Duniani kote huwa vigumu wanaharakati kushika dola sababu huwa hawawezi kufanya kazi na kuiva na makundi yote katika jamii ikiwemo Tanzania

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,910
51,904
Ukiwa mfuatiliaji wa wanadiasa washika dola duniani kote ni vigumu mno kwa wanaharakati kushika dola sababu huwa hawana uwezo kabisa wa ku mobilize makundi yote katika jamii yswapende na yawaunge mkono kuwapa dola

Makundi hayo Ni Kama viongozi wa kiserikali, mahakama,taasisi za kidini,vyombo vya Habari,vyombo vya dola ,vyama vingine vya siasa nk

Kutokana na ugumu wa wanaharakati kujenga mtandao wa kukubalika na kuungwa mkono na makundi yote kwenye jamii huishia tu kushindwa kushika dola

Chama Cha siasa kikitumia wanaharakati hukiondoa kwenye reli ya Kisiasa na kukiweka kwenye reli ya uanaharakati na kukifanya kisikubalike kwenye makundi mengine kwenye jamii kwa kuburuzwa na wanaharakati

Mfano mzuri Ni Chadema kilikuwa chama Cha siasa kizuri tu kilichokuwa kina ushawishi mkubwa na kukubalika na makundi yote katika jamii sababu kilijenga mahusiano rafiki na kukubalika kwa makundi yote zikiwemo taasisi za Dini na vyombo vya habari,dola ,mahakama nk ndio maana kiliweza kila chaguzi kuongeza idadi ya Wabunge na madiwani wakati wanasiasa Kama Mbowe,Slaa na Lowasa waluposhika sukani za ugombea uraisi.Wote tu madhahidi kwa hilo

Ujio wa wanaharakati kushika uogombea wa akina Tundi Lisu umevuruga kila kitu chama kimegeuzwa Cha Kiana harakati mahusiano ya Chadema na makundi mengine ya kijamii
yamesambaratika UKAWA umesbaratika,uhusiano na taasisi za dini imesambaratika, uhusiano mzuri na vyombo vya
Habari imesambaratika, vingine uhusiano na vyombo vya dola imesambaratika ,uhusiano na vyama vingine vya siasa vya ndani na nje ya Nchi imesambaratika, mahusiano na wafadhili wafanyabiashara wakubwa imesambaratika,uhusiano na wafadhili wa ndani na nje umesbaratika

Makundi ya wananchi kukipenda chama kwa dhati na kukigharimia kumesambaratika.Love level ya wananchi kwenye chama kumeshuka kwa kiwango.cha kutisha sababu hawajui ilani ya chama Wala hawajui chama kinasimamia Nini Sababu tatizo la wanaharakati huwa hawana agenda wao husimamia tu matukio yanayojitokeza tofauti na chama !! Raisi akikohoa mfano mkutanoni kwa mwanaharakati kesho hiyo ndio huwa agenda ohh kea nini raisi kakohoa kwenye public alitakiwa asikohoe sisi kama wanaharakati tunapinga kitendo Cha raisi kakohoa hadharani!!!

Wote mashahidi Chadema imegeuka chama Cha uanaharakati kinachoenda na matukio badala ya kuwa na agenda ya kudumu ya kueleweka kwa wananchi

Chadema kimeondolewa kwenye reli ya Kisiasa na wanaharakati na Hivyo kukipotezea mvuto wa ushindi.Kwa maoni yangu hoja ya ufisadi ilitakiwa kuwa agenda Yao ya kudumu ya Kisiasa ya nyakati zote Bila kuyumba lakini wanaharakati wameiyumbisha Chadema kuogeuza kikundi Cha uanaharakati badala ya chama siasa hivyo kukifanya iwe ngumu kwao kushika dola Kama ilivyo kawaida kuwa vigumu kwa wanaharakati kushika dola popote duniani kea kukosa agenda na kuwa watu wa matukio
 
Bado nguvu ya Wapinzani ni kubwa sana tofauti Na ilivyotegemewa na ccm hata awamu hii hakuna uhuru wa vyomb vya habari usifananishe na awamu zilizopita awamu hii tunaona mgombea wa chama kimoja ndo anaendelea kujitapa
 
Kundi la watumishi was umma hawaivi kabisa na Meko. Hali kadhalika wafanyabiashara, wakulima na wafugaji hawataki hata kumsikia. Je, huyu naye in mwanaharakati?
 
We jamaa acha reasoning ya kijinga. Kwani Mandela hakuwa Mwanaharakati?
Mwl. Nyerere hakua Mwanaharakati na akaanzisha harakati za ukombozi kwa Tanzania.
 
Huyu jamaa bila shaka atakuwa ni miongoni wa wale waliofanya lile shambulio haramu lililofeli sasa anateseka!
 
Tulieni ccm acheni woga na hofu mabadiliko ni lazima, ccm sio mama yenu wala baba yenu na Tanzania bila ccm itakuwa kama Ulaya.
Nambie kwenye hizi nchi za Africa weusi tii,ni nchi gani upinzani ulishika dola,kisha iyo nchi ikawa kama ulaya bwashee?.

Kenya hiyoapo juu tunaiona.
Comoro iko kwa chini hapa tunaiona pia.
Zambia inachechemea.
Ivory Cost taabani.
weusi ni weusi tu,atuna jipya.sema na wekina Lissu wanapambana na wao wale.
 
Back
Top Bottom