Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
15,314
31,093
Wanajamvi

Uchaguzi wa US umekamilika jana baada ya D.J Trump kuwa Rais wa 45
Leo ilikuwa siku ya kwanza kamili ya Trump kama Rais wa US

Uzi utakuwa utaangalia serikali mpya na mwelekeo wa siasa na uchumi
Siasa za Marekani , taifa lenye nguvu katika uso wa dunia zinaathari kubwa duniani

Ni kwa kuzingatia hilo, uzi utaleta kwa kadri, yanayojiri katika Taifa hilo

Tutaendelea kumalizia hotuba ya Trump baada ya kutawazwa katika uzi huu
Duru za Siasa: Matokeo ya Uchaguzi Marekani

Rais Trump, mfanyabiashara aliyefanikiwa katika biashara ameondoka katika utawala wa makampuni na sasa ni mtawala wa umma na Taifa la Marekani

Kuchaguliwa kwake kama mtawala wa juu wa Taifa lenye ushawishi umekuja na mshtuko kutokana na nafasi aliyopewa katika uchaguzi wa ndani ya chama cha Republican na ule mkuu

Kuna mitazamo tofauti kuhusu kuchaguliwa kwa Trump. Kwasababu zozote ambazo wachunguzi wanaendelea kuzifuatilia kisiasa , uchumi, jamii n.k. Trump ndiye Rais wa Marekani

Siku ya kwanza, Trump amekumbana na changamoto za utawala wa nchi na si kampuni binafsi

Katika historia ya miongo michache ya Marais wa US, siku ya kwanza haikuwa nzuri kwake

1. Maandamano ya wanawake duniani
2. Ziara iliyozua utata katika Intelligence community (IC)

Tutajadili mambo hayo mawili na picha ya haraka ya nini kitarajiwe kwa siku za usoni

Tusemezane
 
SIKU YA KWANZA

Ilikuwa kuboronga

Jumamosi ilikuwa siku ya kwanza kamili kwa Trump akiwa Rais wa US
Katika siku hiyo kulikuwa na tukio lililoitikisa dunia.

Akina mama waliandama katika miji mikubwa US na dunia wakieleza hisia zao.
Lengo lilikuwa kutoa ujumbe kwa Trump kutokana na mazonge zonge ya kampeni

Maandamano yalibadilika na kuhusisha makundi yanayoona wakati mgumu mbele ya mkono wa kiongozi wa Taifa kubwa dunia.

Mtakumbuka, tulijadili, utawala wa nchi ni tofauti na wa kampuni, shirika au taasisi.

Trump alidhani mbinu zalizotumia kuhamisha mijadala wakati wa kampeni zingedumu. Alijisahau ni Rais na Oval office ni ofisi kubwa

Katika kuondoa watu wasifuatilie maandamano, Trump alifanya ziara ofisi za CIA

Kwanza, aliwahakikishia anawaunga mkono kwa asilimia 100 na ana imani 100%
Pili, aliwashambulia waandishi kwa kumchonganisha na IC akiwaita dishonest people

Mbinu hii badala ya kuhamisha mjadala wa maandamano, ilizua tafrani na kumdhalilisha

Waandishi walimkalia kidete kumthibitisha alivyo kigeu geu na asivyoaminika

Jan 11 2017 alisikikia akisema IC zimefanya jambo kama NAZ hata NAZI wasingeweza kufanya hivyo. Juzi alisema ana imani nao sana

Huko nyuma alisema IC imekuwa ya kisiasa, alipokwenda aliongelea mambo ya siasa

Trump amekuwa katika mzozo na wakuu wa IC kiasi cha kusema wanatengeneza kesi

Juzi kasema hana mzozo nao bali waandishi wa habari wanamchonganisha

Trump akageuka kuongelea nani alikuwa na umati mkubwa.
Alikasirishwa na picha zilionyesha umati wa kutawazwa na siku za nyuma

Hapa ndipo alipodharaulika. Madai yake, alikuwa na umati mkubwa akiapishwa
Mchana akamtuma press sec kwenda kueleza umati ulikuwa mkubwa ktk historia

Suala la umati halikuwa na maana kuongelea akiwa na IC.

