Duru za Siasa: Matokeo ya Uchaguzi Marekani

Okay, John Brenman might have to go after January 20th but how about Trump's cabinet picks whose stand on issues has differed from their master? To name a few; Secretary of Sate Rex Tillerson, Attorney General Jeff Sessions, Secretary of Defence Gen. James Mattis (Ret) and many others. What happens to them after those 4 days? Will they go too unless they toe Trump's line?


The last time I checked Mr. Trump directed his cabinet nominees to be themselves in those hearings.
 
HALI YA MAMBO KUELEKEA SIKU 4 NA KUENDELEA

Sehemu ya I

Ijumaa ijayo saa sita mchana saa za US Trump atakuwa Rais wa 45 wa Marekani

Ataongoza Taifa hilo kwa miaka 4 ijayo kabla ya uchaguzi mwingine

Katika miaka 4 kuna mambo kadhaa yanayosubiri au yatakayotokea katika dunia hii

US ikiwa Taifa kubwa, inaangaliwa kwa uongozi wake kuliko mataifa mengine

Siasa za nje haziwezi kuepukika na hilo limeanza hata kabla ya kuingia Oval office
Trump amesema atatumia Taiwan kufanya negotiations na Taifa la uchumi wa pili China

Hili ni baada ya simu kwa 'Rais' wa Taiwan baada ya uchaguzi.

China ina sera ya 'One China' ikitambua Taiwan ni jimbo na si nchi kamili isipokuwa China

Marekani inatambua sera ya china na wala sera hiyo si ya US kwa China

China imejibu Taiwan haiwezi kuwa katikati ya mkataba au makubaliano yoyote na US

Kwamba inabaki na sera yake ya One China.

China ina influence kubwa katika siasa za dunia ya leo.
Ushawishi upo maeneo kama North Korea na Iran. China imekuwa mshiriki

Matumizi ya Taiwan yatailazimisha China kusimama na N.Korea.

Trump alilaumu utawala wa Obama kuhusu N.Korea. Katika hali hiyo kitatokea nini?

Umoja ulaya
EU imetoa kauli kuhusu Marekani kuhamisha ubalozi wake Jerusalem kutoka Tel Aviv.
Nchi zinasema suala ni hatari kwa amani ya mashariki ya kati , Israel-Palestine

Je, Trump atahamisha ubalozi wake na kuwatenga washirika wake wa Ulaya?

NATO
Kauli ya Trump kuhusu NATO kuwa 'obselete' inaleta kiwewe katika mataifa washirika

Mataifa hayo hayaelewi nini hatma yao na umoja wa NATO katika kipindi hiki

Angela Merkel
Trump amemlaumu Angela kwa sera za Wahamiaji.

Kauli yake imekuja kukiwa na mwezi wa uchaguzi wa Ujerumani.

Katika swali la msingi, Trump alimlinganisha Angela Merkel na Putin katika mizani

Inaendelea
 
HALI YA MAMBO KUELEKEA SIKU 4 NA KUENDELEA

Sehemu ya II

Tendo la kumlinganisha Merkel na Putin linaonekana kama hatua za awali za 'kufutika kwa NATO'

Merkel ni kiungo muhimu kuiweka Ulaya pamoja baada ya Brexit

Trump 'kumpandisha chati' Putin kwa ulingano na Merkel inatishia nchi za Ulaya zinazoona Russia imepania kujitanua Ulaya na mashariki ya kati kama ilivyo Iran, Syria na Ukraine

Nchi za Ulaya ni muhimu kwa ulinzi wa US kama tulivyoona US ikipeleka askari Poland hivi Karibuni

Ujerumani imekuwa kituo kikubwa cha kijeshi cha US kwa muda mrefu

Mtazamo wa Trump ni tofauti na wateule wake kama SoS na CIA Dir.
Hawa ni watu muhimu kwa maamuzi ya Trump ingawa uamuzi wa mwisho anao.

Vipi ata square maoni yake na wateule bila msigishano katika 'dunia' ya leo isiyotabirika?

Kuvurugika kwa Umoja wa Ulaya na NATO kunaipa Russia nafasi ya kujitanua maeneo hayo

Trump na Russia

Uhusiano wa Trump na Russia utakuwa na utata mkubwa.

Russia inatuhumiwa kutaka kuhujumu uchaguzi wa Ujerumani

Kauli ya Trump dhidi ya Merkel italeta utata si Ujerumani tu bali Ulaya

Inaonekana Trump anataka mahusiano na Russia.

