Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

TUJITEGEMEE, ngoja nikusaidie kidogo, mashtaka makuu mawili kwa Roger Stone ni kusema uongo na kuwatisha mashahidi. Mfano mojawapo ni huu hapa chini...

While the indictment provides some new insight into the Trump campaign, it deals largely with what prosecutors say were Stone’s false statements about his conversations with conservative writer and conspiracy theorist, Jerome Corsi, and New York radio host, Randy Credico.

The indictment accuses Stone of carrying out a “prolonged effort” to keep Credico from contradicting his testimony before the House intelligence committee. During that effort, prosecutors note that Stone repeatedly told Credico to “do a ‘Frank Pentangeli,'” a reference to a character in “The Godfather: Part II” who lies before Congress.

Stone is also accused of threatening Credico, including through messages in which he called him “rat” and “stoolie” and accused him of backstabbing his friends. Stone also threatened to “take that dog away from you,” a reference to Credico’s dog, Bianca.

“I am so ready. Let’s get it on. Prepare to die (expletive),” Stone also wrote to Credico.
 
Pole ndugu yangu TUJITEGEMEE...Russian collusion inaingiaje hapa? Je unajua Roger Stone anashtakiwa kwa makosa gani? Je unajua masharti ya dhamana aliyopewa?
Shukrani Mkuu kwa maswali yako. Kwa mujibu wa mtandao wa BBC nanukuu sehemu ya taarifa kutoka mtandao huo kama majibu ya maswali yako. Karibu.
=====

What exactly is Stone charged with?
- - -
The special counsel has accused Mr Stone of attempting to obstruct the investigation into Russian meddling by:

Lying to the House Intelligence Committee about what transpired between him and Wikileaks

Lying to the committee about records of his interactions with Wikileaks

Witness tampering, for trying to keep his Wikileaks intermediary from telling the truth to Congress
**[
The indictment does not say Mr Stone committed any criminal activity during the election.

How did Roger Stone respond?
- - -
He was released on a $250,000 (£189,000) bond, but with restrictions allowing him to travel only for court appearances in Florida, Washington DC and New York.

After his court appearance, Mr Stone spoke on the phone to conspiracy theorist Alex Jones on his radio programme Infowars.

"I intend to fight for my life," Mr Stone said as he launched a fundraiser for his legal battle. "There's no circumstance under which I would plead guilty to these charges.
"There's no circumstance under which I would bear false witness to the president."
He added: "Once again, there is no evidence of Russian collusion, Wikileaks collaboration and I'm not charged with doing anything inappropriate or illegal to assist in his [Mr Trump's] election."
***
Mr Stone then emerged from court grinning broadly while flashing a Nixonian double V-sign and wearing a blue Ralph Lauren polo shirt.
 
"I intend to fight for my life," Mr Stone said as he launched a fundraiser for his legal battle. "There's no circumstance under which I would plead guilty to these charges.
"There's no circumstance under which I would bear false witness to the president."
He added: "Once again, there is no evidence of Russian collusion, Wikileaks collaboration and I'm not charged with doing anything inappropriate or illegal to assist in his [Mr Trump's] election."
Sasa kulingana na source zako (RT?) unadhani kwa nini alivamiwa usiku na FBI na kuchukuliwa akiwa tu na nguo zake za kulala? Ushahidi alio nao Mueller hakuna anayeujua nje ya ofisi yake...
 
Mag3 :Source ilikuwa RT lakini facts check nimeifanya kwa kutumia source ya BBC. Hivyo majibu yangu ni nukuu ya moja kwa moja kutoka BBC.
===
Sasa kama ushahidi huyo Muller hataki kuutoa nje ya ofisi yake (labda anaona utamuumbua), basi hakuna namna inabidi tuwaamini watuhumiwa akina Stone na wenzake!!
 

nixon-jpg.1005030

Richard Nixon akitoka Ikulu mwaka 1974!

stone-jpg.1005032

Roger Stone akitoka Mahakamani mwaka 2019!
tattoo-jpg.1005043

Roger Stone akionesha tattoo ya Richard Nixon mgongoni!
Kweli historia haikuangushi!​
 
SIASA ZA VIUNGA VYA DC
GOV SHUTDOWN YAISHA, TRUMP 'APINDA'
ROGER STONE AINGIA 18, MUELLER SASA YUPO WH

Kufungwa kwa serikali kutokana na mkwamo wa bajeti kumekwisha baada ya Rais Trump kukubali kufungua serikali bila masharti yoyote. Hayo yametokea siku 34 baada ya Trump kuweka ngumu kwa 'offer hiyo'

