Asante kwa kuuhamisha mjadala wa mada hii kutoka jukwaa la GT na kuuleta huku ktk Jukwaa la Siasa kwa sbb wengi wa members hawana privilege ya kuchangia huko kutokana na kutokidhi sifa za kuwa huko.
Binafsi nimpongeze Nguruvi3 mchambuzi na mwanzilishi wa mada hii pana ya kutazama awamu ya 5 ya uongozi ya serikali hii chini ya Rais John P.J. Magufuli na yanayojiri chini ya uongozi wake ktk serikali na nchi yetu.
Na ktk sakata la urushaji wa matangazo ya bunge live, kiukweli Nape amempotosha boss wake Rais na PM. Aidha amekipotosha hata na chama chake na hili litawagharimu sana tu, tena sio muda mrefu.
Hata watetezi wa hili nje na ndani ya mitandao ya kijamii wako kwenye wakati mgumu sana kuutetea upotoshaji huu kwa sababu vyovyote iwavyo vile kutetea uwongo ni kazi ngumu na hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuikubali kazi hii!!
Ni kweli kabisa, huyu Nape katengeneza tatizo mwenyewe na sasa anajaribu kila njia kulikimbia lakini imeshindikana, lipo tu nyuma hatua chache linamfuata kokote aendako!!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.