Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

TATIZO LA KAULI YA TRUMP
Yupo katika rekodi akisema atapiga Marufuku waislam kuingia US kabla ya kupunguza makali

Uwepo wa makundi ya kigaidi yanayojihusisha na imani hauna maana imani nzima ni magaidi

Ingalikuwa hivyo tungekuwa na magaidi wa kiprotestanti, magaidi wa kilutheri au Roman

ISIS wanajihusisha na Uislam kuungwa mkono tu. Wanayofanya hayafanani 1%

Watu wa kufanya nao kazi ni Waislam ambao ni victims wa ISIS kuliko watu wengine

Si kweli kuwa wakristo walizuiwa kuingia US kuliko Waislam.

Katika nchi kama Syria/ Iraq waislam ni wengi na rahisi kupata 80% vs 20% kwa 100.

Pamoja na hayo takwimu zinaonyesha wote walipewa fursa sawa.

Kauli hii ilimlenga Obama kuwa aliwabagua Wakristo jambo lisilo kweli

Kutoa kipaumbele kwa Wakristo kwa msingi ni vulnerable kwa persecution hakuna ukweli

Ukishakuwa persecuted tayari ni victim of circumstance bila kujali imani , dini au kabila

Sunni ni victim wakubwa wa Shia. Wana haki ya ukimbizi popote pale kwa def ya ukimbizi

Tatizo jingine ni nchi saba alizowekea 'vikwazo vya visa' zitazua mjadala vigezo

Hakuna sababu ya nchi hizo kulalamika, mijadala US unatosha kuamsha hisia kilichofanyika ni alichosema kuzuia Waislam' wasiingie US ambayo kama Rais ana haki

Kuna resentment katika mataifa 7,yataungwa mkono kichini chini na wenye imani hiyo

Mapambano ya ugaidi yatachukua sura tofauti kwa kauli za awali hata kama zilikuwa katika kampeni au ni sahihi kwa mujibu wa free speech

Kwa wanajamvi, mijadala kama hii haishii US. Ni Taifa kubwa na athari zinafika kila kona. Kwa haraka unaweza kuona ni Mataifa saba yenye matatizo ikiwemo Syria

Baada ya muda wa exec order hakuna anayejua sheria gani itafuata na na makali gani

Mtanzania unatakiwa ujiulize kama kipaumbele ni kwa Wakristo kwa mtazamo wa Trump ambao ni haki kama Rais, wewe wa Visa upo kundi gani kama jina lako ni Hussein?

Mohamed Ghaillan aliyefungwa kama Mtazania kwa kushambulia ubalozi wa Marekani
Je , kwa mwendo wa Mzee Trump Tanzania ipo katika kundi gani hata kama si la 7?

Haya ndiyo tunayojadili ili kuona yanaweza kuwa na athari gani kwa ujumla

Wasiotuelewa kwa 'mabandiko yasiyowasaidia' na hafifu wanachaguo la kutosoma, tutaendelea kueleza kile kidogo tulicho nacho huenda mtu akapata kipunje kuliko kuambulia hoja za matusi na ushabiki usio na mantiki kwa kila mtazamo

Tusemezane
 
Vyombo vya dunia vinazungumzia habari za US na mwelekeo wa siasa kwa ujumla. Tulizungumzia wakati wa Bush, Obama na sasa ni Trump. Habari hazivumbuliwi bali hujitokeza
Hebu toa link ya thread ya U-Rais wa Bush na Obama ili uondoe hoja ya kwamba upo obsessed na Rais Trump.

Ni wendawazimu kuzungumzia Obama ambaye hata alipo hajulikani. Na ujuha kuongelea Hillary ambaye hana ushawishi akiungana na Romney,McCaine, Kerry n.k
Hukuelewa maelezo.

Sijui unaachaje kumuongelea Obama wakati kwa mfano tukizungumzia kurepeal na kureplace health care law tunazungumzia Obamacare, nani aliongeza regulations ambazo Trump anataka kupunguza kwa 75%, nani ameacha matatizo yote hayo ambayo Rais Trump anatatua? benchmark yake ni Obama na ndio maana Trump alishinda uchaguzi.

Ina maana Obama alikuwa mwendawazimu kumponda Bush (mtangulizi wake) kila mara hata miaka 6 baada kuapishwa kuwa Rais? Halafu kitu kama hukijui sio kwamba ndio hakijulikani, Obama yupo California ame-keep low profile.

Hillary hayupo kwenye kundi la akina Romney, McCain, Kerry n.k! Hivi huwa unafuatilia wale waandamaji wanachokisema? Kwa maelezo yako kumbe na wao ni majuha kumuongelea Hillary ambae hana ushawishi wakati wanaandamana badala ya kumuongelea Rais Trump tu?
Ushawishi na kauli za WH unaonekana kila dakika, na si ushawishi tu utata upo na huo ndio habari. Habari ndizo tunazojadili na wala si vinginevyo. Iwe nzuri au mbaya habari inabaki kuwa habari

WH haijaanza na Trump. It's okay kuwa na obsession na Trump.


Mengi huyajui au una misrepresent kuhusu ugomvi wa waandishi wa habari na Rais Trump. Hivi unajua Trump alianza lini kuwashambulia waandishi wa habari?.

Upinzani anaouzungumzia Rais Trump sio upinzani wa liberals v conservative bali ni kule kusema uongo, kwa mfano kituo cha habari kinaporipoti kuwa MLK bust imetolewa Oval Office na Rais Trump, uliberal na uncoservative upo wapi hapo? BTW liberal (left) na conservative (right) ni kutokana na sera tu wala sio mtu kusema uongo.

Ulivyoona utetezi wako huo hauna nguvu, umerukia kudai kuwa Rais Trump ana ugomvi na vyombo vya habari kwa kuwa hataki kauli zake za nyuma zilinganishwe na za sasa. Hivi na wewe ni sawa na wale libtards waliodhani Mexico itaandika cheque kwa US kwa ajili ya kujenga ukuta?

Rais wa Mexico hawezi kuleta ubabe ndio maana watu smart wamemshauri azungumze na Rais Trump. Huu ni mkakati sir, US wanajenga ukuta, Mexico watawa-reimburse in one way or another. We unajua NAFTA tu, kuna njia nyingi.
 
Agizo la kuzuia wakimbizi wa Syria linaelezwa, ni kutoa muda wa kufanya 'vetting' ili kuzuia magaidi
Jambo hili alizungumzia mara nyingi na hata kutolea mifano ya nchi kama Ujerumani

Kuna agizo la visa kwa nchi saba ambazo hakuna maelezo kwanini zinabanwa katika hilo
Nalo pia kama Rais ana uwezo hasa ikizingatiwa yeye ni Amir Jeshi mkuu na usalama ni jukumu lake

Yaliyojitokeza katika hoja zake
Kwanza, neno 'Islamic terrorist' kwa upana linajumuisha waislam,si tatizo ni mtazamo wake.

Tatizo ni kuwa nchi saba zinazohusishwa na visa zitatafsiri kama nchi za Islamic terrorist.
Hilo litaendelea kushika kasi na kujenga 'sympathy' miongoni mwa mataifa

Litaimarisha 'ISIS' na makundi mengine kwa vile wengi wataona ni 'vita' dhidi ya Uislam. Tatizo


Usiseme hakuna maelezo kwa sababu wewe huna maelezo, maelezo yapo. Kaangalie namna hizo nchi zilivyokuwa categorized na Congress na Utawala wa Obama?

Neno ni 'radical islamic terrorist', na sio mtazamo wake tu, ndio ukweli wenyewe. Kikundi chenyewe kinajiita Islamic State, naamini unajua malengo yao.

Trump amekuta hizo nchi zimeshapewa category kulingana na terrorist threat zao. Rais Trump hafanyi kazi ya kuandika terrorism profile za nchi za duniani bali anapokeaa taarifa na kutengeneza sera kutokana taarifa hizo.

Watakaoona ni vita dhidi ya Uislam wana uwezo mdogo wa kufikiri. Ukpata mda msikilize Democrat Congressional representative Tulsi Gabbard aliyeonana na kuzungumza na Rais Assad.
 
HALI YA MTAFARUKU US KUFUATIA EXEC ORDER

Katika bandiko 20 na 21 tulisema exec order iliyotolewa kuhusu wakimbizi na nchi visa nchi 7 si jambo dogo, litaigusa dunia kwa njia moja au nyingine

Nchi 7 ni Libya, Syria, Iran, Somalia, Iraq, Yemen na Sudan. Tutafafanua kuhusu hilo

Tukasema exec order haikuwa na maelezo ya kutosha inatekelezwaje.

Imetokea wasafiri kutoka nchi zilizozuiliwa wamaporudi US na kuleta hamaki na taharuki

Tangazo lkimewahusu wenye 'Green card' yaani wenye ukazi wa kudumu na siyo Raia

Ukazi wa kudumu ni mtu anaingia na kutoka nchi mwenyeji bila kulazimika kuomba visa

Mwenye green kutoka Iran akitoka hataruhusiwa kurudi katika muda uliosemwa

Hali ya mtafaruku imepelekea mahakama kutoa amri ya kusitisha kuwarudisha waliofika

Hii haina maana ya kukiuka exec order bali kutoa fursa kwa waliofika tayari kuendelea na maisha wakati shauri likiwa mahakamani

Somo:
Katika hili kuna somo dogo la kupatikana. Kwamba, wenzetu mhimili wa mahakama unafanya kazi zake kwa uhuru bila kuingiliwa na kwa kuzingatia sheria.

Shauri lilikuwa la dharura na katika udharura mahakama ilikaa
Hapa kwetu inasikitisha suala dogo tu la dhamana mahakama inaahirisha uamuzi!!

