Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

YANAYOJIRI

Rais Trump alikuwa na hotuba ya state of union akiongelea masuala mbali mbali kwa mustakabali wa nchi
Hakukuwepo na jambo geni zaidi ya siasa za kawaida za Washngton. Tutaiangalia hotuba tutakapojadili mbeleni

MEMO
Habari inayozunguka ni ile memo iliyopo WH kwasasa. Memo inachanganya wengi wakidhani ni 'memo' kama ilivyo kutoka FBI. Memo imeandikwa na Republican kutoka katika nyaraka kurasa 50-60 wakichagua na kubaki na kurasa 4.

Mwenyekiti wa kamati Nunes amekiri kutosoma nyaraka nyingine na hata waliopiga kura katika kamati hawakusoma nyaraka bali memo

Nunes ni yule aliyewahi kwenda WH akisema ana habari mpya kuhusu tatizo la uchunguzi wa Russia, habari ambayo aliipata WH na hivyo kusema anayo wakati ilikuwepo WH. Nunes akaji 'recuse'. Ilikuwa ni March 2017 kwa habari ile ya memo ya leo

FBI chini ya mteule wa Trump wamesema hawajaona lolote lenye tatizo na hivyo wanomba memo waipitie nao

Nunes amekataa kuwapa. Pamoja na hayo, utaratibu wa classified information kujadiliwa unahusisha national security agencies. Nyaraka ilitoka kamati na kwenda WH !!

Dems wametaka kutoa yao kwa jambo lile lile, kamati imekataa na bado inasubiriwa

Kwanini Nunes hakuwapa FBI? Kwanini security agencies hazikushirikishwa?
Wataalaam wanasema hilo linaweza ku debunk memo na kuharibu mpango uliokusudiwa

FBI Dir amekwenda WH kushauri isitolewe. Huyu ni mteule wa Trump mbadala wa Comey

DOJ juzi na jana imekataa kuhusu kutolewa memo.Ni dept ya Sessions na wateule wa Trump

Hofu si contents za memo bali mambo mawili.
Kwanza, inaweza ku expose habari za kiusalama kwa vyanzo vyake
Pili, inaweza kuzua mjadala na ikibainika iliandikwa kwa 'namna'

Rais Trump anayo na ana siku 5 za ku declassify kwa public.

Hilo litafungua mjadala mzima wa FISA Warrant na huenda yakajulikana mengine yasiyotakiwa kwasababu itakuwa ni declassified, na mengi kutoka court yatajulikana

Najaribu kuangalia jambo hili na mwenendo. Kwanza aliyetuhumiwa alikuwa Susan Rice mshauri wa obama wa mambo ya usalama kwamba ali unmask majina ya waliochunguzwa.

Ilikuwa habari kubwa, Susan akaitwa mbele ya kamati. Alichokisema hakuna anayemzungumzia tena

GPS walituhumiwa na dossier ya uongo. Waliitwa mbele ya kamati, mjadala umekwisha
Tena GPS wakata majadiliano ndani ya kamati yawekwe wazi, habari haikuwa nzuri GOP

Kwa nyakati fulani memo imesaidia kubadili mjadala wa Russia Republican wakiitumia

Wanasheria wa Trump wamekataa asihojiwe na Mueller kwani haja meet threshold

Yote yanalenga kuzuia uchunguzi wa Russia. Kumfukuza Mueller litakuwa ni tatizo kubwa

Don McGahn alimshauri Trump asifanye. Uwezo wa kumfukuza anao, je ataweza vishindo vyake?

Mathalani, katika seneti kuna 'margin of error' finyu sana.

Congress na Intel community wanaamini Russia ilihusika katika kuingilia mchakato wa demokrasia

Hapa ndipo baadhi wanachanganya mambo kwa kuzungumzia jambo wasilolielewa.
Congress na Intel community zinathibitisha hilo,hakuna ubishi ila kwa Trump na base yake inayoamini asemacho

Si kila mmoja ataelewa, kuna walioamini Obama alifanya surveillance Trump Tower
Dept of Justice chini ya Sessions mteule wa DJ imethibitisha hakuna upuuzi kama huo

Wapo walioamini kuwa wapiga kura milioni 5 ambao leo kamati ya Trump haikuweza na imefutwa
Na wapo walioamini Mexico italipa Ukuta, leo wanaolipa ni US.

Kinachoangaliwa ni kuwa, Russia walifanya hayo wenyewe au wakiwa na msaada wa watu wa ndani?
Kuna uthbitisho wa collusions kwa kuangalia watu na kampeni hasa mkutano wa Trump Tower

Hata hivyo collusion si crime kwa mujibu wa wanasheria. Crime ni itakapokuwa ni conspiracy

Tusemezane
 
'MEMO' YA NUNES, TRUMP KUITOA?

MUELLER ANASOGELEA WH, TAHARUKI NA SINTOFAHAMU!