Trump atawezaje ku deal na Russia yenye lengo la kujitanua Ulaya na mashariki ya kati?

Kwa mfano, Uhusiano mbaya na Ujerumani utadhoofisha nchi za ulaya.

Trump atawezaje kuizuia Russia akiwa ni rafiki yake?

Usalama wa Marekani utahakikishwaje ikiwa Russia itazidi kusogea Ulaya!

Inaendelea
 
Mashariki ya kati

Trump amezungumzia sana deal ya Iran. Wakati huo huo Iran na Russia ni washirika wazuri
Trump atafanya deal ipi dhidi ya Iran bila kumuudhi Russia au kinyume chake?

Hali inachanganya zaidi kwasababu Israel ina wasi wasi na Iran kuhusu silaha za Nyuklia
Israel inatitegemea sana US katika suala la Iran.

Trump ata deal vipi na Israel akiwa na Russia, mshirika wa Iran,US na Iran zikiwa mahasimu?

Trump anakabiliana na China katika hatua za awali hasa katika mambo ya biashara
Kuna mzozo wa South China sea kati ya US na China. Wakati huo huo China ni mshirika wa Russia

Trump ataweza kuwa rafiki wa Russia na hasimu wa China katika wakati mmoja?

Tusemezane
 
Siku zote Marekani hataki wataAlamu wa hesabu na wale wabunifu wa bobezi watengeneze timu moja! Kuruhusu kitu hicho ni suicidal mission kwa US. Trump anatumia same technique kuvunja uti wa mgongo wa Sino -Russia! Muda huu wa Putin, uti wa mgongo huo hautaguswa.
Ukweli kama nilivyowahi kuandika kwenye post za nyuma,Trump ataingusha US pole pole kuliko HRC ambavyo angeiangusha US kwa haraka sana na kusababisha mtikisiko duniani.
Kwa kifupi, kwa mbali namuona kama Trump ana vitabia kama alivyokuwanavyo Boris Yeltsen wakati inaanguka USSR!
 
Siku zote Marekani hataki wataAlamu wa hesabu na wale wabunifu wa bobezi watengeneze timu moja! Kuruhusu kitu hicho ni suicidal mission kwa US. Trump anatumia same technique kuvunja uti wa mgongo wa Sino -Russia! Muda huu wa Putin, uti wa mgongo huo hautaguswa.
Ukweli kama nilivyowahi kuandika kwenye post za nyuma,Trump ataingusha US pole pole kuliko HRC ambavyo angeiangusha US kwa haraka sana na kusababisha mtikisiko duniani.
Kwa kifupi, kwa mbali namuona kama Trump ana vitabia kama alivyokuwanavyo Boris Yeltsen wakati inaanguka USSR!
Mkuu naomba msaada kidogo hapa katika kuelewa.

Tofauti ya Obama na Hillary katika mitazamo, sera, mikakati, mbinu n.k. ni ipi?
 
Ukweli kama nilivyowahi kuandika kwenye post za nyuma,Trump ataingusha US pole pole kuliko HRC ambavyo angeiangusha US kwa haraka sana na kusababisha mtikisiko duniani
Mkuu tusaidie na hili, hawa wawili wanaiangushaje US kwa hali mbili ulizosema?
I mean haraka haraka na pole pole, tukumbushe kwasababu uliandika kama ulivyosema
 
It has been so wonderful to discuss 2016 US election with you guys. It was fantastic. I have tremendous respect for all of you guys.

I think as you all can appreciate, I engaged in this discussion humbly and in a constructive way.

Many people whined on election results for months. Seems to me with all due respect that some of you guys just wanted your ideas to prevail in these discussions. Its okay, but it is not healthy.

Thomas Jefferson once said, "Every difference of opinion is not a difference of principle"

Obviously, that's part of democracy and Donald J Trump is now the 45th US President. Congratulations Mr. President.

He gave an amazing and genuine inaugural address, he literally touched on all grounds. I couldn't agree with him more.

I was surprised in all fairness, seeing the former US President Barack Obama giving the so called 'final farewell address' just a few minutes after inauguration. I don't know why he did it, I don't agree with his timing, I don't think it was Presidential, but who cares?, all talk no action!

I wonder why he decided to go to California instead of Chicago. It was encouraging seeing Hillary around.

Democrats owe President Trump an open mind and a chance to lead as Hillary said and they should work together on behalf of United States, now that the government is controlled by the People.

President Donald Trump said “when you open your heart to patriotism, there is no room for prejudice.”

I look forward to engaging with you in other topics in this forum and other forums.
 
TRUMP RAIS WA 45 WA MAREKANI

Akiwa na umri wa miaka 70 , mzee zaidi kuwa Rais ameapishwa leo kama Rais wa 45 wa US
Sherehe ya kuapishwa iliambatana na kuondoka kwa Rais Obama kuashiria zama mpya za Trump

Tukio la kubadilisha madaraka lilikuwa na sura mbili, furaha na huzuni kwa kila upande
Kila hatua ilifanyika kwa kuzingatia utamaduni wa Marekani wa miaka nenda rudi

Kubwa ni kubadilishana madaraka kwa njia ya amani na utulivu kwa wahusika kwa kufuata sheria
Pamoja na uwepo wa kupingwa kwa Trump na makundi, kwa US hiyo ni sehemu ya demokrasia

Katika uchaguzi uliokuwa na mazonge zonge ya kila aina, bado sheria zilifuatwa bila shurti
Hata kama kuna aliyechukizwa na lolote, sheria ilikuwa mwongozo katika demkorasia iliyokomaa

Mara nyingi tumeeleza, demokrasia ya US hailinganishwi na vinchi vinavyoendelea.
Katika nchi hizo, Rais huondoka kwa nguvu za kijeshi au chaguzi kufutwa n.k. ubabaishaji tu

Kwa US hata mahasimu wa kisiasa, huweka tofauti zao pembeni na kuliweka Taifa mbele

Tuangalie sura mbili za tukio, Obama na Trump sehemu inayofuata
 
TRUMP RAIS WA 45 WA MAREKANI

Akiwa na umri wa miaka 74 , mzee zaidi kuwa Rais ameapishwa leo kama Rais wa 45 wa US
Sherehe ya kuapishwa iliambatana na kuondoka kwa Rais Obama kuashiria zama mpya za Trump

Tukio la kubadilisha madaraka lilikuwa na sura mbili, furaha na huzuni kwa kila upande
Kila hatua ilifanyika kwa kuzingatia utamaduni wa Marekani wa miaka nenda rudi

Kubwa ni kubadilishana madaraka kwa njia ya amani na utulivu kwa wahusika kwa kufuata sheria
Pamoja na uwepo wa kupingwa kwa Trump na makundi, kwa US hiyo ni sehemu ya demokrasia

Katika uchaguzi uliokuwa na mazonge zonge ya kila aina, bado sheria zilifuatwa bila shurti
Hata kama kuna aliyechukizwa na lolote, sheria ilikuwa mwongozo katika demkorasia iliyokomaa

Mara nyingi tumeeleza, demokrasia ya US hailinganishwi na vinchi vinavyoendelea.
Katika nchi hizo, Rais huondoka kwa nguvu za kijeshi au chaguzi kufutwa n.k. ubabaishaji tu

Kwa US hata mahasimu wa kisiasa, huweka tofauti zao pembeni na kuliweka Taifa mbele

Tuangalie sura mbili za tukio, Obama na Trump sehemu inayofuata
Trump hana miaka 74.

Ana miaka 70.

Check your sources.....
 
KUONDOKA KWA OBAMA

Kulikuwa na majonzi wakatia anaingia katika Marine one ikishiria kumaliza muda wake wa Urais
Majonzi yalitawaliwa na hisia nyingi. Wapo walioamini akiwa Rais mweusi huenda wasione mwingine

Hawana uhakika kwa mgawanyiko wa Taifa katika misingi ya
Trump hana miaka 74.

Ana miaka 70.

Check your sources.....
Thank you
 
KUONDOKA KWA OBAMA

Kulikuwa na majonzi kutoka ndani ya Ikulu na nje.
Kwa US utamaduni wa viongozi hufuatwa waingereza wakisema 'to the letter'.

Alivyoondoka Obama ndivyo ilivyokuwa kwa watangulizi wake

Kifungua kinywa WH kilikuwa na wafanyakazi aliokaa nao miaka 8. Ni utamaduni
Ni utamaduni kama ule wa kumwalika Trump na kupata naye chai kabla na baada

Kwa asili ni rahisi watu kuwa na hisia hasa kwa kiongozi waliyemzoea na kuishi naye.

