Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

The meltdown, uh!? Mwanamke wa shoka Pelosi kakutana mwanaume kisiki-jiwe Trump. Pelosi "ka-retreat", kuna kila dalili za "ku-surrender"

trump meltdown.jpg
Meltdown? Well, a picture is worth a million words!
Trump akipewa vidonge vyake, je somo linaingia?
Pelosi, "The times, to honour our oath of office to protect and defend the constitution of the USA, have found us!"
 
VIUNGA VIKUU VYA DC
UKRAINE INABANA KULIA KUSHOTO
BARR AINGILIA KATI KUTOA NAFASI YA KUPUMUA

Wiki hii viungani DC mengi yameendelea. Kwanza ni taarifa iliyotolewa na state Department ikionyesha hakukuwa na tatizo la dhamira kuhusu email za HR Clinton

Taarifa imetolewa katika wakati Ukraine ikipamba moto ili kuzuia tahayari kwani suala hilo lilishikiwa bango na Rais Trump, na imedhihirika ni uzushi na uongo.

Dems wameendelea na uchunguzi wa awali wa Impeachment wakihoji watu kadhaa akiwemo balozi wa Marekani EU Bwana Gordon Sondland.

Huyu alihusika na 'text' na aliyekuwa mwanadiplomasia wa US nchini Ukraine Bw Bill Taylor

Wote waliitwa mbele ya kamati lakini ni bwana Taylor aliyetoa ushahuda wake akieleza wazi jinsi Rais Trump alivyotumia WH na pesa za msaada kumshinikiza Rais wa Ukraine Bw Zolensky kutoka hadharani na kutangaza uchunguzi wa Bw Biden kuhusiana na mwanae, na pia aeleze kuwa Ukraine iliingilia uchaguzi wa US kwa kuficha kanzi data za Democrats

Ushuhuda huo ulimaliza kabisa ubishi wa quid pro quo.
Republicans wakagawanyika na kumlazimisha Trump kuomba msaada wa kuungwa mkono.

Hoja ya Whistle Blower kutokuwa na first hand information ilikufa, hoja ya quid pro quo ikaaisha, na imethibitika Trump alifanya hivyo.

Hoja ikaundwa na Republicans kwamba hakukuwa na quid pro quo moja kwa moja ikiwa ni kukiri kuwa Trump alifanya madudu ya kutaka mpinzani wake achunguzwe.

Republicans wakaunda mbinu ya kushambulia mchakato, si wa wazi hata kama walishiriki.
Wanachotaka ni mahojiano ya dakika 5 kwa kila mjumbe ili watu wasijue kinachoendelea.

Wakazingira ofisi za Bunge, wengine wakiwa wajumbe wa kamati hizo zinazofanya uchunguzi

Kanuni za kutaka hata wachache (minority) waruhusiwe kuita watu kuhojiwa ilibadilishwa na Republicans mwaka 2015 na leo wanasema siyo ''fair play' hata kama walicheza rafu wakati huo

Taarifa zinasema kiongozi mwandamizi wa WH naye atakwenda kutoa ushuhuda akiunga mkono hoja za Bill Taylor.

Hili limepelekea kiwewe ndani ya kasri jeupe kwani kiongozi huyo ana first hand information na atakachosema huenda ikawa ndiyo tiketi ya impeachment

Unakumbuka tuliwahi kusema kuhusu John Bolton! Huyu naye akiitwa anaweza kumaliza Urais wa Trump. Bolton alikataa uchafu wa Ukraine akiuita ''bomu la mkono''

Impeachment haina maana itapita ndani ya seneti, bado Trump ana command kubwa sana kwa Republicans akiwatisha anavyotaka. GOP wamekuwa mbwiga, mbele ya Trump hawana kauli

Hayo yanaonekana kwa kumsikiliza Seneta Lindsey Graham ambaye kauli zake wakati wa Clinton Impeachment zinazagaa kuonyesha unafiki uliokirthiri. Afanyeje mbele ya DT?

Katika sakata la Ukraine, yule mwanasheria mashuhuri na Meya wa NY Rudy Guliani ambaye washirika wake wamekatwa naye yupo katika wakati mgumu. Trump alishamtupa chini ya Bus

Inafahamika Rudy Guliani alifanya kazi na wizara ya sheria (DOJ) na nyaraka zinaonyesha AG Bill Barr alikuwa mshiriki katika sakata la Ukraine. DOJ wamekiri kushirikiana na Rud Guliani

Baada ya mbinu zote za kuua issue ya Ukraine uonekana zimekwama, Barr akaja na jingine ili kuvuruga mwenendo mzima wa Impeachment process.

Barr anasema uchunguzi ule wa walioanzisha ''Russia Collusion'' unageuka uhalifu.

Kwamba, hata uchunguzi wa kubumba haujakamilika tayari unageuka kuwa uhalifu.
Hili analifanya ili kubadili mwenendo wa mazungumzo katika kumokoa Trump

AG Bill Barr aliyejijengea heshima amegeuka kituko, anakuwa kama ''toilet paper' ya Trump.

AG anafahamu hakuna kitakachofanywa na Trump kikaaminika tena na kwamba tume iliyoundwa kuchunguza original ya Russia collusion haisemwi hata katika TV za Fox

Yote yatafanyika, lakini kubwa ni kuwa Impeachment itatokea.

Hiyo haina maana kwamba Trump ataondolewa madarakani hasa kwa kuzingatia anavyowaogfya Republicans, bali ataingia katika historia

Hilo linamtia wazimu Trump akijua credibility yake hata kwa mazuzu wanaomfuata inaondoka.

Viungani kunachemka, uchaguzi una ''consequences''. Trump alipopoeteza midterm hajatulia.

