Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,406
- 31,387
SHERIA YA LESENI MIAKA 45
Kauli ya waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mh Isack Kamwelwe kuhusu umri wa madereva kuendesha malori na vyombo vya abiria imepamba habari za wiki hii
Ni kawaida ya Watanzania kuzungumzia jambo kwa jicho wanalotaka na si lile linaloona ukweli. Waziri Kamwelwe ana hoja ya msingi kabisa katika mjadala unaondelea
Kauli yake imekuja ikiwa imechelewa. Ongezeko la ajali nchini limekuwa tishio kwetu sote
Kila inapotokea ajali njia zinazotumika kuzuia au kupunguza ni za mkato na za kizamani kama ulivyo mfumo wetu wa kutoa leseni,kudhibiti, kusimamia bima na kutafuta chanzo na suluhu
Hoja ya waziri inaonekana kuwa na mapungufu kwa mtazamo wa haraka, lakini wazo analotoa ni muhimu sana katika kudhibiti na kukabiliana na wimbi la ajali nchini
Mitandaoni na kwingineko baadhi yetu hatuangalia kiini cha hoja, tunaangali mapungufu ya hoja. Ieleweke alichosema Mh Waziri si sheria ni kusudio la kupeleka mswada Bungeni
Kwa kuelewa hivyo , ni makosa kuanza kukosoa hoja zake kana kwamba miaka 45 ni sheria tayari au kdhani pendekezo la miaka 45 linatosha kuwa suluhu ya tatizo
Kama miaka 45 pekee ndicho kinachodhaniwa ni tatizo, hoja nzima inapoteza maana
Tatizo la ajali linachangiwa na 'factors' nyingi si umri pekee.
Katika kukabiliana na tatizo umri ni sehemu ya suluhu na si suluhu yenyewe
Ni kwa mtazamo huo, tunaona ipo haja ya kumsaidia Mh Waziri kuboresha hoja yake yenye mantiki na ya msingi sana kuliko kukimbilia kulaani, kumbeza na kudharau alichosema
Kwa uzito wa hoja hii tutakuwa na mabandiko kadhaa kwa lengo la kumsaidia waziri kuboresha hoja kwani tatizo la ajali linatugusa sote na sote tunawajibu wa kulitafutia jawabu
Sehemu ya kwanza inafuata