Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

Alimshauri Trump kuhusu NK na mazungumzo, kitu ambacho Trump sasa amekubali tena bila kumshirikisha. Kuhusu Iran, Rex anamuuliza Trump, option ipi iliyopo mezani ?
Climate change, Rex aliyeongoza kampuni ya mafuta anakubali.

Kuhusu deep state unayosema, nina shaka kama kweli umeielewa ni nini
Mike Pompeo unafahamu ametokea wapi? Gina Haspel unajua ametokea wapi?
Unajua wamefanya nini siku za nyuma kiasi cha kutishia confirmation yao leo hii?

Mwisho, Trump alisema ana 'hire' smart people. Je, aliachukua deep state? Na Rex unaamini ni deep state? Mabadiliko anayofanya ni kutokana na teuzi zake mwenyewe! Huoni tatizo hapo mkuu
Nikiri kuwa sikupitia makablasha yangu vizuri kabla ya kuleta habari hii ya Rex. Na kuna details nyingi nilizi'overlook'! Nimekubali kukosolewa.
Pia na ungana na wamarekani wanaomshangaa rais wao kukaa kimya kuhusu hotuba ya kikakamavu ya Rais Putin. Yaani Trump alikosa hata mstari mmoja wa tweet kuzungumzia 'mkwara' wa Putin? Yaani hapa na mimi nimebaki sielewi? Sawa baada ya siku kama nne hivi Ndiyo Pentagon na DoD walitoa tamko lakini 'ilionekana' kabisa Walishtushwa na Tangazo la Putin la 'Sasa lazima wasikilize'.
 
AG -J.SESSIONS ATUPIWA 'kaa la moto'

mtakumbuka, tulieza nia ya Rais Tump kuwaondoa watu katika jitihada za kuua suala la Russia.
Jitihada zake za kumshambulia Andrew McCabe, deputy FBI, zilifanikiwa kwa Andrew kujiuzulu

Hata hivyo kikwazo kilichobaki ni AG Jeff Sessions.
Jitihada za kumtia kumdhalilisha, kumsumanga n.k. hazijafanikiwa kumshawishi aachie ngazi

Kumtimua kama ilivyo kwa Rex Tillerson kutahusishwa na Russia na kumweka mahali pagumu.
Kumwacha Sessions kunazuia uwepo wa AG mpya atakayeweza kumdhibiti Mueller

FBI wamemshauri AG Sessions amfukuze McCabe ambaye muda wake wa kustaafu rasmi ni Jumapili
Kumtimua kunamaanisha jambo moja, kwamba, atapoteza mafao ya miaka zaidi ya 20 ya utumishi

Kwavile McCabe alishaachia ngazi, kuna swali linaloweza kuulizwa, je, Trump anataka apoteze mafao?
Jibu ni hapana, Rais Trump hana interest na McCabe kwasababu hana impact yoyote

Kama ni hivyo ni kwanini mtumishi wa miaka 20 afukuzwe kazi akiwa tayari ameshajiuzulu?

McCabe anatumika kumtupia Sessions mzigo. Kwamba, Sessions akikataa kumtimua itatoa upenyo kwa Rais Trump kumtimua yeye, si kutokana na Russia bali alivyo handle suala la McCabe

Sessions ana njia moja ya kufanya ambayo ni kumtimua Andrew.

Hilo litapelekea kesi ya kwamba, Andrew anaweza kuwa na madai mahakamani.
Kufanya hivyo Sessions atabaki ingawa itamuumiza sana Trump, lengo ni Sessions kung'oka

Sessions akifanya kosa la kumsamehe McCabe, yeye atatimuliwa na Trump kwani fursa itakuwa wazi

Kumtimua Sessions kunaweza kusiwe na matokeo tofauti. Senate imeonya haina muda wa kumthibitisha AG na kama ikitokea inaweza kuwa ndani ya miezi 6. Kwa muda huo huenda Mueller atakuwa amemamliza

Pamoja hayo, suala la Russia na Sessions linaangaliwa sana hivyo kila mwenendo unafuatiliwa kwakaribu

Kaa la moto alililotupiwa Sessions analikumbatia kabla ya Jumatatu na hana njia lazima atoe maamuzi

Wakati huo huo , Bob Mueller ameitisha nyaraka kwa lazima kutoka Trump organization

Kuna nini anaangalia inabaki siri yake. Katika chunguzi za House intel, Senate intel, Judiciary comm n.k. hakuna inayomtia kiwewe Trump kama ya Mueller.

Tusemezane
 
ANDREW McCabe ATIMULIWA KAZI SIKU MOJA KABLA YA KUSTAAFU

Kama tulivyoeleza hapo juu, aliyekuwa deputy FBI wakati na baada ya James Comey amefukuzwa kazi
Kufukuzwa kwake kazi kunakuja siku moja kabla ya kustaafu ingawa alishaachia ngazi zaidi ya mwezi uliopita

Jeff Sessions amefanya kile ambacho Rais Trump amekishauri mara nyingi, kwamba Sessions afukuzwe kazi
Kwa muda mrefu, Trump na vyombo kama Fox vimemuandama sana Andrew McCabe

Kwa upande mwingine, Trump alimtega Sessions , mtego ambao umefyatuka kwa muda huu

McCabe hayupo katika utumishi hivyo impact yake ilikuwa ndogo.
Mtego kwamba Sessions angemuacha ili Trump amtimue yeye nao umekwenda kombo. Sababu ni hii;

Rais Trump hana sababu za kumfukuza Sessions tena, wakati Sessions hana influence kwa Russia investigations. Kama atamfukuza, moja kwa moja itakuwa ni suala la Russia, kitu ambacho ni tatizo kukifanya

Andrew McCabe amejibu kufukuzwa kwake akisema ni mwandamano dhidi yake unaoendeshwa na Trump
Amekana kutofanya jambo lolote baya ikiwa ni pamoja na kuvujisha habari za uchunguzi wa Clinton

Kuna sura nyingi katika sakata hili. Kwanza, mkakati wa kumtimua Sessions umekwama na hivyo Roseinstein ataendelea kuwa mkuu wa uchunguzi wa Russia. Trump na watu wake hawamtaki Roseinstein. Hakuna namna

Pili, katika watu walioshea habari za Trump kuhusu kutimuliwa kwa Comey ni McCabe.
James Comey alisema alipoombwa kuwa loyal na Trump, mtu aliyemtaarifu kuhusu hilo ni McCabe
Atakapotakiwa kusema lolote kuhusu Russia investigations, McCabe atawamaliza. Kama ikitokea

Tatu, kuna uwezekano hili limefanyika katika wiki ambayo Rais Trump ana wakati mgumu kuhusu mahusiano na kahaba Stormy wakati huo huo Mueller akiendea kombo kampuni yake 'Trump organization'

Habari hii inaweza kuonekana ni njia ya kufunika habari za kahaba na nyingine

Tatizo ni kuwa itachukua muda mfupi kuwepo katika mazungumzo, habari zingine zitarudi kama ilivyo
Mathalani, wiki nzima kumekuwa na habari za mitafaruku WH ikiwemo kumtimua Rex Tillerson

Ikasemekana HR McMaster na wengine watatimuliwa. Ilikuwa kuweka umma hewani na kuua habari za Stormy

Moja ya njia anazotumia Rais Trump ni 'distractions' kuondoa watu kwa kile asichokitaka na kubadili maongezi
Alichosahau ni kuwa huu ni muda wa ku-govern siyo kampeni, na mbinu hiyo inaonekana kutofanya kazi

Tusemezane
 
Kufukuzwa kwake kazi kunakuja siku moja kabla ya kustaafu ingawa alishaachia ngazi zaidi ya mwezi...
====
Hapa mwalimu unanichanganya ! McCabe alishaacha ngazi wakati huo huo tunaambiwa kafukuzwa masaa 26 kabla ya kustaafu. Ukiachia ngazi si unaenda kuchukua masurufu yako na kuondoka!? Ama Amerika nao wanatumia sheria ya" fao la kujitoa" Tanzania, kwamba mpaka ufikishe umri wa kustaafu ndiyo unapewa mafao yako ya uzeeni!?
- - - -
Taarifa nilizopata ni kuwa McCabe alikuwa likizo! Hivyo alikuwa hajaacha kazi.
 
Hapa mwalimu unanichanganya ! McCabe alishaacha ngazi wakati huo huo tunaambiwa kafukuzwa masaa 26 kabla ya kustaafu. Ukiachia ngazi si unaenda kuchukua masurufu yako na kuondoka!? Ama Amerika nao wanatumia sheria ya" fao la kujitoa" Tanzania, kwamba mpaka ufikishe umri wa kustaafu ndiyo unapewa mafao yako ya uzeeni!?
- - - -Taarifa nilizopata ni kuwa McCabe alikuwa likizo! Hivyo alikuwa hajaacha kazi.
Muda rasmi wa kustaafu ni Jumapili. Fuatilia habari kwa kina utabaini tofauti niisemayo.
 
RUSSIA PROBE YASHIKA KASI

RAIS TRUMP APATA KIWEWE, AWASHAMBULIA

Baada ya kufukuzwa kazi kwa McCabe, ilionekana habari njema kwa Trump kwa muda mfupi akiipongeza
Mwanasheria wake J.Dowd alikaririwa akisema ni wakati Deputy AG Roseinstein kufunga uchunguzi wa Mueller

Kauli ya Dowd ilionyesha wazi McCabe alitumika tu kama chanzo cha kuanzisha mjadala wa kumfuta Mueller
Ilikuwa kuwa kama 'to lay the ground' ili kumshinikiza Rosenstein amuondoe au afute Russia probe

Haikuchukua muda ikabainika McCabe aliitwa na Mueller kueleza alichokijua kuhusu kufukuzwa kwa J.Comey. Kumbuka, mbele ya kamati ya bunge, Comey alisema mtu aliyekuwa na habari kuhusu Rais Trump kumuomba 'loyal' ni McCabe. Sasa imebainika wote wawili, James na Andrew wameshea memo na Mueller

Hilo limemtia Trump hofu kwani suala la obstruction of justice linarudi ni bichi mbali na makando kando mengine. Hivyo, kumfukuza McCabe kumeamsha dude ingawa tayari alishaitwa na Mueller

Kiwewe kimezidi jana ambako Trump amewashambulia Comey na McCabe akisema 'memo yao ni fake' na kwamba Mueller hakupaswa kuendelea na uchunguzi kwasababu ulianzishwa na Comey kwa kutumia dossier fake na kwamba, katika timu ya Mueller wote ni Democrats

Hapa kuna kiwewe kwasababu memo ya Nunes iliyojibiwa na ile ya Adam shchiff wa Democrats inaonyesha kwa tarehe kwamba uchunguzi ulianza kabla ya Dossier na kwa uhakika aliyeleta tatizo ni afisa wa Trump aliyejulikana kwa Papodopoulous ambaye Trump alimkana kwa kumuita 'coffee boy' bila kujua ana mengi ayajuayo

Kiwewe kingine ni pale anaposema timu ya Mueller imeundwa na Democrats.
Mueller ni Republicans na alichaguliwa wakati wa Bush hadi Obama.
Deputy AG anayemsimamia bwana Roseinstein ni Republican aliyechaguliwa na Republican president, Trump

Kiwewe cha mfululizo wa tweets kimeamsha hisia ndani ya congress wengi wa maseneta wa wawakilishi wa Republican wakimuonya Trump kuhusu kumfukuza Mueller.
Sen, Graham amesema huenda huo ndio ukawa mwanzo wa mwisho wa Urais wa Trump

Jumapili jioni baada ya joto la kumpinga kupanda, WH imetoa kauli kuwa hakuna nia ya kumfukuza Mueller

Yote hayo yanakuja wakati Mueller akichunguza Trump organization kwa undani

Maswali yanayowasumbua wachunguzi wa mambo ni kuwa, ikiwa hakuna collusion na ikiwa hakuna baya alilotenda wakati wa kampeni,kwanini Rais Trump anaingiwa na kiwewe kikubwa kiasi hicho?

Kwanini asiache ukweli ukatamalaki ili hali akijua hana kosa lolote?

Hali ya mambo kwa upande wa mahaba nayo inamuelemea Rais Trump.
Kahaba Stormy anajiandaa kwa mahojiano tarehe 26 na ameahidi kuweka mambo wazi.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, WH imetishia kumshtaki na kudai fidia ya mamilioni kwa kuvunja mkataba 'Non disclosure agreement'

Hapa napo kuna mtego. Pesa dola 130,000 alizopewa Stormy usiku wa mkesha wa uchaguzi zilisemekana kutoka kwa mwanasheria wa Trump akidai Trump hakujua lolote kuhusu malipo hayo.

Katika hali ya kujichanganya wanasheria wa Trump wanatishia kumshataki Stormy na kudai fidia.

Kama Trump hakuhusika, iweje amshtaki Stormy? Timbwili lililivyo ni kati ya Stormy na mwanasheria aliyemlipa, katika mshtuko, Trump amejikuta kavutika na kuingia anga za kahaba mzoefu. Nini kitatokea, tutawajuza

Tusemezane
 
Muller siyo wa kumuamini...ni wa kati wa uongozi wake akiwa FBI head, aliridhia uongo kutumika kuishambulia Iraq. Hivyo hatuwezi kushangazwa na hiki anachojaribu kufanya kwa sasa dhidi ya Trump.

Reminder: Liberal hero Robert Mueller lied about Iraq’s non-existent WMDs (VIDEO)
Mkuu, hizi habari ni za RT. Kumbuka hawa ndio wali-mislead suala zima la uchaguzi

Lakini pia jaribu kwenda kwa upana na undani katika haya mambo

Mueller ni Republican, aliteuliwa na Bush na kuendelea na Obama.
Alipoteuliwa kuongoza Russia probe, pande zote zilikubaliana anayeweza kufanya kazi hiyo

Hadi sasa unaweza ona 'leaks' zilivyodhibitiwa na hakuna ajuaye kesho anakuja na nini
Habari zote zinazosikika za kuhojiwa,nyaraka n.k. ni retrospectively kuonyesha integrity yake

Pili, wenzetu wa kitu kinaitwa NSA ambayo wakuu wa vyombo kadhaa. Hawa ndio wenye dhima usemayo
Endapo ni suala la uongo, Hillary na Trump waliunga mkono vita ya Iraq

Unachokisoma wewe ni habari za propaganda, kama unafuatilia mjadala objectively ungetuelewa

Kikwazo kikubwa kwa Trump na suala la Russia ni Bob Mueller, siyo kamati za Bunge
Kamati za Bunge kama ya Nunes unaweza kusema ina integrity iliyobaki!

Tunakuonyesha mtiririko anaoutaka utokee ili aue suala la Russia.
Kwasasa kamati moja ya bunge inataka kumhoji AG Sessions kwa suala la McCabe.

Hapa wanaweza kumsaidia Trump ikiwa watamtaka Sessions ajiuzulu kama atakuwa ametenda sivyo.
Rudi nyuma kidogo usome mabandiko yanayomhusu McCabe

Hivyo RT wanataka ku discredit Mueller, mbioni kumwandama Deputy Rosenstein baada ya kummaliza McCabe. Nina uhakika huna habari kuwa Mueller, Rosenstein na McCabe ni Republican

RT ndio wale wale waliomhoji Michael Flynn ambaye sasa yupo matatizoni akikiri mwenyewe

Lakini ninapokushangaa ni hapo unaposema 'anachomfanyia Trump'!!!
Hebu eleza jamvi, kipi Mueller kamtendea ubaya Trump? Tafadhali tusaidie kwa hili

Mkuu haya si mambo mepesi, yanahitaji information za kutosha
 
Unachokisoma wewe ni habari za propaganda, kama unafuatilia mjadala objectively ungetuelewa
Mkuu, RT wanaweza kuwa wanaleta habari nzuri nzuri kuhusu Russia na habari mbaya mbaya kuhusu US, sawa. Lakini wakileta habari mbaya mbaya (ambazo unaziita propaganda) kuhusu US wanakupa na ushahidi. Ndiyo maana kama unakuwa na mashaka juu ya habari wanazotoa wametoa nafasi ya kuuliza zaidi kuhusu habari hizo. Na hili linathibitika katika kauli mbiu yao ya Uliza zaidi wao kwa kimombo wanaita "Question More". Sina hakika kama MSM (ambazo tuliambiwa na Trump kuwa ni wazalisha fake news) wanatoa fursa hiyo kwa walaji wa habari zao. Kibaya zaidi, wale wanaotetea uhuru wa habari wanafanya hila ya kila aina sababu ili kuua hiyo kitu ya 'Uhuru wa habari'. Kwa nini wasiwaache walaji wakachambua ipi ni habari ya kweli na nyingine si ya kweli endapo tu chombo cha habari hakivunji kanuni na sheria ? Uko wapi uhuru wa kuchagua, iko wapi demokrasia waienezayo?

Tena Kibaya zaidi haya yanafanywa na serikali ya Marekani (US), sasa kama RT inafanya propaganda kwa nini 'msikanushe' propaganda hizo? Hivi Mwalimu wangu na wewe unakubaliana na haya? Sasa hivi wana 'activate' FARA ( Foreign Agents Registration Act) ili kuiminya kabisa RT isiweze kuleta habari murua za kichambuzi kuhusu ulimwengu. Huo ni uhuru gani wa habari, uhuru gani wa kidemokrasia!? Ikifanya serikali ya Tanzania kudhibiti wanahabari tena wanaovunja kanuni halali na sheria zinazoiongoza tasnia ya habari 'mnakuja' juu kuwa huo ni ukiukwaji wa haki ya kupata taarifa. Akifanya US tena kwa 'kubumbabumba' uongo wa kuvunja kanuni na sheria ili chombo fulani huru kisipate nafasi sawia ya kuwahabirisha walimwengu mnakuwa kimya!! Hii si sawa.

When FARA is not far enough: US lawmakers invent new ways to brand RT as propaganda

Sidhani mwalimu wangu utakuwa kwenye 'koti pana' la US kuitawala dunia by hooks and Crooks! Ha ha haaa !
-------
Bila kuwa na mwanafunzi 'mtukutu/mdadisi darasa lako litaku'bore', najaribu kukufanya usi'bore'ke Mwalimu wangu. Mchana mwema Mwalimu.
 
TUJITEGEMEE maelezo yako hayajatueleza hoja, wala RT haijawa mada hata kidogo

Tumeuliza ' Mueller kamfanyia nini Trump kwa mujibu wako"?
Ni kweli hayajajibu hoja kuhusu Muller moja kwa moja, ila nilitaka kuweka taarifa sawa juu ya wewe, Mwalimu wangu, kuituhumu RT kuwa chombo cha Propaganda. Kwenye maelezo nilikuwa napinga hilo. Na kama RT tunakubaliana si chombo cha propaganda basi, hoja ya Muller kukosa 'credibility' kwa kukubali uzushi wa Iraq inakuwa na mashiko.

Hoja ya 'Muller kamfanya nini Trump'...Ni hivi hivi term of reference za Muller juu ya Trump zilihusisha suala la 'Daniella Stormy'? Kwenye uchunguzi wake, Muller, inasemekana anataka kumuhoji pia huyo muuza 'kikapo' juu ya kumuuzia Trump biashara hiyo. Muller alipewa maelekezo haya:

Rod Rosenstein’s letter (pdf) formally appointing Robert Mueller suggests the special counsel may have wide terms of reference.
He is authorised to investigate “any links and/or coordination between the Russian government and individuals associated with the campaign of President Donald Trump; and (ii) any matters that arose or may arise directly from the investigation”.

Source:Special counsel appointed to Trump-Russia investigation – as it happened
----
Taarifa za hivi punde,
House Intel Committee votes to end Russia probe - report
 
TUJITEGEMEE sina tatizo kama source zako za information ni RT.
Kwa wengine kuwa na different sources ni muhimu ili ku-balance information.

Kwasababu ya kukosa info , unaamini kwa dhati suala la Iraq lilikuwa jukumu la FBI!
Kuna Mtanzania naye kasema hivyo akitaja watu hatari, sioni ni jambo la kushangaza

Kwa taarifa,RT waliopigia debe release ya text za maafisa wa FBI,mwisho wake ni nini?
Ni hao RT walipigia debe release ya Nunes Memo, unajua mwisho wake ulikuwa ni nini?

Ukiangalia news za Fox, utaona ipo hoja ya Trump kumpongeza Putin.
Fox wanasema hata Obama alifanya hivyo.

Ni kweli wanachosema,haitoshi kubeba tu habari bila kuiangalia kwa mtazamo tofauti. Mazingira ya wakati ule hayaliangani na sasa ambako hata washauri wa Trump walimkataza asiseme.
Fox hawakuelezi hilo wala hawakuelezi kwanini Trump hataki kabisa kumgusa Putin

Unachotakiwa kuelewa si 'kumpongeza' bali kwanini kuna msuguano katika hoja hiyo
Hilo utaweza kulipata ukisikiliza au ukisoma habari mbali mbali kwa jicho angavu

Kwa hilo la RT sina mjadala , nilichotaka ni kukusaidia kuangalia mambo kwa upana wake
Muhimu, unapoleta hoja tusaidie kuinyumbulisha kwa urahisi ili nasi tuelewe.

Copy and paste kwakweli hazitusaidii ikiwa hakuna kujazia 'red meat'.

Kuwa na maoni au mtazamo tofauti ni jambo lenye afya, lakini argument zilenge kutusaidia kuelewa nini message na nini tunajifunza au kuelewa

Ukisoma terms of reference utaona mstari wa mwisho unasema nini
Sina uhakika kama Mueller atamhoji Stormy huenda hizo ni habari mpya kutoka RT

Kuhusu intel committee, tayari umeiona kwa jicho hilo bila kujiuliza ni partisan au bipartisan
Nunes memo ilisemwa ni ya intel comm, ikawepo ya Adam Schiff. Yaliyoendelea unayajua

Point ni kuwa don't pick up info without a pinch of salt.
Mwisho wa siku hutaweza kujibu au kutetea kile unachoeleza.

Na hapa nimalizie kwa kukuuliza, Mueller alikuwa mkuu wa FBI wakati wa vita ya Iraq. Nini ilikuwa role yake katika ku-influence vita hiyo?
 
WIKI KATIKA SIASA ZA US

MBINU HAZIFANY KAZI, KASHFA MFULULIZO

Wiki iliyokwisha kahaba Stormy alipata mshiriki mwingine anayedai kuwa na mahaba na Rais Trump
Wote wawili wamekuwa katika vyombo vya habari wakieleza mahusiano yao na mkuu wa nchi

Kimtazamo, madai hayana mashiko kisheria isipokuwa pale ambapo pesa zilizotumika kumlipa zinapohojiwa kama zilitoka katika kampeni na kwanini hazikuorodheshwa. Hapo tu

Kwa upande mwingine makahaba wanazidi kutia ufa kwenye ndoa ya Trump na Melanie
Hilo inamchukua mzee kwa kina ikizingatiwa aliwaita wapenzi wa Clinton wakati wa kampeni na kwamba alikuwa 'anachepuka' wakati mkewe akiwa ana kichanga

Jitihada za Rais Trump ni kuzifuta habari hizo katika mzungo wa habari za kashfa
Mbinu zake ni kubadilisha maongezi 'narratives' kwa kuweka kitu kitakachochukua nafasi zaidi

Mbinu hii tumeisema mara nyingi ilikuwa nzuri wakati wa kampeni alipowacharua wenzake wa Republican, hata hivyo kushindwa na media zimebaini hilo na kulisema wazi

Kumtimua SoS Tillerson kulijulikana na MSM muda mrefuTrump akiita fake news
Wakati ulipowadia akiandamwa na kashfa za uzinzi, alimtimua Rex kubadili maongezi
Mbinu haikufanya kazi

Kuweka tariff kwa nchi zinazoingiza aluminium ilikuwa ni distractions tu kwani aliilenga China bila kujua waingizaji wakubwa walikuwa Canada na Mexico.

Hilo likaleta hofu katika masoko ya vita ya biashara. Mbinu haikufanya kazi

Katika hali ya kushangaza kuna maongezi na China baada ya kuwatandika tariff na China kuahidi kulipa kisasi. Maongezi yanaendelea nyuma ya pazia

Majuzi mwanasheria wake John Dowd ameachia ngazi.
Hii ni baada ya Trump kupuuzia ushauri wa kutomshambulia Mueller hadharani.
Trump alifanya hivyo katika kubadili maongezi. Hikusaidia

Kamtimua mshauri wa ulinzi HR McMaster na kumweka J.Bolton katika wakati usiotarajiwa
Trump alijua litabadili maongezi . Mbinu haikufanya kazi, kashfa ya makahaba inarindima

Juzi tena katishia kutosaini mswada wa matumizi ambao ungepelekea gov shut down Baada ya masaa kadhaa kasaini. Yote ilikuwa kubadili maongezi. Mbinu haikufanikiwa

Leo kawatimua wana diplomasia wa Urusi, ni baada ya ushauri wa baraza lake la usalama kwamba lazima waungane na nchi za Ulaya kumwadhibu swahiba Trump.

Kiuhalisia hakupenda lakini hakuwa na namna
Nalo amelifanya Jumatatu kuua maongezi ya 60 minutes ya kahaba na Abderson Cooper

Wakati hayo yakiendelea, kuna maafisa wake wanahusishwa na kampuni ya Cambridge analytica iliyokuwa inafanya tafiti kwa niaba ya kampeni yake.

Tatizo hapa ni ushiriki wa 'wageni' katika kampeni za US
Lakini pia inasemwa, kachero mzoefu wa Russia alikuwa sehemu ya timu

Kwa muktadha huo, Mueller analitupia macho jambo hilo kwa ukaribu
Mueller kaorodhesha anayotaka waongee na Trump huku timu ya wanasheria ikisita sita

Kuondoka kwa Dowd, kiungo kati ya Trump legal team na Mueller ni pigo
Mkanganyiko unamweka pagumu. Makahaba wakiendelea na zogo, Mueller akifukua fukua

Hatua anazochukua kubadili maongezi ni za hatari.

Mfano, vita ya biashara na China si nzuri ikizingatiwa umuhimu wa China,Nkorea na Iran
Kwamba vikwazo vimewekwa kwa Nkorea si mwisho wa tatizo, China ina karata kubwa

Mbinu alizotumia siku za nyuma zinAkwama,anakwenda kila uchao na kila litokealo

Kutawala na kampeni ni vitu tofauti kabisa

Tusemezane
 
Kutawala na kampeni ni vitu tofauti kabisa

Tusemezane
Nje ya mada kidogo.
====
Nimesikitishwa na kitendo cha Marekani na EU kutangaza kufukuza wanadiplomasia wa Urusi (US kufukuza 60), wakati nchi ya Urusi inaomboleza vifo vya raia wake 64 waliofariki kwenye janga la moto ncho Urusi. Huu si utu hata kidogo. Tena wanawafukuza kwa sababu zisizo na ushahidi. Imenisikitisha sana.
 
SIASA ZA MAREKANI WIKI HII
SUALA LA KAHABA STORMY LAZUA BALAA KWA RAIS
UCHUNGUZI WA MUELLER UNAWEZA KUHITIMISHWA KWA KUFUKUZWA

Katika siasa za US wiki hii uchunguzi wa Russia umeendelea kwa baadhi ya washiriki wa Trump kuhojiwa
Habari hizo hazikuchukua nafasi kutokana na sakata la Kahaba Stormy Daniel anayedai kula penzi na Rais Trump

Katika interview iliyofanywa katika kipindi cha 60 minutes, Stormy alieleza wazi, penzi lilikuwa lina ridhaa
Wakati huo huo, mwanamama mwingine Karen McDougal ambaye ni playboy model akimwendea kombo Trump

Hata hivyo habari kubwa ilikuwa ya Stormy Daniel aliyelipwa na mwanasheria binafsi wa Trump, bw M. Cohen

Bwana Cohen anakiri kumlipa Stormy 130,000 kupitia kampuni aliyofungua na kufunga ili kukamilisha malipo masaa machache kabla ya uchaguzi wa 2016, ikidaiwa malipo yalikuwa kumziba mdomo bibie Stormy

Malipo hayo ni kutokana na huduma ya Stormy kwa Rais Trump miaka ya nyuma

Cohen amemtetea mteja wake Rais Trump akisema alitoa malipo hayo binafsi na si kwa ajili ya penzi nono alillopokea Rais Trump ambaye wakati akijivinjari mkewe Melania alikuwa akilea kichanga cha miezi kadhaa

Malumbano ya Cohen na mwanasheria wa Stormy Bwana Michael Avennati yalimleta mchunguzi Mueller

Mueller anayeongoza uchunguzi wa Russia aliliangalia suala hilo kwa undani.
Hapa msomaji usishangazwe kwanini Mueller aliingia.
Mueller alipewa wigo wa kuchunguza jambo linaloweza kuwa na mahusiano na Russia na uchaguzi

Cohen,msiri wa Trump alipoingia katika malumbano alimwalika Mueller wenyewe wakisema 'Follow the money'.

Cohen alimpa 130K Stormy bila kueleza ni kwa huduma gani, Stormy akisema huduma ya penzi kwa Rais Trump, huduma iliyokuwa na ridhaa kabisa. Stormy anasema kukataa ukweli ndio tatizo linalomsumbua

Hivyo Mueller alikuwa anaangalia mahusiano ya fedha na Cohen, hakuwa katika timu ya kampeni bali mshirika na msiri mkubwa wa muda mrefu wa Trump ambaye kwa namna asiyoweza kueleza, alitoa fungu nono kwa kahaba.

Kwa maneno mengine, huenda angelikuwa kiungo kikubwa katia Trump na uchunguzi wa Russia

Inaendelea II
 
Sehemu ya II

SUALA LA KAHABA STORMY LAZUA BALAA KWA RAIS
UCHUNGUZI WA MUELLER UNAWEZA KUHITIMISHWA KWA KUFUKUZWA

Baada ya kupitia nyaraka na taarifa, Mueller aliona suala hilo lina harufu ya uhalifu na hivyo kulipeleka kwa FBI

Leo FBI wameingia katika ofisi na makazi ya Cohen wakiwa na search warrant na kufanya upekuzi
Hakuna anyejua hadi sasa ni nini kilichokuwa kinatafutwa au kilichopatikana

Hapa tuelewe kuwa Michael Cohen, mwanasheria wa Trump ni nguli wa taaluma hiyo. Haikuwa Rahisi tu kwenda kufanya upekuzi bila kuwa na ushahidi wa kutosha wa kwanini afanyiwe upekezi mkubwa kiasi hicho

FBI walikuwa na mwendesha mashtaka, na ili wapate search warrant lazima wapate baraka za Judge

Judge naye ana dhima ya kujidhirisha kuwa zipo sababu muhimu zinazoruhusu FBI kufanya upekuzi

Rais Trump na wafuasi wa mrengo wa kulia wamekuja juu kuhusu upekuzi.

Inaonekana Rais anahofu upekuzi unaweza husisha miamala ikizingatiwa hakuna ajuaye ulipaji wa kodi

Lakini pia haijulikani nini mashtaka yatakuwa kwasababu affidavit bado ni sealed na Cohen hajafikishwa popote

Rais na Mrengo wa wahafidhina wamekuja juu kwa maana ya kutaka kulihusisha suala la Stormy na Russia

Hapa ndipo TV kama Fox zinapotosha kwamba Mueller amevuka mipaka ya uchunguzi
Wengine wakisema tuhuma hizo zinachagizwa na bawa la shoto la Democrats

Kuna mambo mawili ya kutambua. Uchunguzi wa Stormy na kupekuliwa kwa Cohen havihusiani na uchunguzi wa Mueller.

Kilichotokea ni kuwa Mueller katika fukua fukua alihisi jambo 'smell rat' akawapa FBI

FBI walikuwa na hiari ya kuendelea na uchunguzi au kuliacha.

Kwa nchi kama US kulifumbia macho ni tatizo mbele ya safari wahusika wanaweza kujikuta na wakati mgumu.

Hivyo basi, ieleweke Mueller ni Republican, Michael Ray wa FBI ni Republican na mteuliwa wa Trump.
AG-Sessions ni Republican na mteuliwa wa Trump kama ilivyo Deputy Roseinstein
Kwa jicho pana kila jambo limefanywa na Republican wakiwa wateuliwa wa Trump

Hoja kwamba ni Democrats inafia hapo.
Kazi ya Dems kama chama cha upinzani ni kuchagiza tu yanayojiri

Kwanini Mueller anashambuliwa?
Ni ili Kuchanganya mambo hayo mawili kutaka kumuingiza Mueller.

Baada ya hapo Rais Trump atapata sababu za kumtimua na kumaliza uchunguzi wa Russia

Leo kama tulivyowahi kusema amemlaumu AG Sessions akisema kujitoa katika suala la Russia ndilo tatizo

Jitihada za Rais Trump kumuondoa Sessions zimekwama na sasa yupo frustrated kwani hana 'kinga'

Rais Trump ajilaumu mwenyewe kwa harakati zake za twitter huku akipuuza ushauri wa wanasheria

Hadi sasa wanasheria nguli wamekataa kushiriki katika utetezi wakisema Trump ni mteja mgumu kumdhibiti

Pamoja na yaliyotokea, tukumbushe kuwa suala la Bill Clinton lilianza na matatizo ya 'michepuko' likaishia katika perjury na impeachment. Hili la Trump halionekani kama ni tofauti, na sasa hali inazidi kumchanganya

Nini kinakuja kuhusu Syria? Tutajadili

Tusemezane
 
Hii si habari njema kwa utawala wa Trump kwa kipindi hiki ambacho Marekani imetamka wazi haitakaa iwe rafiki wa Russia (US ambassador to UN, Ms. Haley). Kipindi ambacho Trump anatumia lugha za kuudhi dhidi ya Syria, huku Russia ikisema atakaye ishambulia Syria atajutia kitendo hicho. Ni habari kuhusu kujiudhuru kwa Bossert (Trump Homeland security Advisor)

Forced out? Trump’s Homeland Security adviser resigns
 
Hapa ndipo TV kama Fox zinapotosha kwamba Mueller amevuka mipaka ya uchunguzi
Wengine wakisema tuhuma hizo zinachagizwa na bawa la shoto la Democrats

"They found no collusion with Russia....this is a disgrace..." Trump
 
TIMBWILI LA FBI NA COHEN
DEP. ROSENSTEIN, AG-SESSIONS NA MUELLER WAKALIA KUTI KAVU
NI HATUA INAYOWEZA KUREJESHA HISTORIA YA 'SATURDAY MASSACRE YA NIXON'

Tangu alipoonekana jana akiwa na majenerali wa jeshi kwa kile kilichosemwa kutathmini hali ya Syria, Rais Trump ameahirisha safari ya America kusini kutokana na fukuto la upekuzi wa wakili wake Bw. Cohen

Rais Trump katika mkutano wa jana alionekana kuwa 'disorganized' kwasababu alizungumzia suala la Cohen na kugusia maeneo yasiyohusika bila kuwa na sababu. Alimtaja Hillary kufanya 'madudu' na bila hatua.

Rais Trump pengine ni mgeni wa Washington, kwa kumbu kumbu Republican walifanya uchunguzi wa Benghaz kwa zaidi ya miaka 2 tena wakirudisha suala hilo wakati wa uchaguzi

Hillary si Rais wa Marekani na wala tuhuma zake haziondoi tuhuma nyingine kwa mwingine
Rais Trump alimtaja deputy Roseinstein na James Comey bila kuwa na kiunganisho na tukio la Cohen!

Rais Trump alizungumzia uchunguzi wa Mueller kuendelea kwa mwaka, hakuna ''collusion''
Rais Trump alizungumzia hilo si kwa bahati mbaya bali akijua sehemu ya jamii haielewi na itaamini asemacho

Kuna kamati 4 za congress na special counselor Mueller zinazofanya uchunguzi wa Russia.
Kati ya kamati za congress, nyingine zimeshaonyesha kugawanyika kivyama kama ile ya Nunes

Kazi za kamati hizo si sawa na majukumu ya Mueller ambaye kisheria ana nguvu zaidi na ndiyo ameshtaki watu wengine wakisubiri kufikishwa kizimbani kama kampeni meneja wa Trump bw. Manafort

Sehemu kubwa ya watu wasioweza kuchanganua , kujiuliza au kuuliza wanashindwa kuuliza suala muhimu moja!

Ikiwa hakuna collusion, je , ni kwa mujibu wa taarifa gani?
Trump anafahamu kurudia jambo hilo mara nyingi wapo watakao kubaliana naye bila tafakuri ya aina yoyote.

Hakuna anyejua hadi sasa Mueller na kamati zingine zimeona nini, na hapa hasa ni Mueller ambaye tayari ameshtaki watu na baadhi kukiri kudanganya taarifa. Mueller na timu yake wamekuwa wasiri sana!

Kufutailia upekuzi wa Cohen, hali ya WH ni tete. Rais Trump anaogopa sana pengine akijua upekuzi unaweza kuja na nini. Hapa si suala la Russia pekee bali upana wake hadi tuhuma za wapenzi makahaba na hela za kampeni

Rais Trump anamlaumu sana AG-Sessions kwani kujitoa kwake kumeziba mwanya wa kuua suala la Russia.

Kwasasa ana option moja, kumuondoa Deputy Rosenstein ili afanye mambo mawili
1. Amweke mtu wake anayeweza kumfukuza Mueller
2. Aweke mtu wake anayeweza kumdhibiti Mueller hasa suala la financial dealing (miamala)

Kwamba atamwendea Rosenstein kwasababu tulizoeleza. Mueller alinusa harafu ya ''uhalifu'' kwa Cohen, akaona si eneo lake na kumpelekea Roseinstein ambaye aliwasiliana na FBI na kupata baraka za Judge upekuzi ufanyike

Watu wanachanganywa ili kupoteza uelekeo.
Kuna mambo mawili tofauti, kwanza Uchunguzi wa Russia na pili, tuhuma dhidi ya Cohen zikihusisha makahaba.

Cohen akiwa wakili wa Trump anaweza kuwa na connections na sehemu zote, Russia na kabaha Stormy, au anaweza kutokuwa na uhusiano wowote! uchunguzi wa FBI unaweza kuunga au kutenganisha mambo hayo

Mpango wa Trump kumtimua Rosenstein au Mueller unaweza kufanikiwa, lakini pia utakutana na upinzani
Tayari baadhi ya watu wa congress wameonya hatari i kutokea kama ile ya Richard Nixon na Saturday massacre

Mpango wa Rais Trump unaweza kutekelezwa kwani yeye pekee ndiye anajua nini kinaweza kutokea.
Washauri wake wanaweza kumshauri tofauti, lakini mwenye kujua uzito wa masuala hayo mawili ni Trump

Kwa mtazamo huo, anaweza kufanya lolote akijua ''hana cha kupoteza''

Tusemezane
 
Back
Top Bottom