Hisia ya pili ni sehemu ya watu wanaoona ni Rais kutoka jamii ya rangi na huenda wasione mwingine katika umri wao hasa wakiangalia hali ilivyo na mgawanyiko

Na wapo wenye hisia kwa mambo mazuri aliyofanya

Kama mwanadamu hakuwa mtimilifu lakini yapo mazuri yaliwagusa baadhi kwa hisia

Ikiwa ni familia ya kwanza ya weusi WH macho ya wengi yaliekezwa huko
Familia ya Obama imeondoka bila ya kashfa au kwa watendaji wake

Obama ameondoka akiwa na 'approval rating' ya asilimia 60, arguably polls zinafanywa na taasisi tofauti ukweli utabaki kuwa ni nzuri kushinda marais wengi waliomtangulia

Katika moja ya mahojiano,alisema angeingia katika uchaguzi angemshinda Trump
Obama aliwaambia Dem angetumia rekodi yake kushawishi

Tatizo ni kumpima Obama bila kuangalia historia hasa tarehe 20 Jan 2009 hali ilikuwaje

Kwa mfano, wapo wenye hoja za kusikia, ukuaji uchumi wa takribani 1.5% ni mdogo sana tangu vita kuu ya II.Ni kweli ukilinganisha na ukuaji wa wakati huo

Si kweli kwa upana. Kwanza, hakuna mdororo mkubwa kuliko 2008 tangu WWII.

Ni kigezo gani kimetumika kusema ukuaji ni mbovu post recession ikiwa hakuna ulinganifu mwingine katikati isipokuwa wa vita kuu ya II?

Pili, wakati anaingia ukuaji ulikuwaje na alipoondoka ulikuwaje?

Ndivyo anavyopaswa kupimwa kwa usalama, uchumi , siasa na mambo ya kijami
Hayo ndiyo yanagusa wananchi na kuleta hisia kuliko hoja za chai na kuita mkutano

Overall kukabidhi Taifa kubwa kiongozi duniani baada ya miaka 8, anastahili pongezi

Kwa alivyojiheshimu, yeye, familia na serikali yake katika kumechangia kuleta hisia kwa jamii wakati anapunga mkono kuondoka

Trump na hotuba ....Inafuata
 
HOTUBA YA TRUMP KATIKA KUTAWAZWA

Utamaduni na desturi ya US ni ni Rais kutoa hotuba baada ya kutawazwa

Trump akiwa mbele ya umma na marais 4 walio hai kati ya 5 (Bush seniorhakuwepo) alitoa hotuba

Kwa kawaida ni hotuba ya kulileta Taifa pamoja baada ya kampeni kali zenye michubuko

Hotuba ya Rais Trump ilikuwa na mchangyiko uliohitaji umakini sana kumwelewa
Hotuba iliyokosa vionjo vya kuleta ummoja, na ilizidi kuchanganya kwa mengi

Kwanza, kwa 'base' yake matumizi ya kauli kali kama za kampeni yalisisimua.
Hilo ni jema kuleta hamasa akielekea WH. Hata hivyo, wakati huo alikuwa Rais wa US.Hapo lipo tatizo

Pili. Kuna kundi la wanaosubiri matumaini kutokana na hali za kiuchumi.
Nalo lilisimkwa kwa matumaini ya US kwanza, kutengeneza ajira na kuimarisha hali za maisha

Tatu, kuna kundi lililokuwa na shaka juu ya kauli zake akiwa mgombea na mteule.
Kwa hotuba aliyotoa, shaka katika kundi hili imeongezeka badala ya kupungua

Nne, kuna kundi lililokuwa inasoma kauli zake kubaini mwelekeo wa US.
Hili liliishia katika kuchanganyikiwa. Kuna maeneo aliyojichanganya sana. Tutaeleza baadh tu

Tuanze na kundi la nne. Rais Trump ameeleza kutotumia rasilimali kwa ulinzi wa mataifa mengine

Kwamba rasilimali zinazotumika huko zitarudi kujenga nyumbani na kuimarisha uchumi

Hoja
Sera ya US ni kujitanua kiulinzi.Ni sera za mbabe mmoja wa dunia. Sera zimetumiwa na Marais 4 waliokuwepo. Alipaswa kujiuliza , je ni kwanini? Sababu za kuweka majeshi nje zimeondoka?

Trump aelewe, dunia ya sasa ina super power wanaojitutumua. US kuondoa vituo vya ulinzi ni kutengeneza upinzani usio na maana na vita itarudi ufukweni na si nje

Katika moja ya hotuba za Rais J.Kennedy alieleza suala hili akisema, ni muhimu kwa US kuwafuata maadui walipo kuliko kuwasubiri wafike ufukweni. Je, Trump anataka wafike ufukweni kwanza?

US haina vituo vya kijeshi Ujerumani, Poland, Korea kusini, Japan, Philipine n.k. kama hisani

Hizo ni sehemu muhimu za mkakati wa ulinzi wa US na si fadhila kama anavyodai

Pili: Trump amedai kuifuta ISIS katika uso wa dunia na kupambana na Islamic terrorist.

Hoja:
Kwa kauli za nyuma dhidi ya Uislam na muunganisho wa Islamic terrorist na ISIS katika hotuba, itaonekana nia yake dhidi ya Waislam bado ipo pale pale. Hili litamsumbua katika njia mbili

1. Kwa siasa za ndani kutakosekana ushirikiano katika ya serikali na moderate kwavile zipo hisia tayari
2. Kwa siasa za nje, picha itakuzwa na hatapata ushirikiano na mataifa ya 'kiislam'

Kwa mantiki hiyo, ataifuataje ISIS ikiwa ameondoa majeshi katika maeneo nyeti ya ulinzi?

Atapambanaje na islamic terrorist wakiwa katika maeneo salama yasiyofikiwa na US huko nje ?

Atapambana vipi bila washirika wa 'kiislam' kutokana na kauli wanazohisi ni 'za kuwatenga'?

Hayo yana maana, US haitakuwa na nguvu za ushawishi wa siasa za dunia na kuwa weak again.

Kuondoa majeshi kutaanzisha mashindano ya nguvu na kuibuka kwa visuper power kama Iran, huku superpower kama China na Russia zikjitanua

Inaendele
 
HOTUBA YA TRUMP

Inaendelea...

Trump anaposema anaondoa majeshi yanayolinda mataifa mengine inaleta mjadala mwingine

Moja ya misingi mikubwa ya Republican ni ulinzi na usalama ukiambatana na kujitanua kijeshi
Je, Trump anasimama wapi ikiwa hakubaliani na 'Republican Dogma'

Kwa muda mrefu ndani na nje ya kampeni, Trump alimlaumu Obama kwa kuondoa majeshi Iraq
Trump hakuwa mkweli, aliyeondoa ni Bush. Hoja,ikitokea kama ya Iraq atapeleka majeshi huko?

Je, huko hakutakuwa kulinda 'shore' za nchi nyingine

Ndivyo alivyolaumu kuhusu Syria akimshambulia Obama hata mkurugenzi wa CIA.
Bila majeshi karibu au majeshi katika maeneo ya mkakati atafanikiwa vipi katika mission zake?

Huu ni ujumbe uliochanganya kundi la nne tulilosema linalofuatilia mwelekeo wa siasa za US
Republican nao wamechanganyikiwa, hawaelewi Trump ni Rais kutoka GOP, Dem au independent

Hotuba ya jana si kigezo pekee cha kuchanganyikiwa kwa 'kundi la nne na Republican'

Tukitoka nje kidogo ya hotuba yake, kuna suala la 'Obamacare' ambalo hakulizungumizia
Jana akasaini executive order kuhusu ACA inayoitwa Obamcare.

Hakuna details zaidi ya kuzipa taasisi nguvu za kubadili yanayoonekana mzigo

Wiki iliyopita ali tweet kuwa insurance ni kwa kila mtu kama ambavyo Obamacare ilivyo

Republican wanaandika ACA inayoondoa serikali katika usimamizi na kutoa access kwa kila mmoja

Kuchanganyikiwa:

Hizo institutions zitaondoa vifungu gani vya ACA bila kuharibu ACA yenyewe?
Trump anaposema insurance kwa kila mmoja, wakati GOP hawataki hilo kuna message gani?

Kuchaganyikiwa kwa makundi ya jamii kunaenda mbali katika hotuba na suala la uchumi

Hili tutalijadili. Inaendelea.....
 
HOTUBA YA TRUMP

Inaendelea

Katika otuba yake ya kwanza kama Rais , Trump alizungumzia kuhusu ajira za US

Alisema uongozi wake 'only America first' akisisitiza dhana ya masilahi ya USA kwanza

Kwa muda, Trump amekuwa na falsafa ya 'protectionism' kwa viwanda vya ndani.
Ametishia kuweka kodi ya takribani 35% kwa bidhaa zinazotengenezwa nje kuuzwa US

Trump hakubaliani na mkataba wa NAFTA na ule wa TPP

Amekuwa mwiba kwa China hata kutishia kutumia sera ya China moja 'one China Policy' Akimaanisha mikataba ya biashara kuiweka China katika meza kwa kutumia Taiwan

Katika makundi tuliyotaja bandiko 495,kundi la kwanza na la pili lilifurahia hotuba
Kundi la tatu lenye mashaka liliendelea kupata mashaka

Kundi la nne, linalotazama mwelekeo wa serikali mpya linataabika.Kuna sababu za msingi

1. Misingi ya Republican ni free market, serikali ikae mbali na shughuli za biashara

Republican hupendelea serikali ndogo ikiacha soko liamue hatma ya uchumi

Bunge linapata wakati mgumu kubadili au kuandika ACA au Obamacare kwasababu linataka afya lisiwe suala la serikali ili kupunguza ukubwa

Kwa upande mwingine Obamacare imekuwa maarufu kuiondoa kutatibua nchi na uchumi

Trump haamini katika free market anataka 'protectionism' kuendesha uchumi

Katika mkutano wa 'uchumi' kule Davos, Rais wa China alipigia upatu free market

China iliyokuwa namba moja kwa 'protectionism' sasa ndiye kinara wa Free market

Hofu ya kwanza inaanzia hapa.

Je, mwelekeo wa US ni kujitoa katika soko huria na nafasi hiyo kuchukuliwa na China?

'Make America great again' itakuwaje successful under China clout?

Je, Republican inaachana na 'hallmark' yake ya Free market?

Ni kosa kusema Trump ameutupa ubepari (Capitalism)kwa kutoeleweka anasimamia nini

Trump ni muumini wa ubepari wa mahusiano ' Crony Capitalism'

Crony capitalism ni ubeapari wa mahusiano ya mabepari na serikali tofauti na soko huria.

Mfano, Trump anapoingia deal na CEOs wa makampuni wasiondoe uzalishaji, ni mahusiano kati ya serikali na mabepari na si serikali na nguvu ya soko huria

Kwa mtazamo tofauti, sera ya Trump kuhusu uchumi itakuwa na sura mbili

1. Kwa muda mfupi atafanikiwa kutengeneza ajira na sekta ya uzalishaji viwanda
2. Kwa muda mrefu sera itakuwa na tatizo kuliko inavyodhaniwa, na kuleta matatizo

Tutaeleza ni kwanini bandiko lijalo

Inaendelea
 
TRUMP NA SERA ZA UCHUMI
Kabala ya kueleza athari za muda mfupi na mrefu wa sera za Trump, tuangalie nyuma

2009 Obama akichukua madaraka kwa recession ,mabenki na viwanda vilifunga au kupunguza wafanyakazi.

Hali ilikuwa mbaya kiasi cha kupoteza ajira kwa mamia na maelfu kwa mwezi

Trump yupo katika rekodi akipinga udhamini 'bail out' wa makampuni kama GM n.k.

Hoja yake, makampuni yaachwe yafe kwani nguvu ya soko itaamua yatakayo survive

Trump hakutilia maanani ajira zitakazopotea . Alipinga serikali kushiriki biashara

Kwa wakati huo alikuwa anasimamia sera za republican za soko huria 'free market.

Leo ni kinara wa kunusuru makampuni kama alivyofanya Obama tena kwa vitisho

Hakubaliani na free market hadharani huku akitekeleza crony capitalisma kwa kukutana na CEOs wa Makampuni na kuingia deal

Hatua za Obama zilikuwa na mafanikio licha ya kusemwa na wapinzani wake

GM imerudi katika ubora wake ikiuza magari hadi nchi za nje

Haya yalipotendwa na Obama Trump wafuasi wake wakasema 'talk, talk no action'

Trump yupo bize akitishia CEOs wa makampuni na kodi wakati wa kuleta badhiaa zilitengenezwa nje

Lengo lake ni kutengeneza ajira Marekani ambalo ni jambo zuri.

Hata hivyo, mafanikio yake ni ya muda mfupi yakiwa na athari kwa ajira kwa muda mrefu kama anavyoeleza Profe B.George wa Harvard Business school. Tutajadili kwa undani

Inaendelea
 
Back
Top Bottom