Bandiko la nyuma tulieleza kuwa fukuza fukuza inayoendelea kwa sehemu kubwa inachangia suala la Russia
Kuondoka kwa Comey, Sally Yates , McCabe na wengine kama swahiba wa Trump Bannon kutavujisha habari
Kabla ya wiki tulizosema tayari hali inazidi kutatiza

'Memo': Ile memo iliyoandikwa na Nunes imefika katika oval office ili ima isainiwe kutolewa au kutosainiwa
Duru zinasema editing kwa ajili ya mambo ya usalama inaendelea na ni huenda memo ikatolewa kesho

Nunes alijiondoa katika suala la Russia baada ya kuibukia WH akidai kuna memo yenye kuudhi
Leo inafahamika memo iliyopo WH ni ile ile aliyokuwa anaifanyia kazi mwezi March

Nunes alikuwa katika transition team ya Trump baada ya uchaguzi na ni mwenyekiti wa 'house intel committee'
Memo imepelekwa kwa mbinde WH, na habari zilizopo ni kiongozi wa Dems katika kamati kutoa statement kuwa memo iliyojadiliwa ndani ya kamati Nunes ameifanyia editing kabla ya kwenda WH

FBI na DOJ wamepinga kutolewa kwa memo hiyo hadharani. DOJ wanasema ni kwasababu za kiusalama

FBI wanatoa statement inayosema kuna 'ommission of facts... fundamentally misleading'
Kwa lugha nyingine Christopher Wray wa FBI na DOJ wanapingana na WH wakitaka isitolewe

WH inataka kutoa kurasa hizo nne zilizoandikwa na Republican ambazo Nunes na wanakamati wanakiri kutoona kabra lote. Kwa maana hiyo kulikuwa na voting ya majumuisho(conclusion) bila kujua maudhui (contents)

Nunes ameulizwa leo kama hakuna ushirika wa WH kuandika memo. Kwa kuelewa mtego hakukana au kukubali
Hapa kuna habari ambayo 'mtu' anawekewa kitanzi , Nunes ameng'amua lakini si mwisho wa fukunuku

Hata hivyo, WH na Republican wanataka itolewe ili kuvuruga mwelekeo wa maongezi, kuleta shaka kwa uchunguzi na kubadili mtazamo wa wananchi dhidi ya nini Russia ilifanya na uchunguzi unahusu nini

SINTOFAHAMU
Kuna habari kuwa Rais Trump alimuuliza Roseinstein aambaye ni deputy AG kama ni katika timu 'in our team'
Kumbuka Trump aliwahi kumuuliza Deputy wa FBI McCabe aliyejiuzulu alimpigia nani kura wakati wa uchaguzi

Hawa waliulizwa kufuatia uchunguzi wa Mueller na Russia ,unaeleza zaidi nini WH inafikiria kuhusu 'loyal'

Habari hizi zinatoka kwa kasi wiki hii !

Inaendelea
 
  • Thanks
Reactions: dtj
SINTOFAHAMU
Inaendelea....

Peter S ,aliyetuhumiwa kuandikiana text na mpezi wake na Republican kumtumia kuonyesha bias ndani ya FBI, habari nyingine imeibuka dhidi yake. Ni yeye akiwa senior intel officer wa FBI aliandika email akishauri uchunguzi wa Hillary Clinton utangazwe unaendelea. Ni tangazo hilo lililochangia kuzima ndoto za Bi Clinton

Tatizo kwa Republican ni kumtuhumu kama mtu wa Dems, kwa email za Peter hoja itakuwa imekufa
Habari hizi zinatoka katika media zikiwa ni za ndani kabisa. Je, ni gharama za timua timua ya Trump?

MKUTANO WA TRUMP TOWER
Mkutano maarufu wa Trump tower unarudi ukiwa na details nyingine

Communication officer wa WH Hope Hicks amekaririwa akisema 'email za Don Jr hazitatoka'
Lawyer wa Hicks amekanusha madai ya NYT akisema hayana ukweli

Pamoja na hayo, mkutano ule uliosemwa wa adoption na baadaye kujulikana ulikuwa wa dirty of Clinton ulizaa suala jingine. Wakiwa katika airforce one wakitokea Ulaya inasema Rais Trump alishiriki kuandika statement
Kumbuka kulikuwa na statement ya kwanza ya Don ambayo ilibadilika baada ya ile ya Air force one

Mkanganyiko mkubwa ni wa wanasheria wa Trump, Don, Trump , Hicks n.k. ambao kwa mtazamo wa kiuchunguzi unavuta kinachoitwa curiosity. Endapo hakukuwa na tatizo kwanini kulikuwa na kubabaika babaika?

Ikumbukwe, kauli za kwanza za Trump na wanae pamoja na wapiga debe ilikuwa ' hakukuwepo na contact na Russia'. Leo inajulikana kulikuwa na contact na watu wameshtakiwa kwa kuongopa

Kauli ya pili ikawa, ni maongezi ya kawaida hakuna 'there there'. Inajulikana sasa kuwa kulikuwa na contact, zilihusu kampeni na Don Junior alisema 'I love it' alipoahidiwa dirty za Clinton

Hadi sasa hakuna aliyetoa taarifa endapo kulikuwa na collusion au la. Kuna mambo yanayotia hofu WH
Kwanza, washirika wa Trump wanaotoa ushirikiano kwa FBI wanasema nini?
Pili, Miamala ya fedha (financial dealings) za Trump na washirika wake zinaeleza nini?
Tatu, kwa mkusanyiko wa matukio kadhaa, kulikuwa na obstruction of justice?
Nne, je, Russia alitenda peke yake au ilikuwa na washirika katika hacking ya email ziwe za Dem au GOP?
Tano, washirika wa ndani wa WH wamehojiwa na Mueller, wameeleza nini?
Sita,Kwanini Mueller anataka kuingia oval office na ana kitu gani asichojua au anachojua kuhusu Russia?

Hakuna shaka uchunguzi wa Mueller unaleta sintofahamu na kiwewe WH.

Ili kuondoa watu katika focus hiyo 'memo' itatolewa iwe maongezi dhidi ya zuio la DOJ na FBI

Kwa upande mwingine, ikitokea memo ikawa 'debunked' hali hiyo itatia nguvu uchunguzi wa Mueller

Njia ya pili ni kuondoa Roseinstein au Session ili kufungua milango ya kumtimua Mueller
Rais Trump akimtimua tu kwa kuamua atakabailiana na nguvu ya Congress, hakuna shaka juu ya hilo

Republican wamekalia 'bomu', wakifanikiwa kulidhibiti ni mafanikio , kinyume chake chaweza kuwa mlipuko

Tusemezane
 
  • Thanks
Reactions: dtj
'TORPEDO KWA RUSSIA INVESTIGATION'
ROSENTEIN KAKALIA KUTI KAVU, MUELLER AELEKEA KUTIMULIWA

Hoja inayotanda katika vyombo vya habari ni kuhusu 'memo iliyoandikwa na Chairman intel comm' Bwana Nunes

Nunes ni memba wa Trump transition team na ndiye aliyeibuka WH na hoja hiyo ya memo hadi alipo ji 'recuse'

Nunes amehojiwa ikiwa memo iliandikwa kwa ushirika na WH, naye akajibu 'kwa kadri anavyojua hakuna' .
Kwa maneno mengine hana uhakika kama memo imeandikwa na nani au kumshirikisha nani

Ukweli ni kuwa anajua memo imeandikwa na nani, kwa kuchelea media za US akahisi jibu linaweza kumrudi
Nunes hajasoma nyaraka zima linalihusu memo hiyo. Wajumbe wa kamati hawajasoma nyaraka bali memo

Na wala memo hiyo haijasomwa na chairman wa senate intel committee ambaye ni Republican, DOJ au FBI.
Kuna habari zilizothibitishwa kuwa memo ilifanyiwa editing tofauti na ile iliyopigiwa kura na kamati

Memo imetua WH na inategemewa asubuhi hii itasainiwa ili itoke kwa hadharani

Dems wamekataliwa kutoa memo yao, FBI wamepinga kutolewa memo hiyo kwa kauli ' omission of fact...and fundamentally misleading, dept is gravely concern'
FBI Association nao wametoa kauli kama ilivyo DOJ waliokataa memo isitolewe

Mkuu wa FBI ni mteule wa Rais Trump bw Christopher Wray, Deputy FBI Bw Rosenstein ni mteule wa Trump, DOJ inaongozwa na wateule wa Trump akiwemo Sessions ambaye ni AG

Trump amekaririwa na hakuna kanusho akisema ' memo itasaidia ku discredit Russia investigation'

Tayari kuna concern kuwa Wray anaweza ''kujiuzulu' hata hivyo zinabaki tetesi hadi itakapotokea

Mpambano uliopo ni WH Vs DOJ, FBI na Dems kuhusu uthabiti wa memo ,taratibu na tatizo la kuitoa

Kwa Rais Trump hii ni karata muhimu sana kuua suala la Russia kama tulivyoeleza bandiko 515
Memo nzima inasemekana kuhusu FISA court na hapa inamgusa Rosenstein deputy AG aliyeidhinisha FISA

Hivyo memo lazima imlenge Rosenstein ili Trump apate mwanya wa kumuondoa.

Hilo litawezesha kumtimua Mueller na uchunguzi wote kufikia mwisho.

Hizo ndizo hesabu baada ya AG Session kukataa kujiuzulu licha ya masumango kutoka kwa Rais Trump kwasababu tulizoeleza bandiko 515

Rosenstein na Mueller wapo katika target waksubiri torpedo ya Trump kuzima Russia investigation

Ni gambling ya hali ya juu inayoweza 'kulipa'' au ''kuzamisha meli na mzigo'' kama Saturday Night Massacre

Tusemezane
 
MEMO YA NUNES YAWEKWA HADHARANI

SPIKA RYAN ASEME YA DEMS NAYO SASA RUKSA

Rais Trump alisaini memo ya House intel comm chairman Nunes leo na hivyo imetolewa hadharani
Ilitegemewa hivyo kwani siku ya state of union Trump alisema ataisaini japo hakuwa ameipitia

Republican katika kamati ya Bunge walikataa ile ya Dems isitolewe kwa sababu maalumu

Memo ilikuwa na mambo mengi yanayojichanganya na mengine yakiacha maswali. Hata hivyo, siku ya leo media zote zinazoegemea bawa la kulia kama Fox wamekuwa bize kueleza memo hiyo

Ikumbukwe memo iliyoandikwa chair Nunes hakuwahi kusoma nyaraka yake. Kurasa nne tu zimetumika kueleza kile kinachoitwa abuse kutoka DOJ na FBI

Hoja kubwa inahusu FISA (Foreign intelligence survaillance act) sheria inayotoa fursa kwa vyombo vya usalama kufuatilia mawasiliano ya mhusika.

Sheria hiyo lazima iidhinishwe na FISC, mahakama, ili kuridhiwa kuwa kuna sababu za kufanya hiyo surveillance.

Sheria inasema baada ya siku 90 lazima aliyetoa ombi awasilishe ushahidi kuwa uchunguzi unaendelea na una matokeo tarajiwa, vinginevyo inafutwa

FBI/DOJ waliomba FISA kutoka FISC ili kufanya survey kwa Carter Page kutokana na mawasiliano na Russia, na FISA iliridhiwa na mahakama kurudiwa mara 3

Carter Page alikuwa katika kampeni ya Trump kabla ya Trump mwenyewe na watumishi wa WH akiwemo Kellyanne Conway kumkana hakuwa sehemu yao.

Katika hali ya kushangaza waliomkana wanamtumia, kwamba kuna hujuma dhidi ya Trump katika uchunguzi unaoendelea

Republican wanaotetea memo ya Nunes wanasema DOJ na FBI hawakueleza mahakama msingi wa uchunguzi wao ulikuwa katika ile dossier wanaoyesema ni ya kupikwa, hivyo FISA iliyotolewa kwa Page ilikuwa na hujuma

Kisichoelezwa katika memo ni kuwa uchunguzi dhidi ya Page ulianza baada ya dossier kujulikana.
Dossier iliombwa na Republican kama opposition research kabla ya kuitosa na Clinton kutumia GPS

Pamoja na hayo memo inamtaja Papadopolous ambaye amekiri kuidanganya FBI kuhusu ushiriki wake na anayeshirikiana na FBI kwa sasa huku akiwa amekanwa na Trump kampeni kwa kumwita coffee boy

Kuna information zinakosekana katika memo. Kwa mfano ikiwa DOJ na FBI walishindwa kuiambia mahakama ukweli, je, ni nini walichosema hadi kupewa FISA mara 3?

Wengi hawasemi nini kilichokuwemo ndani ya mjadala kati ya FBI na FISC.
Watetezi wote wanakiri hawajaona nyaraka ya FISA application lakini wanakubali kurasa 4!!!

Pili, Russia investigantion ilianza kutokana na habari za Papdopolous. GPS walipofikisha dossier FBI tayari kulikuwa na habari za mahusiano katika ya Russia na Trump kampeni kuhusu dirty za Clinton

Swali jingine, kwanini kamati isikubali memo ya Dems kuwekwa hadharani sambamba na ile ya Nunes?

Sehemu ya II inaeleza mchezo unaoendelea
 
Kwa kuboresha kumbukumbu, Clinton Campaign walichangia fungu la ela tena za kutosha katika kuandaa dossier ya Steele.Ni dossier hii inayodhaniwa kupikwa ilikuwa msingi wa kuruhusu kumdukua Page.
===

The four-page memo compiled by the GOP Chair of the House Intelligence Committee accuses the FBI and DOJ under the Obama administration of securing a warrant to spy on the Trump campaign based on the notorious ‘Steele dossier.’
Declassified by President Donald Trump and published by the committee Friday over strong objections by Democrats, the DOJ and the FBI, the memo lays out the origins of the warrant to spy on Trump adviser, Carter Page, in the dossier funded by Hillary Clinton's campaign.

The so-called Steele dossier “formed an essential part” of the FISA probable cause order obtained by the FBI from the Foreign Intelligence Surveillance Court (FISC) on October 21, 2016. The warrant was extended three times, also on the basis of the Steele dossier.

Republican memo: What you need to know about alleged FBI & DOJ abuses
 
MEMO HADHARANI

Sehemu ya II

Spika Ryan amesema memo ya Dems itatolewa kama ya Nunes. Amesema hayo baada ya Trump kusaini memo
Memo nzima imelenga FISA kwasababu maalumu kama tulivyoeleza mabandiko 515 na kuendelea

Kuna watu wanaotakiwa kuondolewa ili 'ku torpedo' uchunguzi mzima wa Russia na Trump kampeni
Kwanza aliondolewa act AG Sally Yates ambaye alikuwa mteuliwa wa Obama.

Ms Yates aliondolewa kwa kuitahahdarisha WH kuhusu utata wa M.Flynn ambaye siku chache alibainika kudanganya FBI na sasa ameshtakiwa akishirikiana na FBI. Yates alitafutiwa sababu hakuwa na kosa

James Comey aliombwa na Trump 'apotezee' suala la Flynn, aliokataa Trump akamtimua
Kosa alilofanya Trump ni kwenda katika radio na kusema alimfukuza Comey kutokana na suala la Russia

Kuondoka kwa Comey kukatoa mwanya kwa Trump kumteua Christopher Wray kuongoza FBI
Deputy wa Wray akawa ni Andrew McCabe. Huyu kaundiwa Zengwe ili kuondoa 'mabaki' ya Comey

Kizaa zaa kikatoke pale ilipobainika AG Sessions naye alidanganya mahusiano yake na Russia
Alitakiwa ajiondoe katika kusimamia suala la Russia 'recuse' kwani hawezi kusimamia uchunguzi anaotuhumiwa

Jambo lilimkasirisha sana Trump ambaye alianza kumsimanga hadharani ili Sessions ajiuzulu na kuteuliwa AG

Kuteuliwa kwa Roseinsten kunatokana na Sessions kujiondoa katika usimamizi wa uchunguzi na kumlazimu Rosensten kumteu mchunguzi Robert Mueller

Uchunguzi wa Mueller umeingia kila kona ya Trump na washirika wake. Wiki chache wanasheria wa Trump walikuwa na majadiliano na Mueller ili Trump naye ahojiwe kama ilivyo kwa washirika wake wote

Hili limeleta sintofahamu kwa Trump ambaye wanasheria wake hawataki ahojiwe kwasababu kadhaa
Kwanza, uwezo wa Rais Trump kujieleza na hivyo uwezekano wa kujichanganya na kulikoroga
Pili, wanaotoa ushirikiano kwa FBI haijulikani wanasema nini na kisheria linaweza kumweka Trump pagumu
Tatu, kuna dalili za kufunuliwa 'deal' za Trump, kuna dalili za obs of justice na haijulikani mahusiano na Russia

Kwa maana hiyo, FISA application zilisainiwa na Deputy Rosenstein anayemsimamia Mueller
Huyu ni key figure ambaye kuondoka kwake kutafungua milango ya kuhujumu uchunguzi wa Mueller

Hivyo ili kuzima au kuhujumu uchunguzi wa Mueller kuna njia mbili zinazoweza kutumika

Kwanza,kumtumia AG ambaye amejiondoa na aliyekataa kuachia ngazi, jambo lililoshindikana
Pili, kumuondoa Rosenstein anayemsimamia Mueller ili kufanyike mambo mawili
i) Kumteua mtu mnyenyekevu atakayezima uchunguzi kabisa au
ii) Mtu atakyeweza kufanyia marejeo hadidu rejea ili kuondoa maeneo yanayoonekana kuwa na 'tatizo'

Kumbuka, Mueller alipewa hadidu za rejea 'terms of reference' na Rosenstein na wigo wa uchunguzi wa Russia

Inaendelea sehemu ya III
 
Sehemu ya III

Ni kwa msingi huo, memo imelenga katika kutimiza mambo yafuatayo

Kwanza, Spika Ryan na Nunes kukataa memo ya Dems isitoke ili kutoa nafasi kwa memo ya Nunes kusikika
Katika wiki mbili zijazo itakuwa imeanika hata kama Dems wataruhusiwa kutoa yao

Pili,Kum 'frustrate' Rosenstein ili aachie ngazi na kuteuliwa mtu mwingine 'loyal' atakayechukua nafasi

Tatu,kuandaa mazingira ya kumfukuza Rosenstein ili kutoa mwanya wa kuhangaika na Mueller

Nne, kuaminisha umma kuwa kuna hujuma dhidi ya Trump na uchunguzi wa Mueller una biasness

Tano, kumwepusha Trump kuhojiwa na Mueller kwa kigezo cha kutokuwa na imani naye

Jaribio la kumfukuza Rosenstein bado lipo ingawa washauri wa WH wanonya hilo kwa kuangalia upepo wa kisiasa na hasa idadi ya Republican ambao hakuna anayejua kwa uhakika wangapi wanaridhia hali ilivyo

Hilo haliondoi ukweli kuwa Trump anaweza kumfukuza Rosenstein bila kujali nini kitatokea. Inategemea anajua nini uchunguzi unaweza kuweka hadharani na hivyo kuchukua 'risk' akijua anaweza asiwe na cha kupoteza

Hapa kuna mtihani. Kumfukuza Rosenstein na Muller hakutmalizi tatizo kutarefu muda kama lipo.

Ugomvi wa Trump na FBI, DOJ, na watu kama Comey kunaweza uvujisha habari kwa wingi kama lipo la siri lisilojulikana hadi sasa na huenda kukawa na uchunguzi mwingine kwa kutumia special prosecutor

Kuwaacha akina Rosenstein na Mueller kutamjengea 'heshima' ya kisiasa lakini hilo halimhakikishii kuwa matokeo yatakuwa mazuri. Hadi sasa kuna hasira juu ya tuhuma kama za memo na mipango inayoendelea

Dems walizembea ! kwanini? Tutafafanua

Tusemezane
 
Hayawi hayawi, sasa yamekuwa!

Regular season inaisha na sasa muda wowote tutaingia kwenye play-offs kabla ya kuhitimisha kwa fainali. Bila shaka ambao wanafuatilia kwa karibu yanayojiri USA watapata fursa nzuri sana ya kushuhudia demokrasia iliyokomaa inavyoweza kufanya kazi bila papara.

Demokrasia ya kweli inakuwa na mihimili mitatu inayojitegemea nayo ni Executive, Legislature na Judiciary na kama Marekani itavuka salama, huo utakuwa ushindi mzuri kwa demokrasia. Nadhani tuna mengi ya kujifunza kutokana na haya yanayoendelea Marekani.
 



Mwenyekiti wa kamati ya House Intelligence, Nunes. Haya mambo yanahitaji mtu utumie akili huru kupima na kuelewa. Wenzetu humu wapo nyuma sana, wanaendana na matukio, huku mchezo mzima upo wazi.

Democrats walizuia hata kusiwepo na uchunguzi kwenye FISA abuse in the first place. Walijua madudu yaliyomo. Watu wameumbuka mchana kweupee wanatafuta pa kujificha.
 
Ni vizuri kupima na kuchuja taarifa unazokutana nazo.

Sehemu ya III

Ni kwa msingi huo, memo imelenga katika kutimiza mambo yafuatayo
Kwanza, Spika Ryan na Nunes kukataa memo ya Dems isitoke ili kutoa nafasi kwa memo ya Nunes kusikika
Katika wiki mbili zijazo itakuwa imeanika hata kama Dems wataruhusiwa kutoa yao

Hivi unaelewa mambo waliyofanya Dems kuhakikisha hata huo uchunguzi wa FISA abuse haufanyiki? Na hata report zake zisisomwe na members wa House?

Pili,Kum 'frustrate' Rosenstein ili aachie ngazi na kuteuliwa mtu mwingine 'loyal' atakayechukua nafasi

Hivi unaelewa role ya Rosenstein katika FISA warrant ya Page?


Tatu,kuandaa mazingira ya kumfukuza Rosenstein ili kutoa mwanya wa kuhangaika na Mueller

Baada ya madudu ya FISA kuwekwa wazi na uhusika wa Rosenistein katika hayo madudu (kama unaelewa), unaona ni busara akiendelea na nafasi yake? Kuna haja ya kusubiri kufukuzwa? (Katika nchi yenye uwajibikaji mkubwa kama US)

Nne, kuaminisha umma kuwa kuna hujuma dhidi ya Trump na uchunguzi wa Mueller una biasness

Mpaka hapo huoni hujuma dhidi ya candidate Trump, incoming President Trump na President Trump? Unajua kuwa Dossier ililipiwa na DNC na Hillary? Unajua kuwa FISA warrant dhidi ya Page isingepatikana bila ya 'dossier'? Unaelewa uchunguzi wa Mueller ume-base kwenye nini? Unajua kuna maafisa wanaomsaidia Mueller walio na political bias dhidi ya Trump?

Tano, kumwepusha Trump kuhojiwa na Mueller kwa kigezo cha kutokuwa na imani naye

Ukitumia jicho la tatu, kwenye serikali yoyote yenye uwajibikaji wa hali ya juu kama US, huo uchunguzi wa Mueller hauna maana yoyote.

Unajua connection ya uchunguzi wa Mueller na madudu yaliyowekwa wazi kwenye memo?

Jaribio la kumfukuza Rosenstein bado lipo ingawa washauri wa WH wanonya hilo kwa kuangalia upepo wa kisiasa na hasa idadi ya Republican ambao hakuna anayejua kwa uhakika wangapi wanaridhia hali ilivyo

Kwa unavyofikiria wewe sio Trump, Rosenstein ni mtu wa kufukuzwa au kusubiri ajifukuzishe mwenyewe? (Ukingatia uhusika wake kwenye madudu ya kwenye FISA)


Hilo haliondoi ukweli kuwa Trump anaweza kumfukuza Rosenstein bila kujali nini kitatokea. Inategemea anajua nini uchunguzi unaweza kuweka hadharani na hivyo kuchukua 'risk' akijua anaweza asiwe na cha kupoteza
Hapa kuna mtihani. Kumfukuza Rosenstein na Muller hakutmalizi tatizo kutarefu muda kama lipo.

Huyo mtu hafukuzwi na Trump, mbona mnashindwa kuona picha nzima?

'Kama lipo'? Kumbe mpaka sasa hivi hamna kipya.

Ugomvi wa Trump na FBI, DOJ, na watu kama Comey kunaweza uvujisha habari kwa wingi kama lipo la siri lisilojulikana hadi sasa na huenda kukawa na uchunguzi mwingine kwa kutumia special prosecutor

Unajua kuwa Inspector General wa DOJ anaendelea na uchunguzi wake (internal investigation) kwenye madudu ya e-mail server ya Hillary?

Unafahamu kwamba Inspector General wa DOJ kashapata memo iliyokuwa declassified? Subiri uchunguzi wake.

Kama special prosecutor atahitajika, ni katika haya matumizi ya vyombo vya usalama vya nchi kisiasa. Vitu vyenye ushahidi, na hapa lazima Obama aliwe kichwa.

Nunes kashasema kuna memo zingine zinakuja, hila zote zilizofanywa na Dems gizani zinamwagwa kweupe.

Kuwaacha akina Rosenstein na Mueller kutamjengea 'heshima' ya kisiasa lakini hilo halimhakikishii kuwa matokeo yatakuwa mazuri. Hadi sasa kuna hasira juu ya tuhuma kama za memo na mipango inayoendelea

Hao watu kwanza hawana heshima yoyote mpaka sasa. Hao watu wajipime tu, ndivyo accountability inavyofanya kazi.

Dems walizembea ! kwanini? Tutafafanua

Dems hawajazembea, wamehangaika kweli kuzuia haya yasitokee. Ila ukweli hata ukifichwa mbali kiasi gani, huwa unatafuta upenyo na unajulikana tu.
 
Mkuu, unaleta comedy kwenye mambo ya muhimu! Na hapo ni kabla ya memo kuwekwa wazi.
Kuna comedy kuliko Nunes memo! Ndugu yangu El Jefe, hiyo haikuwa comedy, kama unataka kusikia comedy msikilize Hannity wa Fox News ambako Trump anapata intelligence briefings hadi usiku wa manane! Nadhani kuna kitu kimoja hujui kuhusu Marekani ingawa unaamini unajua...flashback 1974! Trump amefanikiwa kwa kiwango fulani ku-demonize media ingawa ni kwa wafuasi wake tu lakini kwa FBI na DOJ he will lose and you can take that to the bank!

FYI: Comey, Mueller, Wray, Sessions na Rosenstein wote ni Republicans.
 
DEMS NA MAKOSA

Bandiko 529 tuliahidi kuzungumzia makosa yanayofanywa na Dems kwa kujua au kwa hali ya mambo ilivyo
Dems ni minority katika senate na House na kamati zinazongozwa na Republican, hii ni disadvantage kwao

Miezi 6 iliyopita waliambiwa ni muhimu wakaweka sheria itakayomlinda Mueller dhidi ya Trump
Republican wakasema hakuna haja ya kufanya hivyo kwani hakukuwepo na tishio lolote

Mwezi mmoja uliopita walianzisha tena vuguvugu na majibu yakawa yale yale
Katika muda wote kuna Republican waliokuwa wanawaunga mkono katika hoja

Imebainika miezi 6 iliyopita Dems walikuwa na taarifa za kufukuzwa kwa mueller ingawa WH ilikanusha
Aliyenusuru hali hiyo ni counselor wa WH Don, aliyemzuia Trump asichukue hatua kuchelea kimbunga

Hivi karibuni Dems wametaka uwepo wa sheria hiyo wakiwa wameshaiandaa wakiungwa mkono na baadhi ya Republican ambao ni moderate na wengine hawatarudi katika uchaguzi wa Senate au House

Kosa walililofanya ilikuwa kuzungumzia Memo badala ya kutilia mkazo sheria itakayomlinda Mueller
Kilichoonekana katika Memo kwa akili za kawaida hakina jambo la kushtua kama ilivyoitwa 'watergate'

Kwanza, memo haionyeshi affidavit yote na hivyo madai mengi yanaacha maswali kuliko majibu

Taarifa za uhakika kutoka ndani na hapa huenda DOJ au FBI zinasema mahakama ilielezwa kuhusu dossier kuwa na uhusiano na mambo ya siasa, hata hivyo sheria hairuhusu kutaja source

Lakini pia mahakama ilielezwa ushahidi mwingine wa kuidhinisha surveillance mara 3 kama si 4 na kila mara lazima iwepo hoja ya kuthibitisha surveillance ina tija na wala si ku renew tu kama nyaraka ya kawaida

Pili, NYT imetoa maelezo aliyotoa Carter Page yakimhusisha na ushiriki wake na Kremlin tangu mwaka 2013
Ni maneno ya Carter Page mwenyewe na si ya NYT, kwa maana surveillance ilianza muda tu

Tatu, muda wa dossier na surveillance ya Carter Page havina uhusiano kwa mujibu wa FBI na Papadopulos

Nne, Rais Trump na washauri wake wamenukuliwa (video) akisema hajawahi kuzungumza na Carter Page
Hivyo, Carter Page hana uhusiano na Kampeni ya Trump kwavile hawamtambui

Surveillance ya Carter Page haina uhusiano na Mueller kwasababu kiungo kati ya pande hizo ni Trump ambaye hamtambui. Uhusiano uliopo ni FBI na Carter Page kwa masuala ya usalama ( NYT) kutoka kwa Page

Wiki hii inategemewa memo ya Dems kutoka. Hapa kuna mtihani, kama WH itakaa hali itakuwa tofauti sana

Kutokana na sintofahamu, wataalam wanasema nyaraka nzima iliyozaa memo iwe declassified ili ukweli ujulikane.

Katika kuonyesha memo ilikuwa na namna, Rais Trump anasema imemsafisha (vindicate)

Hili kalisema Jumamosi likiwaacha wasaidizi wake katika vyombo vya habari na House njia panda.

Haikuwa imelengwa kupigiwa debe bali kuweka doubt.
Baadhi ya maseneta wa Republican wamesema dhahiri memo haikuwa na 'red meat'

Ni unlikely Trump ataweza kumfukuza Rosenstein au Mueller kutokana na picha ya memo isiyokubalika hata ndani ya Republican isipokuwa kwa wale wafuasi wa damu wa Trump

Kumtimua Rosenstein au Mueller ni risk kubwa sana. Inaweza kulipa 100% kwa muda mfupi sana, vinginevyo inaweza kuhitimisha nafasi yake kwa muda mfupi sana.

Kwa Taifa kama Marekani, hoja nzito na usalama na masilahi ya Taifa haiwezi kufa kifo cha kudumu, inaweza kuzimia lakini itasimama

Tusemezane
 
Kwa Taifa kama Marekani, hoja nzito na usalama na masilahi ya Taifa haiwezi kufa kifo cha kuduma, inaweza kuzimia lakini itasimama

Six smoking guns (A summary of the Memo)
  1. Hillary/DNC hire foreign spy to conduct fake dossier on Trump
  2. Hillary/DNC give fake dossier to Obama DOJ and FBI
  3. DOJ and FBI know the dossier is fake and politically motivated
  4. DOJ and FBI present fake dossier to FISA court to get Trump wiredtap
  5. DOJ and FBI don't tell FISA Court the dossier is Fake and from Trump's campaign opponent
  6. FISA court defrauded into ordering wiretapping of Trump Campaign
=====
Je. na content ya Memo hii pia ni fake ?
 
Six smoking guns (A summary of the Memo)
  1. Hillary/DNC hire foreign spy to conduct fake dossier on Trump
  2. Hillary/DNC give fake dossier to Obama DOJ and FBI
  3. DOJ and FBI know the dossier is fake and politically motivated
  4. DOJ and FBI present fake dossier to FISA court to get Trump wiredtap
  5. DOJ and FBI don't tell FISA Court the dossier is Fake and from Trump's campaign opponent
  6. FISA court defrauded into ordering wiretapping of Trump Campaign
=====
Je. na content ya Memo hii pia ni fake ?
Nadhani kwanza hujui utaratibu unaofuatwa hadi FISA inatolewa. Pili hata huyo Nunes mwenyewe aliyetoa hiyo MEMO hadi sasa hajui kilichomo ndani ya hiyo FISA iliyotolewa. Tatu FISA ya kwanza ilitolewa miezi mitatu kabla ya hiyo unayoiita fake dossier. Nne wanaotuhumiwa kwenye MEMO wote ni wateuliwa wa Trump. Tano Trump hakuwa wire-tapped kama unavyodai na MEMO haisemi hivyo. Mwisho, nakuomba uvute subira, usikurupuke kama Sizonje kwani mpaka sasa ingawa wakuu wote wa vyombo vya usalama ni wateule wa Trump hakuna hata moja anayeunga mkono tuhuma zake.

If the facts are not on your side you argue the laws, if the laws are not on your side you argue the facts but if both the facs and the laws are not on your side, you take your shoes and beat it!
 
Back
Top Bottom