Duru: Waziri Kamwelwe asibezwe, ana hoja ya msingi, asaidiwe kuboresha

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
15,401
31,364
SHERIA YA LESENI MIAKA 45

Kauli ya waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mh Isack Kamwelwe kuhusu umri wa madereva kuendesha malori na vyombo vya abiria imepamba habari za wiki hii

Ni kawaida ya Watanzania kuzungumzia jambo kwa jicho wanalotaka na si lile linaloona ukweli. Waziri Kamwelwe ana hoja ya msingi kabisa katika mjadala unaondelea

Kauli yake imekuja ikiwa imechelewa. Ongezeko la ajali nchini limekuwa tishio kwetu sote

Kila inapotokea ajali njia zinazotumika kuzuia au kupunguza ni za mkato na za kizamani kama ulivyo mfumo wetu wa kutoa leseni,kudhibiti, kusimamia bima na kutafuta chanzo na suluhu

Hoja ya waziri inaonekana kuwa na mapungufu kwa mtazamo wa haraka, lakini wazo analotoa ni muhimu sana katika kudhibiti na kukabiliana na wimbi la ajali nchini

Mitandaoni na kwingineko baadhi yetu hatuangalia kiini cha hoja, tunaangali mapungufu ya hoja. Ieleweke alichosema Mh Waziri si sheria ni kusudio la kupeleka mswada Bungeni

Kwa kuelewa hivyo , ni makosa kuanza kukosoa hoja zake kana kwamba miaka 45 ni sheria tayari au kdhani pendekezo la miaka 45 linatosha kuwa suluhu ya tatizo

Kama miaka 45 pekee ndicho kinachodhaniwa ni tatizo, hoja nzima inapoteza maana

Tatizo la ajali linachangiwa na 'factors' nyingi si umri pekee.

Katika kukabiliana na tatizo umri ni sehemu ya suluhu na si suluhu yenyewe

Ni kwa mtazamo huo, tunaona ipo haja ya kumsaidia Mh Waziri kuboresha hoja yake yenye mantiki na ya msingi sana kuliko kukimbilia kulaani, kumbeza na kudharau alichosema

Kwa uzito wa hoja hii tutakuwa na mabandiko kadhaa kwa lengo la kumsaidia waziri kuboresha hoja kwani tatizo la ajali linatugusa sote na sote tunawajibu wa kulitafutia jawabu

Sehemu ya kwanza inafuata
 
Mh. WAZIRI KAMWELWE ASIBEZWE, ANA HOJA ASAIDIE KUIBORESHA

Sehemu ya I (Miaka 45)

Watanzania wanalalamika umri huo ni mkubwa na kwamba utabana ajira kwa watu wengi
Wanasema umri pekee unaweza kuwa chanzo cha ajali kwasababu hauwezi kuwa na uzoefu.

Wanamaanisha dereva mwenye miaka 45 au 50 aliyepata leseni jana hana uzoefu kumzidi kijana wa miaka 30 aliyendesha akiwa na umri wa miaka 20

Ni kweli umri pekee hauwezi kuchukua nafasi ya uzoefu(experience).
Uzoefu una umri tofauti na umri wa maisha ya mtu.Hata hivyo umri una nafasi katika uzoefu

Ukiwa na umri wa miaka 20 ukaendesha kwa miaka 10 utakuwa na uzoefu wa miaka 10 katika umri wa miaka 30. Hapa ni kuonyesha jinsi umri na uzoefu wa maisha vinavyoingiliana

Kwanini watu wadhani umri si kigezo ikiwa tuna sheria inayotamka umri wa mgombea Urais?

Umri wa maisha una vitu vingine visioonekana ikiwa ni pamoja na hekma na busara za maamuzi, kuwajibika kwa mhusika(responsibilities) na uzoefu unaotokana na kuona au kusikia n.k.

Pamoja na hoja iliyotangulia, umri unatumika katika kupima uzoefu na si umri wa kuishi.

Ndicho kinafanyika kwa wenzetu wenye vyombo vya vingi kutuzidi lakini ajali chache kuliko sisi

Ikiwa waziri anamaanisha umri pekee ni lazima tupitie vigezo vingine vitakavyosaidiana na umri ili umri anaosema ulete tija inayokusudiwa na si umri kwa maana ya namba

Mh Waziri anaposema miaka 45 pekee haitoshi, ni muhimu akatumia umri huo kama ''cut off point' akieleza mtiririko wa kufikia umri huo kuanzia mtu anapopata mafunzo na leseni, madaraja ya leseni na muda wa kukaa katika madaraja hao

Maana yake , miaka 45 ya kuishi lazima ieleze( define) uzoefu wa kuendesha hadi kuifikia

Mafunzo na madaraja ya leseni (inaendelea sehemu ya II)
 
Sehemu ya II (MFUMO ULIOZEEKA USIOELEWEKA)

Mfumo wa leseni nchini ni wa kizamani uliozeeka usioeleweka na sehemu ya tatizo la ajali
Mfumo wetu una madaraja ya leseni za pikipiki, magari madogo,ya kati na makubwa

Kwa wenzetu katika madaraja hayo kuna madaraja madogo(sub class) ndani yake

Kwa mfano leseni daraja I, II, III, VI, V katika magari tu. Katika kila daraja kuna muda wa kutumikia kabla ya kwenda daraja jingine, iwe mwaka, miwili au mitatu n.k.

Kila daraja lina sheria zake. Mfano, daraja la kwanza si ruhusa kuendesha bila kuwa na dereva mzoefu pembeni. Daraja la II linaruhusu kuendesha barabara za mitaani, Daraja la III linaruhusu kuingia highway na daraja la IV mtu anakuwa na leseni kamili, Daraja la V ni professional driver

Kwa utaratibu huo, mtu anayekwenda kwa kasi sana ataanza mafunzo na kufikia daraja la 5 mabalo linamruhusu kuendesha mabasi na malori at least akiwa na uzoefu wa miaka 10

1. Kwa Tanzania, waliofikia umri wa kupata leseni, mafunzo ya udereva yamekuwa kukanyaga breki , kuongeza mafuta na kuelekeza gari. Hakuna mfumo wa mafunzo kila mtu ni mkufunzi

Kwa nchi za wenzetu, kuendesha kuna kanuni za kisheria '' defensive driving' kwa maana ya kuokoa maisha yako, ya wenzako katika mazingira unayotumia kwa uchache wa kueleza

Katika hilo, mhusika anapewa muda wa kujifunza darasani na barabarani akiwa na wakufunzi wanaotambuliwa kisheria na si kila mmoja ni mkufunzi hata kama ni mume au mke

Leseni ya kuendesha haipatikani hadi muda wa mafunzo umekamilika na kuthibitishwa na leseni za madaraja zinazingatia muda wa uzoefu, mafunzo na rekodi siyo suala la kuhama daraja moja hadi jingine kwa kulipa ada tu

Tanzania mtu anajifunza Jumatatu, inayofuata, anaweza kuendesha chombo hata kilicho juu ya leseni yake. Hakuna mfumo mzuri wa mafunzo na utoaji wa leseni kwa kuzingatia madaraja

Ni kwasababu ya kutokuwa na madaraja na muda wa kukaa katika madaraja kupata uzoefu watu wanalalamika miaka 45 ni mingi mno. Si kweli, umri huo ukitengenezewa taratibu ni mchache lakini kama hali ni ya short cut ni umri mkubwa sana!!

Kwa nchi za wenzetu, leseni ni kitambulisho kamili kinachokutambulisha popote baada ya Passport. Ni kitambulisho chenye dhamana kwako na kwa wengine, kwamba, umeaniwa kwa maisha yako na wenzako

Huwezi kupewa Bus la abiria bila kuwa na mafunzo, rekodi nzuri ya nyuma na uzoefu wa kutosha. Kwasababu sisi hatuna rekodi, hili nalo ni tatizo

tatizo la rekodi(inaendelea)
 
Sehemu ya III(Rekodi)

Kwa dhamana ya leseni ya kuendesha, nchi za wenzetu zimeweka mfumo wa kumbukumbu. Kwamba, ukiwa Mwanza, Arusha au Mtwara rekodi inapatikana katika dakika moja

Katika zama za digital, inashangaza Tanzania hatuna mfumo wa kubaini nani kaendesha wapi, kafanya nini na kwa athari gani.

Matokeo yake mtu anasababisha ajali na kuua Mbeya, anakuja Dar anapewa ki Hiace anaua tena, anahamia Tanga anapewa Bus kubwa anaua tena n.k.

Kwa nchi za wenzetu, aina za ajali zinaadhabu zake katika leseni.
Inaweza kufungiwa miezi, mwaka, au miaka kutokana na kosa.

Hili linawafanya madereva wawe responsible kwani hawana mahali pa kukimbilia na kama hiyo ndiyo kazi huo ndio mwanzo wa matatizo

Utakuwa mwanzo wa matatizo Waajiri hawawezi kubeba dhama ya Bima kwa mtu hovyo. Hawawezi kulipa mamilioni kwa kuajiri mtu asiyejali Hili linatupeleka katika hoja nyingine BIMA

3.MFUMO HOVYO WA BIMA
Bima ni utaratibu wa malipo unatolewa na kampuni zinazochukua dhama za usafiri
Kwa wenzetu Bima inategemea mafunzo, aina ya leseni, uzoefu wa kuendesha, na rekodi

Mnaweza kuwa watu wawili katika Daraja III, mkalipa Bima tofauti.
Mmoja akipia 100,000 na mwingine 400,000. Mtu hovyo anatozwa zaidi ni ''risk ''

Kwa mantiki hii, waajiri ni waangalifu katika kuajiri ili wasilipe bima kubwa.

Kama una rekodi mbaya au huna uzoefu wa kuendesha vyombo vya abiria kupata kazi ni mtihani

Ukiyatazama hayo, ili uweze kuendesha Bus au Lori, umri wa miaka 45 utaona ni mchache sana

Tanzania, Bima ni 'flat rate'. Kijana aliyejifunza gari September 2018 analipa sawa na mtu mwenye uzoefu wa miaka 20. Inawezaekanaje hii?
Mtu mwenye miaka 50 analipa sawa na kijana wa miaka 20. Inawezakaje hii?

Tanzania, mtu aliyeua miaka mingi mfululizo analipa bima sawa na mwenye rekodi safi.

Hakuna mfumo wa kumbukumbu au uliounganishwa kujua nani anafanya nini?

Kutokana na sababu hiyo, waajiri wanatoa ajira kwa kijana wa miaka 25 kwasababu hakuna tofauti ya Bima na mzee wa miaka 50.

Muhimu, mfumo wa bima ni kama ''TRA''. Haubani wahusika katika kufidia majanga yanapotokea

Watanzania hawajui chombo walichopanda kina Bima na kwamba ikitokea tatizo wanapaswa kufidiwa iwe majeruhi au vifo.

Kama mfumo ungekuwa mzuri, waajiri wasingeajiri watu hovyo kwani 'ingekula kwao' na mashirika ya bima yangetoza waajiri zaidi kwa 'risk' za madereva.

Kubanana huko kungefanya kila mtu, dereva, mwajiri na Bima wawe responsible

Hili nalo linazua tatizo jingine la ufuatiliaji

Inaendelea....
 
Mkuu Nguruvi3

Umefanya analysis ya kina kuhusu factors kadhaa zinazosababisha ajali barabarani. Ni kupitia tafakuri za aina hii ndipo unaweza kuja na solution ya jinsi ya kukabiliana na ajali. Huwezi kutatua tatizo kubwa kama hili kwa njia ya mkato au kuangalia factor moja pekee halafu utegemee kwamba utaona matokeo chanya.

Kwa nini solution isijikite kwa mfano na haya mambo ya msingi;
i) mafunzo, utoaji na usimamizi wa leseni
ii) usimamizi wa sheria za usalama barabarani
iii) ubora wa barabara zetu
iv) usimamizi na ukaguzi ubora wa magari

Kuna research yoyote imewahi kufanyika kuonesha kwamba asilimia kubwa ya madereva wanaopata ajali ni wa umri wa chini ya miaka 45?

Kwa mfumo huu wa mafunzo na utoaji leseni ambao una mapungufu does it matter ikiwa mhitimu ana miaka 30 au 45?
 
Kuna research yoyote imewahi kufanyika kuonesha kwamba asilimia kubwa ya madereva wanaopata ajali ni wa umri wa chini ya miaka 45?

Kwa mfumo huu wa mafunzo na utoaji leseni ambao una mapungufu does it matter ikiwa mhitimu ana miaka 30 au 45?
Baada ya kusoma ya uzi uliohusu hoja ya waziri, kilichonijia kichwani ni kuendelea kusoma uzi huo ili nipate 'findings' zilizomsukuma waziri kuleta hoja hiyo. Kwenye uzi ule sikuona matokeo ya tafiti kuhusu hili. Nikadhani labda mleta mada ile 'amemuhujumu waziri' kwa kuleta habari nusu nusu.

Baada ya kuona uzi huu na kupitia haraka nikagundua yawezekana Waziri ameinyima uzito hoja yake kwa kutotafuta taarifa za kutosha juu ya tatizo hasa la ajali za barabarani hapa nchini. Hata hivyo nampongeza waziri kwa ku'provoke' mjadala huu uwenda tukabahatika kupata 'muarobani' wa kadhia hii. Mbinu hii ya ku'provoke' mjadala usaidia sana kuelekea kupata suluhu ya tatizo husika ingawa aliyeprovoke anaweza kudhihakiwa mwanzoni ama baadaye ama wakati wote kutoka na hoja aliyoleta. Tumeyaona kwa RC Makonda, alipo'provoke' vita dhidi madawa ya kulevya; baadhi walimbeza lakini 'provocation ya Makonda' imetupatia 'Tume' iliyochini ya Mh. Siang'a na wenzake. Bila provocation ile Tume tusigepata mpaka muda huu.

Kwa maelezo hayo hapo juu, naunga mkono hoja ya mleta mada ( Nguruvi3 ) kuwa Waziri asibezwe, asaidiwe kuboresha hoja yake. Twaweza kupata 'muarobani' wa ajali za barabari kutokana na 'provocation' ya Mh. Waziri Kamwelwe.
 
Baada ya kusoma ya uzi uliohusu hoja ya waziri, kilichonijia kichwani ni kuendelea kusoma uzi huo ili nipate 'findings' zilizomsukuma waziri kuleta hoja hiyo. Kwenye uzi ule sikuona matokeo ya tafiti kuhusu hili. Nikadhani labda mleta mada ile 'amemuhujumu waziri' kwa kuleta habari nusu nusu.

Baada ya kuona uzi huu na kupitia haraka nikagundua yawezekana Waziri ameinyima uzito hoja yake kwa kutotafuta taarifa za kutosha juu ya tatizo hasa la ajali za barabarani hapa nchini. Hata hivyo nampongeza waziri kwa ku'provoke' mjadala huu uwenda tukabahatika kupata 'muarobani' wa kadhia hii. Mbinu hii ya ku'provoke' mjadala usaidia sana kuelekea kupata suluhu ya tatizo husika ingawa aliyeprovoke anaweza kudhihakiwa mwanzoni ama baadaye ama wakati wote kutoka na hoja aliyoleta. Tumeyaona kwa RC Makonda, alipo'provoke' vita dhidi madawa ya kulevya; baadhi walimbeza lakini 'provocation ya Makonda' imetupatia 'Tume' iliyochini ya Mh. Siang'a na wenzake. Bila provocation ile Tume tusigepata mpaka muda huu.

Kwa maelezo hayo hapo juu, naunga mkono hoja ya mleta mada ( Nguruvi3 ) kuwa Waziri asibezwe, asaidiwe kuboresha hoja yake. Twaweza kupata 'muarobani' wa ajali za barabari kutokana na 'provocation' ya Mh. Waziri Kamwelwe.
Sina hakika kama hii mbinu ya "kuprovoke" ni muafaka sana na kwa upande mwingine inahalalisha "uholela" fulani hivi.

Umetoa mfano mzuri wa Makonda, sina hakika juu ya mafanikio yaliyopatikana kwenye vita ya madawa ya kulevya lakini sarakasi zilizuata za kutaja majina ya "watuhumiwa" hadharani huku wengi wao wasikutwe na makosa yoyote ndio "uholela" wenyewe ninaouzungumzia.

Mh waziri Kamwele kwa nafasi yake ana fursa ya kulichukulia suala hili kwa mapana yake na kiuweledi zaidi kuliko hii approach inayotaka kutumika sasa...
 
Sehemu ya IV

Mkuu Mwalimu kabla sijarejea hoja zako naomba nimalizie kutoka bandiko# 4

MFUMO WA REKODI
Huu si kwa ajili ya leseni tu, mfumo lazima uweze kuonyesha kitakwimu wapi kuna tatizo

Wataalamu wafanyie kazi eneo husika badala ya kuamini kuna CHUNUSI eneo fulani

Kwasehemu kubwa, kukosekana kwa takwimu kunachangiwa na mfuno pamoja na wanaotumia mfumo huo ambao ni askari wa usalama barabarani

Asakari wa usalama hukimbilia kupima eneo la ajali. Hatua ile ni kwa ajili ya kujenga kesi mahakamani na haielezi kwanini tukio limetokea. Kupima ni kutafuta ushahidi si chanzo

Askari wa usalama barabarani wanatakiwa wawe naufahamu wa masuala ya mwendo na vyombo husika. Hili si jambo gumu, technician wakisaidiwa na Eng wanaweza kuwa msaada

Haiwezekani kona fulani iwe na ajali kila siku bila kubainisha chanzo.
Pengine kona ni kali sana,mwinuko unaozuia uonekano,barabara au makazi ya wananchi n.k

Kinachoelezwa ni ni uchunguzi unaendelea, mwisho hakuna anyejua unatoa majibu gani.
Neno uchunguzi unaendelea ni kiashirio cha kushindwa kutafuta jawabu kwa kuahirisha mjadala

Kikosi cha usalama barabarani ni tatizo na kinahitaji wataalam na mafunzo si suala la kuhamisha askari wa FFU na kumvalisha magwanda meupe kama askari wa usalama

Kama ni rahisi kiasi hicho,Dr wa moyo anaweza kuwa mtaalam wa magonjwa ya akili siku moj!
Architect anaweza kuwa Mech Eng siku moja!Haiwezekani isipokuwa kwa Polisi tu! kwanini?

Tatizo la askari wa usalama linaonekana katika wiki ya usalama.
Ni wiki ya kukumbusha watumia vyombo kuhusu usalama wa vyombo vyao.

Ni wiki ya ukaguzi kwa mkazo kwani ukaguzi ni suala endelevu.

Kinachoshangaza, wiki hiyo hutumika kukusanya mapato na si ukaguzi wa magari

UDHAIFU WA ADHABU

Ni kawaida Bus kujaza kupita kiasi. Wanaofanya hivyo wanaelewa adhabu ni faini yanaisha

Kwa nchi za wenzetu adhabu ni faini na kufungia leseni ya usafirisjhaji kwa mmiliki ili apate machaungu. Ni kufungia leseni ya dereva ili apate machungu

Utaratibu huo hautazamwi hapa kwetu kwasababu lengo la askari limekuwa kukusanya mapato na si kusimamia sheria.

Tunasikia kila siku wiki moja milioni kadhaa zimekusanywa! hii si kazi ya Polisi, ni matokeo ya kazi zao lakini matokeo hayo lazima yawe na funzo na yazuie matatizo siku za baadaye

RUSHWA (Inaendelea....)
 
Sehemu ya V (Rushwa)

Hili ni eneo linalochagiza sana ajali.

Askari wa usalama barabarani wamepewa kazi ya kuandika na kukusanya faini za wakosaji.
Hii si kazi ya askari!

Wajibu wa askari ni kusimamia utii wa sheria. Leo kila askari ana kitabu cha kukusanya faini

Laiti kungekuwa na mfumo wa kisasa, faini ikiandikwa mhusika anapewa machaguo.
Kwanza, kwenda mahakamani kupinga au kukubali kosa na kulipia popote kwa njia yoyote

Malipo yafanywe popote kwa kutumia mfumo unaoonyesha rekodi kama amelipa au la

Tukiwa katika mfumo wa digital na mkongo wa Taifa, nini kinashindikana?
Ikiwa TRA wana mifumo ya mawasiliano nchi nzima kwanini Polisi wasitengenezewe?

Hili lingesaidia kuwapunguzia polisi kazi ya kukusanya 'kodi' ili wajikite katika kusimamia sheria.

Katika zama hizi ambazo watu wanatumiana pesa, wanalipa bill zao kwa digital, ni ujima uliokithiri kuona Polisi na kitabu akikusanya pesa. Kwao ni jambo 'zuri' kwa nchi ni aibu

Inaendelea....
 
Mkuu Nguruvi3

Umechambua kwa kina.

Swali linarudi kwamba; suluhisho la changamoto zote hizi kama ulivyozichambua ni kuwa na madereva wenye umri mkubwa? Ikiwa shule za udereva zina mapungufu kwenye mafunzo wanayotoa does it matter ikiwa mhitimu ana miaka 20, 30 au 45?

Tungeweza kwa mfano kufanya utafiti kwa kutumia data za ajali zinazokusanywa na jeshi la polisi usalama barabarani na tukaweza kupata takwimu za kutosha kwenye maeneo kama;

-Umri wa madereva wanaopata ajali
-Validity ya leseni za madereva wanaopata ajali
-Maeneo ambayo ajali zinatokea
-Aina ya magari yanayopata ajali
-Condition na ubora wa magari yanayopata ajali
na kadhalika....

Takwimu zitakazokusanywa kutoka utafiri wa aina hii ndio zitaweza kutuongoza kuja na mapendekezo ya jinsi ya kupunguza ajali badala ya kujaribu kutatua kwa njia ya zimamoto.
 
SEHEMU YA VI

Tuhitimishe mchango wetu kwa kumkumbusha waziri Kamwelwe, bali mkusanyiko wa ''factors '' na hizo ni lazima kwanza zifanyiwe kazi

Hoja ya waziri kuhusu miaka 45 imejikita kisaikolojia zaidi. Kwamba, ni umri mtu anakuwa na majukumu yanayomwandama na hawezi kufanya upuuzi barabarani kuchelea athari zake

Hoja inathibitika kwa kuangalia BIMA hasa za nchi za wenzetu.
Umri ni sehemu ya Bima. Mfano, miaka 45 ni umri mtu anajali akitazama gharama za uzembe

Miaka 20 kijana anafikiria Team Mobeto vs Wasafi, anafikiria Ney wa Mitego vs Hamorapa
Umri huo kijana ana jazba akizongwa na mawazo ya akina Aisha au Williams

Katika umri huo kijana haoni madhara ya speed 150 km/hr , anaona tatizo maduka ya kuuza kondomu yakifungwa kabla hajafika

Waziri ametoa miaka 45, hiyo isiwe kigezo. Ni muhimu leseni zzikiwa na madaraja yakitoa muda na sifa za kuhamia daraja jingine.

Kama kuna madaja 5 kufikia hatua ya Bus na Lori rekodi inaweza kusaidia kutupa umri sahihi. Madaraja 5 kwa miaka 2 na rekodi safi inamaana miaka 10. Kwa kijana aliyeendesha akiwa na miaka 25 muda huo atakuwa na miaka 35. Suala laumri lijadilika si lazima liwe 45

Pili, Mh Waziri makampuni ya BIMA yawajike katika ajali kuanzia malipo kwa wahusika na mafao yanayoambatana na uzembe wa mteja wao, yasiwe vijiwe vya kupora pesa

Makampuni yatoe BIMA kulingana na chombo, umri, uzoefu na rekodi. Ni ujinga wa hali ya juu kuwa na flat rate ya BIMA. Hili linaeleza kutowajibika kwa makampuni na uporaji unaofanywa

Bima iwe ya mtu na si gari ili kuzuia ''madei waka'' kupewa magari na wamiliki

Tatu, wenye vyombo wabanwe na serikali na mashirika ya BIMA kupitia malipo makali kutokana na ajali za vyombo vyao. Hapa mchango wa BIMA utaonekana dhahiri

Ni tajiri gani atakayeajiri mtoto wa miaka 25 kubeba roho za watu 50 akijua madhara yake?

Nne, mfumo wa kutoa leseni upitiwe upya. Kuwepo na mafunzo na wakufunzi waliofuzu si mafunzo katika viwanja vya mpira bora liende.
Leseni ziwe na madaraja, zitolewe kwa uhakika na si kugawa kama vocha za simu au njugu

Tano, mfumo wa kujua nani anaendesha kwa namna gani na anadhibitiwaje kama ni mkosaji

Sita, Askari wa usalama kiwe kitengo chenye wataaluma wa vyombo na ujenzi
Ikitokea ajali, kitengo kitoe sababu ni kwanini na ni njia gani zimewekwa kuzuia nyingine

Saba,kuondoa ujima wa askari kusimama na vitabu ili ku 'discourage' rushwa
Kama Jeshi halina uwezo wa teknolojia, wakala ateuliwe kufanya kazi hiyo kwa malipo

Mh Waziri aelewe, usalama wa barabarani ni wajibu wa serikali, makampuni ya bima, watumiaji na madereva. Hakuna solution bila kuhakikisha wadau hao wanabanwa na sheria

Kubana maeneo yote kutawafanya wawe responsible wakijua madhara yatakayowasibu

Hivyo suala la umri linajadilika, haliwezi kuwa muarobaini kama lilivyo

Swali la muhimu, tunaungaje factors zote ili kupata jibu?

Tusemezane
 
Mkuu Nguruvi3

Umechambua kwa kina.

Swali linarudi kwamba; suluhisho la changamoto zote hizi kama ulivyozichambua ni kuwa na madereva wenye umri mkubwa? Ikiwa shule za udereva zina mapungufu kwenye mafunzo wanayotoa does it matter ikiwa mhitimu ana miaka 20, 30 au 45?

Tungeweza kwa mfano kufanya utafiti kwa kutumia data za ajali zinazokusanywa na jeshi la polisi usalama barabarani na tukaweza kupata takwimu za kutosha kwenye maeneo kama;

-Umri wa madereva wanaopata ajali
-Validity ya leseni za madereva wanaopata ajali
-Maeneo ambayo ajali zinatokea
-Aina ya magari yanayopata ajali
-Condition na ubora wa magari yanayopata ajali
na kadhalika....

Takwimu zitakazokusanywa kutoka utafiri wa aina hii ndio zitaweza kutuongoza kuja na mapendekezo ya jinsi ya kupunguza ajali badala ya kujaribu kutatua kwa njia ya zimamoto.
Mkuu nimejitahidi sana kuepuka TAKWIMU kwasababu kwasasa ni jambo ''haramu'

Sheria ya takwimu inakwaza katika kufikiri kwa kina.
Kwamba, tukubali zitakazotolewa hata kama zimepikwa.

Hivi unategemea Jeshi la Polisi kutoa takwimu za askari wala rushwa?
Hawawezi kutoa takwimu zozote zitakazoonyesha uzembe wao

Ni kwa muktadha huo, matumizi ya takwimu yanatukwaza.
Hata hivyo, bandiko la juu nimeeleza kuhusu suala la umri wa miaka 45

Nimesema ni la kisaikolojia kuliko takwimu kwa muktadha wa waziri, kwamba, ni umri wa watu matured wakiwa responsible.

Nilichosema ni kuwa umri pekee hauwezi kuwa dawa, na unajadilika.

Kuna uwezekano wa umri kuwa miaka 35 au 30 lakini lazima ielezwe umri huo unaakisi vipi maturity na experience ya kuendesha.

Nikashauri madaraja ya leseni, nikitoa mfano kama leseni ina madaraja 5, baada ya mafunzo mtu anapewa masharti ya wapi aendeshe

Sio suala la leseni halafu huru kuingia barabara yoyote. Baada ya muda, daraja la kwanza kwa mfno, liwe miaka 2.

Katika muda huo mtu asiwe na ajali na akiwa nayo anafidia miaka mingine 2

Dararaja la 3, 4 navyo hivyo hivyo hadi daraja la juu la 5

Katika daraja la 5 iwe ''professional license' nayemiliki anawajibika kwa kiasi kikubwa.

Leseni yake inaweza kurudishwa daraja la chini au kufungiwa kwa muda maalumu au kufutwa kama ana matatizo ya rekodi mbaya

Kwa mwendo huo tutaweza kufikia hatma ya umri gani ni sahihi na si suala la namba tu
Umri wa mtu lazima uakisi uzoefu katika uendeshaji.

Miaka 45 bila kigezo ni tatizo maana umri huo mtu ajatjifunza leo kesho anapewa Bus
Ni muhimu kuwa na 'trend' ndiyo maana nikasisitiza uwepo wa rekodi na suala la BIMA

Umri hauwezi kuwa jibu bila kuangalia 'factors' nyingine
 
"
Mwalimu, post: 28694718, member: 11689"]Sina hakika kama hii mbinu ya "kuprovoke" ni muafaka sana na kwa upande mwingine inahalalisha "uholela" fulani hivi.
Nadhani hili linatugusa sote. Waziri ka provoke nakubaliane naye kwa maana moja. Ni heri yake ametoa suluhisho hata kama ni baya kuliko kukaa kimya au kujiunga na mfumo wa rambi rambi

Rambi rambi hazielezi chochote zaidi ya kusema 'pole'. Hatuwezi kuendelea na maisha ya rambi rambi kila siku bila kufanya kitu. Ndiyo maana nikasema waziri anaweza kuwa na mapungufu, hata hivyo mapungufu yake uyaangalie kwa jicho chanya ili TUJINUSURU. Hili ni letu
Umetoa mfano mzuri wa Makonda, sina hakika juu ya mafanikio yaliyopatikana kwenye vita ya madawa ya kulevya lakini sarakasi zilizuata za kutaja majina ya "watuhumiwa" hadharani huku wengi wao wasikutwe na makosa yoyote ndio "uholela" wenyewe ninaouzungumzia.
Hili la waziri ni tofauti na Makonda.

Makonda alichokifanya si kuamsha mjadala ni ku impose sheria zake , kukiuka haki za watu kwa kuwataja hovyo na kutafuta political stunt
Waziri amesema atapeleka mswada, akijua ni jambo la mjadala, at least , hatuwezi kuwaweka katika mizani.
Mh waziri Kamwele kwa nafasi yake ana fursa ya kulichukulia suala hili kwa mapana yake na kiuweledi zaidi kuliko hii approach inayotaka kutumika sasa..
Njia anayotumia ni 'community participation' ili kupata mawazo mbadala.

Ni jambo baya kama angeamka asubuhi na kutoa amri tu, nisingekuwa naye.
Kwavile ametoa hoja, nadhani asaidiwe

Ana mapungufu hebu tuyaangalie kwa kuyafanya chanya badala ya kumbeza

Kumbeza kama ilivyo katika mitandao ni kwa madhara yetu.

Tutambeza kesho tunaamkia rambi rambi na inakuwa vicious circle.

Hebu tuangalie ana hoja na ina mapungufu? Na tumsaidieje kuelewa?
 
BIMA YA TANZANIA NA UTATA

1. Eneo la BIMA (Insurance) ni muhimu kama sehemu ya kuzuia ajali za kizembe

Bima inamlazimisha mteja kuwa ''responsible' katika kuendesha na kulinda usalama wa wote

Kwa nchi zilizoendelea, bima inatolewa kwa kuzingatia aina ya chombo(vehicle), make , model and year. Zaidi ya hapo inazingatia umri, idadi wa madereva na watumiaji

BIMA inategemea aina ya uendeshaji, na hupanda au kushuka kutokana na rekodi ya dereva

Bima inamlinda na kumhakikisha mteja X anaye endesha gari Y ikitokea ajali.
Kwa maana BIMA ni kwa dereva na gari husika. Hili linasaidia kuzuia kuazimana magari hovyo

Kwa Tanzania Bima inatolewa kwa gari bila kujali dereva, watumiaji au madereva wengine

Jambo hili linafanya gari kuwa ya ''umma',kwavile ina insurance yoyote anaweza kuendesha.

Gari inatumika na ma-house boy, watoto , mashangazi n.k. ilimradi ina BIMA

Gari haiwezekani kuwa controllled kwa aina ya madereva wanaoendesha au waliofunzwa

2. (i)BIMA si kodi ni huduma kwa mteja ikiwa ni kuhakikisha shughuli zake za maisha hazikwami.

Kwingine duniani kama ni ajali ndogo iliyoharibu gari, shirika linawajibu wa kutoa gari hadi matengenezo au malipo ya uharibifu yatakapokamilika

(ii)Kama ni majeruhi, Bima inagharamia shughuli za matibabu zikiwemo siku za kazi zilizopotea
Katika hilo Bima hulipa viungo vilivyoumia au kupotea. Kama ni msiba Bima inafidia wafiwa

Tanzania mashirika hayajali kifungu 2(i) kwasababu yanataka pesa.
Hayana hasara kutokana na kutozingatiwa kifungu 2(ii).

Mashirika yanachofanya ni kukusanya malipo na ndiyo mwisho wa shughuli

Kama yapo malipo ni kwa watu wanaojua taratibu, Watanzania wengi hawajui haki hiyo

3. Kuna sababu kwanini mashirika ya BIMA Tanzania yanashamiri kwa kasi.

Ni biashara inayolipa isiyo na wajibu kwa maana kuwa ni kukusanya pesa.

Zipo Kampuni za 'briefcase' na hilo linatoa loophole ya sticker fake n.k.
Mashirika na kampuni hazijali, zimeshachukua pesa inatosha

Jambo hilo linachagizwa kwa kiasi kikubwa na influence ya mashirika na kampuni za BIMA

Kote duniani, mashirika ya BIMA yana nguvu sana katika ku ''influence policy na Viongozi''

Ni nadra sana kusikia viongozi wakikemea mashirika hayo kutokana na 'influence'.

Si serikalini si Bungeni au kwingine, mashirika hayo yana ''nguvu kubwa'' za kutuliza mambo

Hoja hii aliyoleta waziri Kamwelwe mara itapogusa mashirika ya BIMA, inaweza kupindishwa kuyakwepa au hoja ikafa. Kuzungumzia mashirika hayo ni kugusa 'interest' za watu, haikubaliki!

Bima ni eneo lenye 'pristine corruptions'' haliguswi hata kama halitekelezi wajibu

Tunamshauri Waziri Kwamwelwe kuwa hoja ya miaka 45 inatukumbusha tu machungu ya ajali.
Bila kuyagusa mashirika ya BIMA yatekeleze wajibu wao, hata miaka 60 haitatoa jibu

Kwamba, hoja inaweza kujadiliwa, jibu ni ndiyo.

Kwamba itagusa maeneo yote kwa ujumla, jibu ni hapana

BIMA haitakuwa katika mjadala, ni eneo 'sacred'
 
1. Mkuu nimejitahidi sana kuepuka TAKWIMU kwasababu kwasasa ni jambo ''haramu'

2. Sheria ya takwimu inakwaza katika kufikiri kwa kina.
3. Kwamba, tukubali zitakazotolewa hata kama zimepikwa.

4.Hivi unategemea Jeshi la Polisi kutoa takwimu za askari wala rushwa?
5.Hawawezi kutoa takwimu zozote zitakazoonyesha uzembe wao
Mwalimu wangu nina haya kuhusu hoja zako nilizozipa namba hapo juu:
1. Ni kweli kuna ugumu wa kutekeleza sheria hii ya takwimu (vibali nakadhalika) lakini sidhani kama sheria imekataza kutumia takimwu amabazo zipo tayari na zimepitishwa na mamlaka. Kusema suala la takwimu ni "haramu" kunaweza kutafsiriwa vibaya kwamba serikali imezuia kutoa maoni kwa kurejea takwimu ambazo zipo tayari na mamlaka imeziidhinisha zitumike. Nadhani hapa Mwalimu ungetumia lugha kidogo inayoakisi ukweli huo kama niliilewa kwa usahihi sheria ile.

2. Hapa naomba ufafanuzi. Si nia yangu kuhamisha mjadala; nadhani baadhi ya kauli ambazo ni tata kwa sisi wanafunzi wako naomba utusaidie kuzielewa vizuri. Kwani, nashindwa kuelewa kufiriki kunakwazwaje na sheria?
3. Hapana hili halikubali hata kidogo. Zikipikwa zitakaliwa na nadhani zipo mbinu za kutambua data zilizopikwa tutatumia mbinu hizo.
4 & 5. Katika suala la Rushwa kwenye jeshi la polisi yawezaka kukawa na ugumu kutoa takwimu sahihi. Hata hivyo tunachombo kilichopewa mamlaka ya uchunguzi kuhusu masuala ya Rushwa, PCCB (kama sijakosea kifupi chake). Kama PCCB haiwezi kutoa takwimu sahihi juu ya hili basi hapo nitatizo kubwa sana.
------
Hata hivyo kutokana na hili nitalazimika kurudia upya sheria ya takwimu yawezekana kuna vipengele sikuvielewa vizuri.
Nitarejea.
 
Mkuu Nguruvi3

Umefanya analysis ya kina kuhusu factors kadhaa zinazosababisha ajali barabarani. Ni kupitia tafakuri za aina hii ndipo unaweza kuja na solution ya jinsi ya kukabiliana na ajali. Huwezi kutatua tatizo kubwa kama hili kwa njia ya mkato au kuangalia factor moja pekee halafu utegemee kwamba utaona matokeo chanya.

Kwa nini solution isijikite kwa mfano na haya mambo ya msingi;
i) mafunzo, utoaji na usimamizi wa leseni
ii) usimamizi wa sheria za usalama barabarani
iii) ubora wa barabara zetu
iv) usimamizi na ukaguzi ubora wa magari

Kuna research yoyote imewahi kufanyika kuonesha kwamba asilimia kubwa ya madereva wanaopata ajali ni wa umri wa chini ya miaka 45?

Kwa mfumo huu wa mafunzo na utoaji leseni ambao una mapungufu does it matter ikiwa mhitimu ana miaka 30 au 45?
Mwalimu mwenzangu, kama umemsoma vizuri Nguruvi3 visababish ni vingi sana lkn yy kajikita zaid kujadili swala la umri ambalo tayar limesha leta negative connotations kwa watu.

Btw unazo point nzur sana na itabidi tuzijadili kwa kina
 
Mwalimu mwenzangu, kama umemsoma vizuri Nguruvi3 visababish ni vingi sana lkn yy kajikita zaid kujadili swala la umri ambalo tayar limesha leta negative connotations kwa watu.

Btw unazo point nzur sana na itabidi tuzijadili kwa kina
Tatizo la waziri ni kuangalia suala kwa factor moja.

Insurance ni tatizo lililosumbua wenzetu wakafanya research, wakazijaribu na kupata matokeo.

1. Kwamba, kupata leseni ya kuendesha si haki ni fursa(privilege)
Kwamba dhamana hiyo inaweza kusitishwa, kuondolewa au kunyimwa katika misingi ya sheria

2. Wakaangalia factors zinazohusu madereva kama mfunzo, umri na aina ya vyombo

3. Wakaangalia maeneo mengine yanayoweza kusaidia kuzuia tatizo kama Polisi, Bima (insurance), Waajiri na wamiliki wa vyombo vya moto

4. Wakachukua 1-3 na kuzifunga pamoja ili kulinda wananchi wanaotembea au kupanda vyombo hivyo. Kulinda madereva na waajiri wao na kulinda makampuni ya Insurance

Katika kutekeleza hayo walihakikisha kila eneo linachukua dhamana ya uwajibikaji

Kwetu sisi hakuna utaratibu ni holela tu. Ninajiuliza swali hili la umri bila majibu
Hivi mtoto wa miaka 18 analipaje Bima sawa na mtu wa miaka 50 au 60?
Watu hawana wanafikiri sawa? Wanamajukumu yanayowafunga? Wana uzoefu sawa?

Hapo nikabaini suala la BIMA si kulinda watumiaji wa vyombo, abiria na madereva
BIMA imekuwa kama kampuni za kukusanya mapato na kisha kugawa kinachopatikana TRA

Polisi hawana utaalamu wa kutosha kubaini vyanzo au kuzuia matukio.
Uchunguzi wa Polisi wa eneo X lenye ajali 20 kwa mwaka ni kupima kwa tape measure.
Hakuna anayefanya kazi kama ''engineering'' kuangalia barabara , au uimara wa vyombo

Uimara wa vyombo unathibitika pale wiki ya usalama inapotumika kukusanya mapato ambapo Polisi wanatoa takwimu kutokana na makosa bila kutoa takwimu za matukio na vyanzo vyake. Hili linatoa loophole kwa madereva na waajiri kutowajibika

Tajiri atatoa pesa chombo kipate sticker ya wiki ya usalama. Dereva hatajali kwasababu haiathiri leseni yake. Mashirika ya bima hayajali kwasababu hayafidii wahanga.

Mashirika hayafidii wahanga kwasababu yana influence katika kutengeneza policy
Influence yao ipo kwa viongozi na si watumiaji wa vyombo, they have nothing to lose

Hoja ya Mh Waziri inakuwa na mashiko eneo moja. Kwamba, at least ameona kuna tatizo. Solution yake inaweza kuwa si sahihi, lakini kwamba kuna tatizo kubwa yupo sahihi

Yupo sahihi kwasababu badala ya kutuma rambi rambi, yeye ameona heri kujadili
Ndiyo msingi wa kusema, ana hoja asaidiwe kuliko kumbeza tukiendelea na rambi rambi
 
SHERIA YA LESENI MIAKA 45

Kauli ya waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mh Isack Kamwelwe kuhusu umri wa madereva kuendesha malori na vyombo vya abiria imepamba habari za wiki hii

Ni kawaida ya Watanzania kuzungumzia jambo kwa jicho wanalotaka na si lile linaloona ukweli. Waziri Kamwelwe ana hoja ya msingi kabisa katika mjadala unaondelea

Kauli yake imekuja ikiwa imechelewa. Ongezeko la ajali nchini limekuwa tishio kwetu sote

Kila inapotokea ajali njia zinazotumika kuzuia au kupunguza ni za mkato na za kizamani kama ulivyo mfumo wetu wa kutoa leseni,kudhibiti, kusimamia bima na kutafuta chanzo na suluhu

Hoja ya waziri inaonekana kuwa na mapungufu kwa mtazamo wa haraka, lakini wazo analotoa ni muhimu sana katika kudhibiti na kukabiliana na wimbi la ajali nchini

Mitandaoni na kwingineko baadhi yetu hatuangalia kiini cha hoja, tunaangali mapungufu ya hoja. Ieleweke alichosema Mh Waziri si sheria ni kusudio la kupeleka mswada Bungeni

Kwa kuelewa hivyo , ni makosa kuanza kukosoa hoja zake kana kwamba miaka 45 ni sheria tayari au kdhani pendekezo la miaka 45 linatosha kuwa suluhu ya tatizo

Kama miaka 45 pekee ndicho kinachodhaniwa ni tatizo, hoja nzima inapoteza maana

Tatizo la ajali linachangiwa na 'factors' nyingi si umri pekee.

Katika kukabiliana na tatizo umri ni sehemu ya suluhu na si suluhu yenyewe

Ni kwa mtazamo huo, tunaona ipo haja ya kumsaidia Mh Waziri kuboresha hoja yake yenye mantiki na ya msingi sana kuliko kukimbilia kulaani, kumbeza na kudharau alichosema

Kwa uzito wa hoja hii tutakuwa na mabandiko kadhaa kwa lengo la kumsaidia waziri kuboresha hoja kwani tatizo la ajali linatugusa sote na sote tunawajibu wa kulitafutia jawabu

Sehemu ya kwanza inafuata

What we need is not age limit but improved regulations kwenye governance ya motor vehicle transportation.

1. 100% Liability ya reckless driving iende kwa dereva na owner wa Gari, pikipiki, basi na Lori : this means:- Bima za magari zipitiwe na kuwe na breakdown ya liability ya causing an accident, including footing all expenses (medical, funeral, car repair and replacement) for the driver who is at fault.

2. Reclassification ya leseni za udereva na kuweka masharti magumu na requirements. Wanaoendesha abiria, wanaoendesha mizigo ya kawaida hata kwa uzito na aina ya cargo (hazard versus non hazard)

3. Leseni zote za udereva ( Gari, Lori, trekta, pikipiki, magreda etc) ziwe na 2 year limit kisha renewal ambapo lazima recertification ifanyike (point ya 4) na driving record kutoka Usalama Barabarani na kampuni ya Bima zitoe points. Good driving record Iwe incentive ya low premium kwenye Bima. Bad driving record premium ziwe kubwa na ikibidi kufungia leseni.

4. Recertification and testing. Madereva wa magari ya abiria na mizigo regardless ya idadi ya watu, aina na uzito wa mizigo lazima kila 2 or 3 years waende kwenye designates shule ya udereva ya Mkoa, kanda au Chuo cha Usafirishaji for recertification na testing, then wapate renewal ya leseni.

5. Annual vehicle inspection kabla ya registration kuwa renewed. Fitness ya Gari ifanywe na certified mechanics (si polisi wa Usalama Barabarani), kuanzia body, electronics, drivability, emissions, suspension-springs, brake system, lighting system, Matairi. Kuna mafundi wengi wa kutoka Veta, Technical colleges na NIT, kuwe na special program kwa kila fundi na garage ya vehicle inspection for road worthiness. Gari liki-pass inspection, na proof of insurance , a digital certificate inatumwa TRA ambapo wata-issue renewal ya registration. Hiyo registration na proof of insurance ifike mahali tutumie ICT ziwe kwenye Database ambayo ita link Insurance company, service stations za vehicle inspection, na Usalama Barabarani. Ukisimamishwa they can link the digital certification ya Gari, bima na leseni ya udereva na driving records. Hapa you kill to birds with one stone: unazuia Rushwa kwa polisi na kufanya fine ziwe captured electronically including driving record za offender, pili unaongeza efficiency ya Polisi wa Usalama Barabarani kwenye traffic na road violation management.

6. Polisi wa Usalama Barabarani wawe trained na wApate annual certification ya oversight ya mfumo mzima wa uendeshaji magari na necessary knowledge wafanye kazi more efficiently.

7. Driving record; hapa bad driving record na poor score za recertification na testing zilasimishe dereva kuwa na high premium ya Bima na kulazimishwa awe na full coverage including liability.

8. Madereva wa malori na mabasi- public transportation ( teksi, bajaj, pikipiki) lazima wakati wa renewal ya leseni wafanyiwe medical test ya macho, reflexes, drug/substance and alcohol usage/abuse kabla ya kupewa pass grade to renew leseni.

Ukiweka mfumo kama huu, kisha watu wakajua they will be responsible zaidi ya makosa ya Barabarani na fines... udereva utanyooka na kupunguza recklessness na neglect inayofanywa.

Kuongeza accountability kuokoa maisha ya abiria na mali ni through clearly refining responsibility na monetary liability kwa dereva na owner wa vehicle.

That is better solution kuliko kutumia age as qualifier ya kuendesha magari more responsibly!
 
Back
Top Bottom