Duru: Waziri Kamwelwe asibezwe, ana hoja ya msingi, asaidiwe kuboresha

"Rev. Kishoka, post: 29492192, member: 18"]What we need is not age limit but improved regulations kwenye governance ya motor vehicle transportation.
Mkuu ndiyo hoja yangu kwamba, Waziri ana hoja ya uwepo wa tatizo. Kwa bahati mbaya ameangalia picha kwa ufinyu akichukulia age kama solely problem bila kujua kwa kuangalia factors nyingine suala la age lina dissolve automatic. Mfano, muda wa leseni, madaraja na aina ya chombo
1. 100% Liability ya reckless driving iende kwa dereva na owner wa Gari, pikipiki, basi na Lori : this means:- Bima za magari zipitiwe na kuwe na breakdown ya liability ya causing an accident,
Hili ni tatizo kubwa Tanzania, kwamba, liability inakuwa katika chombo si mtumiaji. Kwa mfano, gari likiwa insured yoyote anaendesha. Kwa nchi za wenzetu liability ipo kwa mwenye leseni na chombo husika. Kama anawatumiaji wengine inabidi awaingize katika Bima yake. Huwezi kukuta mtu anampa house boy au kijana wake gari hovyo akijua tatizo likitokea BIMA haitamlipa.
2. Reclassification ya leseni za udereva na kuweka masharti magumu na requirements.
Yes, kutoka daraja moja hadi jingine ili kuwafanya wahusika wawe responsible
3. Leseni zote za udereva ( Gari, Lori, trekta, pikipiki, magreda etc) ziwe na 2 year limit kisha renewal ambapo lazima recertification ifanyike (point ya 4) na driving record kutoka Usalama Barabarani na kampuni ya Bima zitoe points. Good driving record Iwe incentive ya low premium kwenye Bima. Bad driving record premium ziwe kubwa na ikibidi kufungia leseni.
Yes, nimelijadili na kuuliza, hivi inawezekanaje mtu aliyeendesha miaka 30 awe na BIMA sawa na kijana aliyepata leseni Jana pale TRA! Kwa kuangalia risk assessment wawili hao hawawezi kuwa sawa. Swali jingine, mashirika ya BIMA yanajali? Laiti yangekuwa yanajali yasingechukua risk ya 30 yrs experience vs 2 days driving record katika daraja moja
4. Recertification and testing. Madereva wa magari ya abiria na mizigo regardless ya idadi ya watu, aina na uzito wa mizigo lazima kila 2 or 3 years waende kwenye designates shule ya udereva ya Mkoa, kanda au Chuo cha Usafirishaji for recertification na testing, then wapate renewal ya leseni.
Wengine wamepungua nguvu za macho, hawajapima, na hawatumii miwani. Ilimradi alipata leseni miaka 20 iliypita nobody cares ana hali gani
5. Annual vehicle inspection kabla ya registration kuwa renewed. Fitness ya Gari ifanywe na certified mechanics (si polisi wa Usalama Barabarani),
Jeshi la Polisi liajiri watu wenye ujuzi katika mechanics na civil engineering wanaoweza kujua tatizo la gari au la ujenzi wa barabara, makutano n.k. Watu wanaoweza kutumia takwimu kubaini tatizo
Haiwezekani kumhamisha Polisi wa FFU na kumvalisha magwanda meupe tayari ni traffic
kuanzia body, electronics, drivability, emissions, suspension-springs, brake system, lighting system, Matairi. Kuna mafundi wengi wa kutoka Veta, Technical colleges na NIT, kuwe na special program kwa kila fundi na garage ya vehicle inspection for road worthiness.
Na hao mafundi wawe certified na kupewa 'liability' kwamba tatizo likitokea kwa gari iliyofaulu ikabainika hawakuikagua wawe responsible kwa matatizo. Hili ni kuzuia rushwa
Gari liki-pass inspection, na proof of insurance , a digital certificate inatumwa TRA ambapo wata-issue renewal ya registration. Hiyo registration na proof of insurance ifike mahali tutumie ICT ziwe kwenye Database ambayo ita link Insurance company, service stations za vehicle inspection, na Usalama Barabarani. Ukisimamishwa they can link the digital certification ya Gari, bima na leseni ya udereva na driving records. Hapa you kill to birds with one stone: unazuia Rushwa kwa polisi na kufanya fine ziwe captured electronically including driving record za offender, pili unaongeza efficiency ya Polisi wa Usalama Barabarani kwenye traffic na road violation management.
Jeshi la Polisi ni wazito kukumbatia mabadiliko ya nyakati
Waangalie sehemu kama JWTZ ambako kuna 'the best' kwa kila fani.
Ni rahisi sana kufanya kazi yoyote. Wana wataalamu kila fani tena waliobobea.

Nilishangaa Polisi walioniandikia risiti wakiwa 2 na vitabu 3
Nilipokataa wakanitisha kunilaza kituoni, nikakomaa wanipeleke. Kesi ikaisha

Vitabu 3 ina maana kuna vya serikali na kingine. Katika mazingira hayo, huwezi kujua faini zinakwenda wapi, hakuna rekodi ya dereva BIMA, TRA au Polisi kwenyewe.
Kwanini mwaka 2018 haya yatokeo?
6. Polisi wa Usalama Barabarani wawe trained na wApate annual certification ya oversight ya mfumo mzima wa uendeshaji magari na necessary knowledge wafanye kazi more efficiently.
Hapa nadhani ni kuwa na Polisi kutoka Technical colleges
7. Driving record; hapa bad driving record na poor score za recertification na testing zilasimishe dereva kuwa na high premium ya Bima na kulazimishwa awe na full coverage including liability.
Tz mashirika ya BIMA hayana hasara, hayafidii wahanga wa ajali. Kwa mantiki hiyo hawajali kuhusu driving record.
Wao wanakusanya pesa na faida kwa mabilionKuna utitiri wa mashirika ya BIMA ya briefcase, ni lucrative business.
Ukiweka mfumo kama huu, kisha watu wakajua they will be responsible zaidi ya makosa ya Barabarani na fines... udereva utanyooka na kupunguza recklessness na neglect inayofanywa.Kuongeza accountability kuokoa maisha ya abiria na mali ni through clearly refining responsibility na monetary liability kwa dereva na owner wa vehicle.That is better solution kuliko kutumia age as qualifier ya kuendesha magari more responsibly!
Ni kweli kabisa, tatizo ni moja, wanasiasa ni beneficiaries wa mashirika ya BIMA. Mashirika ya BIMA ni sehemu ya wachangiaji wa kampeni ili yaendelee kulinda masilahi yao

Mh Waziri na viongozi wanajua nini kinaendelea na mashirika ya BIMA, hawawezi kuyakabili kwasababu ya influence. Ndiyo maana hutasikia wakiyaogelea

Sehemu kubwa ya tatizo haipo kwa madereva, ni kwa Polisi na BIMA.
Ni kushindwa kuunganisha mfumo wa rekodi na kuwawajibisha wazembe kwa teknoloji.

Polisi wanatoa hati ya leseni, TRA wanatoa leseni hawana rekodi, BIMA wanatoa bila kujua mhusika kafikaje kwao. In this day and age!
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom