Duru Za Siasa: U.S Chini ya Donald J. Trump


Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
Wanajamvi

Uchaguzi wa US umekamilika jana baada ya D.J Trump kuwa Rais wa 45
Leo ilikuwa siku ya kwanza kamili ya Trump kama Rais wa US

Uzi utakuwa utaangalia serikali mpya na mwelekeo wa siasa na uchumi
Siasa za Marekani , taifa lenye nguvu katika uso wa dunia zinaathari kubwa duniani

Ni kwa kuzingatia hilo, uzi utaleta kwa kadri, yanayojiri katika Taifa hilo

Tutaendelea kumalizia hotuba ya Trump baada ya kutawazwa katika uzi huu
Duru za Siasa: Matokeo ya Uchaguzi Marekani

Rais Trump, mfanyabiashara aliyefanikiwa katika biashara ameondoka katika utawala wa makampuni na sasa ni mtawala wa umma na Taifa la Marekani

Kuchaguliwa kwake kama mtawala wa juu wa Taifa lenye ushawishi umekuja na mshtuko kutokana na nafasi aliyopewa katika uchaguzi wa ndani ya chama cha Republican na ule mkuu

Kuna mitazamo tofauti kuhusu kuchaguliwa kwa Trump. Kwasababu zozote ambazo wachunguzi wanaendelea kuzifuatilia kisiasa , uchumi, jamii n.k. Trump ndiye Rais wa Marekani

Siku ya kwanza, Trump amekumbana na changamoto za utawala wa nchi na si kampuni binafsi

Katika historia ya miongo michache ya Marais wa US, siku ya kwanza haikuwa nzuri kwake

1. Maandamano ya wanawake duniani
2. Ziara iliyozua utata katika Intelligence community (IC)

Tutajadili mambo hayo mawili na picha ya haraka ya nini kitarajiwe kwa siku za usoni

Tusemezane
 
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Messages
9,976
Likes
8,299
Points
280
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined May 31, 2008
9,976 8,299 280
As such, the investigation’s focus has shifted this year from looking for collusion to finding obstruction. Mueller’s team have combed through Trump’s tweets and looked at his firing of former FBI Director James Comey with a view to finding this obstruction, so far unsuccessfully.

Cohen's plea comes two weeks before the lawyer is due to be sentenced for the earlier tax and campaign finance violations. He is facing a possible term of 46 to 63 months in prison and a potential fine of up to $1 million. His voluntary cooperation with Mueller, however, could see this punishment lessened significantly.
===
Cohen anachokifanya, ni kumchomoa Trump kwenye 'makandokando' ingawa anadhani ndiye anampaka hayo makandokando. Kwa hili Trump atapeta tu.
Hakika huko unakopata habari zako kunatisha. Ndugu yangu TUJITEGEMEE kama tulivyotabiri awali ndo ndo ndo sasa imekuwa chururuuuuu! Kabla ya Krismasi ya mwaka huu tutashuhudia mengi kwani Marekani mambo hayaendi kwa pupa wala kwa kukurupuka na kupayuka hovyo. Yanayomsubiri Rais Donald Trump mbele ya safari hata yale yalliyomkuta Rais Nixon miaka 40 iliyopita, yataonekana kama cha mtoto. Wewe endelea kuota tu.
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
SENETI YAPIGA KURA KUKATAA SERA ZA TRUMP
KIWEWE CHA UCHAGUZI WA MHULA WA KATI KINAVUMA

Katika hali isiyokuwa ya kawaida seneti imepiga kura 63-37 ya mswada wa kuiondoa Marekani katika vita ya Yemen kama msaidizi wa Saudia Arabia. Hili limekuja kufuatia mauaji ya Khashoggi

Licha ya Secretary Pompeo na Jim Mattis kuwashawishi maseneta, bado haikufanikiwa

Wawili hao walikwenda katika senate kueleza mkasa wa Khashoggi bila uwepo wa CIA Director

Hilo ilifanyika makusudi ili Director Gina Haspel asiwezi kuanika ushahidi wa uhusika wa MBS

Ni pigo kwa Rais Trump likionyesha maseneta wameanza kuchoka sera zake

Maseneta hawakubaliani na maelezo ya biashara na Saudia bali kusimamama na 'values' za US

Suala la Khashoggi licha ya mizengwe linaanza kumwinda Rais Trump.

Kuna jitihada za kutafuta mahusiano ya Trump na Saudia ikiwa ni kwa masilahi yake au ya nchi

Kupoteza House nako hakutasaidia. Democrats wanasema kamati ya Nunes wakati ikiongoza imeficha nyaraka muhimu zinazohusiana na miamala yake na Russia
Kwamba, Dems wakichukua House na kamati, yote yatakuwa hadharani

Mueller anaendelea kumwendea kombo Trump 'under the skin' baada ya kumalizana na vismaki

Uchunguzi wa Russia upo katika viunga vya WH, mzee akikabiliana nao ana kwa ana

Taarifa ya msiri wa Trump bwana Cohen kuhusu biashara za Trump wakati wa kampeni zinazidi kuchagiza udadisi wa mahusiano ya Rais Trump na Russia

Inaelezwa, Trump amekuwa 'seethed, spooked and unhinged' katika siku za karibuni

Kumbukumbu za Helsink na hizi za Khashoggi zinazomlazimu Rais kutosa vyombo vyake vya ulinzi na usalama vinazidisha udadisi juu ya masilahi yake binafasi na ya nchi dhidi ya Russia na Saudia

Kukatiza mkutano wake na Putin wiki hii kule Buenos aires kunaelezwa ni katika kupunguza ubwabwaji kama ule wa Helsink huku suala la Ukraine likiwa linachemka na bichi kabisa

Kwa mtazamo huo, kuna kuchoka 'fatigue' miongoni mwa maseneta na House reps.
Baadhi wanaona Republicans inapoteza misingi yake kwa kukumbatia 'Trumpism'

Kuelekea uchaguzi mkuu na kwa kuangalia kipigo cha midterm, kuelekea mbele si rahisi kusema uwepo wa seneti pekee unaweza kumsaidia Trump.
Kuna resistance isiyo ya wazi inayovuma chini chini

Tusemezane
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
MKUTANO WA G20 ARGENTINA
COHEN NA TAHARUKI

Mkutano wa G20 unaendelea Buenos aires, Argentina. Mkutano unawakutanisha viongozi wa nchi zenye viwanda na zenye ushawishi katika masuala ya uchumi na ulinzi duniani

Ni muda wa viongozi kuchangamana na kubadilishana mawazo au kuweka mikakati
Mikutano ya namna hii huwa na vituko na matukio mbali mbali

Katika kituko kimoja, ni pale Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe alipokutana na Rais Trump
Abe alimpongeza Rais Trump kwa ushindi mnono wa muhula wa kati ''midterm elctions'

Wapo wanaodhani PM Abe hajui nini kimetokea katika siasa za US.
PM ni mwerevu , kama viongozi wengine duniani ,anatambua njia rahisi ya kuelewana na Rais Trump ni ''kumjaza upepo'' wa misifa hata pasipotakiwa. Hilo limekuwa kichekesho katika G20

Trump ni mwepesi wa kulewa sifa. Katika mikutano yake anaposhangiliwa hakawii kutoka katika mistari na kauli zinazomtia matatani kila mara. Crowd humjaza jazba zisizokuwa na maana

Rais Trump amefuta mkutano na Rais Putin kwa kilichoelezwa mgogoro wa Ukraine.
Wachambuzi wanasema hiyo sababu, huenda ni kutokana na bomu la mwanasheria wake Cohen kuhusu miradi ya Trump Russia

Ikitazamwa kisheria, hakuna kosa lolote. Tatizo ni pale ambapo Trump amekanusha mara nyingi
Inapounganishwa na 'unyenyekevu kwa Putin' kuna maswali endapo miradi binafasi inamkwaza kutekeleza majukumu ya kitaifa kuhusu Russia

Ndivyo inavyoonekana kwa MBS huku kukiwa na habari za Wasaudia kuwa na biashara na Rais Trump.

Sababu anazotoa hazijaridhisha Wamarekani ikiwemo seneti iliyokataa Khashoggi na Yemen kwa 63-37

Hili la Cohen limemchukua sana Rais Trump. Hata hivyo anapaswa kujilaumu

Cohen aliapa 'kupokea risasi' akilimlinda Rais Trump. Ni baada ya wawili kukutana Malalago Florida, Trump alimuelezea Cohen kama mshauri wa mambo madogo madogo

Kauli hiyo inaonekana kumhakikishia Cohen si miongoni mwa wanaoweza kupata msamaha wa Rais kwani Trump alishaanza kumtelekeza. Hapo ndipo akaamua kutoa ushirikiano kwa Mueller

Kauli za Trump na hatua zake zinamtia matatani hata anaposhauriwa. Kumfukuza Comey, Sessions na wengine hakuwezi kumwacha salama. Habari zinazovuja zinatoka kwa waliokuwa wasiri wake

Uchunguzi wa Mueller unamtia Rais Trump 'wahka' Hii si kwasababu ya collusion kama ipo au la, ni kutokana na mueller kupiga kambi ndani ya viunga vya WH.

Haijulikani hofu ni ya nini ikiwa uchunguzi ni 'hoax' kama anavyodai

Tusemezane
 
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Messages
9,976
Likes
8,299
Points
280
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined May 31, 2008
9,976 8,299 280
Kifo cha aliyewahi kuwa Rais wa Marekani, George H.W. Bush akiwa na umri wa miaka 94, umempa ahueni (breathing space) Rais wao wa sasa, Donald Trump, kwani habari kuu hadi anazikwa zitahusu wasifu wa Marehemu. Hivyo Trump ajipange sana na katika wakati huu ajichunge sana na matamshi yake. Kupayuka kwake kuliifanya familia ya Bush isimpe mwaliko katika msiba wa aliyekuwa First Lady, Barbara Bush, mapema mwaka jana akimtangulia mmewe kwa mwaka moja akiwa na umri wa miaka 73. Watu wanasubiri kuona jinsi ukoo wa Bush utakavyompokea Rais Trump kama atahudhuria mazishi.
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
MKUTANO WA G20
MWANGI WA MIDTERM WAMLAZIMU TRUMP KULEGEA
MUELLER HAONEKANI KUTOA NAFASI, SASA YUPO 1600 PENN

Mkutano wa wakuu wa kundi la G20 wamemaliza mkutano wao wa kawaida Buenos Aires
Rais Trump alifanya majadiliano na Rais wa China Xi Jinping kuhusu vikwazo vya biashara

Wakuu hao wamekubaliana kusitisha vikwazo kwa siku 90 wakitafuta muafaka wa tatizo hilo

Rais Trump ame 'tweet' kuwa makubaliano ni China kununua zaidi bidhaa za US
Hakuna maelezo kutoka afisa mwingine kuhusu makubaliano, hilo libaaki ''kuwafariji watu wake''

Uchaguzi wa mhula ambao Trump amepoteza House kwa kiwango tangu Rais Nixon alipkuwa madarakani umeacha makovu. Takribani wiki 3 za kampeni amezuai seneti kwa taabu sana

Kupoteza House, magavana na mabunge ya state halikuwa jambo dogo.

Hii inachangiwa na Democrats kuelewa udhaifu hasa wa Obamacare uliowalazimu Republicans kuikubali ili kujinusuru. Wananchi wanaguswa na suala la afya kuliko tambo za kisiasa

Majibu ya China kwa Trump kuweka vikwazo kwa bidhaa za wakulima kumewaumiza Wakulima.

State kama Ohio, Pennyslavania, Michiga na Wisconsin ni muhimu sana katika uchaguzi mkuu

Kampuni ya GM imetangaza kufunga viwanda, waajiriwa takribani 15,000 kutoka maeneo kama Ohio kupoteza ajira. Hili litaambana na kupotea ajira kwa huduma na hivyo kuwa katika malaki

GM pamoja na mbinu nyingine za kibiashara kama kutumia masoko ya mitaji kujinufaisha kutokana na tax cut ya Trump pia ni mtengezaji wa magari kule China wanakokumba na vikwazo

Ukiyaweka pamoja yote hayo ni wazi Rais Trump anahisi hali kuwa ngumu kama hatafanya jambo. Hilo limemlazimu arudi katika meza ya majadiliano na China, kalegea kwa kiasi fulani

Katika kumaliza mkutano Rais Trump aikwepa mkutano na waandishi kwa hoja ya kifo cha rais wa zamani George H.W. Bush (41) aliyefariki akiwa na miaka 96.
WH ilitumia msiba kama kisingizio ili kukwepa dhahma kama ile ya Helsinki, Finland

Bush yupo DC kuagwa akilala katika Bunge 'rotunda' ambako watu wa kipekee huwekwa.
Mwili wake utalala hapo kwa kuagwa kwa masaa 41 ikiashiria ni rais wa 41 wa Taifa hilo.

Rais Trump amealikwa kanisani Cathedral akiwa miongoni mwa marais 4 walio hai, Carter, Clinton, Bush na Obama. Katika hali isiyokuwa ya kawaida Trump hatatoa hotuba.

Macho yatakuwa Cathedral kuona atakavyochangamana na marais hao aliyowacharua

Msiba wa Bush umetoa 'ahueni' kwani habari za Mueller zinarindima huku Trump akiweweseka.

Mwanasheria wake Cohen hawapo pamoja, Trump akimwendea kombo kwa hofu na kihoro
Cohen anafahamu mengi ikiwemo mkutano wa Trump Tower na deal nyingi za Mzee

Kila uchao bila kujali msiba, Trump anaonekana kupoteza mwelekeo dhidi ya Mueller, akimshambulia atakayekuja mbele

Inaendelea...
 
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Messages
9,976
Likes
8,299
Points
280
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined May 31, 2008
9,976 8,299 280
Masikini Trump! Kiza kinene mbele, nyuma, kushoto na kulia...je kutakucha salama?
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
MSIBA WA BUSH 41
MUELLER APIGA KAMBI 1600 Penn Ave,DC

Rais Bush 41 wa Marekani ameagwa kitaifa katika kanisa la Cathedral DC
Viongozi wa US wastaafu walikuwepo akiwemo Rais wa sasa Trump

Kabla ya jeneza kuingia ukumbini viongozi hao (Carter,Clinton, Obama) na wake zao walibadilishana mawazo kwa tabasamu. Kuingia kwa Trump kulibadilisha hali na kuwa 'tense'

Kiprotokali Rais Trump alikuwa karibu na Obama, walishikana mikono iliyobaki kuwa gumzo

Tofauti, Rais Bush anayeombeleza msiba wa baba yake alisalimiana nao kiungwana
Rais Trump akiwa mwenye WH hakupewa nafasi ya kuomboleza, kinyume na taratibu

COHEN NA FLYNN
Wiki ilirindima kwa Rais Trump kumshambulia mwanasheria wake wa miaka 10 bw Cohen.
Kuhitilafina kunatokana na Cohen kutoa ''ushirikiano' kwa Mueller kwa kadhia ya Russia

Cohen alishiriki mkutano wa June 21 Trump tower na miadi ya uwekezaji Russia ya Trump
Anahusika na pesa zilizowalipa makahaba wanaomtuhumu Trump kula nao ''tunda'' nje ya ndoa

FLYNN
Hati ya mahakama inayomhusu mshauri wa zamani wa usalama Bw Flynn imewekwa wazi ikiwa imefutwa maeneo nyeti kwasababu za mwenendo wa kesi. Siyo taarifa kuhusu Russia Collusion

Hati imemuomba hakimu kutompa kifungo bw Flynn kwani ametoa ''ushirikiano' wa kutosha
Flynn alihusika sana kutengeneza ''back channel'' akishirikiana na balozi wa Russia Kislyak
Hilo lilitokea wakati Rais Obama anawatimua maafisa ubalozi wa Russia kabla ya kuondoka

Flynn amehojiwa mara 19 na Mueller, kinachoshtua wengi hasa WH ni Mueller kuomba asipatiwe kifungo kutokana na kukiri makosa. Je,Flynn kaeleza nini? Hakuna ajuaye isipokuwa Mueller

ROGER STONES
Ni mshirika wa Trump na alihusika katika kutoa taarifa za awali kuhusu email za Democrats
Anashukiwa kuhusika kama kiungo kati ya Trump kampeni na Wikileaks , ingawa anakana

Naye ametumia kifungu ''cha 5'' kuzuia nyaraka zake kutolewa popote
Rais Trump ameashiria kumsamehe akifungwa ikiwa atakomaa bila kutoa ushahidi

Hadi hapo tunawaona washirika hao katika sura za zamani na za sasa kama ifuatavyo;
1.Cohen, aliahidi kuchukua risasa''take the bullet' kumlinda Trump. Sasa anatoa ushirikiano
2.Flynn, alikuwa mpiga debe wa kauli mbinu 'lock her up. Sasa anatoa ushirikiano
3.Stone, alisema hana cha kuficha na hana hofu, sasa ametumia kifungu cha 5

Watatu hao ni 'privy' na ''inner circle'' ya Rais Trump. Kutoa kwao ushirikiano kwa mchunguzi Mueller kuna ashiria jambo moja, Mueller kapiga kambi jengo # 1600 au WH, na kuna kila sababu Trump kuweweseka.

Tusemezane
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
VIUNGA VYA DC VYA ZIZIMA KWA SIASA ZAKE
RAIS TRUMP ASEMEKENA KUTWETA( SEETHING)

Sehemu ya I

Kwa wanaofuatilia tumeeleza jinsi uchunguzi wa Mueller kuhusu Russia unavyoendelea. Tulieleza, nchi kama Marekani taasisi hufanya kazi kwa mnajili ya taifa kwa utaalam na weledi

Baada ya uongo, uzushi na kukana ushiriki wa Russia katika uchaguzi mkuu, Rais Trump anajikuta katikati ya timbwili kubwa linalotishia nafasi yake.

