Duru Za Siasa: U.S Chini ya Donald J. Trump

Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,134
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,134 2,000
Wanajamvi

Uchaguzi wa US umekamilika jana baada ya D.J Trump kuwa Rais wa 45
Leo ilikuwa siku ya kwanza kamili ya Trump kama Rais wa US

Uzi utakuwa utaangalia serikali mpya na mwelekeo wa siasa na uchumi
Siasa za Marekani , taifa lenye nguvu katika uso wa dunia zinaathari kubwa duniani

Ni kwa kuzingatia hilo, uzi utaleta kwa kadri, yanayojiri katika Taifa hilo

Tutaendelea kumalizia hotuba ya Trump baada ya kutawazwa katika uzi huu
Duru za Siasa: Matokeo ya Uchaguzi Marekani

Rais Trump, mfanyabiashara aliyefanikiwa katika biashara ameondoka katika utawala wa makampuni na sasa ni mtawala wa umma na Taifa la Marekani

Kuchaguliwa kwake kama mtawala wa juu wa Taifa lenye ushawishi umekuja na mshtuko kutokana na nafasi aliyopewa katika uchaguzi wa ndani ya chama cha Republican na ule mkuu

Kuna mitazamo tofauti kuhusu kuchaguliwa kwa Trump. Kwasababu zozote ambazo wachunguzi wanaendelea kuzifuatilia kisiasa , uchumi, jamii n.k. Trump ndiye Rais wa Marekani

Siku ya kwanza, Trump amekumbana na changamoto za utawala wa nchi na si kampuni binafsi

Katika historia ya miongo michache ya Marais wa US, siku ya kwanza haikuwa nzuri kwake

1. Maandamano ya wanawake duniani
2. Ziara iliyozua utata katika Intelligence community (IC)

Tutajadili mambo hayo mawili na picha ya haraka ya nini kitarajiwe kwa siku za usoni

Tusemezane
 
El Jefe

El Jefe

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2016
Messages
281
Points
500
El Jefe

El Jefe

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2016
281 500
Naona humjui Nancy Pelosi, DEMS wako pamoja tena sana tu. Impeachment itaendeshwa na House na hapo ndipo ushahidi wote wa alichonuia Mueller utakapoonekana wazi hata kwa waliopofuka kimapenzi na Trump.

Nancy anawataka DEMS kutokurupuka, anataka kwanza ripoti kamili ya Mueller ikiwepo kuwa-subpoena wahusika pamoja na Barr, Rosenstein na Mueller mwenyewe lakini mwisho ni impeachment, hakuna namna.

Kumbuka hata hiyo ripoti iliyotolewa na Barr bado ni redacted...zinazopenyezwa ni kwamba ripoti nzima ya Mueller ambayo lazima itapatikana kwenye impeachment process imemkaanga vibaya Trump mpaka kwenye tuhuma za conspiracy. Collusion is a non-issue.

Issue ya Rais Clinton ilikuwa ni ndogo sana kisheria labda kimaadili...eti kufanya mapenzi na intern. Kama Senate haitaafiki maamuzi ya House, hilo ni jambo lingine lakini halizuii House kutekeleza wajibu wake. Je unasemaje kuhusu Richard Nixon?

Je aliyofanya Trump angefanya Obama, kweli leo Republicans wangekaa kimya? Je unakumbuka walivyotaka kum-impeach kwa kutumia tu Executive Action kwenye swala la DACCA?
Sidhani kama kuna kipya kwenye hii kesi. Dems kwa hesabu zao wanataka waungwe mkono na public na Republicans kwa kufanya partisan hearing taratibu kwa mda mrefu, huku wakitafuta "conspiracy" ambayo Mueller amehitimisha haipo.

Hii ya kusema kwamba "unredacted report" inaonyesha "conspiracy" au "imemkaanga Trump" kwakweli sijui mnaitoa wapi, maana aliyehitimisha ni aliyefanya uchunguzi. "Conspiracy" ingekuwepo sehemu zilizofichwa, hitimisho la ripoti ingekuwa tofauti na ilivyo, it's just common sense.

Kuhusu "obtruction of Justice" ya Clinton kasome vizuri, ni zaidi ya "kufanya mapenzi na intern".

Dems waliopo House wafanye wanachofanya kwenye huo mkakati wao, lakini mwisho wa siku wakipeleka hiyo "trial" Senate itaishia "Acquittal". Huo ndio ukweli mchungu.

Kesi ya Nixon ilikuwa "too clear", "obstruction" yake ililenga kuingilia uchunguzi wa kosa la msingi alilofanya (underlying crime) ambayo ilikuwa ni kutuma watu kufanya "wiretapping" kwenye DNC HQ. Ushahidi ukawekwa, mtu hawezi kubisha, na ndio maana aliondoka mwenyewe mapema.

Kwa Trump, kesi ya "obstruction" imesimama hewani.
 
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Messages
10,485
Points
2,000
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined May 31, 2008
10,485 2,000

El Jefe, kwa ufahamisho wako, fumbo la kwa nini ripoti ya Mueller ilibidi iwe redacted, imefumbuliwa na kidole kinanyoshwa kwa mtu aliyesimamia uchunguzi huo Rod Rosenstein. Kama unakumbuka kuna wakati Republicans walitaka kum-impeach Rosenstein kwa kutaka kuvaa waya kumnasa bosi wake Rais Donald Trump. Kiajabu ajabu jambo hili lilisha hivi hivi na Rosenstein akaweza kuendelea na kazi yake...umejiuliza kwa nini?

Juzi Barr kadai redaction aliyokuwa akiifanya hakuwa peke yake, alishirikiana na Rod Rosenstein ambaye ndiye alikuwa akimsimamia Mueller katika uchunguzi. Sasa sababu ya kwa nini Barr hakumshirikisha Mueller mwenyewe imeanza kujulikana; ripoti yake ilikuwa mbaya sana kwa Trump hivyo ilibidi baadhi yake ifunikwe. Barr na Rosenstein waliifanya kazi hii pamoja na kwa ustadi mkubwa ili kumlinda bosi wao Donald Trump.

Labda utauliza kwa nini Rosenstein alikubaliana na mpango huu...nakuomba tu uvute subira, chungu liko jikoni na muda si mrefu chakula kitawekwa mezani...kaa tu mkao wa kula. Hii ndiyo sababu kubwa inayowalazimisha DEMS kutaka kuwahoji watatu hao; Barr, Rosenstein na Mueller. Tayari habari ilishavuja kwamba wasaidizi wa Mueller waliilalamikia barua na hitimisho la Barr katika taarifa yake ya kwanza...jiulize Mueller yuko wapi?
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,134
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,134 2,000
El Jefe, Rod Rosenstein. Kama unakumbuka kuna wakati Republicans walitaka kum-impeach kwa kutaka kuvaa waya kumnasa bosi wake Rais Donald Trump.Jambo hili lilisha hivi hivi na Rosenstein akaweza kuendelea na kazi...umejiuliza kwa nini?

Juzi Barr kadai redaction aliyokuwa akiifanya hakuwa peke yake, alishirikiana na Rod Rosenstein ambaye ndiye alikuwa akimsimamia Mueller katika uchunguzi. Sasa sababu ya kwa nini Barr hakumshirikisha Mueller mwenyewe imeanza kujulikana; ripoti yake ilikuwa mbaya sana kwa Trump hivyo ilibidi baadhi yake ifunikwe.

Barr na Rosenstein waliifanya kazi hii pamoja na kwa ustadi mkubwa ili kumlinda bosi wao Donald Trump.

Labda utauliza kwa nini Rosenstein alikubaliana na mpango huu..
Mkuu, tangu Mueller akabidhi ripoti hajaonekana na kiongozi yoyote wa DOJ. Kwanini!

Pili, Roseinstein alikuwa aondoke Barr alipoingia, akakubali kuendelea hadi taarifa itakapotoka

Tatu, Rod anachokifanya ni kujilinda. Kuna hilo la kuvaa uzi ambalo kwake ni gumu sana
Kuna suala la surveillance inayoitwa spying ambayo Rod ndiye aliyeiidhinisha

Repblicans waliahidi kumwendea kombo kwa hayo mawili na moja lingemtia matatani
Hivyo kaamua kuwa loyal kwa Barr

Kuna kitu watu hawajakifuatilia. Siku alipotangaza ripoti ya Mueller masaa machache kabla ya kuitoa, Barr alisema '' kuhusu suala la obstruction of justice, tulikuwa hatkubaliani mwisho tukakubaliana'' Wachunguzi wanafuatilia, alikuwa hakubaliana na nani Roseinstein au Mueller?

Ukitaka kujua kuna kitu kinafichwa, kwanza, ni jitihada za kutaka ripoti isitoke hata kwa congress
Congress ina haki ya kuona siri zaidi ya general public. Fursa hiyo wamenyimwa

AG Barr akatoa fursa ya gang of 8 kuona less redacted. Hapa tu unaweza kuhisi jambo
Gang of 8 yenye GOP 4 na Dems 4 inaona kila siri ya nchi. Haina limit
Barr alitaka gang of 8 waione taarifa tena less redacted akijua wana kiapo cha kutosema lolote

Ndani ya gang of 8 ukitoa habari hakuna faini wala nini ni kifungo kikubwa sana
Hivyo Barr alitaka waone less redacted na kutoka hapo wakae kimya akidai congress imeona

Kwa siasa za DC, watu wa Mueller hawana raha kwasababu ripoti yao inabadilishwa kisiasa

Mueller anayeshambuliwa na Trump akienda katika congress atanwagwa kila kitu
Atakuwa chini ya oath na taarifa ipo hivyo siku yoyote anaweza kuhukumiwa akidanganya

Mueller atataka kumthibitisha Trump wrong na hapo kutakuwa na ufafanuzi zaidi
Kuna Mcgahn anayesakamwa na Trump naye atakuwa huru kumwaga mambo

Kwa wasiojua siasa za viunga vikuu DC hawana habari media zina taarifa kutoka vyanzo

Ndani ya DC sources ni nyingi kinachosubiriwa ni mwanya
Kwamba, itatoka hilo ni suala la muda tu

Republicans wanamlaumu sana Barr. Summary yake na jinsi alivyoitoa taarifa zimejenga mazingira ya shaka na kuchagiza udadisi zaidi. Mbele ya kamati za Bunge, Barr ataibua mjadala zaidi na hatima yake ni ripoti kuwekwa hadharani
 
El Jefe

El Jefe

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2016
Messages
281
Points
500
El Jefe

El Jefe

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2016
281 500
El Jefe, kwa ufahamisho wako, fumbo la kwa nini ripoti ya Mueller ilibidi iwe redacted, imefumbuliwa na kidole kinanyoshwa kwa mtu aliyesimamia uchunguzi huo Rod Rosenstein. Kama unakumbuka kuna wakati Republicans walitaka kum-impeach Rosenstein kwa kutaka kuvaa waya kumnasa bosi wake Rais Donald Trump. Kiajabu ajabu jambo hili lilisha hivi hivi na Rosenstein akaweza kuendelea na kazi yake...umejiuliza kwa nini?

Juzi Barr kadai redaction aliyokuwa akiifanya hakuwa peke yake, alishirikiana na Rod Rosenstein ambaye ndiye alikuwa akimsimamia Mueller katika uchunguzi. Sasa sababu ya kwa nini Barr hakumshirikisha Mueller mwenyewe imeanza kujulikana; ripoti yake ilikuwa mbaya sana kwa Trump hivyo ilibidi baadhi yake ifunikwe. Barr na Rosenstein waliifanya kazi hii pamoja na kwa ustadi mkubwa ili kumlinda bosi wao Donald Trump.

Labda utauliza kwa nini Rosenstein alikubaliana na mpango huu...nakuomba tu uvute subira, chungu liko jikoni na muda si mrefu chakula kitawekwa mezani...kaa tu mkao wa kula. Hii ndiyo sababu kubwa inayowalazimisha DEMS kutaka kuwahoji watatu hao; Barr, Rosenstein na Mueller. Tayari habari ilishavuja kwamba wasaidizi wa Mueller waliilalamikia barua na hitimisho la Barr katika taarifa yake ya kwanza...jiulize Mueller yuko wapi?
Rosenstein amezungumzia hizo taarifa ulizoandika na kusema ni "nonsense", hazina ushahidi. Ina maana Mag3 umeandika vitu ambavyo hauna uhakika navyo?

"Some of the nonsense that passes for breaking news today would not be worth the paper it was printed on, if anybody bothered to print it”

Rosenstein amewakwaza Dems kwa kumtetea AG Barr namna alivyoshughulikia ripoti ya Mueller, na kusema ni mtu mwaminifu. Hawakutegemea! Rosenstein alisema katika kazi yake, wanahitaji kuthibitisha ukweli kwa kutumia ushahidi usio na shaka.

"The difference is in the standard of proof. In my business, we need to prove facts with credible evidence, prove them beyond any reasonable doubt, and prove them to the unanimous satisfaction of a neutral judge and an unbiased jury of 12 random citizens”

Politico waliandika jambo la muhimu kuwa wasaidizi waliolalamikia barua ya Barr waliridhika na "redactions" zilizofanywa na Barr. Kama kulikuwa na "kufichwa kwa taarifa mbaya" unadhani wangeridhika?

"Even Mueller’s prosecutors, who were upset with how Attorney General William Barr initially portrayed their conclusions in a four-page summary letter in March, feel comfortable with the redactions, according to a source close to some of the special counsel’s attorneys"

Dems wengi hawaoni "impeachable offense" kama Article II, Section 4 ya katiba inavyotamka. Jerry Nadler na wenzake wanahangaika na "innuendos".

Kwenye ripoti ya Mueller ambayo ni "less redacted", taarifa za "grand jury" peke yake ndizo zimefichwa kwa sababu za kisheria. Dems wanataka kuona taarifa za "grand jury" pia, AG Barr anasema kikanuni hawaruhusiwi!

"Barr has pledged not to provide grand jury material to Congress, stating that he is operating within the guidelines of the special counsel regulations"

Hata hivyo, kuna wawakilishi ambao tayari wameshaona ripoti hiyo ambayo ni "less redacted", kama Rep. Doug Collins (ranking Republican kwenye Judiciary Committee) aliyesema hamna kilichobadilika.

"The report’s 182-page look at obstruction questions includes only four redactions in total, and both volumes reinforce the principal conclusions made public last month."

Nadhani suala la "full report" na "underlying documentations" ya ripoti ya Mueller litaamuliwa na mahakama, na sio kwa kumlazimisha AG Barr avunje sheria na kanuni za DOJ.

Kuhusu Mueller alipo nadhani sio suala la msingi kwa sababu ataonekana kwenye "hearings" za HJC.

Dems wange-'move on' tu, hamna kitu hapa, wanapoteza mda, hata Mitch McConnell (Senate Majority Leader) kawaambia.

"Well, look, I think it's time to move on. This investigation was about collusion, there's no collusion, no charges brought against the president on anything else, and I think the American people have had quite enough of it"
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,134
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,134 2,000
VIUNGANI DC
ROD KUACHIA NGAZI MAY 11
JOTO LAPANDA, AG BARR ANG'AKA

Deputy AG Rod Roseinstein ametangaza kuachia ngazi May 11.

Rod alitaka kuachia ngazi kabla ya ripoti ya Mueller hata hivyo aliombwa ''ku land ndege'' salama

Sijambo geni na ilitarajiwa kutokea. Kinachotia shaka ni siku 11 zijazo ambazo kutakuwa na mtifuano kati ya DOJ na House. Rod anajua kauli zake nyingi zina utata

Baada ya maazeti kuanika ''loyality' yake kwa Trump, Roseinstein hana njia

Rod ana utata sana hasa unaonasibishwa na kibarua zaidi ya itikadi yake ya kihafidhina

Kuondoka kwake ni katika kukwepa mkono wa mahojiano unaowasubiri katika House

Mkono huo umemgusa AG Barr ambaye amtakiwa kutokaea katika kamati ya Bunge ya Nadler

Katika hali isiyo ya kawaida, Barr anatishia kutokwenda akitaka kuhojiwa na wajumbe tu
Mwenyekiti Nadler anasema kutakuwa na muda maalumu wa wanasheria wa kamati kumhoji

Barr ni mwanasheria nguli akiwa na wadhifa wa AG mara mbili. Haieleweki kinachomtia hofu ni kipi ikizingatiwa wanasheria watakaomhoji hawana viwango alivyofikia katika taaluma ya sheria

Kuhojiwa na 'staff' wa kamati inaonekana ni jambo geni hasa kwa wageni wa siasa za viungani
Mwenyekiti Nadler amesema Barr hawezi kuratibu namna ya mahojiano

Suala la kuwatumia wanasheria katika mahojiano limefanyika wakati Republicans wakiongoza kamati za seneti katika kumsikiliza Jaji Kavanaugh. Je, wanachofanya GOP ni unafiki?

Barr anafahamu fyongo za nyuma zitamtia matatani, anatishia kutotokea mbele ya kamati.

Huyu ni Barr aliyeandika vikurasa 4 akiwafinyanga watu kuhusu ripoti ya Mueller
Vipi Barr aliyesimama mbele ya wanahabari mara mbili anasita kwenda mbele ya kamati?

