Duru-Ulaya: Kura ya maoni 'Brexit'

Mimi kwa hili la Brexit niko interested zaidi na athari kwa masoko ya fedha hasa kwa pair ya GBPUSD, hali hii ya sintofahamu mpaka sasa naona itapelekea pound kudondoka hadi kufikia low ya 1985 ambabo mpaka sasa ni takribani miaka 34 imepita (je soko litakumbuka hii historia?).Pound crash ya mwaka 1992 ,2008 na ile crash ya June 2016 wakati wa kura ya kujitoa EU yote naona iliashiria kuileta pound chini zaidi, ila mwisho wa siku naamini muafaka utapatikana utaopelekea uchumi uanze kuimarika tena .
Nimegusia hili la masoko ya fedha baada ya kujaribu kuianalyse chart ya currency pair husika ya tangu mwaka 1971 mpaka sasa
 
Mimi kwa hili la Brexit niko interested zaidi na athari kwa masoko ya fedha hasa kwa pair ya GBPUSD, hali hii ya sintofahamu mpaka sasa naona itapelekea pound kudondoka hadi kufikia low ya 1985 ambabo mpaka sasa ni takribani miaka 34 imepita (je soko litakumbuka hii historia?).Pound crash ya mwaka 1992 ,2008 na ile crash ya June 2016 wakati wa kura ya kujitoa EU yote naona iliashiria kuileta pound chini zaidi, ila mwisho wa siku naamini muafaka utapatikana utaopelekea uchumi uanze kuimarika tena kuanzia mwakani.
Nimegusia hili la masoko ya fedha baada ya kujaribu kuianalyse chart ya currency pair husika ya tangu mwaka 1971 mpaka sasa

Bandugu,

Hitimisho la Brexit ni lipi? Wengine tushapoteza uelekeo ni upi.
 
Bandugu,

Hitimisho la Brexit ni lipi? Wengine tushapoteza uelekeo ni upi.
Malikia anataka nchi yake...EU wanamchimba mkwara...!!! Malkia kasema liwalo na liwe kupitia kwa Boris Jonson(UK-PM) kwamba lazima UK ijitoe EU kwa makubaliano ama bila makubaliano ifikapo mwishoni mwa mwezi huu. Scotland nao wanasema hawataki kujitoa EU...na wanasea wako mbioni kuitisha 'referendum' nyingine kujitoa UK. Yaani UK ni 'volatile' kuelekea October 31, 2019 !!!

Kwa kifupi ni hayo.
 
Ina maana Brexit itakuwepo wiki ijayo?
 
I will believe in Brexit happening when I see one actually happened... TPTB won't let that happen, IMHO.

Januari 2019

Kukiwa na Brexit kweli [Next week], itanibidi niajasti parameter za modeli yangu ya mzunguruko wa ulimwengu.

OK. November Mosi. Ya nini kumung'unya maneno:

Brexit ni dog and pony show kwenye smoke and mirrors. Danganya toto. Hakuna Brexit. Hakutakuwa na Brexit. Hakutakuwa na Brexit wakati TPTB hawataki.
 
Mkuu Brexit isingeweza kutokea. Boris ni sawa na Trump wote wakidhani wana nguvu kubwa kuliko za wananchi kupitia uwakilishi wao.

Cameron aliona tatizo akaamua kuachia ngazi. Theresa May akadhani ana mworabani akaishia '' The country I love...''.

Boris alipewa matumaini na Trump kwamba akifanya lolote lile Brexit ikatokea basi watafanya biashara na UK itastawi.

Alimsikiliza Trump hakumfahamu wala kujua nguvu ya mabunge na nguvu ya demokrasia ya nchi za Magharibi.

EU wanajua kujitoa kwa UK kutaanzisha mlolongo wa nchi kujitoa zikidai kubaki na mahusiano na EU. Vikwazo inavyokumbana navyo UK imekuwa fundisho kubwa kwa wanachama wengine

Kuna mambo kadhaa yanaingiliana kwa kuangalia Brexit.

Kwanza, Kasri la Buckingham Palace linataka Brexit ili kuendeleza tawala zilizokuwepo

Palace wanaamini sheria za UK hazitengenezwi Brussles kwani mwisho Mama atabaki ''ceremonial''

Hoja ya Palace inaungwa mkono na wahafidhina (conservatives) wanaoamini katika UK na kwamba UK ni kubwa.

Wanaamini mchango wa UK katika EU ni mkubwa sunaotosha kuiendeleza nchi yao bila kufikiria pia ''kura'' muhimu waliyo nayo ndani ya umoja huo

Ikumbukwe matakwa mengi ya UK kama kuacha Pound Sterling na masuala ya Visa walipewa upendeleo maalumu. Hilo likawatia vichwa conservatives kwa kudhani UK ni zaidi ya EU.

UK kama mkusanyiko wa mataifa una Ireland na Scotland. Kura ya Scotland bado ni pasua kichwa kwani Waskochi wanaamini kutotendewa haki sawa na wengine.

Ndani ya EU Ireland na Scotland zimeonekana kufaidika zaidi, Brexit kwao ni mwiba.
Hii maana yake ni kuwa ugomvi wa Brexit unahama na kuwa ugomvi wa ndani ya UK

Kujitoa bila makubaliano na EU maana yake ni kuumiza nchi hizo
Nazo zinasema hazikubali kufuata mkumbo wa kujitoa na kuacha fursa ndani ya EU

Wakati huo huo, England na Wales nazo zinasema kujitoa EU kutapunguza fursa za watu wao

Kwa mkanganyiko na ''family feud'' imekuwa ngumu kwa Wabunge kufikia muafaka.

Hilo ndilo linasababisha kura kutotimia, si suala la vyama ni suala la ''constituents'' zinasema nini

Kwa mantiki hiyo, EU wametoa muda zaidi wa UK kufikiria namna ya kujitoa ifikapo Jan 31

Muda huo umetolewa makusudi kabisa kwasababu kuu mbili
1. Ima Bunge (House of common) ivunjwe uchaguzi ufanyike na kauli za wananchi zitawale
2. Uwepo uwezekano wa kura ya pili ya Brexit ambayo EU wana uhakika itabadili mwenendo

Tusemezane
 
Mkuu Brexit isingeweza kutokea. Boris ni sawa na Trump wote wakidhani wana nguvu kubwa kuliko za wananchi kupitia uwakilishi wao.
...

Wananchi ndio waliopiga kura za kutaka kuondoka EU. Ingekuwa pana kuheshimu maamuzi ya wananchi, basi kura za walio wengi zingeheshimiwa, na Britain ingeondoka EU.

[Tin-foil hat fully in place]
1. Hapo kale, Utawala ulikuwa unazingatia kabila. Kila kabila na utawala wake.
2. Utawala ukahamishiwa kwenye mkusanyiko wa makabila ulioitwa taifa. Kwa mfano, Wazungu walipokuja Afrika walitukuta tukiwa hatua Na. 1., na wakavunja tawala za kikabila na kuanzisha mataifa ya Kiafrika. Wao wenyewe wamepitia mengi mpaka kufikia hatua ya utaifa.
3. Kwa sasa, Mfumo unavunja taifa mojamoja na kuleta mkusanyiko wa yaliyokuwa mataifa (ukanda). Hapa ndio tunaona EU, EAC na miradi mingine ifananayo. Baadhi ya wananchi, kicking and screaming, wanatamani mfumo ungebaki wa "Taifa Kwanza" -- ndio hao wa Brexit -- lakini wamezidiwa nguvu. Taifa mojamoja, kama vile Uingereza, imebaki jina tu. How mighty have fallen!
[/Tin-foil hat]

Kwa hiyo, mkuu Nguruvi3 , siyo suala la demokrasia -- kwenye demokrasia wengi-wape; wengi wametaka Brexit -- na hawatopewa.
 
Mkuu Mlenge
Mwanzo wa Brexit katika uzi huu tulieleza kosa kubwa lililofanywa na ''wengi''
Wananchi wa UK waliongozwa na opinion poll zilizosema majority wanataka kubaki EU

Wengi wanaotaka EU hawakwenda kupiga kura kwa mazoea na matumaini haitatokea

Nigel Farage akaongoza wanaotaka kujitoa, wakajitokeza na kupiga kura na kushinda
Usemi wa ''election have consequences' ukatimia

Ushahidi wa hili unaonekana jinsi England walivyohamaki baada ya matokeo
Na jinsi Scotland na Ireland walivyoshangazwa na matokeo.

Kilichofuata ni kuheshimu maamuzi ya wananchi.
Ndipo UK ikatumia article 50 of Lisbon treaty kuwaandikia EU kuhusu kujitoa.
Hili linasemwa ''trigger article 50'' kuwaambia wanachama nia ya kujitoa. Lilifanyika

Hadi hapo maamuzi ya wananchi yaliheshimiwa kwani UK ilitumia article 50 ya mkataba wa Lisbon, EU wakakubali UK kujitoa. Narejea tena hadi hapo Maamuzi ya wananchi yaliheshimiwa

Tatizo likajitokeza si kwa EU bali kwa UK. Kwamba, UK inaondokaje EU?

Je, wanaondoka bila mahusiano yoyote na EU?
Je, wanahitaji mahusiano ''mahususi ' yatakayowafanya washiriki EU bila kuwa wanachama?

Ilipofika hapo ndipo mzozo ukaondoka EU na kutua nyumbani ''House of Common''

Ndiyo maana unasikia kitu kinaitwa ''Brexit deal'' siyo tena ''Brexit'' kwani hatua hiyo ilishapita

Brexit deal inajadiliwa ndani ya House of common ambao ni wawakilishi wa wananchi.
Uwakilishi wao si kuhusu kujitoa au kubaki, ni jinsi gani ya kuendelea na mahusiano na EU

Hapa ndipo pa kueleweka, kwamba, mzozo si kujitoa wananchi walishaamua.
Mzozo ni Brexit deal, yaani wanajitoa ''mazima'' au wanajitoa wakiwa na deal na EU?

Sasa Brexit deal ambayo ni ugomvi wa ndani wa familia ya UK(Family Feud).

Kwamba N.Ireland na Scotland wanasema wao wanataka kubaki EU
England na Wales wanasema, tusijitoe na tukijotoa tuwe na deal na Brexit

Wahafidhina wanasema tujitoe jumla hatuhitaji deal na EU

Boris Johnson anasema Ireland ibaki na mahusiano ya single market na EU.
Wa-Irish wanasema hilo litakuwa kuwatenga na Great Britain lakini pia wanataka kubaki EU

Katika kulinda masilahi ya kila kundi, upigaji wa kura wa namna ya kujitoa EU unashindwa kupata idadi inayotakiwa. Kumbuka kura ni ''non binding'' kwamba hazifuati chama.

UK wana proposal ya kujitoa lakini wapewe fursa za kiuchumi ndani ya EU.

EU wanasema hilo litategemea UK nayo itatoa fursa gani kwa wananchi wa EU.

Wahafidhina wa UK wanasema walijotoa kuepuka tatizo la fursa hasa ajira, hawataki

EU wanasema kama hamtaki basi ondokeni bila mahusiano na EU

Pro-EU wanasema kuondoka bila mahusiano na EU ni kujitia kitanzi kiuchumi na ki fursa

Option zote hizo zinazaa maswali haya
1. Kura irudiwe tena ili wananchi waseme tena
2. Bunge livunjwe ili wananchi wachague wabunge ili kufanikisha au kutofanikisha Brexit deal

Kwa kumalizia na mtiririko huo nilioueleza, maamuzi ya wananchi yameheshimiwa kwa UK kuruhusiwa ku trigger article 50 of Lisbon Treaty.

Ugomvi si kujitoa tena, ugomvi ni namna gani ya kuondoka na ugomvi huo upo house of common ukichagizwa na interest tofauti za makundi tofauti.

Tusemezane
 
Mkuu Mlenge
Mwanzo wa Brexit katika uzi huu tulieleza kosa kubwa lililofanywa na ''wengi''
Wananchi wa UK waliongozwa na opinion poll zilizosema majority wanataka kubaki EU

...
Option zote hizo zinazaa maswali haya
1. Kura irudiwe tena ili wananchi waseme tena
2. Bunge livunjwe ili wananchi wachague wabunge ili kufanikisha au kutofanikisha Brexit deal

Kwa kumalizia na mtiririko huo nilioueleza, maamuzi ya wananchi yameheshimiwa kwa UK kuruhusiwa ku trigger article 50 of Lisbon Treaty.

Ugomvi si kujitoa tena, ugomvi ni namna gani ya kuondoka na ugomvi huo upo house of common ukichagizwa na interest tofauti za makundi tofauti.

Tusemezane

Mkuu Nguruvi3, Nitanukuu Waingereza wasemavyo kuhusu hoja kama hiyo:

Of course there is. A Remainer Parliament failing to carry out the wishes of the people and then going back and saying you got it wrong vote again is not democracy.

Dear Voters,

Parliament has considered the recent opinion proffered by the electorate that the UK should leave the EU, and regrettably has found that opinion to be rabid, pig-ignorant and stultifyingly ill-informed.

As such, we will not be bringing forward legislation to enact this terrible opinion at this time.

Parliament thanks you for the opportunity to be involved in your poorly thought out opinions, and hopes you will consider us again next time you need somebody to point out when you're being massive idiots.

Kindest Regards,

Parliament

Its the same thing. The politicians telling the electorate they got it wrong and have to do it again. We can point to the same thing in plenty of other EU votes where the EU side lost and they told the electorate to do it again. If you think that is a message that will be welcomed by most people who voted Leave then you really are out of touch.

That is certainly the message all of us on the Leave side will be pushing from now on.

Parliament thinks you are too stupid so you have to vote again until you vote the way they want.

Wanaposukuma ajenda zao, EU hufanya miundombinu kuhakikisha kura za maoni zinarudiwa mpaka wapiga kura wapige kura "kwa akili" -- yaani, kwa kuendana na malengo ya EU. Yote haya ni katika kutekeleza mfumo uleule wa kuua utaifa (nationalism) na kuibua ukanda (regionalism). Baada ya ukanda, mafanikio ya kuelekea hatua namba nne (utandawazi -- globalism) itakuwa ndio nyepesi kuliko yote. Kwa sasa, ajenda yao ni kufuta kabisa utaifa (nationalism) na kufuta familia (kama ilivyozoeleka) ili kudhibiti idadi ya watu na kupunguza idadi ya serekali wanazodili nazo.

Kwa ujumla, matokeo ya awali yatakuwa ni kama vile wakati wa Himaya ya Kirumi (Roman Empire). Wakati ule, palikuwa na makundi mawili makubwa: Wakulu (Patricians) na Makabwela (Plebs).

Wakulu wao walikuwa na familia za aina ya BMW (Baba, Mama na Watoto), na viwango vyao vya maisha vilikuwa bora. Makabwela walikuwa na familia ambazo siyo BMW (Baba, Mama na Watoto), zenye viwango duni vya maisha. Kitendo cha Makabwela kuiga BMW za Wakulu, kilipelekea kuimarika kwa taifa la Warumi, kiasi cha kuwa taifa kubwa lenye himaya ambayo matokeo (legacy) yake tunaiona hadi leo.

Kwa sasa, hatua ya utandawazi ilipofikia, pana mataifa machache yanayoweka msimamo dhidi ya utandawazi wa kufuta utaifa, na mengine yanaelekea ukabwela:

1. China -- hii inajikita kuhakikisha familia ni BMW, na inabaki kama taifa huru. Vurugu za Hong Kong, IMHO, ni baina ya kambi mbili za utaifa vs utandawazi. Inaonekana think-tanks za China ziko vizuri kuusoma upepo unapoelekea.

2. Russia -- hawa ni kama teja lililoacha unga: zamani walipitia michakato yote ya kuua utaifa, na ya kuvunja familia ya aina ya BMW -- na sasa wanajitahidi kurejea kwenye misingi. Uelekeo wao ni wa kujenga utaifa na familia, lakini wameachwa na mbali na mshirika wao China.

3. India -- hawa wamewekewa miundombinu ya kubomoa familia ya BMW -- na wanaelekea kuporomoka kama taifa kwa kasi.

4. Marekani -- taifa kubwa. Lakini na lenyewe limewezwa na Cultural Marxists waliofanikiwa kuvunja misingi ya familia ya BMW, ubepari na utaifa. Kuchaguliwa kwa Donald Trump ni abberration tu kwenye mchakato huo (ndio maana kampeni yake ilikuwa ni MAGA - akitaka kurudisha utaifa Marekani), lakini yeye ni wa mrengo wa kulia ya mbali; na atakayefuata baada yake atakuwa ni wa mrengo wa kushoto ya mbali.

5. Nchi za Kiafrika Kusini ya Sahara -- hizi nyingi ni Bendera Fuata Upepo.

6. Uingereza na nchi nyingine za Ulaya -- Nazo zimewezwa na Cultural Marxism na ziko njia moja kupotea kama taifa.

7. Korea Kusini -- Hii ina viashiria vya kupitiwa na upepo wa Cultural Marxism na japo kwa sasa haijadumbukia sana humo kama nchi nyingine zilizokuwa za Kibepari.

But I digress... EU and its backers will never allow UK to get out of it, hasa pale inapomaanisha kuondoka kwa UK ndio mwanzo wa kuvuruga mafanikio makubwa ya EU iliyoyafikia kuelekea kuwa The United States of Europe.
 
Mkuu Mlenge

Kura ya maoni ya Brexit ilikuwa na vitu viwili, Yes kwa maana ya kujitoa na No kwa maana ya kutojitoa EU. Wananchi walio wengi walipiga kura ya Yes kwa kutazama matokeo yalivyo

Kura ya Yes ikaheshimiwa ''by triggering the article 50 of the Lisbon Treaty''.
EU wakapokea ombi la article 50 kwamba UK inajitoa, hivyo ukapangwa muda wa kujitoa

UK wakakubali kulipa gharama za michango yao ndani ya EU kwa mujibu wa mkataba nakupewa tarehe ya kumalizana na EU ambayo ilikuwa ni October 30.

EU kama nilivyoeleza walichukua maamuzi yatakayohakikisha nchi nyingine wanachama hazichukui uamuzi wa UK kwa kudhani zitapata fadhila za EU zikiwa nje ya EU.

UK wanataka kupata fursa ya soko la EU kwa kile kinachoitwa common market
Wanataka kupata fursa za Raia kunufaika na uwepo wa EU wakati wakiwa si wanachama

Mfano, bandari za UK zimekuwa lango la ku access EU market kutoka masoko ya dunia
Nje ya EU, Bandari hizo zitapoteza mapato ikiwemo ajira za wananchi ambao ni wa UK

UK wanashauri N. Ireland iendelee kuwa mwanachama wa EU.
EU wanasema huwezi kuwa na sehemu ya nchi ndani ya EU hilo litaipa UK fursa ile ile

Ugomvi ukaondoka EU na kuwa wa ndani ya UK kama tulivyoeleza hapo awali

Sasa baada ya BREXIT kuheshimiwa kwa kutimiza matakwa ya article 50 of Lisbon treaty kazi ya kuandaa sheria zinazohusiana na kujitoa EU si za wananchi ni za Bunge, House of common. Hapo ndipo Brexit ilipotua ndani ya House kisheria kama watunga sheria

EU wameridhia kabisa kwamba UK inaweza kuondoka bila kuwa na mahusiano na EU

Kwa maana hiyo EU haina mkono wowote kwa ugomvi wa ndani ya UK

Kuchelea hilo, kujitoa bila kuwa na mkataba mahususi na EU kumeligawa Bunge.

Hilo limefanya kazi ya kupata vote kutoka quorum ya 650 MPs kuwa ngumu.

Ikitafutwa kitu kinachokubalika kwa pande zote, BREXIT DEAL.

Hii iliundwa ili kuhakikisha UK inajitoa kukidhi matakwa ya wananchi, lakini pia wahafidhina.

Hilo halitoshi kupata majority vote, Brexit deal imelenga pia kuwapa kidogo pro-EU

Kitu kinachounganisha makundi yote ni ukweli kuwa huwezi kuwa ndani ya Europe, halafu ukawa huna mahusiano na EU.

Wote wanataka kuwepo na ''kamkataba' na EU. Tatizo ni je,Brexit deal inakubalika kwa wote?

Kwahiyo si tatizo la EU hata kidogo, UK wana option ya kuondoka bila deal.

Nifanyaje ili nami niwe naelezea vitu kwa kina na maarifa kama wewe?
 
Nifanyaje ili nami niwe naelezea vitu kwa kina na maarifa kama wewe?
Mkuu unaweza sana tena utaeleweka vizuri. Baadhi ya mambo ya kuzingatia ni;
Kwanza ondoa uoga, pili jifunze jambo kabla ya kulisemea, tatu fuatilia habari unazozipenda, nne, ujue kukosolewa si kosa ni sehemu ya weledi na kwamba miongoni mwetu hakuna aliyemtimilifu.
Anza taratibu ninauhakika utaweza zaidi
 
BREXIT NA BREXIT DEAL ZAPELEKEA UCHAGUZI

Katika zile ''option'' mbili tulizoeleza huko nyuma moja ndiyo mwelekeo wa UK ndani ya EU

Kwa marejeo, tulisema kuna njia mbili, kuvunja bunge ili kupata Wabunge wapya huenda kukawa na mtazamo mpya wa Brexit deal, au kuiondoa UK bila Brexit deal

Johnson Boris , Waziri mkuu aliiwaahidi Wanchi kwamba ataitoa UK bila Brexit bila deal.
Maana yake ni kuwa na Brexit tu na kuachana na EU bila mpango wowote
Aliahidi ikifika October 30 atakamilisha kazi hiyo

October imefika na hakuweza. Njia moja aliyodhani itafanya kazi ni kuliahirisha Bunge kwa muda mrefu ili ikifika October 30 aitoe UK bila majadiliano kwa maana bila kura ndani ya Bunge

Boris hakujua kisheria hilo lisingewezekana, wapinzani walipokwenda mahakamani walishinda.

Hoja kubwa ilikuwa ni kuwa hilo ni suala la nchi na Wabunge walipaswa kushiriki.
Kuliahirisha Bunge kwasababu hiyo haikuwa halali. Boris akapigwa chini

PM Boris akawa hana ujanja maana mahakama imesema, ilidbidi arejee katika Bunge lile lile alilotaka kuliruka akiwa na Brexit deal mkononi. Tatizo ikabaki pale pale, kura hazitoshi.

Boris akarejea katika option zilizopo ambapo moja ni kuitisha uchaguzi wa mapema.

Uchaguzi huo ulipingwa na Labor ambao ni Wapinzani wakuu ndani ya Bunge.

Hata hivyo Labor wamekubaliana na uchaguzi kwasababu hata wao hawana mbadala wa kuiondoa UK katika mkwamo huo wa kisiasa ''political impasse''

Uchaguzi umepangwa Dec 12, 2019 ikiwa ni muda nadra sana katika historia ya nchi hiyo.

Bunge litakapoitishwa kutakuwa na mabadiliko ya aina ya Wabunge na idadi ndani ya vyama.

Boris amelazimika kuomba radhi kwa wananchi kwa kushindwa kuitoa UK October 30 akijua hilo linaweza kutumika kama fimbo ya kumchapa katika sanduku la kura.

EU nao wamewapa muda zaidi hadi January 30 kufikia maafikiano ikiwa wanataka kuondoka bila brexit deal au wanataka Brexit deal na ya namna gani.

Tatizo la Brexit deal ni lipi?
Tatizo lipo kwa UK hasa kwa ''nchi'' zinazounda Union jack(Bendera yao).

Haijulikani Scotland wataamua nini, N.Ireland watasema nini, Great Britain watasema nini

EU wanasema UK kama inataka kubaki katika common market, ihakikishe nchi za EU zina access market yao. Hilo ni tatizo kwani ndicho chanzo cha Brexit

EU hawataki kuwa na N.Ireland au Scotland tofuati kwani Great Britain itatumia mwanya huo ku access common market wakati ikiweka kauzibe kwa wananchama wa EU

No deal maana yake ni moja, UK itakuwa ''kisiwa' ndani ya EU jambo litakalozorotesha uchumi
Wahafidhina wanasema UK inaweza bila EU. Tatizo miongoni mwao ni kuwa wahafidhina wa vijijini wanaamini UK ya Malkia na Pound sterling, hawa wengi hawana weledi mpana.

Wahafidhina matajiri wanasema yes wajitoe lakini kuwe na deal ili ku access common market, people, goods and capital movement

Waliberali wanasema hilo ni kuumiza wananchi, ima warudi EU au kuwe na Brexit Deal

Tusemezane
 
BREXIT NA BREXIT DEAL ZAPELEKEA UCHAGUZI

Katika zile ''option'' mbili tulizoeleza huko nyuma moja ndiyo mwelekeo wa UK ndani ya EU

Kwa marejeo, tulisema kuna njia mbili, kuvunja bunge ili kupata Wabunge wapya huenda kukawa na mtazamo mpya wa Brexit deal, au kuiondoa UK bila Brexit deal

PM Boris akawa hana ujanja maana mahakama imesema, ilidbidi arejee katika Bunge lile lile alilotaka kuliruka akiwa na Brexit deal mkononi. Tatizo ikabaki pale pale, kura hazitoshi.

Boris akarejea katika option zilizopo ambapo moja ni kuitisha uchaguzi wa mapema.

Uchaguzi huo ulipingwa na Labor ambao ni Wapinzani wakuu ndani ya Bunge.

Hata hivyo Labor wamekubaliana na uchaguzi kwasababu hata wao hawana mbadala wa kuiondoa UK katika mkwamo huo wa kisiasa ''political impasse''

Uchaguzi umepangwa Dec 12, 2019 ikiwa ni muda nadra sana katika historia ya nchi hiyo.

Bunge litakapoitishwa kutakuwa na mabadiliko ya aina ya Wabunge na idadi ndani ya vyama.

Tatizo la Brexit deal ni lipi?
Tatizo lipo kwa UK hasa kwa ''nchi'' zinazounda Union jack(Bendera yao).

Haijulikani Scotland wataamua nini, N.Ireland watasema nini, Great Britain watasema nini

EU wanasema UK kama inataka kubaki katika common market, ihakikishe nchi za EU zina access market yao. Hilo ni tatizo kwani ndicho chanzo cha Brexit

EU hawataki kuwa na N.Ireland au Scotland tofuati kwani Great Britain itatumia mwanya huo ku access common market wakati ikiweka kauzibe kwa wananchama wa EU

No deal maana yake ni moja, UK itakuwa ''kisiwa' ndani ya EU jambo litakalozorotesha uchumi
Wahafidhina wanasema UK inaweza bila EU. Tatizo miongoni mwao ni kuwa wahafidhina wa vijijini wanaamini UK ya Malkia na Pound sterling, hawa wengi hawana weledi mpana.

Wahafidhina matajiri wanasema yes wajitoe lakini kuwe na deal ili ku access common market, people, goods and capital movement

Waliberali wanasema hilo ni kuumiza wananchi, ima warudi EU au kuwe na Brexit Deal

Tusemezane
TATHMINI YA UCHAGUZI WA UK itafanywa kwa kuangalia nukuu za bandiko hapo juu.
 
TATHMINI YA UCHAGUZI WA UK

WAHAFIDHINA WAIBUKA KIDEDEA

NJIA KUELEKEA BREXIT INAZIDI KUPANUKA

Bandiko#58 kama lilivyonukuliwa kwa mkazo wa wino#59 limejieleza kama ilivyodhaniwa kutokea

Kwamba, mkwamo 'impasse'' wa Brexit si Labor wala conservatives waliokuwa na suluhu.
Njia iliyobaki ilikuwa kuitisha uchaguzi, na kama tulivyosema matokeo yatakuwa na mabadiliko ya aina ya Wabunge na idadi yao.

Aina na idadi ni muhimu kuzingatia katika mjadala, tutajadili hili mbele ya safari ni kwanini.

Bunge la UK lina wajumbe 650.Kwa nchi ambazo kiongozi hutokana na idadi ya Wabunge kuna mambo matatu yanatokea;

1. Kuunda serikali kwa kupata vingi zaidi ya jumla ya Upinzani wote ''absolute majority''
2. Kuunda serikali kwa kupata idadi zaidi ya Wapinzani ''mmoja mmoja'' Minority
3. Kuunda serikali kwa kupata vingi, Wapinzani wakiungana idadi inapungua '' coalition gov'

Tunaeleza haya ni muhimu kuyajua ili kujua nini kinafuata siku za baadaye.

Wabunge ni 650.
Chama kitakachopata viti 325 itabidi kitafute mbunge japo 1 ili kupata 326 ya maamuzi.

Hapa ndipo kunapotokea serika Mseto(coalition) kama # hapo juu inavyoonyesha

Chama kitakachopata chini ya 325 lakini zaidi ya vyama vingine kimoja kimoja kitakuwa na Minority gov. Na hapa pia kunahitajika 'coalition'' ili maamuzi yapite Bungeni(#2Minority)

Chama kitakachopata zaidi ya 326 kitakuwa na maamuzi bila kushirikisha chama kingine

Hata Wapinzani wakiungana idadi ni chini ya 325. Hapa ndipo absolute majority inapokuja

Kabla ya uchaguzi wa Jana Dec 12,2012 Conservatives walikuwa na viti 317.

Maana yake walikuwa na minority gov kwani Wapinzani wakiungana inakuwa zaidi ya 333.

Uchaguzi wa Dec 12 umetoa matokeo ya Conservatives viti 365. ''absolute majority''.

Kwamba, wanaweza kutoa maamuzi na kuyapitisha bila Wapinzani.

Matokeo yanaonyesha chama kikuu cha Upinzani cha Labor kupoteza Wabunge zaidi ya 50

Idadi hiyo imechukuliwa na conservative na pia kutoka vyama vingine vidogo na kuipa 365

Hapa kuna hoja ya aina ya Wabunge. Kwamba, wale Labor wamepoteza, conservative wameongeza hivyo conservative wameongeza pengo kwa kuchukua viti vya Labor na vyama vingine, Wabunge wanaounga mkono Boris na Conservative.

Ukirudi katika bandiko#59 katika wino mwekundu, tulisema uchaguzi ulilenga kupata Wabunge na kupata AINA ya Wabunge.

Ilikuwa ni bahati nasibu kwa Boris ambayo imelipa sana

Boris Johnson na Conservatives wamepanua wigo wa BREXIT
Haina maana wamefanikiwa, la hasha, wameongeza uwezekano wa kushinda BREXIT

Kwanini tunasema uwezekano?

Ni kwamba conservatives 365 wakipiga kura ya BREXIT hilo litatokea.
Lakini kura ya BREXIT ni non-binding (kwamba si ya kufuata chama).

Kura zote za nyuma conservative walishindwa kwasababu baadhi ya Wabunge wao waliungana na Wapinzani tena hadi kufikia idadi ya 150.

Lakini aina ya Wabunge inampa uwezekano mkubwa, hata akipoteza 39 bado atafanikiwa

Matokeo hayo ya jana yanakuja na matatizo mengine.

Labor Wamepoteza Wabunge, UKIP na BREXIT party ya Nigel Farage hawakupata kiti, Liberal Wamepata kidogo, green party n.k. Kazi ipo Scotland ambapo SNP wameongeza viti

Hili ni kasheshe nje ya BREXIT kwani msala wa Scotland kujiondoa UK unarudi upya

Wakati huo huo N.Ireland wanasema wao wanataka kubaki EU.

Scotland na Ireland wakikomaa kutakuwa na songombingo jingine ''political turmoil''

Boris Johnson ana njia nyeupe ya kuiondoa UK kutoka EU(BREXIT)

Hakuna masika yasiyo na Mbu. Uwezekano wa kuvunjika UK na Uimara wa ''Union Jack'' unatishiwa. Kwahiyo ushindi wa Boris Johnson jana ni bittersweet

Tusemezane
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom