mueller aende kueleza maongezi ya simu. Hii ni baada ya kusema kamati yake haitajadili tena suala hilo akitumia maneno ''it's over''

Lindsey anajua tayari ameshamtibua Mueller ambaye inaelekea atakwenda kamati ya House
Hivyo anataka kumpooza kwa kumpangusa na si kumpa fursa ya kueleza nini kilichomo

AG Barr kusema hana tatizo na Mueller kueleza taarifa yake huku Rais akimshawishi kwa tweet Mueller asiitwe tayari wanajichanganya. Ikumbukwe wiki iliyopita maamuzi ya Mueller kwenda mbele ya kamati Rais Trump aliyaacha mikononi mwa Barr

Kwanini hawataki Mueller aende mbele ya kamati?
Kwanza, ni wazi Mueller ataiumbua taarifa ya kurasa 4 ya Barr na utetezi wake wote
Pili, Mueller ataeleza ni kwanini aliamua kumuandikia barua Barr kueleza kutoridhishwa naye
Tatu, Mueller ataeleza nini kilichomo ndani ya executive summary na kumuumbua Barr
Nne, Mueller atafafanunua hasa kipengele kinachohusu obstruction of justice
Tano, itabidi aeleze kuhusu memo ya Ms Anne Donaldson ambayo ni mwiba kwa Trump
Sita, itabidi afafanue kuhusu utata wa nani anapaswa kuchukua hatua, congress au Barr

Hofu kubwa ya Rais Trump ni kufikiri kuwa Mueller atajibu mapigo ya matusi ya ''hoax'' angry democrats, Mueller ni conflicted n.k.

Na kwa uhakika kabisa Mueller ameishika karata ya Rais Trump WH.
Hahitaji kurasa nne, anatakiwa aseme kwa mistari miwili tu ''ndiyo kuna abcd'

Huku joto la shinikizo kutoka kwa waendesha mashtaka zaidi ya 500 wakisema kuna uhalifu uliofanyika na kwamba katika hali ya kawaida Trump angefikishwa mbele ya grand jury

Kama tulivyowahi kusema vile vikaratasi 4 vya Barr (bandiko 765) vililenga kuwapunza wakimbiza ''mwenge'' wasiojua siasa za viunga vikubwa vya DC. Ngoma ndiyo kwanza inaanza

Tusemezane
Trump na wapiga debe wake wamekuwa wakishangilia kwamba ripoti haijathibitisha kuhusu tuhuma COLLUSION na urusi. Lakini walipoingia mkenge na kuja kushituka baadae ni kwamba ripoti ya Mueler pamoja na kutosema wazi kuhusu collusion, imeanika ushahidi wa kutosha kuonesha kosa la OBSTRUCTION OF JUSTICE ambalo kisheria ni serious zaidi mtu anaweza kushtakiwa nalo.

Ndio maana hawataki full report (unredacted) ya Mueller ipelekwe bungeni sababu wanajua yatakayoanikwa humo hata wao watashindwa kumtetea mtu wao.

Ngoma bado mbichi!
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,138
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,138 2,000
Trump na wapiga debe wake wamekuwa wakishangilia kwamba ripoti haijathibitisha kuhusu tuhuma COLLUSION na urusi. Lakini walipoingia mkenge na kuja kushituka baadae ni kwamba ripoti ya Mueler pamoja na kutosema wazi kuhusu collusion, imeanika ushahidi wa kutosha kuonesha kosa la OBSTRUCTION OF JUSTICE ambalo kisheria ni serious zaidi mtu anaweza kushtakiwa nalo.

Ndio maana hawataki full report (unredacted) ya Mueller ipelekwe bungeni sababu wanajua yatakayoanikwa humo hata wao watashindwa kumtetea mtu wao.

