Duru Za Siasa: U.S Chini ya Donald J. Trump


Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,037
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,037 2,000
Wanajamvi

Uchaguzi wa US umekamilika jana baada ya D.J Trump kuwa Rais wa 45
Leo ilikuwa siku ya kwanza kamili ya Trump kama Rais wa US

Uzi utakuwa utaangalia serikali mpya na mwelekeo wa siasa na uchumi
Siasa za Marekani , taifa lenye nguvu katika uso wa dunia zinaathari kubwa duniani

Ni kwa kuzingatia hilo, uzi utaleta kwa kadri, yanayojiri katika Taifa hilo

Tutaendelea kumalizia hotuba ya Trump baada ya kutawazwa katika uzi huu
Duru za Siasa: Matokeo ya Uchaguzi Marekani

Rais Trump, mfanyabiashara aliyefanikiwa katika biashara ameondoka katika utawala wa makampuni na sasa ni mtawala wa umma na Taifa la Marekani

Kuchaguliwa kwake kama mtawala wa juu wa Taifa lenye ushawishi umekuja na mshtuko kutokana na nafasi aliyopewa katika uchaguzi wa ndani ya chama cha Republican na ule mkuu

Kuna mitazamo tofauti kuhusu kuchaguliwa kwa Trump. Kwasababu zozote ambazo wachunguzi wanaendelea kuzifuatilia kisiasa , uchumi, jamii n.k. Trump ndiye Rais wa Marekani

Siku ya kwanza, Trump amekumbana na changamoto za utawala wa nchi na si kampuni binafsi

Katika historia ya miongo michache ya Marais wa US, siku ya kwanza haikuwa nzuri kwake

1. Maandamano ya wanawake duniani
2. Ziara iliyozua utata katika Intelligence community (IC)

Tutajadili mambo hayo mawili na picha ya haraka ya nini kitarajiwe kwa siku za usoni

Tusemezane
 
TUJITEGEMEE

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Messages
13,713
Points
2,000
TUJITEGEMEE

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2010
13,713 2,000
Kwa taratibu za DOJ Rais akiwa madarakani hawezi kushtakiwa
DOJ wanasema hata kwa mtu asiyeshtakiwa ni makosa kumtaja kwa mujibu wa sheria zao
Halafu mnataka Rais wetu hapa JMT ashitakiwe...! Tuna matatizo gani ?
 
TUJITEGEMEE

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Messages
13,713
Points
2,000
TUJITEGEMEE

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2010
13,713 2,000
Duh, Cohen hakumung'unya maneno, kamwita bosi wake wa zamani ambaye sasa ni Rais wa Marekani mbaguzi wa rangi (a racist), tapeli (a conman) na mdanganyifu (a cheat).

Ingekuwa Tanzania, huyu jamaa angeokotwa pwani ya Kunduchi akiwa ndani ya kiroba.
Ripoti ya Muller imeishatua kwa Barr...na Barr kaitoa, tunaomba tathmini yako juu ya matokeo ya uchungu huu.
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,037
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,037 2,000
TAARIFA YA MUELLER

Hadi sasa hakuna anayejua kwa kina taarifa ina kitu gani ndani yake isipokuwa maafisa wa DOJ pamoja na AG Barr

Kuna misconception kubwa kwamba taarifa inaeleza ABCD. Taarifa ya Muelller haijatoka!
Taarifa inayotarajiwa ni summary ya AG Barr ambayo si taarifa ya Mueller

Kuna msemo maarufu wa kiingereza usemao ''the devil is in the details''
kwa maana kuwa ili kuelewa jambo kuna information zinazopatikana si moja kwa moja.
Kuna maneno kama implicitly na explicitly yenye maana sana katika weledi wa jambo

Hivyo kinachoendelea katika media na social network ni misleading information, hakuna aliyeona taarifa na kujua details zake. Habari za kusikia zinategemea msomaji na taarifa yake

Pili, kuna mjadala mzito unaoendelea na unaoibuka kila baada ya muda fulani kuhusu indictment ya Rais wa US. Haipo wazi kama anaweza au hawezi. Ukifuatilia kauli za wasomi wa sheria suala hilo lina utata. DOJ wanachokifanya si sheria bali ni utaratibu wao

Tatu, kisheria kuna makosa ya kushtakiwa na yapo yasiyofikia kiwango cha kushtakiwa
Collusion kama tulivyosema siku zote si kosa, bali linakuwa kosa ikiwa kuna 'conspiracy'

Nne, ni kitu cha ajabu kidogo kwamba WH haitaki taarifa iwe wazi.
Hakuna aliyejua kuwa Paul Manafort aslishirikiana na Mrusi wa Kremlin katik kushea internal data polling.Katika court filling ilikuwa katika sealed affidavit.
Kosa lilifanywa na Lawyer wa Manafort aliyeshindwa kufuta sehemu muhimu.

Hilo likatoa nafasi kwa wana habari kujua nini kilikuwemo.
Ndiyo maana watu wanasema the devil is in the details.

Hadi taarifa itakapopatikana ni mapema mno kuwa na conclusion ya aina yoyote

Tusemezane
 
El Jefe

El Jefe

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2016
Messages
238
Points
500
El Jefe

El Jefe

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2016
238 500
Barua ya AG William Barr ya uchambuzi wa ripoti ya Special Counsel Mueller kwenda Congress ikionyesha hakuna "Collusion" kati ya Kampeni Trump na Russia kuingilia uchaguzi wa US 2016 na pia Trump hakuzuia upatikanaji wa haki (Obstruction of Justice).20190325-0001.jpeg20190325-0002.jpeg20190325-0003.jpeg20190325-0004.jpeg

Democrats na wanaomchukia Trump wameumbuka. Bado wapo katika hali ya kutotaka kukubaliana na ukweli.

It's time to move on.