Kamati za Dems zinamfanyia kazi kikamilifu. Mwanamana Pelosi anamwingia kichwani haswa

Viungani hali inazidi kubana

Tusemezane
 
VIUNGANI DC KUNACHEMKA
ALBAGHDAD NA IMPEACHMENT

Yule kiongozi wa ISIS Bw Baghdad ameuawa katika shambulio la majeshi ya Marekani
Baghdad aliyeongoza ISIS kwa vitisho amekutwa na mauti kwa ''kuchomewa' utambi na mshirika
Kazi ya kumpata Baghdad aliyenusurika mara kadhaa ilikuwa na mkono wa serikali ya Iraq

Rais Trump aliuambia umma kuhusu kuuawa kwa Baghdad siku ya Jumapili saa 3.20 asubuhi.
Hiyo ilikuwa ni zaidi ya masaa 10 tangu kuuawa kwa Baghdad.
Muda wa masaa 10 kupita na ule wa kutangaza habari saa 3.20 ulikuwa makusudi kabisa

Siasa za viunga vikuu vya DC zinahitaji mambo mengi, muda ukizingatiwa.
Jumapili asubuhi ni wakati wa habari zinazohusu nchi kwa wiki nzima na hupendwa na wanasiasa iwe kupeleka ujumbe , kujitetea au kutetea hoja.

Kwa Rais Trump Jumapili ililenga kufunika habari zinazomhusu kuhusu watu kadhaa wanaotarajiwa kutoa ushuhuda''testimony'' mbele ya kamati za Bunge.

Ni kuua habari nzito za Bw William Taylor aliyeeleza mengi kuhusu Ukraine

Baada ya habari kutobeba uzito alioutarajia, Rais Trump akachomeka hoja za kumlinganisha Osama na Baghdad huku akimnanga Rais Obama.

Ni Trumo huyo huyo aliyewahi kusema Obama hakupaswa kuchukua credit kwa kumuua OBL, ingawa leo anataka credit za Baghdad

Kwa wajuvi, hii ilikuwa mbinu ya kuendeleza mjadala wa Baghdad ili kuua habari za Ukraine.
Katika kuvuruga habari, Trump hakuwafahamisha viongozi wa Democrats wa Bunge akiwemo Spika Pelosi na Chuck Schumer.

Hawa wanaunda kundi linaloitwa ''Gang of 8'' lenye Republicans 4 na Dems 4 ambao hupewa siri za juu za nchi. Trump akawapiga chini

Leo kuna habari kuwa Bunge la Marekani(House) litapiga kura kuhusu Impeachment ya Trump.
Hili linaashiria kuanza mchakato wa kumshtaki huku mashahidi wakiendelea kuitwa na kuwa mwiba kwa Trump.

Mwambata wa Kijeshi atafika leo mbele ya kamati huku ikisemwa alikuwa shuhuda mzuri wakati wa simu kati ya Trump na Zolensky wa Ukraine

Wakati huo huo kuna maongezi ya kumwita John Bolton, mshauri wa ulinzi aliyetimuliwa na Trump kwa fedheha. Bolton ni mtu asiyetabirika hivyo ushuhuda wake unaweza elekea popote.

Wiki hii ambayo Trump alipaswa kusherehekea ushindi wa kuua gaidi kubuhu inageuka kuwa shubiri. Akiwa katika uwanja wa baseball, Trump alikutana na zomea zome, mashabiki wakipiga mayowee ''lock him up'' kuakisi msemo wake kwa Hillary Clinton ''lock her up''

Republicans walitaka mchakato wa impeachment uanzishwe, haijulikani hoja yao itakuwa ipi.

WH ilisema itatoa nyaraka mchakato wa impeachment ukianza, sasa hoja itakuwa wapi?

Kama kuna mtu anayejua kumwingia Trump '' under the skin'' ni mwanamama Pelosi

Pelosi anajua kuchanga karata zake, anajua ''fair play'' lakini pia hachelei kukata buti hata kama yupo 18 za eneo lako.

Tusemezane
 
Pelosi anajua kuchanga karata zake, anajua ''fair play'' lakini pia hachelei kukata buti hata kama yupo 18 za eneo lako.
Malalamiko haya hapa chini si mazuri kwa mama huyu. Wamarekani wote wanaona.
 
DC HAMKANI SI SHWARI
MCHAKATO WA ''IMPEACHMENT' SASA RASMI

Kwa kumbu kumbu tu suala la Ukraine lilivyoanza na Whistle blower na Inspector general wa national intelligence tulisema hali ni mbaya kwa picha ya suala zima

Ilionekana wazi kulikuwa na jitihada za kuitumia DOJ chini ya Bill Barr kuficha jambo zito.

Mwenyekiti wa kamati ya intelejensia bwa Adam Schiff alipolianzisha kulikuwa na taarifa kamili

Haikuwa kawaida taarifa ya Inspector general kufichwa isifike bungeni.

Baada ya taarifa ya Schiff , White House wakaachia pesa za Ukraine mara moja.

Kukawa na jitihada za kuficha hotuba za Rais Trump kwa kisingizio cha kutovuja siri

WH na Trump wakacheza karata nzuri sana ya kutoa ''transcript'' hadharani, kitu kisicho cha kawaida . Hili lilifanyika makusudi na leo tunajua ni kwanini

Zikawepo jitihada za kuzuia watu kutofika mbele ya kamati au kutoa nyaraka kwa kitu kinachoelezwa hakina tatizo. Hapa kukawa na doubt kuna jambo linafichwa.

Well, mashahidi wameitwa na kuthibtisha yale ya whistle blower kwa nukta na kina

Mashahidi hao wameeleza kila kitu kiasi cha Republicans kukosa mahali pa kushika

Wakahamia katika mchakato wa wazi kwa matumaini kuwa mahojiano ya hadharani yatakuwa ya dakika 5 kwa kila mjumbe na hivyo kupitisha na kupoteza muda suala zima lifilie mbali

Spika Pelosi akawajibu kuwa ile kura ya kuanzishwa mchakato itakuwa leo kama walivyoomba.

Kura mepigwa na sasa mchakato unaanza rasmi wa kumshtaki ''impeach'' Trump

Democrats wanasema mchakato mzima utakuwa hadharani kama walivyoomba Republicans.

Hapa kuna karata, kwamba, tayari kuna kila mahojiano na mashahidi wataulizwa point kwa point

Republicans wanaonekana kutokubaliana na hilo, wanataka kurudi mafichoni waliokolaumu

Kikubwa sana kichoonekana haraka ni suala la ''cover up'.

Ile transcript ambayo Trump ameipigia upatu sana hadi kutia shaka imebainika ''ni summary'' iliyonyofolewa baadhi ya maneno. Hili ni tatizo kweli kweli.

Mbele ya safari itaombwa ''original'' na ikitofautiana na ''transcript'' inayosemwa kama ilivyo na si memo basi kutakuwa na cover up

Kwa hali inavyokwenda haionekani kama Republicans watabadili msimamo kwa jinsi wanavyo ogofywa na Trump. Wamegeuka kuwa cowards kiasi kwamba hata wakiulizwa hawana jibu.

Trump kawaita maseneta kuwashawishi chonde chonde kesi ikifika mbele tafadhalini sana

Wasi wasi wa Trump una ukweli ndani yake.

Kila siku kuna jipya linakuja. Leo inafahamika hotuba zilifichwa baada ya kujulikana wapo watu waliofikisha malalamiko na WH walijua hilo ni tatizo.

Tunajua kuna ''memo'' na si transcript kama ilivyodaiwa huku ikiwa imenyofolewa.

Suala la Russian collusion lilizimwa na AG Barr kwa kuficha ukweli ambao leo Jaji mmoja ametoa hukumu ya nyaraka kupatika. Of course kuna appeal ili kupitisha muda

Republicans wamekubali kuna tatizo, hoja yao ya sasa ni kuliacha suala hilo uchaguzi uamue.

Tunajua US imegawanyika, wafuasi wa Trump watabaki kama walivyo na wa Dems pia

Hata seneti ikikataa kwa wingi wa Republicans, damage kwa independents itakuwa kubwa

Lakini pia Marekani ina namna zake, katika mchakato ushahidi unaweza kubadili mwenendo

Kama tulivyowaambia siku za nyuma ''hesabu ya mayai ya seneti si tatizo, imetimia''
Tatizo ni wabeba vikapu vya mayai kama Lt Colonel Vindman na Bill Taylor

Trump anakuwa Rais wa tatu kuwa impeached, Nixon alijiuzulu kabla.

Tusemezane
 
VIUNGA VYA DC VINACHEMKA
IMPEACHMENT SASA NI KWELI. KILA MTU ANABEBA MZIGO WAKE

Inafuata
 
DC INACHEMKA
IMPEACHMENT INACHUKUA SURA MPYA KILA UCHAO

Habari hii ni mwendelezo wa mabandiko #985 na kuendelea likihusisha sakata la Ukraine
Kwa marejeo sakata hili linaonekana kuwa zito kila uchao kwani mbinu ya kufukia ni ngumu

Kinachoendelea kwa wiki kadhaa ni ''udadisi' kuhusu tuhuma zinazomakabili Rais Trump
Tuhuma za kuzuia pesa takribani milioni 50 kwa ukraine hadi VP Biden na Hunter wachunguzwe

Udadisi ulikuwa nyuma ya pazia kwa kuchelea habari za kintelejensi zisitolewe moja kwa moja
Pia ilikuwa ni mbinu ya intelligence committee kuhakikisha hakuna mawasiliano ya mashuhuda.

Kama mtakumbu Republicans walilalamika mchakato huo kutokuwa hadharani ingawa ni jambo la kawaida. Kwasasa mashuda wanaitwa hadharani jambo linalowakwaza sana Republicans

Huko nyuma tulisema wapo watu muhimu watakaozua balaa la kutajana.
Tuliwataja kama Rudy Giullian, balozi Yonavovitch na Balozi Sondland

Giullian ametajwa na kila shuhuda na hakuna shaka kama mhusika mkuu.

Balozi Sondlan ambaye kimamlaka ni wa EU naye amekuwa kiungo kizuri.
Tatizo la Sondland ni kutoa ushuhuda wa ''uongo'' huku akijirudi kila siku

Sondland ametajwa na ushahidi wa simu zake na Rais Trump mgahawani umewekwa wazi.

Watumishi wote wa state Dept wanahojiwa wanamhusisha na sakata zima.
Imefika mahali suala zima sasa limetua katika meza ya mashauri ''resolute desk'' ya WH

Pamoja na mashahidi muhimu kama John Bolton (Rejea #985 na Chief of staff Maulveny kukataa kutoa ushahidi) wapo wanaojitokeza kwa hiari yao hasa watumishi wa State dept

Kila siku kumekuwa na jipya kiasi kwamba watetezi wa Republican wanakaukiwa hoja

Walisema habari ni za uzushi kutoka kwa whistle blower, sasa zimethibitishwa na kila mtu
Wakataka whistle blower aitwe kutoa ushahidi, wajuvi wakaonya Trump itabidi aitwe pia
Wakasema ni second hand information, well, leo kuna wenye first hand information
Wakasema mchakato ni wa siri, leo umewekwa hadharani wanataka urudi kuwa siri
Wakasema hakuna nipe nikupe ''wuid pro quo'' ushahidi unasheni na kwenda mbali zaidi.

Katika kutafuta unyasi wa kushika kujibusuru na kumnusuru Trump na kadhia, wanasema vyovyote iwavyo pesa zilitoka. Hapa hawana majibu kwanini zilizuiwa

Kwa mwendo wa chururu churu za kila siku, kuna sababu mkazi wa 1600 Penn a kuweweseka.

Inaonekana hakuna mwisho wa habari, ikichuja moja inaingia nyingine.
Hilo linafanya kasri jeupe la WH kuingiwa na mawaaa kila mawio na machweo.

Hakuna ajuaye nini kesho italeta, kinachojulikana ni wazi ''article of impeachment' itaandikwa. Ushahidi unazidi soni ya kufumbia macho suala zima

Kinachowasumbua Wamarekani ni jinsi Rais Trump anavyogeuka kuwa mbwiga kama si kunyongea linapokuja suala lolote linalomhusisha na Russia. Hili la Ukraine nalo ni mojawapo

Kama tulivyowahi kunene, kinga ya seneti kumuondoa anayo.
Wala hilo halijawahi kuwa tatizo

Tatizo ni hawa wanotajana. Balozi Sondland amezingirwa kulia kushoto , hana jinsi.
Ameitwa mbele ya kamati! ni ima amwage ugali wao wamwage mboga au afe na tai shingoni.

Kwa kihoro alichoonyesha wiki iliyopita kwa kuiangukia kamati na habari za kumhusisha Trump na quid pro quo, lipo tatizo atakalozua . Ni kubwa

Kama kuna mtu anayemtia wazimu Rais Trump na ambaye anaweza kubadili maono ya seneti ni bwana Sondland. Huyu bwana anafahamu Ukraine deal kuliko mtu mwingine

Republicans wanamkana wakisema anadanganya kamati kwa taarifa zinazongezeka na hiyo alipe gharama ya udanganyifu ambayo ni kifungo! Democrats wamemzunguka na mashahidi

Ingawa wengi hawamjui Sondlan kikamilifu, Rais Trump anajuta kumjua.
Sondlan ameshika baadhi ya makomeo ya kasri jeupe mtaa 1600 Penn!

Tutaendelea kuhabarisha katika nyakati za kawaida kama ilivyo ada.

Tusemezane
 
Ingawa wengi hawamjui Sondland kikamilifu, Rais Trump anajuta kumjua.Sondland ameshika baadhi ya makomeo ya kasri jeupe mtaa 1600 Penn!
Mashahidi wameendelea kufika mbele ya kamati ya Bunge

Kwa marejeo, tulisema Balozi Gordon Sondland atakuwa tatizo, na hadi leo amekuwa tatizo
Gordon ameeleza mengi akimhusisha Rais Trump, SoS Pompeo, WH Maulveny na Guillian.

Kwanini ushahidi wake umekuwa mzito?
Kwanza, Gordon alikuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na Rais Trump.

Alikuwa na mawasiliano na viongozi wote akiwemo VP Pence
Yeye anasema ''kashfa ya Ukraine, kila mmoja alikuwa ndani ya ''loop'' '

Hii maana yake amevunja nguvu ya hoja moja ya Republicans kwamba ni habari za kusadikika na kwamba hakuna first hand information. Hoja hiyo imekufa kwa sasa.

Gordon Sondland ni mfanyabiashara aliyeteuliwa na Trump kuwa balozi wa US katika EU
Gordon alimchangia Trump milioni 1 dola katika kampeni na kupewa ubalozi kama ahsante

Ukraine ilipopamba moto Trump alikuwa na Gordon pamoja baada ya mahojiano ya awali na kamati ya Bunge ambako alionekana kumtetea Trump.

Trump akamsifia kama mtu mwema na anayeheshimika '' well respected man''

Huko nyuma tuliwaambia kuhusu watu watatu , Balozi Yonavovitch, Volker na Rudy Guilllian

Tulisema wingi huo unatosha kuingiza waliokuwemo na wasiokuwemo na hivyo kutajana.

Kutajana ndiko kulikomweka Balozi Gordon katika wakati mgumu kwani ushahidi wake wa awali aliomtetea Trump ulionekana kuwa na matatizo.

Ili kuepukakikombe cha kudanganya chini ya kiapo, Gordon akapeleka nyongeza ya anachokijua akimtuhumu Trump kufanya nipe ni kupe au quid pro quo.

Trump akamtosa chini ya basi kama kawaida yake, ndipo Gordon akaona hamkani si shwari tena na kwamba jela inamuandama, akaamu kueleza wazi nini kimetokea.

Gordon ni mfanyabiasha hana cha kupoteza kisiasa hana sababu za unyenyekevu kwa Trump.

Alibanwa kulia kushoto, kwamba, akiendelea na Trump ataenda jela,wakati Trump keshamtosa.

Mashahidi wengine nao wamevunja nguvu za Republicans.

Leo imejulikana Ukraine walijua uhusu kuzuiwa kwa msaada na Trump tangu mwezi wa saba, Republicans walisema Ukraine walijua mwezi wa 9 hakuna uwezekano wa quid pro quo.

Republicans wanabadili hoja. Sasa wanalalamika mashahidi kama Joe Biden na Hunter hawaitwi. Balozi Volker kavunja hoja hiyo kwa kusema hakuna kosa lolote analojua juu yao.

Utetezi wa Republicans kuna nyakati unaleta matatizo.
Hoja ya kwamba whistleblower aitwe, inapingika kisheria kuna kinga ya kisheria kuhusu hilo.

Muhimu ni kuwa ikiwa wanahitaji mashahidi kama whistleblower na Biden,itabidi waeleze kwanini Trump hataki Maulveny, Pompeo na Giullian kuja kutoa ushahidi?

Katika kuhangaika na utetezi, Republicans wanasema Trump ana haki ya kuzuia misaada.

Wasichokumbuka ni kuwa Rais Nixon alifanya hivyo na mwaka uliofuata ikatungwa sheria kuwa misaada inayoidhinishwa na Bunge Rais hawezi kuizuia. Hivyo kuizuia ni kukiuka sheria.

Pamoja na ushahidi wote Republicans wamesimama na Trump na wala haionekani kama yupo atakayebadili msimamo. Hata hivyo, impeachment itakuwepo, hoja itabaki seneti.

Kuna vitu vinamsaidia Trump. Kwanza, ni muda ambao Democrats wanataka suala lisiingiliane na uchaguzi na hivyo hawana subira ya mahakama kuamua ikiwa wanaozuiliwa kutoa ushahidi na Trump wanalazimika kufika mbele ya Bunge.

Pili, Trump amewakamata Republicans kiasi kwamba hata kwenye ukweli hufikiri hatma yao.

Rais Trump ni popular sana kwa GOP na base yake. Ingawa ameshindwa kufanikisha chaguzi mbili za mgavana, bado ana nguvu. Hivyo Republicans katika congress ni mbwiga

Tatu, Rais Trump haachi alama. Michael Cohen alisema huongea kwa ''code' hatoi maandishi, wala hawasiliani moja kwa moja.

Hapa Giullian ndiye alikuwa mpambe hivyo kuna utetezi kuwa wapi alitoa maagizo?
kwa maana hakuna 'tape wala maandishi''

Suala linalobaki ni moja, nani anajua kesho italeta nini?

Tusemezane
 
VIUNGANI DC, WIKI MBILI KUELEKEA ''IMPEACHMENT''
MKAKATI WA KUZIMA 'MAONGEZI' WATUMBUKIA NYONGO

Bandiko 11,011 tulimalizia kwa kusema ''nani anajua kesho italeta nini viungani DC''

Wiki mbili za mashahidi wa sakata la aUkraine zimekamailika.
Mshahidi wameeleza sintofahamu kuhusu kuzuiwa misaada.
Hawa ni pamoja na wana Usalama na Wanadiplomasia

Republicans walishindwa kujibu hoja na kuingiza hoja zisizohusiana na sakata zima.

GOP wanaelewa kilichofanyika hakikuwa sahihi lakini wafanye nini ndani ya mikono ya Rais Trump anayewatisha na kuwaogofya kama mbwiga kila uchao kuhusu hatma zao kisiasa?

Kilichokwamisha hitmisho la haraka la Urais wa Trump ni mbinu ya kuwakataza amashahidi muhimu kama Mulvaney wa WH, John Bolton na SOS Pompeo.

Hawa wametajwa kama chimbuko la kinachoitwa irregular channel ikiongozwa na Rudy Giullian

Jana account ya Tweeter ya John Bolton ''ilifunguliwa'' akiinyoshea kidole WH kuifungia kwake.

Bolton ni mshauri wa usalama aliyesema '' hataki kujihusisha na biashara ya madawa na kwamba hilo lilikuwa bomu la mkono itakalolipuka'' akimaanisha sakata la Ukraine

Rais Trump amemjibu kwa ustaarabu akikanusha WH kuhusika na Tweeter

Trump anaelewa Bolton akifika mbele ya kamati hali itakuwa tete kama si mbaya

Baada ya mahojiano WH wakapanga mbinu ya kuua maongezi yanayorindima viungani

Kwanza, mpambe Seneta Lindsey Graham akataka nyaraka kutoka State dept kuhusu namna Joe Biden alivyoshughulikia suala la Ukraine.

Inaeleweka hakuna, mbinu ni kuleta mshatuko na kubadili habari.

Ni mbinu ya kujenga hoja dhidi ya Biden na si kutetea kwanini Trump alizuai misaada.

Republicans walikuwa na house, senate na WH, nini kiliwashinda kuchunguza nayakati hizo.

Hii ni sawa na sakata la Benghaz ambalo GOP walishikia bango, wiki mbili zilizokwisha imebainika hakukuwa na tatizo kwa Hillary Clinton. Walimchezea rafu tu

Mbinu ya Pili, wakatoa kidokezo FBI walibadili baadhi ya nyaraka katika sakata la Russia.

Taarifa iliyopo, Inspector general amethibitisha FBI hawakuwa na kosa

Nyaraka za uchunguzi ni halali na kwamba makosa yaliyofanywa na viongozi wa chini hayaondoi au kubadili ukweli kuwa uchunguzi wa Russia ulikuwa halali

NI Pigo kwa Trump aliyetaraji taarifa ya Inspector general ingeonyesha FBI kumhujumu na hivyo kuwaendea kombo waliokuwa viongozi wa FBI na kumpa hoja kuwa Russia collusion ni hoax.

Ikumbukwe hoja ya Russia haijafa, mahakama ilitoa amri AG Barr atoe nyaraka zilizofichwa zinazoaminika zina mengi makubwa kwa Trump.

WH imekata rufaa mahakama za juu
Hivi kama Russia collusion ni hoax kwanini Trump anahangaika kuficha taarifa ya Mueller?

Leo imeelezwa na mwanasheria anayewatetea washirika wa Rudy Guillian kuwa ikiwa FBI watatoa kinga, mashahidi watafika mbele ya kamati kisheria na kueleza kuhusu Nunes

Nunes alikuwa kiongozi wa kamati ya intelejensia wakati GOP wakiwa na House.
Alikuwa mpambe aliyetoa ile ''memo'' ya uongo. Kibao kimebadilika sasa ni kiongozi wa minority

Wiki nzima alikuwa anawashambulia mashahidi kama kiongozi wa Republicans katika kamati

Sasa inajulikana kwamba naye pia alikwenda Vienna kukutana na washirika wa Ukraine kuhakikisha serikali ya Ukraine ili kumwandama Biden na Mwanae

Akiwa meza kuu alijifanya hajui kinachoendelea, kumbe ni mshirika katika sakata la Ukraine

Kibao kinamgeukia naye huenda akatakiwa kutoa ushahidi chini ya kiapo.

Ndiyo maana tunasema siasa za DC ni nzito. Kuna 'timing' na hakuna ajuaye kesho imebeba nini

Tusemezane
 
VIUNGA VYA DC
'IMPEACHMENT'', KILA UCHAO NA LAKE

Bandiko# 1011 tulisema '' nani anajua nini kesho italeta viungani DC''

Siasa za DC ni endelevu na kila uchao unakuja na jipya kama si kuendeleza lililopo

Wiki hii, mahakama ya DC imeamuru AG Barr atoe sehemu ya uchunguzi wa Mueller aliyokataa hata kuonwa na 'gang of eight'' la congress.

Inaaminika Barr alifanya hivyo kuficha uchafu dhidi ya Bosi wake Trump.
Kesi hiyoimechukua takribani miezi 7, kuanzia March 2019

WH na DOJ wamekata rufaa kuzuia sehemu ya taarifa isionwe, ibaki siri kati ya Barr na Mawakili wa Trump. Hii ina maana ya kurefu muda ili uchaguzi ukaribie na hivyo kuua hoja nzima.

Ikiwa hakuna cha kuficha kwanini AG Barr na Trump wamegoma kuitoa taarifa hiyo?
Kwanini wanahamgaika hadi supreme court kuizuia taarifa ya ''Russia collusion''

Wachunguzi wanasema laiti ingewekwa hadharani, ilikuwa ni impeachment na Republicans wasingekuwa na nguvu za kumtetea Trump

Wiki hii tena imeelezwa uwepo kwa emails miongoni mwa watumishi wa WH baada ya kugundua whistle blower kalianzisha.

Emails hizo zinaonyesha kuhaha ndani ya WH katika kutafuta sababu za kufunika kombe

Wiki imekuja na jingine, The post inaripoti kuwa Rais Trump alidokezwa kuhusu uwepo wa whistleblower na mawakili wake mwezi wa 8 na kumpigia simu balozi Gordon Sondland aseme hakuna 'quid pro quo'' hivyo amwambie rais wa Ukraine

Maneno ya quid pro quo ameyatumia mara nyingi na inaaminika ni kutokana na kauli za whistleblower kwa Inspector general wa Intelligence aliyopokea malalamiko.

Hili limehitimisha hoja za Republicans wakibaki na hoja moja, pesa zilizotolewa, hakuna shida.

Katika hali ningine inayoashiria ufa , Rais Trump anamkana Rudolph Giullian kumtuma Ukraine.

Mashahidi wote kuanzia Mulvaney wa WH, Pompeo(SoS), Balozi Sondland na wengine walisema, Giullian alitumwa na Rais Trump kushughulikia Ukraine nje ya mfumo Rasmi

Giullian kajibu akisema kama trump atamtosa '' throw under the bus'' yeye ana insurance.
Hapa alimaanisha anafahamu uchafu wa kutosha, ''mwaga mboga namwaga ugali''

Kauli hiyo imemtisha sana Trump na kujirudi akimkwepa Giullian kiaina.

Kumbuka, Trump alimtosa Michael Cohen kwa mtindo huo huo.

Anachofanya Trump ni kujinasua na 'wabaya'', ukiingia naye deal hakawii kukuacha njia panda

Katika watu wanaoshikilia Urais wake ni acting WH Chief of Staff Mulvaney, SoS Pompeo, na mashauri wa usalama John Bolton.

Hawa Trump amekataa wasohijiwe kwa namna yoyote ile kwani ni wahusika wakubwa wa Ukraine. Bolton alikataa mpango huo lakini aliufahamu vema, ni shahidi mzuri

Katika impeachment inquiry , kamati ya intelejensia chini ya Adam Schiff imemaliza kazi na kumkabidhi Nadler ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya House ya sheria kuendesha machakato

Katika kuhakikisha fairness, Rais Trump au mawakili wake wameitwa mbele ya kamati ili kuwahoji watakaoitwa kutoa ushahidi kabla ya andiko la impeachment.

WH inasemekana wamekataa wito, na sababu zi wazi ushahidi unatosha hivyo kwao jambo la muhimu ni kuvuta muda ili usogee karibu na uchaguzi

Baada ya andiko la impeachment(kama litakuwepo na inaonekana lipo) shauri litakwenda seneti kwa McConnel na Lindsey Graham, maseneta ambao ni wapambe wa kuaminika wa Trump.

Hapa ndipo suala zima la impeachment litakapofinyangwa na Wapambe hao

Graham ni mwenyekiti wa kamati ya seneti ya intelligence, McConnel ni senate majority leader.

Hawa wawili wana nguvu za kufifisha suala zima ima kwa kuficha ukweli, kuchagua nani ahojiwe au hata kuvuta muda kadri wanavyotaka.Ndio watakaoendesha shughuli ndani ya seneti

Impeachment inaweza kutokea kwa ushahidi uliopo ambao Republicans wameshindwa kujibu kwani kila siku kuna jipya. Ngome kubwa ya Trump ni seneti ambako majority ni Republicans

Hata hivyo, viungani vya DC kuna timing, lolote na chochote kinaweza kutokea muda wowote.

Yupo mwanasiasa wa Uingereza alisema '' siku moja katika maisha ya siasa ni sawa na mwaka mmoja'' na hakika siku moja ndani ya viunga vikuu vya DC imebeba mengi

Tusemezane
 
VIUNGA VYA DC
'IMPEACHMENT'', KILA UCHAO NA LAKE

Bandiko# 1011 tulisema '' nani anajua nini kesho italeta viungani DC''

Siasa za DC ni endelevu na kila uchao unakuja na jipya kama si kuendeleza lililopo

Wiki hii, mahakama ya DC imeamuru AG Barr atoe sehemu ya uchunguzi wa Mueller aliyokataa hata kuonwa na 'gang of eight'' la congress.

Inaaminika Barr alifanya hivyo kuficha uchafu dhidi ya Bosi wake Trump.
Kesi hiyoimechukua takribani miezi 7, kuanzia March 2019

WH na DOJ wamekata rufaa kuzuia sehemu ya taarifa isionwe, ibaki siri kati ya Barr na Mawakili wa Trump. Hii ina maana ya kurefu muda ili uchaguzi ukaribie na hivyo kuua hoja nzima.

Ikiwa hakuna cha kuficha kwanini AG Barr na Trump wamegoma kuitoa taarifa hiyo?
Kwanini wanahamgaika hadi supreme court kuizuia taarifa ya ''Russia collusion''

Wachunguzi wanasema laiti ingewekwa hadharani, ilikuwa ni impeachment na Republicans wasingekuwa na nguvu za kumtetea Trump

Wiki hii tena imeelezwa uwepo kwa emails miongoni mwa watumishi wa WH baada ya kugundua whistle blower kalianzisha.

Emails hizo zinaonyesha kuhaha ndani ya WH katika kutafuta sababu za kufunika kombe

Wiki imekuja na jingine, The post inaripoti kuwa Rais Trump alidokezwa kuhusu uwepo wa whistleblower na mawakili wake mwezi wa 8 na kumpigia simu balozi Gordon Sondland aseme hakuna 'quid pro quo'' hivyo amwambie rais wa Ukraine

Maneno ya quid pro quo ameyatumia mara nyingi na inaaminika ni kutokana na kauli za whistleblower kwa Inspector general wa Intelligence aliyopokea malalamiko.

Hili limehitimisha hoja za Republicans wakibaki na hoja moja, pesa zilizotolewa, hakuna shida.

Katika hali ningine inayoashiria ufa , Rais Trump anamkana Rudolph Giullian kumtuma Ukraine.

Mashahidi wote kuanzia Mulvaney wa WH, Pompeo(SoS), Balozi Sondland na wengine walisema, Giullian alitumwa na Rais Trump kushughulikia Ukraine nje ya mfumo Rasmi

Giullian kajibu akisema kama trump atamtosa '' throw under the bus'' yeye ana insurance.
Hapa alimaanisha anafahamu uchafu wa kutosha, ''mwaga mboga namwaga ugali''

Kauli hiyo imemtisha sana Trump na kujirudi akimkwepa Giullian kiaina.

Kumbuka, Trump alimtosa Michael Cohen kwa mtindo huo huo.

Anachofanya Trump ni kujinasua na 'wabaya'', ukiingia naye deal hakawii kukuacha njia panda

Katika watu wanaoshikilia Urais wake ni acting WH Chief of Staff Mulvaney, SoS Pompeo, na mashauri wa usalama John Bolton.

Hawa Trump amekataa wasohijiwe kwa namna yoyote ile kwani ni wahusika wakubwa wa Ukraine. Bolton alikataa mpango huo lakini aliufahamu vema, ni shahidi mzuri

Katika impeachment inquiry , kamati ya intelejensia chini ya Adam Schiff imemaliza kazi na kumkabidhi Nadler ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya House ya sheria kuendesha machakato

Katika kuhakikisha fairness, Rais Trump au mawakili wake wameitwa mbele ya kamati ili kuwahoji watakaoitwa kutoa ushahidi kabla ya andiko la impeachment.

WH inasemekana wamekataa wito, na sababu zi wazi ushahidi unatosha hivyo kwao jambo la muhimu ni kuvuta muda ili usogee karibu na uchaguzi

Baada ya andiko la impeachment(kama litakuwepo na inaonekana lipo) shauri litakwenda seneti kwa McConnel na Lindsey Graham, maseneta ambao ni wapambe wa kuaminika wa Trump.

Hapa ndipo suala zima la impeachment litakapofinyangwa na Wapambe hao

Graham ni mwenyekiti wa kamati ya seneti ya intelligence, McConnel ni senate majority leader.

Hawa wawili wana nguvu za kufifisha suala zima ima kwa kuficha ukweli, kuchagua nani ahojiwe au hata kuvuta muda kadri wanavyotaka.Ndio watakaoendesha shughuli ndani ya seneti

Impeachment inaweza kutokea kwa ushahidi uliopo ambao Republicans wameshindwa kujibu kwani kila siku kuna jipya. Ngome kubwa ya Trump ni seneti ambako majority ni Republicans

Hata hivyo, viungani vya DC kuna timing, lolote na chochote kinaweza kutokea muda wowote.

Yupo mwanasiasa wa Uingereza alisema '' siku moja katika maisha ya siasa ni sawa na mwaka mmoja'' na hakika siku moja ndani ya viunga vikuu vya DC imebeba mengi

Tusemezane

Mkuu,
Kwa utaratibu wa Marekani, Rais hawezi kushtakiwa hata baada ya kuustaafu ikigundulika alifanya ufisadi, uhaini, au kakosa kama haya yanayomwandama Trump?
 
Mkuu,
Kwa utaratibu wa Marekani, Rais hawezi kushtakiwa hata baada ya kuustaafu ikigundulika alifanya ufisadi, uhaini, au kakosa kama haya yanayomwandama Trump?
Mkuu kuna mambo yanayotokea ambayo huko nyuma ima hayakuangaliwa, au yaliangaliwa ''for granted'' kwa kuangalia ukubwa wa ofisi n.k.

Katiba imetenga mihimili kwa uwazi, executive, Judicial and Legislative.(co equal branches of government). Kwa mantiki hiyo Rais anaondolewa madarakani kwa njia ya impeachment tu

Impeachment ni utaratibu mgumu sana, kwamba, House itaandika article of impeachment kama inavyotokea sasa hivi.

Halafu article itapelekwa mbele ya senate kwa mjadala.
Kama kutakuwa na mashtaka kutokana na mijadala ya senate, atakaye preside ni Chief Justice

Ipo katika katiba kwamba lazima kupatikane 2/3 ya wajumbe wa senate ambao ni 99 na VP ili kumuondoa Rais.

Hilo liliwezekana zama hizo si kwa nyakati hizi ambapo senate imepoteza ile nguvu yake (inherent powers) kama tunavyoshuhudia sasa hivi.

Katiba haisemi kama Rais anaweza kushtakiwa akiwa madarakani. Watalaam wanasema ingalikuwa haiwezekani basi walioandika katiba wangeweka kifungu cha'' immunity''

Kwa tafsri ya idara ya sheria imekubalika Rais akiwa madarakani hawezi kushtakiwa

Ieleweke kutoshtakiwa ''is not enshrined in the constitution '' ni legal opinion kutoka DOJ na OLC

Kitu kikiwa ''enshrine'' katika katiba hakiwezi kukwepeka, ni andiko lisilo na utata wa kisheria

Ni kwa msingi huo, Robert Mueller akifikisha uchunguzi wa Russia alisema katika kamati ya Bunge kwamba hawakuweza kumshtaki Rais Trump kutokana na ukweli kuwa Rais aliye madarakani hawezi kushtakiwa kama DOJ inavyosema

Alipoulizwa endapo anaweza kushtakiwa baada ya kumaliza muda wake, Mueller alisema ''Yes''

Swali hilo aliulizwa na Nadler mwenyekiti wa kamati ya sheria ya House kwa sasa

Baadhi ya wasomi wanasema kuna utata katiba haikusema hivyo kwahiyo ni suala lililobaki wazi

Wengi wa Wasomi wa sheria wanakubaliana na maoni ya Mueller kwamba anaweza kushtakiwa

Kitu kilichowazi ni kuwa Rais baada ya muda wake anaweza kushtakiwa kwa ''criminal'' kesi kwani muda huo anakuwa Raia na nguvu au kinga inakuwa haiopo.

Huo ndio msingi wa DOJ kusema Rais aliye madarakani hawezi kushtakiwa
 
VIUNGANI DC WIKI HII

MVUMO WA IMPEACHMENT NA MKUTANO WA NATO

Rais Trump yupo London kwa mkutano wa NATO.

Hali ya utangamano miongoni mwa wanachama ni tata kwa kuzingatia kauli za Trump huko nyuma kwamba NATO ni ''obsolete''

Rais wa Ufaransa wiki iliyopita alisema ''NATO imekufa kifo cha fikra'' akimaanisha brain death

Kauli hiyo imemwingia Trump ambaye sasa anadai Macron anaidhalilisha NATO ile ile aliyosema ni obsolete na kwamba ataitoa Marekani katika umoja huo

Kwakweli NATO imepoteza uongozi wa Marekani na viongozi wa Ulaya wakisema bila kificho

Mkutano unaendelea katika hali ya kubebana bebena , kwamba ndio hivyo tena! Ni Trump

Nyumbani katika viunga vya DC, hali nayo si nzuri.
Kamati ya intelejensia imekamilisha na kutoa taarifa yake kwa kamati ya sheria.

Leo kuna mjadala wa kitaaluma wa wanasheria kubaini uzito wa tuhuma dhidi ya Rais Trump

Taarifa ina mambo yale yale yaliyosemwa wakati wa mahojiano, hata hivyo, siasa za DC zina namna zake. Namba za simu za washirika wa Trump zimewekwa wazi bila kuonyesha maneno

Miongoni mwa simu hizo zipo za kiongozi wa Republicans ndani ya kamati ya intelejensia iliyokuwa inaendesha mahojiano, bwana Nunes.

Kwamba, alikuwa anahoji watu akijua nini kilichotokea kwa kuwa mshirika wa tuhuma hizo

Mwingine ni Rdolph Giullian Meya wa zamani NY na mwanasheria binafsi wa Rais Trump
VP Pence, Nick Mulvaney, Perry na Pompeo nao wapo katika namba zilizoorodheshwa

Namba zilipigwa kwa washirika, muda na tarehe unawiana na ushahidi wa waliohojiwa.

Bw Nunes anaelezwa kwenda Ulaya kukutana na wa-Ukraine kushinikiza uchunguzi wa Biden akiwa mwenyekiti wa kamati ya intelejensia kabla ya Republicans hawajapoteza House

Giullian na Washirika wake wa Ukraine wanachunguzwa, wapo kikaangoni FBI-SDNY

Namba za simu zimepatikana vipi? Well, kamati ya Bunge iliitisha kampuni za simu kisheria
Kwanini hazikuwekwa wazi mapema? Ni katika kuhakikisha ''wahusika wanajichanganya''

Kwasasa Republicans wametoa hoja zao kwamba simu ya Trump na Zolensky wa Ukraine hazikuwa na tatizo, na kwamba hakuna ushahidi wa kujitosheleza.

Hii ni baada ya hoja za quid pro quo kuisha, kwamba, Rais hakuhusika sasa kumalizwa, kwamba, siyo suala a impeachment sasa ushahidi unazidi kuwaelemea.

Kutoka kwa namba za simu kunatia kiwewe, ni wazi, maongezi ya simu hizo yapo pia

Jitihada za kuzuia mashahidi na nyaraka nazo zinagonga mwamba, kuna ushahidi mwingine

Kwa kutoa namba za simu na hofu ya maongezi kuwekwa wazi, SoS Pompeo, Rick Perry, Mulvaney, John Bolton, Rudy Giullian, VP Pence , kuna uwezekano mmoja akamwaga mboga.

Kunapokuwa na wimbi la watu, na kwa kumjua Trump anavyoweza kuwatosa hali si shwari ndani ya WH. Kabla ya hoja kwenda WH kuna mmoja anaweza ''kutosa'' jahazi

Ngome kubwa aliyo nayo Trump ni seneti, na kuzuia mashahidi na nyaraka.
Kama si Republicans walioamua tu kumkingia kifua, historia ingeshajirudia, Nixon part II

Tusemezane
 
Back
Top Bottom