Tafrani katika ulimwengu:
Tafrani iliyotokea ni mashirika ya ndege kuhakikisha wanaokwenda US kutoka nchi 7 hawasafiri kufuatia tangazo lililotolewa

Lakini si kwa nchi 7, hata wasafiri kutoka US kwenda nchi kama Iran nao wameathirika

Hili limeleta kashakshi katika sekta ya usafiri,kuonyesha tunachosema ukuu wa US

Tafrani ya pili ni 'Diplomatic row' yaani mzozo wa kidilpomasia

Inaendelea
 
Tafrani ya Pili

Diplomatic row (mzozo wa kidiplomasia)

Iran imejibu kauli ya kupiga marufuku wananchi wake kuingia US kwa kufanya kwa US
Hii ina maana Raia wa US wanaolamika kuomba visa kuingia Iran sasa hawatepewa

Nchi nyingine kama Iraq zinafikiria hatua ya kulinda uhuru wake 'sovereignty'

Tuangalie nchi 7

Libya: Baada ya kuanguka kwa dola ya Ghadafi, nchi imekuwa na instability kubwa
Imekuwa sehemu ya kufunzia makundi kama ISIS kwa mujibu wa US

Somalia: Hii haina serikali kukiwa na mgawanyiko wa Somaliland n.k.
Serikali ya Mogadishu haifanyika kazi katika kiwango kinachoeleweka

Hata kabla ya Tangazo, US na mataifa mengine hayakutambua passport za Somalia
Ni failed state ikiwa na kundi la Alshabaabu linalonasisibishwa sana na ISIS

Sudan: Mzozo wa US na Sudan ni wa muda tangu ilipomhifadhi Osama kabla ya kutoroka Hilo lilipelekea US kubomoa kiwanda cha madawa kwa mabomu miaka ya nyuma
Suala la Sudan kaskazini na kusini lilichagiza sana mzozo na kuonekana ni eneo hatari

Yemen: Vita inaendelea,makundi yanayoungwa mkono na Iran (Shia) na Saudi (Sunni)
Yemen imehusishwa na kundi la Alqaeeda penisula, na watu kama Alwaki walifikia huko
Yemen imekuwa kama kiungo cha usafiri wa magaidi katika eneo la mashariki ya kati

Iraq: Hapa walipokuwepo akina Al-Zarqawi aliyesumbua sana US.
Kwasasa kundi la ISIS linaendelea kutetea maeneo iliyomiliki kwa muda mrefu

Syria: Kinachoendeleakinajulikana hasa Allepo. Mzozo wa Syria umehusisha nchi kama Russia na Iran na umesababisha wakimbizi wengi kuingia ulaya na Marekani

Mashambulizi yaliyotokea Ulaya yanahusishwa na Syria na ISIS ambao pia wana makao

Iran:Katika nchi 7 zilizotajwa, Iran haina historia ya wazi ya magaidi.

Iran inahistoria ya kuingilia kati mizozo kama ule wa Iraq, Yemen na Syria.
Imekuwa sehemu ya kutafuta suluhu ya Syria pamoja na nchi nyingine

Katika nchi 7 Iran inapolinganishwa na nchi nyingine zisizo katika orodha kama Afghanistan, Algeria, Tunisia, Pakistan, Saudia Arabia au nchi za UAE , ni hoja inayozungusha vichwa. Kwanini Iran?

Inaendelea
 
KWANINI IRAN?

Kabla ya kujadili hilo , tuseme kuwa katika mashambulizi yaliyofanyika Ulaya, magaidi yamekuwa na uhusiano na Algeria, Tunisia. Kuna nchi nyingine kama Egypt ambazo zimetajwa tajwa mar kadhaa

Zipo ishara za mashambulizi kama yale ya Mali kuhusishwa na makundi ya kigaidi
Nigeria nayo imewahi kuhusishwa na gaidi mmoja aliyeshindwa kulipua na pia Boko Haram

Lakini pia nchi kama Pakistan na Afghanistan zimekuwa katika 'watch list' ya Raia wake kwa muda
Magaidi waliofanikiwa au waliojaribu kwa namna moja au nyingine wamehusishwa na mataifa hayo

Ni nadra sana kusikia magaidi yakihusishwa na nchi ya Iran. Inapotokea nchi hiyo kuwa katika orodha ya 7 ya awali na kuziacha nchi zinazoonekana 'hotbed' inafikirisha kidogo kimantiki

Trump amekaririwa mara nyingi akizungumzia nuclear deal ya Iran kama tatizo.
Majuzi Waziri mkuu wa Israel BB alisikika akisema, inaelekea Trump analielewa tatizo la Iran

Ikumbukwe kuwa Israel ilichagiza sana US ishiriki katika kupiga mabomu au uinge mkono Israel kuishambulia Iran katika vinu vya zana za Nyuklia. Obama hakukubaliana na hatua za vita

Hilo ni moja ya mambo yaliyokuwa na tofauti kubwa kati ya BB Nyahu na Obama

Ni kwa mtazamo huo, inaelekea uwepo wa Iran hata kama ni sehemu ya kuzalisha magaidi bado kuna hoja ya kuitibua 'provoke' ili mpango mwingine ufanyike katika kubomoa vinu vya Nuklia.

Kuna uwezakano wa taarifa za Iran kusaidi au kufadhili magaidi
Pamoja nna hayo suala la vinu vya Nyuklia haliwezi kuwekwa pembeni katika sintofahamu hii

Suala la exec order ya wakimbizi au Visa si kosa.
Ni haki ya taifa lolote kuamua nani anaingia nani anatoka na kwa utaratibu gani.

Tatizo ni kuwa masuala kama haya huanzisha mizozo au malumbano kati ya mataifa
Katika dunia ya leo iliyojaa mawaa na mawenge wenge 'complicated' haya si mambo ya kiutawala tu

Mambo haya yatagusa sekta za uchumi, siasa na mahusiano ya wananchi wa dunia hii.

Kuna uwezekano tension iliyopo ikaathiri sana mwelekeo wa uchumi hasa mzozo wa Iran na US
Athari zingine zitagusa mizozo mikubwa kama wa Syria, North Korea n.k.

Kwa kuzingatia mahusiano mazuri sana ya Trump na Putin wa Russia, uhusiano wa kindugu US na Israel, Urafiki wa Iran na Russia, na ushirika wa Iran, Russia na China, pamoja na turufu ya Taiwan na North Korea, kuna tatizo mbele ya safari.

Rais Trump atakuwa na wakati mgumu kwa siasa za nje at least kwa mwanzo wa utawala

Kwanini mzozo unaweza athiri uchumi wa dunia? Tutajadili hili kwa mantiki.
Si la Dow Jones ina point 25K au 30K kwasababu imenukuliwa na blog. Ni zaidi ya hapo

Tusemezane
 
Nonsense.

Iran ni state sponsor wa terrorism na hiyo ni fact hata Democrats wanajua.

We unakuja hapa na blah blah unatafuta 'utata' ulipo bila kufikiri kwa undani kwa nini Iran yumo kwenye list.

Sir, hivi vitu unatakiwa ufikiri beyond MSM.
 
Unafanya plagiarism. Unachukua habari kutoka CNN unabadilisha lugha ionekane kama vile imetoka kwako, bila ku-appreciate source.

Ndio maana huwa nasema hujui mambo mengi maana source yako ni CNN tu, ukishasikiliza huko unakimbilia kupost bila kufikiri. Too low.

Obsession na Rais Trump inakusumbua sana na itakusumbua kwa miaka 8. Utachoka kutabiri.

Hivi wewe haya mazuri yote anayofanya Trump mpaka sasa huyaoni au hutaki kuyaona? Kuhusiana na jobs, regulations, investments, health care, trade, energy, military n.k Mbona hujawahi kuyapost? Huyajui au wewe kazi yako ni kutafuta tu habari zenye 'utata'?

Ukisikia CNN wakisema habari fulani ya Trump inaleta 'utata' ndipo na wewe unakimbilia humu kupost kama wanavyosema kule.

Unasahau hata Paul Ryan, McConnel na Republicans hadi Democrats wengine wanamuunga mkono kwenye hizo Ex. Orders zote za kudeal na immigration crisis.

Kama upo biased, kila kitu unachoandika humu kinakuwa biased. Unatakiwa kuwa objective.
 
SAKATA LA EXEC ORDER

Katika hali nyingine Senator McCain na Graham wamepingana na Trump kuhusu exec order wakisema itasaidia kuimarisha ugaidi na imefanywa bila mpangilio

Exec order iliyotolewa imeacha homeland security ikiwa haina maelezo ya kutosha ya utekelezaji
Ile amri ya wenye green card sasa imeakuwa rolled back, kwamba wanaweza kurudi

Hilo halijasadia mtafaruku kwa wasafiri. Je, wenye dual citizen wanakuwa katika kundi gani? Je,wanafunzi wanaosoma US waliotoka kwa kwa muda wataruhusiwa?

Maandamano yamefanyika katika baadhi ya miji ya US kuhusiana na sakata zima
Kinachojitokeza katika maongezi ya vyombo vya habari ni kuhusisha amri na Uislam

Kauli ya Rais Trump ya kuzuia watu kutoka nchi za kiislam inaingia kwa nguvu sasa hivi

Iran imetoa kauli, hatua hiyo ni mapambano dhidi ya Uislam.

Akihojiwa na kituo kimoja cha TV Trump alisema 'kuingia Oval office si sawa na kuagiza ujenzi wa jengo New York. Ni eneo ambalo maamuzi yanahusisha maisha ya wanadam moja kwa moja''

Trump alihusiwa na obama 'kauli za kampeni ni tofauti na mtu anapoingia oval office'
Kwa kutambua uzito wa ofisi hiyo, Trump anakiri sasa hivi

Kwanini basi anaendelea na maamuzi bila kupima uzito wake hata kama ni sahihi ?

