Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

Ha ha haa TUJITEGEMEE, utaokotezaokoteza hizi spin za RT News hadi lini? Je, did not participate in any wrongdoing in obtaining the materials in the first place, unaelewa maana yake? Kwa ufahamisho ni kweli kabisa kwamba hao watajwa hawakuhusika katika ku-obtain the materials in the first place kwani wahusika hasa wa hilo walikuwa ni Warusi, over?
Haya Mkuu, sasa na CNN nao wameanza spin kama za RT ?! Hata hivyo hao CNN wamenifahamisha mengi zaidi juu ya ' incompetence' ya "Chief Whip" wa Demo kwa kushindwa kuandaa mashtaka dhidi ya hao waliokuwa wanawatuhumu kuvuruga uchaguzi wa US. Yale maswali ulioniuliza kwa kweli sina majibu yake maana nadhani hizo ni lugha za kisheria ambazo ki-weledi siwezi kuudhibitishia ulimwengu kuwa najua maana yake.
====
180822193630-democratic-national-headquarters-exlarge-169.jpg


Washington (CNN)A federal judge Tuesday dismissed the Democratic National Committee's lawsuit against Russia, the Trump campaign and a number of individuals including Jared Kushner and Donald Trump Jr., saying the claims are either "moot" or "without merit."
Judge John Koeltl in New York ruled Trump campaign officials are protected under the First Amendment and cannot be held accountable for harming the DNC after it was hacked. The lawsuit was filed against a number of individuals the DNC alleged were in so-called collusion, including former campaign chairman Paul Manafort, conservative ally Roger Stone, the Trump campaign, Trump Jr., Kushner, Julian Assange and WikiLeaks.
The DNC had touted the lawsuit as a major way to fight back against the hack it suffered and to hold various Trump campaign officials accountable.
The Russian government cannot be sued in this way, Koeltl found, because it is a sovereign nation.
Additionally, the judge found that Trump campaign officials couldn't be held accountable for the publication of documents because of the way the DNC wrote its lawsuit, attributing the hack only to Russia.
-----
 
Nyongeza kutoka CNN
===
In two tweets, President Donald Trump claimed the suit's dismissal as a win against the collusion allegations and years-long Russia investigation into his campaign's affiliates, writing of "yet another total & complete vindication & exoneration from the Russian, WikiLeaks and every other form of HOAX perpetrated by the DNC, Radical Democrats and others. This is really big 'stuff' especially coming from a highly respected judge who was appointed by President Clinton. The Witch Hunt Ends!"
Former Trump campaign aide George Papadopoulos, one of the defendants, also tweeted about the suit's dismissal: "One more step to ending this witch hunt and going on offense to take on the deep state head on! Big win for America today!"
Another lawsuit against the Trump campaign brought by individuals for breach of privacy as a result of the hack was previously dismissed.
Koeltl was appointed by President Bill Clinton in 1994.
 
Tarehe 17 inaweza kuwa na matokeo mawili, kwanza, kumsafisha Trump once and for all
Pili, kumtia katika matatizo makubwa sana ya impeachment.

Haya ya Mueller si habari njema hata kidogo, ni upanga wenye ncha mbili

Post #933 ilisema kuna matokeo mawili katika mahojiano ya Mueller kwenye Kamati za Bunge.

Mahojiano yameshaisha, na ni dhahiri "Trump alisafishwa once and for all," na "matatizo makubwa ya impeachment" yalizikwa rasmi. Mueller ameboronga sana ni kama vile ile ripoti siyo yake aliandikiwa, lakini ndio tatizo la kutaka kulazimisha uongo kuwa kweli.

Wawakilishi na wananchi wengi zaidi bila kujali vyama vyao, hawana interest tena na uchunguzi wa Mueller au uchunguzi wowote ule dhidi ya Trump.

Chunguzi ambazo zinatarajiwa kwa sasa ni zile za AG Barr na Inspector General (IG) Mike Horowitz, ambazo zinatarajiwa kueleza chanzo cha uchunguzi dhidi ya Trump na washirika wake.

Kwanini FBI walidukua mawasiliano ya Carter Page (mshauri wa sera za kigeni wa kampeni ya Trump)?

Kwanini FBI walitumia taarifa (dossier) za uongo za Christopher Steele (mshirika wa Hillary Clinton) kuhalalisha udukuzi huo dhidi ya kampeni ya Urais wa chama cha upinzani (Republican kwa wakati huo)?

FBI hawakujua kuwa Christopher Steele alikuwa mshirika wa Hillary?

Nani alikuwa anatoa maagizo kutumia FBI kisiasa dhidi ya kampeni ya Urais wa chama cha upinzani?

Kwanini FBI walim-spy pia George Papadopoulos (aliyekuwa mmoja wa washauri wa kampeni ya Trump kuhusu sera za kigeni) kwa kutumia watu wao kama akina Halpert, Downer, Mifsud, Thompson, na mwanamke aliyejiita Azra Turk?

Baada ya kumfuatilia Papadopoulos, FBI walianzisha uchunguzi dhidi ya Trump July 31, 2016 kwa madai kuwa waliambiwa na "Mwanadiplomasia fulani" aliyeambiwa na Papadopoulos kuwa "Russia wana taarifa mbaya ya Hillary." Papadopoulos yeye aliambiwa na Joseph Mifsud. Miezi 22 FBI walimchunguza Trump kwa sababu ya Mifsud. Huyu Mifsud ni nani na yeye aliambiwa na nani?

Mueller hakujibu maswali haya na mengine mengi, ambayo yangetoa mwanga kuhusu chanzo cha uchunguzi wake na uchunguzi wa FBI dhidi ya Trump na washirika wake.

Tayari Trump alisha-declassify taarifa za kiintelligensia ili kumruhusu AG Barr kupata taarifa zote katika uchunguzi wake na alishawaagiza wakurugenzi wa FBI, CIA na NSA wampe Barr ushirikiano.

Hili zigo linaenda moja kwa moja kwa serikali ya Obama na team yake. Wao ndio waliofanya njama zote hizi kuhakikisha Trump hawi Rais wa US. Uchunguzi wa FBI dhidi ya Trump ulilenga kumpaka Trump kama puppet wa Russia ili ashindwe Urais, lakini ikawa vinginevyo, alishinda.

Hillary ikabidi aombe kura irudiwe kuhesabiwa upya Michigan, Pennsylvania, and Wisconsin kwa madai kuwa Russia walidukua mashine ili kumuibia kura zake kumpa Trump. Kura zikahesabiwa upya, majibu yakawa yaleyale.

Baada ya Trump kuapishwa, Dems wakaanzisha uchunguzi wa Mueller ili kuhakikisha Trump anaanguka au hachaguliki 2020, lakini nayo imeshindikana.

Dems na wafuasi wao, hata waliopo humu wakafananisha uchunguzi dhidi ya Richard Nixon na Trump na kudai Trump ataondoka kama Nixon, lakini matokeo yake waliumbuka.

Dems wamekata tamaa, badala ya kushughulika na maendeleo na mambo mengine ya muhimu, waliona kushinda House ni fursa ya kudeal na kumzuia Trump kutekeleza ahadi zake, ili asichagulike 2020, ili waje waambie wananchi kuwa Trump ameshindwa kazi wachague Rais wa Democrat, lakini wananchi ni kama wameziba masikio.

Media zimeishiwa headlines za maana against Trump, na ndio maana hata waliokuwa wanamponda Trump humu ni kama vile wamepigwa ganzi.
 
Media zimeishiwa headlines za maana against Trump, na ndio maana hata waliokuwa wanamponda Trump humu ni kama vile wamepigwa ganzi.
Hivi sasa hali yake ni mbaya kuliko wakati wowote uliopita ila ni vile tu Marekani sheria na taratibu zinaheshimiwa na hivyo ni lazima zifuatwe.
 
Hivi sasa hali yake ni mbaya kuliko wakati wowote uliopita ila ni vile tu Marekani sheria na taratibu zinaheshimiwa na hivyo ni lazima zifuatwe.
Hizo ni hisia tu, Trump anakuwa kwenye hali mbaya kwa sababu gani? Testimony ya Mueller? Au McGahn? Au kesi zilizopo mahakamani?

Mwanzoni Trump na Republicans walikuwa wakiwaendekeza sana Dems na chunguzi zao uchwara kila mara.

Dems na wakereketwa wao wamechanganyikiwa vibaya, ni wa kuhurumiwa tu! Hivi Dems wame-achieve nini kwenye House? Kukubali kuwa Trump kawapiga tena knock-out ndio taabu.

"It is a characteristic of the wisdom not to do desperate things" Henry Thoreau.
 
Hizo ni hisia tu, Trump anakuwa kwenye hali mbaya kwa sababu gani? Testimony ya Mueller? Au McGahn? Au kesi zilizopo mahakamani?
Nakuhurumia sana, unaweza kudhani unajua kumbe hujui kitu. Gurudumu limeanza kuzunguka na muda si mrefu mambo yatakuwa hadharani. Marekani si Tanzania ambako raia wanaamini Rais wao ana uwezo hata wa kuzuia tsunami.

Siwashangai Watanzania wanaomsujudu jiwe wakimsifu Trump. Tatizo ni kwamba tuna watu ambao kwao Tanzania ndio dunia. Vituko vya Trump hivi sasa ni, kwa lugha ya wenzetu, the last kicks of a dying horse...kalaghabaho!
 
VIUNGANI DC

Katika wiki kadhaa yamejiri mengi katika viunga vya Washington, DC
Kama ilivyo ada mengi yanahusu utawala wa Trump, yakihusisha vitimbwi kadha wa kadha

Tukio kubwa lilosubiriwa ilikuwa la mahojiano kati ya Mchunguzi Mueller na kamati za Bunge
Baada ya taarifa yake kuwekwa hadharani, Mueller alisema hatasema zaidi nje ya ripoti

Hicho ndicho kilichotokea, Mueller hakujibu maswali takribani 206 akitumia privilege ya kutozungumza baadhi ya mambo ambayo mengine yapo katika uchunguzi na mengine yakiwa yamefichwa na AG Barr hadi leo

Kilichokuwa kipya ni baadhi ya utata kufafanuliwa na kumaliza sehemu ya mvutano wa hoja
1. Trump alikuwa anadai kuwa Mueller ana conflict of interest kwani alimuomba awe mkuu wa FBI siku moja kabla ya uteuzi wake

Mueller: Alithibitisha kuwa hakuomba kazi kama madai ya Trump yasemavyo
Hapa ikumbukwe Mueller alikuwa chini ya kiapo na hivyo kauli yake ina uthabiti
Kuanzia siku hiyo hoja ya conflict of interest imekwisha

Mueller: Taarifa yake haiku ''total exoneration'' Trump kwa maana haikumsafisha Trump
Hii ni kuikana kauli ya Trump ya ''taarifa kuwa na total exonerations and vindication''

2. Mueller : Alithibitisha kuwa Russia iliingilia uchaguzi na hadi sasa wanaendelea na kazi hiyo kwa nia ya kumsaidia Trump ashinde uchaguzi. Hii inathibitika kwa kauli ya Putin akiwa na Trump nchini Finland akisema ni kwe
li Russia ilitaka ashinde uchaguzi.

3.Mueller: Alithibitisha kuwa Trump alikataa mahaojiano na kamati kinyume na madai ya Trump kwamba hakuitwa na kwamba kama angeitwa angalikwenda kwani hana la kuficha

4.Obstruction of justice: Mueller akathibitisha uwepo wake na kusema taratibu za kisheria zilimzuia kumshtaki Rais kama ilivyo utaratibu wa DOJ.

5. Conspiracy: Mueller alisema hakukuwa na ushahidi wa kutosha wa mashtaka.
Hapa alithibitisha kauli kuwa conspiracy ilikuwepo lakini haikuwa na ushahidi wa kimashtaka

5. Mueller: Hakujibu baadhi ya hoja kwa kusema hatakwenda nje ya taarifa na kwamba habari nyingine ni nyeti kuwekwa hadharani

Katika hali isiyotarajiwa Mueller alisema ''Rais Trump anaweza kushtakiwa baada ya Urais'' ingawa baada ya mapunziko alisahihisha kauli yake baada ya kuulizwa na mjumbe wa GOP.

Kuna shahidi muhimu aliyewekewa uzio na utawala wa Trump. Huyu ni bwana Macgahn ambaye ni shahidi muhimu sana katika jaribio la obstruction of justice

Huyu bwana ametajwa zaidi ya mara 50 katika taarifa ya Mueller
Mchakato wa kumwita una ugumu wake ingawa suala limeenda mahakamani

Hayo ni baadhi ya yaliyojiri yakiacha swali, je, kuna sababu za impeachment?

Katika mazingira ya kawaida jibu ni ndiyo! Uchunguzi ungeachwa hadharani na AG Barr uchafu mwingi ungetosha. Kama mashahidi wangeatikana kwa urahisi ingalikuwa dhahma

Kwasasa jibu la ndiyo lina tatizo na hilo ndilo linawasumbua Democrats
Karata kubwa ipo katika Senate!

Tutafafanua zaidi
 
Nakuhurumia sana, unaweza kudhani unajua kumbe hujui kitu. Gurudumu limeanza kuzunguka na muda si mrefu mambo yatakuwa hadharani. Marekani si Tanzania ambako raia wanaamini Rais wao ana uwezo hata wa kuzuia tsunami.

Tatizo umeruhusu kuongozwa na hisia! Hivi ulisikiliza testimony ya Mueller kweli?

Siwashangai Watanzania wanaomsujudu jiwe wakimsifu Trump. Tatizo ni kwamba tuna watu ambao kwao Tanzania ndio dunia. Vituko vya Trump hivi sasa ni, kwa lugha ya wenzetu, the last kicks of a dying horse...kalaghabaho!

Hii inaitwa "spinning", jitahidi usiongozwe na hisia! Tunarudi palepale, Mueller ameboronga na amemsha hisia zaidi za watu wengi kutaka kujua chanzo cha uchunguzi wake na uchunguzi wa FBI dhidi ya Trump.
 
Tatizo umeruhusu kuongozwa na hisia! Hivi ulisikiliza testimony ya Mueller kweli?
Unajua kwa nini Mueller hakum-indict Trump? Unajua sababu ya Burr kupingana na uamuzi huo wa Mueller? Je ni kweli Mueller alimpata Trump na hatia lakini akasita kuchukua hatua sahihi? Kwa ufahamisho tu ni kwamba proceedings tayari zimeanzishwa na chombo husika kuhusu mkanganyiko huo.
Hii inaitwa "spinning", jitahidi usiongozwe na hisia! Tunarudi palepale, Mueller ameboronga na amemsha hisia zaidi za watu wengi kutaka kujua chanzo cha uchunguzi wake na uchunguzi wa FBI dhidi ya Trump.
Naona tunakubaliana kwamba Mueller yawezekana aliboronga kwa kutomtia hatiani Trump kwa kisingizio cha a sitting President cannot be indicted...sababu iliyopingwa na AG Burr. Kwa ufahamisho zaidi ni kwamba matayarisho ya awali ya impeachment tayari yameanza na Mueller anategemewa kuwa shahidi.
 
Tarehe 17 inaweza kuwa na matokeo mawili, kwanza, kumsafisha Trump once and for all. Pili, kumtia katika matatizo makubwa sana ya impeachment.

Baada ya taarifa yake kuwekwa hadharani, Mueller alisema hatasema zaidi nje ya ripoti. Hicho ndicho kilichotokea, Mueller hakujibu maswali takribani 206 akitumia privilege ya kutozungumza baadhi ya mambo ambayo mengine yapo katika uchunguzi na mengine yakiwa yamefichwa na AG Barr hadi leo

Mara nyingi Mueller alishindwa kuelezea hata yaliyomo kwenye ripoti yake (redacted). Mda mwingine aliulizwa maswali ili kuthibitisha jambo anakataa kujibu wakati maelezo yapo wazi kwenye ripoti.

Mueller alitegemewa kukazia hoja ya Dems ya "impeachment" lakini matokeo yake mahojiano yake yameanika uwezo wake usioridhisha wa kujibu hoja na kupelekea kuwapa credit zaidi Republicans.

Mueller hakuzungumzia chanzo cha uchunguzi wake na ule wa FBI dhidi ya Trump sio kwasababu yamefichwa kwenye ripoti yake na AG Barr, hapana! Ni kwa sababu ya uchunguzi unaondelea wa AG Barr ulioanza baada ya ripoti ya Mueller.

1. Trump alikuwa anadai kuwa Mueller ana conflict of interest kwani alimuomba awe mkuu wa FBI siku moja kabla ya uteuzi wake
Mueller: Alithibitisha kuwa hakuomba kazi kama madai ya Trump yasemavyo. Hapa ikumbukwe Mueller alikuwa chini ya kiapo na hivyo kauli yake ina uthabiti. Kuanzia siku hiyo hoja ya conflict of interest imekwisha

(A) Hoja ya 'conflict of interest' ya Mueller haijaisha, kwa kifupi mambo mengi hayajaisha. Kwahiyo kusema kwamba imekwisha kwa sababu Mueller alikuwa chini ya kiapo, sio hoja kwa sababu watu wanaweza kusema uongo chini ya kiapo pia.

Lakini pia nafasi ya mkurugenzi wa FBI ni nafasi ya uteuzi ambayo Rais anapendekeza jina ili kupigiwa kura na Senate. Kwa kuwa sio nafasi inayotangazwa ili watu waombe, unaweza kukuta Rais ana mtu wake au anachambua baadhi ya watu kwa kuzungumza nao. Lakini pia wanaohitaji nafasi kama hizi za uteuzi huwa wanazungumza na watu walio karibu ya Rais ili wawapendekeze kwake. Kitendo hiki kimantiki ni sawa na kuomba nafasi hizo.

Mueller alimwambia Mike Pence (VPOTUS) kuwa nafasi ya Mkurugenzi wa FBI ndiyo inaweza kumfanya arudi kufanya kazi serikalini.

"FBI director is the only job I'll come back for"

Hii kauli ni sawa na kuomba aangaliwe katika nafasi ya Mkurugenzi wa FBI, ndio maana Mike Pence alimkutanisha na Trump ili apigwe interview ya nafasi hiyo, ila Trump akampiga chini.

Mueller alipigwa chini "leo", "kesho" yake akateuliwa na Rod Rosenstein (Deputy AG) kuwa Special Counsel kumchunguza Trump. Yaani mtu kakupiga chini leo kesho yake unaanza kumchunguza!!!

(B) Ukisikiliza mahojiano ya Mueller na Rep. Louie Gohmert (R-TX), Mueller alizungumza na Trump kuhusu kufukuzwa kazi kwa James Comey (Frm FBI Director) katika interview yake siku moja kabla ya kuteuliwa kuwa Special Counsel. Kufukuzwa kwa Comey ndio chimbuko la uchunguzi Mueller dhidi ya Trump kuhusu Obstruction of Justice. Unachunguzaje suala ambalo wewe ni shahidi??

(C) Muller aliteua wasaidizi 13 katika uchunguzi wake, wote wakiwa ni wanachama wa Democrat na wanachangiaji wazuri wa kampeni zao! Mmoja wa wasaidizi aliowateua ni Peter Strzok ambaye sms zake na mpenzi wake Lisa Page zilizonaswa kwenye uchunguzi mwingine zilionesha kuwa ana chuki dhidi ya Trump na walikuwa na nia kumzuia Trump kuwa Rais. Unateuaje wasaidizi ambao unafahamu wana chuki ya wazi dhidi ya unayemchunguza?

Mueller hajajibu haya maswali kwa ufasaha.

Mueller: Taarifa yake haiku ''total exoneration'' Trump kwa maana haikumsafisha Trump
Hii ni kuikana kauli ya Trump ya ''taarifa kuwa na total exonerations and vindication''

Mueller hana mamlaka ya kufanya au kutofanya "exoneration". Trump alitumia neno hilo kisiasa ila Mueller amelitumia kwenye ripoti yake kwamba hajamu-'exonerate' Trump. Lakini pia Prosecutor kama Special Counsel hana mamlaka ya kutimisha hatia ya anayemchunguza.

Mahojiano ya Mueller na Rep. John Ratcliffe (R-TX) na Rep. Michael Turner (R-OH) yalimfumbua macho Mueller kuhusu mamlaka ambayo hana kisheria, ambayo alikuwa anafikiri anayo.

2. Mueller : Alithibitisha kuwa Russia iliingilia uchaguzi na hadi sasa wanaendelea na kazi hiyo kwa nia ya kumsaidia Trump ashinde uchaguzi. Hii inathibitika kwa kauli ya Putin akiwa na Trump nchini Finland akisema ni kweli Russia ilitaka ashinde uchaguzi.

Mueller alishindwa kumjibu Rep. Tom McClintock (R-CA), alipoulizwa kwanini hakutoa ushahidi mbele ya jaji wakati wa uchunguzi wake, unaoonyesha uhusiano wa IRA (Internet Research Agency) na Serikali ya Russia, ingawa kwenye ripoti yake anasema uhusiano huo upo!!

Marais wangapi walitaka Hillary ashinde? Au Trump ashinde? Marais wengi hawawezi kusema kwa kuhofia mahusiano mabaya iwapo waliyemtaka hakuwa Rais.

Hadi sasa Russia wanamsaidia Trump ashinde? Una ushahidi mkuu au ni hisia tu?! FBI walishasema hakuna ushahidi wa "impact" ya "Russia influence" kwenye uchaguzi wa US. Anayesababisha Trump ashinde ni utekelezaji wa ahadi zake.

3.Mueller: Alithibitisha kuwa Trump alikataa mahaojiano na kamati kinyume na madai ya Trump kwamba hakuitwa na kwamba kama angeitwa angalikwenda kwani hana la kuficha

Kwa mazingira yale Trump alifanya uamuzi sahihi wa kujibu kwa maandishi.

4.Obstruction of justice: Mueller akathibitisha uwepo wake na kusema taratibu za kisheria zilimzuia kumshtaki Rais kama ilivyo utaratibu wa DOJ.
Mueller hajathibitisha uwepo wa Obstruction of Justice katika testimony yake. Wala hakusema taratibu za kisheria zilimzuia kumshtaki Rais bali masuala magumu (difficult issues) ndizo zilizomzuia kuamua kushtaki au kutoshtaki.

Ukisikiliza mahojiano ya Dems na Mueller kwa mfano Rep. Hakeem Jeffries (D-NY), utagundua kuwa Mueller hakuthibitisha uwepo wa Obstruction of Justice. Rep. Hakeem kama Dems wengine alitaka Mueller athibitishe lakini Mueller hakuthibitisha.

Lakini huo unaoitwa "utaratibu wa kisheria" aliotumia Mueller kwenye Obstruction of Justice haupo kisheria, maana kwanza, kutokana na kanuni zinazomuongoza Special Counsel, anatakiwa afikie uamuzi wa kushtaki au kutoshtaki na sio uamuzi wa kutoamua kushtaki au kutoshtaki. Pili, hamna kanuni yoyote ya DOJ inayomruhusu Special Counsel 'kutoku-exonerate' mtu kwa sababu ameshindwa kufikia uamuzi kuhusu 'hatia' ya anayechunguzwa.
5. Conspiracy: Mueller alisema hakukuwa na ushahidi wa kutosha wa mashtaka.
Hapa alithibitisha kauli kuwa conspiracy ilikuwepo lakini haikuwa na ushahidi wa kimashtaka
Kama tendo fulani halijafikia kiwango cha kuwa kosa kisheria, unawezaje kusema tendo hilo ni kosa kisheria?. Na kama tendo hilo sio kosa kisheria, linawezaje kuwa kosa kwa misingi ya haki?

Viwango vya kutambua kosa kisheria vimewekwa kulinda haki. Mueller amehitimisha hakukuwa na conspiracy, ina maana ni mahusiano ya kawaida. Kutaka kufanya mahusiano ya kawaida yawe "conspiracy" kutahitaji definition nyingine ya "conspiracy" ambayo sio ile iliyotambulika kama kosa.
5. Mueller: Hakujibu baadhi ya hoja kwa kusema hatakwenda nje ya taarifa na kwamba habari nyingine ni nyeti kuwekwa hadharani
Mueller alisema hatazungumzia unredacted materials (zile catogory nne). Tusi-insinuate kuwa kwa kusema kwamba "habari nyingine ni nyeti kuwekwa hadharani" kunamaanisha kuna taarifa mbaya inafichwa kwa makusudi.

Maana kuna baadhi ya watu humu walidhani AG Barr alitoa redacted report ili kumbeba Trump na sio kufuata sheria na kanuni za DOJ.
Katika hali isiyotarajiwa Mueller alisema ''Rais Trump anaweza kushtakiwa baada ya Urais'' ingawa baada ya mapunziko alisahihisha kauli yake baada ya kuulizwa na mjumbe wa GOP.
Mueller hakusahihisha kauli yake kuhusu kumshtaki Rais baada ya kuondoka madarakani, alisema inawezekana na hakubadilika. Aliulizwa kuhusu hili na Rep. Ken Buck (R-CO).

Ila Mueller alisahihisha swali la Rep. Ted Lieu (D-CA) aliyemuuliza Mueller kama hakumshtaki Trump kwa sababu ya maoni OLC yanayosema Rais aliye madarakani hawezi kushtakiwa, mara ya kwanza alijibu ndio, halafu baadae akarekebisha kuwa hawakufikia uamuzi kama Rais alitenda kosa.
Kuna shahidi muhimu aliyewekewa uzio na utawala wa Trump. Huyu ni bwana Macgahn ambaye ni shahidi muhimu sana katika jaribio la obstruction of justice.
Huyu bwana ametajwa zaidi ya mara 50 katika taarifa ya Mueller. Mchakato wa kumwita una ugumu wake ingawa suala limeenda mahakamani

Mueller ameshindwa kuwapa Dems wanachokitafuta sasa wamehamisha nguvu kwa McGahn, sijui baada ya McGahn atafuata nani? Maana Dems walituambia Mueller ndiye alikuwa "mtu wa muhimu sana" na kwamba Trump na AG Barr walikuwa wakimzuia kuhojiwa Congress. Hata huko mahakamani Dems wanafikiri wanahujumiwa! Mara wanamtaka Jaji huyu, mara Jaji huyu hawamtaki, ili mradi wapate wanachokitaka.

Nawaza tu kwa sauti haya maamuzi yakipelekwa Supreme Court, sijui Dems watampanga Justice gani kule?
Hayo ni baadhi ya yaliyojiri yakiacha swali, je, kuna sababu za impeachment?
Katika mazingira ya kawaida jibu ni ndiyo! Uchunguzi ungeachwa hadharani na AG Barr uchafu mwingi ungetosha. Kama mashahidi wangeatikana kwa urahisi ingalikuwa dhahma. Kwasasa jibu la ndiyo lina tatizo na hilo ndilo linawasumbua Democrats

Mueller aliulizwa na Dems na Republicans kuhusu "impeachment", vikiwemo vile visententensi tulivyoambiwa humu kuwa tafsiri zake ni "Congress waamue" au "impeachement", lakini alikataa kuzielezea au kutoa mapendekezo hayo. Juhudu za akina Rep. Veronica Escobar (D-TX) ziligonga mwamba.

Again, AG Barr analaumiwa kwa ku-hide grand jury materials (among others) na watu ambao hawajasoma Fed. Rules of Criminal Procedures 6(e).

Tatizo la Dems sio mashahidi, tatizo ni kwamba kesi haina nguvu dhidi ya wanaemchukia a.k.a Trump. Wasingekuwa wanadunduliza na kutumia nguvu nyingi kushawishi watu kuwa Trump ametenda kosa.
Karata kubwa ipo katika Senate!

Kwenye Senate hamna "karata" yoyote huko labda kama hamuwasikilizi Republicans. Ni 'far-fetched' hata kuwaza kuwa Republicans walio Senate watadandia treni ya 'impeachment' ya Dems!!
 
Unajua kwa nini Mueller hakum-indict Trump? Unajua sababu ya Burr kupingana na uamuzi huo wa Mueller? Je ni kweli Mueller alimpata Trump na hatia lakini akasita kuchukua hatua sahihi? Kwa ufahamisho tu ni kwamba proceedings tayari zimeanzishwa na chombo husika kuhusu mkanganyiko huo.
Mkuu, haya maswali yako Mueller alishayajibu kwenye testimony yake. Baadhi ya waliomuuliza ni Rep. Ted Lieu (D-CA), Veronica Escobar (D-TX) na Mike Johnson (R-LA).

Nikukumbushe tu, Mueller alisema hakupendekeza impeachment, hajasema impeachment ni sahihi au lah! na sio kweli kwamba hakum-indict Trump kwa sababu ya maoni ya OLC, kama ulivyotaka aseme.
Naona tunakubaliana kwamba Mueller yawezekana aliboronga kwa kutomtia hatiani Trump kwa kisingizio cha a sitting President cannot be indicted...sababu iliyopingwa na AG Burr. Kwa ufahamisho zaidi ni kwamba matayarisho ya awali ya impeachment tayari yameanza na Mueller anategemewa kuwa shahidi.

AG Barr alisham-clear Trump na Obstruction of Justice.

Hayo matayarisho unayozungumzia hayajaanza leo, yalianza hata kabla Trump hajaapishwa kuwa Rais. We subiri maamuzi ya mahakama ambapo Dems wanampanga Jaji fulani ndio aamue.

Mueller alishasema hawakuamua kuhusu mashtaka.

"We did not reach a determination as to whether the president committed a crime,"
 
VIUNGANI DC

Katika bandiko# 968 tulimalizia kwa kusema jibu la ndiyo kwa impeachment lipo, lakini karata kubwa ipo kwa senate. Hapa kuna namna mbili, ni lazima impeachment ipate ridhaa ya House ambayo Democrats ni majority na Senate ambayo GOP ni wengi

Lakini article of impeachment si jambo linalopigiwa kura kirahisi

Ndani ya House Dems wana wingi na huko suala litapita hata bila kuungwa mkono na GOP
House inahitaji kura 218 ambazo ni chache kwa Dems wenye takribani kura 237

House ndiyo itaandika article of impeachment na kuipeleka kesi mbele ya seneti

Ndani ya Senate lazima ipatikane 2/3 ambayo kwa hesabu ya sasa ni takribani maseneta 67
Kumbuka GOP ni 53 kwa 47 Dems kwa wakati huu

Kwa maneno mengine lazima wapatikane Republicans takribani 20 wa kuunga mkono hoja

Republicans iliyopo ni ya Trump ndiyo maana huuita ''Trump-ism''
Uwezekano wa kupata maseneta hao ni hakuna

Hili si kwasababu hakuna hoja, ni kwasababu Republicans wanamhofia sana Trump
Hakuna mwenye uhakika 20 itatoka.
Ikitokea ikapelea basi GOP waliopiga kura dhidi yake watakuwa matatani kupoteza nafasi zao.

Kwavile article of impeachment itaandikwa na House ni lazima kuwa na kesi ya kutosha

Mwaka 1998 Bill Clinton alikumbana na impeachment chini ya House Speaker Gingrich
Impeachment ikaishia seneti na hivyo hakuondolewa madarakani

Ni kwa mtazamo huo kuna mgawanyiko ndani ya Dems. Wapo wanaotaka kuharakaisha machakato wa impeachment na wapo wanaotaka kujenga hoja ya impeachment

Spika Pelosi ni mmoja wa wanaotaka kujenga hoja na ndiyo maana wameenda mahakamani kulazimisha nyaraka zilizofichwa na AG Barr wazione na mashahidi waliozuiliwa kufika mbele ya kamati za Bunge kama McGhan waamriwe kufika.

Suala linalowasumbua Dems si article of impeachment, wana majority.
Ni matokeo ya impeachment ambayo ni dhahiri hayataweza kumuondoa Trump yakifika Senate

Wapo Dems wanaosema impeachment iwepo hataka kama haitakuwa na matokeo

Wapo wanaosema kosa hilo alifanya Ginrich ambapo uchaguzi uliofuata Dems waliongeza viti 5 ndani ya House licha ya kashfa. Popularity ya Clinton ikaongezeka

Lipo kundi la 3 la Dems wachache linaloamini njia ya kumuondoa Trump ni kupitia sanduku la kura kwa muda uliobaki na kwamba impeachment inaweza kumpa kauli kuwa hakuondolewa kwasababu hakuwa na kosa.

Hoja hiyo inachagiza hoja ya wanaotaka impeachment kuwa ni heri ashtakiwe ili asiwe na kauli ya kwamba hakuna kilichotokea .

Mchezo mkubwa ulichezwa na AG Barr, kwanza, kuchelewa kutoa taarifa na pili kuficha hoja nizto zinazoweza kuwafanya Republicans baadhi waangalie suala hilo kwa jicho la utaifa

Tusemezane
 
Mkuu Nguruvi3, umeeleza vizuri kwenye post#954, ila paragraph ya mwisho haijakaa sawasawa. AG Barr hakuficha "hoja nzito" au taarifa za grand jury au zingine kwa matakwa binafsi bali kwa matakwa ya kisheria na kikanuni.

Ndio maana Dems wapo mahakamani kuomba Jaji aondoe zuio la Barr. Imekuwa ni desturi mahakama kutoa amri ya kuwekwa wazi kwa taarifa za grand jury, kwakuwa taarifa hizo huwa generally haziwekwi wazi (ingawa kuna exemptions).
 
Naomba nikuulize maswali manne mepesi El Jefe...
  1. Je unadhani kama uchaguzi wa mwaka jana, ungehusisha Senators wote, GOP ingekuwa bado ina majority kwenye Senate?
  2. Je unadhani ni kwa nini Wamarekani waliwapa Democrats kura nyingi katika uchaguzi huo mpaka kuweza kuitwaa House?
  3. Je, pamoja na hali ya uchumi kuwa nzuri kama unavyodai, kwa nini Wamarekani walio wengi waliwakataa wagombea wa GOP?
  4. Je unadhani hiyo inayoitwa base yake, ambayo hata afanye vituko gani wako naye, inapungua, inaongezeka au iko pale pale?
 
...Kwa vile article of impeachment itaandikwa na House ni lazima kuwa na kesi ya kutosha
Kesi ya kutosha ipo na preliminary deliberations zinaendelea. GOP imepigwa butwaa!
Wapo wanaotaka kuharakaisha machakato wa impeachment na wapo wanaotaka kujenga hoja ya impeachment
Huo mchakato ulishaanza kitambo na kila kitu kinaenda kilivyopangwa. Hii ropoka ropoka ya Trump si bure!
 
Naomba nikuulize maswali manne mepesi El Jefe...
[*]Je unadhani kama uchaguzi wa mwaka jana, ungehusisha Senators wote, GOP ingekuwa bado ina majority kwenye Senate

Uchaguzi ungehusisha Senators wote mwaka 2018, GOP wangepata zaidi ya Senators 60.

Obama alishinda Urais mwaka 2008, Dems wakatwaa Senate mwaka huo (D-57 vs R-41) - viti 34 kati ya viti 100 viligombewa. Dems wakatwaa pia House (D-257 vs R-178).

Miaka miwili baadae (2010) Dems wakapoteza House (D-193 vs R-242), sawa na kupoteza wawakilishi 64 huku Republicans wakiongeza wawakilishi 64. Ila mwaka huo Dems waliendelea kutwaa Senate (D-51 vs R-47) huku wakipoteza viti 6 na Republicans kuongeza viti 6 - viti 34 kati ya 100 viligombewa.

Tukilinganisha na Trump:

Trump alishinda Urais mwaka 2016, Republicans wakatwaa Senate (R-52 vD-46) - viti 34 kati ya 100 viligombewa. Republicans wakatwaa pia House (R-241 vs D-194).

Miaka miwili baadae (2018) Republicans wakapoteza House (R-199 vs D-235), sawa na kupoteza wawakilishi 42 huku Dems wakiongeza wawakilishi 41.Ila mwaka huo Republicans waliendelea kutwaa Senate (D-53 vs R-45) huku WAKIONGEZA viti *2 na Dems kupoteza viti *2 - viti 35 kati ya 100 viligombewa.

Kwahiyo, kwa miaka miwili chama D kilichopoteza wawakilishi 64 na kupoteza viti 6 vya Senate Vs chama R kilichopoteza wawakilishi 42 na kuongeza viti 2 vya Senate, unadhani ni chama kipi kingepoteza Senate kama uchaguzi wa mwaka 2010 na 2018 ungehusisha Senators wote?
[*]Je unadhani ni kwa nini Wamarekani waliwapa Democrats kura nyingi katika uchaguzi huo mpaka kuweza kuitwaa House?
Nitakujibu swali lako ila kwanza nijibu haya maswali yangu.

Obama alishinda Urais mwaka 2008 na Dems wakaendelea 'kutwaa' House mwaka huo, ila kuanzia 2010 hadi 2018 hawakuwa na House.

Je unadhani kwanini wamarekani waliwapa Republicans kura nyingi kwenye midterms za 2010, 2012, 2014 na 2016 na kuwawezesha kutwaa House kwa miaka hiyo yote minane (8)?

Kwanini Dems hakutwaa House kwa miaka sita (2010-2016) ya uongozi wa Obama?
[*]Je, pamoja na hali ya uchumi kuwa nzuri kama unavyodai, kwa nini Wamarekani walio wengi waliwakataa wagombea wa GOP?
Unaweza kusema wamarekani walio wengi waliwakataa wagombea wa GOP, ila kwa maoni yangu naona GOP wangejipanga vizuri kama Dems wangeendelea kuwa na House.

Republicans walipoteza viti 42 kwenye House ambazo ni chache ukilinganisha na viti 64 walizopoteza Dems mwaka 2010. Idadi yao kwa sasa kwenye House sasa ni 199.

Wawakilishi wengi wa GOP walikuwa wame-resign au ku-retire kuliko Dems (R-41 vs D-21). Hii ilipelekea Republicans kushikilia viti 28 tu na kupoteza 13 kati ya 41, huku Dems wakishikilia 18 na kupoteza 3 kati ya 21.

Wawakilishi wengi wa GOP (18) kati ya 30 waliokuwa wanagombea kuchaguliwa tena walipoteza kwenye blue States ambazo Dems waliwekeza sana kama California (viti 5), Colorado (1), Illinois (2), Minnesota (2), New Jersey (2), New York (3) na Virginia (3).

Kwahiyo Republicans wasingeachia ngazi wengi, pengine wasingepoteza hivyo viti 13. Pia wangekomaa zaidi kwenye States alizoshinda Trump pengine wasingepoteza viti 11 au 12 (30-18). Kwahiyo wangetwaa House, idadi yao ya wawakilishi ingekuwa 199+13+11= 223 ambayo ni zaidi ya 218.
[*]Je unadhani hiyo inayoitwa base yake, ambayo hata afanye vituko gani wako naye, inapungua, inaongezeka au iko pale pale?
Nikikwambia Trump anakubalika na wananchi wengi kuzidi hata kuliko mwanzo utakataa kwa sababu hutegemei kusikia hicho.

Obama alipoteza Urais 2008 na Dems wakatwaa House 2008 ila wakaupoteza 2010. Wakapoteza tena House 2012, mwaka wa uchaguzi wa Urais, ila Obama akashinda tena Urais 2012.

Obama alikuwa Rais wa kwanza tokea Franklin Roosevelt (mwaka 1944) kushinda uchaguzi wa awamu ya pili kwa Electoral votes na kura za jumla pungufu ukilinganisha na ushindi wa awamu ya kwanza.

Kumbe chama kinaweza kupoteza House, ila Rais akaendelea kushinda uchaguzi?

Wapo waliotuambia Trump hakuwa na namna ya kufika 270 (electoral votes), wakatuonesha tafiti zao zote zinazoonesha Trump anapoteza tu mda wake. Ila matokeo ya uchaguzi yakawaaumbua.

Ukitaka kujua kuwa base ya Trump inaongezeka au inapungua, fuatilia kampeni zake sasa hivi halafu linganisha na rallies zilizopita na rallies za Dems. Usisubiri maoni ya waliokuambia kuwa Trump hawezi kushinda hata iweje.
 
2. Mueller : Alithibitisha kuwa Russia iliingilia uchaguzi na hadi sasa wanaendelea na kazi hiyo kwa nia ya kumsaidia Trump ashinde uchaguzi. Hii inathibitika kwa kauli ya Putin akiwa na Trump nchini Finland akisema ni kwe
li Russia ilitaka ashinde uchaguzi.
Mkuu na wewe uliinunua hii....!?
Hivi ulielewa sababu alizozitoa Putin kwa nini Russia ilikuwa inaona bora Trump ashinde kuliko H. Clinton?



Mkuu, Ebu msikilize vizuri tena Rais Putin kwenye clip hii ya hapa chini kuanzia dakika ya 27.
 
VIUNGANI DC
WIKI YA MAWENGE WENGE KWA RAIS TRUMP

Wiki hii ina mambo kadhaa yakionekana kumsumbua Rais Trump kichwani na kumtia mawenge.

Habari ya uchumi kuanza kudorora (recession) na masoko ya mitaji kupoteza pesa imechukua vichwa vya habari na kumtia Rais Trump kiwewe, kwamba, Uchumi unafia mikononi mwake!

Moja ya vitu anavyojivunia ni uchumi ambao umekua kwa kiasi kikubwa kwa kuangalia vigezo vingi kama consumer confidence, unemployment rate, GDP n.k.

Hivi ni vitu vilivyoanza kuimarika wakati wa Obama na namba za ajira za sasa hazina tofauti na za wakati wa Obama. Ni haki kusema Trump alirithi uchumi unaoimarika tofauti na Obama aliyerithi uchumi wa mdororo, na kwamba hakuna jipya kwa kuangalia takwimu.

Kuyumba kwa uchumi kunamtia hofu kubwa kwani hakuna kingine anachoweza kujivunia.
Hofu kubwa ni uchumi kudorora mikononi.

Mkutano wa G7
Huu nao haukuwa mzuri kwa washirika kumkalia kidete wakihoji kujitoa katika nuclear deal na vita yake ya uchumi na China inayoonekana kuchagiza mdodoro wa uchumi.

Kubwa zaidi ni kutaka 'kulipa' fadhila kwa Rais Putin kwa kumrudisha kundini (G7) jambo lililokutana na kizingiti kikali ukiacha nchi moja tu, Italy

Vita ya Uchumi
Huku akiweka tariff kwa bidhaa za China, Wachina nao wameweka ushuru kwa bidhaa za kilimo kutoka Marekani wakilenga maeneo ambayo Trump alishinda.

Wakulima wa vijijini ambako ni kambi yake wanaonekana kuchukizwa na vita hiyo na Uchina

FOX News
Kura za maoni zilizoendeshwa na TV ya Fox ambayo ni semeo la Trump imeonyesha Trump akiwa nyuma ya wagombea 3 wanaoongoza kutoka Democrats.

Habari hizi zimemfanya aanzishe Timbwili na Fox akisema '' they no longer with us''

Kwa tweet yake ya leo,Rais Trump haikutendea haki Fox, kwani ameonyesha dhahri shahiri hiyo ilikuwa TV yake ambayo sasa anaona inamgeuka, haitangazi propaganda tena

Kubadilika kwa Fox na kuwashirikisha Democrats kunakuja baada ya Dems kususia Fox kuendesha mijadala yao na hata wagombea kugomea mahojiano na TV hiyo.

Kibiashara inaonekana wazi Fox inatetereka na hivyo wameamua kujaribu kurudi katika mstari wa habari na si propaganda kwa Trump.

Lakini pia kuna kuchoka kunakotokana na kauli za kila mara za Trump ima za uongo, uzushi au zisizoendana na hadhi yake achilia mbali maadili ya ofisi kubwa katika anga hili la Wadudi.

Kimbunga cha Dorian
Kimbunga hicho kinavuma maeneo ya Puerto Rico na vingine vikatarajiwa Florida

Kilichojitokeza ni Trump kuchukua pesa za dharura za FEMA kuelekeza katika ujenzi wa ukuta.

Ukuta unamtia wazimu kwani ni moja ya ahadi zake.
Hata hivyo, suala hilo litachukua sura mpya ikiwa atafanikiwa kurepea kuta kwani kiasi hakiwezi kujenga kuta mpya.Hoja inayomwandama Trump ni kuwa je, Mexico wamelipia Ukuta?

Katika mfululizo wa mabandiko tulieleza wazi, hakuna namna Mexico italipia ukuta.
Baadhi yetu wageni wa siasa za viunga vya DC walisisitiza linawezekana.
Trump anawajibu sasa haliwezekani.

Vita ya Uchumi na China ina upande mwingine ambao Trump hajauona au hataki kuambiwa.

Kwamba, China haina vikwazo zaidi vya biashara ulikilinganisha na soko la Mrekani kwao.

Hata hivyo, China ina karata muhimu sana itakayomsumbua Trump wakiamua kuicheza.
Karata hiyo inaitwa North Korea.

Tusemezane
 
Back
Top Bottom