Ni mambo ya kisiasa yasiyohusiana na shughuli na zaidi ya hapo ni jambo lisilo la maana

Siku hiyo vyombo vya habari viliifanya Marekani 'laughing stock'

Inaendelea....
 
KWANINI SIKU YA KWANZA HAIKUWA NZURI?

Kilichoamsha mjadala wakati wa ziara ya Rais Trump CIA ni hoja ya umati uliokusanyika

Trump ni Rais wa Marekani, kaapa mbele ya dunia hakuna tena wa kupunguza Urais wake

Akiwa katika chombo cha usalama na kuongelea crowd iliyokusanyika imesikitisha.

Kulikuwa na sababu gani za kulinganisha umati?

Ni Rais agani aliyepoteza Urais kwa sababu tu hakuwa na umati wakati wa kuapishwa?

Pres sec akajitokeza katika mkutano wake wa kwanza kutetea hoja ya umati
Hoja hiyo ilikuwa na ulazima wa kutetewa na WH? Akajikutaakiwa na wakati mgumu

Tuliwahi kusema meneja ambaye ni mshauri wake ana walakini katika ujenzi wa hoja

Kufuatia suala la umati uliohudhuria, na baada press sec kutoa taarifa, Kellyanne Conway alijitokeza kueleza kwanini ililikuwa muhimu kulifafanua kama alivyoseam Rais

Kellyanne alisema hizo ni jitihada za kueleza 'alternative Facts' .

Neno limekuwa kejeli, ndio msingi wa kusema habari ya J'mosi 'laughing stock'

Trump alishambulia vyombo vya habari akiwa IC kwamba vinatengeneza migogoro
Rais wa US amesahau tweets na video zinazofanyiwa marejeo

Waandishi wametunga habari gani zaidi ya zile anazoeleza katika tweets na hotuba zake?

Kwa mfano, zipo habari zilizozagaa kuhusu kukutana na wajumbe wa Bunge huenda kesho likawa maongezi kama litathibitika.

Kwa namna fulani ataweza kubadili mazungumzo ya Jumamosi.

Hata hivyo, yeye ni Rais si mteule au mgombea. Kila analosema linapewa uzito stahiki.

Baada ya hizo flipflop za Jumamosi, Trump aliendelea na ratiba yake Jumapili
Ilionekana akiwa kama Rais na mwenye kauli zisizo na utata.

Hata hivyo uharibifu wa Jumamosi ni mkubwa kufunika habari zilizofuata

Vita ta Trump na media aliyosema, itamsumbua.
Anapokashifu media za dunia kwa uzito wake, ategemee makubwa.

Frustrations zitakazotokea zita derail message yake kwa kiasi fulani

Trump alipomsema Obama na uzawa wake, Obama alikuwa na 'thick skin'.
Hakupeleka mzozo katika shughuli zake ingawa ilimsumbua na kumuuma sana.

Trump atarajie habari za maudhi ni sehemu ya ukubwa wa utawaka wa Taifa kubwa

Anapo react anawapa wasaidizi wake kama Kellyanne Conway au Sean wakati mgumu achilia mbali embarrassment anayopata VP Pence ambaye ni mtu makini sana

Tusemezane
 
KAULI YA RAIS NA WASAIDIZI WAKE NI KAULI YA WH

Marekani wana utaratibu wa kuheshimu sana taasisi zao
Katika uchaguzi uliomalizika, wote wanaitambua taasisi ya Urais (WH)

Kauli ya WH kutoka kwa wenye mamlaka hupewa uzito unaostahili
Hili ni tofauti na kauli za kampeni au kipindi cha mpito (transition)

Upo utaratibu wa Marais wastaafu kutotoa kauli zinazohusu utawala uliopo
Hata hivyo, wagombea wa nafasi hiyo huwa na nafasi ya maoni kwa serikali

Ni kwa mintaarafu hiyo, kauli ya Trump ndiyo ya US si ya Obama wala Clinton
Hakuna nafasi ya kufanya ufanano wa Rais na waliostaafu au kushindwa

Rais Trump na wasaidizi watawajibika bila ufanano wala ulinganifu isipokuwa tu pale kutakuwepo na marejeo ya sera au mambo mengine

Obama aliwajibika kwa kauli kuhusu ugomvi wa Profesa rafiki yake na Polisi.
Mwisho wa siku aliita 'beer summit' kama njia ya ku apologize

Ndivyo utaratibu wao ulivyo. Watu wasitarajie 'balance' ya information

Trump aliposema ataweka kodi ya bidhaa, maCEOs wanahaha kuweka mikakati.
Ingawa inahitajika mjadala bungeni, lakini kusema tu 35% tayari ni habari

Kauli ya Press sec na mshauri Kellyanne Conway ni ya WH
Hawa si watu wa kampeni au transition, ni watu wenye mamlaka kamili

Kellyanne ametoa taarifa,ya audit kukamilika, Trump hataweza kutoa 'tax returns'

Ni kauli ya WH si ya kampeni au transition na inajadili kwa muktadha huo

Equally, kauli ya Kellyanne ya 'alternative facts' inapewa uzito ule ule ni ya WH

Wanaokubaliana au kutokubaliana na Trump wana kitu kimoja in common.
Kwamba Trump ni Rais wa US na WH ni taasisi, watumishi wanakuja na kuondoka

WH itakuwa accountable kwa yote na kwamba ni taasisi ya umma

Itakuwa ni non sense kulinganisha WH na Hillary,Romney, Obama au Bush.

WH itawajibika kwa Wamarekani na Rais aliyepo madarakani

Tusemezane
 
TRUMP NA UHALALI WA URAIS WAKE

Ilianza na kuhoji matokeo ya baadhi ya state, Trump akasema ni jitihada za ku 'deligitimize'

Likaja suala la Russia na hacking, hoja ikawa hiyo hiyo

Likarudi suala la popular vote, majibu yakawa kuingia kwa wapiga haramu 3-5milioni

Juzi kulikuwa na suala la crowd( umati) ambalo Trump alilikuza bila sababu ya maana
Umati uliofika hauwezi ku deligitimize urais, Trump akasema ni ku deligitimize Urais wake

Hilo likawaweka wasadizi,Kellyanne, katika mazingira mabovu ya kauli 'alternative facts'

Hata kama angeapishwa akiwa na mkewe, Trump anabaki kuwa Rais wa Marekani

Leo kumetokea jingine likirudia, kwamba, kulikuwa na fraud ya wapiga kura 3-5milioni

Hoja: Uthbitisho wa madai yake ya wapiga haramu ni study zilizofanyika 2012 ambazo pia hazikuwa na conclusion ya kutosha ya ku back up madai hayo

Trump ni Rais ana uwezo wa kuagiza uchunguzi. Kwanini asifanye ili ukweli ujulikane?

Je, popular vote inaathiri vipi matokeo ya electoral college 270+ na state zaidi ya 30?

Kuna umuhimu gani wa popular vote ikiwa nguvu ya Marco Rubio ni kubwa kuliko Hillary?

Haya yanasaidia kuji 'deligitimize' mwenyewe akiyaleta mijadala na kisha kulaumu media

Wengi wanadhani Trump ni mjinga, si kweli.

Katika wiki hii ameanza na mambo mazuri aliyoahidi hata kama kuna asiyeyakubali
Yote yamefunikwa na habari 'trivial' zinazoendelea

Trump amefanikiwa kuhamisha mjadala wa mshauri wake Flynn nayechunguzwa kwa maongezi na balozi wa Russia siku Obama apoweka vikwazo kwa Russia!

Anahamisha mjadala alioanzisha wa crowd ambao sehemu umekuwa kichekesho cha US

Pili, suala la tax returns limerudi baada ya audit kukamilika.Nalo linaonekana tatizo kwake

Kama tulivyosema bandiko la awali, Trump ni Rais wa US na kila kitu kipo katika rekodi.

Kunaweza kutokea kuahirisha kwa hoja lakini zitarudi mbele ya safari. Ndivyo US ilivyo ushahidi upo

Tusemezane
 
TRUMP NA UHALALI WA URAIS WAKE

Leo kumetokea jingine likirudia, kwamba, kulikuwa na fraud ya wapiga kura 3-5milioni

Hoja: Uthbitisho wa madai yake ya wapiga haramu ni study zilizofanyika 2012 ambazo pia hazikuwa na conclusion ya kutosha ya ku back up madai hayo

Trump ni Rais ana uwezo wa kuagiza uchunguzi. Kwanini asifanye ili ukweli ujulikane
Katika tuliozungumzia uzi uliotangulia baadhi yanapata uelekeo.

Suala la fraud ya watu milioni 3-5 waliopiga kura limechukua sura mpya.

Rais Trump anategemewa kupitisha exec order ili uchunguzi ufanyike.
Hili ni swali tulilouliza mapema, kwani hafanyi hivyo

Katika hali nyingine , aliyeandika study inayotumiwa na Trump na wasaidizi 'amejitokeza'

Katika aliyoeleza ilikuwa study na yaliyotokana ikipingana na madai ya fraud

Wasaidizi wametafuta study inayoonyesha mamia ya fraud na baadhi kushtakiwa

Hapa kuna mambo mawili au matatu yatakayotokea
1. Kufanya uchunguzi kutapunguza uzito wa tuhuma zisizo na ushahidi wa kisayansi

Tuhuma zisizo za kisayansi: GOP wanaona madai hayana msingi. Hawamuungi mkono
GOP wanajua matokeo hayabadili ukweli. Wanatambua kuweka 3-5M ni kujifunga'kitanzi'

Republicans wana magavana wengi na hiyo itazua maswali, fraud ilifanyikaje wakitazama

Na je uchunguzi unaweza kutoa matokeo yanayofikirisha katika wapiga mamilion ?

2. Limeanza kutibua Democrats, wanasema hiyo ni mbinu ya kuweka voter 'suppression'
Waliofuatilia uzi wa 'uchaguzi wa US' tumeongelea voter suppression na Gerrymandering.

3. Uchunguzi utachagiza uchunguzi wa Russia na Tax returns

Kama kuna fraud inachunguzwa 'hacking ya Russia'' itakuwa na nguvu na kufuatiliwa

Trump atajfunga kamba, hawezi kukataa uchunguzi wa hacking akifanya wa fraud.

Kama mtakumbuka Obama alitoa msamaha kwa askari aliyetoa habari kwa Wikileaks.
Ilichukua masaa GOP wakaja juu. Ulikuwa mtego na walipobaini, habari imekufa kabisa

Trump haongelei kwasababu kuna suala la ku encourage hacking alilowahi kusema.
Ni ngumu sana ku square mambo matatu kwa wakati mmoja
 
incorrigible - not easily swayed or influenced
obsessed - dominated, pre-occupied

The following defns should suit your buddy;

An incorrigible person or incorrigible behaviour is bad and impossible to change or improve.

Obsessed: Unable to stop thinking about something; too interested in or worried about something.

Mmh! Interesting...I wonder who really fits the above descriptions, Nguruvi3 or El Jefe!

I was checking but I failed to find a thread like 'US chini ya B.H. Obama' in Jamii Forums. Does it mean Pres. Trump is more popular than the former President after inauguration? or does it mean someone is obsessed with Pres. Trump? you tell me

You and your pal are getting worked out on footnotes, the Dow has hit 20,000, a lot of good things have happened in just 5 days and will continue to happen, but you can't see those stuffs in your pal's mediocre posts because he doesn't know much.
 
UTAWALA NA KAMPENI NI VITU VIWILI TOFAUTI

Ni kawaida viongozi kuwa ya kutenda baadhi ya mambo wakiwa madarakani
Haya hujidhihirisha katika kampeni au muda ambao kiongozi husika hana mamlaka

Mwl Nyerere aliwahi kuulizwa ni kitu gani anajutia hakufanya vizuri.
Mwl alijibu, kuua vyama vya ushirika lilikuwa kosa. Hii ni wakati akiwa amestaafu.

Ndivyo alivyoulizwa Mkapa na kujibu ubinafsisha ungeweza kufanywa kwa umakini zaidi.

Viongozi wote duniani wanamtazamo huo iwe mataifa makubwa au madogo

Kauli nje ya utawala au wakati wa kampeni si lazima zilandane na kila hali anayoikuta kiongozi

Kuna watu wanahji maamuzi ya Trump katika siku chache za utawala wake

Trump hana kitu tofauti kwa kutoa exec orders. Ndivyo ilivyokuwa kwa watangulizi

Anachokifanya ni ku 'deliver' ahadi zakampeni. Trump aliahidi mambo kadhaa anayotekeleza

1.Kufuta ACA inayojulikana kama Obamacare siku ya kwanza ofisini.
Baadaye akasema ata repeal and replace baada ya kuulizwa akifuta itakuwaje

Siku ya kwanza alisaini 'symbolic' exec order ya ku repeal and replace ACA.
Hakuna details ni kutimiza ahadi kwa wapiga kura kama mkakati wa kisiasa

Kuzungumzia Obamacare katika majukwa ni rahisi. Katika utawala ambapo watu milioni zaidi ya 20 wamejiandikisha ni suala linaloleta mtafaruku kwa jamii likiathiri maeneo kama uchumi

Ugumu unaonekana kutokana na ukweli premiums kwa baadhi ya state imeongezeka kufikia 100%.
Kwa upande mwingine wapo waliofaidika na Obamacare,wasingetaka itoweke

Katika idadi ya mamilioni, maamuzi yanahitaji umakini wa hali ya juu.
Si suala la kusema bali kusema na kueleza inafanyikaje na kwa njia gani.

Republican wanaohodhi mihimili miwili ya Bunge na utawala wapo katika kusigishana

Kwanza, hakuna mbadala wa obamacare, kwa maana ndio kwanza wanaandika

Pili, Trump anasema 'insurance for everybody' . Republican katika house- 'accessible insurance'

Coverage ya kila mwananchi na kutoa access ya insurance kwa wote ni vitu viwili tofauti

Hapa ndipo tunaona kauli za kisiasa zinapokuwa na ugumu katika kutawala

Tunakuja katika hoja ya pili ya Uchumi ya Trump kuhusu 'protectionism and crony capitalism'

Inaendelea
 
You and your pal are getting worked out on footnotes, the Dow has hit 20,000, a lot of good things have happened in just 5 days and will continue to happen, but you can't see those stuffs in your pal's mediocre posts because he doesn't know much.
Do you even know how the Dow got to where it was on Trump's inauguration day? From a miserable 6,000 to 19,000 during Obama's term, do you even know what that means? That was more than three times or to put it more bluntly from a mathematical perspective a 280% increase. And Trump calls him stupid...yet do you know how much Trump made out of this, how he benefitted financially?

And now to obsession, consider these two scenarios...one agrees and believes in everything Trump does or says while the other doesn't agree and questions everything said or done. As you can see it is all in the eyes of the beholder but if I had a choice, and judging from what is happening, I'd be very cautious with a man who believes nobody else, but only he, can accomplish what's best for America.
 
Do you even know how the Dow got to where it was on Trump's inauguration day? From a miserable 6,000 to 19,000 during Obama's term, do you even know what that means? That was more than three times or to put it more bluntly from a mathematical perspective a 280% increase. And Trump calls him stupid...yet do you know how much Trump made out of this, how he benefitted financially?
As said, 280% amid great recession of our times, 9% unemployment, and two front wars raging
 
UTAWALA NA KAMPENI NI VITU TOFAUTI
Sehemu ya II

Trump anasema 'Buy America hire America'

Katika kutimiza azma, ameonyesha sera za 'crony capitalism, mahusiano ya watawala na mabepari

Mfano, kuongea na maCEO wa makampuni na kuwashawishi wawekeza
Kuweka tishio la kodi asilimia 35 ili kuwatisha kuhusu uwekezaji nje ya nchi

Hapa kuna hoja mbili

Kwanza, crony capitalism ni tofauti na free market ambayo ni sera ya Republican
Pili, kazi ya serikali za kibepari ni kujenga mazingira na kuacha nguvu ya soko ifanye kazi

Trump anapozungumzia kupunguza kodi hilo ni jambo jema, anajenga mazingira ya uwekezaji

Hatua anazochukua zimelenga kutengeneza ajira na ustawi wa jamii yake
Kuwatisha CEOs kwa kodi tayari kumepelekea makampuni kutangaza uwekezaji wa mabilioni

Hili pia litazuia makampuni kuondoka na kuwekeza nje ya Marekani.

Hii ina maana moja,makampuni na uwekezaji yataleta neema ya ajira . Ajira zinazolipa vizuri sana.

Makampuni mengi ya magari na vifaa yamewekeza Mexico na Canada. Hatua za makampuni kuwekeza Marekani na serikali kutoza kodi kwa yanayotoka nje itaongeza ajira kwa sehemu kubwa

Hatua za kupunguza kodi (corporate tax), kulegeza masharti ya biashara yatasisimua uwekezaji

Hata hivyo ongezeko la ajira litakuwa la muda mfupi, kwa muda mrefu inaweza kuwa tatizo tena

Matatizo: Kwanza, crony capitalism itakuwa na limitations. Kuna sera zinazotakiwa kuidhinishwa na Bunge ili zifanye kazi. Lakini pia exec order kwa sheria za US inaweza kupingwa mahakamani

Pili, gharama kubwa za uendeshaji ndizo zimesukuma wawekezaji nje ya Marekani.
Mfano, mfanyakazi anaweza kulipwa dollar 5 kwa saa nchini Mexico wakati US akilipwa 20 hadi 30

Inaendelea
 
Inaendelea

Ongezeko la gharama za uzalishaji itazilazimu kampuni hizo kupitisha gharama kwa mnunuzi
Ina maana bidhaa zitakuwa ghali ukilinganisha na wakati huu.

Tatu, protectionism italazimisha nchi nyingi kuchukua hatua kama hizo kulinda masilahi yao
Jambo hili litapunguza wigo wa soko za bidhaa za Marekani katika dunia

Kwa masuala ya kodi, Bunge hujadil kwa kutambua uhusiano kati yake na wananchi.
Hakuna uhakika kama corporate tax au import tax anazopendekeza Rais ni za uhakika

Kutokana na mambo hayao matatu mbele ya safari haya huenda yakajitokeza

1. Makampuni kuelemewa na gharama za uzalishaji na hivyo kutafuta njia za kupunguza
Utengenezaji utahama kwa watu na kufanywa na mashine. Ajira zitaanza kupungua

2.Ongezeko la gharama za uzalishaji zitafanya bidha 'non competitive' katka soko la dunia
Kunaweza tokea trade deficit itakayoathiri uchumi

3. Protectionism itazua trade war kati ya US na Mataifa wapinzani kama China

Anachofanya Trump ni ku deliver alichoahidi. Hata hivyo, suala la buy America hire America likely litakuwa na repercussions na si furaha ya ajira tuu

Siasa inayotaka kutumika katika negotiations itaishia kwa sakata la Mexico na US lililotokea leo

Tusemezane
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Do you even know how the Dow got to where it was on Trump's inauguration day?

The Dow Jones Industrial Average hit 20,000 in trading on Wednesday (25 th Jan) and not on Trump's Inauguration day (20th Jan). Kindly fact check.
From a miserable 6,000 to 19,000 during Obama's term, do you even know what that means? That was more than three times or to put it more bluntly from a mathematical perspective a 280% increase. And Trump calls him stupid...yet do you know how much Trump made out of this, how he benefitted financially?
The Dow has punched through the 20,000-point barrier for the first time. It's called Trump effect, it means the stock market is seeing a pro-business administration that is minded to action.

Seems you don't have a 5 days figure to compare that with, instead you brought an 8 years figure, it's okay.

750x422


And now to obsession, consider these two scenarios...one agrees and believes in everything Trump does or says while the other doesn't agree and questions everything said or done. As you can see it is all in the eyes of the beholder but if I had a choice, and judging from what is happening, I'd be very cautious with a man who believes nobody else, but only he, can accomplish what's best for America.

When Pres. Trump was asked about 'torture' and 'waterboarding' by ABC's David Muir in an interview in the WH on 1/25/17, do you remember how he answered that question? And you tell me how someone who believe nobody but himself would give such an answer.

And you tell me how President Trump's directive to his cabinet nominees to be themselves in senate confirmation hearings is consistent with someone who believe in only himself.

There is a difference between 'believing in oneself' and 'believing in only oneself'. Pres. Trump believes in himself and believes in consultations with others to get the job done.
 
YALIYOJIRI LEO KATIKA SIASA ZA US

Kwanza, tuseme kuna misconception ya kwanini tunazungumzia siasa za Marekani
Dhana hiyo si kwel tunazungumzia siasa za dunia ambazo US kama Taifa kubwa linaushwishi

Leo amekutana na PM May, kesho anaongea na viongozi wa Russia, Germany na France
Haya ni mataifa yanayoweza kubadilisha mitazamo ya siasa za dunia.

Kwanini tumuongelee Rais wa Gambia ambaye hata uwepo wake Ikulu haujulikani?

Vyombo vya dunia vinazungumzia habari za US na mwelekeo wa siasa kwa ujumla
Tulizungumzia wakati wa Bush, Obama na sasa ni Trump. Habari hazivumbuliwi bali hujitokeza

Ni wendawazimu kuzungumzia Obama ambaye hata alipo hajulikani.
Na ujuha kuongelea Hillary ambaye hana ushawishi akiungana na Romney,McCaine, Kerry n.k

Ushawishi na kauli za WH unaonekana kila dakika, na si ushawishi tu utata upo na huo ndio habari
Habari ndizo tunazojadili na wala si vinginevyo. Iwe nzuri au mbaya habari inabaki kuwa habari

Mashambulizi ya habari

Rais Trump ameshambulia vyombo vya habari a kuviita 'upinzani' na viko biased
Ni kweli vyombo vina 'interest zake' ndio maana US kuna vya conservative na Liberal

Vyombo vya right or left hupata habari, habari si 'mbwa kuuma mtu bali mtu kumuuma mbwa'.
Nani anatengeneza utata? Hakuna shaka ni Trump na utata anaouzua si kwa bahati mbaya

Asichotaka Trump ni vyombo kulinganisha nini amesema jana na leo anasema nini
Huo ndio ugomvi wake mkuu na vyombo vya habari. Mfano ni mzozo kati yake na Mexico

Trump aliahidi kujenga 'wall' na kuhakikishia wapiga kura Mexico italipa gharama

Amejaribu kutumia 'wall' ili kuwalazimisha Mexico kukubaliana kwa mkataba wa NAFTA

Mexico wanaonekana kukataa kuburuzwa ikiwa ina 'set precedent' kwa mataifa mengine

Inaendelea
 
NAFTA, MEXICO NA US

Kabla ya kujadili kwa ufupi NAFTA na mzozo wa Trump na Mexico, turudi nyuma kidogo
Wakati wa Transition Trump alimpigia simu Rais wa Taiwan jambo lililoikasirisha China

Trump alipoulizwa kama haitaleta 'mzozo wa kidiplomasia' na pengine trade wars, alisema
'kama kutumia Taiwan kutaileta China katika meza ya mazungumzo ya biasha, atafanya hivyo'

NAFTA ni mkataba wa biashara wa nchi 3 za Amerika kaskazini kuondoa vikwazo vya biashara

Mkataba huo umewezesha biashara kati ya Canada, US na Mexico.
Canada na Mexico zimenufaika na soko la US na makampuni yaliyowekeza katika nchi hizo

Mkataba umewezesha uwekezaji katika nchi mbili kwasababu ya gharama kubwa za uzalishaji US
Matokeo ni ajira na export kwenda US .Hili limekuza uchumi wa nchi hizo

Kwa US, NAFTA imeongeza soko kubwa la Mexico na Canada lenye milioni 150
Malalamiko ya US ni kuwa ajira zimekwenda Mexico na Canada yenyewe ikiwa ni soko

Kauli ya Trump kuhusu hilo inapokelewa vema hasa wakati ambapo watu hawana ajira US

Trump alisema atarejea upya mkataba uwe win win situation.

