Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,390
- 31,338
- Thread starter
- #1,061
Mwalimu hili limekuwa suala lenye utata kidogo.Katika mazingira haya ya covid19 kampeni za uchaguzi zitafanyika vipi? Kutakuwa na mikutano ya hadhara? Kutakuwa na midahalo baina yao?
Kwa wagombea , Trump anaonekana kutojali sana suala la Corona kwasababu angependa kwenye base yake awajaze upepo wa habari za kutunga.
Anajua wazi kabisa na alishawahi kusema ''base'' yake inamsikiliza
Huko vijijini ndiko kabisa huwaambii kitu chochote hasa ukizingatia ndiko 'ubaguzi' ulipobobea
Pamoja na hayo , Joe Biden anamtishia sana hasa kumega sehemu ya wapiga kura wa vijijini.
Kuna independents ambao wengi wameondoka kwa Trump kutokana na chaos ya utawala wake
Juzi kulikuwa na ruling kuhusu Obama care na suala la birth control. Washauri wa Trump hawataki kurudisha Obamacare katika mjadala, ni kitu kinachoonekana kuwa maarufu kwasasa kuliko miaka 4 iliyopita.
Kitendo cha Trump kutumia DOJ kumega Obamacare nacho kinamweka mahali pagumu, hana mbadala wake
Kuhusu uchumi nako hali si nzuri. Unemployment ipo 14% kiwango kikubwa tangu depression post WWII
Kwa hili kauli za Trump zitamgharimu kwasababu zinaeleza kutokuwa makinini na Corona na kufika ilipo ambapo Wamarekani 30 milioni wamepoteza ajira zao.
Kampeni zitafanyika kwa mikutano?
Ni suala la muda na ikifika July tutaweza kupata uelekeo.
Kuhusu kura, state zimeanza kufuata mfumo wa kupiga kura kwa njia ya Posta
Trump hataki kabisa upiga huo wa kura
Kukataa kwake ni kwasababu Republicans kwa kutumia ''Gerrymandering na vote suppression'' walifanikiwa
Mfano, waliweka vituo vya kura mbali hasa kwenye maeneo ya Democrats.
Walichelesha kufungua vituo vya kura na wengi kutoweza kupiga kwa wakati
Kubwa zaidi walilazimisha kuwa na ID wakijua hata Raia hasa weusi wengine hawana
Trump hataki kusikia hilo na sasa anatumia DOJ kutaka kuzuia upigaji kura wa namna hiyo.