Jibu la swali hiyo ni kuwa akiwa mtawala tofauti na kampeni bado anahitaji 'base'

Katika kufurahisha 'base' kuna maamuzi anayotoa bila maelezo ya kina.
Mfano, exec order ya ku replace and repeal Obama care ilikuwa 'symbolic'

Exec order ya obamacare imezipa taasisi kupunguza mzigo unaotokana na obamacare
Mzigo gani? Haikueleza na hadi sasa Obamacare inabaki pale pale.

House inatengeza 'accessible care', Trump anatengeneza ' everybody will be insured'
Katika hali hii kuna kipi kizuri cha kujadili? Wanaona mazuri wako wapi kuandika nyuzi tusome?

Hii ya ban ya nchi 7 nayo ipo katika kusisimua base yake kuwa anatimiza ahadi.
Kinachotokea sasa ni immigration kutoelewa nini wafanye kwasababu hakuna maelezo ya kutosha

Katika muda mfupi WH imetoa kauli kuwa tangazo si dhidi ya Waislam, yeye ni Rais wa wote
Hapa kunaokeana ku back off kidogo baada ya reaction kubwa.

Je, suala la 'temperament' lilikuwa hadithi tu za kampeni?

Trump akiwa Rais ana haki za kisheria kutekeleza sera zake.
Anapaswa kutambua si suala la 'base' yake kisiasa, popular vote itamsumbua kiasi

Tusemezane
 
Naunga mkono hoja, Trump ametumia profile iliyotengenezwa na Tawala zilizopita kupiga marufuku hizo nchi saba!! Hili linajidhihirisha kupitia kukosekana kwa Saud Arabia na Quatar na hata Uturuki kwenye marufuku hiyo! Saudia, Quatar na Turkey zimetuhumiwa sana kufadhilili 'ugaidi'! Nilitegemea nazo ziwemo.
 
SAKATA LA EXEC ORDER
Kinachojitokeza katika maongezi ya vyombo vya habari ni kuhusisha amri na Uislam..
Kauli ya Rais Trump ya kuzuia watu kutoka nchi za kiislam inaingia kwa nguvu sasa hivi...
Tusemezane
Mwalimu wangu, hapa unafanya upotoshaji nadhani bila kujua. Hivi Mwalimu, ni kweli nchi za kiislam ulimwenguni ni saba tu zilizo semwa kwenye Executive Order ya Trump!? Mtindo huu wa kufanya 'collateral damage ' na mwishoni mwa taarifa ndiyo hiyo damage inajaribu kukarabatiwa hutumiwa sana na BBC na members wengine ndani MSM !
_______
Halafu Ban yenyewe ni ya muda mfupi, siku 90 , siyo lifetim ban . Hivi hapa hamuwezi kumuelewa Trump kuwa anaangaika kuimarisha, ulinzi wa nchI wake kweli!? Utaratibu huu wa Trump tuuchukulie kama ule wa rais wetu kupiga marufuku kwamuda ajira za serikali, kupanda vyeo, mishahara ili kuimarisha uchumi wa serikali yetu! Lazima wakati mwingine tutumie theocracy(utashi wa haki wa vioNgozi waadilifu) badala ya democracy ili tuweze kusonga mbele!!
====
Kwa kifupi ulitakiwa kufafanua nchi hizo zilizopigwa ban kama nchi zinazotuhumiwa kuzalisha ama kufadhilili ugaidi wa makundi ka IS, Al Sham n.k. Kutumia lugha ya jumla ya kuwa eti "Nchi za kiislam " bila ufafanuzi wa kutosha mwanzoni, inaweza kuleta tafsiri isiyosahihi ambayo wala Trump hajailenga!
 
Mwalimu wangu, hapa unafanya upotoshaji nadhani bila kujua. Hivi Mwalimu, ni kweli nchi za kiislam ulimwenguni ni saba tu zilizo semwa kwenye Executive Order ya Trump!? Mtindo huu wa kufanya 'collateral damage ' na mwishoni mwa taarifa ndiyo hiyo damage inajaribu kukarabatiwa hutumiwa sana na BBC na members wengine ndani MSM !
====
Kwa kifupi ulitakiwa kufafanua nchi hizo zilizopigwa ban kama nchi zinazotuhumiwa kuzalisha ama kufadhilili ugaidi wa makundi ka IS, Al Sham n.k. Kutumia lugha ya jumla ya kuwa eti "Nchi za kiislam " bila ufafanuzi wa kutosha mwanzoni, inaweza kuleta tafsiri isiyosahihi ambayo wala Trump hajailenga!
Jamani naomba mnisome vizuri.

