Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

Breaking News: Huko Marekani kumekuchaa ...Donald Trump aumbuka! Ilikuwa ni swala la muda tu na sasa la kuvunda halina tena cha ubani! Asie na mwana aeleke jiwe!

Januari 6, 2017 wiki mbili kabla ya kuapishwa, Donald Trump aliishapewa ushahidi wa jinsi uchaguzi wa Marekani ulivyoingiliwa na Putin wa Urusi kumsaidia!

giphy.gif

Hii ina maana siku zote hizi ukweli anaujua ila amekuwa akizuga tu akijitahidi kuficha ukweli na kuishia kumtukana kila aliyehoji ushirika wake na Warusi!
 
MKUTANO WA HELSINSIKI UMEJENGA 'UZIO' KWA MUELLER
MASAA 48 YALIYOPITA YAMEFUNGUA MENGI

Uchunguzi wa Russia uliendelea kukiwa na harakati za kupiga kombora usitishwe
Kamati za bunge zimejikita kuwahoji Strzok na Page ili kupata uhalali wa kumaliza uchunguzi

Katika mahojiano ya awali ya ndani ya kamati yasiyo wazi Strzok alieleza mambo ambayo kamati inayoongozwa na Republicans haitaki kuyaweka wazi. Katika mahojiano ya wazi, ilikuwa wazi Strzok 'alilinda' maslahi ya kikazi kwa Rais Trump, na kumwendea kombo Hillary

Hata hivyo, Peter amekiri text zake zilikuwa na makosa kwa kuzingatia nafasi yake

Jitihada za Republicans zikiongozwa na Trey Gowdy na Nunes zimeingia nyongo wiki hii
Taarifa ya Rais Trump na Putin kutoka mkutano wa Helsinki umelowesha jamvi la Republicans

Kwanza, Rais Putin amekiri alitaka Trump ashinde uchaguzi kinyume na kauli za GOP

Pili, Rais Trump alilinganisha vyombo vyake vya ulinzi (Intel comm) na Russia.

Hili limewatibua wengi wakiwemo Republicans na kulazimisha Trump kusahihisha kauli zake kwa siku mbili mfululizo bila mafanikio ikizingatiwa ushahidi wa Technology upo wazi

Rais Trump akasema anakubali 'ofa' nzuri ya Russia kuhusu kbadilishana majasusi wa Russia walioingilia chaguzi na wale wa Marekani wanaodaiwa na Russia

Hoja ilitolewa na Rais Trump akijua ni suala gumu kutekelezwa na ilikuwa 'cover up' ya majasusi wake. Putin alitambua Marekani haiwezi kumtoa Balozi wake Michael McFaul anayetuhumiwa na Mfanyabiashara William Browder na Michael Steel

Russia inawatuhumu kwa kuchota pesa na kumchangia mgombea Hillary Clinton

Madai hayo ni mapya kwa namna moja na yanazua maswali.
Michango ya kampeni kwa Marekani ni suala la wazi, hivyo, kwa namna moja au nyingine majina yangeonekana.Hata kama yapo, suala hilo lingeshahojiwa na Republicans

WH inafikiria wazo la Putin, kwamba, limetoe Balozi wa US akahojiwe Moscow
Kauli hiyo imeshangaza wengi na kuendelea kumtenga na Republicans

Ni rahisi kusema kauli ni ya kijinga, nyuma ya kauli hiyo kuna mbinu anazotumia Trump
Mbinu hizo ni nzuri kwa muda lakini zinamweka mahali pabaya sana kwa uchunguzi wa Mueller unaondelea, kunapunguza nguvu ya Republicans wanaoona ni usaliti
Kwanini?

Inaendelea kwa kuangalia uhusiano wa Rais Putin, Balozi McFaul, Michael Steele na Bill Bwoder
 
MKUTANO WA HELISINKI NA UZIO WA MUELLER

Sehemu ya II

Mkutano umetia hofu kuhusu uhusiano wa Trump na Putin hasa kuhusu uchaguzi wa 2016
Trump amepingwa na watu kutoka mrengo wa Kulia, kushoto na kati kuhusu uzalendo wake

Inahojiwa nini kiliongelewa kati ya wawili hao ikizingatiwa kauli za uongo za Rais Trump
Kwasasa kuna jitihada za kutaka kujua nini hasa kilizungumziwa na iwapo Trump 'aliuza' nchi

Ni kutokana na jinsi alivyonywea kwa Rais Putin hata kuhojiwa ikiwa putin anakitu dhidi yake

Kwa mantiki hiyo, Rais Trump hawezi kumfukuza Mueller wala Dep AG Roseintsein kwasababu tayari watu wa mirengo yote wanaonyesha wasi wasi kuhusu mahusiano na Russia

Pili, Mabalozi wa Marekani huchaguliwa kwa 'vetting' ya juu na huwakilisha nchi yao
Kwa mkataba wa kidiplomasia kumrudisha Russia ni usaliti wa nchi na kwamba Russia wangeweza kumtimua au kumkataa ikiwa alitenda kinyume

Kumrudisha McFaul kuhojiwa Russia ni kichekesho na state dep imedharau kauli hiyo

Tatu, Bill Browder ni mfanyabiashara aliyehusika na sheria ya haki za binadamu ya ''Magnistsky act''. Jina limetokana na Mwanasheria Sergei Magnistsky aliyeuawa na utawala wa Putin na mwanasheria wa Browder

Browder mbali na kuhanikiza sheria ya Magnistsky , pia alihusika na uchunguzi ulioonyesha mamilioni ya pesa za Putin nje. Alikuwa ni Raia wa Marekani hata hivyo katika kukwepa kodi za uwekezaji nje 'foreign investment' alihamia UK miaka 29 iliyopita na sasa ni Raia

Marekani haiwezi kumrudisha bila kuhusisha UK . Kwa kuzingatia mauaji ya gesi yanayoendelea UK , huku Urusi ikinyooshewa vidole, hakuna uwezekano wa kurudishwa
Ombi la Putin halina maana kwasababu Trump hawezi kumtoa, bali Theresa May

Kuna majaribio ya kutumia Intepol kumrudisha Browder yaliyoshindwa kwasababu ya suala zima kubeba sura ya kisiasa na si uhalifu

Michael Steel alipewa kazi na Republican ya Opposition research kabla ya kutoswa na kuchukuliwa na Hillary Clinton. Aliyendika Dossier inahusiana na uchunguzi wa Mueller.

Si taarifa yote lakini dossier ina mambo yaliyohakikiwa kuhusiana na yanayofanyiwa kazi. Kumtoa akahojiwe Russia ni suala litakalochukua sura ya kisasi dhidi ya Mueller

Kwa kuelewa ukweli huo, mtu anaweza kujiuliza kwanini Putin anataka kisichowezekana?
Kwanini Trump anakubali kisichokubalika nchini kwake?

Tutaangalia bandiko lijalo


Inaendelea..
 
MKUTANO..
Sehemu ya II

Rais Trump ameweka sharti ili kukinga majasusi wake wasihojiwe Marekani.

Ni sharti analojua litamaliza madai ya Marekani kwa kuzingatia udhaifu wa Rais aliyepo
Wenyewe wanasema ni 'leverage katika negotiations'

Rais Trump anajua kumtoa Balozi kutaudhi Wamarekani.
Anachokifanya ni kutishia kuwa kama anashinikizwa kumtia presha alete majasusi naye yupo tayari kumtoa Balozi, anataka kuzima mjadala wa majasusi asibanwe kumkabili Trump

Swali la pili, je, Trump atafanikiwa? Je, Putin atafanikiwa?

Putin amefanikiwa hata kwa kufikiri WH inataka kumtoa mwanadiplomasia ahojiwe Russia!!!
Wazo hilo halingewezekana kwa kiongozi mwingine yoyote wa nchi ya Marekani

Trump hatafanikiwa.
Mahojiano ya Helsinki yamemfunua vibaya hata washirika wake kama akina Newt Gingrich na Wabunge wakimkemea na kuunga dots kuhusiana na mkutano maarufu wa Trump Tower

Mkutano ule ulimhusisha mwanadada Velstinistkaya, Donald Trump Jr na wengine 8
Mkutano ulihusisha Trump kampeni kupewa 'dirty' za Clinton na Russia

Akiwa katika ndege akirudi Marekani, Rais Trump alibadilisha kauli na kusema mkutano unahusiana na sheria ya Magnistsky ambayo kama tulivyosema inamhusisha Bill Browder

Hivyo kushauri Browder arejeshwe Russia japo haiwezekani, si raia, kunamhusisha Rais Trump na mkutano wa Trump Tower, Magnistsky na kuunganisha na madai ya Rais Putin

Tumalizie kwa kusema, baada ya Helsinki Rais Trump ameweza kuondoa uhalali wa kumtimua Mueller na Roseinstein. Ametengeneza doubts kwa mnyenyekevu kwa Rais Putin, akiwaendea kombo EU na nchi nyingine bila simeli wala haya

Swali wanalouliza wengi, iweje Rais Trump awe mwiba kwa washirika huku akiwa mnyenyekevu kwa Putin kupita kiasi? Ni kitu gani Putin alichonacho dhidi yake?

Trump anazidi kujenga mahusiano ya uchunguzi na mambo yanayojitokeza.

Tusemezane
 
Breaking News: Huko Marekani kumekuchaa ...Donald Trump aumbuka! Ilikuwa ni swala la muda tu na sasa la kuvunda halina tena cha ubani! Asie na mwana aeleke jiwe!

Januari 6, 2017 wiki mbili kabla ya kuapishwa, Donald Trump aliishapewa ushahidi wa jinsi uchaguzi wa Marekani ulivyoingiliwa na Putin wa Urusi kumsaidia!

Hii ina maana siku zote hizi ukweli anaujua ila amekuwa akizuga tu akijitahidi kuficha ukweli na kuishia kumtukana kila aliyehoji ushirika wake na Warusi!
Mkuu tulisema siku nyingi , ugomvi na Washington hautamsaidia
Karibuni amewaandamana akina Clapper, McCabe, Comey etc utamwacha pabaya.

Hawa wanajua siri nyingi na sheria ziliwazuia kusema.
Kutokana na mashambulizi habari zinavuja na kupoteza

Sasa inasemwa wazi Jan 6 alipewa white envelop ikiwa na seal.
Ndani kulikuwa na 'details na evidence' za kutosha.

Hili ni katika kumweleza jinsi gani mambo yalivyo na kwamba Mueller anaweza kuwa na mengi Ni katika kukanusha Witch hunt anayosema na pengine kumtahadharisha kwa siku zijazo

Update: Bandiko 624 tulisema mbinu ya kutaka kumpeleka Balozi kwa Russia anayoitumia ili kuua suala la majasusi haitafanikiwa.

Senate ime vote 98 kupinga balozi kurejeshwa
Yaani ni karipio kali sana na hata kushangaza, leo balozi wa US anapelekwa Kremlin?

Katika hali nyingine, Trump ana mipango ya kumkaribisha Putin Washington wakuu wa vyombo vya usalama wakiwa hawana habari.

Hali ya WH ina mikanganyiko mingi, hata hivyo kwa siasa za nje kafeli

Tusemezane
 
Mkuu tulisema siku nyingi , ugomvi na Washington hautamsaidia
Karibuni amewaandamana akina Clapper, McCabe, Comey etc utamwacha pabaya.
Mkuu Nguruvi3 na kama vile hiyo haitoshi...

Amini usiamini wakati umefika, kila siku habari mpya inayomuumbua Donald Trump itaibuka. Hii inafanywa kwa sababu wako watu ambao hata Trump angefanya nini, wapo naye. Unakumbuka alivyowahi kusema huko nyuma!

Alidai angeweza kusimama mtaani na kumpiga mtu risasi na bado watu wake hawangemwacha. Naam Robert Mueller analijua hili na ndiyo maana wanatoa dose kidogo kidogo taratibu kuwatayarisha washikaji wake kwa bomu ambalo litawaacha midomo wazi!

Aliyekuwa lawyer wake Michael Cohen kachoka...kasema basi kama ni keba keba. Amekaa na mwanahabari Rev Al Sharpton na kumwaga kila kitu. Yote aliyosema Mueller anayo na mashataka zaidi ya 50 tayari yameandaliwa dhidi ya Paul Monafort aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa kampeni wa Trump. Tusubiri makubwa...

Na leo Donald Trump kaumbukaaa...! Kanda za audio alizokuwa nazo the fixer, Michael Cohen, zaanza kutolewa taratibu. Sasa kila siku tusubiri kusoma/kusikia habari mpya.

The downfall ya Donald Trump yaanza...!
 
Karibuni amewaandamana akina Clapper, McCabe, Comey etc utamwacha pabaya
White House mulls revoking clearances of Trump-bashing officials
Wakiwemo hao...Clapper na wenzake...tuone jeuri yao wataipeleka wapi. Inasemekana clearence zinawasaidia kupata mshiko kwenye makampuni ya kutengeneza silaha kwa kuwa ma'board of directors'...Ndiyo maana wanaendeleza msigano wa US na Russia ili makampuni haya yapate faida kwa kuuza silaha kwa kisingizio cha kujihami. Pia clearence inawawezesha kusoma makabrasha ya 'intel secret' wakati tayari hawana tena wadhifa kwenye maeneo hayo.
 
Swali wanalouliza wengi, iweje Rais Trump awe mwiba kwa washirika huku akiwa mnyenyekevu kwa Putin kupita kiasi? Ni kitu gani Putin alichonacho dhidi yake?
Hili swali ni rahisi sana...wote hao EU officials na marais na viongozi wengi wa Ulaya...walikuwa hawamtaki Trump kuwa rais wa US na walionyesha wazi wazi kumuunga mkono H.R. Clinton. Trump naye hawezi kukuacha hivi hivi...na uzuri Trump anatekeleza ahadi zake bila kujari matokeo ya athari ya utekelezaji huo. Ki-ufupi Mpaka sasa Trump kafanikiwa kutekeleza ahadi zake kwa asilimia nyingi ingawa Democrat na wale (1%) wanamkwamisha!
 
WIKI KATIKA SIASA ZA US
KUTA ZINABANA KAMBI YA RAIS TRUMP. NI WIKI NGUMU

Baada ya kufeli mkutano wa Helisink na kulazimika kufanya masahihisho WH, hali haijatengemaa kwa Rais Trump
Ni wiki iliyojaa mawaa, kwa jicho kali inaonekana kuta zinabana hasa uchunguzi wa Russia

WH ilitangaza kuondoa 'security clearance' kwa wakuu wa zamani wa vyombo vya usalama, hatua ya kuwafunga midomo
Kosa lilianza kwa kuwataja Comey na McCabe ambao waliondolewa security clearance.
Ilionyesha kukosa umakini bali kuongozwa na jazba. Unaondoaje clearance isiyokuwepo?

Kwanini wakuu hao wanabaki na security clearance?

Siyo favor ya wakuu hao kupata access kwa intelligence document. Nyaraka za Intel hutolewa kwa umakini hata wabunge 'congress' wanaelezwa kwa kiasi. Si suala la clearance kumwezesha yoyote kuzipitia
Sababu ya kuachwa na security clearance ni kurahisisha mawasiliano pindi watakapohitaji kwa ushauri wa kazi za nyuma

Obama alimwacha Republican Robert Gate kama waziri wa ulinzi na ndiye alisimamia shughuli nzima ya Osama
Kazi hiyo haikuanza na Obama bali Clinton na kisha Bush mdogo. Waliotoa mwongozo ni maafisa wastaafu
Ieleweke kwamba clearance ni kwa faida ya uongozi uliopo madarakani, na una haki ya kuondoa kama utaona inafaa

TARIFF ZALETA TABU
Tariff alizoweka Rais Trump kwa Ulaya na China zimejibiwa kwa kisasi. Madhara yamewakumba wakulima wa US ambao bidhaa za mabilioni ya dola zimedoda. Katika kutuliza pressure Rais Trump ametoa billion 12 kama bail out wakulima
Pesa zitaidhinishwa na bunge wakihoji mantiki ya tariff. Trump amekutana na kiongozi wa EU kuweka mambo sawa.

Hata hivyo, hali haijatengemaa kwa China ambayo hununua bidhaa za Soya kwa Bilioni 12 ukilinganisha na bilioni 1.6 kwa EU
Kwa maneno mengine hata deal ya EU ikikamilika hakutakuwa na unafuu. Kuelekea midterm hilo ni tatizo, inamtia Trump pressure

Kana kwamba haitoshi, Mwanasheria wa Trump na msiri mkubwa 'fixer, Michael Cohen ameachia video inayomhusu Rais Trump na kahaba McDugal. Huyu ni kahaba mwingine tofauti na Stormy, katikati ya wawili hao yupo fixer Cohen

Hakuna kitu kikubwa zaidi ya kuthibitisha uongo wa Trump kuhusiana na mahusiano yake
Kwa sura nyingine ni dalili kuwa Cohen sasa ameachana na kambi ya Trump na ni vita kwa mbele

Inaendelea....
 
Sehemu ya II

FREEDOM CAUCUS YATISHIA KUMSHTAKI ROSENSTEIN
Kundi la wahafidhina la freedom caucus la Republican limetishia kumshtaki katika bunge deputy AG Roseintein
Freedom wanataka Rosenstein anayesimamia uchunguzi wa Mueller awape nyaraka za uchunguzi

Freedom caucus ina washirika wa Rais Trump na hiyo wanaitumia kama njia ya kujua uchunguzi umefikia wapi
Rosenstein amewapa nyaraka zilizokuwa na 'reduction' kama sheria inavyotaka, hata hivyo hawaridhiki

Kumshtaki (Impeach) kuna mtego, kwamba bunge halina imani naye na hivyo Rais Trump amuondoe

Kuondoka kutalazimisha kuwepo na uteuzi wa 'mtu' wa Trump na kumaliza uchunguzi wa Mueller
Hatua ya awali ya kupiga kura imeshindikana hadi september kutokana na kutoungwa mkono

Ili impeachment ikubalike, ni lazima senate ipitishe kwa 2/3. Hilo linaonekana kutokwezekana kwa kuangalia hali ilivyo
Taarifa ya kamati za seneti na ile ya House yenye freedom caucus zinatofautiana, seneti ikiunga mkono Mueller

MAMBO YAZIDI KUWA MAGUMU
Mhasibu wa siku nyingi wa Rais Trump ameitwa kuhojiwa. Huyu alitajwa katika mkanda uliohusu McDugal na Trump tulioeleza mwanzo
Mhasibu anaitia kambi ya Trump kiwewe, anajua mengi kuhusu fedha za makahaba, na hata kodi alizolipa Trump

Ni mtu aliyedumu na Trump kwa miaka zaidi ya 20 na hivyo kujua mengi kuhusu miamala ya fedha
Tunajua Rais Trump hajaonyesha kodi zake tangu akigombea. Hivyo chini ya kiapo, mhasibu ana wakati mgumu kidogo

Jioni hii Mwanasheria Cohen tuliyeeleza amesema atamweleza mchunguzi Mueller kuhusu mkutano wa June pale Trump Tower
Cohen anasema, Rais Trump alijulishwa kuhusu mkutano huo uliomhusisha mwanae na maafisa wa Russia
Mkutano huo una umuhimu sana kwani utata aliuzua Rais Trump kwa kubadili kauli na kusema hakuujua unatia hofu

Nini hasa kinaendelea? Tutafanya jumuisho la wiki bandiko lijalo
 
Sehemu ya III
Michael Cohen, mwanasheria wa Rais Trump hana jambo lolote kuhusu uchunguzi wa Russia
Kesi yake ilipelekwa south district ikitokea kwa Mueller kwaviile inaingiliana na mambo mengine ya kihalifu

Cohen anajua mengi kuhusu Trump kama mwanasheria wake, na hapo ndipo anaopingia katika suala la Russia collusion
Cohen yupo katika kesi na Stormy na McDougal, hata hivyo kwa kuwa msiri wa Trump, ni shahidi wa kutazamwa sana

Inasemekana kambi ya Trump inavujisha habari wanazohisi Cohen anazo ili kuvuruga ushahidi
Siku za nyuma walivujisha habari kutoka kwa Mueller. Ni mkakati mzuri wa kuvuruga ushahidi

Kuboronga kwa Rais Trump kule Helsinki na Sec Pompeo katika kamati ya bunge kumeendelea kuzua maswali
Kuna nini kimeongelewa kati ya Putin na Trump na kwanini Trump anaonekana kumwogopa Putin

Jaribio la freedom caucus kutaka impeachment ya Roseinstein nalo limechagiza jambo

Kwa ukaribu , ukitazama kwa undani, ''vita'' ya Rais Trump na maafisa wa usalama wa zamani, msiri Cohen, na kuitwa kwa Mhasibiu wake chini ya kiapo kunasema jambo muhimu. Kwamba, mzunguko na kuta zinazidi kubana

Haikuwa wiki ya amani kwa Rais Trump, kila jambo lilionekana kumweka pagumu, si kilimo , kesi za makahaba, washirika wake au uchunguzi wa Russia collusion

Tusemezane
 
Hili swali ni rahisi sana...wote hao EU officials na marais na viongozi wengi wa Ulaya...walikuwa hawamtaki Trump kuwa rais wa US na walionyesha wazi wazi kumuunga mkono H.R. Clinton. Trump naye hawezi kukuacha hivi hivi...na uzuri Trump anatekeleza ahadi zake bila kujari matokeo ya athari ya utekelezaji huo. Ki-ufupi Mpaka sasa Trump kafanikiwa kutekeleza ahadi zake kwa asilimia nyingi ingawa Democrat na wale (1%) wanamkwamisha!
TUJITEGEMEE, wakati mwingine nakushangaa kweli kweli, sijui habari zako unazipata kupitia propaganda za mtandao gani. Kumbuka huko Marekani watu hawakurupuki na hata ukishukiwa umetenda uhalifu wa aina gani unakuwa huru mpaka pale unapokuwa indicted na Grand Jury! Ahadi za Trump alizofanikiwa kuzitekeleza hazifiki hata asilimia 10%, amebakia tu kuhamisha magoli na kusema uongo (kuna daftari zima inaorodhesha uongo wake ndani ya siku 500 na ushee alizokaa madarakani)

Na kwa ufahamisho tu Trump ana hofu kweli kweli na ndio maana haishi kukurupuka na kuropoka hovyo kuficha mapungufu yake. Marekani ni tofauti ndugu yangu, naomba tu utulie, the walls are closing in around Trump na kupona kwake ni majaliwa tu lakini amini usiamini atapata taabu sana. Hivi sasa mhasibu wake wa mwaka mingi anayetayarisha tax return zake ameitwa kuhojiwa, tusubiri kushuhudia makubwa zaidi, kama angekuwa Rais wa nchi kama Tanzania raia wengi wangeshapoteza maisha.
 
Mkuu Mag3

Mkutano wa Helsinki umeondoa shaka watu kuhusu Uhusiano wa Russia na Trump

Kiongozi wa US alipowatupa Intel community yake under the Bus imeacha maswali mengi.
Ni kitu gani ambacho Putin anacho kiasi cha kumfanya Trump amnyenyekee?

Ni kitu gani alichonacho Putin kiasi cha Trump kuwadharau washirika wa G6, NATO na EU?
Hayo si maswali rahisi ''Leo yamekuwa rahisi sana!'' na majibu!

Mhasibu kaitwa kisheria chini ya kiapo, suala la tax return haliepukiki.
Huyu alifanya kazi kuanzia nyakati za Mzee wake. Hapa ndipo Trump anapoingiwa na kiwewe
Kwamba, kama tax return zisingekuwa na tatizo Trump angezitoa. Kuna nini hataki kionekane?

Hii yote ni baada ya Wamerekani kumshtukia kiongozi wao kwamba amekuwa 'compromised'
Marekani si mahali pa kukurupuka bila kuwa na ushahidi wa kutosha

Mwisho nisaidie kuhusu security clearance, kama ni kwa ajili ya ajira za wahusika baada ya kustaafu!
 
Mkuu Mag3
...Mwisho nisaidie kuhusu security clearance, kama ni kwa ajili ya ajira za wahusika baada ya kustaafu!
Mambo ni hivi, viongozi wote wakuu wastaafu walikuwa bado wanaweza kuombwa ushauri kuhusu mambo mbali mbali ya usalama yanayolikabili taifa la Marekani. Ili waweze kutoa huo ushauri ilibidi wawe na fursa ya kuweza kuona/kusoma mambo ya siri na kwa hali hiyo lazima waendelee kuwa na security clearance ili wakiombwa ushauri wawe wanajua mipango ya usalama nchini humo.

Kulingana na tamko la Rais Trump ni kwamba anataka wafutiwe hiyo clearance ili wasiweze kuona/kusoma tena hayo mambo ya siri. Hii haihusiani kabisa na ajira zao za sasa baada ya kustaafu na sana sana itawawezesha kutoa maoni yao kwa uhuru zaidi kama raia wengine. Ni kwamba tu hawataweza tena kufahamu mambo yanayojiri ndani ya idara kuu za usalama nchini humo.
 
"
Mag3, post: 27754552, member: 10873"]Mambo ni hivi, viongozi wote wakuu wastaafu walikuwa bado wanaweza kuombwa ushauri kuhusu mambo mbali mbali ya usalama yanayolikabili taifa la Marekani. Ili waweze kutoa huo ushauri ilibidi wawe na fursa ya kuweza kuona/kusoma mambo ya siri na kwa hali hiyo lazima waendelee kuwa na security clearance ili wakiombwa ushauri wawe wanajua mipango ya usalama nchini humo.
Haswaa! na zaidi ni kuwa, wakiombwa ushauri iwe rahisi wao kutoa kulingana na shauri husika haraka ndani ya vikao vya usalama
Kulingana na tamko la Rais Trump ni kwamba anataka wafutiwe hiyo clearance ili wasiweze kuona/kusoma tena hayo mambo ya siri. Hii haihusiani kabisa na ajira zao za sasa baada ya kustaafu na sana sana itawawezesha kutoa maoni yao kwa uhuru zaidi kama raia wengine. Ni kwamba tu hawataweza tena kufahamu mambo yanayojiri ndani ya idara kuu za usalama nchini humo.
Kuntu, nilidhani kuna kitu sielewi niliposoma mahali kuwa teuzi zao katika mashirika au makampuni zina pre-requisite ya security clearance ya serikali
 
WASHIRIKA WA TRUMP MATATANI

'KITANZI KINABANA, TEMBO ANANYEMELEA JUMBA JEUPE'

Kwa kipindi sasa yametokea mengi kuhusiana na siasa za Marekani hasa utawala wa Rais Trump

Wiki iliyokwisha ilikuwa timbwili la mwanadada Omarosa, mweusi aliyefanya kazi na Trump WH

Amarosa ana utata sana, kwanza, alikuwa mshabiki na mtumishi mtiifu wa Rais Trump
Mahusiano ya kikazi yalianza wakati wa 'apprentice', vipindi vya TV vya Trump

Mahusiano yamezorota na kulazimu kutimuliwa WH huku akibeba siri nyingi kifuani
Omarosa aliahidiwa kiasi cha dola 15,000 kwa mwezi ili anayamaze

Pesa ya nchi kama Marekani ina mahesabu, Omarosa akaamua kuandika kitabu.

Hadi sasa inaelezwa ameuza kopi zaidi ya 30,000 kwa wiki ya kwanza ya kitabu cha 'Unhinged'

Mtifuano na Trump ulianza wakati wa kunadi kitabu chake, huku Trump akimkejeli katika tweet
Ilifahamika Omarosa alimrekodi Trump na baadhi ya sauti zimewekwa wazi.

Kuna habari kuwa rekodi zaidi zipo. Hilo limemlazimu Rais Trump kuweka pingamizi akisema Omarosa amekiuka kitu kinachoitwa NDA (Non disclosure agreement)

Hata hivyo NDA haipo katika taratibu za WH na kesi inaendelea. Hilo limepunguza kasi kidogo

MICHAEL COHEN ATIA HATIANI
Mwanasheria aliyejulikana 'fixer' kwa mambo ya Trump naye alibadili kibao baada ya timu ya Trump kumtosa. Licha ya kuachia mikanda ya kurekodi, Cohen ametoa ushirikiano kwa wachunguzi.

Katika hati ya kiapo, Cohen ameweka wazi pesa za kuwalipa makahaba zilitokana na amri ya Rais Trump. Kumbuka kuna makahaba wawili, Stormy na McDougal

Tatizo si pesa wala malipo ya makahaba, tatizo ni jinsi na dhamira ya kuzitoa. Ni wazi zilitoka katika kufunika madhambi ya ufuska ya Rais Trump.

Pesa hizo hazikuanishwa katika sheria ya kampeni na hapo ndipo tatizo lilipo. Kesi ya makahaba imefumua tatizo la kukiuka taratibu za uchaguzi

Inaendelea...
 
Kama siyo misingi imara na thabiti ya mihimili ya utawala iliyowekwa nchini Marekani kulinda haki, uhuru na usawa si ajabu hiki kizazi chetu kingebahatika kushuhudia udikteta unavyozaliwa, kulelewa na kukomazwa. La kushangaza na kusikitisha dunia ni kama hali hii ingeweza kufanikiwa katika nchi ya Marekani (of all places!) na katika karne hii (of all times!) Kwa sasa dunia yote inafuatilia kwa makini...je Marekani, kimbilio la walioelemewa na mizigo ya uonevu, umasikini na ujinga, itapona?

Udikteta hauoti tu kama uyoga, huzaliwa, hulelewa, huwezeshwa na hukomazwa na jamii. Sehemu moja ya jamii ikikaribisha utawala wa manyanyaso na kuukubali kama sehemu ya maisha, udikteta hufunguliwa milango na, kama zimwi, hushamiri na kunawiri kwa damu ya jamii nzima. Kwa bahati nzuri nchini Marekani sehemu kubwa ya jamii ipo tayari kuhakikisha kufuli za chuma, zilizowekwa kulinda hatma ya taifa lao huru waliyoapa kuilinda, ziko salama na hazichezewi hovyo.
 
YANAYOJIRI SIASA ZA US
UTEZI WA JAJI WA MAHAKAMA KUU YA MAREKANI
''BOMU' LA DOJ, HATMA YA ROSENSTEIN NA MUELLER

Siasa za viunga vya Washington zimekuwa na mengi katika kipindi cha muda mfupi

Kumekuwepo na matoleo ya vitabu na maandiko kuhusu utawala wa Rais Trump
Yamekuwepo maafa ya vimbunga ya mwaka jana na mwaka huu
Kumekuwepo na uteuzi wa Jaji wa mahakama kuu ya Marekani n.k.

Tutayapitia kuangalia maeneo yenye utata zaidi na yatakayopanda duru za habari
Mfululizo wa vitabu na maadiko magazetini kuhusu utawala huu yametia shaka juu ya hatma ya Taifa hilo katika uongozi wa nchi. Yote yanaeleza kuyumba 'wobbling' kwa shughuli za kiutawala

Jambo hilo linachagizwa sana na uchunguzi wa Mueller unaozidi kulisogelea jumba jeupe kuliko ilivyotegemewa. Washirika wa Bwana Trump wa ndani wote wamekabiliwa na mashtaka wamebwaga manyanga na kujiungana kambi ya ''ushahidi'' kujinasua na dhahama.

Kujiunga huko kuna maana moja, mengi yasiyotakiwa kujulikani yatawekwa wazi

Watu wa karibu sana kama mwanasheria binafsi Bwana Cohen, na mwenyekiti wa kampeni bwana Manafort ni sehemu ya kundi la ndani lililoamua kurudi upande wa 'mashahidi'

Jitihada za rump na mshirika Rud Giullian kupiga mzinga uchunguzi zinagonga mwamba.
Kuna jitihada chache zilizobaki zinazoanza kuzaa matunda ya kuzima uchunguzi wa Mueller

Rais Trump amekuwa akimkashfu Attorney general Bw Sessions hadharani kumkatisha tamaa. Kama mtakumbuka, tumejadili sana kuhusu hili na kwamba kuondoka kwa bwana Sessions kutatoa fursa ya kuteua AG mwingine atakayeweza kuzima uchunguzi wa Mueller

Sessions kagoma kujiuzulu na Rais Trump amesema baada ya midterm Sessions ataondoka. Kuchelewa kuondoka kwa Sessions kuna tatizo, uchunguzi unaendelea kwa ukaribu zaidi.

Njia mbadala ni kumuondoa msimamizi deputy AG Rosenstein
Kumuondoa Rosenstein kutaleta hisia za kuzima uchunguzi, na hilo limekuwa kikwazo

Leo gazeti la NewYork timeslimeandika kuhusu yale yaliyosemwa katika magazeti soma hapa

Kwamba Rosenstein alishauri kutumika 25th ammendment ya katiba kumuondoa Bw. Trump madarakani. Habari imevujishwa kwa makusudi na mrengo wa kulia 'conservative' ambao kila siku kwa hutumia TV ya FOX wameshauri kutimuliwa kwake

Kutimuliwa kwa Rosenstein kutatoa nafasi ya uteuzi wa deputy AG mwingine atakayesimamia uchunguzi wa Mueller hadi AG atakapoondolewa.

Hii maana yake ni kuwa uchunguzi unaweza kufutwa na mteule deputy AG au AG mpya.

Habari hiyo ni njema kwa Bw Trump kwani itampa fursa ya kutekeleza azma yake

Je, azma hiyo itakuja bila maruwe ruwe au mizigo myuma yake?

Inaendelea.....
 
Sehemu ya pili.....
Kwa sababu zinazosemwa hakuna tatizo lakikatiba kumtimua deputy AG Sessions.
Kwamba lengo linatimia bila kuwa na msuguano au hisia za kutimuliwa ili kuzuia uchunguzi

Itategemea senate inasema nini ikiwa itatokea. Kwasasa senate inaongozwa na Republican kama majority na hilo linaweza kufanikiwa.

Hata hivyo,ndani ya siku si zaidi ya 50 kutakuwa na uchaguzi wa midterm wa house na senate. Hilo nalo linaweza kuwatia kiwewe wagombea wanaotarajiwa kuingia katika sanduku la kura

Fursa ya kuzima uchunguzi wa Mueller ipo katika siku 60.
Kwa kura za maoni inaelekea Democrats wanaweza kuchukua House na kwa tofauti ya kura 2 katika senate si rahisi kusema ipo salama kwa Republicans.

Hayo yatachagiza Republicans kumshauri Trump asitibue hali, kufanya hivyo kutakuwa tatizo

Senate na House wanamuogopa sana Trump. Kila aliyejaribu kutofautiana naye aliishia kushindwa katika kura za maoni ndani ya chama isipokuwa maeneo machache

Ni sahihi kusema Trump ndiye ana control Republicans na si kinyume chake.
Political base yake ni tiifu atakayekwenda kinyume na Trump anaweza kuwa na wakati mgumu

Kwa upande mwingine, kura za maoni zimekamilika na wagombea wa Republicans wanajulikana

Rais Trump akienda 'rogue' na kumfukuza Rosenstein inaweza kuwagharimu wagombea wa Republicans. Hilo litamrudi mwenyewe kwani kupoteza senate au House ni kukaribisha matatizo

Kwa mwenendo huo haijulikani nini atafanya Rais Trump dhidi ya Rosenstein au Sessions katika kipindi kuelekea uchaguzi wa midterm. Hatua yoyote atakayochukua inagharama zake

Uteuzi wa Jaji ,inaendelea....
 
Utawala wa Demokrasia unaoheshimu sheria na kulinda uhuru na haki ya mwananchi bila kutazama sura.

Donald J. Trump
✔ @realDonaldTrump

Avenatti is a third-rate lawyer who is good at making false
accusations
, like he did on me and like he is now doing on
Judge Brett Kavanaugh. He is just looking for attention and
doesn’t want people to look at his past record and relationships -
a total low-life!

Michael Avenatti
✔ @MichaelAvenatti

“False accusations?” Like those crimes your fixer Cohen pled to?
You are a habitual liar and complete narcissist who also is
a disgrace as a president and an embarrassment to our nation.

You are so inept that your “best and brightest” are Cohen and Giuliani.
Let’s go.

Raisi mwenye nguvu duniani lakini nchini mwake anapewa vidonge vyake kama mtu yeyote tu...sijui hapa kwetu ingekuwaje kwa huyo mwanasheria Avenatti.
 
Back
Top Bottom