Tulieleza makosa aliyofanya na anayoendelea kuyafanya, uchunguzi unavyozunguka na sasa upo ndani ya nyumba nyeupe (WH)

Vyombo vya usalama vilieza pasi shaka kuwa Russia ilijihusisha na uchaguzi wa mwaka 2016
Mtu pekee aliyekana hilo ni Rais Trump hata pale ukweli unapowekwa wazi

Kumtimua Comey lilikuwa kosa la kwanza kwani uchunguzi ulihama kutoka ''FBI' na kupewa mchunguzi maalumu chini ya idara ya sheria (DOJ). Kumwandama AG Session kuliongeza udadis kuhusu Russia. Kumhifadhi na kumuoga Rais Trump kulitiliwa shaka n.k.

Kauli zake za kukana na kuzua mambo kwa mtindo wa ujanja wa New York zinagonga mwamba

Mueller hajakamilisha uchunguzi, hata hivyo miongoni mwa wanahojiwa au kushtakiwa , 16 ni washirika wa Kampeni ya Trump kwa njia moja au nyingine tena wakihusishwa na Russia.
Kuna nini kinaendelea? Ieleweke bado taarifa haijatolewa kuhusu ''colussion'

Tuhuma za makahaba wawili , Stormy Daniel na Miss Mcdugal hazihusishi suala la Russia.

Pamoja na yote tuhuma hizo zimezaa mambo mengi yakihusisha Russia si moja kwa moja bali kutumika dhidi ya Watuhumiwa na kuwafanya watoe ''ushirikiano'' kwa Mueller

Leo mwanasheria binafsi wa Rais Trump Bwana Michael Cohen kwa miaka 10 aliyejulikana kama ''fixer''(michongo) amehukumiwa miaka 3 jela.
Cohen amemgeuka Trump 'flip' kujinusuru baada ya Trump kuonekana kumtosa

Kuna vipande vingi vya kuunga ili kupata picha ya kinachoendelea katika viunga vya DC.
Tutajaviweka bila mpangilio kisha tutaviunga ili kuona vina uhusiano gani

Makahaba Stormy na Karen McDugal hoja yao ni kuwa Mzee Trump alishiriki nao kudhalilisha moja ya amri 10 kwa kumega tunda la kati.
Kitendo cha Trump kukana kilichochea makahaba kuja na ushahidi

Wakili wa Stormy, Michael Avinatti alishikia bango suala hilo na kupelekea uchunguzi
Uchunguzi ukawa wa aina mbili , 1. Kupitia Mueller aiyeangalia miamala 2. FBI South dist NY

Inaendelea...
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
VIUNGA VYA DC VYA ZIZIMA KWA SIASA ZAKE
RAIS TRUMP ASEMEKENA KUTWETA( SEETHING)

Stormy alidai kulipwa na Cohen pesa ili kuficha sakata la 'mahaba na Trump' kabla ya uchaguzi
McDugal anasema gazeti la National enquirer lilificha habari ya kumegeana tunda na mzee

FBI wakavamia ofisini mwa Cohen wakifuatilia mambo mengi la makahaba likiwemo
Waliondoka na nyaraka za kutosha wakishirikiana na Mchunguzi Mueller wa suala la Russia

Cohen ni msiri mkubwa wa Trump na alishiriki mambo mengi hivyo alionekana mtu muhimu

Trump baada ya kubaini Cohen yupo katika 'kitanzi' alimtambulisha kama 'afisa mdogo' wa mambo madogo madogo. Jambo hilo lilimuudhi Cohen aliyetegemea ikiwa angefungwa Rais Trump angemnusuru kwa msamaha wa Rais. Cohen akaamua kuacha u- 'fixer' na kuwa flipper

Cohen alicheza katika mikono miwili, ya FBI wa NY na Mueller wa DOJ.
Ni wazi alibanwa na kutoa ushirikiano. Hata hivyo, FBI walimkuta na makosa ya kudanganya kamati ya Bunge, kufanya malipo kwa makahaba na miamala ya Pesa na kupendekeza kifungo

Kinyume chake Mueller hakupendekeza kifungo kwasababu Cohen anatoa 'Ushirikiano' mzuri sana. Hapa ndipo kuna tatizo la pili kubwa kwa Rais Trump

1. Cohen anafahamu deal nyingi za Rais Trump na leo baada ya hukumu alijilaumu kwa kumhifadhi Trump katika ' dirty deed' yaani kwa madhambi. Ni kipi anajua zaidi, haijawekwa wazi

Cohen atatumikia kifungo mwezi March 2019, na kabla ya hapo atarudi katika kamati za Bunge zitakazokuwa chini ya Dems.

Kwa kujua tayari ana miaka 3, Cohen hana chakupoteza tena hivyo anaweza kusema chochote zikiwemo 'deeds' mbaya za Rais Trump

2. Cohen alishiriki ule mkutano wa June 21 Trump Tower na timu ya Kampeni akiwemo Don Jr, Kushner, Manafort na mwanadada wa kirusi Natalia, mkutano uliokanushwa kisha Trump kuandika taarifa kwa niaba ya mwanae.

Kadri siku zinavyokwenda, washiriki wote wa Trump tower wapo katika uchunguzi.
Cohen anajua nini kilichokuwa kinaendelea

3.Cohen alikuwa kiungo kati ya miradi ya Trump na Russia( Trump tower Moscow).
Trump alikana kutojua lolote au kutokuwa na mahusiano na Russia , jambo ambalo Chohenamethibitisha kutokea na kwamba yeye alikuwa Kiungo

Ni kwa muktadha huo, Cohen ni mmoja wa washirika 16 wa Rais Trump wanaohusishwa na Russia. Ni wa kwanza kuchukua miaka mingi jela na ni mtu mwenye siri za kutosha za Trump

4. Cohen ndiye alifanya malipo kwa Stormy hivyo kujua kwa kina jinsi Rais Trump alivyoyanasa makahaba, wapi na kwa ujira gani.