Nilichosema ni kuwa maongezi katika vyombo vya habari ni kuhusisha suala zima na Uislam.
Hapa sijasema mimi ninaeleza kilichotokea

Halafu nikasema hivi, ile kauli ya Trump aliyowahi kuitoa wakati wa kampeni 'atapiga marufuku waislam kuingia US' inapata nguvu.

Hapa nilichoonyesha ni kuwa hali iliyopo ya nchi hizo saba ikiunganishwa na kauli yake, kitakachotokea ni kuonekana kuwa nchi hizo zimepigwa marufuku kwasababu ya Uislam. Ndicho nilichoeleza

Hakuna mahali nimeweka maneno yangu, nilichofanya ni kuunganisha nini kinasemwa, nini kilitokea na hali ipoje.

Sijasema kuwa Trump amepiga marufuku waislam kama kama kauli yangu. Please

Sehemu ninapoweka kauli zangu binafsi, huwa natanguliza neno 'hoja' au ufafanuzi au mtazamo. Utajua tu kuwa ni maoni binafsi.

Rudia kuisoma nukuu yangu kama ulivyoitumia kwa umakini sana
 
Kwa kifupi ulitakiwa kufafanua nchi hizo zilizopigwa ban kama nchi zinazotuhumiwa kuzalisha ama kufadhilili ugaidi wa makundi ka IS, Al Sham n.k. Kutumia lugha ya jumla ya kuwa eti "Nchi za kiislam " bila ufafanuzi wa kutosha mwanzoni, inaweza kuleta tafsiri isiyosahihi ambayo wala Trump hajailenga!
Mbona nimezieleza nchi 7 kila mmoja ! Nikaenda mbali na kusema kwa Iran inawezekana wana taarifa za ugaidi, hata hivyo suala la nyuklia haliwezi kuwekwa pembeni.

US wanasema Iran ni sponsor wa magaidi, kwa mtazamo wangu hakuna link iliyowazi ya Iran na matukio ya Ugaidi.

Nina tumia 'inawezakana kuna taarifa' kwa kuelewa inaweza au isiwe

Nikasema vizuri tu BB Nyahu amekaririwa akisema Trump anamwelewa katika suala la Iran

Mimi sivumbui Iran, wala Trump wala ugaidi, ni vitu ambavyo vipo katika dunia.

Kauli anazotoa Trump sizivumbui, zipo. Ninatumia kidogo kushea na wenzangu.

Kuna uwezekano nikawa au nisiwe sahihi.
Muhimu , kama kuna hoja mbadala ijadiliwe, ndiyo mjadala

Mfano, Trump kasema wakristo hawakupewa kipaumbele kama Waislam kutoka Syria
Kauli hii ni rahisi lakini kiundani ni kauli nzito.

Uzito wake si wa dini, ni ku insinuate kuwa Obama alikuwa na preference na Waislam

Ni lini visa ya US iliwahi kuwa rahisi au ilitolewa kwa upendeleo wa dini?

Nilienda mbali kwa takwimu zilizopo Waislam kwa Wakristo kutoka Syria ni 38 kwa 37
Ukizingatia nchi kama Iraq almost 95% ni waislam, uwezekano wa wakimbizi wengi kuwa Waislam upo.

Nilichokifanya hapo si kumwekea Trump kauli au Obama.
Ni kufafanunua kwanini kauli ina utata

Tatizo la kufafanua lipo wapi? Mimi sipo katika kundi la kunukuu blog au maandishi

Ninashea habari na lengo likiwa kwa lugha rahisi ili kueleweka japo kidogo

Unaweza kuwa na maoni tofauti, yalete hapa tuyajadili kufunguana vichwa na macho.

Lau unaona una kingine ungependa kukieleza kwa uzuri zaidi una nafasi ya kufanya hivyo katika uzi huu au hata mwingine.

Kinachosikitisha ni watu kusoma si kwa kuelewa bali kutafuta spelling error au kufanya spinning kwasababu tu hawakubaliani na mtazamo.

Na wengine wanajitahidi ku discredit kwasababu tu hawakubaliani na maoni

Matokeo yake ni watu kusoma kwa prejudice au bila kuwa na feedback ya nini kinazungumziwa.

Kama kuna la kujadili hilo ni jema, lakini tujadili kwa maana na mantiki.

Huwezi kusema mbona hujadili repeal and replace ya ''Obamacare''!
Kwanini usijadili wewe

Halafu nitajadili nini wakati hakuna ACA ya rep au Trump, iliyopo ni ''Obamacare''
Unajadili vipi kitu kisichokuwepo eti kufurahisha watu.