Rais Trump huko nyuma alimshambulia sana Spika Nancy Pelosi kama 'public enemy'.
Pelosi akajenga kampeni iliyompa House na kuwa Spika akimpa tabu Trump katika kuburuza Wamerekani

Trump amefungua serikali bila senti ya 'wall'' akionekana kupinda bila masharti licha ya nguvu za wahafidhina

Jana kulikuwa na kura za miswada miwili ya GOP uliopata 50 kwa 47 na wa Dem uliopa zaidi ya hapo
Hii ilionyesha GOP wanamegeuka na kuungana na Dems na nguvu ya Trump inapungua

Kumbuka, Rais anaweza ku veto mswada , hata hivyo super majority ya 60 inazuia nguvu hiyo

Nancy Pelosi alimwekea ngumu Trump kuhutubia mabunge 'state of the union'

Kulegea kwa Trump kunachagizwa na mambo kadhaa hata kuwaacha wachambuzi midomo wazi

1. Kauli ya Trump kuwa atawajibika kwa kufunga serikali inamrudi kwani alikubali 'ndiye mmiliki wa shutdown'
2. Kuzuiwa kuhutubia state of the union kulimnyima uwanja wa 'kupika' propaganda dhidi ya Dems
3. Kura za maoni zinaonyesha kumomonyoka kwa wafuasi hata independents
4. Maseneta wa Republicans wanahofia ile 'blue wave' inaweza kuwasomba miaka 2 ijayo
5. Trump anaona senate ikiunga mkono Dems hatakuwa na ushawishi siku za mbeleni
6. Lakini wachambuzi wanasema ' kushtakiwa kwa mshirika wake' Roger Stone amekutumia kubadilisha mazungumzo yanayotokana na shutdown

Roger Stone Mshirika wa siku nyingi wa Trump alikamatwa mapema alfajiri na kushtakiwa kwa makosa kadhaa

Katika makosa hayo hakuna kosa la 'collusion' kama hati ya mashtaka inavyoeleza

Hata hivyo, Roger alikuwa ashtakiwe siku nyingi na haieleweki nini mkakati wa Mueller.

Roger ni kiungo kati yake na Wikileaks yenye mahusiano na makachero wa Russia mmoja akiwa ''Gucifer 2''

Kauli za Trump siku za nyuma kuhusu Wikileaks, emails za Dems na Clinton na hasa alivyozitoa ilionyesha uwepo wa mahusiano kati ya Wikileaks, Roger Stone na Trump campaign ambao haukuwa wa moja kwa moja

Mtu anayeongelewa kuwa kiungo ni Roger Stone. Kushtakiwa kwake hakuonyeshi jambo jipya lakini kunaeleza kitu. Moja ya mambo yaliyoainishwa ni mahusiano yake na Wikileaks na mawasiliano akipokea maagizo kutoka 'senior campaign official' wa Trump. Afisa huyo ndiye akitoa maelekezo kwa Wikileaks

Hakuna anayemjua afisa mwandamizi. Lugha ya Mueller ni ya kitaalamu inayowaacha wachambuzi na maswali.

Kwa mfano, wiki iliyopita mtandao wa Buzz-feed ulisema Trump alimzuia Cohen asitoe ushahidi

Habari hizo zilileta taharuki kwani ilikuwa ni obstruction of justice tena kwa congress.

Mchunguzi Mueller katika hali isiyo ya kawaida akatoa taarifa za 'kanusho' akisema taarifa haikuwa ''accurate'.
Lugha iliwaacha wachambuzi hoi kwani 'accurate' haina maana ni false

Wapo wanaojiuliza mbona 'hakuna collusion''? Well, watu waelewe suala linalomhusu Rais wa US ni nyeti

Mueller anahabari ambazo watu huzipata miezi kadhaa baada ya yeye kuzifanyia kazi

Taratibu alianza kukamata 'vidagaa' akisogea kwa uangalifu ndani ya DC, sasa yupo katika viunga vya WH akielekea oval office. Ni kosa kusema Mueller ana kitu au hana kitu

Pamoja na hayo, kwa jinsi alivyodaka washirika 16 wa Rais Trump wengi waki 'flip' na kiwewe cha Rais Trump ni wazi kuna jambo. Je, ni collusion? Je, ni Rais kuwa wakala wa mataifa?