Ngoma bado mbichi!
Naam bado mbichi sana ndani ya DC na viunga vyake, tulisema

Taarifa ya Barr ilionekana dhahiri kuegemea utetezi na si taarifa ya Mueller.
Tulijiuliza sana ikiwa alikuwa na muda wa kuosha wa kudurusu kurasa 400 za kitaalamu

Tulifahamu lengo la kwanza la summary ilikuwa ni kumpa nafasi Trump ku-shape maongezi
Kwa wiki tatu alimuacha na kisha kutoa taarifa siku siku moja kabla ya long weekend

Halafu alifanya quotation ya Mueller kwa kudokoa sehemu na si sentensi kamili

Wajanja wa DC walijua kuna moshi unafuka, wakamwacha Trump na Kellyanne wajianike
Hawakuwa peke yao mababusa kwingine katika anga la wadudi wakabeba kila kilichosemwa

Barr alitaka kuficha sehemu kubwa sana ya redacted report, leo tunajua Mueller alimjia juu

Katika report kuna grand jury materials ambazo zinaweza kufanyiwa kazi kupitia mahakama
Barr akagoma

Baada ya kibano cha seneti uwanja wa republicans Barr akachomoa kamati ya House.

Madhila na dhalili aliyokutana nayo ya akina Kamala Harris yalimuonyesha hamkani si shwari

Alipoulizwa kama Mueller anaweza kwenda mbele ya kamati, Barr alijichanganya kwa kusema haoni tatizo. Wanasheria wamepitia taarifa na kubaini kuna watu watatu wanaoweza kuhitimisha safari ya Rais Trump haraka sana, Anne Donaldson mwenye kimemo, McGahn aliyeagizwa amtimue Mueller na Mueller mwenyewe mwenye tafsiri kamili ya taarifa

Barr baada ya kuona kila kona imebana, leo kamwandikia barua rais Trump akimtaka atumie executive privilege kuzuia taarifa na mashahidi wote akiwemo Mueller ku testify

Hii maana yake ni moja, ni kutaka kuficha uchafu mkubwa uliofunikwa chini ya mwamvuli wa grandjury materials. Barr kabanwa na Trump kabanwa wote wanakimbilia executive privilege

Kama mtakumbuka ulisema DC hakuna siri. Jana baada ya Munichin kukataa kutoa taarifa ya kodi ''tax file' ya Trump, media zime-mbip kwa kutoa taarifa ya miaka 10 ya miaka ya 90

Ni kuwaeleza akina Barr taarifa za kodi zipo zinasubiri muda si ubabe si ndani ya DC

Lakini pia ni kueleza taarifa ya Mueller ipo mahali inasubiri wakati muafaka

Jitihada zinazofanyika ni kufunika na kuendeleza muda muda, mwisho wa yote uchafu wa Trump dhidi ya Marekani utawekwa hadharani, ni suala la muda

Tusemezane
 
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Messages
10,495
Points
2,000
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined May 31, 2008
10,495 2,000
Jitihada zinazofanyika ni kufunika na kuendeleza muda muda, mwisho wa yote uchafu wa Trump dhidi ya Marekani utawekwa hadharani, ni suala la muda
Mkuu Nguruvi3, taarifa za ndani zinasema Mueller ni kiboko. Hizi jitihada zote za Trump na AG wake, Mueller alijua (ali-foresee) kwamba zitatokea na alihisi njama zitafanyika kuzuia ripoti yake isitoke kama ilivyo. Alijua uwezo na ujanja wa Trump katika kula njama kuhusu mambo muhimu aliyoshauri kwenye ripoti kutatafutwa mbinu za kuzipotosha kumnusuru Trump kwa tuhuma zinazomkabili kwani anamjua vizuri Barr.

Kesi zinazoendelea kwenye mahakama mbali mbali zipo ambazo zitalazimu unredacted report zitolewe na tayari baadhi ya mahakama zimeishatoa maagizo sehemu ya ripoti fulani fulani zitolewe. Kwa mfano kesi inayoendelea ya Roger Stone ni mojawapo tu ambapo jaji wa Mahakama tayari ameagiza waendesha mashataka wa serikali wanaleta unredacted ripoti ya Mueller kuhusu mashtaka dhidi ya Roger Stone.

Kesi nyingine ambayo pia inategemewa Mahakama itaagiza documents zinazohusu tax returns za Trump zitolewe kama ushahidi nayo inaendelea jijini New York. Kwa hiyo WH kukataa kutoa tax returns za Trump kwa Congress ni kazi bure, lazima zitatolewa kwa amri ya mahakama ya jimbo la New York. Mambo haya na mengine yalipangwa kwa ubunifu mkubwa na ni swala la muda tu mambo kuwekwa hadharani.
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,138
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,138 2,000
McGahn AZUIWA KUSEMA, AJIBU MAPIGO
Trump Jr AITWA MBELE YA KAMATI YA SENETI

Katika siku za karibuni kumekuwa na kauli za ''it's time to move on' kutoka kwa viongozi wa Republicans kama McConnel, Lindsey na wengine. Kauli hiyo ina maana '' waachane na''

Ni mkakati wa kufunika suala la Mueller linalozidi kugubiga habari za Marekani kila uchao Vichwa vya habari ni Mueller, McGahn, Don Jr n.k. Hiyo ndiyo habari ya viungani DC

Kamati ya senate intelligence chini ya R. Burr imemwita Don Trump Jr
Hilo limewaudhi GOP ambao lengo ni ''move on''

Mwito ni baada ya kusoma redacted version, na inaelekea Don ana la kujibu!

Wito wa Don umemvuruga mzee wake Trump aki tweet bila huruma wala mpangilio.

Huku Don akitakiwa seneti, wanasheria wanamtaka afanye ''plead the 5th''

Ndani ya WH, McGahn ameuziliwa kutotoa ushirikiano na kamati hata kama ni Raia.

Magazeti ya NY Times na Wall Street yameeleza kuhusu WH kumtaka McGahn aseme '' hakukuwepo na obstruction of justice na kwamba Trump hakumuagiza amfukuze Mueller''.

Habari zinaeleza kuw alitakiwa kusema hayo kabla ya redacted report na baada ya kutolewa.

Maana yake ni moja AG Barr aliwatonya WH kuhusu ushuhuda wa McGahn

Ni kutokana na hilo, hakuna shaka kinachoitwa grand jury material ni uchafu wa Rais Trump na Familia yake dhidi ya Marekani.

Hiyo ndiyo sababu kubwa taarifa ya Mueller inafanywa jando

Kama ilivyoelezwa bandiko#856 Mag3 kesi zingine zipo katika state na si federal

Nguvu ya Barr kuziingilia ni ndogo, na kila kilichofichwa kitatoka hadharani

Hasira za Trump dhidi ya kuitwa mwanae zinajengeka katika msingi kuwa Don Jr atakuwa chini ya kiapo, taarifa za redacted material zipo hivyo kuna nyakati atalazimika kusema ukweli

Rais Trump anagoma kila kitu huku akisema taarifa ni total exoneration and vindication
Ikiwa ni hivyo kwanini anawazuaia akina McGahn kusema wanachojua huku akiwahukumu?

Taarifa za McGahn kumkatalia Trump mara mbili kuhusu ombi lake na huko nyuma kutaka kujiuzulu kunaeleza mengi na kwamba ana kitu anachojua ambacho ni mwiba kwa Trump

Kila mbinu inaoenekana kubuma. Jana Rud Guillian alianzisha mjadala makusudi kuhamisha habari ya Mueller. Hilo halijafanikiwa zaidi ya ku back fire WH na kampeni ya Trump

Muda si mrefu watu watajua zaidi ya wanachojua.
Watabaini Barr ameficha nini na hapo kunaweza kuwa na tatizo tena kubwa.

Tusemezane
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,138
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,138 2,000
Trump will be impeached soon.
Bavaria impeachment kwasasa hivi haitatokea kwasababu zifuatazo
1. Ili kuandika article of impeachment na ipitishwe lazima kuwe na ridhaa ya House na senate
Kwahouse Dems ni majority na ipo hofu kwa Republicans ambao wanaweza kuongeza idadi

Tuliona wakati wa mjadala wa taarifa ya Mueller, Republicans wote ndani ya house waliunga mkono taarifa hiyo iwekwe wazi

Katika senate, majority ni Republicans na inahitaji 2/3 ambayo ni sawa na maseneta 67
Kwa woga aliowajengea GOP kupata maseneta 18 kuunga mkono hoja ni ngumu sana

2. Hilo ndilo linasababisha AG Barr afiche taarifa ya Mueller, Rais Trump akiweka executive privilege kwa taarifa, huku akikataa mashahidi muhimu sana kutokwenda mbele ya kamati akiwemo Mueller

Trump anafahamu taarifa iliyofichwa kwa kisingizo cha grand jury inaweza kubadilisha kabisa mawazo ya baadhi ya maseneta kama Richard Burr ambaye sasa anamtaka Don Jr

Kwa mantiki hiyo Democrats wanaogopa kwamba impeachment haitatoa matokeo tarajiwa na hilo linaweza kumjenga Trump kuelekea uchaguzi mkuu kama ilivyokuwa kwa Bill Clinton

Lakini pia kukiwa na siku si zaidi ya 500 kuelekea uchaguzi , kuna uwezekano impeachment ikatumiwa kama hoja ya kumshindwa Trump katika sanduku la kura na kutaka kumuondoa kwa kutumia Bunge
 
Bavaria

Bavaria

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2011
Messages
45,820
Points
2,000
Bavaria

Bavaria

JF-Expert Member
Joined Jun 14, 2011
45,820 2,000
Bavaria impeachment kwasasa hivi haitatokea kwasababu zifuatazo
1. Ili kuandika article of impeachment na ipitishwe lazima kuwe na ridhaa ya House na senate
Kwahouse Dems ni majority na ipo hofu kwa Republicans ambao wanaweza kuongeza idadi

Tuliona wakati wa mjadala wa taarifa ya Mueller, Republicans wote ndani ya house waliunga mkono taarifa hiyo iwekwe wazi

Katika senate, majority ni Republicans na inahitaji 2/3 ambayo ni sawa na maseneta 67
Kwa woga aliowajengea GOP kupata maseneta 18 kuunga mkono hoja ni ngumu sana

2. Hilo ndilo linasababisha AG Barr afiche taarifa ya Mueller, Rais Trump akiweka executive privilege kwa taarifa, huku akikataa mashahidi muhimu sana kutokwenda mbele ya kamati akiwemo Mueller

Trump anafahamu taarifa iliyofichwa kwa kisingizo cha grand jury inaweza kubadilisha kabisa mawazo ya baadhi ya maseneta kama Richard Burr ambaye sasa anamtaka Don Jr

Kwa mantiki hiyo Democrats wanaogopa kwamba impeachment haitatoa matokeo tarajiwa na hilo linaweza kumjenga Trump kuelekea uchaguzi mkuu kama ilivyokuwa kwa Bill Clinton

Lakini pia kukiwa na siku si zaidi ya 500 kuelekea uchaguzi , kuna uwezekano impeachment ikatumiwa kama hoja ya kumshindwa Trump katika sanduku la kura na kutaka kumuondoa kwa kutumia Bunge
Asante mkuu kwa maelezo yako.

Naomba pia kuuliza maana ya neno "GOP"

Nimekuwa nikilisoma mara kwa mara kwenye siasa za marekani.
 

Forum statistics

Threads 1,307,001
Members 502,311
Posts 31,598,982
Top