Ikiwa hatatokea ataitwa kwa lazima na hapo gogoro la kisheria linanukia
Ni utaratibu mpya unaoendelea wa WH kupoka nguvu ya House

Tusemezane
 
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Messages
10,485
Points
2,000
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined May 31, 2008
10,485 2,000
Barr ni mwanasheria nguli akiwa na wadhifa wa AG mara mbili. Haieleweki kinachomtia hofu ni kipi ikizingatiwa wanasheria watakaomhoji hawana viwango alivyofikia katika taaluma ya sheria...

Tusemezane
Barr kalikoroga mwenyewe sasa anashindwaje kulinywa? Kwani hakujua uchungu wake? Watanzania tunayo mengi ya kujifunza hapa na kubwa ni kwamba Mwanasheria Mkuu ingawa anateuliwa na Rais, hatakiwi kuwa mwanasheria wa Rais bali mwanasheria wa wananchi. Haapi kumtii Rais, anaapa kuitii katiba ya nchi. Rais hayuko juu ya sheria.
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,134
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,134 2,000
SONGOMBINGO ZA JIMBO KUU LA DC
MUELLER ALIANDIKA BARUA KWA BARR
AG BARR KIKAAONGONI, ALIPOTOSHA UMMA

Marejeo:
Tulieleza shaka kuhusu kurasa nne (bandiko 765) za AG Barr kwamba zililenga kubadili mawazo ya umma ''public perception' na kwamba aliacha wiki 4 Trump na wapambe wake waidhoofishe taarifa ya Muller

Pili; Tulieleza kuwa Mueller lazima atakuwa na executive summary ambayo haina classified info, intel au grand Jury material. Hiyo ndiyo ililenga kutolewa kwa umma kabla ya redacted version

Tatu; tulihoji kuwa kwanini Mueller hakuwepo katika kutangaza taarifa au popote pale

Nne; Tukahoji kwanini watumishi wa Mueller walilalamika kuhusu kupotoshwa kwa taarifa

Tano: Tukasema taarifa ilipotosha, kurasa 400 kuwa summarized katika vikurasa vinne
Lengo lilikuwakuwakusanya wasiojua siasa za DC na kuanza kuikimbiza kama mwenge!

Sita: Tulihoji kuhusu timing ya kutoa taarifa huku Barr akijipa fursa ya kueleza anachojua bila taarifa kuwekwa hadharani. Kwamba, waandishi watauliza nini ikiwa hawajasoma taarifa

Hizi ndizo siasa za viunga vya DC zinazohitaji kusikiliza, kusoma na ku digest na wala si kubeba vikaratasi , kubeba habari za tea party kupitia The Beast, kumsikiliza Mitchell McConor kana kwamba ni mtu fair sana n.k. Siasa za DC zinahitaji utulivu na si ushabiki, huumba na huumbua

Juzi tulieleza kwanini Rosenstein anakimbia siku 11 ingawa alijulikana ataondoka. Hii ni baada ya mawasiliano yake na Trump kunaswa. Na kwamba, anajua fyongo ya Barr itambeba mzima

Tulieleza Barr atakaangwa na tulijua kuna 'bomu' linasubiri dakika za majeruhi kabla hajaenda mbele ya kamati ya Bunge

Bomu limepasuka, kwamba, Mueller alichukizwa na upotoshaji wa taarifa yake (mischaracterization) Huyu ni Mueller siyo waandishi wa The Beast

Mueller alimpigia simu Barr na kuweka barua kama kumbu kumbu ili muda ukifika akaangwe

Maongezi ya simu yalihusu nini kifanyike baada ya taarifa, na hakukuwa na makubaliano

Kesho Barr atakuwa ndani ya kamati ikiwa ni masaa machache tu ya kujiandaa kwa utata wa summary yake na barua ya Mueller inayoeleza wazi alipotosha

Barr sasa itabidi aeleze ukweli kwasababu Mueller ataitwa na kamati ya Bunge
Barr ataanza kesho na akisema uongo , ni kibano tu. Mueller atafuata

Tutaendelea kuwajuza zinazojiri, kwasasa ni hilo taarifa ya Mueller ilipotoshwa kwa mujibu wa Mueller na siyo Banon au Hanity. Taarifa ya Mueller inaendelea kumtesa Trump

Tusemezane
 
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Messages
10,485
Points
2,000
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined May 31, 2008
10,485 2,000
SONGOMBINGO ZA JIMBO KUU LA DC
MUELLER ALIANDIKA BARUA KWA BARR
AG BARR KIKAAONGONI, ALIPOTOSHA UMMA

Tulieleza Barr atakaangwa na tulijua kuna 'bomu' linasubiri dakika za majeruhi kabla hajaenda mbele ya kamati ya Bunge

Bomu limepasuka, kwamba, Mueller alichukizwa na upotoshaji wa taarifa yake (mischaracterization) Huyu ni Mueller siyo waandishi wa The Beast
Na hii ndiyo sababu hasa inayomfanya Barr asite kufika kwenye mahojiano na Congress na anaogopa kuhojiwa na wabobezi wa sheria kama taratibu zinavyoruhusu...anaogopa kikaango!

Hata hivyo hawezi kukwepa na hapa kapatikana...shuhudia yanayoweza kumpata huyu mwingine...

Cummings to ex-White House official: Answer our questions or face prison!
House Oversight and Reform Committee Chairman Elijah Cummings is threatening fines or even imprisonment for a former White House official if he refuses to satisfactorily answer questions when he appears for a closed-door interview on Wednesday.

“There is no tool in our toolbox that we should not explore,” Cummings (D-Md.) told reporters on Tuesday, warning that he could move to hold former White House Personnel Security Director Carl Kline in contempt of Congress.

Barr anachezea moto na hii ndiyo sababu Rosenstein kajitoa mapema!
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,134
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,134 2,000
Na hii ndiyo sababu hasa inayomfanya Barr asite kufika kwenye mahojiano na Congress na anaogopa kuhojiwa na wabobezi wa sheria kama taratibu zinavyoruhusu...anaogopa kikaango!
Barr anachezea moto na hii ndiyo sababu Rosenstein kajitoa mapema!
Mueller alikuwa na uwezo wa kuongea na Barr moja kwa moja au kwa simu.

Mueller aliamua kuandika barua ili kuwe na kumbukumbu(paper trail) hata atakapohojiwa

Inaripotiwa, barua ilimfikia Rosenstein ambaye aliifikisha kwa Barr.
Kumbuka Rod Rosenstein ndiye alikuwa msimamizi wa Mueller.

Baada ya kutua kwa Barr, ghafla alimtafuta Mueller na maongezi yao hawakukubaliana

Barua ya Mueller inasema, Barr alipotosha umma katika ''context, nature and substance''

Barr alificha substance kwa njia ya intel , classified info na grand jury

Wiki iliyokwisha alipoulizwa endapo Mueller alikubaliana na kurasa zake nne na taarifa katika media, Barr alisema hajui. Wakati anasema hayo tayari alishapokea barua ya Mueller

Hapa kuna mambo mawili. Barr tayari ameshapoteza credibility kama tulivyowahi kusema

Hilo tayari limefungua milango ya kamati za bunge kumtaka asishiriki kesi nyingine 12 zilizopelekwa FBI hasa SDNY. Kaandikiwa Inspector general kuhusu hilo

Pili, sasa kuna kila sababu ya kupata taarifa nzima. Inaelezwa, uchafu mwingine ameufukia kwa hoja ya grand jury material. Kesi ikienda mahakamani kuna njia nyeupe ya kupata taarifa nzima

Deputy Rosenstein aliamua kuachia ngazi akijua barua itavuja tu. Haya tumeyasema sana, ndani ya viunga vinene vya DC hakuna siri. Kuna watu wanafanyakazi mchana usiku

Rosenstein alijua maongezi yake na Trump yapo hadharani wakati anamuahidi wapo timu moja.

Baada ya kupokea barua ya Mueller, Rod akajua hamkani si shwari kunguru mjanja huepusha ubawa wake, akaamua May 11 hayupo katika mjengo wa DOJ

Kwa wanajamvi tuliwaeleza mapema kabisa, Barr analisha watu matango pori

Ameamua 'kujilipua' ili kumkingia kifua Trump. Sasa kuna anatakiwa ajiuzulu yeye

Hofu aliyo nayo inawatia Republicans hofu kwamba kina cha maji kinaweza kumzidi kimo

Taarifa yake ya leo usiku(marekani) inaeleza alivyo panic na anavyohaha kujinasua
Ile timing aliyofanya inamrudi, NY Times na WAPO nao wamejibu. Usiku huu Barr yupo ofisini

Tusemezane
 
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Messages
10,485
Points
2,000
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined May 31, 2008
10,485 2,000
Hofu aliyo nayo inawatia Republicans hofu kwamba kina cha maji kinaweza kumzidi kimo...

Taarifa yake ya leo usiku(marekani) inaeleza alivyo panic na anavyohaha kujinasua
Ile timing aliyofanya inamrudi, NY Times na WAPO nao wamejibu. Usiku huu Barr yupo ofisini
Barr amechezea shilingi kwenye tundu la choo...Kamati ya House inamtaka awasilishe barua halisi aliyoandikiwa na Mueller kesho asubuhi saa nne bila kuchelewa. Huu utakuwa mwanzo tu na kinachofuata ni ripoti nzima ya Mueller kwani Nadler ameshasema Wamarekani wamechoka kulishwa matango pori na WH...kila mtu huko ni muongo. Ikibidi Mueller mwenyewe ataitwa kuhojiwa ili ukweli wote ujulikane. Hatua ya Barr kutaka kufunika kombe mwanaharamu apite imekwama.
 
El Jefe

El Jefe

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2016
Messages
281
Points
500
El Jefe

El Jefe

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2016
281 500
Jana DOJ wametoa copy ya maelezo yaliyoandaliwa na AG Barr kwa ajili ya mahojiano yake kwenye Senate Judiciary Committee leo. Ni maelezo yanayoeleweka.

Barua ya Barr ya March 24 ilikuwa na hitimisho la msingi lililofikiwa na Mueller (bottom line/principle conclusions) na sio upotoshaji. Ndio maana hata Mueller mwenyewe amesisitiza kuwa hakuna opotoshaji au uongo wowote kwenye barua ya Barr kwa umma (kwa mujibu wa Msemaji wa DOJ Kerri Kupec).

"The special counsel emphasized that nothing in the attorney general's March 24 letter was inaccurate or misleading"

Tulisema kuwa AG Barr hawezi kupotosha umma au "kulisha watu matango pori" juu ya ripoti ya Mueller kwa kuandika summary ya kurasa nne, halafu baadae atoe ripoti hiyohiyo kwa umma ili umma usome "alivyopotosha". Ripoti sasa ipo kwa umma kama AG Barr alivyolenga ili nao waamue kama kuna "obstruction" au lah.

"My main focus was the prompt release of a public version of the report so that Congress and the American people could read it for themselves and draw their own conclusions"

AG Barr na Special counsel walikubaliana kuhusu "redactions" ya ripoti pia. Kwahiyo kusema kwamba "Barr alificha substance kwa njia ya intel, classified info na grand jury" ni kutokuelewa.

"The attorney general and the special counsel agreed to get the full report out with necessary redactions as expeditiously as possible"

AG Barr hajapoteza credibility kwa umma, labda kwa partisan Dems walio Congress. Barr ni mtu mwenye msimamo na anayefuata sheria na kanuni na anakataa kuendeshwa na siasa za DC.

Ni muhimu kumsikiliza AG Barr kwa makini hasa atachokisema leo kwenye SJC.
 
Kigarama

Kigarama

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2007
Messages
2,488
Points
1,225
Kigarama

Kigarama

JF-Expert Member
Joined Apr 23, 2007
2,488 1,225
Mjadala huu unaturudisha mara kwa mara kuja kuchungulia JF kuna nini. Nguruvi3 Mag3 na wengineo mnatufanya tukumbuke zama zile. Kwa kweli majadiliano yenu yanatupa faraja kwamba JF itaendelea kuwepo active kwa kipindi kirefu kijacho..
 
Kigarama

Kigarama

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2007
Messages
2,488
Points
1,225
Kigarama

Kigarama

JF-Expert Member
Joined Apr 23, 2007
2,488 1,225
siasa za Marekani ukizitazama kwa jicho la Tanzania huwezi kuzielewa kabisa. Kwanza kuna vyombo vingi vya habari na kila chombo cha habari kina mlengo wake wa siasa. Kwa ivo usipofanya subira na kulinganisha kile unachopata toka kwenye kimojawapo cha vyombo hivyo vya habari na habari toka vyombo vingine vya habari unaweza kuchanganya mambo.

Marekani hakuna mtu mkubwa dhidi ya sheria, Wenzetu wamefanikiwa kutenganisha nafasi zao za kisiasa na ubinadamu wao. Trump ni mtu na ni rais pia. Huwezi kumshitaki Trump kama Rais kwenye mahakama za Marekani, lakini unaweza kumshitaki Trump kama mtu binafsi kwa nafasi zake za nje ya Urais alio nao.

Lakini kuna Uhuru mkubwa sana wa kutoa maoni na kushiriki kwenye siasa za Marekani. Hakuna kuomba ruhusa kuishitaki serikali wala si aibu ama kosa la kisheria kupingana na maoni ya serikali ama maoni ya Rais.

Kwa ivo kwa suala hili la Trump ni lazima litafika hadi kwenye Kampeni za Uchaguzi wa Mwakani na chama kitakachocheza karata zake vema ndicho kitakachofaidika na sakata hili.

Kwa mtazamo Trump amebanwa sana lakini naye amefanikiwa kuwaaminisha baadhi ya wamarekani kwamba yeye ni Rais anayeonewa gele na Democrats kwa ivo ndiyo chanzo cha vurumai zote hizo za kutaka kuujua ukweli juu ya uingiliaji mambo ya Uchaguzi uliofanywa na Urusi kwenye uchaguzi wa Marekani mwaka 2016.

Trump ni mbabe kwa silka na ni mtu aliyedekezwa na utajiri wa familia yao, Trump haamini kwenye kukosolewa bali anaamini kwenye kukosoa wengine hata kama kwa kutumia lugha mbaya. Yeye amekuzwa katika maisha yake kama bwana mkubwa mwenye akili nyingi sana na asiyehojika.

Ukichunguza hotuba za Trump ni zile zilizojaa majivuno na maneno ya kujaza sifa kuonesha kwamba kila analolifanya hakuna mwinginewe aliwahi kulifanya. Hali hiyo sasa inasemwa imemfikisha kuweka alama ya maneno ya uongo ama yasiyo sahihi aliyoyasema kufika zaidi ya 10,000 hivi sasa.

Lakini hata yeye hakosi wa kumuunga mkono kwani wapo wazungu weupe wa mashambani wenye kuamini kwamba Marekani ni yao peke yao na ni wao tu ndiyo wanaostahili kuitawala. Hao ndiyo wafuasi sugu wa Trump.

Trump anaungwa mkono sana na watu wabaguzi wa rangi na dini, watu wasio na elimu kubwa, wafanyabiashara za silaha na mafuta, na wanawake walioolewa wakaao majumbani (House wives).

Watu hao niliowataja wanajali zaidi maslahi ya kiuchumi hata kama haki za wengine hazizingatiwi wala masuala ya Mabadiliko ya tabia nchi yasipozingatiwa. Na ni watu kwa Kiswahili cha kisasa wanaopenda udaku.

Lakini uzuri wa Marekani vyombo vyao haviwezi kuingiliwa moja kwa moja na hata bunge kwa sasa linalaumiwa na wamarekani wengi sana kwa kuingiza siasa za mirengo ya vyama kwenye bunge.

Kwa ivo sio leo wala Kesho suala hili la uchunguzi wa Muller litamalizwa, bali mwisho wake ni pale ama Trump atakavyoangushwa nalo ama litakavyokiangusha chama cha Democratic kwenye uchaguzi wa mwakani.

Trump mpaka sasa anajivunia Mahakama ya Rufaa ya nchi hiyo ambayo imejaa majaji wahafidhina kwani kati ya majaji 9 waliomo 5 ni wahafidhina. Trump Keshaiteka Republican na kuiweka kwapani na hakuna anayefurukuta mbele yake kwenye chama hicho.

Mpaka sasa tukaze macho yetu na kusubiri na kuona nini kitatokea.
 
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Messages
10,485
Points
2,000
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined May 31, 2008
10,485 2,000
Ni muhimu kumsikiliza AG Barr kwa makini hasa atachokisema leo kwenye SJC.
Barr amekaangwa
Kakaangwa haswaaaaa...! Hebu shuhudia alivyokaangwa na mwanamama Kamila Harris...

Kamila: In reaching your conclusion, did you personally review all of the underlying evidence?

Barr: I did not.

Kamila: Did Deputy Attorney General Rod Rosenstein, who announced his resignation on Monday, look at any underlying evidence before coming to the official conclusion that Trump did not obstruct justice?

Barr: No. We accepted the statements in the report as the factual record. We did not go underneath it to see whether or not they were accurate. We accepted it as accurate.

Kamila: I think you’ve made it clear sir that you have not looked at the evidence and we can move on.

WOW, Kamila Harris just established that neither Barr or his staff read the underlying evidence and yet he decided that evidence wasn't just established...wasn't sufficient!