Je, kuna uhalifu wa shughuli zinazomhusu Rais? Je, kuna uhusiano gani kati ya Russia na uchaguzi wa US? Kwanini Trump anawagwaya Russia kiasi cha kutosa vyombo vya nchi yake na hata washirika wa NATO?

Taarifa ya Mueller itaeleza na si suala la collusion tu. Ikumbukwe, Trump alianza kukana kila kitu, sasa hana cha kukana bali kusema 'je huo ni uhalifu'? Mpiga debe mkubwa ni Rudi Giullian ambaye kila uchao ana hadithi mpya

Tusemezane
 
SIASA ZA VIUNGA VYA DC KWA WIKI KADHAA

RAIS TRUMP ASALIM AMRI KWA HOUSE
MUELLER NA UCHUNGUZI, KIZUNGUMKUTI WH

Sakata la ujenzi wa ukuta 'wall' lilolazimu serikali kufunga shughuli limechukua sura mpya
Serikali haitafungwa, fungu lililotengwa kwa 'wall' ni ''dollar chini ya bilioni 2''

Trump ameshindwa suala zima la ukuta ambalo alilodai Mexico watalipa wakati wa kampeni. Trump hakuweza kutumia House na Senate chini ya GOP

House ilipochukuliwa na Dems, machungu ya kupoteza midterm yalititia kikamilifu WH
Si suala la bajeti tu bali chunguzi lukuki zinazomwandama katika taasisi nyingi

Rais Trump atatumia mfuko wa 'emergency' jambo linalochukua mkondo wa kisheria

Republicans wana hofu, executive order ikitumiwa vibaya ipo siku Rais wa Dem ataitumia hawatakuwa na hoja. Katika hili la exec order Trump alimtuhumu Obama na sasa linamrudi

Kinachomsumbua Trump si ukuta kama dharura,ni ahadi aliyozotoa. Obamacare ipo licha ya hujuma. Ukuta haujengeki licha ya madai ya Mexico kulipa kisha na sasa ni walipa kodi US

Hayo yakiendelea, mazonge zonge mengine yanaendelea kimya kimya ingawa ni kwa nguvu

MUELLER
Katika wiki mbili kumekuwepo na maendeleo yasiyoonekana kuwa tishio kwa haraka.

Kwa undani hali ya uchunguzi inachukua sura mpya kabisa na sasa ipo katika kitovu cha WH

Ili kuelewa nini kinaendelea, tutaweka mtiririko wa matukio kisha kuhitimisha ili kupata ujumla

Tunaanza na Paul Manafort

Inaendelea......
 
MUELLER AKIMWENDEA KOMBO MANAFORT NA STONES

Kwa muda mrefu washirika wa Trump wa kampeni wameshtakiwa kwa kusema uongo.

Hakuna aliyeshtakiwa kwa kosa la ''collusion/conspiracy au kingine labda money laundering

Collusion tuliwahi kusema si kosa lakini miongoni mwa washtakiwa hakuna mtuhumiwa
Takribani washirika 16 wa karibu wanatuhumiwa kuongopa au kutoa taarifa zisizo na ukweli

Mueller amewazunguka kiasi kwamba mmoja anaweza kutoa ushirikiano kuhusu mwingine
Hili limeacha maswali, kwanini washirika wakiwemo wa familia na Trump wanaongopa?

Ikiwa hakuna collusion au conspiracy hofu yao kuongopa inatoka wapi?

# 1
Mmoja wa waathirika wa ''kuzungukwa' ni mwenyekiti wa kampeni Paul Manafort
Huyu alifanya kazi katika vikao vya Trump Tower akiwa na makamu wake Rick Gates

Paul Manafort yupo kizuizini baada ya kukiuka dhamana ya mawasiliano akiwa na kesi

Imethibitika pasi na shaka kuwa ''ule ushirikiano' alioutoa kwa Mueller ulikuwa ni uongo

Hilo limetokea kutokana na ushirikiano anaoutoa bwana Gates aliyekuwa makamu wake

Imeelezwa Manafort alishirikiana na Warusi kama Klimnik, ambaye ni Jasusi wa Kremlin.

Manafort alimpa takwimu za ndani za uchaguzi ''polling' kwenda kuzifanyika kazi
Ushirika wa Manafort na maafisa wa Russia na Ukraine unaelezwa katika utata wa hali ya juu

Hukumu inaymkabili ni kati ya miaka 19 hadi 24 na katika miaka 70+ ya umri huenda ukawa ndio mwisho wa maisha huru.

Kinachoulizwa kwanini ameamua kujitoa kafara kwa kusema uongo?