Mkuu unaposema kuna upotoshaji, well, onyesha upotoshaji kisha tuambie usahihi kwa mtazamo wako
 
Naunga mkono hoja, Trump ametumia profile iliyotengenezwa na Tawala zilizopita kupiga marufuku hizo nchi saba!! Hili linajidhihirisha kupitia kukosekana kwa Saud Arabia na Quatar na hata Uturuki kwenye marufuku hiyo! Saudia, Quatar na Turkey zimetuhumiwa sana kufadhilili 'ugaidi'! Nilitegemea nazo ziwemo.
Aliulizwa Reince Priebus hilo swali, akaulizwa tena kuhusu waliofanya matukio ya kigaidi recently US kutoka nchi kama Pakistan, Afghanistan, Saudi Arabia, kwa nini hizo nchi hazipo kwenye list, akasema nchi kwenye hiyo list zitaongezeka na sio kwamba wameishia kwenye hizo saba.

Mtu anasema Trump ameban muslims, kwani katika hizo nchi 7 ukiwa mkristo (hata kama ni wachache) utaingia US?, wakati hiyo ban ni kwa ALL CITIZENS wa nchi hizo. Na vipi kuhusu waislam wanaotoka kwenye nchi 46 (ambazo hazipo kwenye list) zenye majority muslims, kwani na wao wamezuiwa?

Halafu mtu anapingaje 'extreme vetting measures', kama huna chuki na US na una malengo mabaya wala hupaswi kuwa na wasiwasi.

Rais Trump wakati wake wa kampeni alipenda sana kuwasomea watu poem ya "Snake". Mtu anaingia nchi ya watu halafu anaichukia nchi yenyewe na watu wake!

Nchi yoyote duniani wakimbizi au watu wengine (hata kama sio wote) wakifanya sana vitendo viovu kama mauaji, wizi, ujambazi, ukorofi n.k, serikali na wananchi wanakasirika na kuchukua hatua hasa ya kuwarudisha kwenye nchi zao na kubakisha wale wema tu.

Rais Trump anafanya kuzuia tatizo kabla halijatokea. Waliofanya mashambulizi kuwa wa nchi nyingine tofauti haimaanishi kuwa watu wa nchi hizo 7 hawawezi kufanya tukio au kwamba matukio mabaya yatafanywa na wale wa nchi zile zile.

Ndio maana nchi kwenye hiyo list zitaongezwa.
 
Halafu nitajadili nini wakati hakuna ACA, iliyopo ni Obamacare.
Unajadili vipi kitu kisichokuwepo eti kufurahisha watu.

Jina jingine la ACA (Affordable Care Act) ni ObamaCare, ObamaCare ni a.k.a ya ACA.

ACA na ObamaCare ni kitu kile kile.

Sasa Ex. Order ime-pave way kwa repeal na replace na inaondoa burdens za ACA (premiums zimepanda na deductibles zipo juu).
 
Nitakupa mfano, Trump kasema wakristo hawakupewa kipaumbele kama Waislam kutoka Syria
Kauli hii ni rahisi lakini kiundani ni kauli nzito.

Uzito wake si wa masuala ya dini, ni ku insinuate kuwa Obama alikuwa na preference na Waislam
Ni lini visa ya US iliwahi kuwa rahisi au ilitolewa kwa upendeleo wa dini?

Nilienda mbali na kusema kwa takwimu zilizopo Waislam kwa Wakristo kutoka Syria ni 38 kwa 37
Ukizingatia nchi kama Iraq almost 95% ni waislam, uwezekano wa wakimbizi wengi kuwa Waislam upo.

Kati ya wakristo na waislam akina nani wamekuwa/wanakuwa persecuted zaidi?

Kundi la ISIS linataka kuestablish islamic caliphate katika nchi mbili au zaidi, unafikiri kati ya wakristo na waislamu akina nani wanafanyiwa ukatili zaidi? (consider huo utofauti wa shia-sunny)

Religious minority kupewa treatment ya upendeleo inaonyesha namna gani Rais Trump anaangalia hili suala objectively na wala sio kutafuta kuwa politically correct.

Tunaomba source ya hiyo takwimu yako ya Syria.
 
Ndio maana nchi kwenye hiyo list zitaongezwa.
Yawezekana mnatetea upuuzi wa Trump ku'justify' ujinga unaoendelea kutendekea hapa nchini kwetu. I find it so hard to argue with some of you people; it is like you have eyes but can't see and you have you have ears but can't hear or listen.

Kuitawala Marekani si rahisi kama mnavyodhani...eti mtu, hata akiwa Rais, anaweza kuamka tu na kuanza kutoa kauli za ajabu ajabu na watu wakamnyamazia. The honeymoon will soon be over and somebody is in for a very rude awakening...

Kuna watu wameukata na wakae tu mkao wa kula kwani watalipwa mahela kibao kwa kitendo cha huyo mkurupukaji-in-chief. Marekani mambo hayaendi hivyo kama anavyofikiria, anawapa watu usumbufu usiokuwa na lazima.
 
Yawezekana mnatetea upuuzi wa Trump ku'justify' ujinga unaoendelea kutendekea hapa nchini kwetu. I find it so hard to argue with some of you people; it is like you have eyes but can't see and you have you have ears but can't hear or listen.

Kuitawala Marekani si rahisi kama mnavyodhani...eti mtu, hata akiwa Rais, anaweza kuamka tu na kuanza kutoa kauli za ajabu ajabu na watu wakamnyamazia. The honeymoon will soon be over and somebody is in for a very rude awakening...

Kuna watu wameukata na wakae tu mkao wa kula kwani watalipwa mahela kibao kwa kitendo cha huyo mkurupukaji-in-chief. Marekani mambo hayaendi hivyo kama anavyofikiria, anawapa watu usumbufu usiokuwa na lazima.
Naelewa unachosema na nakubaliana na wewe kwa asilimia kadhaa. Mimi kuna baadhi ya mambo ambayo ningependa Trump arekebishe kuhusiana na namna anavyotawala US ili vitu vingi viende sawa.

Kwa mfano, ku-reach out kwa watu ambao hawakumpigia kura. So far amestick na base yake na wale wengine wanamuona kama hana time nao.

Kuacha ku-pick fight na media na kuwaita 'opposition party', kuna moderate ways za yeye kudeal na dishonest media, so far bado yupo extreme.

Kufanya Press conference badala ya ku-tweet kila mda. Angepunguza ku-tweet na kuacha kutumia Twitter Account yake ya binafsi ile ya zamani. So far akiwa na jambo anaingia Twitter.

Ukiachana na hayo kuna mazuri yanafanyika kwenye huu utawala and those are also worth mentioning.

Kuna companies zishaanza kurudi kuwekeza US na kutengeneza ajira, energy projects zinaendelea na zingine zinaanzishwa, amesave mamilioni ($) kwenye F-35 program, aliipa Dept of Defense siku 30 kuja na plan ya ku-defeat IS, ana-end sanctuary cities, yupo concerned na violence ya Chicago, ujenzi wa border wall upo underway na Netanyahu amesema wazo la Trump linafanya kazi hata yeye border wall imemsaidia kuzuia illegals.

Rais Trump anataka kupunguza regulations kwa 75% -80%, kupunguza corporate tax toka 35% (moja kati ya kubwa kwenye nchi zilizoendelea) hadi 15%, ameitoa US kwenye TPP, ana mpango wa kurekebisha NAFTA n.k Hayo yote amefanya huku Secretaries wawili (Defense na HS), Nikki Haley na Mike Pompeo ndio pekee waliokuwa approved hadi sasa, wengine wakicheleweshwa na Democrats.

Kwahiyo ninavyosema tuwe objective ni kwamba upsides na downsides zote zinakuwa examined.
 
Kamtengua attorney general, kamteua mwingine. Ni baada ya mtenguliwa kuwa mkaidi katika Kutekeleza Ex.orders
===
Bahati mbaya sana, kuna baadhi hawataki kufananisha uendeshaji wa US kupitia Trump na ule wa Rais Magufuli na Tanzania japo hata kwa asilimia 40.
Ila kutokana na kutafutiana kwa asilimia 60, Tanzania itasonga mbele zaidi!
 
MATUKIO KATIKA MASAA 24

Sakata la waandamanaji kupinga kuhusiana na exec order linaendelea US na maeneo mengine

QUEBEC
Kumetokea shambulio katika msikiti wa Waislam jana jioni wakati wa sala ya jioni na watu 6 kuuawa, wengine 5 wakiwa katika hali mbaya na wengine wakiwa wamejeruhiwa

Mtuhumiwa wa shambuli hilo la 'kigaidi' anaitwa Alexander Bisonnete anayeshikiliwa na Polisi
Hakuna taarifa zaidi kuhusiana na tukio kwa vile uchunguzi unaendelea

Imesemwa na baadhi ya wafuatilia wa habari kuwa, mshambulia alikuwa mwanafunzi wa Laval Univ
Miongoni mwa walio uawa ni pamoja na profesa wa idara ya kilimo ya Laval University

Polisi hawajaeleza kama shambulio lilichagizwa na ideology, religious or political motivations
Ni mapema mno kusema lolote kwasababu Polisi wapo 'tight lipped'

Hoja: Mashambulizi yametokea sehemu nyingi duniani kwasababu mbalimbali. Kupotea kwa maisha ya watu hakuwezi kuwa na msamaha wa waina yoyote bila kujali motivation.

Kinachofanya tukio hili liwe 'unique' ni timing yaani muda.
Yamekuwepo maandamano yakihusisha amri ya Trump US na hata nchi kama Canada.

Tukio hili labda liwe na motivation nyingine isiyohusiana na sakata la maandamano
Ikitokea kuna element za chuki, mathalani limefanyika kwa 'religious hatred' au kwa misingi ya 'white supremacist' litaunganishwa na matukio yanayoendelea na kumgusa Trump

MASHAKA KATIKA MASOKO YA MITAJI

Inaendelea...
 
Back
Top Bottom