FACTS ALWAYS. TRUTH MATTERS.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,037
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,037 2,000
RIPOTI YA AG W.BARR

AG Barr ametoa 'principle conclusion' kuhusu Ripoti ya Mueller
Kuna udanganyifu au kutoelewa tofauti ya Ripoti ya Barr na Ripoti ya Mueller

Kinachoonekana katika bandiko 765 siyo ripoti ya Mueller ni barua ya Barr kwenda congress
Kwa wafuatiliaji makini wiki hii kulikuwa na matukio mawili kuhusu ripoti ya Mueller

House ilipitisha kwa kura zote(420-0) kwamba ripoti ya Mueller iwekwe hadharani
Hii ni Republicans na Democrats wote katika house

Walichokihofia ndicho kilichotokea, kwamba watapewa summary ya maoni ya AG na si Mueller
Ukisoma taarifa ya AG kifungu cha kwanza cha ripoti yake anasema hivi '' Although my view is on going, I believe....'' Hapa anaeleza ni maoni yake kutokana na ripoti ambayo ni endelevu

Taarifa hiyo AG ametumia maneno 'I am au My'' akijihusisha na maoni yake mwenyewe

Maana yake ni nini? Kwamba, kwa mtazamo wake ambao si lazima uwe mtazamo wa mwingine kitaalamu kuhusu ripoti ya Mueller, na kwamba, mtazamo wake 'unaendelea'

Tukio la pili ni la kiongozi wa Dems katika seneti Bw Chuck akitaka taarifa iwekwe hadharani
Kiongozi wa Republicans McConnel amegoma na kuzuia hoja hiyo

Ukitazama kwa jicho pevu na weledi, taarifa ya W.Barr imepokewa kwa ubaridi na pande zote, Dems na Republicans kila upande ukichukua tahadhari kwani ni maoni ya Barr na si taarifa ya Mueller

WH haijapata taarifa kamili, furaha iliyopo kwa Rais Trump ni kumalizika kwa uchunguzi
Kwa kufuatilia tweet zake,'ushindi kama unaoonekana' angeupokea kwa kishindo kikubwa

Kila wachunguzi wa mambo wameonyesha wasi wasi kwani kilichotolewa ni ripoti ya Barr
Kinachotakiwa ni ripoti ya Mueller ambayo kila mmoja atajiridhisha kwa kusoma

Wasi wasi unazidi kutokana na Barr kushirikiana na wanasheria wa Trump kupinga uchunguzi wa Mueller kabla ya kuteuliwa kuwa AG

Kwa upande mwingine Democrats wanaonyesha wasi wasi kwa Barr na si ripoti ya Mueller

Kinachoendelea ni Barr, Mueller, Roseinstein kuitwa katika kamati za Bunge kufafanua
Hapo ndipo ripoti ya Mueller inaweza kuelezwa kwa undani na itabidi iwekwe hadharani

Labda kwa wasomaji niwakumbushe kuhusu sakata la Richmond ambapo AG alisimama Bungeni na kusema uchunguzi wa PCCB na vyombo vingine ulikuwa na 'principle conclusion' kwamba hakukuwa na deal. Huyu ni AG wa serikali kwa maoni yake
Ni kamati teule ndiyo iliyoibua kashfa nzima

Mfano huo ni katika kuelewa kuwa principle conclusion haielezi uchunguzi uliona nini
Wanachokitaka wamarekani ni kujua nini kilitokea katika uchaguzi

Soma taarifa kwa umakini kuna kifungu kimeeleza kuhusu Russia na sentensi zikaishia njiani

Hii haina maana kuwa AG atakuwa amepotosha, la hasha. Wingu la mashaka juu yake, na ukweli kuwa kilichotolewa ni tafsiri yake unazidisha hamasa ya kujua Mueller alisema nini

Na mwisho, ukisoma taarifa hiyo ipo kisheria zaidi ikieleza kuwa ilihitajika ushahidi usio na shaka juu ya mambo kadhaa, ikiwemo Russia collusion na kueleza nini maana ya collusion
Lakini pia ukifuatilia maelezo ya mwanzo kuna kauli zinazoshibana na maana aliyotoa

Siasa za viunga vya DC zina tahadhari zake, taarifa hiyo iwe iwavyo itatoka au kuvuja
Hilo limepelekea uangalifu sana katika kuipokea taarifa ya Barr, ya Mueller haijatolewa

Itaendelea.....
 
El Jefe

El Jefe

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2016
Messages
238
Points
500
El Jefe

El Jefe

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2016
238 500
Barua ambayo AG ametuma Congress pamoja na kuwemo maoni ya AG na Deputy AG, imebeba summary ya 'principle conclusions' zilizofikiwa na Special Counsel mwenyewe na matokeo ya uchunguzi wake.

Russia Collusion Hoax ni Case Closed:

Page no.2 ya barua, paragraph ya pili, AG ametoa nukuu (quotation) kutoka kwenye ripoti ya Muller kwamba "The investigation did not establish that members of the Trump campaign conspired or coordinated with the Russian government in its election interference activities."

Hapo bado wengine wanasema kwamba furaha ya Trump ni kumalizika kwa uchunguzi! au taarifa ya Barr imepokewa kwa ubaridi na Republicans! Ama kwamba hiyo ni summary ya maoni ya AG Barr! Kazi kweli!

Kwa wanaoelewa, case ya Russia Collusion imeshindwa chali! Hata Democrats wenye akili zao hawaizungumzii.

Tukumbushe tu, Russia collusion hoax imechunguzwa mara nne kuanzia ilipoanza, walichunguza FBI wakahitimisha kuwa hamna kitu, wakaja Senate na House Intelligence Committees nao hola!, akamalizia Mueller naye hajaona ushahidi! Bado wengine wanasema hayo ni maoni ya AG na Deputy AG!!!! Amazing!

Kuhusu Obstruction of Justice:

Special Counsel ameshindwa kufikia hitimisho kuwa kulikuwa na 'Obstruction' kwa sababu ya kile alichokiita "difficult issues" kwenye sheria.

Kwa sheria, kanuni, na sera za DOJ, katika case kama hiyo, AG ndo anatakiwa atoe hitimisho na yeye na Rod Rosenstein wamehitimisha kuwa hakuna ushahidi wa kutosheleza wa Trump kupatikana na hatia! Mueller ni "Special Counsel" na sio "Independent Counsel" ndio maana anaripoti DOJ.

Sasa kunakuwaje na Obstruction of Justice by the President wakati hata hakushiriki katika kosa lenyewe analotuhumiwa nalo? Democrats wanaoelewa wanajua hapo hamna kitu!

Ripoti ya Mueller kuwekwa hadharani:

AG Barr amezungumzia hili nalo kwenye barua yake kwenda Congress. Kwa sheria, kanuni na sera za DOJ kuna taarifa ambazo zipo kwenye ripoti ya Mueller ambazo haziwezi kuwekwa wazi kwa mfano taarifa za "grand jury" zilizo kwenye uchunguzi na mshtaka ya jinai, kuna baadhi ya "executive priviledges" na taarifa za watu ambao hawakupatikana na hatia kwenye uchunguzi ambazo lazima zilindwe.

AG Barr amesema atafanya kazi na Mueller ili kutambua hizo taarifa na ku-process ripoti ya Mueller na kuitoa hadharani kulingana na sheria, kanuni na sera za DOJ.

AG Barr anachofanya ni kufuata sheria inasemaje. Kumuita Congress kufafanua ni siasa tu!

Democrats wanachotaka sio ripoti ya Mueller iwekwe hadharani kana kwamba kuna kitu kimefichwa na AG Barr! Hapana!.Democrats wanachotaka ni kutafuta chochote kwenye ripoti ya Mueller cha kuanzishia uchunguzi mwingine dhidi ya Trump ili kumuondoa madarakani (impeachment)! Kwa sababu wamesema waziwazi! Na hili hata Mitch McConnell na Republicans wanalifahamu.

Democrats hawana "talking points" kwenye uchaguzi wa 2020 ukizingatia Trump amefanya vizuri kwenye indicators zote za uchumi wa U.S. na ashaanza kupata hela za kujengea ukuta kutoka Pentagon.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,037
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,037 2,000
TAARIFA YA BARR YAZIDI KULETA WASI WASI
MBINU ZA KUFUTA OBAMACARE NI KUPOTEZA HOJA

Taarifa ya AG Barr imeendelea kuleta mashaka makubwa kuliko ilivyokuwa
AG ameandika kwa maoni yake na tafsiri yake si maoni ya taarifa ya miaka 2 ya Mueller

Wasi wasi ni kutokana na maswali yanayojitokeza. Wachunguzi wa taarifa wamenyambua maneno 65 yaliyonukuliwa kutoka taarifa ya Mueller kwa summary ya page 4

Hoja ya kwamba itolewe hadharani inaungwa mkono na House Republicans waliopiga kura kwa 420-0. Hii inaeleza hakuna aliyetayari kukubali summary ya AG Barr

Rais Trump anasema WH haijaona taarifa nzima. Hata hivyo ni ngumu kwa mtu mwenye akili kukubali kauli zake. Hii haina maana hakuna atakayeamini, wapo

Taarifa ya Barr imepokewa kwa ubaridi sana na wakubwa wa DC wakichukua kila tahadhari

Trump anasema Taarifa ya Mueller kupitia AG imemsafisha kwamba hakuna collusion wala obstruction of justice.

Hapa tu pana uongo, ukiisoma taarifa bandiko la hapo juu inaeleza wazi Mueller hakuhitimisha kuhusu Obstruction of justice kwa njia yoyote kwa maana nzuri au mbaya

Ni Trump yule yule aliyesema uchunguzi ni Hoax na unafanywa na watu wasiopigiwa kura tena wakiwa Democrats n.k. Leo anasema Mueller ni ''honorable man''

Inaonekana Mueller ambaye yupo chini ya DOJ angeweza kusema kuna ''criminal act'' kwamfano tu, DOJ ilipaswa kufungua mashtaka. DOJ ina utaratibu wa kutomshstaki

Lakini pia kuna la kujiuliza kwanini WH inasema itatumia executive privilege kuzuia baadhi ya habari? Kimamtiki ingalikuwa vema taarifa ya Mueller ikawekwa hadharani ili kumsafisha Trump

AG Barr ametoa taarifa bila kuwasiliana na Mueller.
Kwanini hakuwasiliana na Mueller kabla ya kuandika barua.

Kisiasa taarifa ya Barr imetoa mistari inayotakiwa kwa ''maongezi'' hakuna collusion hakuna obstruction of justice. Hoja zinazotumiwa na Trump katika kushadidia hoja zake

WH inafahamu taarifa hiyo inaweza kuwa na mambo mengi yasiyotakiwa kujulikana kuhusiana na uchunguzi mzima. Kwa mantiki hiyo, badala ya kusherehekea taarifa mbinu imetafutwa

Mfano, kuna uwezekano taarifa nzima ililenga kuwa jukumu la uamuzi kwa congress akijua DOJ haiwezi kumshtaki Rais aliye madarakani

Kwa mantiki hiyo ikatafutwa mbinu
Kuna taarifa za Trump admin ikihusishwa na DOJ ya Barr wanataka kufuta Obamacare

Wanajua kisiasa maongezi ya taarifa ya Mueller yataisha na taarifa itakayobaki ni ya AG Barr
wanafahamu Obamacare itakuwa ''hot' na kubadili maongezi ili suala la Mueller lipotee

Mbinu hii ni nzuri sana kwa muda mfupi. Kwa Taifa la Marekani, taarifa zitavuja tu na suala zima litarudi na kuendelea kumsumbua Trump.

Hapa atakuwa na mambo mawili, ku deal na Obamacare iliyosababisha akapoteza House huku chururu chururu za Mueller zikiendelea kila siku

Kwa hali yoyote ile, taarifa ya Barr ni nzuri kwa muda mfupi, ni busara taarifa ya Mueller ingetolewa ili kumsaifisha au kuhangaika nayo.

Suala la Mueller na Russia litageuka kuwa taarifa ya Mueller iwekwe hadharani.

Tusemezane
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,037
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,037 2,000
AG BARR KATIKA 'PRESHA''
KUNA KITU KINAFICHWA, BARR AIKANA RIPOTI YAKE

Siku chache zilizopita tuliandika kuhusu barua ya AG Barr kwa Congress

Barua ililenga kumpa Rais Trump hoja ya kuzungumza bila kujua undani wake
Tulisema barua ilikuwa furaha ya muda, suala la Russia bado ni bichi na litaendelea kwa kasi

Rais Trump anakiri kutoisoma taarifa. Ikiwa ni kweli, wapi anaweza kusema taarifa hiyo imemsafisha 'vindicate and exonerate'? Kuna uwezekano kapenyezewa, hakuna uhakika

Habari ndani ya DC zinavuja. Inaeleweka taarifa ya Barr ilisema hakuna obstruction of justice

Hili linahojiwa kwani kabla ya uteuzi wa kuwa AG, William Barr aliandika memo ya kurasa 19 kwa DOJ akihoji suala la obstruction of justice kwamba halipo

Taarifa zinaeleza, Mueller alilirudisha suala hilo DOJ ili taarifa ikitoka congress ndiyo iamue
Mueller alifahamu DOJ haiwezi kumstaki Rais aliye madarakani

Viunga vya DC vikapata habari ya ukubwa wa taarifa wa Mueller.
AG Barr akalijibu bunge akisema anahitaji muda kwani taarifa ni ''substantial''.
Tayari akazua swali, ikiwa ni hivyo aliwezaje kufanya summary ya kurasa nne yenye maneno takribani 100

Shinikizo limezidi na kumlazimu AG Barr kuandika barua nyingine akisema taarifa itatoka katika wiki mbili zijazo.

Hilo likazua jingine, kwamba, kwanini afanye reductions inayolenga kuondoa makundi kama watoto wa Trump

Kubwa zaidi katika barua ya AG Barr ni ''kuikana' barua yake kama ilivyo katika bandiko 765

AG anasema taarifa ina kurasa 400 ambazo yeye ame 'summarize' kabla ya kukana

Barr anasema alichokiandika kwa congress ''siyo summary taarifa ya Mueller'' bali ni notifications kwa Congress, na asingeweza kutoa taarifa kwa vipande vipande''

Hili linafuatilia misleading information za Rais Trump akitambua katika ulimwengu huu kuna mazuzu watabeba kila kitu kama kilivyo pasi kutumia chembe ya akili.
Weledi waliliona mapema

Tumejadili awali, ikiwa hakuna ''there there' au hakuna kitu au hola, ni kwanini AG anajitahidi kuficha taarifa?

Kuna taarifa ya WH kutaka kutumia executive privilege kwa sasa wamemwachia Barr

Hakuna njia itakayoondoa suala la Russia katika mazungumzo ya kila siku isipokuwa kutoa taarifa ya Mueller nzima kama ilivyo.

Hilo halitatokea katika public kwani kuna sensitive information, hata hivyo congress ina haki kisheria kusoma taarifa isiyokuwa na reductions

Joto la siasa za DC limeanza na si kwamba linaendelea, media na watafiti watachimba na taarifa itavuja tu kwanini kuna jitihada za kuficha taarifa ya Mueller

Kuelekea uchaguzi mkuu, Barr anamtia Trump matatizoni.
Itagharimu kampeni ufafanuzi wa habari zinazovuja kila siku badala ya kufanya kampeni

Barr amempa 'headlines' Trump kwa muda, akimtia katika wakati mgumu kwa muda mrefu

Tusemezane
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,037
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,037 2,000
MUELLER AENDELEA KUMTESA TRUMP
JITIHADA ZA KUFICHA RIPOTI ZINAENDELEA

Ndani ya viunga vya Washington kuna yanayoendelea kuhusiana na ripoti ya Mueller

Hii ni baada ya barua ya AG Barr kwa congress aliyoita summary ya Mueller kabla ya kuikana

Barr anasema ile si taarifa kamili ni notifications ya nini kilichomo ndani ya taarifa ya Mueller
Anasema taarifa yake inaendelea kadri muda unavyosonga.

AG ambaye ni mpambe wa Rais Trump kwa maandishi yake kuhusu uchunguzi wa Russia alikumbana na nguvu ya DC kiasi cha kukubali kutoa taarifa ikiwa imehaririwa ndani ya wiki 2

Hilo halijazuia nguvu ya Democrats wanaomiliki kamati za House kumtaka leo afikishe taarifa kama ilivyo na siyo summary ya mawazo yake kwa kusoma taarifa ya Mueller au iliyohaririwa

Kamati ya Bunge imepiga kura kumruhusu mwenyekiti aitishe taarifa kisheria 'subpoena''

AG anaweza kupuuza hata hivyo suala litakwenda mahakamani.
Huu ni mgongano kati ya Branch mbili za kiutawala, Bunge na serikali na utaenda mahakamani

Taarifa inayomsafisha Trump sasa inafichwa hadi kufikiriwa kwenda mahakamani!

Rais Trump alisema taarifa iwekwe wazi hana cha kuhofia.
House ikapiga kura 420-0 kutolewa taarifa. AG Barr anang'ang'ania kuificha kwa kujua kilichomo

Trump kageuza kibao kama kawaida yake ya kudanganya akiweweseka kutaka taarifa isitolewe

Hapa ndipo tulisema ''ushindi' aliosema dhidi ya Mueller ulikuwa wa muda mfupi tu
Mateso na maumivu ya sasa ni makali akijua mwisho wa siku taarifa itatoka au itavuja

Kwa wanaofuatilia tulisema huko nyuma, si Republicans si wapambe wake wote walichukua tahadhari kuijadili barua ya kurasa nne ya Barr wakijua taarifa ya Mueller imebeba mengi mazito

Ni Trump peke yake aliyekuwa anaipigia upatu barua hiyo. Hilo si kwa bahati mbaya, anajua wapo wanaomeza tu ''hakuna kitu, hola, amesafishwa' bila kujua siasa za DC.

Kinachowasumbua wachunguzi ni jitihada za WH na DOJ kuficha taarifa inayosemwa imemsafisha Rais Trump. Ikiwa taarifa ni nzuri nini wanataka kuficha na kwanini?

Katika anga za DC taarifa ya Mueller ni mbichi kabisa na itaendelea kumtesa Trump kwa muda mrefu ujao. Zile tambo za wiki moja zimekwisha na sasa maumivu yamerudi pale pale, Russia!!

Harakati za kupotezea taarifa kwa kuchomeka Obamacare zimekumbana na upinzani kwa GOP

Maseneta na House rep hawataki kusikia Obamacare kwani ndiyo iliyopelekea kupoteza House kwa kiwango cha miaka 40 huku House ikimbana Trump kikamilifu kwa sasa

Rais Trump amekiri, Obamacare itakuwepo hadi 2020 atakapokuja na plan.
Kwasasa hana. Katika uzi huu tuliwahi kuhoji, ikowapi plana ya Health ya Trump?

Tulijua hana, alichonacho niudanganyifu. Obamacare inamtesa na amefunga hoja kwasasa

Hakuna shaka Trump atakuja na vituko vingine, lakini, ukweli unabaki pale pale taarifa ya Mueller imendelea kumtesa na hataki itoke huku akidai imemsafisha. Inamtesa sana

Njia nyepesi ni kuitoa tu watu waisome na kuendelea na maisha. Kuificha kunatengeneza vichwa vya habari na kufunika agenda zake. Hata hivyo, nani anajua kilichomo?

Tusemezane
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,037
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,037 2,000
RIPOTI YA MUELLER YACHIMBIWA DOJ
TRUMP AN'GAKA KUTOLEWA

Kitu kimoja watu wanachochanganyikiwa, Mueller siyo independent counselor ,anafanya kazi chini ya wizara ya sheria '' DOJ'. Taarifa yake inapelekwa DOJ kwa AG Barr

Barr alifanya fyongo baada ya kujivika madaraka ya kufanya 'summary' ya ripoti ya Mueller

Wachunguzi wanasema taarifa ya Mueller lazima ina executive summary iliyochujwa
Hiyo ndiyo inayotakiwa na si maoni ya Mueller ambayo wasiojua wameibeba kama ilivyo

Barr katika barua yake baada ya kukana si summary amejivika jukumu la kuamua kama hakuna obstruction of justice.

Taarifa ya Mueller inasema haikufikia hatima kama tendo hilo lilifanywa au halikufanywa kwa kuangalia sheria

Mueller aliacha suala hilo akijua kusema kuna obstruction of justice angejivika madaraka ya kuamuru Rais ashtakiwe. Akiwa mfanyakazi wa DOJ hilo si jukumu lake na si desturi ya DOJ

Muelller aliacha suala likielea kwa kutambua ni kazi ya congess kbaada ya kulitafakari taarifa

Presha ya DC inamkumba AG Barr ambaye anataka ripoti hiyo inyofolewe mambo manne

1. classified information, 2. intelligence, 3.grand jury na 4. kundi lililotajwa lakini halishtakiwa kwa maelezo ya kuwa habari zinaweza kufanya uharibifu ''damage' kwa kundi hilo

Kundi la wasioshtakiwa wanaotakiwa kuhifadhiwa ni Trump na Familia yake, kwamba, kuna habari chafu ingawa kisheria zinaweza kutokuwa kosa hata hivyo kijamii ni habari chafu

Huo ndio ugomvi wa AG Barr wa DOJ na Congress chini ya Democrats.

Congress ina haki ya kupata taarifa bila kuchujwa.

Dems kwa kuelewa mbinu hiyo chafu wamekataa hata lile kundi linalopata 'nyeti' za nchi ''gang of 8' lenye GOP 4 na Dems 4 lisipewe taarifa bali congress nzima

Mvumo huo unakisiwa na kura ya 420-0 ya house inayotaka taarifa iwekwe hadharani
Ndani ya seneti kuna ''uasi' dhidi ya Trump.
Maseneta kama Chuck (R) Iowa anataka taarifa hadharani

Dems wameshapitisha uamuzi wa kuitaka taarifa ya Mueller kisheria ''subpoena'

Hadi hapo mtinange wa Dems na DOJ unaonekana kwenda mahakamani, taarifa itoke

Rais Trump baada ya kudokezwa uchafu uliopo ndani ya taarifa sasa hataki itoke.
Donald anayewafanya watu katika political base yake waonekana wajinga na kwingine duniani

Ikiwa taarifa ilimsafisha kama anavyodai, nini kinamkwaza kuitoa hadharani?
Kwanini AG Barr amegoma kuitoa kama ilivyo?

Kwa taifa kama Marekani tayari taarifa zinavuja huku wasadizi wa Mueller katika uchunguzi wakionyeshwa kukerwa na taarifa au barua au summary ya Barr ilivyopotosha umma

Habari za Russiagate ni mbichi sana na zitamsumbua sana Trump kwa siku nyingi zijazo

Kwamba taarifa itatoka ni suala la muda. Joto analopata AG Barr na kuvuja kwa taarifa zitamlazimu akubaliane na hali, itoke taarifa na madudu yaonekana hadharani

Siasa za viunga vya DC hazitaki ushabiki au kusoma headlines, zinahitaji weledi

Tusemezane
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,037
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,037 2,000
WAANDISHI WA HABARI WALIKUWA SAHIHI
JITIHADA ZA KUFUNIKA UCHAFU WA RUSSIA ZAENDELEA

Waandishi wa habari wa mataifa makubwa hufanya kazi zao kiuchunguzi na kitalaamu
Ukiwatazama nafasi zao na taalamu utaona kitu kimoja, weledi wa taaluma na uandishi

Suala la Russia halikuwa la kupandikiza. Ni suala lililokuwa na ukweli ndani yake
Summary ya AG Barr ilionekana kama kuwasuta hata waandishi kupigwa na mshangao

Mshangao wao si kuhusu Russia collusion au obstruction of justice, ni kutokana na summary ya AG Barr ilivyobeba maneno yake na kuwa ya Mueller. Walitambua lipo jambo

Muda unavyokwenda inazidi kubainika AG Barr anajitahdi kuficha uchafu wa Rais kwa kila mbinu
Hilo nalo linazidisha hamasa ya kujua nini kinafichwa na kwanini

Leo Barr alikuwa na mahojiano ya kawaida ya mambo anuai na kamati ya Bunge
Katika maongezi, AG alishindwa kujibu swali rahisi ikiwa taarifa ya Mueller imeshafika WH

Hilo tu linajenga mashaka kuhusu DOJ kushirikiana na WH kabla ya taarifa kufika congress

Kwa upande mwingine AG amekataa kushirikiana na Dems kupata ridhaa ya mahakama kuhusu grand jury. Barr anajua mahakama itaruhusu na taarifa ya Mueller itakuwa wazi

Barr amekiri, ile summary ya kurasa nne hakushirikiana na Mueller.
Imebainika kutoka vyanzo kuwa Mueller hakutaka kutia mkono katika summary Barr

Mueller alichelea kuunga mkono summary akijua taarifa yake imebeba uchafu mzito

Kuna taarifa Mueller aliandika summary, haijulikani kwanini Barr hakuitumia

Rais Trump ana ng'aka taarifa isiwekwe hadharani kinyume na kauli zake hahofii lolote

Na kwamba taarifa iliyomsafisha sasa hataki itoke hadharani bali kuaminisha tu umma
Kwa Marekani hilo ni ufumbuzi wa mud, suala zima litamwandama sana

Dems wanasema watatumia sheria kuipata taarifa hiyo na hawakubali iliyonyofolewa na Barr kwa kushirikiana na wanasheria wa Trump na WH. Suala linalekea mahakamani

Matumaini ya Trump ni kuwa ndani ya supreme court kuna watu wake kama Jaji Kavanaugh
Well, matumaini hayo ni mazuri na ya muda mfupi. Bila taarifa hili litakuwa donda mgongoni

Kuna uchafu mzito wa Trump na ni wa kutisha unaofichwa kutoka taarifa ya Mueller.

Trump alifanikiwa kwa siku chache kuwahadaa wahadaika wake, tulisema suala ni bichi
Leo Trump baada ya kuisoma taarifa anayosema imemsafisha hataki kata kata itoke hadharani

Siasa za viunga vya DC hazihitaji papara,picha au copy and paste au kutupiwa mifupa na kuifkamia bila chembe ya fikra bila kuitazama DC kwa kina na ukubwa wake

Tusemezane
 
TUJITEGEMEE

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Messages
13,713
Points
2,000
TUJITEGEMEE

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2010
13,713 2,000
WAANDISHI WA HABARI WALIKUWA SAHIHI
JITIHADA ZA KUFUNIKA UCHAFU WA RUSSIA ZAENDELEA

Waandishi wa habari wa mataifa makubwa hufanya kazi zao kiuchunguzi na kitalaamu
Ukiwatazama nafasi zao na taalamu utaona kitu kimoja, weledi wa taaluma na uandishi

Suala la Russia halikuwa la kupandikiza. Ni suala lililokuwa na ukweli ndani yake
Summary ya AG Barr ilionekana kama kuwasuta hata waandishi kupigwa na mshangao

Mshangao wao si kuhusu Russia collusion au obstruction of justice, ni kutokana na summary ya AG Barr ilivyobeba maneno yake na kuwa ya Mueller. Walitambua lipo jambo

Muda unavyokwenda inazidi kubainika AG Barr anajitahdi kuficha uchafu wa Rais kwa kila mbinu
Hilo nalo linazidisha hamasa ya kujua nini kinafichwa na kwanini

Leo Barr alikuwa na mahojiano ya kawaida ya mambo anuai na kamati ya Bunge
Katika maongezi, AG alishindwa kujibu swali rahisi ikiwa taarifa ya Mueller imeshafika WH

Hilo tu linajenga mashaka kuhusu DOJ kushirikiana na WH kabla ya taarifa kufika congress

Kwa upande mwingine AG amekataa kushirikiana na Dems kupata ridhaa ya mahakama kuhusu grand jury. Barr anajua mahakama itaruhusu na taarifa ya Mueller itakuwa wazi

Barr amekiri, ile summary ya kurasa nne hakushirikiana na Mueller.
Imebainika kutoka vyanzo kuwa Mueller hakutaka kutia mkono katika summary Barr

Mueller alichelea kuunga mkono summary akijua taarifa yake imebeba uchafu mzito

Kuna taarifa Mueller aliandika summary, haijulikani kwanini Barr hakuitumia

Rais Trump ana ng'aka taarifa isiwekwe hadharani kinyume na kauli zake hahofii lolote

Na kwamba taarifa iliyomsafisha sasa hataki itoke hadharani bali kuaminisha tu umma
Kwa Marekani hilo ni ufumbuzi wa mud, suala zima litamwandama sana

Dems wanasema watatumia sheria kuipata taarifa hiyo na hawakubali iliyonyofolewa na Barr kwa kushirikiana na wanasheria wa Trump na WH. Suala linalekea mahakamani

Matumaini ya Trump ni kuwa ndani ya supreme court kuna watu wake kama Jaji Kavanaugh
Well, matumaini hayo ni mazuri na ya muda mfupi. Bila taarifa hili litakuwa donda mgongoni

Kuna uchafu mzito wa Trump na ni wa kutisha unaofichwa kutoka taarifa ya Mueller.

Trump alifanikiwa kwa siku chache kuwahadaa wahadaika wake, tulisema suala ni bichi
Leo Trump baada ya kuisoma taarifa anayosema imemsafisha hataki kata kata itoke hadharani

Siasa za viunga vya DC hazihitaji papara,picha au copy and paste au kutupiwa mifupa na kuifkamia bila chembe ya fikra bila kuitazama DC kwa kina na ukubwa wake

Tusemezane
Tusikimbiane, Mkuu, hapo baadaye
===
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,037
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,037 2,000
VIUNGANI DC NA SIASA ZA SIKU
TRUMP AMGEUKA MUELLER, MASHAMBULIZI YAANZA
AG BARR ATOA NENO, AJARIBU KULIMEZA

DC ni nzito zinazohitaji weledi zaidi ya vichwa vya habari
Rais Trump alisema Mueller na taarifa yake imemsafisha'' vindicate and exonerate''

Tulisema ''the devil is in the details'' kwamba, maelezo nyeti yapo ndani ya maandiko
Jana AG Barr aliulizwa na kamati ya house ikiwa WH wana taarifa ya Mueller

AG Barr alishindwa kusema, ndiyo au hapana. Maana yake ni kuwa WH ina taarifa ya Mueller

Kutokana na hilo Rais Trump na Wapambe wake walikurupuka bila kujua taarifa ina nini

Sasa wameisoma taarifa na uchafu wake kazi mpya ya kumshambulia Mueller imeanza

Taarifa iliyomu 'exonerate and vindicate' akiita golden standard anaiona shubiri kwa uchungu

Tunarudi pale pale, wapambe na wafuasi wake wanaelekea Trump anapotaka bila kujijua

Ameigeuka taarifa kuwe kwa hadharani, sasa hataki kumsikia tena Mueller, yule aliyemsafisha.

AG Barr aliyeandika summary ya kumsafisha Trump anajikuta katika joto na mizigo mizito ya Trump kila uchao. Jana alikuwa na kikao na kamati ya House ya appropriation
Leo akiwa na kamati ya seneti, alitoa neno linalotikisa viunga vya DC

Kumbuka mahojiano na kamati ni ya kawaida ya kikazi.
Kauli yake kuwa kulikuwa na ''spying' wakati wa kampeni imeingia nyongo.
Kama ilivyokuwa kwa summary yake , Barr alikimbia kukana kauli na kusema ''surveillance''

Hili si jambo geni. Kwanza, neno spy halikupaswa kutamkwa na AG.
Neno hilo limejadiliwa sana wakati Trump akitoa tuhuma hizo dhidi ya utawala wa Obama.

Neno hilo si sahihi kwa maana yake halisi.
Serikali haiwezi kufanya 'spy' dhidi ya wananchi wake bali kwa maadui wa nje

Neno surveillance alilotumia baada ya kubaini neno spy linamweka matatani nalo halina maana.

Aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya House Bw Nunes aliandika ''memo'' akishadidia maneno ya Trump kwamba, survaillance au spying ilifanyika

Uchunguzi uliofanywa na DOJ chini ya Trump haukuona tatizo.

Kwamba, taratibu zote ikiwemo kuomba ridhaa ya Majaji zilifuatwa na kulikuwa na sababu za kiusalama kufanya hivyo. Suzana Rice, mshauri wa Obama aliitwa na hoja ikafia hapo hapo

Kuliendekeza suala hilo ni kurudisha suala la Russia mezani na kuialika taarifa ya Mueller.

Kwamba, je, kulikuwa na uhusiano wowote wa surveillance na taarifa ya Mueller?

AG Barr , mpambe mzuri wa Trump ameongopa kwamba kampeni ya Trump hakujulishwa kuhusu hilo. Rekodi zinaonyesha kampeni ilionywa kuhusu kuingiliwa na Russia na Rais Trump alipewa taarifa rasmi siku anaingia WH.

Kauli za AG Barr zitazua kizazaa mbeleni. Alipoulizwa ikiwa ana ushahidi, Barr alisema '' anadhani''. Ni dhani hiyo hiyo ndiyo iliyounda kamati ya forgery ya kura ambayo imekufa bila matokeo. Iliongozwa na Mike Pence, na ndiyo ile ya Nunes iliyokufa kifo cha ghafla

Wakati Barr akibabaika, wiki hii atatoa taarifa iliyohaririwa inayotiliwa shaka sana kwa kuzingatia jinsi anavyojichanganya na kupoteza integrity. Taarifa ya Mueller itaitwa kisheria ''subpoena'

Ni ima aitoe au waende mahakamani wanakomtegemea yule Jaji Kavanaugh

Kujichanganya na mashambulizi ya Trump kwa Mueller yanaeleza kitu kimoja, taarifa ya Mueller imebeba uchafu mzito wa Trump. Ni upi huo? Ni sualala muda katika viunga vya DC

Tusemezane
 
TUJITEGEMEE

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Messages
13,713
Points
2,000
TUJITEGEMEE

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2010
13,713 2,000
pole sana @TUJITEGEMEE na nawatakia kila la heri wachangiaji wote... Tuko pamoja...
Ha haa..! Tupeane pole wote, maana kukatiza likizo kwa dharura hii si jambo dogo. Karibu.
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,037
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,037 2,000
RIPOTI YA MUELLER ILIYOHARIRIWA KUTOLEWA
AG BARR AGEUKA KUWA MWANASHERIA WA TRUMP
MBINU KALI ZA KUFICHA UOZO, DOJ NA WH KITU KIMOJA

SEHEMU YA I

Siasa za viunga vikuu vya DC ni za kiwango cha juu sana kinachohitaji kuvuta pumzi
Kila kinachofanyika kina maana lakini pia kinachunguzwa kwa kina na vina

Ile taarifa iliyohaririwa ya Mueller inatarajiwa kutolewa Alhamis na AG Barr
Kama tulivyowahi kueleza huko nyuma, hakuna siri Washington DC

Wiki tatu zilizokwisha AG alisema taarifa ya Mueller haitaonwa na WH kabla ya Congress(Bunge). Wiki mbili zilizokwisha alipoulizwa akagoma kusema kama ameitoa WH au la

AG Barr amechukua jukumu la kuwa wakili wa Trump na si mwanasheria wa US
Wiki tatu zilizopita Barr alitoa summary (bandiko 765 hapo) juu akidokoa mambo mawili tu
1. Hakuna collusion 2. Hakukuwa na hitimisho la obstruction of justice, akaamua haikuwepo

Barr alifanya hivyo makusudi ili kumpa Trump na wafuasi wake neno la kusema na kubadili mtazamo wa suala zima. Trump amejipigia debe kwa wiki tatu, muda mzuri tu wa kudanganya

Kuhariri ripoti hakuhitaji wiki tatu kwani ripoti yenyewe ilikuwa na executive summary
Barr alijua alichokuwa anafanya, kumpa Trump neno

Wiki hii mawakili wa Rais Trump walisema wameandaa ripoti ya kujibu mapigo ya Mueller

Hata kabla ya taarifa wao tayari walikuwa na ufahamu wa taarifa
Ni kwa msingi huo Barr alipoulizwa na kamati ya Bunge hakukubali wala kukanusha

Inajulikana sasa yalikuwepo mawasiliano kati ya AG Barr na Wanasheria wa Trump kuona nini cha kuondoa nini cha kuacha. Hilo linaikana kauli ya Barr kuwa WH haitaona taarifa kabla ya Congress

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Rais Trump leo amesema taarifa iliyohaririwa itakuwa na mambo mazito. Akatangaza kuwa AG atakuwa na mkutano Alhamisi saa 3.30 asubuhi

Hili tu likaonyesha mawasiliano makubwa kati ya AG na WH ambayo Trump anayajua
DOJ ya Barr haipangiwi muda, vipi Trump alijua yote hayo hata kabla ya media?

Siku ya Alhamisi imechaguliwa makusudi kwa kujua Ijumaa hakuna kazi hivyo vyombo vya habari havitakuwa na muda wa kuongelea.AG Barr alielekezwa na WH nini cha kufanya

AG anataka kuitangaza taarifa kwa kuieleza saa 3.30 asubuhi na taarifa iliyohaririwa itapatikana saa 6 mchana. Hili nalo linafanyika kwa makusudi kabisa

Kwamba, wakati anatoa taarifa waandishi watakuwa hawajasoma taarifa hivyo watajadili anachosema yeye na kuwa ndiyo habari na si kile kilicho katika taarifa iliyohaririwa

Yote hayo yanafanyika kuhakikisha kuwa taarifa na uchafu wa Trump unafichwa

Kwa hali yoyote credibility ya AG ipo njia panda. Hata hivyo, Barr na WH wanajua si wote watang'amua, yapo mazuzu yatakayobeba kila kitu na kuanza kupiga debe

Ndivyo walivyofanya katika summary inayosomeka bandiko 765 ambayo baada ya moto kuwaka AG Barr kasema si summary ni maoni yake huku akiacha uzezeta ukiendelea kutamalaki

Kwanini AG awasomoe Wamarekani taarifa tena iliyohaririwa?
Habari zimevuja kuwa suala la obstruction of justice limefichwa kwani ni hatari kwa WH

Inaendelea.....
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,037
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,037 2,000
SEHEMU YA II
Kamati zote za Bunge zimetoa kauli ya pamoja ya kumtaka Barr aahirishe taarifa ili watu wapate muda wa kuisoma kwanza, na si kueleza maoni yake kama president's defense lawyer

Billy Barr tayari ameongeza mafuta katika moto unaowaka. Kwamba, anachochea taarifa ya Mueller ipelekwe Bungeni kwa njia ya kisheria au wito wa lazima ''subpoena''

AG atakataa lakini kutakuwa na hoja mbili kubwa zitakazo mwandama
1. Bunge lina haki ya kuona taarifa isiyohaririwa, ni kifungu gani atatumia kuzuia hilo?
2. Kisiasa, kuna shauku ya kujua ni kwanini kuna jitihada za kuficha taarifa ikiwa Rais Trump alisema taarifa imemsaifisha? Nini kinachoogopwa kwa taarifa kuonwa na Bunge

