Duru: Matukio na habari za Dunia

VITA YA ISRAEL-HAMAS

Tuliahidi kujadili baadhi ya maswali katika bandiko hapo juu lakini awali ya yote tuangalie yaliyojiri leo

1. Egypt na Jordan Abdulla wamekataa kupokea Wakimbizi wa Palestina katika nchi zao
Rais wa Egypt alisema wakimbizi watashambulia Israel na Israel itajibu kwa kuwashambulia wakiwa Misri. Hataki

Ukweli ni kwamba nchi za Kiarabu hazitaki kuwapokea kwasababu kufanya hivyo kunaipa Israel nafasi ya kuwaondoa katika ardhi yao ya asili. Jordan kwa sasa ina Wakimbizi takribani nusu ya nchi.
Njia rahisi ni kukataa kuwapokea ili Israel ibebe mzigo huo. Japo ni hatua yenye maumivu , kwa muda mrefu ni nzuri

2. Israel ime endelea kuibomoa Gaza kwa makombora , leo imepiga kanisa la Orthodox na kuua watu
Picha za shambulio la jengo moja zimeonyesha maiti 7 za Watoto kupitia Televisheni za Mashariki ya kati

Kushambulia Kanisa kunatoa taswira kwamba Israel ilihusika katika kupiga bomu Hospitali ya Anglican

Pamoja na jitihada zote za vyombo vya magharibi kuweka ''ushahidi' sehemu kubwa ya Dunia imekataa kuwaamini
Taswira ya Israel imezidi ni mbaya kuliko Hamas , ndiyo maana Rais Biden kahutubia na kusema ''maneno'

3. Rais Biden amehutubia Taifa akiomba Bunge liidhinishe pesa kwa ajili ya Ukraine na Israel. Biden amejaribu kuleta ' suluhu' akieleza machungu ya pande zinazohusika. Biden ameitaka Israel ifungue njia za misaada na iache hamaki na makosa na ifuate sheria za kivita. Kauli ya Biden imechukuliwa na vyombo vya habari vya mashariki ya kati kama kukiri kosa la klipua Hospitali.

4. Marekani imedai kuzuia makombora yakitoka Yemen kuelekea Israel.
Ikiwa ni hivyo na si propaganda za vita, makombora hayo ni 'cruise missiles' yanayojiongoza.
Marekani inadai ni ya kundi la 'Huti' linalosaidiwa na Iran. Huenda vita imeingia hatua nyingine na Marekani inaweza kujikuta imeingia, jambo ambao Raia hawataki wakikumbuka ya Afganistan na Iraq

5. Hezbollah wameshambulia kaskazini mwa Israel kwa makombora yenye shabaha.
Wameshambulia miundo mbinu ya mawasiliano na Israel imejibu mashambuli kwa vijiji villivyo karibu.
Mzozo huu wa kaskazini unaonekana kufungua njia nyingine ya vita, Israel haipendi kwani jeshi litasambaa

Wadadisi wanasema hatua ya Hezbollah ni kuiyumbisha Israel katika hatua za kuingia Gaza.

6. Israel yajiandaa kuingia Gaza.
Ni wiki Israel ikijiandaa kuingia Gaza kuwasaka Hamas. Kuna sababu mahususi kwanini Israel imesita sana

Kwanza, kuwanyima 'Hamas' na Wapalestina maji, umeme, matibabu na chakula ili kuwadhoofisha

Pili, kupiga maeneo ya majengo ili kupunguza msongamano na kuepuka vita ya mjini '' Urban war' na vifo vya askari

Tatu, kuna 'mateka' na Israel inataka kuwaokoa lakini inachelea kuingia Gaza watauawa

Nne, Kuna kikosi cha uokoaji kipo kazini kwa mazoezi (simulation) na ili kukipa kikosi muda na nafasi ni lazima hayo matatu juu yafanyike

Tutajadili maswali ya liyotangulia bandiko lijalo
 
1. Ni kweli zaidi ya 90% ya mijadala ya Watanzania ni Simba na Yanga, sijui tulikosea wapi? Ni vigumu kujadili mambo ya kitaifa au ya kimataifa ambayo yanatuathiri moja kwa moja. Tunaathirika.
2. Kuhusu ukatili wa Israel wakati mwingine mimi nafikiri tatizo ni waarabu wenyewe ambao wameshindwa kuungana dhidi ya Israel. Wakati makaburu walipokuwa wanawatesa waafrika kule SA, Waafrika ya akina Nyerere, Kaunda, Mugabe etc waliungana licha ya kuwa hawakuwa na nguvu za kijeshi mpaka makaburu wakaangushwa. Ni nini kinachowashinda Waarabu. Unaambiwa Saudia au misri inapatana na Israel kuliko inavyopatana na Syria.
 
1. Ni kweli zaidi ya 90% ya mijadala ya Watanzania ni Simba na Yanga, sijui tulikosea wapi? Ni vigumu kujadili mambo ya kitaifa au ya kimataifa ambayo yanatuathiri moja kwa moja. Tunaathirika.
2. Kuhusu ukatili wa Israel wakati mwingine mimi nafikiri tatizo ni waarabu wenyewe ambao wameshindwa kuungana dhidi ya Israel. Wakati makaburu walipokuwa wanawatesa waafrika kule SA, Waafrika ya akina Nyerere, Kaunda, Mugabe etc waliungana licha ya kuwa hawakuwa na nguvu za kijeshi mpaka makaburu wakaangushwa. Ni nini kinachowashinda Waarabu. Unaambiwa Saudia au misri inapatana na Israel kuliko inavyopatana na Syria.
Kamili , hoja zako nitaziunga na maswali ya bandiko#60 kwasababu zinawiana sana

1. Mijadala Watanzania imejikita kwa yasiyogusa Taifa au kimatifa. Watanzania wanaungalia mgogoro wa Israel-Palestine kwa jicho la udini. Wengi wanadhani tatizo limeanza October 7,2023, humeza habari kutoka vyanzo vya aina moja. Kizazi cha vijana kimekosa utamaduni wa kujisomea , kujifunza, kudadidisi na kuyatazama mambo kwa upana.

Upeo wa kuielewa dunia ni jambo muhimu katika ushindani wa duni. Huwezi kutenga mgogoro wa Mid East na maisha au Kazi au Biashara popote alipo mwanadamu.

Jaribu kuuliza Watanzania uliza swali hili '' kwanini dollar imeadimika'' majibu utakayopata yatakushangaza.

2. Kuna swali ; Kwanini Israel inakingiwa kifua na Mataifa ya Magharibi?
Israel iliundwa na nchi za Magharibi 1948, saa 11 baada ya kujitangaza Utaifa , Rais Truman wa US aliitambua na kudharau kamati ya Uingereza-Marekani iliyopendekeza nchi mbili 'two sates' solution''

Pili, Wayahudi wanamiliki uchumi wa nchi za Magharibi, kubwa zaidi wanamiliki vyombo vya habari.
Mafanikio ya kibiashara na umiliki wa vyombo vya habari unawapa nguvu sana za kuamua siasa za mataifa.

Katika mgogoro unaoendelea CNN , Fox na MSNBC vimekuwa vyombo vya propaganda vya Israel. Habari zao ni biased hazina weledi wa kiuandishi na zimelenga kuipa Israel eneo la propaganda bila kusikiliza Wapalestina

Marekani kuna taasisi ya Waisrael inayoitwa AIPAC (America-Israel Public Affairs committee.
Ushawishi wa Taasisi hii kifedha na njia za habari ni sehemu muhimu sana ya Uchaguzi wa Marekani.

Wasrael wapo katika serikali za magharibi na wanafanya maamuzi mengi.
Waziri wa mambo ya nje US wa sasa ni Muisrael na wengi tu katika idara na taasisi mbali mbali muhimu

Wakati wa Rais Trump, waandamanaji wa kizungu (white supremacist) walibeba mishumaa na mabango yasemayo ( Jews will not rule us) yakiimanisha Wayahudi hawatutawala. Hawa niWaamerika Wazungu wanaosema hivyo.

3. Kwanini Iran inaunga mkono vikundi vinavyopingana na Israel?
Vikwazo vya nchi za Magharibi kwa Iran ni kutokana na Iran kuendeleza sayansi ya nuclear inayoweza kutoa Bomu.

Israel ina wasi wasi na Iran kwasababu ya nguvu za kitaaluma katika viwanda na Sayansi.
Tumewahi kujadili hapa kwamba Iran ikiwa na SHIA ina Raia walioelimika sana mashariki ya kati

Iran ina rasilimali za mafuta na inazitumia kwa kuelimisha Raia wake takribani Milioni 86 mara 12 ya idadi ya Israel.

Iran ina mpaka na Israel na nchi rafiki kama Syria na Lebanon kupitia makundi ya SHIA.
Iran ni tishio kwasababu haitegemei teknolojia ya Magharibi kujiendeleza na Israel inapata tabu kuipeleleza.

Kuuwa kwa kingozi wa Nuclear Bw Mohsen na Kamanda wa Jeshi Qasem ilitekekelezwa na Israel kwa juificha nyuma ya Marekani. Israel inatambua vita na Iran ni mchezo tofauti kabisa na huu wa Hamas, na huitumia Marekani

Iran imeshapata mashambulizi ya Israel kwa mauaji ya viongozi wake, inajibu mapigo kuipitia vikundi mbali mbali kama Hezebollah, Huti n.k. Kwavile 'adui yao ni mmoja' Iran na Hamas (SUNNI) wanashirikiana

Hamas kimsingi walitakiwa kuungwa mkono na Saudi Arabia, kwa kutoswa wameamua kushirikiana na Iran
Hii haina maana Hamas na Hebollah wanaiva, la hasha, wanaiva dhidi ya adui wa pamoja ''common enemy'

4. Waarabu wameitosa Palestina ? Kwanini Saud Arabia inataka 'normalization''
Ni kweli Palestina imetoswa na nchi za Kiarabu kwasababu moja, hofu ya nani mbeba Mashariki ya kati.

Saudi Arabia ina Sunni wengi kama tulivyowahi kusema. Iran ina Shia wengi. Pakistan , Afganistan, Qatar, UAE, Kuwait, Yemen , Lebanon , Syria , '' Misri , Morocco, Tunisia , Algeria' zenye Waarabu zimegawanyika kwa mrengo wa Shia na Sunni. Kuna vita ya 'dominance' ya mashariki ya kati , Saudia ikipoteza ushawishi

Tutaendelea tulipoishia '' kupoteza ushawishi''
 
Inaendelea kutoka bandiko #63

Ili kufahamu vema mahusiano ya nchi za kiarabu , pitia uzi huu hapa ( Mgogoro wa Qatar vs Saudi Arabia)

Nchi za Kiarabu kama Qatar, UAE , Saudi Arabia, Syria majority ni Sunni. Nchi kama Bahrain , Iran , Iraq ni SHIA.

Iran ina nguvu za kitaaluma, teknolojia na ushawishi mkubwa kiasi cha kuzifanya nchi nyingine ziingie wasi wasi.

Saudi Arabia inahofia ushawishi wa Iran kuliko Taifa jingine, inapoteza ushawishi kama Taifa kiongozi

Israel inazitumia nchi za Kiarabu kama UAE, Kuwait na Saudi Arabia kurudisha mahusiano kwa kuitambua.

Kwa njia hizo huo utakuwa mwisho wa madai ya Palestina. Kwa maneno mengine Israel inataka Palestina kupoteza uungwaji mkono na nchi kubwa za Kiarabu

Nchi ya Saudi Arabi ilikuwa karibu kufikia makubaliano ya ''normalization' yaani kurejesha mahusiano na Israel.

Kilichokwimisha hatua za mwisho ni takwa la Saudi Arabia kutaka ulinzi wa Marekani na pia kujengewa mtambo wa Nuclear. Mtambo huo ni kwa lengo moja, kukabiliana na Iran.

Saudia kama nchi kiongozi ilikuwa tayari kuwatosa Wapalestina ili kujilinda dhidi ya Iran kupitia Israel na US

Kama kuna kiongozi wa Saudia aliyaaewahi kuharibu taswira ya nchi hiyo ni MbS mrithi wa Ufalme.

Huyu kupitia Jerad Kushner aliyeoa mtoto wa Trump na ambaye ni Myahudi wameshirikiana sana katika kupoteza hadhi ya falme kuu ya nchi za kiislam (Saudia)

Mvurugano wa nchi za kiarabu umeharibu jitidaha za Palestina kujikomboa.

Hamas hawakufanya shambulio kwa bahati mbaya, walikuwa na sababu.

Kwanza wamelazimu Saudi Arabia kusitisha mpango wa 'normalization' na Israel.
Saudia imechelea ' vijana wasije leta spring revolution' kwa yanayoendelea Gaza
Pili, Hamas wamerudisha agenda ya two states solution mezani.

Kwa kumaliza ni kwamba, tofauti za nchi za Kiarabu hasa katika madhehebu zimewavuruga sana.
Palestina ni mhanga wa mvurugano huo wa nchi hizo kama tulivyoona.

Hata hivyo, vita inayoendelea imeibua kizazi kipya kinachotaka mabadiliko. Mkutano wa Cairo jana na leo ulikuwa na lengo moja , kutuliza munkari na hasira za vijana wa kizazi cha leo wanao ona Wazazi wao wamewasaliti Wapalestina.
 
3. Rais Biden amehutubia Taifa akiomba Bunge liidhinishe pesa kwa ajili ya Ukraine na Israel. Biden amejaribu kuleta ' suluhu' akieleza machungu ya pande zinazohusika. Biden ameitaka Israel ifungue njia za misaada na iache hamaki na makosa na ifuate sheria za kivita. Kauli ya Biden imechukuliwa na vyombo vya habari vya mashariki ya kati kama kukiri kosa la klipua Hospitali.
Hivi ni kweli Biden anawahurumia wa Palestine, Ili Hali, kwake wagonjwa wanaweza kufika mlangoni mwa hospitali kisa wamekosa fedha za matibabu ? Tuhuma hizi za mgonjwa kufika mlangoni huko US amezitoa Rais wa Russia.

 
Hivi ni kweli Biden anawahurumia wa Palestine, Ili Hali, kwake wagonjwa wanaweza kufika mlangoni mwa hospitali kisa wamekosa fedha za matibabu ? Tuhuma hizi za mgonjwa kufika mlangoni huko US amezitoa Rais wa Russia.

Nadhani hukunisoma vizuri au umesoma hukuzingatia alama . Nilisema hivi Biden anajaribu kuleta '' SULUHU''
Neno suluhu lina alama '' '' hiyo inaeleza kifungu kizima

Hata hivyo kwa minajili ya mjadala, jibu ni kwamba Biden hana utetezi wowote kwa Wapalestina.
Tunachokiona ni kutafuta kura kutoka kwa '' Immigrant' katika majimbo muhimu ya uchaguzi kama Michigan.

Kura za awali za uchaguzi wa Democrats zinaonyesha Michaigan kuna kundi la asilimia takribani 13 ni 'uncommitted' likisukumwa na hali ya kisiasa mashariki ya kati. Hali ni Mbaya zaidi Minnesota ambako asilimia 19 ni uncomitted.

Kwanini tunasema hana msaada kwa Wapalestina
1. Biden amewapa Israel Mabomu yasiyo na shabaha ' precision' ambayo Israel imeyatumia kuua na kuua raia wasio na hatia. Idara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) imethibitisha kwamba haiwezi kutumia mabomu hayo na mara ya mwisho yalitumika Afghanistan tena kwa idadi isiyofikia 10. Israel imepewa ya kutosha.

2. Biden ana uwezo wa kulizamisha Israel ifungue mipaka ili misaada ya kibinadamu ifike Palestina. Tofauti na hilo ameamua kurusha chakula kwa ndege kitu ambacho hakitoshelezi hata 1/10 ya matumizi bali kujikosha

3. Biden ametumia turufu ya Veto kuikingia kifua Israel ili isilazimike kusitisha mashambulizi kwa Raia.
Kwa maana kwamba Biden anarusha chakula kwa ndege, halafu anawapa Israel mabomu yasiyo na shabaha na kisha kukinga kifua UN.

Haya ni kwa uchache tu, yatosha kusema hana lengo la kuwasaidia Wapalestina hasa watoto na Wanawake.

Hata Waisrael wenyewe wanapinga mashambulizi yanayoendelea lakini Biden anacheza na akili za watu katikati ya misiba.

Kuhusu Wagonjwa kufia mlangoni, well, katika nchi za kibepari mambo yanakwenda yakiwa yemenyooka.
Inaweza kuonekana ni ukatili lakini tujiulize mfumo wetu wa Bima ya Afya upoje?
Kuna tofauti gani ya mgonjwa kufia mlangoni na Mzazi kule Mwanza kujiufungulia sakafuni na hata kufa akiwa juu ya baiskeli.
 
Kuhusu Wagonjwa kufia mlangoni, well, katika nchi za kibepari mambo yanakwenda yakiwa yemenyooka.
Asante sana Mkuu kwa ufafanuzi. Nitarudi Tena kwa ajili ya kupanua mjadala huu katika masuala ya multipolars inayoanza kupigiwa debe na "wanyonge".
 
Back
Top Bottom