Kwa kutambua hilo Rais Trump kwa mara ya kwanza amekiri kufanyika malipo akisema ni mambo binafsi bila kujua uhusiano wa malipo na nyakati za Kampeni

Ni kwa mtazamo huo Michael Cohen ni mtu muhimu sana kama alivyosema mchunguzi Mueller
Huyu anakwenda chini , hata muacha Rais Trump salama.
Rais Trump anakila sababu za kuweweseka, kutweta na kuswajika

Gazeti la Enquirer nalo limeamua kutoa ushirikiano jinsi lilivyoficha habari za McDugal ili kumnusuru Rais Trump.

Hii ni baada ya kubaini Cohen anatoa ushirikiano kwa wachunguzi, hivyo ni bora kujinusuru.
CEO David Packer anaeleza jinsi walivyoficha habari ya kahaba McDugal wakati wa Kampeni. Hapa Rais Trump hana pakutokea kupinga ukweli huo

Unaweza ona jinsi wachunguzi wanavyofuatilia habari, wanavyojua kuchonganisha wahusika na wanavyopata habari na kuzifanyia kazi hata kama zipo katika mafaili na si lazima 'surveillance Camera'

Mtu anayedhani la Cohen ni 'upepo tu' halina madhara, hajui siasa za Viunga vikubwa vya DC

Tusemezane
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
WIKI NZITO KWA RAIS TRUMP
''KITANZI KINABANA KUTOKA 'ANGLE' NYINGINE

Habari inayohusu kampeni ya Trump na Russia imetulia kwa muda

Kinachoendelea ni sakata la makahaba Stormy na McDugal

Rais Trump amekiri kuhusu uwepo wa malipo tofauti na awali aliposema hakujua chochote

Hii ni baada ya Michael Cohen, mwanasheria wake na kampuni ya AMI inayomiliki gazeti la udaku la the Enquirer kuthibitisha pasi na shaka uwepo Trump katika mipango ya kuficha habari

Kisheria Trump hata kama akipatikana na hatia, akiwa Rais hawezi kushtakiwa na hivyo muda wa kuchukua hatua za kisheria 'statute of limitations' inaweza kumlinda siku za baadaye

Tatizo ni kuwa Cohen na David Packer wanatoa ushirikiano kwa wachunguzi.

Cohen anajua deal nyingi za Trump sasa haijulikani mwisho wa kauli zake utazaa nini

Kwa mtazamo wa haraka suala la makahaba halionekani kuwa tatizo kubwa

Tatizo ni wahusika hasa Michael Cohen anyeingia katika uchunguzi wa maeneo mengine

Mathalan, Cohen alikuwa katika mkutano wa June 21 Trump Tower wakiwemo Don Jr, Kushner

Haieleweki mkutano wa kupokea 'dirty za Clinton' uliandaliwa vipi na Warusi waliingia vipi.

Familia ya Trump inahusishwa na Mkutano mkuu wa Republicans wakiwemo maafisa wa Russia

Hofu kubwa ya Trump ni kuhusu 'kumwagwa' kwa habari nyingi zinazomhusu na uwezekano wa wanafamilia wake kuhusishwa moja kwa moja na huenda kushtakiwa

Rais Trump ana hofu nyingine, miongoni mwa watu wa karibu, 16 wamesema uongo kuhusu Russia na wanatoa ushirikiano kwa Mueller akiwemo Mhasibu Mkuu wa Trump Org. miaka 40

Kuhusu ''Russia collusion' hakuna ajuaye Mueller ana nini kwasababu taarifa haijatoka

Rais Trump ana kila sababu za kutweta, hoja ipo mezani kwake, kila upande unaendelea kubana

Wapo wanaosema 'Russia collusion' ipo wapi? Swali hili linajibu rahisi, Mueller hajatoa taarifa yoyote na hakuna chombo kingine chochote kilichosema lolote kuhusu hilo hadi muda huu

Jambo moja watu wanasahau, uchunguzi siku zote huanza na jambo moja linaloweza kupanuka na kuzaa jingine. Rais Bill Clinton anajua hili vema.

Rais Trump anajua pia ndiyo maana anaweweseka, si kwa Russia collusion bali kwa mambo mengi, mfano, kwanini amekuwa mnyenyekevu kwa Rais Putin, Kwanini amegeuka kuwa msemaji wa MBS n.k. na tayari yameanza kuingia anga asizotaka

Tusemezane
 
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Messages
9,976
Likes
8,299
Points
280
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined May 31, 2008
9,976 8,299 280
Trump anaendelea kuelekea kutimiza ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeini.
Ha ha haaa, ukuta nao karibu unaisha ukiwa umelipiwa na Mexico! Hakuna Rais amewahi kuchukiwa na Wamarekani kama Rais Donald Trump! Hata yeye anajua siku zake zinayoyoma na anaonesha dalili zote za kuchanganyikiwa. Hakuwahi kujikuta katika wakati mgumu na hali ngumu kama alipo sasa. Hakujua kazi ya Urais ni ngumu kiasi hicho na unaambiwa usiku hata usingizi hapati...ila ni kweli Trump, ingawa mjinga ana roho ngumu kwani angekuwa binadamu wa kawaida angeshajiuzulu zamani.
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
"Mag3, post: 29652471, member: 10873"]ukuta nao karibu unaisha ukiwa umelipiwa na Mexico!
Mkuu hili la ukuta linafurahisha sana. Kila anapoulizwa kwanini anadai pesa wakati alisema Mexico watalipa, jibu limekuwa 'wanalipia kupitia mkataba wa USMCA au NAFTA.
Hakuna pesa yoyote inayoonekana katika ''coffer'.

Chuck-Pelosi walipokwenda WH alijikuta anajitia 'kitanzi' cha 'government shut down'
Ukuta anaosema ulikuwepo kuanzia Bush na Obama ingawa anaaminisha wafuasi wake anajenga na unapanda

Ujanja huo ndio ameutumia kwa Obamacare. Baada ya kushindwa katika congress, sasa anategemea hukumu ya mahakama. Kitu wengi hawaelewi ni kuwa mahakama ya Texas imetoa hukumu na siyo supreme court
Itachukua muda mrefu na wala haina gurantee kwamba SC ita favor maamuzi ya awali

Kama itatoea SC wakaamua, hiyo si repeal and replace aliyosema.

Kuna mambo mawili ya kuangalia ktk hali hiyo
1. Lazima Dems watashiriki kuandika kwani ndio wenye house.

Pelosi ni pioneer of Obamacare, sijui kama atakubali anything less than the same.
Hata Trump anaelewa hilo na ni moja ya consequence za midterm elections

2. Midterm elections iliyoondoa 40 GOP na kuna moja 'itarudiwa' ilikuwa na madhara kwa Trump
Issue kubwa iliosababisha Republicans upoteza ni Health Care
Iliwalazimu hata House rep wa GOP wabadili msimamo na kusema watalinda 'pre existing conditions'

Kwa mtazamo huo, uamuzi wa SC utakuwa na athari kwa Republicans kuliko Dems
Obamacare ilipoanza ilionekana kitu kibaya, kwasasa ni 'hot cake' licha ya kuhujumiwa

Kwa maneno mengine SC ikifuta Obamacare, millions watatupwa nje ya Healthcare, hiyo itakuwa catalyst katika uchaguzi mkuu. GOP watakuwa na wakati mgumu sana kueleza ni kwanini

Hivyo uamuzi wa Jaji wa si mzuri kwa GOP , ni mzuri kwa Dems kwasababu unawalinda na lawama

Kwa upande mwingine, kuna article moja nadhani NY times ikionyesha organization zote zilizowahi kusimamiwa na Trump zinachunguzwa. Kuanzia Trump Organization, University, Campaign, Transition na sasa Admin

Kwa nyaraka za leo zilizotolewa, Flynn na Cohen wanamweka mahali pagumu sana

Rud Gulian sasa amebadili msimamo kutoka 'hakuna collusion, kwenda collusion si crime
Trump kabanwa kutoka kila kona si Russia pekee, huko kwa makahaba na organization zake

Kuna kufuatiliwa kwanini ni mnenyekevu sana kwa Putin na MBS! Hapo wenyewe wanasema 'follow the money'
Hofu yake ni kwa wanawe, kama si Kushner , ni Don au Ivanka. Ana hofu mmoja wao atadakwa
 
TUJITEGEMEE

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Messages
13,369
Likes
5,151
Points
280
TUJITEGEMEE

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2010
13,369 5,151 280
The British ex-spy who authored the infamous dossier alleging collusion between Donald Trump and the Kremlin said one of his goals was to give Hillary Clinton legal basis to challenge the 2016 election results.

Christopher Steele’s salacious 17-page report was commissioned by Fusion GPS , a firm connected to Clinton’s campaign.“Based on that advice, parties such as the Democratic National Committee and HFACC Inc. (also known as ‘Hillary for America’) could consider steps they would be legally entitled to take to challenge the validity of the outcome of that election,” Steele wrote in recently unsealed declaration that was published by the Washington Times.

Trump-Russia dossier was created so Clinton could challenge 2016 election results – Steele
Steele dossier’s main claims ‘likely false,’ admits journalist who helped launch Russiagate
====
Ukweli utajulikana.
 
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Messages
9,976
Likes
8,299
Points
280
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined May 31, 2008
9,976 8,299 280
The British ex-spy who authored the infamous dossier alleging collusion between Donald Trump and the Kremlin said one of his goals was to give Hillary Clinton legal basis to challenge the 2016 election results.

Christopher Steele’s salacious 17-page report was commissioned by Fusion GPS , a firm connected to Clinton’s campaign.“Based on that advice, parties such as the Democratic National Committee and HFACC Inc. (also known as ‘Hillary for America’) could consider steps they would be legally entitled to take to challenge the validity of the outcome of that election,” Steele wrote in recently unsealed declaration that was published by the Washington Times.

Trump-Russia dossier was created so Clinton could challenge 2016 election results – Steele
Steele dossier’s main claims ‘likely false,’ admits journalist who helped launch Russiagate
====
Ukweli utajulikana.
Usiku wa kuamkia leo Trump hakulala hata chembe, amekesha kwenye twitter akipayuka hovyo kama vile kachanganyikiwa. Kwa kweli taratibu hata rafiki zake wa karibu waliokuwa wakimtetea sasa wanaanza kumshtukia na hii ni inatokea kabla hata Congress mpya kuanza kazi mwakani. TUJITEGEMEE ingawa kwa sasa mataifa haya mawili, Tanzania na Marekani, yana viongozi wanaoshabahiana kitabia, kikauli na kimatendo, tofauti kubwa ni kwamba moja yuko wao juu ya Katiba na mwingine yuko chini ya Katiba.
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
TRUMP FOUNDATION NA MADUDU YAKE
YAVUNJWA NA MWANASHERIA MKUU WA NY

Wakati wa kampeni Rais Trump akiwa mgombea alihoji sana kuhusu Clinton foundation akiihusisha na madudu
Licha ya kuchunguzwa, Trump aliendelea kutumia hoja hiyo kushawishi wapiga kura

Bandiko #714 tulieleza mlolongo wa taasisi alizoongozwa Bw Trump ambazo sasa zinachunguzwa
Trump foundation, Trump University(walishamalizana), Trump kampeni, Transition, Inaugural committee na Russia

Leo AG wa NY ameifunga rasmi foundation yake akiieleza kama ' chaka la madudu' lililotumiwa kwa deal
Kuifunga kutapunguza ukali katika sheria, hata hivyo, wahusika wakiwemo wanawe wataendelea kuchunguzwa

Kufungwa kwa foundation si tatizo kwa mfanyabiashara kama Trump mwenye deal za kutosha
Tatizo ni kuwa itabidi kodi 'tax' zake ziifuatiliwe, kitu alichogoma kwa muda mrefu
Kesi ya foundation inaweza isha kwa

MICHAEL FLYNN
Hukumu yake kwa kuidanganya FBI ilitarajiwa leo. Kutokana na maelezo ya mawakili wake, hakimu alitoa 'ofa' ya kuiahirisha wakajipange kwani kifungo kilikuwa kinanukia.
Hata Mueller alipota asipewe adhabu kwa kutoa taarifa, ushahidi ulimlazimu hakimu kumkemea na 'kurushia taulo'

Flynn aliidanganya FBI licha ya kwamba taasisi hiyo ilikuwa na kila ushahidi wa nyaraka na sauti akiwasiliana na watu mbali mbali akiwemo balozi wa Russia bw Kislyak. Flynn alijichanganya kwa kutoa taarifa za uongo

MUELLER ASHINDA MAHAKAMANI
Kesi iliokuwa mahakamani kuhusu kuitishwa kwa nyaraka za kampuni ya kigeni kwa kisheria imeisha kwa Jaji kuamuru kampuni hiyo itoe nyaraka. Hata ya zuio ya mahakama 'sealed' haikueleza ni kampuni gani
Hii si habari njema kwa Trump. Kampuni zenye nyeti sasa zinalazimika kuleta nyaraka

RUD GIULIANI AADHIRIKA
Yule mwanasheria na mpiga debe mzuri wa Trump, meya wa zamani wa NY Bw Giulian alisikika katika TV ya FOX akishadidia kuwa Trump hakuhusika na mpango wa ujenzi wa Trump Tower Russia
Kauli hiyo imekuwa wimbo wahusika wakisema nyaraka iliyokuwepo haikusainiwa, hivyo hakukuwa na mpango
TV imepata nyaraka aliyosaini Trump kuhusiana na ujenzi wa Trump Tower Russia

MASOKO YA YUMBA
Masoko ya mitaji nayo yameanza kuyumba kwa kupoteza point nyingi.
Inaelezwa ni mwezi Dec ni mbaya tokea great depression ilipotokea.
Kuangauka kwa masoko si kigezo cha uchumi kuyumba
Hata hivyo Rais Trump alipigia sana upatu kama kigezo cha uchumi licha ya kurithi kutoka kwa Obama
Kwa mantiko hiyo, kudorora kwa uchumi au kuangauka kwa masoko kunaangukia mikononi mwake

Ukuta unabana na hali ya bw Trump inazidi kuwa ya utata huku aki'tweet' kwa kuparaganyika

Tusemezane
 
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Messages
9,976
Likes
8,299
Points
280
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined May 31, 2008
9,976 8,299 280
Breaking News: The walls are closing in on Donald Trump and now he appears to be losing it...will the 25th amendment be invoked?
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
KIZUNGU ZUNGU CHAKUMBA VIUNGA VYA DC
'' WHEELS ARE COMING OFF''

Viunga vya DC vina taharuki ya kufunga serikali 'gov shut down' kwa kutoafikiana kati ya Congress na WH kuhusu kurefu muafaka serikali ikiwa na bajeti hadi mwezi wa 2

Mvutano upo kati ya WH na Congress na siyo Dems na GOP
Rais Trump katika mkutano na viongozi wa Dems alisema,yu tayari kufunga serikali kama pesa za ukuta 'wall' hazitatolewa. Dems wanasema si busara, wafanyakazi wa umma na taasisi nyeti hawatakuwa na mishahara.
Rais Trump kwa kiburi akasema anachukua dhamana ya tatizo hilo

Hadi jana Republicans walimsihi alegeze msimamo na kukubali kiduchu cha kuendeleza ujenz uliopo
Kiasi hicho si cha kujenga 'big 6'' wall with door' bali kuweka akabadili msimamo kutoka ukuta hadi 'uzio'

Hii ni baada ya watu kumuuliza, ule ukuta utakalopiwa na Mexico haupaswi kulipiwa na kodi za Raia wa US
Hivyo atekeleza ahadi zake ambazo hapa JF tulishasema ni ndoto

Vyombo vya wahafidhina vimemjia juu akabadili msimamo wa mapendekezo ya awali ya pande zote

Haieleweki kama senate itapitisha mswada unaohusisha ukuta kwani inahitaji 60 na siyo majority
Uwezekano wa serikali kufunga shughuli hapo kesho ni 99%

MATTIS AACHIA NGAZI

Waziri wa ulinzi Gen Mattis ameungana na Gen Kelly na HR McMaster kuachia ngazi leo.
Rais Trump ali tweet ''Mattis anastaafu'', ukweli ni kuwa alishastaafu.
Kwa kuelewa upotoshaji Mattis kaweka wazi barua ya kujiuzulu ikionyesha kutokubaliana na tangazo la Tweet la kuondoa askari 2000 kutoka Syria miongoni mwa maduku duku mengi aliyokuwa nayo

Tangazo hilo liliudhi wengi hasa Republicans, likitolewa na Trump bila mawasiliano na vyombo vya usalama
Mzee aliamka kutoka katika Pajama akavaa suti na kutoa tangazo

Gen Mattis alikwenda kumshawishi abadili uamuzi, Trump akagoma na hapo hapo kupewa barua ya kujiuzulu

Mattis anajulikana kama 'adult in the room' hasa wakati Rais Trump anapojidhihiri kama kinda au toto tundu

Kutimka kwa Mattis kumeleta taharuki viunga vya DC, wengi wakiuona mkono wa tweet hatari kuliko ilivyodhaniwa

Kinachoshangaza, Trump alimshambulia Obama kwa kutoingilia mgogoro wa Syria ambao leo anachomoa

Kuondoa majeshi Syria kwa kisingizio cha kuishinda ISIS kinaacha washirika wakiwa hawajui nini la kufanya

Wakati huo huo Russia na Iran wanabaki Syria wakitamba na kusigishana na mkiwa Israel

Kwa jinsi kuta zinavyofunga na kubana kutokana na kuyumba Administration, Uchunguzi wa Russia, tumbuiko la makahaba, kashfa za taasisi zake, kuta zinafunga kwa kasi zikibana kulia kushoto mbele nyuma

Tusemezane
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
GOV SHUT DOWN IKIJULIKANA KAMA TRUMP SHUT DOWN
MWINGINE AACHIA NGAZI BAADA YA GEN MATTIS

Seneti imeshindwa kuafikiana kuhusu bajeti ya muda na hivyo baadhi ya shughuli za serikali kuathirika
Hii ni kutokana na Rais Trump kubadili mwelekeo dakika za mwisho alipofikishiwa mswada na maseneta

Wazungumzaji wa radio za mrengo wa kulia zinazowakilisha wahafidhina akina Rush Limbaugh, Bill O'Reily,
Laura Ingaham, Sean Hannity na wengine kumjia juu Trump wakisema 'amesarenda ujenzi wa wall''

Wazungumazaji hao walisema hiyo ni ahadi ya uchaguzi na kusarenda ni kupoteza wapiga kura

Hata alipofikishiwa mswada uliokuwa na Bilioni 1.3 dollar kuimarisha ukuta, Trump alikataa akidai zaidi
Wakati huo huo Dems wakisema ujenzi wa uzio ni muafaka si ukuta kama anavyosema Trump

Kutokana na kushindwa kuafikiana serikali imefunga baadhi ya shughuli kwa kukosa Bajeti hadi itakapoamuliwa

Majadiliano yanaendelea katika viunga vya DC kukiwa na mtanziko mkali baina ya Seneti na WH

Hayo yakiendelea, kujiuzulu kwa Gen Mattis waziri wa ulinzi na kuleta kishindo kikibuwa, mwangi wake haujatulia.

Aliyekuwa kiongozi wa US katika harakati za kutokomeza ISIS bwana Brett McGurks naye amejiuzulu
Hii ni kufuatia hatua ya Rais Trump kutangaza kuondoa askari takribani 2000 kutoka Syria

Kauli hiyo aliyoitoa kwa tweet imeudhi maseneta, viongozi wa zama na wawakilishi wa mabawa yote
Ni kauli inayoonekana ya hovyo na hatari ikiweka ulinzi na Usalama wa US njia panda

Tayari kuna wanaodai Rais ameshindwa majukumu na hivyo katiba iangaliwe kwa jicho mujarabu
Chagizo kubwa ni kutokana na mazonge zonge yasiyoisha na yasiyo na uelekeo ya bwana Trump

Masoko ya mitaji yamemaliza mwaka kwa rekodi mbaya zaidi katika miaka zaidi ya 10.
Hii ina maana, hata wakati wa mdororo wa uchumi aliokabidhiwa Obama rekodi ya masoko ilikuwa ni nzuri

Katika kutoelewa taratibu, Rais Trump amemjia juu gavana wa reserve bank kwa alichodai kuongeza interest rate.

Trump haelewi kuwa interest rate inapoongezwa au kupunguzwa ni kutokana na sababu za kitaalamu
Na kwamba kitengo hicho cha ''benki kuu'' hakina uhusiano na mambo ya kisiasa

Kana kwamba haitoshi, Trump ameiweka kamati ya Republicans wanaotaka kumhoji AG Loretta Lynch

Lynch alikutana na Bill Clinton uwanja wa ndege wakati Hillary akichunguzwa, kitu kinachoonekana ni kinyume
Kamati ya inayoongozwa na GOP inafanya kazi kabla ya kukabidhi kwa Dems wakitafuta ''mchawi' wa kutoka nae

Rais Trump naye kakutana na Act AG Whitaker akimkemea kuhusu suala la Michael Cohen
Trump alitaraji ingalikuwa rahisi kwa Whitaker kufutilia mbali uchunguzi wa Russia na Mueller

Whitaker anajikuta katika Lindi la sheria huku DOJ ikiwa imejizatiti ikiwa kutakuwa na jaribio
Kwa kitendo hicho cha Trump, nguvu ya kamati ya Bunge inatoweka kwani inaonekana ni double standard

Tusemezane
 
Mlenge

Mlenge

Verified Member
Joined
Oct 31, 2006
Messages
542
Likes
279
Points
80
Mlenge

Mlenge

Verified Member
Joined Oct 31, 2006
542 279 80
GOV SHUT DOWN IKIJULIKANA KAMA TRUMP SHUT DOWN
MWINGINE AACHIA NGAZI BAADA YA GEN MATTIS

Seneti imeshindwa kuafikiana kuhusu bajeti ya muda na hivyo baadhi ya shughuli za serikali kuathirika
Hii ni kutokana na Rais Trump kubadili mwelekeo dakika za mwisho alipofikishiwa mswada na maseneta

...

Whitaker anajikuta katika Lindi la sheria huku DOJ ikiwa imejizatiti ikiwa kutakuwa na jaribio
Kwa kitendo hicho cha Trump, nguvu ya kamati ya Bunge inatoweka kwani inaonekana ni double standard

Tusemezane
Marekani ni nchi inayopitia katika changamoto anuai. Nadhani hakuna changamoto kubwa kwa Marekani kama:

1. Ukubwa wa deni la taifa. Toka binadamu waweko kwenye dunia hii, rekodi zinaonyesha deni la taifa la Marekani ni kubwa kuliko taifa lolote lililowahi kuwapo duniani. Kimahesabu, nasikia deni hilo halilipiki, na itabidi Serekali ya Marekani ikatae kulipa baadhi ya madeni (default)..

2. Nakisi ya bajeti ya taifa. Marekani inatumia fedha nyingi kuliko inazokusanya kwa mwaka, na hivyo kuwa na nakisi kwenye bajeti zake.

3. Ukichanganya changamoto na. 1 na na. 2 hapo juu, utaona kwamba huu ulikuwa ni wakati wa kuchukua hatua kali za kiuchumi (austerity measures) zikiwa ni pamoja na kuimarisha matumizi ya sarafu ya Dola ya Marekani dunia nzima, na kuendeleza matumizi ya SWIFT na miundombinu mingine inayofanya miamala baina ya mabenki duniani kupitishiwa Marekani. Hizo politiki zingine zote ni sawa na kupiga zumari wakati Roma inawaka moto.
 

Forum statistics

Threads 1,250,884
Members 481,523
Posts 29,749,538