Duru: Matukio na habari za Dunia

VIJANA 12 NA KOCHA WA TIMU YA MPIRA WAOKOLEWA
Ni baada ya wiki mbili ndani ya mapango katika hiza totoro bila chakula au malazi

Ni tukio lililovuta hisia kubwa wiki hii ukiachilia mbali kombe la dunia linaloendelea Urusi
Vijana 12 na kocha wao wa timu ya soka walijikuta wamekwama mapangoni

Baada ya mazoezi, timu ilitembelea mapango wanayoyaju. Mvua ilinyesha na kuingia mapangoni. Ilibidi wasogee nyuma kupeuka kuzama.
Mapango yana vilima na mabonde,bonde linapojaa wanahamia nyuma zaidi

Uwepo wa baiskeli nje ya mlango wa pango ulitosha kuutarifu umma watu wamekwama
Jitihada za kuwatafuta zilifutika baada ya siku kadhaa hadi pale mzamiaji kutoka Uingereza alipoingia umbali wa zaidi ya KM 4 na kuwakuta wakiwa salama lakini dhofli hali

Jitihada ziliungwa mkono na wazamiaji kutoka Thailand , US, UK na Australia.

Ugumu wa kazi ulitokana na eneo la kupita limejaa maji kulazimu kuogolea katika madimbwi baina ya sehemu moja hadi nyingine. Kwa udhaifu wa vijana haikuwa rahisi

Vijana wana umri wa miaka 11 n.k. hawana uzoefu wa kuogelea au kuvuta hewa ya mitungi maalum

Ilitarajiwa kazi ya kutoa maji kiwango cha galoni lakini 4 kwa saa ingechukua miezi
Changamoto ikajitokeza ,ni msimu wa mvua za Mansoon upo uwezekano wa kujaa maji

Kiwango cha hewa kilipungua kwa ongezeko wafanyakzi na kukosekana eneo la kubadili hewa

Uamuzi ukafanyika kuwaokoa, wasingeweza kuishi katika siku chache zijazo
Matibabu na chakula maalum vilipelekwa kuhakikisha hawaathiriki na kuwasaidia kisaikolojia

Katika jitihada za kuwapelekea mahitaji, mzamiaji wa Thailand alipoteza maisha.
Hili lililongeza hofu ya kuwaokoa vijana hao na kocha wao

Muda haukutoa nafasi, mvua na kina cha maji havipungui. Uamuzi wa kuwatoa ulifanyika chini ya usimamizi wa timu za wazamiaji, Injia, wanasaikolijia, madkatari na wanaojitolea

Jaribio la kuwatoa waliokuwa na nguvu lilifanikiwa na wote kuokolewa kwa mafungu katika mazingira ambayo wanasayansi, wazamiaji, wanasaikolojia n.k. wameeleza ni magumu sana

Kuna funzo tunalopaswa kujifunza hasa nyakati za majanga ya asili

Inaendelea...
 
FUNZO KUTOKA THAILAND

Janga la mapango limetoa funzo kwa watu wa mataifa na hasa nchi zinazoendelea katika maeneo mengi muhimu. Majanga hayachagui pa kutokea, muda au eneo

1. Wazamiaji wa Thailand walifanya kazi, hawakusita kuomba msaada kutoka Uingereza pengine kwa ubora wa vifaa na uzoefu licha ya kupotea wiki 2, haikusemwa 'ah basi'
Hawakumsingizia mungu, walimuomba kwa imani ya buddhi wakiendelea na jitihada

2. Oganazisheni ilikuwa chini ya Gavana wa jimbo. Gavana alikuwa kiungo cha Familia, Serikali, Timu za kazi na watu wa kujitolea. Taarifa alizitoa kwa usahihi,ukweli na weledi
Hatukusikia viongozi wakishindana kutoa taarifa na kujichanganya au kuchanganyana

3. Gavana alipata msaada wa serikali kuu na kutumia watalaamu kupata taarifa sahihi
Hatukusikia wanasiasa au kamati za siasa bali taarifa za kitaalamu na kisayansi

4. Timu zilijipanga kwa majukumu kwa wakati muafaka. Ikiwa ni Engineers, waliachwa wafanye yao. Wazamiaji wakatenda yao. Wanasaikolojia wakatimizi wajibu
Manesi na madaktari wanatoa huduma za muda mfupi na muda mrefu

5. Daktari aliyebaki na watoto ana utaalamu wa kuzamia 'diver' mbali na utaalam wa afya
Aliweza kuwafikia vijana alipohitajika na kwa wakati mwafaka akitumia taaluma zake mbili

6. Vijana wametengwa eneo maalum na kuonana na familia zao kupitia kioo. Hii ni kuwakinga ikiwa immunity yao ina matatizo.
Ni kukinga jamii ikiwa wana vijimelea vya magonjwa waliochuku.

Hakuna anayelalamika, wananchi wametii utaalam katika wakati mgumu, nidhamu mbele

7. Timu kutoka nje ya Thailand zilifika kwa makusudi mawili
a) Kutoa huduma iliyohitajika kwa dharura
b) Kujifunza janga na kuwa 'resource' katika nchi zao pindi yakitokea kama hayo

Orodha ya mafunzo yanayotokana na tukio ni ndefu, ukiangalia mtiririko wa tukio zima unabaki kujiuliza, nini wenzetu wanatushinda? Tunashindwa nini na kwasababu gani!


Majanga ni tatizo linaloweza kutokea popote na wakati wowote.
Tujiulize, je, katika nyakati kama hizi tumejifunza lolote?
Je, tumejiandaa kifikra? Tuna nidhamu ya kujipanga?
Tuna wataalam katika nyanja mbali mbali?
Tuna vifaa vya kutosha? na muhimu tumejiandaa likitokea?

Tafakuri ya leo, ikiwa hatuwezi kujipanga kupanda daladala au mwendo kasi, kwa nidhamu hiyo tunaweza kufanya nini dunia ikajifunza kutoka kwetu!!

Tusemezane
 
'VITA YA BIASHARA-CHUMI KUBWA DUNIANI
MKUTANO WA NATO, LONDON NA HELISINK

Vita ya biashara 'trade war' kati ya mataifa makubwa imegubika duru za kimataifa
Vita hiyo imeanzishwa na Rais Trump kwa alichodai nchi nyingine kuitumia Marekani

Vita ya biashara ilianza katika mkutano wa wakuu wa nchi 6 tajiri duniani 'G6' uliofanyika Quebec-Canada na kwisha kwa mzozo mkubwa kati ya washirika na Marekani

Kilichofuata ni Marekani kuweka kodi kwa bidhaa kutoka mataifa kama China,Canada, Mexico na nchi za Ulaya. Hofu ya masoko ya mitaji ni kulipiza kisasi kutoka nchi husika

Vita ya biashara inatoa picha tofauti. Rais Trump anasema itasaidia kutengeneza ajira na usawa katika biashara. Ni kweli inaweza kusaidia hata hivyo ina athari pia kiuchumi

Baadhi ya makampuni ya Marekani kama Harley Davidson inayotengeneza pikipiki itahamisha utengenezaji kwenda Ulaya. Kuweka tariff katika bidhaa kwa nchi za Ulaya kutaathiri mauzo ikizingatiwa steel inapanda bei US kutokana na tariff

China nayo inaweka tariff kwa bidhaa za Kilimo na kuathiri wakulima wa Marekani, huku nchi kama Canada, Mexico na zile za EU zikisema zitaweka kodi hiyo

Athari za vita ya biashara zipo katika usalama na uchumi.
Kwa mfano, China inaitumia Korea kaskazini kama 'leverage' dhidi ya Marekani
Tunaona kusuasua kwa makubaliano ya Singapore kati ya Trump na Kim kwa sasa

Vita hivyo imehamia katika eneo jingine la ushirika wa nchi za Magharibi (NATO)
Mkutano wa NATO kule Brussels juzi na jana umekuwa tatizo kuliko ilivyozoeleka

Kama ilivyokuwa mkutano wa G6, washirika wengi wa NATO ni sehemu ya G6
Mtifuano kati ya Chancellor Merkel na Trump ulihamia katika NATO kwa nguvu zaidi

Rais Trump ametumia biashara, gharama na ulinzi na kuchanganya na kuufanya mkutano uwe na tension .Nyuma ya pazia kuna suala la vita ya uchumi inayoendelea.

Trump anataka kutumia NATO katika agenda ya uchumi

NATO ndiyo mjadala unaofuata.....
 
MKUTANO WA NATO

Mkutano ulikwa wa hisia kali kufuatia tuhuma za Rais Trump kwa washirika
Mwaka 2014 chini ya Obama, NATO walikubaliana kila mwanachama achangie 2% ya GDP

Rais Trump anasema Marekani inabeba mzigo wa gharama ukilinganisha na nchi ka Ujerumani. Wanachama wanasema mchango si fedha bali ushiriki hasa wa majeshi

Kilichotokea ni Trump kuishambulia Ujerumani kwa kusema inajenga Bomba la gesi ya asili kutoka Urusi na hivyo ni mateka wa Russia.

Ni kweli ujenzi huo upo tangu mwaka 2009 ukihojiwa pia na utawala wa Obama
Rais Trump anasema ni ni mateka kwasababu inatumia asilimia 70 ya energy ya Russia

Takwimu zinaonyesha ni asilimia takribani '37' zilizobaki zitoka nje ikiwemo Algeria

Kuna mambo mawili aliyotaka kuyafanya Rais Trump kwa hoja hii
1. Kwavile anakwenda kukutana na Rais Putin, alitaka kueleza washirika safari yake si ya kipekee kwani kuna nchi kama Ujerumani zina mahusiano na Russia

Ujerumani ni kiongozi katika kuikabili Russia Ulaya.
Hata kuvamiwa kwa Crimea ni Obama na Merkel walioandaa mpango mzima.
Kinyume chake Rais Trump hataki kuzungumzia suala hilo akimlaumu Obama

Lakini pia Rais Trump akiwa mkutanoni G6 Canada, alisema Russia irejeshwa, kauli iliyoleta kizaa zaa miongoni mwa wanachama wanahofia ushawishi wa Russia

Kuishambulia Ujerumani ilikuwa kujenga uhalali wa safari ya Helsink kukutana na Putin

2. Lengo la pili ni kuitisha Ulaya. Marekani inazalisha gesi asili, ingependa wateja Ulaya. Ujenzi wa Bomba hauwezekani na gharama za zinaifanya gesi ya Urusi kuwa rahisi

Ukitazama Rais Trump alichanganya hoja za mchango wa NATO na nyingine za uchumi makusudi akitafuta leverage ya biashara na kuondoa mtazamo wa watu kuhusu mkutano wake wa Helsink 'Distraction'

Mkutano ulimaliza kwa hati hati ukizikubali nchi za Macedonia na Montegro kujiunga baada ya kukamilisha taratibu nyingine zinazshughulikiwa.

Wanachama kubaliana kuendelea na michango ya 2% pamoja na ushiriki wa vikosi
Kilichotokea G6 Canada na NATO Brussels havina tofauti, Rais Trump akiwa katikati
Wachunguzi wanahoji kwanini anakuwa mkali kwa washirika akiwa laini kwa Russia?

Tuangalie ziara ya UK na Helsink

Tusemezane
 
ZIARA YA RAIS WA MAREKANI UK KUELEKEA FINLAND

Rais Trump alifanya ziara ya kwanza Uingereza akitokea Brussels.
Kawaida mshirika mkubwa kama UK hupewa kipaumbele cha Rais wa Marekani
Kuchelewa kwa ziara kunatokana na mtifuano kati ya Rais Trump na Meya wa London

Ugomvi na Meya Khan ulianza baada ya shambulio la ugaidi, Rais Trump ali tweet kumdhahika Meyana kuzua chuki, Wananchi walijiapiza kutomruhusu kuzuru London

Kidiplomasia ziara ilipangwa kupunguza maandamano kama si kuepuka vurugu.

Kwanza, ilitangazwa ni ziara ya kikazi (working visit) na siyo state visit
Kwa madaraja, state visit ina hadhi kubwa kuliko working visit

Pili, iliandaliwa wakati wa kombe la dunia kwa kujua attention itaelekezwa Russia na hivyo kupunguza misuguano kati ya vyombo vya dola na wananchi

Tatu, ziara ilipangwa kuhakikisha Trump haingii katika jiji la London moja kwa moja

Ndege ilitua uwanja wa Stansted, Helicopter kwenda katika makazi ya balozi wa US-UK

Dhifa ilifanyika katika nyumba ya waziri mkuu nje ya mji 'Chequers House'

Alikutana na Malkia katika jumba la Windsor siyo Buckingham palace

Pamoja na yote maandamano yalifanyika katika miji kuonyesha kutoridhishwa na ujio

Rais Trump hakukosa kauli tatu zikiichambua UK na EU kwa pamoja
Moja ya kauli ni ile ya kusema Wahamiaji wameharibu utamaduni wa Ulaya

Baadaye alielekea Scotland kwenye uwanja wake wa Golf. Mama yake ni ''Mskochi''

Leo anatarajiwa kukutana na Rais Trump Helsinki, ziara yenye makando kando yanayomwandamwa kuanzia nyumbani US hadi Helsinki

Kuna mambo ya kuyatathmini katika matukio hayo

Kwanza, wachunguzi wanasema Rais Trump anabadili 'mpangilio wa dunia'' kwa isiyo rasmi (World Order) tangu kuanzishwa kwa NATO.

Mtifuano wake na washirika haushiria mwendo mzuri wa NATO.
Hili linaungwa mkono na maseneta kwa kura 97 -100 wakiunga mkono NATO

Pili, tunaona njia za kidiplomasia kwa viongozi waliokomaa na Theresa May na Angela Merkel hata pale panapokuwa na maudhi yaliyokithiri

Tatu,tunaona uhuru na haki za wananchi zinavyothaminiwa. Haikuwezekana kuzuia maandamano, kilichofanyika ni kupunguza madhara ya maandamano kwa njia nyingine

Nne, akielekea Helsinki , Rais Trump anakabiliwa na changamoto.
Huku akizataja EU na China kama Foe(maadui) aliitaja Urusi adui mshindani (competitor)

Nyumbani kunafuka moshi kukiwa na shinikizo la kumtaka amkabili Rais Putin kutokana na taarifa ya majuzi ya majasusi wa Urusi kuingilia uchaguzi,majasusi yakihusishwa na matumizi ya gesi ya sumu iliyotumika Uingereza

Inaonekana kana kwamba Rais Trump ana ''dhamana'' aliyobebwa kwa Rais Trump
Swali, je, ataweza kumkabili Putin kama shinikizo la nyumbani US linavyoendelea?

Tusemezane
 
DEMOKRASIA YA TANZANIA
Falsafa, sera na hama hama ya wanachama

Yapo matukio yanayoendelea ya Wabunge na madiwani kuhama vyama kimoja kwenda kingine
Kwa sehemu kubwa, wahamaji wanatoka upinzani kwenda chama tawala

Kuhama vyama si jambo geni na wala si baya. Ni sehemu ya haki za wananchi kuitumikia fursa ya kidemokrasia kama ilivyoainishwa katika sheria za nchi

Kinachoonekana tofauti ni kauli za wahamaji.
Mwanachama ni 'muumini' wa sera , falsafa na mitazamo ya chama

Vyama hutengenezwa na falsafa zinazo wavuta au kuwakimbiza wanachama kutegemea namna gani mtu anaiona jamii na nafasi yake katika jamii husika

Yupo diwani aliyeacha kazi hiyo akisema ' biashara zake zinakwama na mambo hayaendi vizuri' Diwani alikuwa mkweli , kwamba uwepo wake katika chama unamkwaza, na hakuwa tayari kutumikia falsafa ya chama zaidi ya shughuli zake binafsi

Huyu ni mmoja wa waliosema ukweli, wakautumikia kikamilifu bila kumung'anya maneno
Kwa maneno mengine, diwani aliamini falsafa ya chama chake, akakwaza na mambo ya maisha

Yupo Mbunge aliyeacha ubunge kwa kuamini misingi ya chama chake haizingatiwi na kwamba chama chake cha zamani kimepoteza misingi hiyo.

Wakahama wengine wakisema 'wanakwenda' kuunga mkono jitihada. Hapa panafikirisha.
Hivi watu hao wanaamini falsafa na sera au jitihada binafsi za watu mmoja mmoja au kwa makundi ?

Vyama vinasimmamishwa na sera na falsafa zinazotumikiwa na wanachama au viongozi
Wanachama na viongozi huja na kupita, sera na falsafa zipo kama misingi

Swali, ikiwa haawaamini sera na falsafa ,ikitokea viongozi kuja na kupita nini hatma yao? Wataacha vyama walivyohamia? Wanatumikiaje vyama bila kuamini sera na falsafa?
Waliwezaje kuwa viongozi na waliamini au kusimamia nini?

Kuhama vyama, kutokuwa na vyama au kuacha siasa ni haki za mwananchi.
Hakuna sheria inayomlazimisha mtu kuueleza umma kwanini anahama.
Ikitokea hivyo ni kwa hiari, na ili kuutendea umma haki, awaye awe mkweli kwa nafsi yake

Abraham Lincoln, aliyekuwa rais wa Marekani alinukuliwa akisema
'' You can fool some of the people all of the time,and all of the peole some of the time,but you can not fool all the people all of the time'

Tusemezane
 
KUZAMA KWA KIVUKO CHA M.V NYERERE

Habari kubwa nchini ni kuzama kwa kivuko kulikotokea Ukerewe na kupoteza maisha ya Watz
Sisi kama Taifa tunaguswa, tunasikitishwa na tunafadhaishwa na matukio yanayojirudia

Kujirudia kwa matukio hayo siyo bahati mbaya. Kuna nukuu za wanafalasa zikieleza haya
'One's an incidence, two's a coincidence and three's a pattern''

Kwa tafsiri isiyo rasmi, mara moja ni tukio, mara ya pili ni bahati na mara ya tatu ni mwendelezo
Kwa maana kuwa, inapotokea mara moja ni tukio tu, mara ya pili ni 'bahati' imetokea kama mara ya kwanza,ya tatu ni mwendelezo kwamba imetokea mara moja mbili na sasa inaendelea

Kuna ajali kila mara za vyombo vya usafiri. Hizi za majini zimechukua roho za watu wengi kwa wakati mmoja. Mfano ni MV Bukoba, Tukio la Zanzibar na sasa MV Nyerere
Ni ngumu kusema hayo ni incident or coincidence. Hayo ni Pattern bila shaka yoyote

Katika kuangalia suala zima la kuzama kwa kivuko ikiwa ni mwendelezo wa kuzama kwa vivuko na meli , tutakuwa na mabandiko yatakayojadili kutoka mitazamo na kona tofauti

Bandiko la 1 linafuata
 
KUZAMA KWA KIVUKO MV NYERERE
Sehemu ya I

Ni masikitiko makubwa kwamba kwa mara nyingine tumepoteza wananchi kwa mamia kwa wakati mmoja. Huu ni mwendelezo wa mfululizo wa ajali zikiwemo za barabarani

Ajali hutokea pale hali fulani inapokuwa si sawa kwa maana iwe ya kifundi au kitauratibu au vyote

Utaratibu unaotumiwa na wenzetu ni kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo na kurekebisha
Ni katika kuutafuta ukweli na kuueleza ikiwemo kuwajibisha waliohusika au waliosababisha

Ajali ya MV Bukoba miongo kadhaa iliyopita ni kubwa katika historia ya nchi yetu na ulimwengu. Watu kwa mamia walipoteza maisha, wengine hawakujulikana

Iliundwa kamati ya kutafuta ukweli wa chanzo cha ajali. Yakajengwa makaburi ya kumbukumbu kwa heshima ya marehemu , lakini pia kulikumbusha taifa kisa cha mkasa huo

Ilitegemewa kupitia kamati na kumbukumbu tungejifunza somo na kuzuia maafa kama hayo

Ilibainika sababu ya kuzama kwa MV Bukoba ni ujazo wa abiria na mizigo kupita kiasi
Hili lilichagizwa na taratibu mbaya za kupakiza abiria na mizigo bila kuzingatia takwimu

Kana kwamba haikutosha, tulipata ajali za Meli kule Zanzibar zilisoababisha upotevu wa maisha

Kwa matukio ya nyuma tunazo kumbukumbu za kutosha kutueleza tuna tatizo mahali fulani. Tunayo makumbusho na minara inayotukumbusha matukio ya nyuma

Hatuhitaji kujenga minara au kuweka kumbu kumbu nyingine kwani zilizopo zinatosha

Tunahitaji kujiuliza maswali na kutafutia majibu hadharani na kwa ukweli

1. Taratibu zetu zinazoongoza usafiiri wa abiria na mizigo katika bahari na maziwa vinakidhi shinikizo na msukumo wa hali ya maisha na mazingira tuliyo nayo?

Wingi wa abiria na mizigo ni ishara kuwa huduma ima haitoshelezi au haitolewi kwa utaratibu unaokidhi mahitaji na mazingira yaliyopo. Tunafanya nini kukabili hili?

2.Mamlaka zinasozosimama usafiri wa majini zinawajibika katika kufuatilia, kubaini na kutoa ufumbuzi? Inakuwaje kuna bodi , na utawala wa mamlaka bila kuwa na utaratibu unaoeleweka

Inasemekana nahodha wa MV Nyerere alikuwa 'Day worker' au dei waka kwa mtaani

Inatokeaji deiwaka aaondoa chombo bandarini moja na kukikifikisha bandari nyingine ikiwa kuna SOP zinazoongoza kuruhusu, kuwasiliana na kupokea chombo point moja hadi nyingine.

Kwamba, hakuna 'checks and balances' ambazo zingetoa angalizo kuhusu ukiukwaji wa taratibu. Inakuwaje hakuna aliyewahi kuona mapungufu na kuyazuia kabla hayatokea

Inaendelea.....
 
KUZAMA KWA KIVUKO MV NYERERE
Sehemu ya II

3. Mamlaka #2 hapo juu zinatoa 'appraisal' kwa manahodha ikiwa hakuna log ya kujua nahodha ameendesha kwa muda gani na katika hali gani na ufanisi gani.
Utaratibu wa kudhibiti manahodha ungedhibi deiwaka kukabidhiwa chombo

4. Manadhoha wanapata utaalamu wapi, wanasajiliwa na bodi au wanapewa leseni?
Regulated industry au professional yoyote inaweka 'mzigo' au onus kwa mhusika kuwa responsible kwa yanayotokea.

Hata kama nadhodha angekuwepo, responsibility inaangukiwa kwake si kwa deiwaka kwa dhama ya leseni, viapo na maadili ya kazi yake

5. Je kuna taratibu gani zinazowabana wahusika wa kupakia mizigo na abiria kwa viwango?

Utaratibu huu unatumika katika vyombo kama ndege. Kwamba, waliohusika na kucheki mizigo na uzani wake, usalama n.k. wanasaini kukubali wajibu itakapotokea vinginevyo. Kwanini si meli

6. Kwasababu tulizosema #1 hapo juu, vyombo vinasafiri bila ratiba.

Hakuna muda wa kuandikisha wasafiri kwasababu haijulikani muda au siku chombo kitaondoka.
Hili ni kutokana na kukosekana uwiano wa taratibu za usafiri na pressure ya wasafiri

Matokeo yake hakuna anayejua idadi ya abiria, hakuna anayejua uzani wa mizigo na hakuna anayejua majina ya abiria husika.

Hoja kwamba ni vijijini haina mashiko,ikifihamika chombo kinaondoka alhamisi saa 2 abiria wanapaswa kuwa na tiketi. Ikizooeleka hakuna tatizo

7. Kwasababu hatujui nani kapanda, yanapotokea maafa hatujui ni abiria wangapi wamefariki, wangapi wamenusurika. Hili linaleta tabu katika harakati za kutafuta.

Nani anaweza kujua chombo cha abiria 100 kinaweza kuwa na 200, 300 au 400.
Rescue (uokozi) na recovery( uopoaji) unafanyika kwa kigezio gani.

8. Kwasababu # 7 , linapotokea jambo abiria na ndugu zao wanapoteza haki muhimu sana
i) Hakuna fidia ya Bima (insurance)

Uwepo wa mifuko ya maafa ni jambo jema lakini uchangiaji wake ni wa hiari.
Si sahihi kufanya hiari kama haki wakati haki (Bima) ikiwa haitolewi au haifuatiliwi

Serikali itatoa sh milioni 1 kwa kila familia ni jambo jema. Hata hivyo, pesa hizo na zile za mfuko wa maafa ni michango ya hali na mali ya kufariji wenzetu si haki. Haki yao ni malipo ya Bima

Kwa hili tunarudi tena kwenye hoja. Je, kuna taratibu za Bima katika vyombo hivyo?
Na kama zipo nini wajibu wake, kama hakuna ni kwanini na sababu gani?

Inaendelea......
 
KUZAMA KWA KIVUKO MV NYERERE
Sehemu ya III

Sababu za mabandiko 2 yaliytangulia ni baadhi tu, kwa undani zinaweza kuwa nyingi zaidi

Wengi wanaeleza sababu za kuzama kwa chombo ni idadi kubwa ya abiria na mizigo
Hiyo sababu iliyozamisha chombo, ni dalili ya sababu zilizozamisha chombo

Sababu halisi ni kukosekana kwa udhibiti na utaratibu wa kuhakiki na kufuatilia vyombo
Kwa sehemu kubwa ni uzembe katika ngazi zote na wala si deiwaka

Haihitaji sayansi kubwa kiasi hicho katika kudhibiti na kuratibu shughuli. Kinachotakiwa ni commitment, na watu wanaojua shughuli hizo. Ubunifu na kufuata taratibu muafaka

Kwa mfano, mtu wa hali ya hewa angeweza kubaini deiwaka si nahodha na kutoa taarifa

Wapanga mizigo na abiria wasingepakiza bila sahihi ya nahodha, deiwaka asingepata mwanya.

Watu wanaopokea vyombo wasingekubali kupokea chombo cha deiwaka

Nahodha asingeondoa chombo kama angejua idadi ya abiria imezidi na uzani wa mizigo n.k.

Kwa maana kwamba kila mmoja angewekewa majukumu yanayombana kisheria chombo kisingeondoka bandarini kwasababu nzuri na za kiusalama

Ni nani wajabike kwa kushindwa kudhibiti na kutoandaa taratibu?

Kwanza, hili ni tatizo letu la kufanya kazi kwa mazoea tu bila kujali taratibu

Pili, ni tatizo la kuwa na watu wasioweza kutekeleza majukumu yao

i. Bodi za mamlaka zimegeuzwa maeneo ya allowance na porojo.
Hazina nguvu, hazina majukumu yanayowabana. Ni kama maeneo baada ya kustaafu

ii. Watalaama wetu uwezo wa ubunifu ni wa kutia shaka.

Hivi kupitia matukio kama MV Bukona hakuna aliyefanya retrospective study na ku project kama itatokea itakuwaje na izuiwe vipi istiokee

iii. Hizi kamati za Bunge tunazosikia zinatembelea maeneo , kiuhalisia zinakagua nini?
Hakuna aliyeona tatizo kwa kuangalia yaliyotokea MV Bukoba

iv. Sheria zetu hasa za bima ni laini na hazina meno. Kote duniani wenye vyombo huhofia fidia ikiwa litatokea tatizo, ndiyo maana kuna recall za magari hata kama kiti kimezidi inch kadhaa
kutoka kilipopaswa kuwepo.

Bima huwawajibisha wahusika vilivyo na hivyo kutimiza wajibu wao

v. Ukitazama mlolongo mzima hakuna eneo la serikali au Bunge lisilokuwa na 'mkono' katika matukio haya. Haya ni mambo yanayoweza kudhibitiwa hata kama si kumalizwa

Maana yake ni moja, serikali na Bunge vipitie upya taratibu za usafiri, viweke sheria kali na kuzisimamia. Zisimamie mamlaka husika na Watendaji na kwamba, yanapotokea majanga wahusika wanatafutwa mara moja wanafikishwa mbele ya sheria na kupata haki wanayostahili

Tumalizie kwa kusema meli haikuzama kwasababu ya wingi wa abiria, au abiria kuhamia eneo la mbele au kuendeshwa na deiwaka. Hizo si sababu aslani. Ni majibu mepesi kwa hoja nzito

Ni majibu ya mkato yasiyoeleza tatizo na wala hayapaswi kujadiliwa na jamii yenye werevu

Chombo kilizama kwasababu hakuna udhibiti wa usafiri na usalama wa vyombo, hakuna taratibu za kuongoza kazi na kama zipo hazifuatiliwi.


Tusemezane
 
Wamarekani nao wamepigika...sana bila kujali tofauti zao na rangi ya ngozi. Nao wanagombania mitumba siku ya gulio (Ijumaa Nyeusi) tazama mwenyewe.




View attachment 945011
Black Friday brings out the crazy carnage once again (PHOTOS, VIDEOS)


..nadhani UMETELEZA.

..Wamarekani waliopigika utawaona mitaani kama ombaomba na wasio na makazi.

..Unahitaji kuelewa maana ya black friday ili kuelewa kinachoendelea ktk video uliyoileta.

..black friday ni Ijumaa inayofuatia sherehe ya Wamarekani inayoitwa Thanksgiving.

..siku ya black friday, kila mwaka, maduka mbalimbali huteremsha bei za bidhaa kwa kiwango kikubwa ili kuvutia wanunuzi.

..kwa hiyo siku hiyo unaweza kukuta bidhaa zimeteremshwa bei hata kwa asilimia 60.

..katika mazingira hayo watu wengi wa vipato vya kati na chini hudamka na kwenda madukani kujaribu kununua bidhaa mbalimbali at a DISCOUNTED PRICE.

..Video uliyoileta inaonyesha wateja wakigombea TV mpya na siyo mitumba au bidhaa zilizotumika
kama ulivyodai.

cc Nyani Ngabu
 


Battlefield Paris: Police hit protesters with tear gas as massive fuel rallies grip France (VIDEO)
===
Hawa si ndiyo wanatetea uhuru wa kuandamana...mbona sasa wanawapiga mabomu wananchi wao. Kiasi cha wananchi hao kulazimika kuharibu miundo mbinu baada ya kunyimwa uhuru wa kuandamana. Hakuna cha utawala bora na demokrasia iwe Ulaya ama Amerika ya kaskazini. Ni unafiki unafanywa.


..hivi huoni Polisi wanaoonekana ktk video wanavyojitahidi kutuliza maandamano kwa uangalifu mkubwa? unaweza kulinganisha na UKATILI unaofanywa na Polisi wetu?

..umeona jinsi wanavyowakamata waandamanaji? umelinganisha na jinsi polisi wetu wanavyokamata waandamanaji?

..Ingekuwa hapa kwetu waandamanaji wangepigwa RISASI ZA MOTO, au wangelipuliwa na MAGURUNETI kama ilivyotokea kwa DAUDI MWANGOSI.

cc tindo
 
..hivi huoni Polisi wanaoonekana ktk video wanavyojitahidi kutuliza maandamano kwa uangalifu mkubwa?
unaweza kulinganisha na UKATILI unaofanywa na Polisi wetu?

..umeona jinsi wanavyowakamata waandamanaji? umelinganisha na jinsi polisi wetu wanavyokamata waandamanaji?

..Ingekuwa hapa kwetu waandamanaji wangepigwa RISASI ZA MOTO, au wangelipuliwa na MAGURUNETI kama ilivyotokea kwa DAUDI MWANGOSI.

cc tindo
Majuzi kuna tukio limetokea Marekani katika mall, kuna mtu kaua watu kwa risasi. Katika kutafuta mhusika Polisi wakampiga risasi kijana mwingine
Leo Polisi wamekiri kuua mtu asiyehusika na kwamba, Polisi aliyeua anachunguzwa

Kuna video ya Polisi aliyetoa maneno ya kibaguzi, amewajibishwa kwa kufukuzwa kazi

Kwa wenzetu kila mmoja yupo ndani ya sheria. Inapotokea makosa, wahusika wanakiri
Uchunguzi huru unafanyika na mwenye makosa anafikishwa mbele ya sheria

Tatizo letu ni Polisi kupoteza imani kwa wananchi kwa taarifa nyingi zinazotofautiana na uhalisia wa tukio

Tukio la Mwangosi RIP, tuliambiwa watu waliokuwa katika mkutano walitupa kitu cha ncha kali
Ushahidi ulipotoka ni Polisi tena wakiwa na wakubwa wao

Kuna matukio ya majambazi ''kuwatoroka'' Polisi wakiwaonyesha walipoficha silaha au wenzao walipo.

Unaweza kujiuliza, hivi Jambazi linaachwaje huru bila pingu kiasi cha kujaribu kutoroka!
Utajiuliza, jambazi linawezaje kutoroka likiwa na pingu, na kama halikufungwa ni kwanini

Suala la Kijana Nondo, Polisi walimleta mbele ya TV kwa mbwembwe.
Polisi wakaacha kazi ya uchunguzi wakajikita katika siasa.

Hilo walifanya wakijua ''mtu hana hatia hadi mahakama itakapomtia hatiani''.

Kulikuwa na ulazima gani wa ''kumhukumu'' mtu bila haki ya kusikilizwa

Mwisho wa siku hawakuweza kutoa ushahidi wa kumtia hatiani, walishamhukumu mbele ya umma ''court of public opinion''. Nondo yupo huru, hakudhalilika. Polisi wanatoa taswira gani kwa umma!

Polisi walituonyesha silaha zilizotumika na watuhumiwa kumuua Dr
Wote wameachiwa. Kazi ya hukumu ilikuwa ya nini? Na je ni kazi ya Polisi kutoa hukumu katika media

Tukio la Tarime la kuuawa nduguye Heche lilionyesha weledi wa Polisi msimamizi

Alijitokeza na kusema ni kweli aliuawa na Polisi. Baada ya hapo kumekuwa na amani, wananchi wameshamwamini Mkuu wa Polisi Tarime. Just kusema ni kweli na ni sisi Polisi ni weledi mkubwa

Kuna taarifa nyingine zinashangaza. Polisi wanasema ' watu wenye ushahidi wa tukio' wapeleke habari kwao. Tukio la Nape kunyooshewa silaha picha za wahusika zipo wazi. Nini kilifuata? Hakuna
Kesho wakiomba ushahidi nani atakyedhani wapo serious na taarifa wanazopewa

Imefika mahali watu wanaogopa kutoa taarifa za matukio kwa hofu ya 'kusaidia Polisi''
Kwa nchi za wenzetu, within an hour kunaweza kuwa na tips zaidi ya 1000.

Polisi kufanya makosa kama taaluma nyingine si tatizo pekee, kila mahali makosa yanatokea
Kwetu sisi imekuwa kama mtindo, kutoa taarifa zingine zikipingana na ukweli ulio wazi.

Kulinganisha utendaji wa Polisi wetu na wenzetu si haki. Huko kwingine hukamatwi hadi uwepo ushahidi wa kutosha. Hupelekwi kwenye TV kama mhusika bali utatajwa kama mtuhumiwa kukiwa na ushahidi

Polisi hawezi kukuweka mahabusu kesho akakuachia huru kwasababu tu alitaka.
Hawezi kukuweka mahabusu kwasababu ni Ijumaa ili ulale hadi Jumatatu bila kusomewa mashtaka.

UK maandamano ya Brexit kila siku tena yakiwa na ulinzi
 
At least 278 people have been detained ahead of Saturday’s Yellow Vest rallies in Paris, police say, AFP reported. It comes a day after authorities warned about “radicals” trying to exploit the movement and topple the government.
The nation is preparing for a new wave of mass protests that are gripping France for the fourth consecutive weekend. Some 89,000 officers are patrolling the streets across the country. Armored vehicles belonging to military police were also deployed to the heart of the French capital.
Ahead of the major protests, the police prefecture announced that at least 278 people were detained in the city. Authorities did not elaborate on the exact reasons for the detentions.

Police detain 270+ in Paris ahead of mass Yellow Vest protests
===
NAMNA nchi za ulaya zinavyotekeleza utawala bora na demokrasia na haki ya kuandamana kutoa maoni.
 
Back
Top Bottom