Also, Kamila got Barr to refuse to say he'd consult DOJ ethics to recuse himself from pending cases because of bias he's shown.

Baada ya mahojiano hayo, aliyekuwa AG wakati wa Nixon, John Dean, na ambaye amekuwa akisita kuafiki moja kwa moja na tuhuma dhidi ya Trump alikuwa na haya ya kusema kuhusu Barr...

At Senate hearings, Barr is engaging in the GOP practice of stonewalling. Obviously, he’s not going to admit he has been caught in a lie. The record speaks for itself. Kamala Harris’s questions tied him in a knot, leaving him mostly speechless.

Baada ya mahojiano ya leo mbele ya Republican Senate, naona Barr kaogopa na kakacha kikaango cha Democratic House.
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,134
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,134 2,000
"Kigarama, post: 31305250, member:
siasa za Marekani ukizitazama kwa jicho la Tanzania huwezi kuzielewa kabisa.
Inashangaza wapo wanalinganisha siasa zatu na za Marekani. Siasa za Marekani zina misuguano sana lakini zimejengwa katika misingi, kanuni na taratibu
Kwanza kuna vyombo vingi vya habari na kila chombo cha habari kina mlengo wake wa siasa.usipofanya subira na kulinganisha kile unachopata toka kwenye kimojawapo cha vyombo hivyo vya habari na habari toka vyombo vingine vya habari unaweza kuchanganya mambo
Ukisoma habari ni muhimu kuwa na fikra binafsi. Kwa mfano, suala la Mueller Fox news inayompigia debe Trumo ilisisitiza sana Barr atoe 'summary' ya Mueller kwa kile walichosema umma una kiu ya kujua. Hilo tu lilitosha kufikirisha kwamba kwa miaka miwili wamempiga vita Mueller ghafla wamekuwa wazuri sana kwa Mueller !

Barr alipotoa 'summary' ya kurasa nne tulisema watu wavute subira kuna harufu ya maoni ya Fox kuchukua nafasi ya DOJ. Lakini pia tukauliza kwanini summary ya Barr na siyo executive summary ya Mueller. Kila uchao ukweli na majibu ya maswali yanajidhihiri
Wamarekani wakiwemo GOP walivuta subiri isipokuwa Trump na Kellyanne Conway
Marekani hakuna mtu mkubwa dhidi ya sheria, Wenzetu wamefanikiwa kutenganisha nafasi zao za kisiasa na ubinadamu wao.
Kuanzia zama hizo hakuna mkubwa au aliyejuu ya sheria. Katika modern history, Nixon, Clinton, Bush sr na sasa Trump walithibitisha hilo pasi na shaka. Kwa Rais Trump hili la Russia bado ni donda ndugu na ataishi nalo
Barr anajaribu kuwa juu ya sheria, leo katika uwanja wa nyumbani wa GOP bado amekaangwa
Uzito wa joto la kikaango umemlazimu akimbie kamati ya House!
Trump ni mtu na ni rais pia. Huwezi kumshitaki Trump kama Rais kwenye mahakama za Marekani, lakini unaweza kumshitaki Trump kama mtu binafsi kwa nafasi zake za nje ya Urais alio nao.
Hadi sasa hivi kuna kesi ambazo 'statue of limitation' ni miaka 5
Kama hazitamalizwa sasa na ikiwa hatachaguliwa tena atapambana nazo mbele ya safari
Lakini kuna Uhuru mkubwa sana wa kutoa maoni na kushiriki kwenye siasa za Marekani. Hakuna kuomba ruhusa kuishitaki serikali wala si aibu ama kosa la kisheria kupingana na maoni ya serikali ama maoni ya Rais.
Hii ndiyo nguvu kubwa sana waliyo nayo Wamarekani. Kutoa maoni ni haki na haihitaji ruhusa kutoka kwa mtu
Rais mwenye nguvu duniani anajadiliwa tu. AG Barr anaanikwa tu n.k.
Kwa ivo kwa suala hili la Trump ni lazima litafika hadi kwenye Kampeni za Uchaguzi wa Mwakani na chama kitakachocheza karata zake vema ndicho kitakachofaidika na sakata hili.
Kila siku ipitayo suala hili linapata nguvu sana kuliko hata wakati wa uchunguzi
Katika uchaguzi mwakani kuna maeneo Trump hatakuwa na kauli kwani Mueller kaanika mambo mengi. Kwa mfano, ile kauli ya law and order haitasikika. Tena suala hili litakuwa na nguvu sana katika siasa za nje na litamweka katika wakati mgumu sana Russia ikiwa reference
Ukichunguza hotuba za Trump ni zile zilizojaa majivuno na maneno ya kujaza sifa kuonesha kwamba kila analolifanya hakuna mwinginewe aliwahi kulifanya. Hali hiyo sasa inasemwa imemfikisha kuweka alama ya maneno ya uongo ama yasiyo sahihi aliyoyasema kufika zaidi ya 10,000 hivi sasa.
Kila jambo alilofanya ni kubwa katika historia ya Marekani. Juzi kasema yeye ni Rais transparent katika historia ya Marekani!
Wamarekani wanatengeneza ajira kuliko wakati wowote wa historia ya Marekani!
Kuna kitu kinaitwa grandiosity halafu kimechanganyika na Narcissism
Trump Keshaiteka Republican na kuiweka kwapani na hakuna anayefurukuta mbele yake kwenye chama hicho.
Kama kuna kitu amefanikiwa hili la kuua Republicans amefanikiwa. Ukimsikiliza mtu kama Lindsey Graham utajua wapi GOP ilipo
GOP imepoteza kabisa ile misingi yake na sasa ni Trumpism

Small government, free market, fiscal policy n.k. hazipo tena. Kilichobaki ni abortion na gun

Leo akina Ted Cruiz waliomgomea Obama kuhusu infrastructure ndio wanaopiga debe
Akina Lindsey waliosimamia suala la debt sasa ndio wanaokota mipira ya golf
Orodha ni kubwa na inaendelea.
 
Mwalimu

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
1,525
Points
1,500
Mwalimu

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
1,525 1,500
Kakaangwa haswaaaaa...! Hebu shuhudia alivyokaangwa na mwanamama Kamila Harris...

Kamila: In reaching your conclusion, did you personally review all of the underlying evidence?

Barr: I did not.

Kamila: Did Deputy Attorney General Rod Rosenstein, who announced his resignation on Monday, look at any underlying evidence before coming to the official conclusion that Trump did not obstruct justice?

Barr: No. We accepted the statements in the report as the factual record. We did not go underneath it to see whether or not they were accurate. We accepted it as accurate.

Kamila: I think you’ve made it clear sir that you have not looked at the evidence and we can move on.

WOW, Kamila Harris just established that neither Barr or his staff read the underlying evidence and yet he decided that evidence wasn't just established...wasn't sufficient!

Also, Kamila got Barr to refuse to say he'd consult DOJ ethics to recuse himself from pending cases because of bias he's shown.

Baada ya mahojiano hayo, aliyekuwa AG wakati wa Nixon, John Dean, na ambaye amekuwa akisita kuafiki moja kwa moja na tuhuma dhidi ya Trump alikuwa na haya ya kusema kuhusu Barr...

At Senate hearings, Barr is engaging in the GOP practice of stonewalling. Obviously, he’s not going to admit he has been caught in a lie. The record speaks for itself. Kamala Harris’s questions tied him in a knot, leaving him mostly speechless.

Baada ya mahojiano ya leo mbele ya Republican Senate, naona Barr kaogopa na kakacha kikaango cha Democratic House.
Barr jana kashemsha vibaya sana manake maswali mengi aliokuwa anaulizwa hata yale straight forward ya kujibu NDIO au HAPANA amekuwa akizungusha maneno na kupiga chenga bila kutoa majibu... na ndio maana ameamua kukacha kitimoto cha congress manake huko ndio angekaangwa zaidi. Kwa hearing ya jana ndio amethibitisha bila shaka kwamba kwa sasa anasimama kama wakili wa Trump badala ya kusimama kama mwanasheria mkuu wa serikali.
 
El Jefe

El Jefe

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2016
Messages
281
Points
500
El Jefe

El Jefe

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2016
281 500
Kakaangwa haswaaaaa...! Hebu shuhudia alivyokaangwa na mwanamama Kamila Harris...

Kamila: In reaching your conclusion, did you personally review all of the underlying evidence?

Barr: I did not.

Kamila: Did Deputy Attorney General Rod Rosenstein, who announced his resignation on Monday, look at any underlying evidence before coming to the official conclusion that Trump did not obstruct justice?

Barr: No. We accepted the statements in the report as the factual record. We did not go underneath it to see whether or not they were accurate. We accepted it as accurate.

Kamila: I think you’ve made it clear sir that you have not looked at the evidence and we can move on.

WOW, Kamila Harris just established that neither Barr or his staff read the underlying evidence and yet he decided that evidence wasn't just established...wasn't sufficient!

Also, Kamila got Barr to refuse to say he'd consult DOJ ethics to recuse himself from pending cases because of bias he's shown.

Baada ya mahojiano hayo, aliyekuwa AG wakati wa Nixon, John Dean, na ambaye amekuwa akisita kuafiki moja kwa moja na tuhuma dhidi ya Trump alikuwa na haya ya kusema kuhusu Barr...

At Senate hearings, Barr is engaging in the GOP practice of stonewalling. Obviously, he’s not going to admit he has been caught in a lie. The record speaks for itself. Kamala Harris’s questions tied him in a knot, leaving him mostly speechless.

Baada ya mahojiano ya leo mbele ya Republican Senate, naona Barr kaogopa na kakacha kikaango cha Democratic House.
Umesikiliza hearing yote?

Kukubali ripoti ya Mueller kwamba ni sahihi bila kuangalia "underlying evidence" maana yake Mueller atakuwa muongo kama ripoti yake sio sahihi iwapo mtu mwingine akingalia "underlying evidence" na ku-establish kitu tofauti significantly.

Kwa kifupi ni kwamba, Sen. Kamala alitaka ku-establish kuwa kuna uwezekano kuna vitu Meller hakuweka kwenye ripoti yake, na Barr akamjibu kama kuna kitu hakipo reflected kwenye ripoti ya Mueller basi ni Mueller mwenyewe.

Kuhusu suala la bias, Sen. Kamala ameshindwa kuelezea ushahidi wa "bias" zaidi ya hisia binafsi ambazo haziwezi kusimama mbele ya DOJ Ethics Office.

AG Barr pia akiwa anamjibu Sen. Patrick Leahy (D-Vt.) amesisitiza kile tulichokisema humu kuwa Mueller hakufanya uchunguzi wake ili awape Congress wafanye uamuzi kuhusiana na suala la "obstruction". Na kwamba Mueller alivyoona hawezi kutumia "approach" yenye uwezekano wa kumshtaki Rais aliye madarakani asingeendelea na uchunguzi.

"[Mueller] has not said that he conducted the investigation in order to turn it over to Congress...That would be very inappropriate, that is not what the Justice Department does."

"I don't think Bob Mueller was suggesting the next step was for him to turn this stuff over to Congress to act upon,....That's not why we conduct grand jury investigations."

"I think that if he [Mueller] felt that he shouldn't go down the path of making a traditional prosecutive decision, then he shouldn't have investigated,...That was the time to pull up."

Maoni ya John Dean ni maoni binafsi, na tunaendelea kusisitiza kuwa suala la Trump halina mfanano wowote na Nixon kwenye "substance" bali ni "Russiagate" obsession.
 
Forum statistics

Threads 1,304,916
Members 501,588
Posts 31,531,410
Top