Kaanza na Canada kwa kuwataka waruhusu bomba la la Keystone pipeline.
Hili amelifanya mbele ya mkutano na waziri mkuu wa Canada kama sehemu ya negotiations

Karudi kwa Mexico akiwataka walipie gharama za kujenga ukuta.
Juzi ali tweet kuwa Mexico watalipa, Rais wa Mexico akafuta ziara kujadili NAFTA

Kwa kutambua umuhimu wa Mexico kama jirani wenye interest nyingi zikiwemo za kiuchumi, Trump kampigia simu leo na kuongea naye kwa saa 1 kwa mujibu wa habari.

Hapa ina maana tishio la 20% kodi haikufanya kazi au kutumia wall ku negotiate NAFTA limekwama
Hili lingefanikiwa, ugumu wa komba Bunge litoe pesa ungeondoka

Hili linabaki na hoja mbili. Kwanza, Mexico haitalipa gharama za ukuta, na kuweka kodi ni sawa na kuwaadhibu wananchi wa US watakalopia gharama zaidi kufidia kodi ya bidhaa

Pili, njia ya kutumia weakness ya opponent inafanya kazi kwa baadhi ya nyakati na si nyakati zote

Hali hiyo atakutana nayo atakapojadiliana na China kwa kutumia ''nguvu'' ya biashara.
China watatumia karata ya North Korea na hapo patakuwa pagumu

Kauli za kampeni na kauli za utawala ni vitu viwili tofauti

Nini kinaendelea na exec order ya 'visa na refugees?

Inaendelea
 
EXEC ORDER 'YA KUZUIA WAKIMBIZI NA VISA KWA BAADHI YA NCHI'

Rais Trump amesaini exec order ya kuzuia wakimbizi kutoka Syria na nchi nyingine saba kwa muda
Hili si jambo geni, ni katika kutimiza ahadi alizotoa za Kampeni

Agizo la kuzuia wakimbizi wa Syria linaelezwa, ni kutoa muda wa kufanya 'vetting' ili kuzuia magaidi
Jambo hili alizungumzia mara nyingi na hata kutolea mifano ya nchi kama Ujerumani

Kuna agizo la visa kwa nchi saba ambazo hakuna maelezo kwanini zinabanwa katika hilo
Nalo pia kama Rais ana uwezo hasa ikizingatiwa yeye ni Amir Jeshi mkuu na usalama ni jukumu lake

Yaliyojitokeza katika hoja zake
Kwanza, neno 'Islamic terrorist' kwa upana linajumuisha waislam,si tatizo ni mtazamo wake.

Tatizo ni kuwa nchi saba zinazohusishwa na visa zitatafsiri kama nchi za Islamic terrorist.
Hilo litaendelea kushika kasi na kujenga 'sympathy' miongoni mwa mataifa

Litaimarisha 'ISIS' na makundi mengine kwa vile wengi wataona ni 'vita' dhidi ya Uislam. Tatizo

Pili, akihojiwa na TV ya kidini, Trump alisema kipaumbele kwa wakimbizi kitakuwa kwa Wakristo
Akasema Wakristo hawakutendewa haki na ilikuwa ni ngumu kwao kuingia USA kuliko Waislam

Ukweli 1: Makundi kama ISIS yalilenga Wakristo. Kwa mfano, kabila la Yazid la Iraq lilishambuliwa kiasi cha kutaka kulitokomeza. Hili ndilo kabila lenye Wakristo wengi, kwa lugha nyingi persecuted

Ukweli 2: Wakimbizi wana sifa ya watu wanaokuwa persecuted kwasababu za ukabila, rangi, imani n.k.

Ukweli 3: Idadi ya Waislam na Wakristo walipokelewa US ilikuwa karibia 38 kwa 37 Wakristo

Ukweli 4: Persecution inayotokea middle east si ya Waislam na Wakristo. Waislam ni waathirika zaidi

Ukweli 5: Ni kweli makundi yanayojihusisha na ugaidi yamejinasibisha na imani ya waislam

Tatizo la kauli za Trump ...... tunaeleza kwa undani. Inaendelea
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom