Duru za siasa: Sakata la Mawaziri

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
15,389
31,326
MIJADALA MINGINE

SAKATA LA MAWAZIRI

Sehemu ya I

Waziri wa mali asili na utalii mh Kagesheki amejiuzulu kufuatia tuhuma za Operesheni ya Tokomeza.
Operseheni ililenga kukomesha vitendo vya ujangili vya kuua wanyama kwa njia haramu

Waziri amejiuzulu kwa kuwajibikaji kutokana na matatizo yaliyotokea wizara anayoongoza.
Mh Kagasheki amekuwa mstari wa mbele kupambana na mjangili na kumuomba Rais msaada ili kulinda rasilimali ya taifa ambayo imepungua kwa kiasi cha kutisha.

Mh Kagasheki amekumbuna na kesi zinazohusu meno ya tembo mara nyingi.
Hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kufuatilia kubainika kwa ujangili huo.
Meli zimekamatwa Hong Kong na Zanzibar,wamiliki ni Watanzania wengine wakiwa na nyadhifa za juu.

Tatizo la hujuma za rasilimali za taifa halikuanza leo.
Tunakumbuka kukamatwa wanyama wakisafirishwa hai katika uwanja wa ndege wa KIA.
Ndege ya kuwachukua ilikuwa ya kijeshi na kwa tartibu za kimataifa na hata za kitaifa ni lazima kungekuwepo na taarifa ya ndege kutua na hasa ya kijeshi.

Licha ya kelele nyingi kuhusu hujuma zinazoendelea hakuna kiongozi aliyesimama kuliongelea achilia mbali kuchukua dhama kama aliyochukua Kagasheki.

Tunakumbuka kuhusu uvunaji na usafirishaji wa magogo kutoka katika misitu.
Hakuna aliyewahi kuwajibika kutokana na hilo. Na pia tunakumbuka faru chini ya ulinzi mkali kuuawa.
Faru waliosimamiwa na mh rais kurudishwa nchini

Hiyo ni mifano michache sana kuonyesha chanzo na upana wa tatizo.
Yote hayo yakitokea serikali imekuwa ikipanga bajeti kwa vikosi vifuatavyo(Rejea ripoti ya bunge 2.2.1)
Askari wa kuzuia ujangili (KDU)
Askari wa Wanyapori (TANAPA)
Askari wa Misitu (TSF)

Wakati huo huo kukiwa na idara ya usalama wa taifa (TISS) na jeshi la Polisi

Mawazri, ,manaibu mawaziri, makatibu wakuu na wakurugenzi wa taasisi hizo pamoja na zile zinazoingiliana huteuliwa na mh rais kwa kusaidiana na wasaidizi wake na vyombo alivyopewa kikazi.

Mheshimiwa rais alitangaza kupeleka jeshi kupambana na majangili yaliyoonekana kuzidi nguvu vikosi katika taasisi na wizara hizo. Mhe rais akarudia kauli yake bungeni akisema yapo matatizo yaliyojitokeza yanayohitaji marekebisho wakati wa operessheni hata hivyo ilifanikiwa.

Ni wazi serikali ikiongozwa na Rais na Waziri mkuu walipanga na kusimamia opersheni hiyo.
Ni dhahiri kuwa mtandao wa ujangili ni mpana ambao serikali iliufahamu na haikuweza kuushughulikia[Rejea taarifa ya bunge {6.2: XIV, XVII, XVIII,} {7.0: III,VIII,]

Taarifa inaonyesha waziri Kagasheki hakuhusishwa kama kiongozi wa wizara [7.0: II]
Ni wazi kuwa mtandao wa ujangili uliingia katika serikali (infiltrate) kiasia cha kuweza kupata hata siri za opereshini na hivyo waziri aliwekwa pembeni. [7:IX)

Hivyo kufeli kwa Opereshini chanzo chake ni kutokana na kuingiliwa na viongozi wa serikali na siasa ambao kamati haikuwataja waliotoa maagizo ya operesheni isiguse viongozi wa kisiasa wa ngazi yoyote.(Taarifa ya bunge [7.0: IX]

Na pia kuwatenga viongozi wa Mikoa na Wilaya ulikuwa ni mpango maalumu wa kuhakikisha kuwa mtandao unalindwa kutoka ngazi za juu na kuzuia kelele kutoka eneo lingine.

Duru za siasa tunampongeza waziri Kagasheki kwa uamuzi wake wa kuwajibika na kujiondoa katika kazi ambayo ugumu wake si kupambana na majangili tu bali wanasiasa na viongozi wa serikali ambao ni sehemu ya mtandao au ni wanufaika wa mafao yatokanyo na ujangili kisiasa au kimasilahi.

Mawaziri watatu waenguliwa
Tunaendelea sehemu ya II
 
Sehemu ya II

Rais ametengua utezui wa mawaziri watatu kwa lugha laini, kwa lugha halisi rais amewafukuza kazi.
Mwaziri hao ni wa Mambo ya ndani(Nchimbi), wa Ulinzi (Nahodha) na Mifugo (Mathayo)
Taarifa ya kutengua uwaziri wao imetolewa na waziri mkuu.

Rais ndiye mwenye kuteua mawaziri kama wasaidizi wake na hutangaza uteuzi huo na hata kubadilisha baraza ikibidi.
Imeshangaza kuona waziri mkuu akitoa taarifa hiyo badala ya rais kutoa taarifa kama mteule wao.

Katika mazingira ya kawaida yanayofuata utawala wa sheria mawaziri hao walipaswa kujiuzulu kabla ya kuenguliwa.
Kwa utamaduni wa nchi yetu ambao uwaziri si utumishi bali ulaji wao hakuona sababu ya kufanya hivyo.

Mawaziri hawakuchukua hatua kwa kuelewa kuwa katika taifa hili jambo hupita kama upepo na pengine kuelewa udhaifu wa aliyewateua. Udhaifu unaonekana katika lugha ya kutengua badala ya kufukuza, na katika kukwepa lawama kwa kumtupia waziri mkuu mzigo huo ambao hakika si mwenye dhamana nao.

Hata hivyo duru za siasa inashangazwa na hatua za rais kutengua uwaziri wa viongozi hao katika wakati huu

1. Waziri Nchimbi ametuhumiwa sana kwa kushindwa kusimamia wizara kwa matukio yaliyotisha nchi na dunia kama ya mabomu Arusha, waandishi kuuawa, na watu kung'olewa kuchwa. Licha ya hayo tatizo la tindikali na mauji vimekuwa vikiongezeka kila uchao na waziri hakuwa na suluhisho la kitaalam zaidi ya siasa. Hakuwahi kuwajibika au kuwajibishwa

2. Waziri Nahodha: Huyu amechukua wizara ya Ulinzi iliyokuwa inaongozwa na Hussein Mwinyi.
Katika nyakati za Hussein Mwinyi kulitokea mauaji ya mabomu kulipuka hovyo mara mbili na kupoteza maisha ya watu.
Pengine Rais kwa haya ya mtoto wa Mzee Mwinyi angeweza kumuacha katika mabadiliko ya mawaziri, sivyo! alimhamisha wizara nyingine bila kutengua uwaziri wake kama alivyofanya kwa Nahodha. Hakuwajibika au kuwajibishwa

Lakini pia duru za siasa tunauliza, wakati wanyama wanasafirishwa KIA Hussein Mwinyi alikuwa waziri wa ulinzi.
Dege likatua KIA bila taarifa ya vyombo vya ulinzi na usalama.

Kama ilikuwepo taarifa waziri Mwinyi alipaswa aueleze umma ni utaratibu gani ulitumika, vinginevyo angewawawajibisha viongozi wa jeshi waliohusika au Rais amwajibishe yeye.
Vipi leo kwa Noahodha ionekane kama ni tatizo kubwa kuliko tatizo la huko nyuma?

3. Waziri Mtahayo: Kuhusika kwake ni kushindwa kusimamia wizara hasa katika migogoro ya mifugo.
Hapa napo kuna swali, hivi ilikuwaje magogo yakasafirshwa siku za nyuma na hakuna aliyewajibika?
Ilikuwaje rais asione maigano ya wafugaji kama kushindwa kazi kwa waziri husika, hadi ionekane leo

Duru za siasa tunasema mawaziri hao hawakupaswa kuenguliwa.
Sababu za kusema hivyo ni kuwa hili ni la kuvunda na halina ubani.
Hatuwezi kuwa na double standard kama kweli serikali ipo serious.
Tatizo ni kushindwa (Failure of the system) kuanzia juu hadi chini.

Tunachikona kuhusu operesheni ni sehemu ndogo sana ya kushindwa kwa uongozi wa nchi hii.
Tatizo si mawaziri wanne, tatizo ni kubwa kuanzia ngazi za juu.

Hatuwezi kupiga hatua kama tutaendelea na mazingaombwe ya namna hii.
Endapo serikali ya JK ingekuwa serious tusingefika hapa tulipo.
Kulikuwa na taarifa zote kuhusu ujangili na wahusika na ujangili,leo tunadhani kilichofanyika ni kitu kipya zaidi ya usanii.

Endapo serikali imedhamiria kuchukua hatua basi hatua hizo zisiishie kwa watu wanne.
Inapaswa kuchukua hatua zaidi kwa wafuatao
1. Mkuu wa TISS kwa kushindwa kazi ya usalama
2. Mkuu wa Jeshi Polisi linalosimamia mali na usalama wa raia
3. Viongozi wa jeshi walioshiriki operesheni
4. Viongozi wote wa wizara husika, makatibu wakuu na wakurugenzi
5. Waziri mkuu kwa kushindwa kusimamia utendaji wa serikali.

Kinyume na hivyo ni kuonea watu wanne kwa kuwatoa kafara.
Uzembe unaoendelea katika wizara kama ya serikali za mitaa ni kielelezo tu kuwa hii ni system failure and not isolated case(s). The whole system is corrupt the least to say

Kamati ya bunge imetoa maagizo kuhusu serikali kuwachukulia hatua wahusika na taarifa kuwasilishwa bungeni.
Hiki nacho ni kichekesho kama si mazingaombwe.

Katibu Mkuu Jairo alikamatwa akitoa rushwa, akastaafu
Katibu kiongozi Luhanjo alikutwa na kashfa, akastaafu
Bunge lilitoa maagizo mawaziri walipohusika na ufisadi wawajibishwe, hakuna kilichotokea.

Ni kwamba hakuna kitua mbacho kinaweza kumsukuma rais kufanya kile bunge inachokitaka.
Sana sana ni suala la muda unaweza kuwasikia wahusika ni mabalozi nchi za nje.

Hiyo ndiyo Tanzania, na sioni kwanini watu wadhani serikali inafanya kazi kweli kweli na kusahau haikuwahi kufanya kazi kwa tatizo kama hilo siku za nyuma.

Lakini kinachoshangaza zaidi ni jinsi wabunge wa CCM walivyoshupalia hili jambo.
Haiingiii akilini ni lini wabunge wa CCM wamelipenda taifa hili.

Ni wabunge hawa hawa waliopitisha mswada wa marekebisho ya rasimu ya katiba wakiwa 100 na kuridhika.
Ni hawa hawa wanaoficha uchafu wa Kagoda, Meremeta, Dowans na fedha zinazobainishwa kuliwa hovyo katika halmashauri na serikali kutoka kwa taarifa ya CAG.

Leo wamepata wapi ushujaa wa kusimamia rasilimali za taifa? Kuna nini nyuma ya jambo hili?

Tusemezane
 
Mkuu Nguruvi3
Culture ya kufanya mambo bila hofu ya kuchukuliwa hatua (IMPUNITY) ndio imefufikisha hapa tulipo. Matukio ya mateso na mauaji mikononi mwa vyombo vya dola hayakuanza leo, miaka nenda rudi raia wamekuwa ni wahanga wa vipigo, kubambikiwa kesi, mateso na hata kuuawa. Lakini haijawahi kutokea hata mara moja wakuu wa vyombo hivi vya dola kuadhibiwa kutokana makosa yao.....why? Sababu hawa ni ni asset kubwa sana kwa watawala kuhakikisha kuwa wanabaki madarakani kwa hiyo kamwe hawawezi kuwatosa na kuwasulubu kutokana na uhusika wao kwenye unyama huu. Kuwajibisha waziri ni political stunt nzuri kupoza hasira za wananchi ili upepo mbaya hatimaye upite.
 
Last edited by a moderator:
Binafsi kuondolewa kwa mawaziri watatu na mmoja kujiudhuru,kwangu naamini si dawa!Tatizo ni Mfumo,ambao upo serikalini,lazima tuwe na watu wa kweli na waadilifu ili kulinda maslai ya Watanzania,tuwe na kikosi kazi kitakachokuwa kinanguvu ya kunusa na kuhisi na kuitekeleza sheria bila kuwa na Aibu!kama wenyewe hatuwezi tukodi kikosi kazi kutoka nchi zilizoendelea ili kuwasimamia watendaji wa nchi hii,wao kazi yao kusimamia katiba na rasilimari
 
@Nguruvi3

Hili sakata la mawaziri linaonesha ni jinsi gani kuna mapungufu kwenye utawala wa sheria nchi hii. Na kwa maana hiyo double standards ni jambo la kawaida kwa sababu kama wewe ni mnyonge utafanya nini?

Tuanze na Kagasheki

Huyu Mheshimiwa amenukuliwa akisema kuwa mtandao wa majangili una watu wazito. Kwa maana hiyo alijua anapambana na watu wa aina gani. Sasa basi kama ndivyo tunatakiwa kuuliza maswali machache

1. kati ya watu waliouwawa na kuteswa kwenye hiyo operatio ya 'Tokomeza ujangili' walala hoi ni wangapi?

2. Kagasheki anaweza kusema ni 'watu wazito' wangapi wamekamatwa tangu hii operation Tokomeza ujangili ianze?

3. In his right mind, wamama waliobakwa walikuwa ni miongoni mwa 'watu wazito' aliokuwa anasema ndio wenye mtandao?

4. Kagasheki alishawahi kusikia unyama waliokuwa wanafanyiwa wananchi wakati zoezi linaendelea? Ni lini alisikia na alifanya nini?

5. Lakini kubwa, ambalo nadhani hata wewe Nguruvi3 umegusia, ni kuhusu makontena na meno ya tembo. Kagasheki amekamata watu wangapi kuhusiana na makontena yaliyokamatwa?

Haitoshi kusema kuwa Waziri hakuwa anahusishwa kwenye mambo mengi Wizarani, maana kama aliona anaachwa kwenye mambo ya msingi, in principle, angejiuzulu mara moja. Kuendelea kusimamia operation za kutesa walalahoi wakati 'watu wazito' wanaendelea na mambo yao maana yake na wewe ni sehemu yote including hayo yalifanywa nyuma ya mgongo.

Dr Mathayo

Kwa waliomsikiliza huyu Mheshimiwa bungeni watakuwa na swali moja tu. Kazi za Dr ni nini? Maana karibu kila jambo anasema wizara yake haihusiki! Majosho Halmashauri, kupima maeneo ya wafugaji Wizara ya Ardhi, kusimami hata 'kusimamia sera' hana pesa! Sasa anapokea mshahara kwa kazi gani? Kwanini hii wizara isifutwe maana haina kazi.

Hivi Dr Mathayo alipokuwa anaaga familia yake asubuhi na kupanda shangingi kwenda kazi, alikuwa anenda kufanya nini? Mwaka 2013, wafugaji wanarandaranda kama wakati wa Ujima lakini huyu Mheshimiwa yeye anafurahia kiyoyozi! Na amekuwa na ujasiri wa kusimama mbele ya bunge na kusema kuwa ameonewa! Increadible!

Kama Dr Mathayo alijuwa kupima ardhi ni kazi ya Wizara nyingine kwa nini asikabane na hiyo Wizara husika ili wadau (wafugaji) wake wapate sehemu za kufugia wanyama wao? Ni lini au wapi alijaribisha kupima hata nusu Eka kwa ajili ya wafugaji? Angekuwa amefanya hata eneo dogo jana angekuwa na haki ya kulalamika kuwa fedha haitoshi, lakini hajafanya kitu kabisa.

Kwenye majosho, anasema ni kazi ya Halmshauri. Amefuatilia Halmashauri ngapi ili wajenge majosho? Kuna kipindi alifunga machinjio kule Vingunguti, hivi alirudi nyuma, au alikosa ‘fedha’ ya nauli?

Kwa ujumla Dr Mathayo ameonesha ni jinsi gani tuna viongozi wasio na ubunifu hata chembe. Sasa leo wafugaji wameuliwa analalamika kaonewa! Na hapa bado hatujaongelea viwanda vya kusindika nyama. Dr Mathayo hana mtu wa kumlaumu zaidi yake mwenyewe. Kapewa nafasi na ameitumia vibaya, sasa arudi kupigania seat kwenye daladala kama wengine.

Dr Nchimbi
Sijui mtu ataanzia wapi maana Wizara ya mambo ya ndani imesababisha maafa makubwa sana kwa raia. Watoto wameachwa yatima, wazazi wamezika watoto, watu wamepata vilema vya maisha, na vijana wameguzwa kuwa punda'. Vizazi vijavyo vitakuwa na maswali mengi sana kuhusu usimamazi wa Nchimbi. Na maajabu ya Mungu siku chache zilizopita huyu Mheshimiwa alitoa kauli bungeni kuwa serikali haitaunda tume kuchunguza mabomu ya Soweto. Painful!

Uhusiano kati ya raia na jeshi la polisi ni mbaya kuliko wakati wowote tangu nchi hii ipate uhuru.

Shamsi Vuai Nahodha

Mtu yoyote aliyekuwa kwenye hii Wizara wakati wa hii operation ya Tokomeza ujangili inafanyika angekwenda na maji. Hii ni kwasababu, kwa kiasi kikubwa nafasi ya kuongoza hii wizara is 'practically' ceremonial. Waziri huwa hana nguvu sana juu ya nini majeshi yafanye. Na kwa mtu kama Nahodha ambaye ni hivi majuzi kashuka kwenye boti, basi hakujua akanyage wapi. Bad luck!

Mwanasheria Mkuu

Nilianza kwa kusema kuwa kuna mapungufu kwenye utawala wa sheria nchini. Hadi kufikia hatua ya kutumia majeshi kwa shughuli za kiraia kuna hatua zinatakiwa kupitiwa. Mhe Tundu Lissu alijaribu kueleza bungeni ni wakati gani na kupitia hatua zipi majeshi yanaweza kutumika uraiani. Kwa bahati mbaya sana, nafasi ya mwanasheria mkuu Tanzania imekuwa ya kisiasa zaidi kuliko kutoa ushauri wa kisheria kwa serikali.

Kama ofisi ya mwanasheria mkuu ingekuwa inafanya kazi kwa umakini wangeishauri serikali kabla ya kupeleka majeshi uraiani. Na sielewi ni kwanini Mwanasheria mkuu ameachwa maana ukitazama kwa makini ofisi yake ilikuwa muhimu sana kwa hili zoezi. Ilikuwaje majeshi yakapelekwa uraini kinyume cha sheria? Na sasa watu wamekufa, lakini watu wapo ofisini! Wabunge walitakuwa wahoji ushauri uliotolewa na ofisi ya mwanasheria mkuu kwenye hili zoezi. Upo, ulitolewa lini, na unasemaje?

Lakini kuna jambo jengine ambalo linahitaji majibu. Hivi Tanzania imeridhia mikataba ya kimataifa kuhusu conduct za majeshi wawapo kazini? Kuna aina ya mateso waliyopewa wahanga wa hii operation ambayo yanaweza kuwa kinyume na mikataba ya kimataifa (kama Tanzania ni signatory). Mfano, kubaka, wanawake kuingiziwa chupa, kuna wanaume wameumizwa beyond reppair! Haya mateso yanakubalika?

Na je aina hii ya mateso inafanywa na majeshi ya Tanzania wakiwa kwenye mission nje ya nchi? Sote tunajua skandali za Guantanamo Bay. Majeshi ya Tanzania wanafanyaje huko nje ya nchi?
 
Binafsi kuondolewa kwa mawaziri watatu na mmoja kujiudhuru,kwangu naamini si dawa!Tatizo ni Mfumo,ambao upo serikalini,lazima tuwe na watu wa kweli na waadilifu ili kulinda maslai ya Watanzania,tuwe na kikosi kazi kitakachokuwa kinanguvu ya kunusa na kuhisi na kuitekeleza sheria bila kuwa na Aibu!kama wenyewe hatuwezi tukodi kikosi kazi kutoka nchi zilizoendelea ili kuwasimamia watendaji wa nchi hii,wao kazi yao kusimamia katiba na rasilimari
Ndio maaana nasema wananchi wasishangilie! hakuna chochote hapo. Wala CCM wasiseme ni uwazi, huo ni udhaifu mkubwa. Mfumo mzima umeoza
 
Mkuu Nguruvi3
Culture ya kufanya mambo bila hofu ya kuchukuliwa hatua (IMPUNITY) ndio imefufikisha hapa tulipo. Matukio ya mateso na mauaji mikononi mwa vyombo vya dola hayakuanza leo, miaka nenda rudi raia wamekuwa ni wahanga wa vipigo, kubambikiwa kesi, mateso na hata kuuawa. Lakini haijawahi kutokea hata mara moja wakuu wa vyombo hivi vya dola kuadhibiwa kutokana makosa yao.....why? Sababu hawa ni ni asset kubwa sana kwa watawala kuhakikisha kuwa wanabaki madarakani kwa hiyo kamwe hawawezi kuwatosa na kuwasulubu kutokana na uhusika wao kwenye unyama huu. Kuwajibisha waziri ni political stunt nzuri kupoza hasira za wananchi ili upepo mbaya hatimaye upite.
Ni political stunt nakubaliana nawe kabisa. Soon or later utawasikia hawa waliodhihirika kufanya uzembe ni mabalozi wa Tanzania, ni wakurugenzi wa bodi n.k. Ni kulindana tu
 
Mkuu Nguruvi3,

Hongera sana kwa uchambuzi mzuri. Jumuisho la uchambuzi wako na wa FJM imegusia maeneo yote muhimu kuhusiana na sakata husika tena kwa umahiri mkubwa. Kwa kwelin kuchangia hoja zenu bila umakini kunaweza tu kuharibu ladha ya chakula kitamu kilichopo mbele yetu kwani ya muhimu na ya msingi ni hayo mliyokwisha yajadili.

Nitajaribu kuchangia kwa kujadili kidogo juu ya suala zima la mapungufu ya mfumo na utawala:

Nadhani tutakubaliana kwamba Tanzania as a state is not fully formalized. Kwa katiba iliyopo, urais implies "Big Man Rule". Ni kupitia katiba hii hii Mwalimu aliwahi nena kwamba Rais akiamua kuwa dikteta, anaweza fanya hivyo kirahisi kwani nchi inaongozwa zaidi na informal institutions kuliko formal institutions, na matokeo yake, utawala wa rais mmoja hadi mwingine ni lazima upishane kwani kwa mfumo uliopo, it is more of a personal rule. This is highly problematic kwani wanaoumia ni wananchi wa kawaida kwani unawafanya wanasiasa, hasa wanaoteuliwa na Rais, kuishi kama vile wapo above the law. Such nature of politics nchini inazaa maswali on how rules can be made more eefective in holding leaders to the norms and principles of modern institutions. Na ni hapa suala na constitutional reforms linapokuwa na umuhimu wake wa kipekee.

Katika mazingira ambayo the state and its institutions are effectively formalized, kila mtu anaheshimu the rules, no matter how important the individual may be - iwe ni rais, familia yake, marafiki zake au wateule wake.
Lakini in a state ambayo haina effective and formal institutions kama Tanzania, formal rules are ignored if not defied. Viongozi are not bound by office na wanakuwa na uwezo wa kubadilisha mamlaka ya ofisi na mamlaka husika to suit their own personal and political needs or preferences.

Nchini Tanzania, Katiba na formal institutions zipo kwenye makaratasi tu, lakini they don't shape the conduct of individual actors, hasa wale waliopo madarakani. Utawala wa personal rule hau respond to the demands of the public by means of public policies and actions, na ni mfumo ambao the ruler doesn't really aim at policy goals and doesn't steer the state apparatus by information feedback and learning. Badala yake, nchi is more of a seamanship and less one of navigation - kwa maana kwamba, staying afloat rather than going somewhere (rejea hoja kwa watanzania kudumisha amani na utulivu).

Personal rule ni mfumo wa mahusiano ambao badala ya kuunganisha rulers na wananchi, unaunganisha rulers na patrons, clients, supporters, na rivals (upinzani wa ndani na nje ya chama tawala) who constitute the system. Mchezo unaoendelea katika mazingira haya among political actors huwa ni zero-sum game ambapo, kuna very little room for compromise. Isitoshe, compromise hutazamwa kama a LOSS, never a WIN. Hali hii reinforces the sense of insecurity kwa political actors ambao in turn, wanakuwa encouraged ku plot their next move ku safe guard their interests.

Kwa kifupi, chini ya mfumo uliopo, rulers magogoni and their clients will continue to be rational actors, lakini rational in a political sense, sio economic sense. Their action ni juhudi za kutafuta safe attachment na mamlaka ya uteuzi badala ya maslahi ya taifa, kwani hakuna action wanayo pursue bila ya kuwa na primary attention to the demands that must be met to keep the system of personal rule going. Chini ya mfumo wa namna hii, rulers hawapo concerned kabisa na "transaction costs" - kwani kila wanachofanya ni ruksa tu kuwa a cost kwa nchi as long as it enables them to stay in power, hivyo hofu yao ipo zaidi on "transgression costs". Such rulers wanatazama kwa uangalifu madhara ya actions zao kwa clients na followers wao, sio kwa wananchi. Matokeo yake ni kulindana au kulinda maovu kwa lengo la kulinda na kudumisha big man rule. Rulers become constrained sio na formal rules au availability of resources (fedha za walipa kodi), bali the limits of their personal authority and power.

Mfumo huu ndio sumu kubwa kwa taifa letu. Kuna umuhimu wa kuondokana na mfumo wa big man rule kwani unafanya upatikanaji wa Rais bora kuwa ni suala la bahati nasibu. Ni kwa mantiki hii, katika hotuba yake jana bungeni, Kagesheki akaeleza kwamba aliteuliwa na rais uwaziri kutokana na pleasure of the president, which means hakuwa anatumikia wananchi bali mfumo wa big man rule niliojaribu kuujadili hapo juu. Mchakato wa katiba mpya utatusaidia sana kuondokana na mfumo huu, sio mabadiliko ya sura za watu katika baraza la mawaziri kama mlivyokwisha jadili.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Nguruvi3,

Hongera sana kwa uchambuzi mzuri. Jumuisho la uchambuzi wako na wa FJM imegusia maeneo yote muhimu kuhusiana na sakata husika tena kwa umahiri mkubwa. Kwa kwelin kuchangia hoja zenu bila umakini kunaweza tu kuharibu ladha ya chakula kitamu kilichopo mbele yetu kwani ya muhimu na ya msingi ni hayo mliyokwisha yajadili.
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Mkuu na wenzio ahsanteni sana kwa maneno yenu. We have along way to achieve what we are missing in good governance.
 
Mkuu FJM
Ahsante kwa bandiko lako tena. Nilipoongelea kuhusu Kagasheki kwa hakika ninampongeza kwa kujiuzulu at least ameona sababu za kuwajibika kwa yaliyotokea katika himaya yake ya utawala.

Ninampongeza kwasababu hakusubiri kusukumwa.
Kuna hoja muhimu sana umezileta. Umesema yalipotokea matatizo kwanini hakujiuzulu.
Huo nao ni ugonjwa mpya nchini. Naafiki kuwa Kagasheki alipogundua hakushirikishwa na wala haungwi mkono na viongozi wa juu yake alipaswa kuachia ngazi mara moja.

Tumemsikia Mathayo akilalama kuhusu mabawa ya mifugo.Naungana nawe kumuuliza endapo kila jambo si chini ya wizara yake , je hakuona umuhimu wa kuli rise lijadiliwe?

Haiwezekani awe mtawala wa mifugo na asijue mifugo inatibiwaje na inapataje mahitaji.
Anapolalama dakika za mwisho ni ugonjwa ule ule wa kujitetea kwa kitu alichokiona bila kuchukua hatua.

Nahodha, alichotendewa hakikuwa katika standard. Ametolewa kafara tu kwasababu Hussein Mwinyi alipaswa kuwa si waziri siku nyingi, lakini alichokisema Mchunguzi ndicho kinafanya kazi, i.e kulindana tu.

Mwanasheria mkuu wa serikali,si mwanasheria mkuu ni mwasiasa anayejua sheria.
Katika tatizo linaloikabili nchi hii ni watu kama mwanasheria mkuu aanyedhani kazi yake ni kulinda masilahi ya mtandao wa uongozi na pengine mitandao ya ujangili, ujahilia na ufisadi. Another sad story.

Mkuu Mchambuzi
Katika bandiko lako umesema kuhusu 'big man rule'.Kazi za big man endapo zingegusa masilahi ya taifa japo kidogo hali isngekuwa hii.

The big man yupo kwa ajili ya kusimamia masilahi ya subordinate wake ambao nao wapo kuhakikisha big man hapati misuko suko ''quid pro quo''

Kama ulivyosema hakuna system, yote ime fail si kwasababu ya taifa bali kundi la watu wachache tu.

Mkuu wa TISS alipaswa kuelewa ujangili na mtandao husika. Wakati wa Nyerere na Sokoine walibaini mbinu za wahalifu kutoka nje, iweje tembo wanauawa hadi kufikia nusu kwa muda mfupi bila uongozi kufahamu.

Ilikuwaje kukawa na uhalifu bila TISS kugundua na kuzuia kabla ya rais hajasema operesheni inaendelea vizuri kumbe watu wanateswa. TISS wamemsaidiaje Rais kubaini hali ya taifa.
Kamati ya bunge iliwezaje na TISS wasijue hilo.

Katika kile mchambuzi anachosema ni kulindana kamati ya bunge imeendeleza utamaduni wa kulindana.
Kamati imeeleza kuwa kuna maagizo yalitolewa viongozi wa kisiasa wasiguswe.

Ni wazi maagizo hayo alipewa Mheshimiwa Kagasheki.
Katika ngazi ya uwaziri kuna watu watatu walio juu ambao ni waziri mkuu, makamu wa rais na Rais.

Kuna kila sababu ya watu kaumini maagizo yametoka kwa viongozi hao unless kamati itoe ufafanuzi zaidi.
Kama itabaki ilivyo basi ni mmoja kati ya hao watatu.

Wengine wanaoweza kuwa na ushawishi kuhusu kauli za viongozi kutoguswa ni viongozi wa CCM.
Miongoni mwao wapo wanaotajwa kuhusika na biashara ya pembe na kwa ushahidi wa kimazingira.

Hadi hapo kamati ilipaswa kueleza ni akina nani waliotoa kauli hizo.
Tunachokiona ni kamati kuendeleza utamaduni wa kulindana.

Kuhusu kubadili hali iliyopo na kutengeneza mfumo wa formal state, nako kuna tatizo.
Mabadiliko ya katiba yalikuwa ni sehemu muhimu,wameteka mchakato mzima ili kuendelea kulindana.

Fikiria Rais amepewa wabunge 160 atakaochagua kwa matakwa yake.
Wabunge wa kuchaguliwa na rais ni nusu ya wabunge wa kuchaguliwa.

maana yake ni kuchagua watu watakaokwenda kusimamia mfumo unaomaliza maisha ya watu na tembo uendelee. Ni jambo la aibu na kusikitisha sana na hapo matumaini ya kuwa na formal state yanafifia sana.

Kuwaengua mawaziri ni dalili ya udhaifu mkubwa na ombwe la uongozi la taifa hili.
Rais haengui anafukuza lakini kwavile JK hupenda kujificha aonekane mwema kwa kila mtu tuansikia maneno kama ya kuengua.Tatizo si mawaziri wanne, tatizo ni uongozi wa nchi umefeli kuongoza taifa.

Kuongoza ni kutangulia si kukimbia na kuachia watu wabebe mizigo.
Hatuna uongozi wa nchi, ombwe ni kubwa na udhaifu unatisha.

Msishangilie kuondoka kwa mawaziri wanne, tatizo sio mawaziri narudia ni uongozi na system iliyo feli na tutabaki nyuma wenzetu wakichanja mbuga. Tatizo ni uongozi wa taifa usiojali taifa, wenye udhaifu na ombwe kubwa sana.
 
Kuna taarifa (@Mzizimkavu)inayomhusu Nape Nnauye. Taarifa hiyo haina shaka kwasababu vyanzo vyote vimetajwa.Ningependa kumwalika Nape Nnauye aje hapa tujadiliane kuhusu kauli zake hasa kwa yaliyotokea.

*Asema ni fundisho kwa watakaolala*Ataka hatua zaidi zichukuliwe*ziara za Kinana zimesaidia sana kutatua kero*Bado moto wa ziara hizo haujapamba
NA BASHIR NKOROMO
1. KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye amesema amepokea kwa faraja kubwa, hatua ya mawaziri wanne kuenguliwa nyadhifa zao kwa ridhaa ya Rais Jakaya Kikwete.

2."Najisikia vizuri, maana kwa kitendo cha mawaziri hao wanne kuchuliwa hatua, ninaamini kitasaidia wale wengine waliolala nao waamke. Bila shaka sasa hakuna atakayelala na akilala anajua itakula kwake.", alisema Nape akijibu swali la mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Emmanuel Buhohela, kwenye kipindi cha 'mahijiano' cha televisheni hiyo, mjini Dar es Salaam, leo asubuhi.

Mtangazaji huyo alitaka kujua, Nape kama kiongozi wa ngazi ya juu CCM, amejisikia au kupokeaje hatua ya Bunge

3.kumuomba Rais kuwawajibisha mawaziri hao wanne na kisha Rais kuridhia ombi hilo kwa kutengua uteuzi wake wa nafasi za mawaziri hao jana.

4. Kutenguliwa kwa uteuzi wa mawaziri hao kulitangazwa rasmi Bungeni jana jioni, na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, hatua inayoaminika kuwa imetokana na shinikizo la bunge, baada ya Kamati yake ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kubaini 'uozo' katika
operesheni
iliyofanyika hivi karibuni ya tokomeza ujangili.

Chini ya Mwenyekiti wake, James Lembeli, Kamati hiyo ilieleza kwamba pamoja na mambo kadhaa iliyoyaeleza kuwa ya hovyo yaliyojitokeza kwenye operesheni hiyo, vitendo vingi ikiwemo ubakaji na udhalilishaji vilifanyika ambapo ni kinyume na utu na haki za binadamu.

5.Kufuatia kadhia hiyo, Kamati hiyo kupitia kwa Lembeli, iliwataka mawaziri wanaohusika kutazama kama wanafaa kuendelea na nyadhifa zao au wajiuzulu, na pia Kamati hiyo ikaenda mbali zaidi kwa kumuomba Rais Jakaya Kikwete kuchukua hatua ya kuwawajibisha.

6. Nape alisema, pamoja na mawaziri hao kuwajibika, lakini ipo haja ya kwenda mbali zaidi kwa kutazama mifumo na sheria zilizopo sasa kwa kuwa inaonekana navyo ni miongoni mwa vyanzo vya vikwazo katika utekelezaji wa utawala bora.

7. "Kwa mfano leo hii, mawaziri wameng'oka, sawa ni jambo jema, sitetei, lakini inawezekana kabisa kuna mifumo na sheria ambazo zilimkwaza Waziri huyu kutimiza wajibu wake. Mfano, alihitaji kumfukuza mtu kazi kwa kuzembea jambo fulani, lakini malmaka ya kufukuza kazi mtumishi yapo kwa Katibu Mkuu wa Wizara, hapa atafanyaje!", alisema Nape na kuongeza;

8. "La msingi hapa ni lazima sasa hatua hizi ziende mpaka chini huku kwa watendaji, ili isiwe mawaziri wanawajibishwa tu kwa sababu ya dhamana zao za kusimamia kisiasa, huku watendaji wanazidi kuvuta shuka bila hofu wakati baadhi yao ni sehemu ya matatizo".

9. Akijibu swali kuhusu ziara za Katibu Mkuu mikoani, Nape alisema, ziara hizo ndiyo kwanza zimeanza, na mado moto wake mkubwa zaidi unakuja hasa itakapokaribia uchaguzi mkuu wa 2015.

10.Alisema, ziara hizo, zimeonyesha matunda makubwa sana, klwa kuwa zimesaidia kupunguza kero nhyingi katika maeneo zilikofanyika.

11. mfano wa ziara hiyo ilivyoweza kuondoa msongamano wa malori wilayani Tunduma mkoani Mbeya, akisema kwamba wakati Kinana na msafara wake wanaingia tunduma walikuta msongamano ni mkubwa sana kutokana na wafanyakazi wanaohudumia malori hayo kufanya kazi kwa mda mfupi.
"Baada ya kuiagiza serikali isimamie wafanyakazi wa eneo hilo wafanya kazi kwa saa 24, kwa zamu, siku ya pili yake ya agizo hilo, msongamano ulionekana kupungua sana na kuleta nafuu kwa madereva na wafanya biashara kwa jumla pale Tunduma", alisema Nape.

Nape alisema, pia kutokana na ziara hizo, mgogoro uliokuwa mkubwa baina ya wananchi na wenye mgodi wa machimbo Nyamongo, umepungua kwa asilimia 90 sasa, na hali imekuwa ya kuridgisha sana.

Akizungumzia wabunge wanaodaiwa kulipwa posho bila kuzifanyia kazi, Nape alisema, kurudisha fedha pekee hakutatosha, kwa upande wa CCM ambayo ndiyo yeneye wabunge wengi itabidi ichukue hatua zaidi dhizi ya waliohusika na kadhia hiyo bila kuoneka mtu.

Kuhusu ajira kwa vijana, Nape alaisema ili kutimiza hilo, ni lazima viwanda vifufuliwe kwa dhati kabisha, ikiwa ni kuchukua hatua za kuwanyang'anya wawekezaji waliochukua viwanda mbalimbali kwa lengo la kuviendeleza lakini baadhi yao majengo ya viwanda hivyo wakayafanyia shughuli zingine tofauti ikiwemo kuyageuza maghala.

Nape aliitaka pia serikali kupunguza au kuondoa kabisa urasimu katika kupokea wawekezaji katika sekta mbalimbali za uchumi hapa nchini akisema, kwamba, kwa sasa vikwazo na urasimu bado ni vingi sana kiasi kwamba wawekezaji waanakwazika na hivyo kupunguza kasi ya uwekezaji ambao wakiongezeka haraka ajira kwa vijana nazo zitakua haraka.

Alisema, hatua ya sasa inayofanywa na CCM kusimamia serikali ni ya kawaida kabisa kwa kuwa kazi hiyo haipaswi kufanya na wapinzani kwa kuwa sera inayotekelezwa siyo yao, na wahaijui.

Nape aliahidi kwamba katika uchaguzi zijazo CCM itakomba viti vyote vya ubunge na udiwani vililivyopo sasa chini ya wapinzani, akisema, kwamba, baada ya wapinzani kujaribiwa wameshindwa kuonyesha matunda yoyote ya kusaidia wananchi na hivyo kutokuwa mbadala wa CCM.chanzo.
Nimeyasoma maoni ya katibu mwenezi wa CCM na kuomba aje tujadiliane kama Member wa JF.Tangu mwanzo mwa bandiko hili nimesema CCM hawana sababu yoyote ya kushangilia zaidi ya kuhuzunika.

Hakuna uzembe unaoweza kusifiwa kwa maisha ya watu kupotea. CCM,chama chenye serikali sidhani kama yupo mwanachi atakayemwelewa Nape kwa dhihaka hii kubwa.

Hoja za Nape zinachanganya, tuzipitie ili kuona viongozi wa taifa hili wanafikiria nini na wana maono gani.

Nape anajisikia faraja mawaziri kujiuzulu,anataka kuuaminisha umma hilo ni tatizo lililotokea kama uyoga. Kuna mambo lukuki yanayosikitisha ambayo kwa Nape ni ya kawaida ila la mawaziri limetoa faraja.

Kuna viporo vya suala za rushwa, pesa Uswiss, meli za tembo Hong Kong na Zbar, wizi katika halmashauri, kuvuja mitihani ya kidato cha nne, kashfa ya kuongeza div 5, ufujaji na ujumu wa nchi ambazo CCM imezifunika

Wanyamapori wamebebwa na dege la Qatar KIA, majina ya wabunge wa CCM wanaohusika na biashara ya pembe yapo wazi na TANAPA (Ref Mikael P Aweda JF Oct 4 2013), si CCM wala serikali yake iliyowahi kushughulikia.Nape, kipi cha ajabu kilichokupa faraja kwa hili la jana?

Nape amefarijika kwa rais kuwaengua mwaziri, si kuwafukuza kazi kwa shinikizo la Bunge.
Amezidi kufarijika na utaratibu wa rais kumtuma waziri mkuu badala ya yeye kusimama na kuliomba taifa radhi kwa misiba na mateso waliopata watu.

Ni mwenyekiti wa Nape na CCM aliyesema operesheni inaedelea kwa mafanikio, hee! vipi leo ajifiche na kumtuma PM kuwajibisha mawaziri?

Lugha ya kuengua ni lugha dhaifu sana. Hakuna kuengua katika kazi, ni ima kufukuzwa au kufukuza.
Neno kuengua linatumiwa na watu waoga waisokuwa tayari kukabiliana na changamoto za taifa, na ni udhaifu mkubwa sana wa mwenyekiti wa CCM na Nape amefarijika na udhaifu huo.

Nape ameunga nasi kusema tatizo ni la mfumo zaidi ya watu wanne, tofauti yake nasisi ni kuwa yeye amefarajika kutumia aspirin kuponya malaria na si kutafuta chanzo na tiba ya malaria.
Anadhani mfumo mbaya unasababishwa na mawaziri 4

Nape kasema inawezekana waziri akawajibika kwa nafasi yake kisiasa kwasababu katibu mkuu ameshindwa kuwafukuza walio chini yake. Asichokijua ni kuwa waziri ni mshauri mkuu wa rais katika wizara na kama haridhiki na utendaji wa katibu mkuu anayo nafasi ya kumshauri rais.

Lakini kwanini alaumiwe waziri kwa utendaji mbovu wa katibu mkuu ambaye ni mteule wa Rais?
Hivi hapa Nape si anatueleza uzembe na udhaifu wa kiongozi wa serikali na chama chake?

Wakati Nape akilaumu mfumo usio na umakini wakati huo huo anasifia mfumo huo kwa njia tofauti.
Nape anasema ziara za katibu mkuu wa CCM zimepunguza foleni kule tunduma n.k. kwa siku moja aliyokuwepo.

Katibu mkuu wa CCM si serikali na kama alifanya hivyo ni ushahidi mzuri kuwa Nape na Kinana hawajui kuwa mfumo una matatizo ingawa wanaongelea mfumo kuwa na matatizo.

Si kazi ya katibu mkuu wa CCM kusimamia utendaji wa serikali. Huu ni ushahidi wa viongozi tulio nao wasiojua mipaka ya kazi wala majukumu yanayowakabili. Nape anafarijika na mfumo huo unapowagusa watu 4.

Hata kwa mantiki, waziri hachaguliwi na chama anachaguliwa na rais.
Taasisi ya uraisi ni institution na si corporate.

Kuwaita na kuwahoji mawaziri katika vikao vya CCM ni kuifanya taasisi ya urais kama corporate inayoendeshwa na bodi.

Huu ni udhaifu mkubwa sana wa uongozi wa nchi na ushahidi kuwa ombwe la uongozi halina kificho na ni janga kwa sasa.

Kuhusu tatizo la ajira Nape anashauri viwanda vifufuliwe ili kutoa ajira. Sijui maana ya kufufua ni nini,kwasababu kiwanda kilichoondolewa mashine na kubaki ghala la chumvi huwezi kukifufua.

Aliyeuza viwanda hivyo ni serikali inayosimamiwa na CCM. Kwanini leo eti ionekane CCM inaweza kusimamia foleni za mgari lakini haiwezi kusimamia viwanda vilivyotolewa sadaka kwa matajiri wa nchi hii.

Nape vifo vya viwanda vimefanywa na Mkapa. Alichokiendeleza Kikwete ni kutoa tenda ya kung'oa reli kwa wahindi.Hayo yote yamefanywa na CCM leo unataka kutufanya wendawazimu kwa hadithi za kitoto namna hii.

Nape njoo hapa utueleze umefurahishwa na kitu gani hasa.
Uwaambie wananchi waliofiwa na ndugu zao kipi kizuri wanakipata kwa Kagasheki kujiuzulu.

Na mwisho, Nape anasema hakuna kulala atakayelala imekula kwake.
Mbona Nape kalala siku 30, alipoamka akalala 60, na kisha 90 na sasa ni miaka tangu atuambie anashughulikia mafisadi?

Kabla hajaamsha walio lala labda tumkumbushe kuwa yeye bado amelala na tunasubiri aamke atuambie mafisadi wameishia wapi.
 
Kuna taarifa (MziziMkavu)inayomhusu Nape Nnauye. Taarifa hiyo haina shaka kwasababu vyanzo vyote vimetajwa.Ningependa kumwalika Nape Nnauye aje hapa tujadiliane kuhusu kauli zake hasa kwa yaliyotokea.

Nguruvi3,
Kwa kuongezea, kama unakumbuka, vyombo vya habari vilitamka kwamba miongoni mwa mawaziri mizigo waliotajwa na nape ni Waziri wa Elimu - Shukuru Kawambwa. Umma haukushangazwa na jina hilo kwani kwa hali ilivyo, huyo ni waziri mzigo namba moja; Lakini cha ajabu ni kwamba Nape akaenda kwenye vyombo vya habari na kukanusha kwamba hakumtaja Kawambwa, suala ambalo liliwachanganya sana wananchi. Tunasubiri mzunguko wa pili wa pongezi za Nape kusikia ataliongeleaje suala la Kawambwa iwapo na yeye atawajibishwa.

Kuhusu suala la viwanda, nchi hii ni ya ajabu sana. Waziri Kigoda ndiye aliyesimamia uuzwaji wa viwanda miaka kama kumi iliyopita, then ten years later, anapewa dhamana ya kusimamia industrialization process in the country, hivi tumepatwa na kitu gani?

Na nikirudi kwenye suala la mawaziri mizigo, wengi wanashabikia kwa sababu tu ya wivu kwani uwaziri ni ulaji, sio utumishi kwa wananchi. In the process, wengi ndani ya ccm wanashangilia kwa kudhania kwamba pengine wao au watu wao watapata ulaji. Na media zetu zinaendeleza upuuzi huo kwani wakiteuliwa watu, vichwa vya habari magazetini vinakuja na habari "fulani kaula"; this is a disgrace;

Na nadhani umeshaona humu makada fulani fulani wa ccm wameshaanza kujipigia debe za uwaziri kwa kutumia fake IDs humu JF; yote hii ni ushahidi kwamba furaha za wahusika kwa yanayoendelea hazina uhusiano na maslahi ya wananchi, wala ccm, bali matumbo yao;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Kuna haja kubwa sana ya kuiondoa Natural Resources from Tourism......kuna too much confusions/conflicts of who does what........hii Natural Resources inabidi iende Wizara ya Mazingira...Tourism ibaki peke yake.....iongeze nguvu kutafuta na kuvutia utalii nchini........potfolio za ulinzi ziachiwe Mambo ya Ndani, Ulinzi na TISS......
 
Yes Ogah. inaweza kufanyika kama unavyoshauri na naona mantiki ya point yako.
Hiyo itakuwa ni just a partial but not wholesome solution.

Tatizo lipo katika uongozi wa nchi. Kuna kuingiliana sana kikazi kwa masilahi binafsi.Kesi ya wanyama kutoroshwa KIA ilikuwa kashfa kubwa ambayo nashangaa si waziri mkuu, makamu wa rais a Rais aliyeiongelea.

Kitendo cha ndege ya kijeshi kutua nchini bila 'taarifa' kilitosha kabisa kuwa concern kwa wizara ya ulinzi, TISS na Uongozi wa KIA. Tulitarajia kusikia watu wametimuliwa na pengine kufunguliwa mashtaka. Guess what! hakuna, narudia hakuna kiongozi wa nchi katika top brass aliyeongelea tatizo hilo. Hivi hapo kuna message gani inayopatikana.

Kuondoka kwa wanyama ilitosha kabisa TANAPA, NCCA, TISS mkoa kuwekwa kitimoto, watu kupoteza kazi na pengine kufungwa kwa uzembe. Wamekamatwa watu wachache wakatolewa kafara.

Mgogoro wa uongozi wa TANAPA unajulikana, hakuna kiongozi wa juu anayeteua hao wajumbe au viongozi anayezungumzia au kuingilia kwasababu mtandao uliopo ni mkubwa sana.
Ndivyo ambavyo TAZARA imekuwa katika mtatizo utadhani ni shirika binafasi, serikali haina habari na mradi huu mkubwa wenye masilahi ya kiuchumi.

Sakata la Tokomeza, limejadiliwa ngazi za juu, rais akatangaza na akarudia kusema kuna mafanikio.
Mpango ulikiuwa chini ya ofisi ya waziri mkuu na definite Rais alikuwa briefed kila mara.

Kama alipewa habari 'fake' bado alikuwa na TISS na Polisi waliopaswa kumpa real info from the ground.
Leo anawaengua mawaziri tena kwa shinikizo la bunge na kuacha waliopaswa kumpa taarifa wakiwemo viongozi wa TISS na Jeshi kwa pamoja

Kuwaengua tu ni lugha ya udhaifu na unyonge sana. Rais anaengua vipi watu waliosababisha mauaji kwa raia?
Halafu rais alikuwa hana habari zinazoendelea hadi tume ya bunge ilipokuja na mapendekezo.
In other words serikali haijui nini kinaendelea ingawa kulikuwa na Polisi, Jeshi, na kila idara husika!!!

Kwa mtazamo wangu tatizo hili si la mawaziri wanne. Tume imesema mtandao ni mkubwa sana na ikasema yapo maagizo kwamba asiguswe mwanasiasa. Kwamba wanasiasa wanaruhusiwa kusafirisha pembe za ndovu kama walivyoruhusiwa kubeba katika malori na meli zao.

Anayeweza kutoa amri kwa Kagasheki ni lazima awe juu yake.
Leo tunaambiwa Nchimbi, Nahodha, Kagasheki na Mathayo wamezembea! Not true!

Tatizo ni uongozi wa nchi, hili tukubaliane,. Udhaifu wa uongozi wa nchi na ombwe la uongozi ndilo tatizo kubwa.
Haiwezekani serikali imfukuze Nahodha leo wakati Hussein Mwinyi alishuhudia dege la kijeshi likitua tu bila taarifa na hakuna hatua zozote.

Mawaziri wanne wamefukuzwa ili kuendelea kuficha udhaifu wa mfumo, uongozi wa nchi na ombwe lililopo.
Tatizo si mawaziri suala hili ni la Uongozi wa nchi
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3,
Kwa kuongezea, kama unakumbuka, vyombo vya habari vilitamka kwamba miongoni mwa mawaziri mizigo waliotajwa na nape ni Waziri wa Elimu - Shukuru Kawambwa. Umma haukushangazwa na jina hilo kwani kwa hali ilivyo, huyo ni waziri mzigo namba moja; Lakini cha ajabu ni kwamba Nape akaenda kwenye vyombo vya habari na kukanusha kwamba hakumtaja Kawambwa, suala ambalo liliwachanganya sana wananchi. Tunasubiri mzunguko wa pili wa pongezi za Nape kusikia ataliongeleaje suala la Kawambwa iwapo na yeye atawajibishwa.

Kuhusu suala la viwanda, nchi hii ni ya ajabu sana. Waziri Kigoda ndiye aliyesimamia uuzwaji wa viwanda miaka kama kumi iliyopita, then ten years later, anapewa dhamana ya kusimamia industrialization process in the country, hivi tumepatwa na kitu gani?

Na nikirudi kwenye suala la mawaziri mizigo, wengi wanashabikia kwa sababu tu ya wivu kwani uwaziri ni ulaji, sio utumishi kwa wananchi. In the process, wengi ndani ya ccm wanashangilia kwa kudhania kwamba pengine wao au watu wao watapata ulaji. Na media zetu zinaendeleza upuuzi huo kwani wakiteuliwa watu, vichwa vya habari magazetini vinakuja na habari "fulani kaula"; this is a disgrace;

Na nadhani umeshaona humu makada fulani fulani wa ccm wameshaanza kujipigia debe za uwaziri kwa kutumia fake IDs humu JF; yote hii ni ushahidi kwamba furaha za wahusika kwa yanayoendelea hazina uhusiano na maslahi ya wananchi, wala ccm, bali matumbo yao;
Mkuu Mchambuzi , wakati watu wanamwagiwa tindikali wakiwemo wageni tena katika chuki za kibiashara na za kidini, na wakati wanahabari wakifaytuliwa mabomu na wengine kupelekwa mabwepande kwa ajili ya kung'olewa kucha Nape hakusema lolote kuhusu Nchimbi.
Leo anafarijika kwa lipi kwa Nchimbi kufukuzwa?Kipi kigeni katika yale yanayomzonga Nchimbi ?

Kuhusu kutaifisha viwanda, kazi hiyo ilifanyika JK akiwa waziri. Ikaendelea akiwa Rais na akina Kigoda.
Leo Nape analiona kama tatizo jipya. Hivi Nape hajui kuwa Mang'ula ikibinafsishwa na kuwa ghala la chumvi yeye alikuwa UVCCM na hakusema kitu. Hatuwezi kupiga hatua kama tuna viongozi wanaofikiria matukio na si maono.
Viwanda kufa ni CCM policy Nape hana ubavu wa kutushawishi tofauti, he is part of the failures za nchi hii.

Nimeshangaa hata wasomi wanapongeza mawaziri kujiuzulu. Aliyejiuzulu ni Kagasheki wengeni wame enguliwa na rais.
Lugha ya kuenguliwa narudia ni dhaifu sana kutoka kwa mkuu wa nchi. Mkuu wa nchi ni authority hivyo alipaswa kuwafukuza hii lugha ya kuengua ni kutaka kuwa mwema, ni kuongoza kwa kujificha ni kielelezo cha ombwe(vacuum)

Hao mawaziri wameonewa kwasababu wamefanya mabaya zaidi huko nyuma na Rais aliwakubalia kuendelea na kazi.
Hili la Tokomeza Rais alisimama na kusema opersheni imefanikiwa na kuna makosa kidogo.

Rais amesema makosa kidogo kwa roho za watu halafu leo anatuambia ametengua uwaziri wa watu wanne.
Makosa kidogo kwa unyama wa namna ile!!! Leo badala ya kuomba taifa radhi kwa makosa ya watendaji wake, anajificha nyuma na kumtuma Pinda! Huu ndio udhaifu unaoliumiza taifa hili. Tusemeni ukweli jamani!

Rais anajua habari alizopewa na kusema makosa kidogo ni za uongo, tulitegemea lundo la watu kufukuzwa kazi na kufikishwa mbele ya sheria. Kwa vile anajua huu ni upepo utapita mbele ya Watanzania, anawatoa kafara mawaziri wanne wasiokuwa na sababu zozote za kufanya hivyo. Wapi makatibu wakuu, wapi TISS, wapi Polisi, Wapi PCCCB n.k

Nape anafarijika taifa likiwa katika mgao wa umeme. Hakuna waziri aliyewajibika na serikali ya CCM inajua kuwa mgao huo ni matokeo ya hujuma kama ilivyowahi kuripotiwa.

Hakuna anayeshughulisha kichwa kujiuliza kuliko ni, Kinana na Nape wanasimamia foleni Tunduma kazi ya mkurugenzi wa halmashauri. Wanashangilia Nahodha kujiuzulu hawaoni impact ya umeme kwa uchumi wa taifa.
Muhimbili watu wanalala kwa kubebana wakisubiri misiba Nape haaoni anachokiona ni kujiuzulu Kagasheki.

Inasemwa mfumo mzima haupo sahihi ni kweli the whole system is rotten and corrupt, tatizo la Watanzania hawaangalii chanzo ni nini wanaanglia 'bendeji' zilizofunikwa kidonda kinachonuka.
Kama Wakurugenzi na makatibu wakuu ni tatizo hizo ni dalili, tatizo ni mamlaka zilizowateua.

CCM wanashangilia, hawajui kuwa jambo hili limeidhalilisha sana serikali yao.
Kuna kashfa na mambo lukuki yamefanyika na hayana majibu hili linawafurahisha kitu gani.

Kwamba kuna mawaziri wanne wameondoka! Shame on the government.
Tatizo ni la uongozi wa nchi si la watu wanne.

Tusikwepe ukweli huo kwasababu sasa imekuwa too much.
CCM wamweleza mkuu wa serikali yao atulie nyumbani na kushughulikia matatizo.

Si kazi ya Nape na Kinana kusimamia foleni za magari au migodi.
Ni kazi ya serikali yao ambayo imeshindwa na sasa nchi inajiendea kama boti iliyozimika injini, no leadership at all.
Hakuna leadership matokeo ndio haya ya Tokomeza.

Mawaziri wanne si tatizo Watanzania, ni dalili za tatizo la udhaifu wa uongozi, na ombwe la uongozi.
It is time wananchi waueleze uongozi kuwa sasa muda wa hadithi na mazingaombwe ya kutoa watu kafara umekwisha.

Hii ni aibu hakuna jipya watu wasishangilie, roho za watu zimepotea na wala hazitarudi kwa kutengua mawaziri.
Anyehusika asimame na kueleza taifa nini kimetokea, vinginevyo wataendelea kucheza na roho zetu nasi tukilia kila siku kuelekea makaburini, wao wakitung'omg'a kwa kuengeua uwaziri. Tusiposimama kidete watatufanya nodnodcha ifike mahali tuwe binadamu na tuwaambie ukweli. Tatizo ni uongozi wa taifa si mawazir narudia tena
 
Last edited by a moderator:
Katika kuonyesha unafiki wa viongozi wa CCM na serikali yao, bajeti ya mwaka huu ilikuwa na kodi ya Simcard.
Bajeti hiyo ilipitishwa na CCM na serikali yake na kuingia bungeni na kupitishwa na wabunge wa CCM.

Kilio cha wananchi kupinga kilikuwa kikubwa na mmoja wa watu waliozungumzia uhuni wa kodi hiyo ni Nape Nnauye ali. Mswada wa kurudishwa hoja bungeni ulipelekwa kwa hati ya dharura ya Rais ku score political point pamoja na timu yake.

Katika kuhakikisha wanawafanya Watanzania majuha na wajinga kwasababu wanajua ni wajinga, kodi hiyo imewekwa kwa njia nyingine ikimlenga mtumiaji.
Hapa sijamsikia Nape kuhuzunika eti anahuzunika na foleni ya malori. Ujanja ujanja tu wa maneno
Sikumsikia Nape akizungumzia waziri wa fedha kujiuzulu, leo anazungumzia Nahodha kufukuzwa kama faraja

Sijui ni faraja gani anayoipata wakati akijua kuwa wananchi watazidi kuumizwa na kodi ya simu iliyowekwa mahali pengine kijanja tu. Kwamba kufukuzwa kwa waziri ni faraja kuliko kodi ya simu inayowaumiza masikini.

Ndio mana nasema hawa viongozi wanajua Watanzania ni watu wa ajabu ambao hawana uelewa na wala hawana uwezo wa kuwafanya lolote. Wanaamua kucheza mazingaombwe kwasababu wanajua wanacheza na audience isiyojua na itashangilia kama watu wanavyoshangilia mawaziri kujiuzulu na kufukuzwa, ukweli ni kuwa tatizo ni la uongozi wa nchi.

Watanzania wabadilike na kuangalia mambo kwa upana , wasidanganywe kwa pipi.
Leo ni miaka 50 bado hatujaona tatizo letu ni nini.

Kama Rais alikuwa waziri wa nishati halafu amekuwa rais na sasa ni mwaka wa 8 mgao wa umeme upo na alikuwa sehemu yake ukitengenezwa bado hana solution na nchi ipo katika giza, watu wanshangilia nini mawaziri kufukuzwa.

Nchi haiweze kuendelea kama tutaruhusu usanii tu kila siku, porojo na kudanganyana tu.
Tatizo letu ni udhaifu mkubwa wa uongozi, na ombwe kwasababu hakuna leadership ya nchi! hakuna!
Inasikitisha sana.

Hivi kweli tuna uchungu kuuawa kwa Tembo na kuwafukuza mawaziri wakati ndege ya jeshi ilitua KIA na kutaka kuondoka na wanyama hai hatukuwahi kusikia kiongozi yoyote akitoa kauli.

Leo tunaaminisha uongozi amechukizwa na operesheni wakati hakuwahi kuzungumzia wanyama kuchukuliwa hai. Please!
Watanzania wanafurahi na kusema ni hatua nzuri mawaziri kufukuzwa, uzuri upo wapi! mazingaombwe yana uzuri gani.
 
Last edited by a moderator:
UTETEZI DHAIFU

Kumekuwa na utetezi dhaifu kuwa mawaziri waliowajibishwa wamefanya wameonewa kwasababu mfumo hauwaruhusu kuwawajibisha watendaji kama makatibu wakuu, wakurugenzi n.k. na hivyo wao kubeba mzigo wa kuwajibika kisiasa.Huu ni utetezi dhaifu sana tunaoweza kuuita mfamaji haachi kutapa tapa.

Mawaziri hao na wengine waliopo wametumikia mfumo huo wanaoulaani bila kuwa na concern yoyote kuhusu ubaya wake.

Mfumo huo umetumika miaka mingi tu na hakuna aliyeonyesha kushtushwa nao.
Hivyo wao walikubali kuishi na 'tembo' ndani ya nyumba vipi leo waone ni tatizo.

Pili, endapo mfumo ulikuwa ni tatizo yalipotokea matatizo walipaswa kujiuzulu kwanza na kutoa madai ya mfumo mbaya.

Kinyume chake wamesubiri hadi shinikizo la kisiasa ukiacha kwa mh Kagasheki.
Kwa sasa wapo wanaodaiwa ni mizigo katika wizara, nao pia wanasubiri wawajibishwe ili wadai ubaya wa mfumo wanaoutumikia sasa. Siasa za namna hii ni za ulaghai na hazifai kabisa.

Tatu, ni jambo la kuisikitisha kuona mamlaka zilizowateua hazikuona tatizo hadi shinikizo la kisiasa. Haiwezekani udhaifu huu usionekana kwa mamlaka za uteuzi bali kwa mawaziri.
Kuna tatizo kubwa la kiutawala ambalo ndicho chanzo cha matatizo yote tunayoyaona.

Nne, katika taarifa yake tume haikubainisha kama yalikuwepo matatizo ya kimfumo

Muhimu ni kutambua kuwa wakati wanasiasa wanavurugana majangili yanatumia udhaifu huo kujipanga tena na kuendeleza mbinu chafu. Sijui kama tunalitendea taifa haki kwa malumbano ya kisiasa tembo wakiangamia.

Kushindwa kushghulikia tatizo la wanyama KIA ilikuwa ni ushindi wa wazi kwa majangili.
Kuna kila dalili kuwa uhalifu wa KIA ulikuwa na mkono mrefu na unaogopwa na vyombo husika.

Haiwezekani leo tuone tembo wanauawa nasi tubaki kuhesabu waliouawa wakati kuna wanyama walikuwa wanasafirishwa na ndege ya kijeshi bila kuchukua hatua.
Huu nao ni unafiki wa kisiasa, kwamba tembo wanaouawa ni tatizo zaidi ya lile la KIA.

Twende mbele turudi nyuma tatizo letu ni la kiungozi kwa ujumla na wala si tatizo la wanasiasa wanne.
Tuna ushahidi wa wanasiasa waliopo madarakani ambao katika hali ya kawaida walipaswa kuwajibishwa.

Mfano, milipuko ya mabomu iliyochukua roho za watu, waziri husika yupo madarakani kana kwamba hakukuhitajika uwajibikaji. Hizi ni double standards zinazoonyesha kuwa si mfumo ambao ni tatizo bali uongozi wa nchi kwa ujumla.

Hadi hapo Watanzania tutakapojifunza utamaduni wa kuwawajibisha viongozi wenye dhamana, hizi excuse za mfumo zitaendelea na madhara zaidi yatataukumba.
 
Tunaishi dunia ya ajabu sana tena kuna watu wameanzisha Minakasha eti Kagasheki ameonewa daah!ameonewa na nani?hivi na wale manaibu wa hizo wizara wanasubiri nin kuachia ngazi
 
Sehemu ya I

Waziri wa mali asili na utalii mh Kagesheki amejiuzulu kufuatia tuhuma za Operesheni ya Tokomeza.
Operseheni ililenga kukomesha vitendo vya ujangili vya kuua wanyama kwa njia haramu

Waziri amejiuzulu kwa kuwajibikaji kutokana na matatizo yaliyotokea wizara anayoongoza.
Mh Kagasheki amekuwa mstari wa mbele kupambana na mjangili na kumuomba Rais msaada ili kulinda rasilimali ya taifa ambayo imepungua kwa kiasi cha kutisha.

Mh Kagasheki amekumbuna na kesi zinazohusu meno ya tembo mara nyingi.
Hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kufuatilia kubainika kwa ujangili huo.
Meli zimekamatwa Hong Kong na Zanzibar,wamiliki ni Watanzania wengine wakiwa na nyadhifa za juu.

Tatizo la hujuma za rasilimali za taifa halikuanza leo.
Tunakumbuka kukamatwa wanyama wakisafirishwa hai katika uwanja wa ndege wa KIA.
Ndege ya kuwachukua ilikuwa ya kijeshi na kwa tartibu za kimataifa na hata za kitaifa ni lazima kungekuwepo na taarifa ya ndege kutua na hasa ya kijeshi.

Licha ya kelele nyingi kuhusu hujuma zinazoendelea hakuna kiongozi aliyesimama kuliongelea achilia mbali kuchukua dhama kama aliyochukua Kagasheki.

Tunakumbuka kuhusu uvunaji na usafirishaji wa magogo kutoka katika misitu.
Hakuna aliyewahi kuwajibika kutokana na hilo. Na pia tunakumbuka faru chini ya ulinzi mkali kuuawa.
Faru waliosimamiwa na mh rais kurudishwa nchini

Hiyo ni mifano michache sana kuonyesha chanzo na upana wa tatizo.
Yote hayo yakitokea serikali imekuwa ikipanga bajeti kwa vikosi vifuatavyo(Rejea ripoti ya bunge 2.2.1)
Askari wa kuzuia ujangili (KDU)
Askari wa Wanyapori (TANAPA)
Askari wa Misitu (TSF)

Wakati huo huo kukiwa na idara ya usalama wa taifa (TISS) na jeshi la Polisi

Mawazri, ,manaibu mawaziri, makatibu wakuu na wakurugenzi wa taasisi hizo pamoja na zile zinazoingiliana huteuliwa na mh rais kwa kusaidiana na wasaidizi wake na vyombo alivyopewa kikazi.

Mheshimiwa rais alitangaza kupeleka jeshi kupambana na majangili yaliyoonekana kuzidi nguvu vikosi katika taasisi na wizara hizo. Mhe rais akarudia kauli yake bungeni akisema yapo matatizo yaliyojitokeza yanayohitaji marekebisho wakati wa operessheni hata hivyo ilifanikiwa.

Ni wazi serikali ikiongozwa na Rais na Waziri mkuu walipanga na kusimamia opersheni hiyo.
Ni dhahiri kuwa mtandao wa ujangili ni mpana ambao serikali iliufahamu na haikuweza kuushughulikia[Rejea taarifa ya bunge {6.2: XIV, XVII, XVIII,} {7.0: III,VIII,]

Taarifa inaonyesha waziri Kagasheki hakuhusishwa kama kiongozi wa wizara [7.0: II]
Ni wazi kuwa mtandao wa ujangili uliingia katika serikali (infiltrate) kiasia cha kuweza kupata hata siri za opereshini na hivyo waziri aliwekwa pembeni. [7:IX)

Hivyo kufeli kwa Opereshini chanzo chake ni kutokana na kuingiliwa na viongozi wa serikali na siasa ambao kamati haikuwataja waliotoa maagizo ya operesheni isiguse viongozi wa kisiasa wa ngazi yoyote.(Taarifa ya bunge [7.0: IX]

Na pia kuwatenga viongozi wa Mikoa na Wilaya ulikuwa ni mpango maalumu wa kuhakikisha kuwa mtandao unalindwa kutoka ngazi za juu na kuzuia kelele kutoka eneo lingine.

Duru za siasa tunampongeza waziri Kagasheki kwa uamuzi wake wa kuwajibika na kujiondoa katika kazi ambayo ugumu wake si kupambana na majangili tu bali wanasiasa na viongozi wa serikali ambao ni sehemu ya mtandao au ni wanufaika wa mafao yatokanyo na ujangili kisiasa au kimasilahi.

Mawaziri watatu waenguliwa
Tunaendelea sehemu ya II
Ukiingia ndani zaidi utakuta haikuwa makosa isipokuwa ni mfululizo wa kimfumo (utekelezaji wa ilani) ulotuleta Richmond na sasa Symbion.
 
Back
Top Bottom