Paul Manafort amebeba siri nzito kifuani, amekubali kuihifadhi akitaraji msamaha wa Rais

# 2
Bwana Roger stones aliyeshtakiwa hivi karibuni naye yupo matatani.
Imethibitika uwepo wa mawasiliano kati yake na Wikileaks, na inaonyesha alikuwa kiungo

Hili limesemwa makusudi kabisa na Mueller kwasababu tutakazoeleza

#3 William Barr amethibitishwa kuwa AG wa Marekani kwa mara nyingine baada ya kuwa AG wa Rais G.H.W. Bush. Kuthibitishwa kwake kunafuatia kujiuzulu kwa AG Sessions na kukaimiwa na Whitker ambaye si tu ameonyesha uwezo duni bali ni mshabiki wa Rais Trump

Wote wawili, Barr na Whitker waliwahi kuhoji uhalali wa mchunguzi Mueller.

Tofauti ni rekodi zao ambapo Barr anaonekana kuwa imara na Whitker kama kibaraka wa WH kujua nini kinaendelea

Inaendelea...
 
MUELLER, BARR NA DOJ

#4
Kumekuwa na mjadala wa hatma ya taarifa ya Mueller kama itawekwa hadharani au la

WH haitaki taarifa iwekwe hadharani na ndicho chanzo cha kuisakama idara ya sheria DOJ

Act. AG Whitker alisema, taarifa itapitiwa na kuona kipi cha kuwekwa hadharani kipi kifichwe

Jambo hilo limewatibua GOP na Dems katika congress wakichagiza taarifa iwekwe hadharani

Moja ya kazi ngumu za AG Barr ni hilo la kuamua kama taarifa iwekwe hadharani au la

#5 Mueller na Dep. AG Rosenstein walifahamu mbinu za kutaka kuua uchunguzi

Kwanza, kulikuwa na mpango wa kumtimua Mueller, jambo lililpingwa kisiri siri na wajuvi wa mambo ndani ya WH akiwemo Gates wakati huo, na ndani ya Senate na House

Nyaraka zote za Mueller zilihifadhiwa na FBI kila hatua ili hata akifukuzwa uchunguzi ukianzishwa siku za baadaye ijulikane wa mwanzo ulifikia wapi

Mpango wa pili ulikuwa kumtumia acting AG Whitker kuiba siri za uchunguzi.

Hilo halikufanikiwa kwani kila hatua ilishaidhinishwa na Roseinstein kabla ya Whitker.
Hivyo hakuwa na uwezo wa kuidhinisha au kuzuia uchunguzi , bali kupata za juu juu tu

# 6
Kwa kuangalia mtiririko wa matukio hapo juu kinachoendelea ni hiki.
Kwanza, Mueller hakutaka kufikisha mahakamani madai ya conspiracy au collusion.

Hili likajenga imani kwa Trump na wafuasi wake kuwa hadi sasa hakuna collusion au conspiracy. Mueller hakutaka kuweka wazi

Mueller amewazunguka vidagaa na kukamata mapapa hatua ya mwisho akiwaghilibu wanaomhujumu kwa kuwapa matumaini ya kutokuwa na jipya.

Mwisho amekamata papa wawili akiwa na Mapapa 2 pembeni pengine na Nyangumi

Paul Manafort na Roger Stones wanaonekana kuwa viungo muhimu sana.

Kwa mantiki hiyo kwa mara ya kwanza, Mueller ametoa taarifa ya wazi ya ushahidi wa email za Roger Stones na Wikileaks, na kuna ushahidi wa Manafort na Klimnik, jasusi la Kremlin

Mueller ameweka wazi kwa makusudi ili umma ujue uhusiano wa watuhumiwa na Russia.

Hilo linamweka AG Barr katika wakati mgumu sana wa kuficha taarifa.

Alichokifanya Mueller katika mashtaka dhidi ya Manafort na Stones ni pre-preemptive strategy kuhusu taarifa atakayoifikisha DOJ kwa kumfunga mikono AG Barr kuzika taarifa au kunyofoa taarifa

Taarifa ya Mueller kuhusu Stones na ushahidi wa email imetolewa siku ya kwanza tu, Barr alipoingia ofisini. Huu ni ujumbe kwa Barr kwamba asiingie kichwa kichwa au mkenge

Kwa miaka 2, Mueller kwa mara ya kwanza na rare ameeleza haya;

Kuhusu Manafort na kwanini anaongopa(rejea#1).

Kwanini ameeleza Roger stones na email na Wikileaks( #2), uhusiano wa taarifa na hisia za kufichwa taarifa (#3), kwanini wamechukua hatua hizi dakika za mwisho (#5) na nini tutarajie (#6)

Tusemezane
 
NDANI YA VIUNGA VYA DC
TAARIFA YA MUELLER WIKI HII

Taarifa ya mchunguzi maalumu Mueller imeelezwa kukamilika na wiki hii ataikabidhi kwa DOJ

AG Barr atakuwa na mpira wa kuamua taarifa iwekwe hadharani au isitolewe au itolewe kwa 'summary''

Tayari kuna mvutano kati ya House na WH. Senate haijasema chochote kwani ipo chini ya GOP

Hata hivyo ndani ya senate GOP kuna mgawanyiko, wapo wanaosema wananchi wana haki na wapo wanaosimama na utetezi kwa Trump

Rais Trump hataki taarifa iwekwe hadharani, kinyume na kauli zake za ''no collusion na uchunguzi wote ni kutafuta mchawi''. Kama hakuna lolote hofu inatoka wapi?

Suala hapa si ''hukumu'' dhidi ya Trump. Kuna uwezekano taarifa ikamsafisha yeye na kampeni

Lakini pia inaweza kumtia matatani, na yote yatategemea ushahidi utakaotolewa
Kwa upande mwingine, Wamarekani wanataka kujua uchagauzi wao uliangiliwaje na Russia

Vyombo vyote vya usalama akiwemo SoS Pompeo wamesema wazi Russia iliingilia uchaguzi

Kazi kwa AG Barr ni kubwa kwani kutoa taarifa kwa vipande haitaweza kusaidia kuvuja kwa taarifa nyeti kama ilivyozoeleka viungani DC

Lakini pia, Barr anaweza kuitwa kwa hati ya kiapo ya Bunge kueleza nini kilichomo kwa undani

Hata kama taarifa itafichwa kwa kisingizio cha kulinda siri za usalama, ndani ya House na senate kuna kundi linaloitwa 'gang of 8' genge la watu 8,wanne kutoka kila House na Senate

Hawa wanahaki ya kuona taarifa yoyote ile ya usalama wa nchi bila kuchuja.
Katika hali hiyo ni ngumu kwa taarifa kutovuja. Kumbuka ndani ya genge hilo,waane ni Dems

Kitendo cha kumshtaki Roger Stones na Paul Manafort dakika za mwisho kinaeleza jambo

Kwamba umma ''unataarifiwa' kulikuwa na jambo nyeti miongoni mwa hao

Kumwacha Don Jr na Jerad Kushner kunatia shaka kama upo ushahidi wa kutosha au ni kuwaacha kwani mvumo unaokuja ni mkubwa. Haieleweki Mueller amedhamiria nini

Kukiwa na washirika 16 wa karibu sana wa Rais Trump walioomnyesha ushirikiano na Mueller na wengine kushtakiwa au kwenda magereza kuna mshindo unaofikirika

Inatosha kusema Mueller peke yake ndiye anajua nini kimo katika taarifa yake na tuhuma zote ikiwa zina ukweli au la

Tusemezane
 
SIASA VIUNGANI DC

COHEN AMWAGA 'MBOGA' AKISUBIRI GEREZA
HANOI YAISHA BILA MAFANIKIO, KIMBEMBE KIPO DC

Wiki hii ilikuwa na matukio kadhaa wakati taarifa ya Mueller ikisubiriwa
Gharama za kupoteza House zinatitia kama tulivyowahi kujadili, Rais Trump ni mhanga mkubwa

Kamati za Bunge za House zinazoongozwa na Democrats na ile ya senate zimemhoji aliekuwa mwanasheria wa Trump kwa zaidi ya miaka 10. Mr Cohen anasubiri kwenda magereza

Cohen alieleza mambo mazito akimkaanga boss wake vilivyo hadharani na nyuma ya pazia
Anamweleza Boss wake katika kila nyanja zote zinazozungumziwa iwe racism, Russia n.k.

Mahojiano yake yatalazimu baadhi ya watu aliowataja kuitwa na kamati kinyume na ilivyokuwa wakati Republicans wakitawala chini ya Nunes.