Kwa mwendo wa ''spinning' zinazofanyika, ndani ya DC tayari mambo yanatoka hadharani
Inajulikana kwanini obstruction of justice inataka kufichwa na Mueller alisema nini

Habari zote zinazoandikwa na magazeti zilijulikana kilichokuwa kinasubiriwa ni 'timing'
Leo Barr amepata surprise kusikia vikao vyake na wanasheria wa Trump vinajulikana
Kapata mshangao taarifa anayotaka kuficha ni ipi na kwasababu gani

Kesho kitakachotolewa ni kile AG Barr na WH wanataka wananchi wasikie
Huu ni mkakati mbovu sana, utakuwa kama bazoka inayoisha utamu kwa muda mfupi

Kwa muda mrefu suala litamtesa sana Rais Trump. Kutakuwa na drip drop za taarifa ya Mueller kila uchao. Kuelekea uchaguzi mkuu kisiasa ni tatizo kubwa. Trump itabidi ajibu kwa mantiki na kila jibu litakuwa na swali. Hivyo, suala la kuhariri taarifa ni dawa ya kutuliza maumivu si tiba

Email na Benghaz zilimwandama H.Clinton mwanzo mwisho. Hili la Mueller ni kubwa zaidi

Watu wakumbuke kuwa anachoeleza Rais Trump kuhusu collusion si kweli
Mueller alichunguza Russia kuingilia uchaguzi (interference) na ushiriki (conspiracy)
Halafu kuna obstruction of justice

Halafu kuna suala la collusion. Neno collusion halina maana uhalifu. Mueller anasema ''investigation did not establish the collusion between campaign and Russia''

Maneno hayo hayana maana hakuna collusion. Inawezekana ilikuwa ilikuwepo, lakini je, ni unaweza kumshtaki mtu kisheria kama uhalifu?

Mwisho, Mueller anasema '' obstruction of justice'' hakuweza kufikia tamati kama alifanya au hakufanya.

Haina maana hakufanya, kuna sababu za kuliacha suala hilo pengine liamuliwe na congress
Trump anasema taarifa imesema hakufanya!!!

Hadi taarifa nzima itakapoonwa na watu zaidi ya DOJ, AG Barr atawalisha watu matango pori siku ya kesho.

Swali linaloulizwa tena na tena, ikiwa hakukuwa na uhalifu kwanini kunajitihada za kuificha taarifa hata kwa congress?

Tusemezane
 
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Messages
10,217
Points
2,000
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined May 31, 2008
10,217 2,000
Ha haa..! Tupeane pole wote, maana kukatiza likizo kwa dharura hii si jambo dogo. Karibu.
TUJITEGEMEE, wakati tunasubiri vituko vya AG wa Marekani kuhusu ripoti ya Mueller, naomba mawazo yako kuhusu msimamo wa Fox News kulingana na hii video...


Hiyo ndiyo FOX NEWS unayoisifia...huwezi kuamini wanayemsema hapa ni Obama, tazama hapa chini...

 
El Jefe

El Jefe

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2016
Messages
238
Points
500
El Jefe

El Jefe

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2016
238 500
Kuna watu wanaongozwa na hisia zaidi kuliko FACTS kwenye suala zima la kutolewa ripoti ya Mueller. Kwa sababu mtu hajamsikiliza Bill Barr anasemaje tayari ameshaandika atachokisema au atakachokimaanisha!! Amazing!

Kwa mfano, kusema kwamba suala la 'Obstruction of Justice' Mueller aliliachia Congress liamue sio kweli!! imeandikwa wapi? Kwa sheria na kanuni zipi za DOJ?

Kusema kwamba Bill Barr anaficha taarifa sio kweli!! Ametoa redacted version kwa ajili ya umma na Congress na ameelezea sababu labda mtu useme hujamuelewa na makundi manne ya taarifa zilizoondolewa! Lakini pia atawapa 'Congress' (sio umma) unredacted version isio na grand jury material peke yake! Kwa maana hiyo hata Congress hawaruhusiwi kuona material za grand jury! Ni muhimu watu waelewe sababu!

White House wameacha Executive privileges kwenye taarifa ya Mueller ingawa Trump ana haki ya ku-invoke hilo na kuzidi kupunguza taarifa ya Mueller inayotakiwa kwenda Congress na kwa umma! Lakini kwanini hawajafanya hivyo kama lengo lao ni kuficha yaliyomo?

Barr anachokifanya ni kufuata sheria na kanuni za DOJ, asipozifuata haohao Democrats ndio watakuwa wa kwanza kumtaka aondoke kwenye nafasi yake kwa kushindwa kufuata sheria na kanuni za DOJ.

Hivi AG alishe watu matango pori ili iweje wakati ripoti ya kurasa zaidi ya 400 ameitoa kwa umma? Hivi hiyo ni akili kweli? Yaani adanganye wananchi halafu awape ripoti wasome, kwani wamarekani ni wajinga baada ya kusoma ripoti wenyewe washindwe kujua kuwa AG aliwadanganya? AG akidanganya hiyo kazi atabaki nayo kweli? Hebu tuwe tunafikiri kwanza!

Kudai kwamba amekosea kuongea na waandishi wa habari, kwanini asiongee nao? Kwanini awasilishe kimyakimya? Kwanini hiyo ripoti ya Mueller ilipelekwa kwake na si Congress? Ana prerogatives zake na mamlaka kama AG wa US! Kwa mfano, kikanuni anatakiwa atoe uamuzi kama suala limemshinda Independent Counsel kama suala la Obstruction of Justice ! Kwanini asitoe wakati anaruhusiwa kisheria? Kwanini aogope kutekeleza majukumu yake?

Barr amesema ataenda kwenye kamati za Judiciary za House na Senate kwa ajili ya kutoa ushuhuda! Wale wanaoshindwa kumuelewa wafuatilie ili waje wamuelewe vizuri atakapoenda kuzungumza kwenye hizo kamati! Lakini pia amesema atamruhusu Mueller (ambaye bado ni muajiriwa wa DOJ) kwenda kutoa ushuhuda kwenye hizo kamati!

Tatizo kuna watu humu wakishajua msimamo wa Democrats ni upi basi na wenyewe wanafuata hukohuko bila kupima ili kusimamia ukweli! Mwisho wa siku wanatoa maoni ya Democrats\Liberals na sio maoni yao binafsi! Dems wakiingia chaka na wenyewe chaka, visingizio watavyokuja nazo Dems ndio hizohizo wanakuja nazo na wao! What happened to reasoning?realdonaldtrump-20190418-0001.jpeg
 

Forum statistics

Threads 1,285,934
Members 494,834
Posts 30,879,420
Top