Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,399
- 31,352
- Thread starter
- #861
GOP inasimama badala ya maneno Grand old party ambayo ni RepublicansNaomba pia kuuliza maana ya neno "GOP"
Nimekuwa nikilisoma mara kwa mara kwenye siasa za marekani.
Ni jina la utani ambalo lilianzia na maneno gallant old party, nyumbani kwa wahafidhina(conservatives) hawa ukisikia neno right wing au bawa la kulia ndio wenyewe
Ukisikia left au bawa la kushoto ni Democrats
Conservatives ni watu wanaolinda thamani zao za asili wasiokubali mabadiliko kirahisi
Kwa Marekani wengi ni waumini au kwa jina lingine utawasikia 'evangelical''
Hao ndio wasiotaka kusikia abortion au ushoga at least kwa nyakati hizo za real GOP
GOP wanaamini katika fiscal conservatism na fiscal policy ambazo zinaundwa na vitu kama kodi , serikali ndogo , soko huria na uangalifu katika madeni n.k.
Lakini si hilo pia ni ''waumini' wazuri wa sera za ulinzi na ubabe
Hapo nyuma nimekueleza kuhusu iliyokuwa GOP kwa kuangalia zama hizo si hizi za Trump
Ni kwanini!
- Trump si conservative , huyu aliwahi kuwa Democrats na wala hajulikani anasimamia wapi
-Soko huria kwasasa siyo soko la maana iliyokusudiwa.
Kuna monopoly ndiyo maana unaona mtifuano kuhusu biashara.
Hapa kuna element za ubabe,nguvu ya Marekani haipo katika jeshi tu, ipo katika uchumi pia
-Abortion, haieleweki Rais Trump anasimamia wapi, leo anasema hili kesho anasema lile
- Ubabe ni kama unaouona sasa kwa mizengwe dhidi ya Iran
Orodha ni ndefu, inatosha kusema zile thamani na misingi ya GOP hazijulikani.
Kwa mfano, serikali ya sasa ina madeni makubwa kufika kiwango cha ''debt ceiling''
Kwa bahati mbaya wahafidhina waliomsumbua sana Rais Obama , sasa wamekaa kimya hata pale misingi na thamani za Republicans zikigeuzwa kulia kushoto na Trump
Republican iliyopo ni ile ya mfano wa GOP siyo hii Republican ya Trump
Arguably, kutokana na mabadiliko ya nyakati na jamii ''demographic' GOP wanapaswa pia kubadilika wakisimama katika misingi yao kwa kuzingatia hali ya wakati uliopo
Kwa mfano, siku za nyuma kidogo GOP walianza kujipenyeza katika ngome za Democrats kama vile watu wa rangi mbali mbali, kushirikisha akina mama na hata kufikiria namna ya umiliki wa silaha kutokana na matukio.
Walianza kushirikisha vijana na kuondoka katika zama za wazee weupe ili kuvuta kundi hilo
Republicans ya Trump haieleweki ipo wapi. Hili ndilo linawapa taabu sana kama ilivyokuwa katika chaguzi ya 2018 ambapo vijana wengi wa Dems waliwatupa nje wazee wa GOP
Sasa kama ni hivyo, swali linalokuja inakuwaje Trump ameshinda uchaguzi?
Kuna sababu nyingi sana ikiwemo uwepo wa wahafidhina wa vijijini ambao huwaelezi kitu
Hawa ni wale walioaminisha ''Mexico italipa gharama za ukuta'' wakashangilia kwa nguvu
Ukiangalia ramani ya uchaguzi utaona vijijini ni GOP na mijini ni Democrats
Kosa la Democrats hasa uchaguzi uliopita ni kutoingia vijijini wakijua mijini tu inatosha
Kosa la pili ni kujiamisha kuhusu majimbo. Kwa mfano, uchaguzi uliopita walipoteza Indiana au Michigan. Kumbuka uchaguzi wa Marekani siyo popular vote ni electoral college
Kwahiyo hesabu hufanyika si kushinda tu bali wapi pa kushinda
Pamoja na hayo,Russia ilichangia kubadilisha matokeo. Hakuna takwimu za wapi walifanikiwa kwa namba ingawa leo May 14 kuna taarifa za ''hacking' za Russia kule Florida
Kuathiri matokeo si kuiba kura, ni pamoja na kitu kinaitwa voters suppression kwamba kuna ushawishi kwa wapiga kura kutoshiriki kwa kulenga makundi kadhaa
Uchaguzi uliopita uliona hilo kwa upande wa Democrats ambapo wengi hawakupiga kura
Voters suppression ilionekana maeneo ambayo Republicans walikuwa na magavana kwa kufanya gerrymandering, kudai vitambulisho, ukazi na kuweka vituo mbali sana ili wapiga kura wasiweze kwenda hasa maeneo ya watu wa rangi
Huu ni mtazamo wa jumla na si lazima ushabihiane na maoni mengine
Tusemezane