Baada ya siku tatu, Cohen atarudi tena wiki ijayo kuendelea na mahojiano na kamati husika
Katika aliyoongea Cohen kwa namna fulani anatengua baadhi ya vitendawili

Kwa kumsikiliza Cohen ambaye hana cha kupoteza akielekea gerezani, ni wazi taarifa ya Mueller itakuwa na mengi ya kushutua kama si kutisha kuhusu Rais Trump

Cohen amefunguka kuhusu uchunguzi unaoendelea kule SDNY unaowahusu watu wa karibu sana wa Familia ya Trump pengine ndiyo maana hawajashtakiwa!!

Hayo yakiendelea Rais Trump alikuwa mjini Hanoi, Vitetnam kukutana na kijana Kim UN
Suala la Korea limepewa kipaumbele kwasababu za kisiasa hata kuwatosa washirika wengine

Mkutano umemalizika bila maafikiano ukiashiria mbio za Trump huenda zimegota kwa Kim UN
Hili ni tatizo kwani karata ya kisiasa ya kufanya jambo kubwa imepoteza uelekeo

Mkutano wa Hanoi haukuisha bila utata. Rais Trump alisimama kidete kumtetea UN kwa kifo cha Mmarekani Wambier aliyerudisha US akiwa mahututi na kufa siku chache baadaye

Kama ulivyokuwa utetezi kule Helsinki kwa Rais Putin, Trump alimtetea UN kwamba hakujua uwepo wa mfungwa huyo licha ya kuwa serikali za nchi zote zilikuwa na taarifa hiyo

Hilo linakumbusha anguko la Helsinki kuhusu Trump kutetwa mbele ya Putin na sasa Kim UN

Wakati anarejea viungani DC, mazonge zonge yanazidi kumwandama na hali inazidi kuwa tete
Sasa wanasheria wake wanahaha kuhakikisha taarifa ya Mueller haiufikii umma

Ikiwa hakukuwepo na baya lolote hofu inachagizwa na nini?

Tusemezane
 
Kamati za Bunge za House zinazoongozwa na Democrats na ile ya senate zimemhoji aliekuwa mwanasheria wa Trump kwa zaidi ya miaka 10. Mr Cohen anasubiri kwenda magereza

Cohen alieleza mambo mazito akimkaanga boss wake vilivyo hadharani na nyuma ya pazia
Anamweleza Boss wake katika kila nyanja zote zinazozungumziwa iwe racism, Russia n.k.
Duh, Cohen hakumung'unya maneno, kamwita bosi wake wa zamani ambaye sasa ni Rais wa Marekani mbaguzi wa rangi (a racist), tapeli (a conman) na mdanganyifu (a cheat).

Ingekuwa Tanzania, huyu jamaa angeokotwa pwani ya Kunduchi akiwa ndani ya kiroba.
 
Next election labda wamsimamishe Joe Biden,huyu ndo anaweza kupambana na Trump.Sio hawa wapiga domo kina Kamala Haris na awengine.Yaani umsimamishe Trump na Kamala Harris utegemee Trump ashindwa,Dems bana.Ben Senders kidogo anaweza,sema alishapoteza Taste baada ya kukosa kusimamishwa mwaka 2016.
Halafu nimegundua wala Trump hachukiwi marekani kama Media zinavyoaminisha watu.
Facts:Mid term elections zote huwa zinakuwa mbaya kwa marais walio madarakani,Lakini mwaka jana,Trump alipoteza viti 19 bunge la wawakilishi(House of representative),compared to Obama alipoteza viti 65+,alipoteza both senate na House of Reps.But Trump alifanikiwa Ku retain bunge la senate kwa mara ya Pili.Sasa inahitaji akili za malaika ku convinse kwamba Trump anachukiwa na wamarekani kuliko Wengine waliopita,Kwa USA midterm ndo kipimo cha kuonyesha performance ya Marais wakiwa madarakani.
Huu ni Mchango wa Ndugu yetu SirChief
 
WIKI HII VIUNGANI DC
MANAFORT APEWA HUKUMU YA KWANZA

Ilikuwa wiki iliyotandwa na habari za mwanasheria wa zamani wa Trump Bw Michael Cohen
Cohen ametoa ushuhuda hadharani na nyuma ya pazia akimwaga anachojua kutoka kwa mteja

Bw Cohen anataraji kuanza kutumikia kifungo cha miaka 3 bila tegemeo la msamaha wa Rais

Habari za Cohen zilifunika ziara ya Rais Trump mjini Hanoi alipokutana na Kim Un wa Korea
Ni ziara iliyokuwa na matumaini Trump akitegemea kutanzua kitendawaili cha Korea Peninsula

Hata hivyo kinyume na matarajio, hakuna kilichofanyika, Trump akirudi DC bila mafanikio

Habari za Cohen zilisaidia sana kufunika anguko la Hanoi lililokuwa na kauli tata kama Helsinki

Wakati huo huo aliyekuwa mwenyekiti wa Kampeni ya Trump Bw Paul Manafort amehukumiwa
Paul atakwenda jela miaka 4 akiwa tayari amekaa mahabusu miezi tisa hivyo kuwa miaka 3

Paul amehukumiwa kutokana na kutotoa ushirikiano kwa Mueller huku akikabiliwa na mashauri yanayohusu miamala ya pesa. Kesi hiyo ilikuwa Virginia na ipo nyingine New York

Kwa maana hiyo Manafort anaweza kuhumiwa miaka mingine zaidi au kifungo cha pamoja

Katika hukumu , Jaji alisema adhabu ya Paul si kutokana na ''Russia collusion' bali shauri jingine
Rais Trump akaichukua kauli hiyo na kusema ''Jaji amesema hakuna Russia collusion''

Nguvu ya Trump ipo katika kusema anachotaka bila aibu hata kama ukweli upo wazi
Hili linamsaidia sana hasa kuliteka kundi lisiloweza kung'amua au kutofautisha mambo
Kurudia rudia uongo huo kunawafanya wengi kuamini anachosema hata kama ni uongo

Kundi analolenga si Wamarekani wote ni ile asilimia chache inayoamini kila asemacho

Kwa mtazamo huo wengi wanadhani wote walio na kesi au waliohukumiwa ni kutoka na Russia collusion. Ukweli ni kuwa hakuna hata mmoja, isipokuwa 'collusion' imewatia matatani

Matata mengi ni kusema uongo, wengi wanajiuliza, kuna nini kila mmoja aongope?

Kwa sasa kundi zima linalomzunguka Rais Trump lipo matatani isipokuwa familia yake tu
Michael Cohen, Paul Manafort, Roger Stones, Gates, mhasibu wake n.k. wamebanwa

Taarifa ya Mueller inasubiriwa kukiwa na lindi la maswali. Kwanini Familia ya Trump haikuitwa kuhojiwa? Huenda hawana tatizo, au huenda wakawa kishindo!

Je, alichosema Cohen kuhusu Trump kuongea kwa ''codes'', kitakuwa kimemnasua?
Roger Stone anayeonekana kuwa kiungo alikuwa na ushiriki upi na akihusisha akina nani?

Je kulikuwa na obstruction of justice? Comey na Sessions watakuwa ni jeraha alilojitakia?

Je, majibu kwa Mueller yalijitosheleza kumuondoa Trump katika mzunguko wa ''collusion''?

Hata kama hatakuwa na tatizo, kinachoweza kumtia matatani ni 'goli la mdomo wake''
Bila kujali collusion, ripoti ya Mueller inaonekana kufumua mengi Trump aiyoyataka hadharani

Tusemezane
 
RIPOTI YA MUELLER YAKAMILIKA
SASA IPO MIKONONI MWA AG W.BARR

Baada ya siku 675 hatimaye taarifa ya mchunguzi Mueller imekamilika na kukabidhiwa kwa AG William Bar. Ieleweke Barr ni Boss wa Mueller na Deputy AG Roseinstein

Inaelezwa taarifa ya awali 'principle conclusion' itafikishwa na Barr katika kamati za Bunge mwishoni mwa wiki.

Tayari kumezuka sintofahamu ambapo Democrats wanataka taarifa ya Mueller siyo ya Barr

Kimsingi taarifa hiyo itachujwa ili kulinda vyanzo au taarifa nyeti hata hivyo Dems wanaonekana kutaka taarifa kwa kina hata kama itachujwa

Wasi wasi wa Dems upo katika ukweli kuwa AG Barr alishiriki na wanasheria wa Trump kabla ya kuteuliwa na huenda akaandika taarifa itakayotoa picha tofauti

Pili, wanahofia Rais Trump anaweza kugeuza maneno kwa jinsi anavyotaka kama alivyoda ''Jaji kasema hakuna collusion'' ingawa jaji alisema kesi haikuwa ya clollusion

WH na Trump wanataka taarifa isitoke, si kwasababu ina mambo yanayomgusa Rais Trump bali hofu kuwa yapo yasiyojulikana huenda yakatoka hadharani

WH na wanasheria sasa wanajipanga kuhakikisha taarifa inabaki siri

Hapa kuna mambo mawili, kwanza, kuna suala la kisheria halafu kuna masuala ya kisiasa

Clinton na emails ilibainika haikuwa kesi ya jinai lakini kisiasa emails zilimuathiri sana.

Halafu kuna suala la kushtakiwa. Wataalam wanalumbana iwapo Rais anaweza kushtakiwa au la. Kwa taratibu za DOJ Rais akiwa madarakani hawezi kushtakiwa
DOJ wanasema hata kwa mtu asiyeshtakiwa ni makosa kumtaja kwa mujibu wa sheria zao

Na mwisho kuna mvutano ikiwa nyaraka na taarifa inaweza kuitishwa Bungeni kwa lazima ya kisheria 'subpoena'' ikizingatiwa kuna executive privilege na Oversight ya kisheria ya Bunge

Kuelekea mbele tutajua mwelekoeo mpya baada ya taarifa. Jambo muhimu ni kuelewa jinsi nchi ya Marekani isivyo na mkubwa. Pamoja na matishio yote na harakati zote Mueller amelindwa hadi kukamilisha kazi. Hili lilimkera sana Rais Trump aliyetaka kufutilia mbali uchunguzi

Katika viunga vya DC hakuna siri, kidogo kidogo habari zote zitavuja iwe nzuri au mbaya

Inasemwa ''the devil is in the details'

Tutaendelea kuwajuza nini kinajiri

Tusemezane
 
Kwa aliyefuatilia namna "Russia Collusion" ilivyoanza (July 2016) hawezi kushangaa kuona hakuna yeyote kwenye Timu ya kampeni ya Trump aliyepatikana na hatia ya kushirikiana na Russia kuingilia uchaguzi wa US (Russia Collusion) na pia Trump kutokwamisha upatikanaji wa haki (Obstruction of justice).

Kwa lugha nyingine, ripoti ya Mueller imepigilia msumari kile tulichokisema na alichokuwa akikisema Trump kila kukicha toka aingie madarakani kuhusiana na huo uchunguzi, kuwa yeye na Timu yake hawakushirikiana na Russia kuingilia uchaguzi wa U.S., ndio maana akawa anauita "Witch hunt", au "Hoax".

Kwa miaka miwili Democrats na hawa wenzetu humu jukwaani wamekuwa wakitoa taarifa kwa kila hatua ya uchunguzi wa Mueller kuashiria kuna ushahidi wa kumtoa Trump madarakani (impeachment) au kufungwa gerezani. Leo wameumbuka! Ila bado watatafuta cha kushikilia maana hawaamini!

Tukumbuke tu Rod Rosenstein (Deputy AG) alimteua Robert Mueller (ambaye Trump hakumkubali) kuwa Special Counsel ili kuwaridhisha Democrats waliokuwa na wasiwasi kuwa Trump atasimamia uchunguzi dhidi yake. Mueller alichagua democrats tupu kwenye timu yake ya uchunguzi ili kuwaridhisha Democrats walio Congress, hadi Trump akawa anawaita "13 angry democrats".

Trump akawa hakubaliani na uchunguzi wa Mueller kusimamiwa na Rosenstein kwa kuwa naye alikuwa na 'conflict of interest' ambazo ziliashiria kuleta 'bias', na hivyo alimtaka Rosenstein naye ajitoe kama Jeff Seesions (AG wa zamani), lakini Democrats walimtaka huyohuyo Rosenstein ndiye Mueller a-ripoti kwake na ikawa hivyo na yeye (Rosenstein) ndiye aliyekabidhiwa repoti ya uchunguzi kabla ya kumforwadia William Barr (AG).

Kwa kiasi kikubwa Democrats wame-control huu uchunguzi mwanzo mwisho, na bado wametoka kapa! Badala ya 'impeachment' Trump ndio atazidi kupaa kwenye approval ratings, ndio maana hata baadhi ya wachambuzi wa CNN wameeleza kuwa hiyo ripoti ni ushindi (victory) kwa Trump.

Baada ya karibia miaka miwili ya uchunguzi wa Mueller na miezi tisa kabla ya FBI, hamna kitu!!!!!. Tuwe tunachunguza, kutafakari na kupima kabla ya kumeza tunayoyaona, kusoma au kusikiliza kwenye media zenye mrengo flani au wanasiasa wenye chuki dhidi ya Trump. Sasa Russia Collusion imeisha, hamna ushahidi (zero evidence), media na hawa wanasiasa wameumbuka pamoja na wafuasi wao.

FACTS ALWAYS. TRUTH MATTERS.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom