Duru: Matukio na habari za Dunia

MGOGORO WA IRAN NA US

Hali katika mashariki bado ni tete na hainekani kuimarika katika siku za usoni
Mazishi ya Qassem, Kamanda wa kikosi cha mapinduzi yamefanyika nchini Irani

Umati uliojitokeza ni mkubwa kuwahi kuonekana katika miaka ya karibuni ukiachilia wakati wa kurejea kwa kiongozi wa kiislam Ayatollah Khomeni. Umati ulijawa na jazba ya kisasi

Kama tulivyowahi kusema si rahisi Iran kujibu mapigo kwa wakati huu wa mshtuko mkubwa.
Iran wanafahamu Marekani watakuwa wamejiandaa kukabiliana na kisasi chochote

Kwingine mashariki ya kati kama Lebanon, kauli za kisasi ndizo zilizotanda kumuadhimisha Qassem. Viongozi kama Nasrallah wa Hezbollah na makundi mengine wameapa kisasi

Hasira za watu zimeelekezwa kwa Israel pia ambayo nayo imesifu mauaji hayo
Inaeleweka shambulizi hilo limechagizwa pia na Israel inayotaka kuona Iran inapunguzwa nguvu

Israel inahofia kuwa nguvu za Iran katika mashariki ya kati zitaiweka katika wakati mgumu
Kwamba, makundi kama Hezbollah na Hamas yatapata nguvu licha ya Iran yenyewe

Nchini Iraq Bunge limeatoa azimio kwa majeshi yaMarekani kuondoka nchini humo
Marekani inajikuta katika wakati mgumu kimkakati.

Kuondoka Iraq kunapunguza nguvu za Marekani kimkakati (strategic position) kwasababu Iran na Iraq ni majirani, hivyo uwepo wa majeshi yake Iraq unafanya kazi kuwa rahisi .

Hofu ya Marekani ni kuwa kuondoka Iraq kutatoa nafasi kwa Shia wa Iraq kuungana na wenzao wa Iran, wale wa Qatar na kwingineko katika mashambulio dhidi ya Marekani kama ikitokea.

Rais Trump anatishia kuweka vikwazo Iraq, wachunguzi wanasema hilo litaileta mashariki ya kati karibu zaidi kwa kuwa na ''adui'' mmoja kwa wote

Marekani isingependa kwenda vitani na Iran kutokana na funzo la Iraq.
Hofu kubwa ni kuhusu mihemuko ya Rais Trump anayeweza kuamua jambo bila kufikiri

Iran sasa imejitoa katika nuclear deal na nchi za Ulaya ingawa inasema ipo tayari kuzungumza
Shambulio la Qassem limewapa nafasi (upper hand) katika majadiliano na nchi za Ulaya

Lengo na mkakati wa Marekani ni upi? Je, leo baada ya Qassem ipo salama kuliko jana?

Tusemezane
 
IRAN YASHAMBULIA KAMBI YA MAREKANI
HALI NI TETE, VITA YA KISAIKOLOJIA INAENDELEA

Tofauti na ilivyofikiriwa Iran imeshambulia kambi ya kijeshi ya Al-Asad air base nchini Iraq.

Shambulio hilo limeonyeshwa wazi na TV na kwamba kikosi cha kulinda mapinduzi kimefanya.
Hakuna majeruhi walioripotiwa kutoka upande wa Marekani au Iraq kufuatia shambulio hilo.

Kwasiku mbili Rais Trump amewatisha Iran kuhusu majibu ya kipigo ikiwa watalipiza kisasi.
Hili lilikuwa kuwatisha Wairan kisaikolojia ili kuzuia shambulio na pengine vita.

Iran nayo imeshambulia haraka tena kwa makombora kutoka ndani ya Iran kwenda Iraq.

Inaelezwa makombora hayo yenye usahihi yameelekezwa kwa makusudi pembeni.

Hili ni kuzuia mauji ya askari ambayo huenda yangemchefua Trump na kuanza piga piga.

Kisaikolojia Iran inamweleza Marekani ina uwezo wa kumfikia kwa makombora ikizingatiwa kuna vituo na manowari nyingi za Marekani mashariki ya kati.

-Shambulio limelenga kutuliza hasira za Wairan na washirika wake eneo la mashariki ya kati

-Shambulio ni kuwaeleza Iraq, kuwakumbatia Wamarekani, vita itapiganwa Iraq na si Iran

-Iran imetangaza, shambulio lolote dhidi yake litajibiwa kwa shambulio nchi za UAE na Israel.

Rais Trump atatoa kauli kuhusu shambulio hilo asubuhi ya leo.

Zaidi ya hayo kutangaza shambulio dhidi ya Israel ambayo ni mshirika wa Marekani linalenga kuivuta Israel katika mgogoro, jambo litakalowaunganisha Waarabu na kushambulia Marekani

Rais Trump ana machaguo kadhaa.Marekani ina nguvu za kijeshi na kiteknolojia kuiharibu Iran.

Tatizo ni pale itakapotokea Iran ikaiotea Marekani hata kuzamisha manowari moja

Hadithi ya vita itakuwa ile ya Israel kuvuruga Lebanon lakini mwisho wa siku ikabainika Israel na walikiri wenyewe kuwa vita ile walishindwa. Kwa silaha na teknolojia Hezbollah waliwasumbua.

Chaguo la pili ni kuanzisha vita na kuivuta Marekani katika vita nyingine kama ile ya Iraq.
Marekani itavuja damu taratibu lakini kwa muda mrefu kama ilivyo ya Iraq

Kuelekea uchaguzi mkuu mwezi November, chaguo la vita halitamsaidia Rais Trump

Chaguo jingine ni kuingia vitani na Iran na kuwapiga.
Madhara si Iran kuwajibu bali kuvuta makundi kama Hezbollah, Houth na mengine dhidi ya Marekani na masilahi yake.

Chaguo la mwisho ni kuingia vitani na Iran na kuiweka Israel katika majaribu makubwa.

Israel inaigopa sana Iran, kwa wanaofuatilia uzi huu tulieleza kuwa Marekani inatafuta sababu za kumpiga Iran baada ya kujitoa katika nuclear deal iliyopingwa sana na Israel

Hapa tunamaanisha nini? Kwamba, nguvu za kuipiga Iran watakavyo Markani wanazo.

Tatizo ni madhara yakayofuata baada ya kufanya hivyo.

Bado kuna kumbu kumbu za kumuondoa Ghadafi na Saddam ambapo nchi husika hazijatulia.

Kwa Iran, habari ni tofauti.

Tusemezane
 
Haitakuwa rahisi Iran kujibu mapigo haraka, kitakachotokea ni kuchukua muda na kupitia makundi yao yaliyosambaa mashariki ya kati kuna jambo litatokea
They(Iran) have proved you wrong!

Hakukuwa na namna zaidi ya kutuliza hasira za mamilioni ya wairan waliojitokeza kumuaga kamanda wao zaidi ya kulipiza kisasi proportionately kwa kuanzia kupiga kambi mbili za US ndani ya Iraq.

Kama mifumo ya ulinzi ya US imeshindwa kudhibiti makombora yale ni hatari kwa jeshi la Marekani. Lakini kama US wamezima mitambo ya ulinzi kwa makusudi ili mabomu ya Iran yafike kwenye lengo, basi US ametumia busara sana maana kwa kiasi hii imepunguza kidogo hasira za baadhi ya wairan na raia wengine kule Mashariki ya kati.
 
IRAN YASHAMBULIA KAMBI YA MAREKANI
HALI NI TETE, VITA YA KISAIKOLOJIA INAENDELEA

Tofauti na ilivyofikiriwa Iran imeshambulia kambi ya kijeshi ya Al-Asad air base nchini Iraq.

Shambulio hilo limeonyeshwa wazi na TV na kwamba kikosi cha kulinda mapinduzi kimefanya.
Hakuna majeruhi walioripotiwa kutoka upande wa Marekani au Iraq kufuatia shambulio hilo.

Kwasiku mbili Rais Trump amewatisha Iran kuhusu majibu ya kipigo ikiwa watalipiza kisasi.
Hili lilikuwa kuwatisha Wairan kisaikolojia ili kuzuia shambulio na pengine vita.

Iran nayo imeshambulia haraka tena kwa makombora kutoka ndani ya Iran kwenda Iraq.

Inaelezwa makombora hayo yenye usahihi yameelekezwa kwa makusudi pembeni.

Hili ni kuzuia mauji ya askari ambayo huenda yangemchefua Trump na kuanza piga piga.

Kisaikolojia Iran inamweleza Marekani ina uwezo wa kumfikia kwa makombora ikizingatiwa kuna vituo na manowari nyingi za Marekani mashariki ya kati.

-Shambulio limelenga kutuliza hasira za Wairan na washirika wake eneo la mashariki ya kati

-Shambulio ni kuwaeleza Iraq, kuwakumbatia Wamarekani, vita itapiganwa Iraq na si Iran

-Iran imetangaza, shambulio lolote dhidi yake litajibiwa kwa shambulio nchi za UAE na Israel.

Rais Trump atatoa kauli kuhusu shambulio hilo asubuhi ya leo.

Zaidi ya hayo kutangaza shambulio dhidi ya Israel ambayo ni mshirika wa Marekani linalenga kuivuta Israel katika mgogoro, jambo litakalowaunganisha Waarabu na kushambulia Marekani

Rais Trump ana machaguo kadhaa.Marekani ina nguvu za kijeshi na kiteknolojia kuiharibu Iran.

Tatizo ni pale itakapotokea Iran ikaiotea Marekani hata kuzamisha manowari moja

Hadithi ya vita itakuwa ile ya Israel kuvuruga Lebanon lakini mwisho wa siku ikabainika Israel na walikiri wenyewe kuwa vita ile walishindwa. Kwa silaha na teknolojia Hezbollah waliwasumbua.

Chaguo la pili ni kuanzisha vita na kuivuta Marekani katika vita nyingine kama ile ya Iraq.
Marekani itavuja damu taratibu lakini kwa muda mrefu kama ilivyo ya Iraq

Kuelekea uchaguzi mkuu mwezi November, chaguo la vita halitamsaidia Rais Trump

Chaguo jingine ni kuingia vitani na Iran na kuwapiga.
Madhara si Iran kuwajibu bali kuvuta makundi kama Hezbollah, Houth na mengine dhidi ya Marekani na masilahi yake.

Chaguo la mwisho ni kuingia vitani na Iran na kuiweka Israel katika majaribu makubwa.

Israel inaigopa sana Iran, kwa wanaofuatilia uzi huu tulieleza kuwa Marekani inatafuta sababu za kumpiga Iran baada ya kujitoa katika nuclear deal iliyopingwa sana na Israel

Hapa tunamaanisha nini? Kwamba, nguvu za kuipiga Iran watakavyo Markani wanazo.

Tatizo ni madhara yakayofuata baada ya kufanya hivyo.

Bado kuna kumbu kumbu za kumuondoa Ghadafi na Saddam ambapo nchi husika hazijatulia.

Kwa Iran, habari ni tofauti.

Tusemezane
Nguruvi,
Nimekuwa nikiifuatilia Iran from time to time tangu 2011 au 2012 walipoweza kudungua ndege mbili zisizo na rubani za Israel ambazo kwa kawaida hazionekani kwenye rada, halafu baadae waliweza kui divert na kuishusha drone ya Marekani ikiwa nzima baada ya kufanikiwa ku intercept mawasiliano yake. Ninachokiona japo sina hakika kama niko sahihi ni kuwa:
1. Iran wameendelea sana kijeshi japo si kiasi cha kuishinda Marekani au Israel lakini yeyote atakayejaribu vita na Iran atapata ushindi wenye majuto makubwa na ya muda mrefu. kwa maana nyingine huyu ni mbabe anayekuwa kwa haraka sana mashariki ya kati na ni tishio kwa Marekani, Israel na washirika wao kama Saudia.
2. Rais Trump anafahamu vikwazo vya tangu 1979 havikufanikiwa kuidhoofisha Iran kiasi cha kushindwa vita kwa urahisi. Na anafikiri labda katika utawala wake atumie njia zozote kuhakikisha anauondoa utawala wa kiislam ili mbabe abaki Israel peke yake. lakini si kuuondoa tu bali kuruhusu makundi ya kigaidi ambayo yatahakikisha Iran haitulii kama ilivyo Iraq, Syria na Libya.
3. Inafahamika kwamba tangu kabla ya 2010 Israel imekuwa ikiishinikiza Marekani iishambulie Iran, lakini Marekani siku zote imesita kufanya hivyo. Hofu ya Israel ni maendeleo ya technologia ya Iran ambayo huenda ikaisumbua Israel baadae.
4. Siamini kama kweli Trump alitaka kumuua Soleiman halafu iishie hapo. nadhani anatafuta sababu za kuanzisha vita na Iran ili apate fursa ya kuisambaratisha Iran na kisha kuweka kibaraka wao.
5. Baada ya mashambulizi ya Iran hakujatolewa habari za uhakika kuhusu madhara ya mashambulio hayo, lakini swali la msingi ni je mfumo wao kutungua makombora wa Marekani kwa nini haukutumika? au tuseme haukugundua makombora yote 22?
6. Iran imechokezeka. na huenda Trump akatumia mwanya huu kucheza kamari na Iran. Kamari ambayo haitabiriki.
mwisho nimekuwa nikivutiwa sana na diplomasia ya Iran ikiongozwa na Zariff, laiti dunia ingekuwa inamsikiliza huenda mashariki ya kati pangekuwa salama.
 
"kamili, post: 34030770, member: 37121"]1. Iran wameendelea sana kijeshi japo si kiasi cha kuishinda Marekani au Israel, ni mbabe anayekuwa kwa haraka sana mashariki ya kati na ni tishio kwa Marekani, Israel na washirika wao kama Saudia.
Kamili Iran ni mbabe wa muda mrefu. Kilichomzuia ni uwepo wa kibaraka wa Marekani Mfalme Shah.
Baada ya 1979 Imam Khomeni alijaribu kuibadilisha Iran na kuirudisha katika ubabe.

Vita ya Iraq na Iran ilichagizwa sana na Marekani na hasa Israel.
Baada ya msaada wa mafunzo Saddam akawageuka Wamarekani na kuwa tishio kwa Israel
Kilichofuata ilikuwa kumtafutia sababu na kwa bahati mbaya Saddam akaingia katika mtego.

Baada ya Saddam ambaye unakumbuka alituma Qasam kule Israel, Iran ilichukua ukanda.
Tofauti na Iraq, Iran inawekeza sana katika elimu siyo ya jeshi hata sayansi na teknolojia.

Angalia popote duniani, Shia ni wazuri sana katika mambo ya kielimu ukilinganisha na wenzao kama Sunni au Sufi.

Iran wametumia uwezo wao wa fedha kusaidia makundi yanayohusiana nao na kujitanua sana mashariki ya kati. Jambo hilo limetia hofu mataifa mawili, Israel na Saudi Arabia.

Israel inaona makundi kama Hezbollah na Hamas yanayopata ufadhili wa Iran ni tishio kubwa.
Vita ya Israel na Lebano ya Imam Nasrallah miaka 10 iliyopita ili ieleza Israel kuna tatizo.

Jitihada za Israel ni kutaka kuona Iran inasambaratishwa na hasa suala la Nuclear
Kama unafuatilia nyuzi zetu tumeeleza mara nyingi, Marekani ilikuwa inatafuta sababu za kumpiga Iran si kwasababu ni tishio bali ''maagizo'' ya Israel

Saudia ina hofu kwamba kujitanua kwa Iran ni kuruhusu Shia kutawala mashariki ya kati.
Hofu siyo Shia kutawala maeneo ya Sunni, bali ushawishi wa Shia dhidi ya Saudia Kingdom.
Wasi wasi wa Saudia si kwa masilahi ya Sunni au makundi mengine, ni masilahi ya Kifalme.

Kwa kuelewa hilo, Wasaudia ambao miaka dahari wameongoza jamii ya Waislam dhidi ya Israel wamengana na Israel ili kumkabili Iran. Haya si kwa amasilahi ya dini ni kwa kulinda Kingdom tu.
Saudia wamewatosa Wapalestina kwasababu tu ya kulinda ufalme.

Kwamba Israel ina nguvu, kuna hoja mbili. Israel wana utalaamu na teknolojia ya juu sana.
Kijiografia, ukubwa wa eneo na population Israel hana nguvu kwa Iran bila msaada wa Marekani. Ndiyo maana Israel wanataka Iran ashambuliwe, wao wenyewe hawasimami .

Kwamba, Iran imeendelea hilo halina mjadala. Wana teknolojia na utaalam sana hasa ukizingatia wapo katika vikwazo kwa miaka zaidi ya 10.
 
"kamili, post: 34030770, member: 37121"]
2. Rais Trump anafahamu vikwazo vya tangu 1979 havikufanikiwa kuidhoofisha Iran kiasi cha kushindwa vita kwa urahisi. Na anafikiri labda katika utawala wake atumie njia zozote kuhakikisha anauondoa utawala wa kiislam ili mbabe abaki Israel peke yake. lakini si kuuondoa tu bali kuruhusu makundi ya kigaidi ambayo yatahakikisha Iran haitulii kama ilivyo Iraq, Syria na Libya.
Kosa la Trump ni kuiondoa Marekani katika nuclear deal. Hili Rais Trump alilifanya kwa chuki tu dhidi ya Obama bila kuwa na plan.
Iran ina survive vikwazo na kuelekea uchaguzi Trump ataulizwa kumepatikana nini baada ya kuiondoa US katika Deal? Tena alifanya hivyo bila washirika wa Ulaya.

Trump aisukumwa na vitu viwili, chuki dhidi ya Obama na Israel ikatumia mwanya huo.
Tatizo kwa Trump ni kuwa ali kampeni kuondoa majeshi middle east, atawaambia nini Wamarekani kuelekea uchaguzi?

Kumuua Qassem ni kuchukua credit kwamba anafanya jambo, hata hivyo huko Marekani watu wanahoji sana hatua alizochukua.

Changamoto inayomkabili sasa hivi ni kuondoka au kubaki Iraq.
Kuondoka ni kupoteza ukaribu na Iran. Kubaki ni kuanika askari katika mazingira hatarishi.

Utaona, baada ya shambulio la Qassem , Iran wanasema hakuna nuclear deal tena na ikibidi watarudi mezani na nchi za Ulaya.

Leo Trump anaziangukia nchi za Ulaya zijihusishe baada ya kuiona hatari inayomkabili mbeleni.
3. Inafahamika kwamba tangu kabla ya 2010 Israel imekuwa ikiishinikiza Marekani iishambulie Iran, lakini Marekani siku zote imesita kufanya hivyo. Hofu ya Israel ni maendeleo ya technologia ya Iran ambayo huenda ikaisumbua Israel baadae.
Iran ni homa kwa Israel. Jana Iran walionya kuishambulia tena watajibu mapigo dhidi ya Israel.
Israel inafahamu bila Marekani ya Hezbollah yatakuwa madogo, Iran ni Taifa kamili
5. Baada ya mashambulizi ya Iran hakujatolewa habari za uhakika kuhusu madhara ya mashambulio hayo, lakini swali la msingi ni je mfumo wao kutungua makombora wa Marekani kwa nini haukutumika? au tuseme haukugundua makombora yote 22?
Jana asubuhi kabla ya shambuli mfumo wa Marekani ulibaini ''movement'' za silaha ndani ya Iran na ilitangazwa na TV zote kubwa za Marekani.

Mitambo ya Marekani hazimwi na hakuna sababu za kuizima.
Kazi zake ni zaidi ya kuiangalia Iran.

Kumbuka middle east kuna Mchina na Russia na hivyo hakuna nafasi ya kuzima mitambo ili isione makombora ya Iran!! Yaani wanajua makombora yanakuja halafu wanazima mitambo!
Hilo linawasaidiaje? Bado wangeweza kuangalia bila kufanya lolote, wana uwezo huo.

Habari hizo ni hadithi za za kuokoteza vijiweni zisizo na chembe ya weledi

Habari zilizopo na ambazo zimethibitishwa ni kuwa Iran iliwataarifu Iraq kuhusu makombora.

Marekani ilitaarifiwa na Iraq pamoja na ukweli kuwa makombora yaliporushwa mitambo ya Marekani ilibaini trajectory na inatokea wapi. Uwezo wa Marekani kiteknolojia ni mkubwa sana

Iran nao walijua mauaji au uharibifu utasababisha madhara makubwa kwao.

Kumbuka kuna askari na manowari za Marekani kuanzia Israel, Saudia, Iraq, Qatar , UAE na hivyo Iran ingekuwa katika wakati mgumu. Hawakutaka vita.

Walichotaka ni mambo mawili, kwanza, kuwashusha morali watu wao walioghadhabika.

Pili, kuwaeleza Marekani na Israel kuwa makombora yao yanafika wanapotaka middle east.

Iran ina makombora ya masafa mafupi na Marefu na yanayoongozwa katika kufanya precision.

Yale ya jana si zana kamili, ni taarifa tu ya uwezekano wa kufikia manowari na kambi zao

Kwanini missile hazikuzuiwa na ''iron dome'' kama za Israel inajieleza.
Missile za Iran kama Shahab zimetengenezwa kitaalamu sana siyo ''Katushi'' za Hamasi

Wamarekani wana uwezo wa kuzizuia lakini si rahisi kiasi hicho.
Wanachoweza kufanya ni kushambulia vyanzo kabla ya makombora hayajarushwa.
 
''VITA HAINA MACHO''

Ni msemo wa Wahenga kimaanisha vita ni vurugu zisizochagua nani yupo wapi au kwanini.

Hali iliyokuwepo mashariki ya kati na iliyopo ni ya ''tension'' sana baada ya kuawawa Qassem

Qassem Soleiman alikuwa ni kamanda wa vikosi, alijulikana na wala hakujificha
Uratibu wake wa shughuli za vikundi vinavyosaidiwa na Marekani ulijaulikana

Qassem aliwapa tabu sana Waisrael kwa kufanya makundi kama Hezbollah kuwa na nguvu.
Alikuwa kiungo muhimu sana cha jeshi la Iran na mshauri mkuu wa masuala ya ulinzi

Baada ya kifo chake inaelezwa kuwa Qassem aliweza kuwadhibiti makanda wa vikosi mbali mbali wenye misimamo mikali na wasio na subira.

Marekani na Tawala ilizopita miaka takribani 20+ wanamjua Qassem Soleiman.

Suala la kumuua halikuwepo kwa kuchelea athari zinazoweza kujitokeza ambazo ni kubwa kuliko kumuondoa peke yake.

Kitendo cha kumuua kimeleta taharuki mashariki ya kati na Duniani kwa namna mbali mbali.

Kubwa ni kutunguliwa kwa ndege Boeing 737 iliyokuwa inatoka Tehran kuelekea Ukraine

Mataifa ya Magharibi yalijitokeza kwa uhakika kabisa yakieleza kutunguliwa kwa ndege hiyo

Maelezo ya Mataifa hayo ikiwemo US, Canada, France n.k. yalieleza tukio kama bahati mbaya.

Iran baada ya kukanusha sasa imekiri kuwa ndege hiyo iliyokuwa na watu 176 ilitunguliwa kwa bahati mbaya au kwa kauli zao ''makosa ya kibinadamu''

Kosa la Iran ni kutojitokeza mapema na kukiri mapungufu waliyojua yamejitokeza.

Inaeleweka hali ya usalama haikuwa nzuri na kwamba usalama wa vyombo haukuwa mzuri.

Hili linatupeleka mahali pengine , kwamba, kifo cha Qassem Suleiman kinachopigiwa upatu na Rais Trump kimeondoka na watu 176 wasio na hatia wakiwemo akina mama na watoto.

Haya ni madhara ya haraka na kwa muda mrefu kifo cha Qassem kitaendelea kugharimu maisha ya wanadamu kwa njia mbali mbali.

Je, Marais wa Marekani waliopita kama Obama, Bush, Clinton hawakuwa na busara?

Je, haya yanayotokea ndiyo Rais Trump anaweza kusema Dunia ni salama bila Qassem?

Rais Obama aliwahi kusema, tweet moja tu inaweza kuleta madhara makubwa duniani.

Leo Familia 176 zimebaki na upweke, ukiwa, simanzi na maisha yao ya juzi si ya leo.

Unaweza kumuua mbu kwa kutumia rungu, lakini je hiyo ni busara?

Haya yanayotokea ni madhara ya ''vita'' ambayo siku zote haina macho.

Tusemezane
 
''VITA HAINA MACHO''

Ni msemo wa Wahenga kimaanisha vita ni vurugu zisizochagua nani yupo wapi au kwanini.

Hali iliyokuwepo mashariki ya kati na iliyopo ni ya ''tension'' sana baada ya kuawawa Qassem
..
Hili linatupeleka mahali pengine , kwamba, kifo cha Qassem Suleiman kinachopigiwa upatu na Rais Trump kimeondoka na watu 176 wasio na hatia wakiwemo akina mama na watoto.

Haya ni madhara ya haraka na kwa muda mrefu kifo cha Qassem kitaendelea kugharimu maisha ya wanadamu kwa njia mbali mbali.
...
Tusemezane

Kiongozi Nguruvi3 ,

Hayo maandishi yaliyokolezwa rangi ya rediredi yanaashiria wapo watu wenye hatia wasipokuwamo akina mama na watoto. Ni kina nani hao?
 
Kiongozi Nguruvi3 ,

Hayo maandishi yaliyokolezwa rangi ya rediredi yanaashiria wapo watu wenye hatia wasipokuwamo akina mama na watoto. Ni kina nani hao?
Mkuu sikumaanisha hivyo! pengine ningetumia neno ''non combatant'
Kusema akina mama na watoto ni kuonyesha jinsi walivyo ''vulnerable'' na kwamba hili hawawezi kujitetea kwa namna yoyote. Haina maana wanaume hawapo bali ni msisitizo tu wa kuonyesha jinsi watu wanavyoumia bila kuwa sehemu ya wapiganaji au hata kujua mzozo.
 
''ROYAL-EXIT''
PRINCE HARRY AONDOLEWA CHEO CHA ''HRH''

Wakati UK ikiendelea kutafakari hatma ya BREXIT, kuna tukio la Wanafamilia wa ''Kifalme'' kujiondoa katika shughuli za 'Royal''

Prince Harry na Meghan wamejiondoa shughuli za royal bila kuwashirikisha Buckingham P.

Tukio lilitikisa anga za habari za London ikizingatiwa Harry ni Senior Member of Royal Family.

Wadhifa wa Harry ni His Royal Highness (HRH) The Duke of Sussex, na Mkewe ni Her Royal Highness The Duchess of Sussex.(HRH)

HRH ni cheo kinachowapa nafasi za uwakilishi wa Malkia na shughuli zote za Buckingham.

Nafasi hiyo inagharamiwa na walipa kodi na ni full time job

Kikao cha dharura cha Queen, Prince Charles, Prince William na Prince Harry kiliitishwa kujadili mustakabali wa tangazo la Harry kuachana na shughuli za Royal Family.

Leo imeamualiwa Prince Harry na Mkewe Meghan waendelea na masiha yao wakiwa wanafamilia,bila cheo cha HRH.wataendelea na nyadhifa za Prince

Harry na Meghan hawatapata public Fund, wametaka kurudisha gharama za ukarabati wa jengo lao uliogharimu takribani pound milioni 2.5.

Utaratibu mzima wa watakavyoishi , ulinzi na vyanzo vyao vya pesa bila kuchafua tasira ya Buckingham Palace vimebaki kuwa kitendawili kama siyo siri ya kasri la Malkia

Ni habari kubwa sana UK. Royal Family ni Brand ya UK yenye heshima sana.

Ujio wa Meghan uligeuza taswira ya Royal na kumpaisha sana Harry katika jamii na mataifa.

Katika mfuatano wa utawala, anayefuata baada ya Malkia ni Prince Charles na Prince William. Wanaofuata wengine ni Watoto wa William, George, Charlotte na Louis.

Ikiwa hao hawatakuwepo, Royal itakwenda kwa Prince Harry ambaye ni 6 katika line of throne

Halafu utawala utaendelea kwa baby Archie , mtoto wa Harry na Meghan.

Ni wazi, tawala itabaki kwa William kwa muda mrefu ujao na uwezekano wa kurudi kwa Harry ni kama hakuna. Yaani Charles, William, George, Charlotte, Louis itabidi wasiwepo !

Kitu muhimu walichotegemea Waingereza ni Prince Harry kumsaidia kaka yake William katika majukumu wakati ukifika. Kwa umri wa Charles miaka 71 muda wa kutawala utakuwa mfupi .

Habari hizi tata kwani si jambo la kawaida na hivyo kuna mambo mengi hayajulikani itakuwaje.

Na hili limetokea kwa kuzingatia maamuzi ya Harry na Mkewe ya kushtukiza

Kutofanya majadiliano kabla ya tangazo ilikuwa dharau kubwa kwa kiti cha Malkia
Kutomshirikisha kaka yake au baba yake katika maamuzi ni kukosa busara

Kwa upande mwingine, magazeti ya Uingereza yamemwandama sana Harry na Megha mengine yakionyesha mbegu za ubaguzi na udhalilishaji bila Buckingham kukemea.

Waingereza hasa wahafidhina hawakubaliana na Harry kuoa Megha wanayemwita ''colored''

Hivyo suala hili lina pande mbili ambazo kwa pamoja zimekosa busara, Palace na Harry

Maswali yanatanda, nani atahudumia ulinzi wa Harry , Meghan na Archie?
Je, nini itakuwa hatma ya Archie katika utawala wa Uingereza? Naye atakuwa nje ?

Harry atafanya shughuli gani bila kuathiri brand ya Malkia?
Utaratibu wa fedha kutoka katika mfuko wa Prince Charles utakuwaje?

Kuna mengi sana nyuma ya tukio hili, ni suala la muda tu. Kwa muda mfupi inaonekana kama kuna suluhisho, kwa muda mrefu ni donda litakaloumiza brand ya Buckingham

Tusemezane
 
atafanya shughuli gani bila kuathiri brand ya Malkia?
Utaratibu wa fedha kutoka katika mfuko wa Prince Charles utakuwaje?
Harry ana sababu ya msingi ya kukimbia 'nyumba ya malkia'. Anasema kwa hali hilivyo kuna hatari kubwa kwa mkewe sawa na hatari ile iliyomkumba marehemu Mama yake(Diana).
====
Wasiwasi wangu, Familia ya Harry ina weza 'kupotezwa'.
 
Marekani siyo Sanctuary Nation, tulidanganywa. US ni suffocating/chocking Nation..... Kumuua Mwafrika kwa goti huku amefungwa mikono nyuma Huko Marekani imetondelea uongo sasa tuna jua kuwa Marekani haina cha kufundisha juu ya haki za binadamu na demokrasia!!!
 
TANZANIA : NJELU KASAKA

MBUNGE NA KIONGOZI WA G55

Njelu Kasaka , alyekuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri wa Tanzania amefariki dunia wiki hii kwao Mbeya
Msiba wa Kasaka haupewi uzito na chama cha mapinduzi kinyume na ilivyotarajiwa

Ingawa maisha ya kasaka kisiasa yalikuwa na hama hama, uzito wake katika zama za Bunge la chama kimoja hauwezi kuwa mwepesi kama ambavyo CCM wameufanya

Kasaka alikuwa kiongozi wa kundi lililojulikana kama G55 wakiwemo magwiji wengine kama Jenerali Ulimwengu
Kundi hili lilitaka uwepo wa serikali ya Tanganyika baada ya Zanzibar kuchukua hatua za kujiunga na OIC yenyewe

Spika wa Bunge wakati huo alikuwa Pius Msekwa, na kulikuwa na harakati za mataifa mbali mbali kama vile kuanguka kwa USSR na Russia ikaangukia mikononi mwa Boris Yeltsin, na mwisho anguko la Soviet

Huko Ujerumani nako hali haikuwa shwari baada ya ukuta wa Berlin kuvunjwa, mashariki na mgaharibi kuungana.

Kuna nadharia kuwa kuundwa kwa serikali ya Tanganyika kulikuwa na baraka za Pius Msekwa, Spika aliyetarajiwa kuwa kiongozi wa Tanganyika. Hivyo suala la OIC lilihanikiza tu ushawishi wa kuundwa kwa Tanganyika.

Ilikuwa ni dhahiri kwamba Rais Mwinyi alizidiwa nguvu na G55 na kundi hilo likiendelea kujitanua kwa kuungwa mkono huku Spika Msekwa akilipigia chapuo ndani ya Bunge .

Ni kuchelea hilo Mwalimu Nyerere aliingilia kati akijua hatma ya muungano ilikuwa mashakani

Katika moja ya hotuba zake kali, Mwalimu hakuwafukuza G55 na wala hawakuundiwa Zengwe, au kutishiwa maisha ndani au nje ya Bunge. Wabunge hao waliachwa huru kujadili kile walichokisimamia.

Mwalimu Nyerere aliwaambia, ' uwepo wao ni kutokana na sera za chama zinazotambua uwepo wa serikali mbili''

Kama wanataka hoja ya Tanganyika, kwanza, wanapaswa kuondoka ndani ya chama ili waweze kujenga hoja.

Ni kuanzia hapo , hoja ya Tanganyika ikapatwa na kigugumizi na kundi zima la G55 likasambaratika.

Njelu Kasaka alikuwa kiongozi wa hoja na kundi la G55 na hilo atakumbukwa kwalo.

Uzito wa hoja ya Tanganyika ulijirudia tena wakati wa tume ya Warioba. Ni CCM hawa hawa wakaipiga topito hoja hiyo kwa mizengwe na kufilia mbali. Pengine ni kujidanganya, hoja haijafa imezimia tu, wakati ukifika itazinduka.

Na hilo ndilo linawafanya CCM wasimtaje kabisa Njelu Kasaka wakihofia kuamsha hisia za Tanganyika.

Njelu kafariki, hatuna uhakika kama mawazo yake na historia nayo itakuwa imefariki kama CCM wanavyoamini

Pumzika kwa amani Njelu Kasaka
 
Sehemu ya I

'VITA' MASHARIKI YA KATI

HAMAS WASHAMBULIA ISRAEL, NA ISRAEL YASEMA ITAJIBU MAPIGO


Tunauridisha uzi huu kwa sababu mahususi ya mahusiano yake na yanayoendelea Mashariki ya Kati.

Kundi la HAMAS kupitia 'wing' ya kijeshi ya Al Qasam Brigade imeshambulia Israel na kuua watu kwa mamia, maelefu wakijeruhiwa. Israel kwa kutumia ndege za kijeshi imeshambulia Gaza ambako ni makao makuu ya Hamas

Mapitio ya nyuma
Uchaguzi wa Palestina uliwapa HAMAS ushindi lakini nchi za Magharibi zikakataa kwasababu walitaka Fatah ya West Bank ya Rais Mahmoud Abbas iongoze. Israel ikatenga Gaza ya HAMAS na West Bank ya Fatah na Abbas.

Kwamba kutoka Gaza kwenda West Bank lazima mtu apate kibali kutoka jeshi la Israel. Israel ikidhani ni mkakati mzuri wa kuwagawa uwatawale. Nchi za Magharibi zikawa kimya hata pale Demokrasia ya matakwa ya watu iliposiginwa.

Kwa kipindi cha January 2023 hadi August 7 2023 Takribani Wapalestina 250 wameuawa na Israel kwa kile ilichoita opersheni ndani ya maeneo ya Gaza. Mashambulizi ya Israel yalikuwa 'unprovoked'

Hakuna nchi ya Magharibi iliyolaani vitendo hivyo hata pale akina Mama wa Palestina walipopiga vifua vyao kuonyesha machungu ya kupoteza watoto au vijana wao. Uchungu wa Wapalestina hauonekani katika Dunia

Katika miaka kadhaa sasa Waisrael kupitia Masetla wamepanua maeneo yao kwa kuwafukuza Wapalestina.
Kwa maana kwamba mtu anaamka asubuhi nyumba yake inabomolewa na kiwanja anapewa Muisrael.

Kwa muda mrefu Wananchi wa Palestina wameishi bila uhuru wa kutembea au kutumia rasiliamli zozote ikiwemo Maji hadi watakapopata ridhaa ya Israel ndani ya maeneo yao.

Kwanini Watu hawaelewi haya?
Kuna sababu nyingi na kwa upande wa Tanzania ipo ya ziada

1. Wayahudi (Jews) wanamiliki vyombo vya habari vya nchi za Magharibi.
Inapotokea Wapalestina 100 wakauwaw na Israel hiyo siyo habari pengine habari ya Trump itakuwa na nguvu zaidi.

Vyombo vya Magharibi vinaeleza kwa undani pale tu Israel inaposhambuliwa ili kuonyesha ubaya wa Wapalestina
Kupitia nguvu ya vyombo vya habari na umiliki wa mashirika makubwa Waisrael wamemudu kuiweka ''serikali 'ya Marekani mkononi. Kwamba, Urais au Useneta au Uwakilishi unategemea jinsi mhusika anavyoiunga mkono Israel

Jambo hilo limezua mjadala sana katika nchi ya Marekani. Kundi la White Supremacist lililoimba 'Jews will not rule us' ni kielelezo. Trump aliunga mkono kundi hilo ingawa mkwewe ni Muisrael kwa kwasababu anaamini nadharia ya kundi la Proud Boys. Hata hivyo kwa kuelewa nguvu ya Israel, Trump alichanga karata zake vema akiwaridhisha kwa kujitoa katika makubaliano ya silaha za Nuklia na Iran, na kuua viongozi wa Iran ili kuficha ukatili wa Israel

2. Propaganda: Israel imefanikiwa kueneza propaganda za Mashariki ya Kati. Kwa mfano, Israel imeshawishi nchi za Magharibi ziite kundi la HAMAS ni la Kigaidi. Wakati huo huo Israel imekuwa inafanya matendo ya kuwatishia Wapalestina katika maana ile ile ya '' Terror'. Kwa vile wana umiliki wa vyombo vya habari nani wa kuhoji?

3. Israel imefanikiwa kupitia dini kuwapumbaza Watu. Kwamba ni Taifa teule la Mungu na shambulio kwao ni shambulio dhidi ya Mungu. Upofu huo unawafanya wengi kutoweza kufikiri au kutazama mambo kwa upana.

4. Kwa Tanzania, kuna tatizo la kuamini katika Taifa la Mungu wengine wakiamini Palestina wanapigana vita ya dini.

Pamoja na tatizo hilo, watu wetu wakishamaliza ubishi wa Simba na Yanga hawana muda wa kusoma au kufuatilia habari za Dunia kutoka vyombo mbali mbali dunia ili kuchuja na kupata ukweli wa nini kinajiri.

Kwa mfano, mbali ya dini, yapo malumbano ya kipuuzi kwamba Vita kati ya Israel na HAMAS , Israel litashinda.

Ukweli, hakuna vita kati ya Taifa linalopata Dollar Bilioni 3 kutoka Marekani, Silaha na kila msaada likitumia zana kama Vifaru, Magari ya Deraya na ndege za Kijeshi za kisasa kabisa dhidi ya HAMAS wanaotumia makombora ya Katusha yasiyo na precision au Wapalestina wanaorusha Mawe kupasua vioo vya magari ya Polisi ya Israel

Hakuna ulinganifu kati ya Israel na HAMAS kwasababu hawana uwiano wa nguvu.

Swali linalorindima katika vichwa vya wasomaji ahapa, imekuwaje HAMAS wakafanya walichofanya ikiwa ni dhalili ?

Shambulio la HAMAS mapema jana limeacha maswali zaidi.
Kwanza, ni jinsi walivyoweza kuwaduwaza Waisrale kwa shumbilo kubwa kwa miaka 50 ukiacha lile la mwaka 1973.

Je, kuna washirika nyuma ya HAMAS? Kwanini imeweza kurusha makombora mengi na hata kuteka askari wa Israel? Nini hatma ya ugomvi na 'stability' ya mashariki ya kati? Je, kurejesha mahusiano na nchi za KIARABU kutaisadia Israel?

Inaendelea sehemu ya II
 
Sehemu ya II

'VITA' MASHARIKI YA KATI

HAMAS WASHAMBULIA ISRAEL, NA ISRAEL YASEMA ITAJIBU MAPIGO


Inaendelea..

Shambuli la HAMAS lilipangwa kwa muda mrefu na kwa utalaam kwa maana kwamba walishambulia kutoka angani, majini na ardhini wakitumia makombora , drone na utekaji wa askari wa Israel.

Ni kundi la makomandoo waliofanya utafiti wa kutosha hata kuishtukiza idara ya usalama ya Israel MOSAD na CIA.

Swali linaloumiza wadadisi wa habari ni, kwanini, shambulio lililohusisha watu wengi namna hiyo halikuweza kuvuja?

Katika kuonyesha umahiri, HAMAS wamerusha makombora zaidi ya 5000. Wengi wanajiuliza ni kwanini.

Jibu ni kwamba Israel ina makombora ya 'Iron dome' yanayozuia makombora ya Wapalestina.
HAMAS walirusha makombora mengi ili ku 'overpower iron domes' na hilo limefanikiwa sana

Pili, makombora ya HAMAS kwa mara ya kwanza yamefika Tel Aviv, ikiashiria utaalam zaidi wa kuyatengeneza kutoka nje ya GAZA. Tayari vidole vinanyooshwa kuelekea Tehran, Iran kama mshirika mkuu wa HAMAS

Katika uzi huu mabandiko #39,40,41 tumeeleza kifo cha Kamanda wa kijeshi wa Iran Bw. Qasem Suleiman kilichofanywa na Marekani kule Iraq.

Tulieleza kwamba aliyefanya shambulio ni Marekani kwa niaba ya Israel, ili kutotibua nchi za Kiarabu

Iran ilijibu pigo kwa kushambulia ngome ya Marekani IRAQ na kuumiza askari wengi, ikiapa kulipiza kisasa mbeleni

Mwaka 2020 Israel alimuua mwanasayansi wa IRAN aliyekuwa kiongozi wa mpango wa kutengeneza Nuklia Bw Mohsen Fakhrizadeh , mauaji yaliyowauma sana Iran.

Baada ya shambulio la jana, Bunge la Iran lilipitisha kauli ya kuunga mkono shambulizi la HAMAS.

Pamoja na Iran, kuna maandamano sehemu mbali mbali za Dunia katika kuunga mkono shambuli la HAMAS

Kwa mantiki, Iran imeweza kulipa kisasi ingawa GAZA italipa gharama kwa mashambulio ya Israel.

Sahambulio la HAMAS linakumbusha jinsi Israel ilivyoshindwa vita dhidi ya HEZBOLLAH ya Imam Nasrallah.

Vikosi vya Marekani vimeelekea Israel na Rais wa Marekani akisema wataisaidia Israel kwa kila msaada wanaoutaka
Hii maana yake ni kwamba Israel kwa ushirika na Marekani inapigana vita na kundi la HAMAS.

Hali ya usaidizi kutoka Marekani inaeleza udhaifu wa Israel kama yenyewe ni dhaifu kusimama yenyewe.

Ugomvi uliopo kati ya ISRAEL na HAMAS unaweza kusambaa mashariki ya kati kama hautatafutiwa ufumbuzi

HAMASA wamefanikiwa sana katika kupanga mkakati wa kuiunganisha Mashariki ya kati kwa kutumia dini.

HAMAS wanatumia makosa ya Israel ya kuuvamia Msikiti Maarufu wa Al-Aqssa pale Jerusalem, moja ya shemu muhimu sana katika Ibada ya Waislam wakihusisha Msikiti na Ziara ya Mtume Muhammad S.A.W kwenda Mbinguni.

Katika mashambulizi, HAMAS wanatumia kikosi cha kijeshi kinachoitwa Al-Qasam kwa maana wapiganaji waKiislam wakichukua jina kutoka kwa mwanazuon Izza -Din na kuyafanya mapambano yao ni dhidi ya eneo la Waislam

Pili, HAMAS wanasema shambulio lao ni kulinda Msikiti wa Al-Aqsa ulioingiliwa na Israel. Haya yamewaunganisha Waislam mashariki ya kati dhidi ya Israel

Tumeona maandamano Tehran, Istambul, Kuwait, Sanaa Yemen na yatapamba zaidi hadi kufikia Jumatatu.

Hata Mahasimu wa HAMAS kule WEST BANK nao wameandamana kuwaunga mkono HAMAS

Mzozo huu unaziweka nchi zifuatazo katika wakati mgumu; Marekani, Israel, na Saudi Arabia. Tutajadili sehemu ya III

Tutafafanua

Charles kilian
 
MZOZO WA ISRAEL-HAMAS

Shambulio la HAMAS limeleta kiwewe Israel. Nchi inajulikana kwa ujasusi upitia shirika lake la MOSSAD, jeshi lenye vifaa na utalaam wa hali ya Juu. Vita mashariki ya Kati ya 2006 dhidi ya Hezbollah na ya HAMAS inaonyesha matundu na udhaifu.

Marekani, mshirika wa Israel imeingilia kati kwa kupeleka silaha na Watalaam wa kivita
Hii ni ishara na kama tulivyowahi kusema, nguvu inayosemwa ya Israel inategemea sana Marekani.

Mathalani tumeona silaha zinazoongozwa na mionzi na zinazoweza kunasa mienendo ya watu na vifaa zikitumika baada ya Marekani kutoa kile kinachosemwa '' Unique and Specific' military assistance

Vita inahusiaha Taifa lenye kutumia Manowari, Deraya, Ndege za kivita n.k. dhidi ya Wanamgambo wanaotumia miamvuli na makombora yasiyo na shabaha. Israel imeita askari wa akiba 300,000 kukaliana na HAMAS

Israel inapiga Mji wa Gaza kwa makombora , ndege na kila Silaha. Serikali ya Tel Aviv imekata mawasiliano ya umeme na Maji, dawa na Chakula kwa wakazi takribani milioni 2.5 ikiwa ni ' mauaji' ya raia wasio na hatia.

Makosa yanafayika katika kujibu mashambulizi ya HAMAS. Kwanza, kukata maji, umeme, dawa na chakula kunayaleta mataifa yaliyo pembeni ndani ya Mzozo. Tumeona Saudi Arabia ikitoa kauli ya kuunga mkono Palestina, kama ilivyo Qatar, Turkiye na Iran. Nchi za Kiarabu zinahisi ni mauaji kwa adhabu ya jumla '' collective punishment'

Kosa la Pili, ni Israel kushambulia misikiti. Kitendo hicho kilisubiriwa na HAMAS kama njia ya kuvuta hisia kwa Waislam. Mataifa yaliyokuwa pembeni sasa yanaona si vita ya HAMAS na Israel bali ya Israel na Waislam

Tatu, Marekani kupeleka manowari na silaha zinazifanya nchi za Kiarabu kukumbuka mateso yaliyotokana na uvamizi wa Marekani Afghanistan na Iraq na hivyo kutoa huruma 'sympathize' na Wapalestina

Nne, kwa nchi za Magharibi, UK, US, Ufaransa, Australi, Canada, Italy kusimama na Israel zinaeleza jinsi zinavyoibeba Israel '' Impunity' hata pale inapofanya makosa mengi kwa miaka mingi ikiwemo kukiuka maazimio ya UN.

Kwa wakati huu kuna vita kati ya Israel na Hezbollah lakini vyombo vya Magharibi havielezi ili kutolikuza tatizo.

Kuna hoja pia kwamba Iran inasaidia HAMAS na vikundi mbali mbali ikiwemo hezbollah.
Inawezekana kabias kwa kzuingantia jinsi Israel ililivyoshiriki kuua Wanasayansi na Askari wa juu wa Iran.

Swali wengi hawajiuliza, kwanini ni makosa Iran kuisadia HAMAS wakati Marekani na Manowari wakisaidia Israel?

Makubaliano ya ushirikiano wa Israel na nchi za kiarabu apo mashakani.

Kuna dalili mzozo utasambaa, ni sauala la Muda. Upigaji wa GAZA na kuifanya kifusi unatia hasira sehemu za dunia.

Katika mazingira yasiyotegemewa Watu katika miji mbali mbali wamejitokeza kuunga mkono HAMAS, na hilo linawalazimisha viongozi hasa wa nchi za Kiarabu kufanya jambo na si kuungana na Israel.

Tunakumbuka aliyetengeneza Alqaeda na Osama ni Marekani ili kumpiga Mrusi.
Mwisho wa siku wakageuka na kuwa shubiri kwa nchi za Magharibi.

Aliyetengeneza HAMAS ni Waziri Mkuu BB Nyahu na Marekani pamoja na nchi za Magharibi. Tutafafanua
 
MZOZO WA ISRAEL-HAMAS

Tulieleza kwa ufupi kwamba Israel na nchi za Magharibi zimeitengeneza HAMAS.
HAMAS ilikuwepo na nadharia ya kupinga kukaliwa kwa ardhi ya Wapalestina kwa kutumia njia zote ikiwemo mabavu

Chama kilichoongoza Palestina ni Fatah, mwaka 2006 HAMAS walishinda Uchaguzi mkuu wa Palestina

Sababu kubwa ya HAMAS kushinda ni jinsi walivyowafikia Wananchi kwa huduma na misaada waliyopata.

HAMAS waliitumia vema sana kuimarisha huduma za Maji, Afya, Shule n.k huku chama cha Fatah kikigubikwa na rushwa, utoroshaji wa fedha n.k.

Nchi za Magharibi zikagoma kutambua ushindi wa HAMAS. Mwakilishi wa Marekani Rais Jimmy Carter bila kuuma maneno alisema '' HAMAS wameshinda kihalali''.

Israel kwa kutambua msimamo wa HAMAS wakaungana na nchi za Magaribi kukataa ushindi wa HAMAS.

Mkakati wa Israel ni '' Wagawe uwatawale' kwa maana kwamba West Bank watatawala Fatah na Gaza HAMAS.

Mkakati wa kuwagawa ulifanikiwa na Gaza ikawekewa vikwazo na Israel , Wananchi wakawa '' Boxed in'

Kwa miaka 17 Israel imepiga Gaza kwa kadri ilivyotaka. Mwezi July 2023 Israel ilishambulia maeneo ya Jenin
Katika kipindi cha miaka 17 Israel ili control kwa kila kitu.
Masetla wa Israel wameongeza maeneo kwa kuwaondoa Wapalestina kwenye ardhi zao

Kwakuwa Waisrael wamekamata vyombo vya habari za Serikali za nchi za Magharibi, Israel imefanikiwa kuwafanya watu wasifikiri sawa sawa wakidhani hali ya mambo mashariki ya Kati ilikuwa safi sana hadi Jumamosi iliyopita

Ukweli ni kwamba Wapalestina wawe wa West Bank au Gaza wameteseka na Wanateseka kwa miaka takribani 75

Kitendo cha kuwabana HAMAS kililenga kuwadhoofisha na kuwatenga na Dunia.
Kitendo hicho kilizuia uwezekano wa serikali ya Gaza kuongea na serikali nyingine kwasababu ni kundi la 'Kigaidi'

Pamoja na madhara kwa Raia wasio na hatia wa Israel, Dunia Watu wamejitokeza kuunga mkono HAMAS.

Uungaji mkono si kwasababu wametekeleza mauji bali wanonyesha hisia zao kwamba '' Wanyonge' wameishtua Dunia iwasikilize hata kwa njia mbaya. Kwa maana miaka 17 hakuna aliyejadili mateso ya Gaza

Katika hali ya kutahamaki kwa kipigo cha Jumamosi, Israel inafanya makosa mengine.

Kwanza, inaua Raia wakiwemo watoto na akina Mama kama walivyofanya HAMAS na kuleta chukizo.

Pili, Israel inashambulia kwa jina la Magaidi wa kiislam na kupungaza kuungwa mkono na chuki Mashariki ya Kati.

Tatu, Israel inavurumisha mabomu kuimaliza Gaza na kuifanya kifusi
Kuipiga Gaza hadi kifusi hakutamaliza tatizo.

Mwaka 2006 HAMAS Walikuwa na makombora yanayovuka Gaza, baada ya miaka 17 chini ya ''kifungo cha Israel'' wana makombora yanayofika Tel Aviv.

Marekani imewapiga Afghanistan kwa mabomu kwa miaka 20 leo Talibani wana serikali inayoongea nao

Hoja ni kwamba hakuna Bomu linaloleta suluhu au Amani, wanachokifanya Israel ni hamaki tu hawawawezi kumaliza mzozo hadi watakapokubali 'two states solution' au kinyume chake wataishi kama nguchiro wakiwa na hofu kila siku , kila dakika na kila sekunde
 
VITA MASHARIKI YA KATI
ISRAEL IMEPIGA GAZA, HILI LA HOSPITALI LIMECHAFUA TASWIRA


Mashambulizi ya Israel Ukanda wa Gaza yamendelee mfululuzo kwa makombora ya ardhini, majini na angani. Hamas inarusha makombora yanayozuiliwa na 'Iron dome yl'' na upande wa kaskazini kuna mtifuano na 'Hezbollah'

Vifo vya watoto, Wanawake na Wazee ni vikubwa. Huduma za maji , umeme na za kibinadamu zimesitishwa na Israel kama sehemu ya adhabu kwa Hamas ingawa waathirika ni Wapalestina wa rika zote '' collective punishment'.

Jitihada za kusitisha vita kupitia Mswada wa Urusi na Brazil UN zimekwama kwa kura za Marekani, Ufaransa na UK.
Nchi hizo zinataka Israel ieendelee kuitwanga Gaza kadri iwezavyo

Rais Biden Yupo Israel kwa ziara ya kuunga mkono . Biden alipangwa kukutana na Rais Sisi wa Misri, Kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas , na Mfalme Abudllah wa Jordan.

Mkutano umevunjika, Rais Abbas karejea Ramalla kufuatoi Shambulizi la Israel katika Hospitali ya Al Ahli, Gaza.

Hospitali imejengwa mwaka 1905 ikimilikiwa na Waangalikana wa Uingereza

Watu 500 wamekufa , Wagonjwa na waliojihifadhi Watoto kwa mamia , akina mama na Wazee

Tukio la kushambulia Hospitali ni kinyume na sheria za Kimataifa ( Gneva convention) na limelaaniwa Duniani kote.

Katika jitihada za kujikosha, Israel imetoa kauli za kujichanganya. Msemaji wa Serikali anadai ni Bomu la Hamasi lililoshindwa kulipuka vema 'misfire'' .

Msemaji wa jeshi la Israel (IDF) anasema Si Israel wala Hamas bali ni kundi la Islamic Jihad limelipua.

Islami Jihadi imetajwa makusudi na Israel kwasababu jina linaonyesha ''uovu' kama wengi walivyokariri
Kwamba kuna neno ''jihad' basi inahalalisha kuhusika kwa kundi hasa likiwa na jina la Islamic

Hizi ni propaganda za Israel kwasababu tangu vita ianze hakuna mahali kundi la Islami Jihad limetajwa.
Wachunguzi kutoka Gaza wamethiitisha Islamic Jihad halina zana za kusababisha mlipuko huo

Israel inasema itatoa picha za kuonyesha tukio kabla na baada na si jinsi shambulio lilivyotokea.
Yaani inajichunguza na kueleza ''ukweli' , Israel ilitokana kumuua Mwandishi Sheen kisha kukiri, na asubuhi ya jana kushambulia shule ya UN na kuua watoto. Historia ya Historia katika hili si nzuri na ni ngumu sana kujisafisha


Mahushuda waliokuwepo Hospitali, Waandishi waliofika eneo wanatoa ushahidi shambuli lile ni la mlipuko mkubwa wa Bomu lililokusudia eneo hilo na Israel inahusika. Anglikan na Medicin frontier wamesema ni Israel

Ingawa Israel inajitahidi kusafisha taswira, ukweli unabaki kwamba tukio hilo limeichafua sana
Kila siku Isral imepiga mabomu leo inawezaje kujikosha na shambuli hilo?

Dunia ya Kiarabu imewaka moto kwa maandamano kila kona.
Ukingo wa Gaza Rais Mahmoud yupo kikaangoni kwa jinsi alivyowatosa Gaza. Vijana wanamtaka ajiuzulu mara moja

Tukio la leo si kwamba limeichafua Israel na kubadilisha mtazamo wa wa watu duniani, bali pia umeathiri taswira ya Marekani inayoonekana kudhamini mauaji ya Watoto na Wagonjwa

Ziara ya Rais Biden imeingia doa , hatari ya vita kusambaa ni kubwa sana.

Hata kama haitasambaa madhara ya kinachotokea Gaza yatafika kila kona za Dunia kwa njia moja au nyingine
 
VITA : ISRAEL -HAMAS
PIGO LA HOSPITALI LAITAFUNA ISRAEL, DUNIA IMEIGEZIA KIBAO


Habari Duniani ni Israel kupiga Bomu Hospitali na kuua watu takribani 474 kwa mujibu wa idara ya afya ya Palestina, lakini namba hiyo inatagemewa kuongezeka kutokana na majeruhi na huduma za afya ni duni

Israel inakanusha kuhusika wakitoa Data za kijeshi kuonyesha sambulio ni la kombora la Islamic Jihadi kushindwa mwelekeo. Islamic Jihad ni tofauti na Hamasa , lakini limetumika kwa vile neno Jihad na Islamic yanapewa maana tofauti na ilivyo.

Rais Biden kasema data za Pentagon zinaonyesha hakuona uwezekano wa Israel kupiga Bomu.
Jitihada za Israel na United States kufuta picha mbaya ya mauaji Hospitali ni kubwa.

Hoja za Israel na US zinakumbana na upinzani kwasababu;
Si mara ya kwanza Israel kukanusha kuhusika na matukio mabaya. Mwaka jana ilikanusha kumuu mwandishi wa AL Jazeera bibi Shireen Abu Akleh. Ushahidi ukaonyesha Israel ilimuua na Israel baada muda mrefu ikakiri

Kumuu Shireen inaonekana ni jaribio la kuzima waandishi wa habari wanaofichua maouvu ya Israel kule Gaza.
Hili tu limetumika kama sababu za kutowaamini

Pili, hivi inawezakanaje Israel ikajichunguza? Kwamba, tukio baya la uhalifu wa vita ''war crime' Dunia itegemee Israel itasema imehusika au US itasema Israel imehusika! akili za kawaida zinakata hili kwa mtu yoyote

Tatu,Israel imeshambulia ambulance na kuua wafanyakazi wa afya ikiwemo Hospitali na shule siku za karibuni

Nne , Kanisa Anglican linaoendesha Hospitali iliyopigwa linatoa ushahidi, Israel imelipua Hospitali

Tano, taarifa ya video na sauti za 'Hamas zilizokamatwa na Israel haziwezi kuaminika kwasababu dunia ya leo ni ya AI (Artificial intelligence) inayoweza kutengeneza tukio likaonekana kama kweli. Huu hauwezi kuwa utetezi

Sita, kuungwa mkono na US hakuna maana. US inatoa silaha na inasimama na Israel.
Leo US ime veto misaada kuwafikia Wapalestina kwa lengo moja, Israel iweze kuwaadhibu Wananchi kwa urahisi.
Pentagon itasema kitu gani cha kuamniwa?

Saba, Pentagon ndiyo ile iliyoiambia Dunia Saddam ana silaha za nyuklia , leo tunajua ulikuwa uongo mtupu
Pentagon hiyo hiyo inataka kuaminisha dunia kwamba Israel haukitenda

Ni kwasababu hizo, mashariki ya kati kumewaka moto vijana wakiandamana kulaa kipigo cha Hospitali kutoka Israel

Viongozi wa nchi za kiarabu imebidi wasikilize umma na kuahirisha maongezi na Rais Biden

Viongozi hao wanakumbuka Arab spring ilivyong'oa wenzao na kelele za kumuondoa Mahmoud Abbas wa PLO zinaeleza ukubwa wa tatizo. Ijumaa wiki hii kutakuwa na moto mkali wa maandamano

Kwa hali ya Dunia ilivyo, kibao kimebadilka. Dunia inaingalia Israel kama mkosaji kwa mashambulizi ya Gaza dhidi ya Raia. Hamas wamepata '' milage' kwa bomu la Hospitali. US ipo katika wakati mgumu ikihofia kusambaa vita

Kuna maswali mengi yanaulizwa na wasomaji
Ni kwanini Israel inakingiwa kifua na mataifa makubwa?
Kwanini Iran inaunga mkono makundi hasimu na Israel?
Kwanini 'normalization' na Saudi Arabia imekuwa ni pigo kwa Israel?

Tutajadili kesho
 
Back
Top Bottom