Duniani kumbe bado kuna watu wema, inafikirisha sana

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,228
9,821
Mwezi wa April 2020, wakati narudi kutoka Ifakara kwenye Biashara zangu nilipanda Bus nafikiri ni Kidinilo Express, Kulikuwa na abiria mmoja kukadiria umri wa miaka kama 45 au 48 alikuwa Karibu yangu, tulipo karibia Kufika Mang'ula, Alianza kulia huku akishika kichwa na kuinama chini

Nilishikwa na hofu kidogo nikawaza isije kuwa Corona au michezo ya mjini, wakati natafakari nianze kumuliza kulikoni, Dada mmoja alikuwa mbele yetu upande wa pili alimuuliza " Vipi Unajisikiaje, njoo upande huu ukae Dirishani" baada ya kwenda kukaa upande ule wakawa wanaongea ndipo nikajua kuwa wanafahamiana na huyo Dada.

Lakini kadri tulipokuwa tunaenda jamaa hali ilizidi kuwa mbaya mpaka yule binti akamuita Konda akaomba washuke pale Mang'ula na mgonjwa, wakachukuwa Mabegi yao hao wakashuka.

Wakati tunaendelea na safiri tukiwa Mikumi, nilipigiwa simu na mtu ambaye ni muda mrefu sana hatujawasiliana, ananipigia simu ananiambia kuna mtu ameshuka na Bag langu hivyo nakupa namba zake nimpigie, ila pia yeye ameacha bag yake, Dah moyo ilipasuka mapigo ya moyo yakienda mbio kwani kwenye Bag, kulikuwa vitu vyenye thamani kidogo kulikuwa na Laptop hp mpya nilinunua 1.6m, pesa taslimu 1.4m jana yake nikishindwa kuwahi kuweka kwenye ac nilifika usiku Ifakara toka Mahenge, simu coolpad 1 nilinunua 380,000 aliexpress ilizima chaji nikaweka kwa bag, Camera ya sony, Mkataba wa Manunuzi ya Eneo na nguo kadhaa.

Baada ya kupewa namba kwa kweli nilipiga huku sina imani, jamaa alipokea simu ila network ikawa haisisiki vema, tukaanza kuchati kwa sms, aliniambia yeye kwenye bag yake kuna shuka ya kimasai, shati, suruali, dawa za kienyeji na simu ya torch mbovu, akanitajia kila kitu kilichopo kwenye bag yangu na akasema nisijali nitavipata vitu vyangu kama vilivyo kwani anasafiri ya kuja Dar akipata nafuu, Ila bag lake nisijali sana maana hakuna vitu vyenye thamani, hapo nilipatwa na shaka kidogo ila nilijipa moyo.

Nikamwambia ngoja nikifika Morogoro nitapata wazo la kufanya ikiwezekana nitakuja mpaka Mang'ula kuja kuchukuwa maana kuna document muhimu sana lazima niende nazo, Lakini pia nilimwambia nitamtuma mtu aje, akanijibu kama ni hivyo sawa ila kama ninamuamini niwe na subira, kwani kesho kutwa yaani Jumatano atakuwa Dar.

Njia nzima nilikuwa na msongo wa mawazo balaa, nikawaza sijui nikaripoti polisi au nimuamini tu, nikawa na mawazo mchanganyiko

Niilipofika Moro nikawa tayari namaamuzi ngoja niunge mpaka Dar, nimwamwini tu maana angekuwa na nia mbaya asingenitafuta, Nikawaza nikiimtilia shaka itakuwa tatizo zaidi basi nikamuachia Mungu.

Kesho yake hakupatikana kwenye simu kabisa, siku hiyo nililala vibaya sana, kesho kutwa yake jumatano saa 5 ndiyo nikampata baada ya kunipigia kwa simu nyingine akinitaarifu amefika Morogoro tukutane stand ya Mbezi kuanzia saa 9 mchana, Nilijitahidi kufika mapema pale Mungu ni mwema tulikutana akanipa bag langu na mimi nikampa la kwake akacheki na mimi nikacheki la kwangu kila kitu kipo sawa.

Nilimpongeza nilibaki kumuuliza wewe ni dini gani, Alinijibu yeye ni mmoja wa Wa Mashahidi wa Yehova, kwakweli aliniomba msamaha sana sana kwa kilichotokea, pamoja na yote kumbe pia siku hiyo alikuwa anakuja kwenye msiba wa mama yake Tabata Segerea nilimpa pole, Niliporudi nyumbani nikahakiki kila kitu kipo sawa nikamtumia tsh 150,000 huwezi amini jamaa aligoma kuzichukuwa, pamoja na jitihada za kumuhakikishia ni za pole ya msiba aligoma kabisa akazirudisha.

Toka hiyo siku tumekuwa marafiki wa karibu sana, mwezi uliopita nilienda tena Ifakara pamoja na kuwa yeye hakuwepo lakini nilienda mpaka nyumbani kwake nikampelekea zawadi, leo amenitembelea yeye na familia yake watakuwa hapa kwa siku 3, waneniletea mchele wa kutosha sijui nitaumaliza lini.

Nimejifunza pamoja na Dunia kuharibika lakini bado watu wenye hofu ya Mungu wapo.
 
206 Reactions
Reply
Back
Top Bottom